MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 129 online users.
» 0 Member(s) | 128 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  MBINU ZA KUFUNDISHIA
Posted by: MwlMaeda - 06-21-2021, 07:22 AM - Forum: Nukuu - No Replies

MBINU ZA KUFUNDISHIA

Mbinu za kufundishia, ni miongozo mbalimbali atumiayo mwalimu wakati wa kufundisha somo aliloliandaa kwa wanafunzi wake. Walimu wanapaswa kuamua kwa kuchagua kwa makini njia na mbinu bora za kufundishia ili wanafunzi wake waweze kujifunza kwa ufanisi. Ziko njia nyingi za kutengeneza mazingira ya mtoto aweze kujifunza na pia ziko mbinu nyingi za kufundishia. Pamoja na wingi huo tunaweza kuzigawa katika makundi makuu mawili kadri ya jinsi zinavyowashirikisha watoto katika tendo la kujifunza, ambazo tunaweza kuziita shirikishi na zisizo shirikishi.
Zifuatazo ni baadhi ya mbinu shirikishi na zisizo shirikishi za kufundishia pamoja na faida na hasara zake:-
Njia ya majadiliano, njia hii imekuwa ikitumika katika ufundishaji kwa muda mrefu. Katika kujadiliana mwanafunzi mmoja mmoja hupata nafasi ya mawazo aliyonayo kuhusu suala linalojadiliwa na yeye pia huweza kupata mawazo yaw engine. Katika majadiliano mwanafunzi hupata ujuzi mpya nje na ule aliokuwa nao kabla hajashiriki katika majadiliano.
Mambo ya kuzingatia.
  • Kazi iwe na changamoto ya kutosha kuhitaji majadiliano ili wahusika wafikie uamuzi wa pamoja.

  • Kazi ilenge wahusika kutoa mawazo na hatimae kupata ujuzi mpya kutokana na majadiliano.

  • Yawepo malengo yanayoeleweka  vizuri na yanayotekelezeka. Ni muhimu malengo haya yawekwe wazi kwa wahusika.
Faida za mbinu.
Ø  Kukuza mahusiano ya wahusika.
Ø  Kuwafanya wahusika wafurahie na kulipenda somo.
Ø  Kukuza stadi za ubunifu na mawasiliano.
Ø  Kujenga uwezo wa wahusika wa kuamini na kuvumiliana.
Ø  Huleta ujuzi na uongozi.
Ø  Kila mmoja huweza kutoa mchango wake na mawazo yake kwani watu ni wachache katika kundi.
Ø  Husaidia kujenga kumbukumbu kwa wanafunzi.
Hasara za mbinu hii.
Ø  Kama hakuna usimamizi na utaratibu mzuri njia hii inaweza isiwe tofauti na mhadhara kwani mtu mmoja tu au kiongozi anaweza kutawala uwanja wa mazungumzo.
Ø  Kama kiongozi si imara, kundi linaweza kushindwa kujadili mada waliopewa na hivyo kujadili nje ya mada.
Ø  Hujenga uhasama kati ya kundi na kundi, wanafunzi na wanafunzi.
Njia ya mhadhara, hii ni njia ya kufundishia kitu kwa kutumia hotuba ndefu. Lengo la kutumia njia hii ni kuwazoeza wanafunzi kuwa wasikivu na kuzingatia mambo muhimu na yenye msingi tu kati ya maelezo mengi yanayotolewa na mhadhiri.
Mambo ya kuzingatia katika mbinu hii.
  • Njia hii itumike kwa wanafunzi waliopevuka kimawazo.

  • Njia hii itumike katika kuanzisha mada mpya ikiwa tu itaonekana haipo njia nyingine ya kufundishia mada hiyo.
Faida za mbinu hii.
Ø  Huwezesha kufundisha mambo mengi kwa wakati mmoja.
Ø  Humjengea mwanafunzi tabia ya kuchambua taarifa na kuzingatia mambo muhimu tu.
Ø  Inapima usikivu wa mwanafunzi kuhusu mada inayofundishwa.
Hasara za mbinu hii
Ø  Haiwashirikishi sana wanafunzi katika tendo la kujifunza.
Ø  Huwachosha wanafunzi kwa sababu watoto hawawezi kuwa wasikivu kwa muda mrefu.
Ø  Wanafunzi huchoka kusikia sauti ya mtu mmoja tu muda wote.
Ø  Ni mtu mmoja tu anayetoa mawazo yake na wengine yaani wanafunzi hupokea tu, hivyo hujenga utegemezi kwa wanafunzi.
Kazi mradi, wanafunzi na walimu wengi wameelekea kuamini kuwa mbinu ya kazi mradi ni ya utendaji wa mda mrefu. Kwa wengi kazi mradi inatumika tu kwa kuwatathimini wanafunzi kwa muda huo mrefu. Kwa mtazamo wa sasa kazi mradi yaweza kufanyika hata kwa kipindi kimoja tu cha darasani. Katika utendaji wanafunzi huunda maana zao binafsi kutokana na jinsi nadharia husika zinavyojitokeza katika maisha halisi ya kila siku.
Mambo ya kuzingatia katika mbinu hii.
  • Mwalimu lazima abainishe kuwa anatumia njia hii katika hatua gani ya mada husika na kuna umuhimu gani wa kutumia njia hii na isiwe nyingine.

  • Wanafunzi wapewe fursa ya kuchagua mambo ya kufanya katika kazi mradi wakishirikiana na mwalimu.

  • Wanafunzi wanatakiwa wajue nini cha kufanya na utendaji wao unatakiwa uwe wa kiwango gani na kwa muda gani.

  • Mwalimu wasaidie wanafunzi katika kuunganisha taarifa na kuzijazia maana.
Faida za mbinu hii.
Ø  Kukuza stadi mbalimbali za kufikiri.
Ø  Kujenga tabia ya kuhusisha mambo wanayojifunza na maisha yao ya kila siku.
Ø  Kujiamini na kupenda kujifunza kwa kujitegemea.
Hasara ya mbinu hii.
Ø  Ni vigumu kuchagua mada ifaayo kufundisha kwa njia hii.
Ø  Kama haikuandaliwa vizuri maarifa au ujenzi wa maana uliokusudiwa hushindwa kuwafikia walengwa.
Njia ya ziara, hii ni safari inayopangwa kwa madhumuni fulani. Hii ni dhiara ya kielimu ambayo hufanywa kwa njia ya kutembelea na kuona mahali ua vitu halisi kwa njia ya kujifunza. Katika mazingira ya kishule waalimu hufanya ziara na wanafunzi wao kutembelea sehemu mbalimbali zenye mambo yanayohusiana na mada wanazofundisha shuleni. Wanafunzi wanaweza kutembelea sehemu kama vyanzo vya mito, madimbwi, viwanda, benki, posta na mbuga za wanyama.
Mambo ya kuzingatia katika mbinu hii.
  • Mwalimu afanye uchunguzi wa kina kuhusu sehemu ya kufanyia ziara kuona kama ina jambo linalokusudiwa kufundishwa.

  • Yawekwe malengo ya ziara hiyo wazi kwa kila mmoja.

  • Kuamua iwapo watafanya kazi kwa vikundi au mmoja mmoja na mwalimu agawe majukumu kwa kila mmoja au kila kundi.

  • Mwongozo au maswali ya kusaidia kupata taarifa zinazotakiwa zitolewe mapema kwa wanafunzi ili uwasaidie wakati wa ziara.

  • Vifaa na jinsi ya kukusanya taarifa wakati wa ziara. Vifaa kama daftari, kamera na vinasa sauti vinaweza kutayarishwa.
Faida za mbinu hii.
Ø  Humpa mwanafunzi nafasi ya kuwa katika mazingira halisi wakati wa kujifunza.
Ø  Hufanya dhana dhahania kueleweka kwa kina zaidi.
Ø  Huongeza motisha na kumuwezesha mwanafunzi kupenda kujifunza zaidi.
Ø  Huondoa utata unaoweza kuwepo kutokana na mawazo ya awali ya wanafunzi na kuwafanya wajenge dhana kamilifu zaidi.
Ø  Hushirikisha wanafunzi wote.
Ø  Wanafunzi hutegemea katika kupata taarifa inayotakiwa badala ya kumtegemea mwalimu.
Hasara ya mbinu hii.
Ø  Gharama huwa kubwa – usafiri.
Ø  Matayarisho huchukua muda mrefu.
Ø  Usimamizi huwa mgumu hasa kama darasa lina wanafunzi wengi na mahali pa ziara ni mbali.
Ø  Sio rahisi kuendesha somo kwa kipindi kimoja tu.
Onyesho mbinu, ni uwasilishaji unaofanywa wa matendo kuhusu jambo au dhana fulani. Onesho mbinu huambatana na maelezo ya ana kwa ana, Matumizi ya zana na maswali na majibu ambayo huwezesha wanafunzi kujifunza stadi mpya.
Mambo ya kuzingatia katika mbinu hii.
  • Andaa dhana mahususi za somo au mada.

