Kuchambua na kuweka wazi funzo litolewalo na kazi ya fasihi.
Kuchambua na kufafanua taswira (picha za kisanii) zilizotumika katika kazi ya mwandishi.
Kumshauri na kumtia moyo mwandishi ili afanye kazi bora zaidi (hivyo mhakiki pia ni mwalimu wa mwandishi)
Kumwelekeza na kumchochea msomaji kusoma na kupata faida zaidi ya ambayo angeipata pasipo dira ya mhakiki (mhakiki ni mwalimu na daraja kati ya mwandishi na jamii)
Kuhimiza na kushirikisha fikra za kihakiki katika kazi za fasihi.
Kukuza kiwango cha utunzi na usomaji wa kazi za fasihi.
Kutafuta na kuweka sawa nadharia za fasihi teule.
Kuthamini na kuheshimu kazi za waandishi kwa kuzitendea haki
Posted by: MwlMaeda - 12-12-2021, 10:16 AM - Forum: Nukuu
- No Replies
FASIHI ni sanaa inayotumia lugha na ambayo hujishughulisha na binadamu pamoja na maisha yake na hugusa au huacha athari fulani na hupatikana katika umbo ambalo linatambuliwa na jamii.
Kwa ujumla fasihi ni sanaa inayotumia lugha na yenye maudhui yahusuyo taratibu za maisha ya binadamu katika jamii husika.
Baada ya kuangalia dhana ya fasihi kwa ujumla sasa tuangalie dhana ya mtindo na nafasi yake katika fasihi.
Senkoro (1982) anasema mtindo katika kazi yoyote iwayo ya fasihi ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi hiyo na kuipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni au kaida zilizofuatwa (za kimapokeo) ama ni za kipekee.
Anaendelea kusema, mtindo ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi kwa njia ambayo hutokeza au huonesha nafsi na labda upekee wa mtunzi wa kazi hiyo.
Katika fasili hii tunaweza kuona anachokieleza mtaalamu huyu ni kwamba mtindo huhusiha upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi ambapo upangaji huu hutegemea upekee alionao msanii.
Kwa maana nyingine, unaposoma kazi fulani ya fasihi unaweza kumwona mtunzi wa kazi hiyo kulingana na jinsi alivyoiandika, kwa maana kwamba jambo moja linaweza kuongelewa na wasanii wawili tofauti lakini namna linavyowasilishwa likatofautiana na hii ni kulingana na upekee wao.
Wamitlia (2003) naye anasema mtindo ni jumla ya mbinu au sifa zinazomwezesha mwandishi kuwasilisha ujumbe wake. Huelezea mwandishi anavyounda kazi yake.
Anaendelea kusema, dhana ya mtindo hurejelea sifa maalumu za mwandishi au mazoea ya mwandishi fulani ambayo hujionyesha kwenye fani yake, mazoea hayo ya mwandishi ya kuandika, kuteua msamiati, tamathali za semi, taswira, uakifishaji, sentensi na kadhalika ndio yanayompambanua mwandishi huyu na mwenzake.
Kitu anachokisema hapa Wamitila hakitofautiani na Senkoro. Kinachoongelewa hapa ni upekee wa mwandishi husika, lakini Wamitila kasema kitu kimoja zaidi ambacho inaonekana Senkoro hakukiweka bayana, kwamba msanii anaonekana kuwa na mtindo fulani kwa sababu amezoea kutunga kazi zake za fasihi kwa namna fulani ambayo inadhihirisha upekee wake.
Kwa kauli hii ya Wamitila, tunaweza kusema kwamba mtindo wa mtunzi huonekana baada ya kuandika kazi zake kadhaa na kimsingi hii ndio huleta maana halisi ya mazoea.
Nakubaliana na kauli hii kwani hata hivyo huwezi ukahitimisha kuwa mtunzi fulani mtindo wake ni huu kama umesoma kazi yake moja tu. Kwa hiyo mtindo (upekee) wa mwandishi huweza kubainishwa baada ya kupitia kazi zake kadhaa.
Kwa ufupi tunaweza kusema kuwa mtindo ni ule upekee alionao mtunzi wa kazi ya fasihi katika kuipa kazi yake sura fulani kifani na kimaudhui ambapo mtunzi mwingine hawezi kufanya hivyo hata kama kitu kinachoongelewa ni kilekile.
Ni namna ambavyo msanii hutunga kazi na kuipa kazi hiyo uzuri kifani na kimaudhui. Mtindo huambatanishwa na tabia ya utungaji ambayo humpambanua mtunzi mmoja kutokana na mwingine.
Katika muktadha huu, mtindo hubainika katika jinsi mtunzi anavyoteua kujieleza kwa kuchanganya ndimi, kutumia methali na mafumbo au kufumbata ujumbe kwenye ufupi au urefu wa sentensi zake.
Aidha, dhana ya mtindo huenda ikajumuisha wasanii wa kipindi fulani cha kihistoria na sifa zao za uandishi kwa kutegemea matumizi ya lahaja au maneno ya kale.
