MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 49 online users.
» 0 Member(s) | 47 Guest(s)
Bing, Google

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  Uchawi katika Riwaya za Kiswahili
Posted by: MwlMaeda - 07-16-2021, 02:47 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Uchawi katika Riwaya za Kiswahili
A.J. Saffari
Utangulizi
Makala haya yanazungumzia nafasi ya uchawi katika riwaya za Kiswahili. Lakini kwa vile riwaya zote, japo ziwe za kubuni, zinakita mizizi na kupata uhai wake kutoka maisha halisi, suala linakuwa: Je, uchawi wenyewe ni kitu dhahiri au dhana tupu?
Waama nadharia na suala zima la uchawi limezungumziwa na kujadiliwa mwahala mwingi na watu wa kawaida tu mitaam, viongozi wa nchi pamoja na wanazuoni wa vipeo vya juu masomoni. Vitabu vya dini mbili kubwa duniani Kuruani2, yaani Msahafu, na Biblia3, vinazungumzia uchawi katika sehemu mbalimbali kadiri itakavyoonyeshwa baadaye. Nao Geofrey Parrinder4, Middleton5, Murray6, Michael7, Harwood8, Alastair Scobie9, Amold,10, Mary Douglas11 , kwa kutaja baadhi tu, wamejitoma katika mjadala kuhusu uchawi.
Makala baya yataanza na tafsiri ya uchawi, baadaye kujadili ushahidi mintaarafu ya uchawi, sababu zake, uchawi na utamaduni, pamoja na maendeleo.
Tafsiri ya Uchawi
Maana au tafsiri ya uchawi imezua utatanishi kama suala lenyewe la uchawi. Hivyo George Parrinder hajakosea anapodai kwamba ni masomo machache tu yamewakanganya watu kuliko uchawi.12 Kamusi, Encyclopaedia, na vitabu vya waandishi mbalimbali vimezidi kutatanisha maana ya uchawi. Vingi vinachanganya uchawi, wanga na uganga.
Kamusi ya Oxford inaanza kwa kudai kuwa mchawi (witch) ni mwanamke anayetumia madawa kwa madhumuni mabaya hasa miongoni mwa washenzi.13 Kwa upanae mwingine Kamusi ya Kiswahili Sanifu inaeleza kuwa uchawi ni ufundi wa kutumia dawa, aghalabu mitishamba na vitabu maalum vya uganga, ili kuleta madhara kwa viumbe, yaani sihiri. Baadaye kamusi hiyo inamwelezea mwanga kama mtu afanyaye mazingaombwe ya uchawi usiku, mtu achezaye ngoma ya mahepe.14
Ni dhahiri matatizo kadha yanajitokeza kutokana na maana au tafsiri zilizoelezwa hapo juu. Kwanza, ni kutoainishwa baina ya uchawi, wanga na madawa. Pili, madai kuwa mchawi ni mwanamke. Madai hayo yameungwa mkono na waandishi wengine kadhaa, bila ya ushahidi wowote. Na tatu, dai kuwa uchawi ni suala linalowahusu washenzi tu”. Maana yenyewe ya ushenzi haikuelezwa hapa, iwapo ni mtu ambaye hakustaarabika, yaani yuko nyuma kimaendeleo, au habithi wa matendo.
Katika mkanganyiko huo wa maana nastahabu ile inayodai kuwa uchawi ni ufundi, yaani utaalamu wa kutumia sio dawa tu, bali mbinu nyingine mbalimbali pamoja na vitabu maalum vya uganga ili kuleta madhara kwa viumbe. Bora kufafanua hapa kuwa hii ndiyo maana inayolingana na matumizi ya neno uchawi miongoni mwa watu wa Afrika. Lakini basi, kwamba taaluma au ufundi huu (uitwao uchawi) aghalabu huaminika na kutumika kuhasiri viumbe, haina maana kuwa hauwezi kutumiwa kwa manufaa.