  • Andaa vifaa vyote vinavyotakiwa katika onyesho.

  • Fanya zoezi la onyesho lako kabla ili kuona kuwa onyesho lako linafanikiwa.

  • Waeleze hatua zitakazo fuata katika onyesho.

  • Washirikishe wanafunzi wako kila mara na kila hatua inayofanywa.

  • Toa nafasi kwa wanafunzi kufanya onesho wenyewe.

  • Toa muhtasari wa maelezo kuhusu dhana uliojifunza mala baada ya onesho.
Faida za mbinu hii.
Ø  Kujifunza kwa kuona kuna mahamasisho makubwa katika kujifunza.
Ø  Kujenga ari ya kujifunza.
Ø  Wanafunzi hujifunza kwa kutenda chini ya kiongozi au mtaalamu.
Ø  Njia hii huwezesha kufanya masahihisho ya moja kwa moja katika kujifunza.
Hasara za mbinu hii.
Ø  Maandalizi makini hutakiwa na muda mwingi wa vitendo hutakiwa.
Ø  Hairuhusu idadi kubwa ya wanafunzi.
Ø  Maandalizi mabaya yanaweza kupotosha maana ya onesho.
Kwa kuhitimisha, inaweza kusemwa kuwa mbinu au njia za kufundishia na kujifunzia ni ujanja anoubuni mwalimu kila awapo darasani, kwa lengo la kurahisisha uelewekaji wa somo husika katika tendo la ufundishaji na ujifunzaji. Hivyo basi kila suala au jambo analolifanya mwalimu wakati wa somo darasani huweza kusemwa kuwa ni mbinu au njia ya kufundishia na kujifunzia.
                                                            MAREJELEO
Ø  Mgombele J.Mwiga (2003). Mbinu za kufundishia na kujifunza: mwandiga bookshop.
Ø  Jiandae.wordpress.com/zana za kufundishia.
Ø  Paulmeela.wordpress.com/mbinu za kufundishia Kiswahili.

Print this item

  TOFAUTI YA LUGHA NA LAHAJA
Posted by: MwlMaeda - 06-21-2021, 07:16 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

Tofauti baina ya lugha na lahaja ni jambo ambalo watu wengi huliona rahisi. Ukimuuliza mtu ambaye anaijua lugha ya Kiswahili akuambie lahaja ni nini pengine atasema kuwa ni aina moja tu kati ya aina nyingi za Kiswahili. Baada ya hapo atakutolea mfano kama vile kimvita (Kiswahili cha Mombasa) kiamu (Kiswahili cha Lamu), kiunguja (Kiswahili cha mjini Zanzibar), kingazija (Kiswahili cha kisiwa cha Ngazija) kimwiini (kiswahilli cha kusini mwa Somallia), kingwana (Kiswahili cha mashariki mwa Zaire) n.k. Je mtu huyu amekwambia lahaja ni nini?

Kusema kweli jibu lililoko hapa juu la tosha kwa mtu wa kawaida lakini lina upungufu kiasi hasa tunapoangalia ulimwengu wote kwa jumla. Katika baadhi ya nchi tutaona kuwa watu ambao hawafahamiani moja kwa moja waweza kujiita watu wa jamii moja na yenye lugha moja. Baadhi ya mifano inayotolewa ni Uchina. Ingawa wachina wengi hujiona kama watu wanozumgumza lugha moja baadhi yao hawawezi kuelewanana kwa kutumia lugha ya mazungumzo. Kwa sababu hii wao hutumia maandishi badala ya kuzungumza moja kwa moja.
Kwa upande mwingine tunayo mifano ya watu ambo hujiona na kudai kuwa wao ni tofauti na wenye lugha tofauti lakini ambao lugha zao huelewana moja kwa moja bila huduma za mkalimani. Katika nchi hii tunayo mifano kama ya Wakikuyu, Waembu, Wambeere, Watharaka na Waweru. Wengi wa watu hawa huzungumza kwa kutumia kila mtu lugha yake. Ukiwakuta wakikuyu na waembu wakizungumza utaona kuwa wanaelewana moja kwa moja, pia Muembu na Mtharaka au Mmeru huwasiliana kwa kutumia kila mtu lugha yake. Kila mmoja wa watu hawa husema “mimi sisemi lugha ya fulani.” Hali hii pia hutokea baina ya Wakikuyu na Wakamba. Wengi wao waweza kuzungumza bila kutumia Kiswahili au kiingereza. Je tukilinganisha hali hii na ile ya Uchina tutasemaje?
Kwa kawaida neno lahaja humaanisha aina moja tu ya lugha katika eneo kubwa ambapo watu hujiona na kukubali kuwa wanazungumza lugha moja. Lahaja yaweza kuwa ya kijiografia, yaani inataumiwa katika eneo fulani tu la nchi, au ya kitabaka, yaani iwe inatumiwa na watu wa tabaka fulani tu.
Mtu anayeongea lugha nyingi k.m Kiswahili, Kikamba, Kiingereza n,k hasemwi kuwa ana lahaja nyingi. Huyu ni mtu mwenye ujuzi wa lugha nyingi; lakini mtu ambaye aweza kuzitumia lahaja tofauti za lugha moja hasemwi kuwa ana lugha nyingi k.m mtu ambaye anajua na aweza kuzungumza Kimvita, Kiamu, Kimrima, Kiunguja, Kingwana, Kingazija anao ujuzi mwingi wa Kiswahili.
Tuliyoyasema hapo juu yana maana kuwa neno lahaja si neno rahisi kulielewa. Ikiwa wachina ambao hawaelewani moja kwa moja hujiona kama watu wa lugha moja, na ikiwa watu wanaozungumza lugha ambazo zaelewana moja kwa moja wanaweza kusema kuwa wao huwazungumzi lahaja za lugha moja tu wataelewaje maana ya lahaja?
Lahaja yaweza kueleweka kwa kutumia mbinu za kisimu wala sio madai ya wazungumzaji. Ikiwa lugha mbili zinaelewana moja kwa moja lakini tofauti zinajitokeza katika matamshi au baadhi ya maneno yanayotumiwa Wanaisimu wataziita ‘lugha’ hizo lahaja za lugha moja.
Tukiachanan na mahali penye ubishi itakuwa rahisi kusema kuwa lahaja ni aina ya lugha inayotumiwa na baadhi ya watu katika nchi au eneo la wazungumzaji wa lugha moja. Mara nyingi lahaja hutumiwa katika eneo fulani tofauti tofauti za nchi, ikiwa kila eneo lina lahaja yake hizo ndizo lahaja za lugha hiyo.
Lugha sanifu pia ni mojawapo wa lahaja za lugha. Kwa mfano kiingereza sanifu cha Uingereza na pia kile cha Marekani ni lahaja mbili za Kiingereza. Zaidi ya lahaja hizi mbili kunazo lahaja nyingine za Kiingereza ambazo hupatikana nchini Uingereza, Marekani, Canada, Afrika, Australia, Asia, n.k. Kiswahili pia kinazo lahaja nyingi ambazo zimesambaa nchini Somalia, Kenya, Comoro, Tanzania, Zaire, n.k. Pia Kiswahili sanifu ni moja kati ya lahaja za Kiswahili. Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya tofauti kati ya lahaja za Kiswahili.
[Image: pg15-kitukuu.gif]
Shingazidja (Comoro)
[Image: pg15-shingazija.gif]
Shingazidja (Comoro)
[Image: pg16-coromo_shingazija.gif]
Kivumba
[Image: pg17_kivumbi.gif]
Pengine umegundua kuwa tofauti kati ya lahaja mara nyingi huwa za kifonolojia. Ifuatayo ni baadhi ya mifano kutoka kivumba.
n.k[Image: pg17-mabadiliko.gif]
Tofauti za kimofolojia pia hujitokeza. Mifano ifuatayo yatoka katika kivumba.
[Image: pg17-kivumba_kisanifu.gif]
Mifano tuliyoitoa huoyesha tofauti za kimofolojia k.m tunaona kuwa badala ya –ta– kivumba kina –cha-; tutalala ya kisanifu huwa ruchayaa. Pia katika kukanusha Kiswahili sanifu hutumiwa ha au hu pamoja na ku k.m. hakula au hukula lakini kivimba hutumiwa k’u au k’a pamoja na li k.m. k’ulinipa, k’alimpa badala ya hukunipa na hakunipa.
Kutokana na mifano hii tunaona kuwa tofauti baina ya lahaja mara nyingi hutokea katika fonolojia na mofolojia. Haya ndiyo mambo ambayo huwatambulisha wazumgumzaji wa lahaja fulani. Hata hivyo watu wenye lugha sanifu huwasiliana kwa kutumia lahaja moja katika nchi au eneo lote. Hii ndiyo hali ulivyo katika Afrika ya Mashariki ambapo sote hutumiwa Kiswahili Sanifu katika mawasiliano baina ya wazungumzaji wa lahaja mbali mbali.
Katika kumalizia kijisehemu hiki ni muhimu kutaja kuwa lugha zote huwa na tofauti za kilahaja. Hapa nchini Kenya tunazo lugha nyingi ambazo zina lahaja tofauti tofauti k.m Kiluyia, Kijaluo, Kikalenjini, Kikuyu, Kimeru, Kikamba, Kisomali n.k. Kila mojawapo ya lahaja za lugha huwa na uhumimu wake katika mawasiliano. Pia lahaja hizo ndizo ambazo huchangia maendeleo ya lugha sanifu.