MTINDO
Tunapotaka kujua mtindo wa msanii katika kazi husika hususani riwaya tunaangalia matumizi ya lugha; matumizi ya daiolojia; namna na nafsi ya usimulizi; ukuaji wa wahusika; hisia za mwandishi; namna anavyopanga sura au matukio katika hadithi; tamathali za semi; mandhari na uteuzi wa msamiati.
Baada ya kuangalia dhana ya mtindo, ni vyema sasa tukaangalia nafasi yake katika fasihi. Kwa ujumla, mtindo una nafasi kubwa tu katika kazi ya fasihi.
Mtindo humtambulisha mtunzi wa kazi ya fasihi. Watu hupenda kazi ya msanii fulani kwa sababu mtindo anaoutumia huwavutia wasomaji wake.
Mtindo ndicho kipengele kinachotenganisha kazi nyingine za kisayansi au za kawaida. Bila mtindo, kazi za kifasihi zisingepata mashabiki wengi. Kwa hiyo mtindo ndio huibua hisia na kuwafanya wapende zaidi kusoma kazi za msanii husika.
Kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa, tunapozungumzia dhana ya mtindo tunakuwa tunarejelea mwandishi husika, kwa maana kwamba ubinafsi wake ndicho kile kinachoonekana kwenye kazi yake.
Kwa hiyo tunaposema hadithi fulani ina taswira nyingi, ina sitiari nyingi au lugha yake ni rahisi au lugha yake inavutia, imetumiwa kwa uwazi, ufiche au ugumu na kadhalika tunakuwa tunarejelea mtindo wa mtunzi husika.
Kwa mantiki hiyo dhana ya mtindo kama ilivyokwisha jadiliwa inaonekana kwa namna mtunzi anavyopanga kazi yake kifani na kimaudhui, yaani namna anavyotumia lugha, anavyopanga visa na matukio, uteuzi wa mandhari, falsafa anayoiwasilisha, ujumbe anaoudhamiria na kadhalika.
Posted by: MwlMaeda - 12-12-2021, 10:11 AM - Forum: Nukuu
- No Replies
Mwandishi atakuwa huru kuikosoa jamii au tabaka lolote litakaloenda kinyume nautaratibu wa jamii bila matatizo.Mwandishi atakuwa huru kuonyesha dhuluma, ukatili na ujangili unaofanywa katika jamii na tabaka lolote bila matatizo yoyote.
Kukiwa na uhuru wa mwandishi, msanii atakuwa na falsafa inayoeleweka pamoja na utashiwake.Hii itamfanya mwandishi awe na msimamo unaoeleweka.Msimamo wake utamsaidia kuifundisha na kuielimisha jamii bila uoga.Ataijiulisha jamii hali yake na ataonesha jamii njia za kufikia haja na kutatua matatizo ya jamii bila uoga
Mwandishi atakuwa huru kutoa mwongozo katika jamii kwa kuikomboa jamii kutoka katika fikra mbovu za kugandamizwa,kunyonywa na kuonewa na tabaka tawala ili jamii ipate haki na heshima bila woga wa kuliondoa tabaka ambalo ndilo lenye mamlaka yote katika jamii.
Uandishi wa kikasuku utapungua, waandishi au wasanii huacha tabia ya kuwa vipaza sauti vya tabaka fulani katika jamii, wasanii makasuku huandika mambo bila kufikiri na kurudiarudia mawazo yaliyokwisha semwa na wanasiasa majukwaani bila fikra mpya kwa hali hii hupotosha jamii.Hivyo kunapokuwa na uhuru wa mwandishi wa kutosha hali hii haiwezi kutokea kwa sababu mwandishi ataandika mambo mbalimbali yanayojitokeza katika jamii na hataweza kujikomba au kujipendekeza kwa tabaka tawala lenye mamlaka yote katika jamii.
Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi fasihi inakuwa chombo cha kuikomboa jamii kiuchumi,kisiasa, kiutamaduni na kifikra (kimawazo). katika jamii ya kitabaka fasihi ni mali ya tabaka tawala na hutumia fasihi kutetea na kulinda maslahi yao.Hivyo inapokuwa mali ya jamii nzima inatumiwa na jamii hiyo katika kuwakomboa wanajamii wote.
Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi, mwandishi anakuwa huru kuichokoza na kuisukasuka (kuichochea)jamii bila matatizo yeyote. Mwandishi atachokoza jamii ya wakulima na wafanyakazi kufikiri ili waweze kulichunguza tabaka tawala kwa jicho pevu na kutoa hadharani uozo uliopo katika kunyonywa, kupuuzwa,kuonewa, kugandamizwa na kunyanyaswa na tabaka tawala
Mwandishi atakuwa huru kuelimisha na kuishauri jamii katika mambo muhimu yanayojitokeza katika jamii bila woga.Mwandishi ataishauri jamii kuhusiana na mambo kama vile afya, elimu na ichague mambo gani yanafaa kuhifadhiwa na yapi hayafai vile vile msanii anakuwa huru kuirekebisha jamii bila woga kwa kuangalia yapi ni mazuri na yapi ni mabovu yanayotendeka katika jamii