MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

VITENZI VYA KISWAHILI SANIFU - Printable Version
|
VITENZI VYA KISWAHILI SANIFU - Printable Version
+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9)
+--- Thread: VITENZI VYA KISWAHILI SANIFU (/showthread.php?tid=164)
|
VITENZI VYA KISWAHILI SANIFU - MwlMaeda - 06-21-2021
Aina hii ya neno huweza kufafanuliwa kwa kutumia vigezo mbalimbali vya kiisimu ambavyo ni; kisemantiki, kimofolojia na kisintaksia. Hata hivyo maana inayotokana na semantiki ndiyo huegemewa zaidi. Tazama hapo chini namna ya kufasili kitenzi kwa kutumia vigezo mbalimbali.
Kisemantiki, kitenzi ni aina ya neno inayotaja tendo au hali ya kuwa. Kwa mfano;
- Juma analima.
- mama anapika.
- Suzana yu mgonjwa.
- John alikuwa mzembe
Kimofolojia, kitenzi ni aina ya neno iliyojengwa na mzizi tenzi pamoja na viambishi. Kwa mfano; Lim – a, ku – l – a, imb – a, som – a.
Kisintaksia, kitenzi ni aina ya neno ambayo hupokea nomino au kiwakilishi mwanzoni na hupokea nomino au kiwakilishi au kielezi mwishoni. Kwa mfano, neno lililoandikwa kwa herufi mlalo ni kitenzi; 1. Musa analima. 2. Justina anatembea polepole. 3. Wewe ni mwanafunzi bora. 4. Tanzania imepata rais.
AINA ZA VITENZI
Kisemantiki, kuna aina tatu za vitenzi. Aina hizo ni; kitenzi kikuu, kitenzi kisaidizi na kitenzi kishirikishi.
Kitenzi Kikuu
Ni aina ya kitenzi ambacho humiliki uhusiano baina ya vipashio arifu katika tungo au sentensi. Hii ni sehemu muhimu ya sentensi kwani bila kitenzi kikuu sentensi haikamiliki. Pamoja na kuwa sentensi zote si lazima zikamilishwe na kitenzi kikuu, lakini kitenzi hiki ndicho kinachobeba taarifa nyingi zaidi. Tazama mifano ifuatayo, neno lilioandikwa kwa herufi mlazo ni kitenzi kikuu. 1. Mama anafua nguo za watoto.
- Daftari langu limechanika.
- Wasomi hufanya utafiti.
- Amenipotea.
- Ngamizi imezima.
Kitenzi Kisaidizi
Ni kitenzi ambacho uamilifu wake ni kukisaidia kitenzi kikuu kukamilisha uarifu wake. Hii ina maana kuwa vitenzi visaidizi haviwezi kusimama peke yake bila kuwa na kitenzi kikuu. Vitenzi hivi hutoa taarifa ya ziada kuhusu tendo. Vivyo hivyo, vitenzi hivi vikiondolewa katika sentensi haviathiri maana ya sentensi. Tazama mifano ifuatayo, neno lililoandikwa kwa herufi mlazo ni kitenzi kisaidizi.
- Pili alikuwa anataka kula.
- Mazoea alitaka kwenda shambani.
- Bibi hahitaji kuhifadhi mazao.
Kitenzi Kishirikishi
Hiki ni kitenzi ambacho huonesha zaidi hali ya kuwa. Pamoja na hilo, kitenzi hiki huonesha uhusiano uliopo baina ya nomino au kiwakilishi kinachotajwa na tabia au hali inayozungumzwa. Vitenzi vishirikishi vyote lazima viwe na pande mbili. Upande wa nomino au kiwakilishi na upande wa sifa au hali. Tofauti na vitenzi vikuu, vitenzi hivi haviwezi kusimama pekee na kutoa maana. Tazama mifano ifuatayo, neno lililoandikwa kwa herufi mlazo ni kitenzi kishirikishi.
- Maeda ni mwalimu.
- Yeye si mtoto mdogo.
- Ashura ni mgonjwa.
- Huyu ndiye mkorofi
- Hapa ndipo penyewe.
- Baba alikuwa mpole
Tabia za Vitenzi vya Kiswahili Sanifu
- Kitenzi ni sehemu kuu ya sentensi. i.e Sentensi haiwezi kukamilika bila kuwa na kitenzi.
- Kitenzi hupokea viambishi vya; nafsi, wingi-umoja, njeo, urejeshi, ukanushi, uyakinishi, kauli mbalimbali na viambishi vya hali.
- Kitenzi kinaweza kupokea nomino mwishoni au kisipokee (elekezi na sielekezi).
- Kitenzi huonesha tendo.
- Kitenzi huonesha hali ya kuwa.
- Huweza kuonesha upatanishi wa kisarufi.
- Kitenzi huweza kunyumbulishwa.
- Kitenzi huweza kuwa na alomofu mbalimbali za mofu moja.
Dhana Mbalimbali za Kitenzi
- Kitenzi Jina: Hiki ni kitenzi ambacho huchukua hadhi ya nomino.
- Kitenzi Elekezi: Hiki ni kitenzi ambacho uamilifu wake hulazimisha kupokea nomino mwishoni.
- Kitenzi Sielekezi: Hiki ni kitenzi ambacho uamilifu wake si lazima kuwepo na nomino mwishoni.
- Kitenzi cha Msingi: Hiki ni kitenzi kilichojengwa na mzizi tenzi na kiambishi tamati maana.
- Kitenzi cha Myumbuliko: Hiki ni kitenzi kilifanyiwa mchakato wa unyumbulishaji.
RE: VITENZI VYA KISWAHILI SANIFU - MwlNkonosha - 06-21-2021
Bwana Maeda,umeweza kuonesha vizuri tabia za vitenzi.Kuna jambo ambalo huwa linanichanganya kuhusu hizi dhana mbili; Tabia na kazi za vitenzi.Kwa nini baadhi ya Tabia hizo ulizozitaja zinaonekana kuingiliana na kazi za vitenzi,mfano kuonesha nafsi?.Asante.
Au kazi hasa ya vitenzi vya kiswahili sanifu ni ipi?
|