Print this item

  MAANA YA KATEGORIA KATIKA SINTAKSIA
Posted by: MwlMaeda - 06-21-2021, 07:11 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

Dhana ya kategoria imejadiliwa kwa namna tofauti tofauti. Khamis na Kiango (2002) wameigawa kategoria katika mitazamo miwili wanamapokeo na wanausasa. Ambapo wanamapokeo walitumia dhana ya kategoria kumaanisha sifa bainifu zinazoambikwa kwenye aina za maneno kama vile nafsi, idadi, njeo, dhamira, na ngeli. Wakati wanausasa wanaona kuwa kategoria ni zile aina za maneno kama vile Nomino (N), vivumishi (V), vielezi (E), viunganishi (U), vitenzi (T), viwakilishi (W), na Kihusishi (H).

Massamba (2009) anaeleza kuwa kategoria ni jumla ya maumbo, faridi au vipashio vingine ambavyo huchangia sifa fulani au ambavyo viko katika kiwango kimoja.
Samwel (2) anaeleza kategoria kwa mtazamo wa kisarufi mamboleo kuwa ni darajia mbalimbali katika uundaji wa tungo. Anaendelea kueleza kuwa kuna kategoria za darajia mbili ambazo ni kategoria ya neno (kileksika) na kategoria ya virai. Ambapo kategoria ya kileksika huhusika na aina mbalimbali za maneno kama vile nomino, vivumishi, viwakilishi, vielezi, vitenzi, viunganishi, vihusishi na vibainishi. Naye O’Grady (1996) katika kufafanua kategoria za kileksika anaona kuwa ni kategoria za kiwango cha neno mojamoja na anataja aina nne za maneno ambazo ni nomino, kivumishi, kitenzi na kielezi. Darajia ya pili ni kategoria ya virai Samwel (keshatajwa) anaeleza kuwa hii ni kategoria inayofuata katika ile ya neno. Hivyo anaeleza kuwa kategoria ya virai imeundwa na kirai nomino (KN), kirai kivumishi (KV), kirai kitenzi (KT), kirai kihusishi (KH) na kirai kielezi (KE).
Kwa ujumla kwa kurejelea mtazamo wa sarufi mamboleo kategoria ni jamii au makundi yanayofanya kazi kwa kufanana na yenye sifa zinazofanana.Wesana-Chomi (2003) anaeleza kuwa dhana ya kategoria za maneno ni muhimu sana katika sarufi kwani maelezo ya sarufi ya lugha hayana budi kurejea kategoria za maneno kwa namna moja au nyingine. Hivyo zifatazo ni hoja zinazofafanua faida ya kuwa na kategoria.
Husaidia katika utungaji wa sentensi, O’Grady (1996) anaeleza kuwa neno fulani liko katika kategoria fulani kutokana na linavyofasiliwa, mfano nomino hutaja vitu, vitenzi ni maneno yanayotaja vitendo, vivumishi ni maneno yanayotaja sifa za nomino na vielezi ni maneno ambayo hueleza namna tendo linavyofanyika. Hivyo kutokana na maelezo ya O’Grady (keshatajwa) ni wazi kuwa mwanagenzi anapotaka kutunga sentensi ni lazima ajue kategoria za maneno kwani hawezi kutunga sentensi pasipo kuhusisha kategoria za manneno.  Hivyo kategoria husaidia katika utungaji wa tungo mbalimbali katika lugha husika. Kwa mfano;
                                            Wanafunzi wanasoma
                                                 N                    T
                                              Mtoto anacheza mpira
                                                 N            T            N
                                       Baba analima na mama anafua nguo
                                          N        T       U      N         T        N
Hivyo mifano ya juu inaonesha namna kategoria za maneno zilivyotumika katika kuunda ama kutunga sentensi mbalimbali.
Husaidia kujua miundo ya sentensi katika lugha, Obuchi na Mukhwana (2015) wanaeleza kuwa kategoria za maneno hufahamisha kwamba muundo wa sentensi huelezwa kwa kutaja kategoria za maneno yanayounda sentensi hiyo. Hivyo kategoria za maneno husaidia kujua miundo mbalimbali ya sentensi kwani kuna sentensi zenye muundo wa (N + T) yaani Nomino na kitenzi, kuna sentensi zenye muundo wa nomino + kivumishi + kitenzi + kielezi (N + V+ T+E), sentensi zenye muundo wa nomino + kitenzi + kielezi (N + T+E). kama inavyojidhihirisha katika mifano inayofuata;
Muundo wa (N + T + E)
                                    Mama ameenda sokoni
                                      N            T            E
Muundo wa (N + V + T +E)
                                  Msichana  mzuri ameenda shuleni
                                           N         V          T            E
Hivyo mifano tajwa hapo juu dhahiri inaonesha namna kategoria mbalimbali za maneno zilivyotumika katika kuonyesha miundo ya sentensi.
 Kategoria husaidia kujua aina za maneno katika lugha husika na dhima zake katika tungo, Wesana-Chomi (2003) anaeleza kuwa maneno ya lugha hufanya kazi mbalimbali katika tungo. Mfano kuna maneno yanayofanya kazi kuonesha nani katenda tendo, nani katendewa tendo au nani katendwa tendo. Maneno yenye kazi hizo katika tungo huitwa nomino. Pia, maneno mengine hutoa taarifa juu ya nomino na maneno hayo ni kivumishi. Aidha, maneno mengine hutaja tendo au jambo lifanywalo na mtenda tendo na maneno hayo huitwa vitenzi. Kwa mfano;
                                                Mwalimu anafundisha
                                                      N
                                                      Mtoto mzuri
                                                                       V
Hivyo katika mifano hii neno Mwalimu ambalo ni nomino limesimama kama mtenda wa jambo na katika mfano wa pili neno mzuri limesimama kama kivumishi ambacho kinatoa sifa juu ya nomino. Hivyo kategoria husaidia kujua aina za maneno.
Husidia kujua aina mbalimbali za virai pamoja na miundo yake, Massamba na wenzake (2012) wanaeleza kuwa miundo ya virai hukitwa katika aina za maneno ambazo ndizo chimbuko la mahusiano maalumu ndani ya vipashio hivi. Mfano wa virai hivyo ni KN, KV, KE, KT na KU. O’Grady (1996) anaeleza kuwa
Husaidia na kutuwezesha kutunga sentensi zisizokikomo na zinazoeleweka. Sentensi zisizokikomo ni sentensi ambazo ni ndefu na zisizo na mwisho, kwa mfano;
Baba na mama walipanda mlima Kilimanjaro ambao mlima huo upo mpakani mwa Kenya na Tanzania ambapo
Mama alimnunulia mtoto zawadi iliyokuwa ikiuzwa sokoni kariakoo karibu na mtaa wa mama lishe uliopakana na mtaa wa kongo pembezoni mwa  maduka ya vitambaa vya kihindi vinavyouzwa na wahindi kutoka India ambao walikuja Tanzania kufanya biashara zinazowaingizia kipato kikubwa kiasi cha kuweza kumudu na kukidhi mahitaji ya familia yao.
Husaidia katika uchanganuzi wa sentensi za lugha husika, katika kuchangua sentensi za lugha kategoria za maneno hutumika kwani huwezi changanua sentensi pasipo kuhusisha kategoria za maneno kwa mfano;
Baba analima
  N           T
                                                                S.S
                                                  KN                           KT
                                                   N                                 T
                                                   Baba                       analima
Husaidia kuunda nadharia mbalimbali za sintakisia, kutokana na uchambuzi wakategoria za kisintakisia kumepatikana nadharia mbalimbali kama vile sarufi miundo virai na sarufi geuza maumbo zalishi.
Husaidia kupata sarufi inayojitosheleza kwa usahihi katika lugha, lengo la uchambuzi wa kisintakisia ni kutafta ukubalifu au usioukubalifu wa tungo zisizo sahihi.

MAREJELEO
Besha, R.sM (2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
Massamba, D na Wenzake. (1999) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu,Sekondari na vyuo. Dar es  Salaam: TUKI.