Ushabidi Mintaarafu ya Uchawi
Leo hii watu wengi, nata wasomi, hawaelewi namna bomu la Neutron la Wamarekani linavyoweza kuua viumbe vyenye uhai na kuviacha visivyo na uhai bila ya athari yoyote. Hata hivyo kweli ni kuwa jambo kama hilo hutokea ingawa wanaojua kwa nini inakuwa hivyo ni wale wachache wenye taaluma hiyo. Wataalamu hao huishi chini ya ulinzi mkali kuliko marais wao na kuficha siri za utaalamu wao kama wafichavyo sehemu zao za siri. Basi ndivyo hivyo kwa elimu nyingi pamoja na uchawi wenyewe.
Baadhi ya waandishi, akiwemo George Parrinder, wanashikilia kuwa msingi wa uchawi ni imani tu. Ya kwamba imani hiyo ilianzia na kuzagaa Ulaya katika karae za kati. Hadi leo hii imani ya uchawi imelikumba Bara la Afrika na kusambaza hofu na vifo. Mwandishi huyo anaendelea kusema kuwa imani hiyo ya uchawi ilisababishwa na dhiki ya maisha. Kutokana na maradhi ya kuambukiza, uchafu na vifo vingi binadamu walitafuta sababu za maafa hayo. Walipozikosa au kutozijua, wakaanza kusingizia uchawi.15 Kama ambavyo itaelezwa baadaye, naafiki kuwa taaluma ya uchawi kwa maana ya kudhuru viumbe, imeshamiri zaidi katika jamii ambazo ziko nyuma kimaendeleo. Lakini wachawi sio masikini tu. Hata Mary Douglas anathibitisha kwamba matajiri wakubwa huko Uingereza na Ujerumani walitumia uchawi kuwaroga wenzao.16 La maana zaidi ni kuwa siafikiani na George Parrinder kuwa uchawi ni imani tu. Uchawi ni jambo la hakika wala sio dhanatupu.
Hapa sitathubutu kujinadi kujua kunga za uchawi kama vile ambavyo sijui namna bomu la atomiki linavyoua, japo linaua. Ila nitajitahidi kuthibitisha kuwa uchawi sio dhana wala imani tupu ya washenzi kama ambavyo George Parrinder na wenzake wanavyotaka tukubali.17
Je, ushahidi gani unadhihirisha kuwepo kwa taaluma ya uchawi?
Kwanza vitabu vya dini mbili kubwa duniani, yaani Korani na Biblia, vinazungumzia kwa ufasaha jambo hili. Aya ya 102, Surat l’Baqara18, inaeleza kuwepo kwa taaluma ya uchawi. Na katika tanbihi ya 105 ya Sura hiyohiyo Mungu anaelezea namna taaluma hiyo inavyoweza kutumiwa vizuri mikononi mwa watu ashrafu kama vile Hart na Marut, stadi wa taaluma hiyo walioishi Babylon awali hizo.19 Ikumbukwe kwamba katika siku hizo ayani Babylon ilivuma kuwa kitovu cha sayansi, hususan elimu ya nyota. Hata hivyo, hapohapo Mungu anaonya nanma ambavyo taaluma hiyo ya uchawi inavyoweza kutumiwa vibaya mikononi mwa mahabithi wenye ghera, choyo na tadi. Pamoja na yote hayo Mungu anasisitiza kuwa uwezo au taaluma hii ya uchawi ina ukomo; kwamba mchawi hawezi kutenda akafanikiwa kama Mungu hapendi. Yaani mchawi, japo awe fundi mangungu kiasi gani, hawezi akatumia uchawi kuroga au kuopoa akafanikiwa pasi Mungu kupenda. Kwa wale waumini wanaelewa fika kuwa kila kheri na shari humuelea Mungu.
Kuna hadithi moja iliyopokelewa enzi na enzi inayosimulia kwamba aliishi stadi mmoja wa taaluma ya uchawi kwa jina Maalim Kisisina. Hadithi inaeleza kuwa Maalim Kisisina alikuwa anabuni mipango ya kuzuia kudura za Mungu. Basi Mungu akamtuma malaika wake Jibrili kumfuata Maalim Kisisina na kumtaka undani wake. Jibrili alimwasilia Maalim Kisisina kwa umbo la mwanadamu. Kufika akamuomba amueleze aliko Jibrili kwa wakati ule. Basi Maalim Kisisina akapekua buku kubwa na taaluma ya uchawi na kumjibu kuwa kama Jibrili siye yeye mwenyewe Maalim Kisisina, basi Jibrili ni yule mtu aliye mbele yake, yaani Jibrili mwenyewe. Hadithi inasimulia kuwa mara hiyohiyo Jibrili akatumia wahyi ya Mungu kumpokonya Maalim Kisisina buku hilo la uchawi. Kufumba na kufumbua Jibrili alimpora Maalim Kisisina, naye kwa kutumia taaluma yake ya uchawi, akaapa kumuandama Jibrili. Kwa pamoja wakapaa juu na juu mbinguni hadi Mungu akamtumia tena wahyi Jibril kuwa achane karatasi moja la buku lile la taaluma na uchawi amtupie Maalim Kisisina. Jibrili alitii amri hiyo. Kuona kataa linaanguka kutoka mikononi mwa Jibrili, Maalim Kisisina akalidaka kataa hilo akiamini kuwa ni buku lake lote kumbe sivyo. Inadaiwa na hadithi hiyo kuwa taaluma yote ya uchawi duniani imo kwenye kataa lile moja alilotupiwa na kuachiwa Maalim Kisisina.
Hadithi ya Maalim Kisisina inasadikiwa na baadhi kuwa ya kweli. Lakini kama itazua ubishi bado kuwa ushahidi mwingine mwingi unaothibitisha taaluma ya uchawi. Tumeona maelezo ya Korani, sasa tuangalie Biblia.
Agano la Kale linaelezea miujiza baina ya Musa na wachawi wa Farao, namna ambavyo wachawi wa Farao walivyoweza kugeuza fimbo kuwa nyoka.20 Lakini hata hapa tunaelezwa kuwa Musa, kutokana na kubuli ya Mungu, aliweza kuitupa chini fimbo yake ikageuka joka kubwa lililowameza nyoka wote wa wale wachawi wa Farao.
Mnamo mwaka 1958 aliishi mpigania uhuru mmoja huko Tanga akiitwa Osale Otango kwa jina la utani. Waingereza waliamua kufanya msako mkubwa dhidi yake; na hatimaye kumkamata na kumpeleka Gereza la Maweni. Gereza hilo lilikuwa maarufu na humo ndani Osale aliwekwa kwenye chumba cha pekee akiwa ametatikwa pingu na minyororo ya mikono na miguu. Asubuhi iliyofuatia Mkuu wa Gereza, Mwingereza, alifika ofisini kwake mapema akakuta karatasi imeachwa juu ya meza yake imeandikwa: “Kwa heri, tutaonana. Osale Otango.” Upesi alikimbilia kule rumande na kukuta chumba salama lakini Osale Otango hayumo. Hakuna mtu aliyeiba funguo za rumande na wala hapakuweko sehemu iliyovunjwa katika rumande hiyo.
Tukio jingine lilitokea Mwanza mnamo miaka ya sabini. Tukio hili lilielezewa sana na magazeti yote ya Uhuru na Daily News. Mvulana mmoja alifariki ghafla, akazikwa. Siku nyingi kupita akapatikana hai, ingawa hakuwa na fahamu nzuri wala kuweza kuzungumza. Mvulana huyo alipelekwa Hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi.
Aidha kuna ikirari na maungamoya wachawi wenyewe. Kwa kawaida, na hata kwa mujibu wa sheria, ikirari 21 na maungamo22 ni ushahidi muhimu sana dhidi ya mtuhumiwa; madhali tu uwe umetolewa kwa hiari, bila vitisho wala ahadi za uongo. Waandishi wa vitabu kadhaa wanaelezea ikirari na maungamo haya ya wachawi. Geofrey Pamnder, kwa mfano, anaelezea kuwa wachawi huungama kukutana usiku kujadili masuala yao na kula nyama za watu ambao wamewaua kwa njia za uchawi.23 Wachawi hao hufanya mashindano kuonyeshana ujuzi na maajabu yao. Anazidi kuelezea kuwa wachawi wa Basuto hukiri kukutana usiku wakiwa uchi, hutumia madawa kuwafanya watu walale kisha huiba ng’ombe zao.24 Yafaa ikumbukwe hapa kuwa matendo hayo ya wizi wa ng’ombe kwa njia za uchawi yanafanyika mno Mwanza na Shinyanga. Wakati fulani yalifikia kiwango kikubwa cha kutisha, hata watu binafsi wenye mifugo yao wakaanza kuwasaka na kuwaua watu waliowadhania ni wachawi waliofanya madawa ya kuwaibia ng’ombe wao. Kesi maarufu ya Elias Kigandye25 ni ithibati ya kutosha. Itakumbukwa kuwa mauaji yaliyotokana na upelelezi wake si hiyo yalisababisha Mheshuniwa Ali Hassan Mwinyi, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo, ajiuzulu.
Mary Douglas naye anatoa mifano kadhaa ya maungamo ya wachawi Uingereza na Ujerumani. Anaelezea namna Malkia mmoja alivyokufa kwa miujiza huko Uingereza,26 na jinsi ambavyo watu mbalunbali, waume kwa wake, walivyokiri na kuungama mauaji katika miji mbalimbali ya Ujerumani ya Magharibi. Mmoja kati ya wachawi hao, Paul Camperle, mwenye umri wa miaka thelathini na tano, aliungama kuwa alianza uchawi tangia utoto wake alipofunzwa na nyanya yake. Tangu hapo alijinadi kuwa aliwaroga na kuwaua watoto mia moJa, na kuwalemaza au kuwafanya viwete matajiri kadhaa wajiji la Munich.27 Mkewe, Anne Camperle, naye aliungama kuua watoto mia na watu wazima kumi na tisa. Aidha alijitapa kumshakizia mke wa mtu mmoja kujichoma ndani ya jiko hadi kuiva. Mumewe naye akamfuatia. Akajitapa zaidi kuua idai kubwa ya ng’ombe wa watu.28 Mwanae Simon Camperle naye aliungama kuuwa watoto kumi na sita, watu wazima sita, pamoja na kuwalemaza wengine au kuwafanya viwete.29
Mtu mwingine Olrich Schelltibann, umri miaka themanini, alijifaragua kuua watoto arobaini, watu wazima thelathini, na kuwalemaza au kuwafanya wengine viwete.30 George Smeltes naye aliungama kuua watoto thelathini na sita, watu wazima kumi na tano, na kuwalemaza au kuwafanya wengine viwete.31 Maungamo hayo yanasemekana yalifanywa kwa hiari mbele ya Gavana wa Jiji la Munich. Baadaye wachawi hao walichomwa moto hadi kufa.32
Wachilia mbali maungamo hayo ya vitabuni, ushahidi uko katika sehemu mbalimbali hapa Tanzania wa wachawi kuungama kuwaua watu kwa kutumia uchawi. Wachawi hao, mathalan, wamewahi kuungama mbele ya Tekelo, Dar es Salaam; Kabwere, Tanga; na Mandondo, Korogwe. Tekelo, Kabwere na Mandondo ni waganga maarufu ambao waliweza kuwafichua wachawi katika sehemu hizo. Licha ya kuungama tu, baadhi ya wachawi hao walijitokeza na mafuvu ya vichwa, mifupa ya wafu na hata makoba yao ya uchawi na vyungu vya kupikia nyama za wafu. Wengine walidiriki hata kuelezea namna walivyogawana na kufaidi nyama ya mtu fulani.
