AINA ZA TASWIRA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=78) +--- Thread: AINA ZA TASWIRA (/showthread.php?tid=1875) |
AINA ZA TASWIRA - MwlMaeda - 12-28-2021 Taswira ni picha inayojengeka akilini mwa msomaji. Kuna aina tofauti tofauti za taswira. Kama vile
Taswira uoni –inajitokeza unapopewa picha ya mtu (umbile)
Taswira sikivu- unapewa picha akilini lakini inayopitia masikio
-(Kana kwamba unaskia sauti masikioni) Mfano katika wimbo aliomtungia mamake Kongowea kuhusu kifo chake
Taswira mwonjo – mfano Musa na Maksuudi wameandaliwa chakula na Kazija – (unasikia kana kwamba kuna harufu na wanakula chakula kwa maelezo)
Taswira mnuso – ni pale ambapo mwandishi anakupa maelezo
yanayokufanya unuse harufu. Mfano: Kongowea anapoinusa harufu ya Kazi-Kwisha alipofika kwake siku ya mwisho kutambua ni babake
Taswira hisi – wakati msomaji anaelezewa kuhusu kitendo kinachotoa hisia mfano wakati mhusika katika Utengano (Tamima) anachapwa na Maksuudi.
Taswira Mguso – msomaji anapohisi yuaguswa anaposoma wakati Vumilia anamshika Kongowea Mswahili akimsihi aende kulala.
|