Print this item

  OTHOGRAFIA KATIKA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 06-21-2021, 07:08 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

Katika utangulizi wa kitabu ‘A Handbook of the Swahili Language’, Askofu Edward Steere alijadili suala la tahajia au hati za maandishi ya Kiswahili kwa undani.
Karibu maandishi yote ya Kiswahili kabla ya wakati wake yalikuwa yameandikwa kwa hati za Kiarabu. Mengi kati ya maandishi hayo yalikuwa ni tenzi na mashairi ya kidini na mambo ya kawaida yaliyoandikwa kwa lahaja ya kishairi ya Kaskazini, ambayo Steere alishuku iwapo ilieleweka na watu wengi.
Ingawa Kiswahili cha wakati wake kilikuwa kikitumiwa katika kuandikiana barua, Steere anasema kwamba barua kama hizo zilianzia na salamu kwa Kiarabu na pia maneno na vifungu vya maneno ya Kiarabu.
Tathmini ya Steere
Stere alitambua kwamba hati za Kiarabu hazifai kuandikia Kiswahili kwa sababu lugha ya Kiswahili inazo irabu tano ikilinganishwa na irabu tatu za Kiarabu. Kuhusu konsonanti, hati za Kiarabu zina upungufu wa konsnanti za ‘g’, ‘p’, na ‘v’. Steere aliandika hivi:
“Kwa hivyo, Waswahili wanalazimika kuandika ‘ba’, ‘f’ au ‘p’ wakikusudia kuandika ‘mb’ au ‘b’; wanaandika ‘’ghai’ badala ya ‘g’, ‘ng’, ‘ng’, ‘fa’ badala ya ‘v’, ‘mv’ na ‘f’, ‘ya’ badala ‘ny’ na ‘y; ‘shin’ badala ya ‘ch’ na ‘sh ; pia wanaiacha ‘n’ inapozitanguia d, j,y na z.”(Steereb 1870:5).
Kwa hivyo, ni wazi kwamba hati za Kiarabu hazifai na hazitoshelezi maandishi ya Kiswahili kwa sababu ya kutatanisha. Ili kuonyesha matatizo ya hati hizi, Steere anaandika hivi:
“Nilipokuwa Zanzibar, kulikuwa na barua iliyotoka Kilwa kuhusu vita. Barua ilitaja kwamba mtu mmoja kati ya wale waliopigana alikuwa amekufa au amevuka na hakuna aliyeweza kusema kile kilchokuwa kimetendeka. Konsonanti mbili za mwisho zilikuwa ‘fa’ na ‘gaf’ zikiwa na vitone vitatu juu yake. Ikiwa vitone viwili vilikuwa vya herufi ya kwanza, mtu huyo alikuwa amekufa. Ikiwa vitone viwili vilikuwa vya herufi ya pili, alikuwa hai, lakini vitone hivyo vilikuwa katikati hivi kwamba hakuna aliyeweza kuvigawanya. Iwapo Kiarabu kingekuwa na herufi ‘v’, ingekuwa wazi (Steere 1870:6).
Hati za Kiarabu
Zikilinganishwa na hati za Kiarabu, hati za Kirumi hazileti matatizo yoyote katika kuandika Kiswahili. Sababu yake ni kwamba wasomi wengi wa Kiswahili waliokuja baada ya Krapf na Steere waliamua kutumia hati za Kirumi walizokuwa wamezizoea baada ya hati za Kiarabu zilizokuwa zikitumika kuandika Kiswahili.
Mara nyingi, maneno na mizani katika Kiarabu huishia kwa konsonanti. Hili pia ni jambo lingine linalozifanya haati za Kiarabu zisifae katika kukiandika Kiswahili.
Dhehebu la UMCA lilichapisha vitabu kwa kufuata mtindo uliotumiwa kuchapisha vitabu vya Steere. Wamisheni wa Kizungu walifanana na waanzilishi wa uchunguzi wa Kiswahili kwa kuwa ilikuwa rahisi kwao kutumia hati za Kirumi badala ya zile za Kiarabu.
Mkutano wa Dar es Salaam wa mwaka 1925 uliamua kutozitumia hati za Kiarabu pamoja na konsonanti za Kiarabu kama vile ‘kh’.
Uamuzi huu wa mwaka 1925 uliwakasirisha wengi, ikiwa ni pamoja na gazeti la Mombasa, Al-Isiah, kama tutakavyojadili.
Profesa Carl Meinhof alipohudhuria mkutano wa Mombasa wa mwaka 1928, waliohudhuria walikuwa na nafasi ya kushauriana naye kuhusu othografia ya Kiswahili. Meinhof alipendekeza ‘c’ itumiwe badala ya ‘ch’.
Badala ya kutumia alama tatu za maandishi (ng) kusimamia sauti moja, alipendekeza kuwa ‘n’ yenye mkia itumiwe kama ilivyo katika maandishi ya kifonetiki.
Lakini mashauri haya ya Meinhof hayakukubaliwa. Wasomi wa Kiswahili wakati huo walijiona kuwa sahihi, na kwamba mapendekezo ya Meinhof yalifaa tu katika maandishi ya kifonetiki katika isimu lakini hayakufaa katka othografia ya kawaida ya Kiswahili.
Katika majadiliano yao, waliona kwamba ingekuwanvigumu kupiga taipu ‘n’ yenye mkia. Tatizo hili lingetatuliwa hapo mwanzoni kwa kupiga taipu herufi ‘j’ juu ya ‘n’ wakingojea kurekebisha kwa mashine na kwa hivyon tatizo la kuandika sauti ya kwanza ya neno ‘ng’ombe’ kwa sauti mbili na alama (ng’) lingali linaendelea.
Upungufu mwingine wa othografia ya Kiswahili unaoweza kutajwa hapa ni kule kukosa kutofautisha konsonanti za kipua (nazali) ambazo ni mizani ‘m’ na ‘n’ za kwanza katika maneno ‘mmea’ na ‘nne.’
Na:
akamau@ke.nationmedia.com

Print this item

  VITENZI VYA KISWAHILI SANIFU
Posted by: MwlMaeda - 06-21-2021, 07:02 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - Replies (1)

Aina hii ya neno huweza kufafanuliwa kwa kutumia vigezo mbalimbali vya kiisimu ambavyo ni; kisemantiki, kimofolojia na kisintaksia. Hata hivyo maana inayotokana na semantiki ndiyo huegemewa zaidi. Tazama hapo chini namna ya kufasili kitenzi kwa kutumia vigezo mbalimbali.
Kisemantiki, kitenzi ni aina ya neno inayotaja tendo au hali ya kuwa. Kwa mfano;

  1. Juma analima.
  2. mama anapika.
  3. Suzana yu mgonjwa.
  4. John alikuwa mzembe
Kimofolojia, kitenzi ni aina ya neno iliyojengwa na mzizi tenzi pamoja na viambishi. Kwa mfano; Lim – a, ku – l – a, imb – a, som – a.
Kisintaksia, kitenzi ni aina ya neno ambayo hupokea nomino au kiwakilishi mwanzoni na hupokea nomino au kiwakilishi au kielezi mwishoni. Kwa mfano, neno lililoandikwa kwa herufi mlalo ni kitenzi; 1. Musa analima. 2. Justina anatembea polepole. 3. Wewe ni mwanafunzi bora. 4. Tanzania imepata rais.
AINA ZA VITENZI
Kisemantiki, kuna aina tatu za vitenzi. Aina hizo ni; kitenzi kikuu, kitenzi kisaidizi na kitenzi kishirikishi.
Kitenzi Kikuu
Ni aina ya kitenzi ambacho humiliki uhusiano baina ya vipashio arifu katika tungo au sentensi. Hii ni sehemu muhimu ya sentensi kwani bila kitenzi kikuu sentensi haikamiliki. Pamoja na kuwa sentensi zote si lazima zikamilishwe na kitenzi kikuu, lakini kitenzi hiki ndicho kinachobeba taarifa nyingi zaidi. Tazama mifano ifuatayo, neno lilioandikwa kwa herufi mlazo ni kitenzi kikuu. 1. Mama anafua nguo za watoto.
  1. Daftari langu limechanika.
  2. Wasomi hufanya utafiti.
  3. Amenipotea.
  4. Ngamizi imezima.
Kitenzi Kisaidizi
Ni kitenzi ambacho uamilifu wake ni kukisaidia kitenzi kikuu kukamilisha uarifu wake. Hii ina maana kuwa vitenzi visaidizi haviwezi kusimama peke yake bila kuwa na kitenzi kikuu. Vitenzi hivi hutoa taarifa ya ziada kuhusu tendo. Vivyo hivyo, vitenzi hivi vikiondolewa katika sentensi haviathiri maana ya sentensi. Tazama mifano ifuatayo, neno lililoandikwa kwa herufi mlazo ni kitenzi kisaidizi.
  1. Pili alikuwa anataka kula.
  2. Mazoea alitaka kwenda shambani.
  3. Bibi hahitaji kuhifadhi mazao.
Kitenzi Kishirikishi
Hiki ni kitenzi ambacho huonesha zaidi hali ya kuwa. Pamoja na hilo, kitenzi hiki huonesha uhusiano uliopo baina ya nomino au kiwakilishi kinachotajwa na tabia au hali inayozungumzwa. Vitenzi vishirikishi vyote lazima viwe na pande mbili. Upande wa nomino au kiwakilishi na upande wa sifa au hali. Tofauti na vitenzi vikuu, vitenzi hivi haviwezi kusimama pekee na kutoa maana. Tazama mifano ifuatayo, neno lililoandikwa kwa herufi mlazo ni kitenzi kishirikishi.
  1. Maeda ni mwalimu.
  2. Yeye si mtoto mdogo.
  3. Ashura ni mgonjwa.
  4. Huyu ndiye mkorofi
  5. Hapa ndipo penyewe.
  6. Baba alikuwa mpole
Tabia za Vitenzi vya Kiswahili Sanifu
  1. Kitenzi ni sehemu kuu ya sentensi. i.e Sentensi haiwezi kukamilika bila kuwa na kitenzi.
  2. Kitenzi hupokea viambishi vya; nafsi, wingi-umoja, njeo, urejeshi, ukanushi, uyakinishi, kauli mbalimbali na viambishi vya hali.
  3. Kitenzi kinaweza kupokea nomino mwishoni au kisipokee (elekezi na sielekezi).
  4. Kitenzi huonesha tendo.
  5. Kitenzi huonesha hali ya kuwa.
  6. Huweza kuonesha upatanishi wa kisarufi.
  7. Kitenzi huweza kunyumbulishwa.
  8. Kitenzi huweza kuwa na alomofu mbalimbali za mofu moja.
Dhana Mbalimbali za Kitenzi
  1. Kitenzi Jina: Hiki ni kitenzi ambacho huchukua hadhi ya nomino.
  2. Kitenzi Elekezi: Hiki ni kitenzi ambacho uamilifu wake hulazimisha kupokea nomino mwishoni.
  3. Kitenzi Sielekezi: Hiki ni kitenzi ambacho uamilifu wake si lazima kuwepo na nomino mwishoni.
  4. Kitenzi cha Msingi: Hiki ni kitenzi kilichojengwa na mzizi tenzi na kiambishi tamati maana.
  5. Kitenzi cha Myumbuliko: Hiki ni kitenzi kilifanyiwa mchakato wa unyumbulishaji.

