ETIMOLOJIA YA NENO ' DARI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO ' DARI' (/showthread.php?tid=1683) |
ETIMOLOJIA YA NENO ' DARI' - MwlMaeda - 12-06-2021 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' DARI'. Neno *Dari* (wingi: *Madari* ) katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Sakafu ya juu ya nyumba iliyo baina ya paa na kuta za nyumba. 2. Sitaha/Staha; sehemu ya mbele au nyuma ya chombo kama Jahazi au mtumbwi iliyo na ubao wa kukalia au kuwekea vitu. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *dari* ( **daarun/daaran/daarin* *دار* ) lina maana zifuatazo: 1. Riziki. 2. (Kivumishi) -enye kuendelea mfululizo bila ya kukatika/kukoma. 3. Mahali panapoungana jengo na uga. 4. Nyumba wanayoishi watu . 5. Mji/Nchi. 6. Kabila. 7. (Neno hili likianza na kiambishi 'al' likawa 'Al-Daar' (soma: Ad-Daar): mji wa Baghdad katika nchi ya Iraq. 8. (Likiongezwa neno 'Al-Salaam' (soma: As-Salaam) likawa 'Daaru Al-Salaam' (soma: Daarus Salaam): Pepo. 9. Likiongezwa neno 'Al-Qaraar' kikawa 'Daaru Al-Qaraar' (soma: Daaril Qaraar': Akhera/Ahera, kuzimu. 10. Likiongezwa neno 'Al-Harb' kikawa 'Daaru Al-Harbi' (soma: Daarul Harbi': miji ya maadui. Katika Lugha ya Kiarabu neno sakafu ( *saqfun/saqfan/saqfin* *سقف*) ndio linalobeba maana ya neno 'dari' katika Kiswahili, 'sakafu ya juu ya nyumba iliyo baina ya paa na kuta za nyumba'. Hii inaonesha kuwa neno hili ( *dari* ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili maana yake katika lugha yake ya asili (Kiarabu) ilibadilika na kuchukua maana mpya zilizobainishwa. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |