MAANA YA KATEGORIA KATIKA SINTAKSIA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: MAANA YA KATEGORIA KATIKA SINTAKSIA (/showthread.php?tid=166) |
MAANA YA KATEGORIA KATIKA SINTAKSIA - MwlMaeda - 06-21-2021 Dhana ya kategoria imejadiliwa kwa namna tofauti tofauti. Khamis na Kiango (2002) wameigawa kategoria katika mitazamo miwili wanamapokeo na wanausasa. Ambapo wanamapokeo walitumia dhana ya kategoria kumaanisha sifa bainifu zinazoambikwa kwenye aina za maneno kama vile nafsi, idadi, njeo, dhamira, na ngeli. Wakati wanausasa wanaona kuwa kategoria ni zile aina za maneno kama vile Nomino (N), vivumishi (V), vielezi (E), viunganishi (U), vitenzi (T), viwakilishi (W), na Kihusishi (H). Massamba (2009) anaeleza kuwa kategoria ni jumla ya maumbo, faridi au vipashio vingine ambavyo huchangia sifa fulani au ambavyo viko katika kiwango kimoja.
Samwel (2) anaeleza kategoria kwa mtazamo wa kisarufi mamboleo kuwa ni darajia mbalimbali katika uundaji wa tungo. Anaendelea kueleza kuwa kuna kategoria za darajia mbili ambazo ni kategoria ya neno (kileksika) na kategoria ya virai. Ambapo kategoria ya kileksika huhusika na aina mbalimbali za maneno kama vile nomino, vivumishi, viwakilishi, vielezi, vitenzi, viunganishi, vihusishi na vibainishi. Naye O’Grady (1996) katika kufafanua kategoria za kileksika anaona kuwa ni kategoria za kiwango cha neno mojamoja na anataja aina nne za maneno ambazo ni nomino, kivumishi, kitenzi na kielezi. Darajia ya pili ni kategoria ya virai Samwel (keshatajwa) anaeleza kuwa hii ni kategoria inayofuata katika ile ya neno. Hivyo anaeleza kuwa kategoria ya virai imeundwa na kirai nomino (KN), kirai kivumishi (KV), kirai kitenzi (KT), kirai kihusishi (KH) na kirai kielezi (KE).
Kwa ujumla kwa kurejelea mtazamo wa sarufi mamboleo kategoria ni jamii au makundi yanayofanya kazi kwa kufanana na yenye sifa zinazofanana.Wesana-Chomi (2003) anaeleza kuwa dhana ya kategoria za maneno ni muhimu sana katika sarufi kwani maelezo ya sarufi ya lugha hayana budi kurejea kategoria za maneno kwa namna moja au nyingine. Hivyo zifatazo ni hoja zinazofafanua faida ya kuwa na kategoria.
Husaidia katika utungaji wa sentensi, O’Grady (1996) anaeleza kuwa neno fulani liko katika kategoria fulani kutokana na linavyofasiliwa, mfano nomino hutaja vitu, vitenzi ni maneno yanayotaja vitendo, vivumishi ni maneno yanayotaja sifa za nomino na vielezi ni maneno ambayo hueleza namna tendo linavyofanyika. Hivyo kutokana na maelezo ya O’Grady (keshatajwa) ni wazi kuwa mwanagenzi anapotaka kutunga sentensi ni lazima ajue kategoria za maneno kwani hawezi kutunga sentensi pasipo kuhusisha kategoria za manneno. Hivyo kategoria husaidia katika utungaji wa tungo mbalimbali katika lugha husika. Kwa mfano;
Wanafunzi wanasomaN T Mtoto anacheza mpira N T N Baba analima na mama anafua nguo N T U N T N Hivyo mifano ya juu inaonesha namna kategoria za maneno zilivyotumika katika kuunda ama kutunga sentensi mbalimbali.
Husaidia kujua miundo ya sentensi katika lugha, Obuchi na Mukhwana (2015) wanaeleza kuwa kategoria za maneno hufahamisha kwamba muundo wa sentensi huelezwa kwa kutaja kategoria za maneno yanayounda sentensi hiyo. Hivyo kategoria za maneno husaidia kujua miundo mbalimbali ya sentensi kwani kuna sentensi zenye muundo wa (N + T) yaani Nomino na kitenzi, kuna sentensi zenye muundo wa nomino + kivumishi + kitenzi + kielezi (N + V+ T+E), sentensi zenye muundo wa nomino + kitenzi + kielezi (N + T+E). kama inavyojidhihirisha katika mifano inayofuata;
Muundo wa (N + T + E)Mama ameenda sokoni N T E Muundo wa (N + V + T +E) Msichana mzuri ameenda shuleni N V T E Hivyo mifano tajwa hapo juu dhahiri inaonesha namna kategoria mbalimbali za maneno zilivyotumika katika kuonyesha miundo ya sentensi.
Kategoria husaidia kujua aina za maneno katika lugha husika na dhima zake katika tungo, Wesana-Chomi (2003) anaeleza kuwa maneno ya lugha hufanya kazi mbalimbali katika tungo. Mfano kuna maneno yanayofanya kazi kuonesha nani katenda tendo, nani katendewa tendo au nani katendwa tendo. Maneno yenye kazi hizo katika tungo huitwa nomino. Pia, maneno mengine hutoa taarifa juu ya nomino na maneno hayo ni kivumishi. Aidha, maneno mengine hutaja tendo au jambo lifanywalo na mtenda tendo na maneno hayo huitwa vitenzi. Kwa mfano;
Mwalimu anafundishaN Mtoto mzuri V Hivyo katika mifano hii neno Mwalimu ambalo ni nomino limesimama kama mtenda wa jambo na katika mfano wa pili neno mzuri limesimama kama kivumishi ambacho kinatoa sifa juu ya nomino. Hivyo kategoria husaidia kujua aina za maneno.
Husidia kujua aina mbalimbali za virai pamoja na miundo yake, Massamba na wenzake (2012) wanaeleza kuwa miundo ya virai hukitwa katika aina za maneno ambazo ndizo chimbuko la mahusiano maalumu ndani ya vipashio hivi. Mfano wa virai hivyo ni KN, KV, KE, KT na KU. O’Grady (1996) anaeleza kuwa
Husaidia na kutuwezesha kutunga sentensi zisizokikomo na zinazoeleweka. Sentensi zisizokikomo ni sentensi ambazo ni ndefu na zisizo na mwisho, kwa mfano;
Baba na mama walipanda mlima Kilimanjaro ambao mlima huo upo mpakani mwa Kenya na Tanzania ambapo
Mama alimnunulia mtoto zawadi iliyokuwa ikiuzwa sokoni kariakoo karibu na mtaa wa mama lishe uliopakana na mtaa wa kongo pembezoni mwa maduka ya vitambaa vya kihindi vinavyouzwa na wahindi kutoka India ambao walikuja Tanzania kufanya biashara zinazowaingizia kipato kikubwa kiasi cha kuweza kumudu na kukidhi mahitaji ya familia yao.
Husaidia katika uchanganuzi wa sentensi za lugha husika, katika kuchangua sentensi za lugha kategoria za maneno hutumika kwani huwezi changanua sentensi pasipo kuhusisha kategoria za maneno kwa mfano;
Baba analimaN T S.S KN KT N T Baba analima Husaidia kuunda nadharia mbalimbali za sintakisia, kutokana na uchambuzi wakategoria za kisintakisia kumepatikana nadharia mbalimbali kama vile sarufi miundo virai na sarufi geuza maumbo zalishi.
Husaidia kupata sarufi inayojitosheleza kwa usahihi katika lugha, lengo la uchambuzi wa kisintakisia ni kutafta ukubalifu au usioukubalifu wa tungo zisizo sahihi.
MAREJELEO Besha, R.sM (2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press. Massamba, D na Wenzake. (1999) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu,Sekondari na vyuo. Dar es Salaam: TUKI. |