Print this item

  SWALI: TOFAUTISHA NADHARIA YA UMUUNDO NA UMUUNDO MPYA
Posted by: MwlMaeda - 06-20-2021, 11:27 PM - Forum: Maswali na majibu - No Replies

UTANGULIZI
Katika makala haya, nitaeleza umuundo na umuundoleo, tofauti kati ya umuundo na umuundoleo na hitimisho.
Huwezi kuzungumzia nadharia  ya umuundoleo bila ya kuhusisha umuundo. Kwa maana hiyo nadharia hizi huzungumziwa kwa pamoja
NADHARIA YA UMUUNDO
Umuundo ni nadharia inayojibainisha kwa kuangalia Ujumla wa uhusiano wa sehemu moja kwa nyingine katika kufanya kitu kizima. Kwa mfano muungano wa maneno hufanya sentensi na sentensi zikiungana zinaunda aya au onesho na onesho kuunda tamthiliya.
Ntarangwi, M (2004) anasema kuwa umuundo waweza kuelezwa kama mtizamo wa kitathimini ambao huzingatia zaidi miundo inayojenga kazi binafsi.
Katika miaka ya kwanza ya karne ya 19, mwanaisimu Ferdinard De Saussure aliyezaliwa tarehe 26 Novemba 1857 huko Geneva, Switzerland alikuwa mwanafalsafa na mwanazuoni wa Ki-swiss aliyejishughulisha sana na isimu, alipendekeza mtizamo mpya kuhusu lugha.   Aliiangalia lugha kutoka mfumo rasmi hadi mfumo wa kinadharia. Kinyume na wataalamu wengine walioshughulikia historia na sura maalum za lugha fulani, Saussure alivutiwa na miundo inayohimili lugha zote, huku akijaribu kuonyesha kwamba lugha zote za ulimwengu zaweza kutathiminiwa kwa kaida maalum za umuundo.
Alizua istilahi `parole'(utendaji) na `langue’ (lugha) kwa mujibu wa maelezo yake anasema langue ni sehemu inayowakilisha welewa wetu wa uhusiano uliopo kati ya sauti na maana . anaeleza kuwa lugha ni alama ambayo imeunganisha kati ya kitajwa na kitaja. Kwake amesema alama ni dhana pana na ina pande mbili yaani mtajo (kitu kilichotajwa) na kitajwa (dhana).
Kwa mujibu wa de Saussere ‘parole’ ‘(utendaji katika lugha) huhusu msemaji kwa ujumla katika matumizi yake au uzungumzi ni lugha katika matumizi.  Kazi hii ya Saussure ndiyo iliyozaa mkondo unaojulikana hivi sasa kama umuundo.  Muundo waweza kuelezwa kama mtizamo wa kitathimini ambao huzingatia zaidi miundo inayojenga kazi binafsi.  Hata hivyo, kazi ya Saussure ilikuwa imetengewa wanaisimu peke yao.
Katika miaka ya 1950, mtizamo huo wa Saussure ulianza kusambaa katika masomo mengine hasa wakati mawazo yake yalipozingatiwa na Mwanaanthropolojia Claude Levi-Strauss.  Kwa kuchukua maoni ya isimu ya Saussure na kuyaingiza katika sayansi ya kijamii .  Hasa alichotaka kuendeleza  dhana, kwamba pana viwango viwili katika kuelewa maisha ya jamii, isimu, lugha na chochote kingine kile.  Viwango hivi ni cha juu juu (surface) na cha ndani (deep).   Kwa ujumla twaona usomi wa kuitizama jamii kwa uwili unaokinzana (binary opposition) ambao ulisambaa katika nyanja nyingi hapo baadae.
 Awali ya hapo, anthropolijia ilizingatia makundi au makabila maalum ya watu ambayo yalizingatiwa kivyao, mifumo ambayo ilidhaniwa kwamba haibadiliki, lakini Levi-strauss alijishughulisha na mifumo inayohimili jamii zote.  Strauss alidai kwamba pana muundo maalum ambao waweza kutumia kueleza jamii zote za ulimwengu, kama vile ilivyo na somo la hisabu au la uchumi ambapo pana njia (formula) ambayo yaweza kueleza maswala mengi katika somo hilio.  Hapo ndipo dhana za umuundo zilipoingia masomo mbali mbali hasa yale ya sayansi ya jamii na fasihi.  Saussure alitoa maelezo ya nadharia changamano kuhusu lugha, na ni misingi ya nadharia zake inayotoa nguzo ya mbinu za umuundo, ( Ntarangwi, 41: 2004).
Ingawa huwa tunatumia lugha kuzungumza kuhusu maisha, Saussure hakulizingatia jambo hilo bali alisisitiza kwamba lugha ni kiungo kamili kinachojisimamia.  Kwamba ni kiungo kilicho na masharti na sheria zake.  Hivyo basi kuwepo kwa vitu duniani hakuathiri aina ya lugha iliyopo.  Isitoshe, alidhamiria kudai kwamba lugha kwa kujisimamia haibadiliki wala vipande vyake haviathiriwi na mabadiliko yoyote ya kijamii.
Katika mkabala huo, neno ni ishara huru inayoelezwa kwa kutofautishwa na nyengine.  Lugha ni mfumo wa uhusiano kati ya viungo kadhaaa vinavyoijenga; ni muundo, sio kitu.  Dhana hii yaweza kueleweka zaidi tukizingatia maneno ya Saussure ya `kionyeshi’ na `kinachoonyeshwa’.  Neno katika lugha ndilo `kionyeshi’ na dhana inayorejelewa ni neno hilo ndiyo `kinachoonyeshwa’.   Kwa mfano neno mtoto ndio kionyeshi picha ya mtoto kama kirejelewa ndio kinachoonyeshwa.
Vyote viwili haviwezi kutenganishwa, lakini umuundo hujishughulisha zaidi na uhusiano wa vionyeshi na jinsi vinavyofanya kazi kuliko kuangalia nje ya mfumo wa lugha, yaani kinachoonyeshwa.  Kwa msingi kabisa, Saussure alizingatia zaidi mpangilio wa ndani wa lugha, ule muundo wake na sio mahusiano ya vipande vyake.  Wahakiki wanooegemea mkondo wa Saussure huzingatia kwamba matini husika ni mfumo unaojisimamia na hivyo basi huwa hamna haja ya kutumia mambo ya nje ili kuhakiki kazi ya fasihi.  wahakiki huzingatia matini kama kiungo kamili kinachoweza kuhakikiwa kivyake.  Hivyo basi mhakiki wa umuundo hujaribu kuweka sarufi ya matini pamoja na sheria za jinsi matini hiyo hufanya kazi.  Mhakiki anayezingatia zaidi muundo wa lugha ya matini bila shaka hupuuza dhana ya jadi kuhusu kile matini hiyo huweza  kutueleza kuhusu maisha; na hivyo basi hufanya mtindo wa kazi yenyewe kiini cha uhakiki wake.
Kwa hivyo wahakiki wanaotumia nadharia ya umuundo hujaribu kuzingatia matini pekee huku wakiepuka kuifasiri kazi ile kulingana na kaida zilizowekwa kuhusu jinsi matini hufanya kazi.  Hata hivyo, huenda njia hii isiwe ya kufaa sana kwa sababu huwa inachukulia kwamba kila kitu kimeundwa katika mpangilio halisi usiotatanika na usiotegemea mambo mengine yaliyo nje yake.  Ama kwa hakika, hata lugha yenyewe haiwezi kabisa kufanya kazi bila kuathiriwa na mambo mengine kama vile mazingira yake
Wahakiki wa muundo walichunguza upatanishi wa sauti, kiimbo, arudhi na utunzi wa maashairi wanaamini matini ya kifasihi huwa na viwango mbalimbali. Mhakiki anachunguza vipengele hivi kwa viwango tofauti tofauti.
Mkondo huu wa mawazo ya umuundo kuhusu sayansi za jamii ulianzia ulaya na kuathiri mtazamo wa elimu mbalimbali (duniani) kama vile: Falsafa, Anthropolojia, Historia, Uhakiki wa kifasihi na Sasiolojia.
