SHAIRI: HACHI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: HACHI (/showthread.php?tid=159) |
SHAIRI: HACHI - MwlMaeda - 06-20-2021 HACHI Hachi kinochwa ni wengi, kisicho ncha kufuma Hachi kisicho na mwangi, kichomacho na kuuma Hachi kisicho kigingi, hakiondoi uzima Hakichi wao wachacho, ana chake akichacho Hachi wewe ukichacho, kinachokupa uzia Hachi kisoziba macho, ukyonacho ukachia Hachi kikuumizacho, akakiachia njia Hakichi wao wachacho, ana chake akichacho Hachi kisicho na kucha, kama cha jogoo kuchi Hakichi hakina ncha, kimviringo ja mchi Hakichi sichi cha kucha, woga kimewishwa hichi. Hakichi wao wachacho, ana chake akichacho Hachi kisicho na meno, kisagacho na kumeza Hachi ye chenye mfano, chenye kula na kusaza Hachi kisicho na bano, kinobana na kumiza Hakichi wao wachacho, ana chake akichacho *M.S.SALUM* |