Kwa hivyo twaweza kuangalia jamii katika muundo wake wa kijuu juu na kuielewa lakini tukitaka kupata maana mwafaka lazima tuchunguze muundo wake wa ndani ambao hupatikana katika kila jamii ya wanadamu. Kwa hiyo hata katika kuielewa fasihi lazima tuifahamu lugha yake.
Katika kupata maana lazima kuwe na uhusiano wa kipembetatu yaani kuna DHANA, ALAMA na KITAJWA.
Upungufu wa nadharia hii ndiyo uliochochea kuzuka kwa Umuundo- mpya.
NADHARIA YA UMUUNDOLEO
Umuundoleo hutumiwa kuelezea mikabala ya uhakiki iliyozuka kuyapinga au kuyaendeleza mawazo yaliyokuwa kwenye umuundo.
Tunatumia neno Umuundoleo kuonyesha mtizamo wa kimuundo katika fasihi ambao ulitokea baada ya Umuundo.  Japo dhana hii haiwezi kupewa maana moja maalum, imehusishwa na maendeleo kutoka au katika kazi za Derrida (1973, 1976), Lacan (1977), Kristeva (1981, 1984, 1986), Althusser (1971) na Foucault (1978, 1979a na b, 1981, 1986).  Kazi hizi nazo zilichangiwa na kazi za Ferdinand de Saussure na Emile Benveniste (kuhusu isimu-jamii ya umuundo), kazi ya umarx hasa kupitia nadharia ya itikadi iliyoendelezwa na Louis Althusser, na kazi ya tathimini-nafsi ya Sigmund Freud na Jacques Lacan.
Kazi hizi zimetoa athari mbali mbali kwa nadharia tofauti lakini zote zinazingatia makisio sawa kuhusu lugha, maana, na ubinafsia (subjectivity). Lugha yachukuliwa kama nguzo maalum ya uainishi wa mpangilio wa jamii, maana za kijamii, nguvu na urazini wa kibinafsi.  Hii ni kwa sababu ni katika lugha ambapo maana za mpangilio wa jamii na matokeo yake ya kisiasa na kijamii hujengwa na kupingwa.
Ni kupitia lugha ambapo hisia na maana yetu ya kibinafsi (ambayo inatufasili) hujengwa.  Aidha, lugha haielezi ubinafsi wa kipekee wa mtu bali hujenga ubinafsia wa mtu kwa njia zilizojengeka katika miundo ya jamii yake.  Katika Umuundo-leo, ubinafsia sio hali yenye umoja au isiyobadilika, bali hubadilika kila mara ili kuchukuana na hali halisi ya kihistoria na kisiasa ili kudumisha nafasi ya mhusika katika jamii.
Umuundo-leo, kama nadharia nyinginezo ina makisio fulani kuhusu lugha, ubinafsia, ufahamu, na ukweli.  Nguzo zake, ambazo zatokana, kama tulivyotaja hapo juu, na mwanaisimu wa kiimuundo Ferninard de Saussure, ni kwamba lugha, badala ya kudhihirisha uhalisi wa kijamii uliopo, huwa yatujengea uhalisi huo wa kijamii.  Kwa hivyo sio uhalisi wa kijamii wala ulimwengu asilia huwa na maana zinazodhihirishwa ni lugha.  Lugha mbali mbali pamoja na matumizi mbali mbali ya lugha moja huugawa ulimwengu na kuupa maana kwa njia tofauti ambazo haziwezi kupatana ili kuunda kigezo kimoja kinachodhihirisha uhalisi wa jamii.  Kwa mfano, maana ya tajiri hutofautiana katika lugha mbali mbali na hata kati ya miundo tofauti ya lugha moja, na hutegemea matumizi na muktadha wa matumizi hayo.  Ndipo sasa hapana maana moja ya neno au fungu la maneno.
Miundo yote ya umuundo-leo huchukulia kwamba maana hujengwa katika lugha na huwa yule anayezungumza lugha hiyo hawezi kuhakikisha maana hiyo.  Kwa hivyo tofauti na maoni ya Saussure, maana huzaliwa na kuundwa kwa njia mbali mbali.
Hata hivyo nadharia hii hukubaliana na wazo lake kwamba lugha haimuliki maana; bali maana hukuzwa katika lugha na kwamba ishara hazina maana ya kivyake bali hupata maana katika mkururo wa lugha pamoja na tofauti yake na ishara nyingine.  Dhana hii ni muhimu sana kwa sababu yadhihirisha lugha kama chombo cha kijamii ambacho chapingwa na kung’ang’aniwa.
Kulingana na nadharia hii basi, neno ‘mama’ kwa mfano, huwa halina maana ya kindani inayotokana na lugha husika bali huwa na maana za kijamii zilizotokana na lugha hiyo na ambazo zinakinzana na kubadilika kulingana na mazingira na kipindi cha kihistoria.
Kwa hivyo kinyume na maoni ya wanamuundo kama vile Levi-Strauss walioshikilia kwamba maana ya kisa, kwa mfano, ipo katika matini na maana hiyo hiyo hutokea katika matini nyengine yoyote, nadharia hii yaeleza kuwa maana ya kisa ni amali ya msomaji/msikizi (hadhira) na kwamba pana fasili mbali mbali za kisa hicho kulingana na muktadha.  Hivyo basi kwa umuundoleo twaweza kueleza kuwepo kwa wingi wa maana pamoja na mabadiliko yake kwa kuona maana sio kama iliyojengwa katika ishara zisizobadilika bali kama iliyo katika viashiria (signifiers) ambapo kiashiriwa (signified) hubadilikabadilika.  Hapo ndipo alipojikita Derrida ambaye aliingiza dhana ya muktadha katika kueleza maana katika lugha na matini.  Wahakiki wanaozingatia nadharia hii basi huongozwa na dhana ya kubadilika kwa maana katika miktadha mbali mbali na hivyo basi kuwashurutisha kuzingatia muktadha wa kazi hiyo kama nguzo ya kueleza kazi hiyo. Mtaalamu huyu anazuka na dhana maarufu ya utofauti (difference), kwa maoni yake maana hutokana na mikakati au mbinu mbili muhimu, ‘tofauti’ (difference) na ‘uahirisho’ Wamitila (2002:179 )  anaiita kuwa ni tofahirisho ambalo linafumbata dhana mbili hizi.
Wanamuumo wanaangalia muktadha wa kiusemi au kimazungumzo na huweza kubadilika  kutegemea mukatadha  wa kiusemaji. Ikiwa muktadha wa kiusemi utabadilika maana nayo inabadilika.
TOFAUTI KATI YA MUUNDO NA UMUUNDOLEO
Kwanza, Nadharia ya umuundo imeeanza karne ya 19 na mawazo yake yanatokana na falsafa ya ya de Saussure na Levi Strauss, nadharia hii ya mwanzo na inalenga katika kuonesha namna mfumo wa lugha ulivyo na jinsi unavyotoa maana ya kitu na matini. Wakati  nadharia ya wanamuundoleo imeanza karne ya 20 ilijikita kwa Jacque Derrila na inalenga zaidi katika kuonesha namna maana inayopatikana. Husisitiza maana hutokana na jamii au mazingira.
Wanamuundo hawatilii mashaka uwepo wa uhalisia yaani baadhi ya vitu, binaadamu au jamii ni uongo tu ni mawazo tu, vitu vyote ambavyo viko katika mazingira havina uhalisia wowote, kwa mujibu wa nadharia hii, wandishi wa vitabu wanachokiandika katika vitabu vyao vya fasihi havina uhalisia wowote katika mazingira halisi. Wakati wanamuundoleo wao wanaona kuwepo kwa uhalisia, na dhana au mawazo ni vitu viwili tofauti, hupatikana kulingana na mazingira kila mtu na ukweli wao, wao hawachanganyi kati ya uhalisia na dhana yenyewe wanaona ni vitu tofauti.
Pia, wanamuundo wanaisitiza uhusiano wa mazingira na maana kutengenezwa, wao huangalia maana kuwa ni kitu cha kutengenezwa, yaani mazingira hutengeneza maana,wao uona ulimwengu wa nje ni wa kiurejelezi mhakiki atahakiki kwa kurejelea jamii yake, kwa mujibu wa nadharia hii katika kazi ya fasihi kuna mambo mengi ambayo mwandishi ameandika, mhakiki wa kazi ya fasihi uhakiki kwa kungalia mazingira yake na kufanya uhakiki kulingana na mazingira yake, kwa mfano katika kitabu cha kivuli kinaishi ( uk 24-25) kumezungumziwa kukithiri kwa rushwa katika jamii Giningi, watu wanatoa na kupokea rushwa, mhakiki ataitazama jamii yake kama swala la rushwa katika mazingira yake ni swala linalokwamisha maendeleo ataitafsiri maana kulingana na jamii yake ndicho anachokirejelea. Atasema kuwa rushwa hukwamisha maendeleo ya jamii yetu, mhakiki atapendekeza kuwa ili tuweze kujenga jamii mpya yenye kufuata haki na usawa hatuna budi kupiga vita rushwa, kwa mhakiki ambaye rushwa ktika jamii yake si tatizo hawezi kusema ni kikwazo cha maendeleo badala yake atazungumzia kama jamii yake inavyoichukulia lugha . Wakati kwa upande wa nadharia ya umuundoleo wao wanasema:
Mazingira na maana hazina uhusiano kwakua hutokea utata katika uumbaji wake, uwepo wa mifumo mingi husababisha utata yaani kinachoelezwa na lugha huwa hakipo kwa maana kwamba hakirejelei kitu kilicho nje yake, kwa mujibu wa nadharia hii mhakiki atahakiki kazi ya fasihi bila kuhusiasha jamii, atasoma kitabu na kuhakiki kwa mawazo yake yeye mwenyewe ili kuondoa utata katika kutoa maana,kwa mfano kwa kitabu cha kivuli kinaishi mhakiki atakiangalia bila kuangalia jamii yake.
Tofauti nyingine ni kwamba, mfumo wa mazingira hujenga fikra na kuleta maana, watu wenye mazingira sawa huchukulia vitu sawa yaani mfumo hujenga mpaka wa maana, wanamuundo huangalia mfumo wa maisha ukoje na kutoa maana ya kitu kulingana mfumo wa maisha ukoje, kwa mfano katika tamthilia ya Ngoswe – Penzi kitovu cha uzembe kilichotungwa na E. Semzaba anaelezea ndoa za mitaala katika familia ya  balozi Ngengemkeni, mhakiki au msomaji wa tamthilia hii kwa kuwa fikra yake iliyojengeka kutokana na mazingira yake atasema kuwa  ndoa za mitaala zinaathari kuwa watoto hawapati malezi bora kutokana au wanawake hawana upendo.
Wakati wanamuundoleo wanasema hakuna maana moja, kuna maana nyingi dhana moja hujenga maana nyingi yaani mfumo kuibua maana nyingi, kwa mujibu wa wanamuundo baada ya uandishi wa kitabu kila mhakiki au msomaji wa kazi ya fasihi atakuwa na maana yake katika kuichambua kazi husika ya fasihi, hakuna maana moja kwa mfano wa methali samaki mkunje angali mbichi atakae sikia methali hii anaweza kusema kuwa samaki anatakiwa kukunjwa akiwa mbichi lakini maana ya methali hii ni mtoto anatakiwa afundishwe akiwa bado mdogo pia anaweza akaja mwingine  kwa maana nyingine kulinganana na dhana husika, kwa maana kwamba lugha ina uwezo mkubwa wa kuzaa maana.
Wanamuundo wanarahisisha maana, na kuonesha vielelezo muhimu kuonesha maana moja, wao uhusisha maana ya vitu mbalimbali kuwa moja, kwa mfano ulevi na utapeli uhusisha kuwa ni uovu, uangalia uhusiano wa maana, kwa mfano katika fasihi waandishi wa vitabu tofauti tofauti wanaeleza mambo mbalimbali ambayo wahakiki au wasomaji uhusisha na kuwa ni dhamira moja, katika riwaya ya watoto wa mama ntilie iliyotungwa na Emmanuel Mbogo riwaya imezungumzia maisha ya walalahoi, katika riwaya hii mwandishi amehusisha mambo yote na umasikini na kuoana dhamira kuu ni umasikini. Wakati wanamuundoleo wao wanadai kuwa kila kitu kielezewe kwa upekee, wanafikiria kuwa tofauti walizoziondoa zina umuhimu na zinaziba mapengo, kwahiyo kuhusisha maana kwao ni kuweka mapengo kila kitu kiongelewe kwa upekee wake.
Tofauti njingine ni kwamba, wanamuundo wanaangalia ukweli ambao utamgusa kila mtu yaani kufuata muundo mmoja, kwao lugha zote zina muundo wa jumla yaani kitakachochambuliwa Zanzibar ndicho kitakacho patikana mtwara, Jamii nzima itakuwa inahusika na jambo hilo kwa mfano maswala ya ukimwi, rushwa na mapenzi.
Wanamuundoleo wao hawakuonesha ukweli wa kimajumui na kuangalia vitu ambavyo vinatutenganisha kila mmoja na muundo wake na kuaangalia kipi kinatufanya tuwe tofauti, wao huuangalia utofauti ambao upo katika jamii husika , utofauti katika mila na desturi mbalimbali za jamii ,kwa mfano jamii moja inaendeleza mila na desturi za kukeketwa mwandishi ataangali utofauti huo kwa jamii nyingine ambayo haina mila hizi.
Vilevile, Wanamuundo hutilia mkazo zaidi kwenye muundo, muundo ndio hutengeneza fikra kwa mfano katika tamthilia, riwaya na ushairi au kazi mbalimbali wanamuundo huangalia muundo wa kazi hizi, wakati wanamuundoleo wanaangalia kuwa mazingira ndio huleta mpaka, huangalia lugha kwenye mazingira ndio hutengeneza fikra zetu, binaadamu ni wabunifu mipaka huwekwa na mfumo, kwa mfano uhakiki wa kitabu cha riwaya ya kusadikika ya  Shaaban Robert ulivyofanywa kipindi cha miaka ya nyuma ni tofauti na mhakiki anayehakiki kazi ya fasihi ya mwandishi huyo kwa sasa.
Wanamuundo kama vile Levi-Strauss anaona maana ya kisa ipo katika matini na maana hiyohiyo hutokea katika matini nyingine yoyote, anahusisha maana moja tu ya kisa na maana nyingine, kisa kimoja na kingine hufanana kimaana wakati wanamuundoleo wao maana ya kisa ni mali ya msomaji au msikilizaji na kwamba pana fasili mbalimbali ya kisa  kulingana na kisa, msomaji au msikilizaji atatoa maana kilingana na muktadha na kusababisha kutoakea maana pana, kwa mfano katika riwaya ya mfadhili iliyotungwa na Hussein Tuwa, msomaji anaweza kuongelea kuwa riwaya hii imeelezea maswala ya mapenzi lakini pia msomaji mwingine anaweza kuielezea kwa maneno mengine na kutoa maana nyingine.
Kwa ujumla Umuundo wamejikita zaidi katika dhana moja, kwamba mfumo wa maana ni jinsi unavyofanya kazi, maana ya kazi ya inatokana na sheria na kaida mbalimbali za mifumo tofauti ya kuashiria. Maana haitokani na mtu ( mwandishi au msomaji). Wakati Umuundoleo unaishia kumpuuza mwandishi na kuishusha hadhi kazi ya fasihi kwa kutia mkazo mkubwa kwenye msomaji wa kazi hiyo. Wanajikita zaidi kwamba mzungumzaji au msomaji ndio wanaongoza mfumo. Nadharia zote mbili zina kamilisha upungufu wa nadharia ya umuundo na ndio walianzisha umuundoleo.

Print this item

  TOFAUTI KATI YA LUGHA YA BINADAMU NA MAWASILIANO YA WANYAMA
Posted by: MwlMaeda - 06-20-2021, 11:18 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - Replies (1)

Kwa mujibu wa Masamba na Wenzake Mwaka (1999: 1) “Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao”.
Pia kwa mujibu wa NKWERA F.M.V (1979) “Lugha ni utaratibu (mfumo) maalumu wa sauti za nasibu zenye maana ambazo hutumiwa miongoni mwa binadamu kwa madhumuni ya mawasiliano miongoni mwao sauti hizi lazima ziwe za kutamkika”.
Hivyo basi kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali walioeleza maana ya dhana ya Lugha. Lugha ni utaratibu maalumu wa sauti za nasibu ambazo huodhi maana katika jamii fulani sauti hizi hutumiwa na wanajamii hao kwa kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao.
Binadamu hutumia lugha kama nyenzo kuu ya mawasiliano tofauti na wanyama wengine. Kwa mujibu wa kamusi ya karne ya 21 kamusi ya Kiswahili. “Mawasiliano ni upashanaji wa habari kwa kutumia barua, simu au vyombo vya habari kama vile redio na televisheni’
Mawasiliano ni kubadilishana ujumbe (habari) baina ya wawasilianaji mfano, mtu na mtu ama mtu na kikundi. Pia wanyama huwa wanawasiliana na mawasiliano yao yana husisha ishara na sauti tofauti na binadamu ambaye hutumia lugha. Hivyo kuna tofauti baina ya Lugha za binadamu na mawasiliano ya wanyama kama ifuatavyo;-
 
Uwili; Lugha ya binadamu huwa na uwili yaani inajitokeza katika viwango viwili Sauti na Maana katika sauti Mofu, Fonimu, na Lekisimu viwango hivi huunganishwa ili kupata neno lenye maana tofauti, kwa mfano fonimu    maneno    sentensi lakini katika mawasiliano ya wanyama hayawezi kuchanganuliwa kwa kuanzia kipashio kidogo hadi kikubwa
Lugha ina sifa ya ubunifu au uzalishaji; Binadamu katika kuzungumza anauwezo wa kubuni na kuweza kuunda maneno mapya na hata kuzungumza maneno mengi katika kuelezea jambo au mada fulani kwa wakati mmoja kwa mfano, kutokana na neno lima tunaweza kupata maneno kama vile limia, limiana, limika, limisha. Maneno haya yana maana tofautitofauti na zinaeleweka. Tofauti na  mawasiliano ya wanyama ambapo wanyama wanaidadi mahususi za ishara na sauti. kwa mfano ng’ombe anapohisi njaa hawezi kutoa mlio tofauti na ule aliozoea kuwasilisha ujumbe kuwa ananjaa anahitaji chakula.
Lugha ya binadamu hutumika ghafla na kuna kubadilishana zamu; lakini katika mawasiliano ya wanyama hamna kubadilishana zamu binadamu anaweza kuzungumza maswala mbalimbali kwa wakati mmoja, pia binadamu hawazungumzi kwa pamoja bali huzungumza kwa zamu, kunakuwapo msemaji na msikilizaji kwa mfano mahojiano kati ya daktari na mgonjwa mgonjwa anapomuelezea daktari, daktari huwa ni msikilizaji na wakati daktari anapomshauri mgonjwa, mgonjwa huwa msikilizaji hivyo hali ya kubadilishana zamu hutokea. Hali hii ni tofauti na mawasiliano ya wanyama. Mfano nguruwe wanapoitaji chakula hulia wote kwa pamoja
Umakinikaji; binadamu huweza kuendelea kuzungumza ilihali anaendelea na jambo lingine mfano anaweza kuwa analima huku anaongea masuala tofauti na kilimo mfano siasa ,michezo na afya  lakini wanyama huzama katika kile wanachokitenda tu , kwa mfano mbwa anapobweka husitisha shughuli zote na kuzama katika kitendo cha kubweka.
Unasibu; lugha ya binadamu haina uhusiano halisi wa dhana ya  kirejelewa au kitajwa na hutumia sauti, ishara, alama na maneno. Mfano neno nyumba halina uhusiano wa  moja kwa moja na kirejelewa chake ndio maana hurejelewa kwa majina tofauti mfano house (kiingereza), enju (kihaya ) na ekhaa (kiganda) lakini mawasiliano ya wanyama yana uhusiano kwani ishara wanazotumia mfano paka hukunjua makucha yake kuashiria utayari wake kumshambulia adui wake . Aidha ni maneno macheche tu yenye uhusiano wa moja kwa moja na virejelewa vyake mfano nyoka (umbo) na pikipiki (sauti).
Viwango vya uundaji; katika Lugha binadamu huwa na viwango maalumu vya uundaji kwa mfano, sauti/b/ huunda fonimu/ba/ na fonimu huunda mofimu au maneno/baba/ ambayo nayo pia huunda kirai (kisu kikali) ambacho huunda kishazi kinachounda sentensi ambayo huunda kifungu cha habari au habari kamili (kisu kikali kimeibiwa) tofauti na mawasiliano ya wanyama hakuna viwango vya uundaji.
Lugha ya binadamu huwa na sifa ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali; utekelezaji huu unaweza kuwa kama vile kusali, kuimba, kutoa nasaha, kutoa hotuba, ahadi kwa mfano,  baba alimwahidi mwanae kumsomesha. Ila  kwa upande wa mawasiliano ya wanyama huwa ni kufikisha ujumbe tu haitekelezi majukumu tu.
Usambavu; Lugha ya binadamu huwa na sifa ya usambavu ambayo humsaidia mwanadamu kuelezea juu ya vitu vilivyombali kijografia na kihistoria, pia matumizi ya maandishi, maneno na ishara, Binadamu hutumia maandishi, Ishara na maneno kuzungumzia dhana yeyote kwa upana wowote ule bila upeo au kikomo pamoja na kuelezea yaliyopita, yaliyopo na yajayo.hii ni tofauti na mawasiliano ya wanyama kwa sabababu hawana uwezo wa huu wa usambavu kwa mfano panya hawezi kuwahadisia watoto wake alivyonusulika kuliwa na paka mwezi uliopita  binadamu huweza kurejelea matukio yaliyopita ya sasa na yajayo.
Hufungamana na utamaduni wa jamii husika; lugha ya mwanadamu hurithishwa kizazi kimoja kwenda kizazi kingine kupitia utamaduni wa jamii husika au utamaduni  na mazingira ambayomtu amekulia , mfano motto yeyote ana uwezo wa kuzungumza lugha yeyote duniani kutegemeana na mazingira auutamaduniambayo amewekewa kukulia, mfano  motto wa kimasai anapozaliwa ,anapolelewa na kukulia katika utamaduni na mazingira ya kizungu tofauti na wanyama ambao huzaliwa na mlio ambayo wanaitoa na wala hawawezi kubadilishana utamaduni na mazingira , mfano hata ng’ombe akiwekwa na mbuzi hawezi kujifunza utamaduni wa mbuzi wala sauti na ishara za mbuzi japo wako katika mazingira  yapamoja.
Hitimisho; kwa mtazamo huu lugha ya binadamu hutofautiana na mawasiliano ya wanyama, hivyo utofauti hizo zinatokana na sifa bia za lugha. Hata hivyo  ni vigumu kuelewa vipengele mbalimbali vya mawasiliano ya wanyama kwa uwazi unaodhihirika tofauti na lugha ya  binadamu kwani wanyama hawana lugha halisi iliyodhahiri bali huwasiliana kwa ishara tu.
 MAREJELEO
Matinde R.S (2012) Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia, Serengeti Editor Publishers (T) Ltd, Mwanza –Tanzania.
J.S.Mdee,K. Njogu,Shafi,A. (2011) .Kamusi ya kiswahili ya  karne ya  21,Longhorn Publishers (T)  Ltd, Dar es salaam –Tanzania.

Print this item

  MAENDELEO YA FASIHI KATIKA MIFUMO MBALIMBALI (VIDEO)
Posted by: MwlMaeda - 06-20-2021, 11:00 PM - Forum: Nukuu - Replies (1)

FASIHI KATIKA MIFUMO MBALIMBALI

Print this item

  Shukrani
Posted by: MwlNkonosha - 06-20-2021, 08:26 AM - Forum: Maswali na majibu - No Replies

Asante sana Mr Maeda nimefanikiwa

Print this item

  SHAIRI: HACHI
Posted by: MwlMaeda - 06-20-2021, 08:16 AM - Forum: Ushairi - No Replies

HACHI
Hachi kinochwa ni wengi, kisicho ncha kufuma
Hachi kisicho na mwangi, kichomacho na kuuma
Hachi kisicho kigingi, hakiondoi uzima
Hakichi wao wachacho, ana chake akichacho

Hachi wewe ukichacho, kinachokupa uzia
Hachi kisoziba macho, ukyonacho ukachia
Hachi kikuumizacho, akakiachia njia
Hakichi wao wachacho, ana chake akichacho

Hachi kisicho na kucha, kama cha jogoo kuchi
Hakichi hakina ncha, kimviringo ja mchi
Hakichi sichi cha kucha, woga kimewishwa hichi.
Hakichi wao wachacho, ana chake akichacho

Hachi kisicho na meno, kisagacho na kumeza
Hachi ye chenye mfano, chenye kula na kusaza
Hachi kisicho na bano, kinobana na kumiza
Hakichi wao wachacho, ana chake akichacho

*M.S.SALUM*

Print this item