Sababu za Uchawi
Kila kitu kina nia na madhumuni yake. Uchawi nao, kwa maana hii yake mbaya ya madhara, una sababu zake kuu zifuatazo. Kwanza ni sababu ya kiuchumi. Katika jitihada ya kupata, mathalani mifugo, kama ambavyo imeelezwa awali wachawi hutumia uchawi kuswaga ng’ombe wa wenzao. Au, ili kupata mavuno mengi, wachawi huhitaji huduma ya watu wengi mithili ya watumwa. Hivyo hutumia mbinu za kuwafanya watu waonekane wafu, kumbe wazima, kisha huwatumikisha kulima mashamba na kuyahudumia. Aina hii ya uchawi ni maarufu kote Afrika, na hapa Tanzania hujulikana kwa majina mbalimbali. Mathalan huko sehemu za Kusini, kama vile za Lindi, huitwa ndondocha. Sehemu za Mwanza na Shinyanga huitwa mitumba. Tanga huitwa msukure. Na kwajumla neno kizuu lina maana ya mtu ambaye anafungwa na kutumikishwa baada ya watu kumzika wakidhani amefariki.33
Alistaire Scobie anaelezea mauaji ya kutisha huko Basuto, yaani Botswana, kwa minajili ya kupata mali.34 Mtu mzima hukamatwa usiku na kukatwa viungo mbalimbali huku yu hai. Viungo hivyo kama vile macho, maini, huchanganywa na vitu vingine na kutumiwa kama dawa ya mavuno makubwa. Ayi Kweyi Annah pia anaelezea mauaji ya aina hiyo katika Nigeria.35
Mauaji kama hayo pia yako sehemu nyingi hapa Tanzania kwa nia ileile ya kutafuta mali. Kwa mfano, mara nyingi watu hukutwa wameuawa na kukatwa sehemu za siri. Baadhi ya wakazi wa Nyanda za Juu huamini kuwa sehemu hizo zinavutia utajiri wa biashara.36
Sababu nyingine mbili hukaribiana mno na hii ya kwanza, nazo ni sifa na uwezo. Kwa mfano, baadhi ya viungo vya mwanadamu vikikatwa yungali hai, kama vile maini na moyo, hutumiwa kumpa mchawi au yeyote anayekusudia uwezo, sifa na ujasiri. Vijiji vingi Afrika vina baadhi ya watu, waganga ambao hutisha na kuogopesha kutokana na sifa, uwezo na utajiri wao utokanao na uchawi.
Sababu ya mwisho ni kustarehe. Wachawi wanatumia taaluma hiyo kufanya ufidhuli wa kuchezea watu usiku, kama vile kuwapanda, kuonyeshana miujiza, kucheza uchi, kula nyama za watu waliowaua, n.k. Zaidi ya yote wachawi hutumia taaluma hiyo kuwapora watu wake zao, ikibidi hata kwa kuwaua waume zao kwanza.
Uchawi na Utamaduni
Matendo yote ya mwanadamu hutokana na mfumo wa kuzalisha mali na mahusiano ya uzalishaji mali yenyewe katika jamii inayohusika. Taaluma mbalimbali hubuniwa kwanza kwa kukidhi haja ya jamii inayohusika. Uchawi nao ni hivyohivyo.
Awali niliafikiana na hoja ya Parrinder kuwa mara nyingi uchawi hustawi kwenye umaskini kwa sababu aghalabu umaskini hutokana na zana duni za kuzalisha mali. (Sitazungumzia mahusiano ya uzalishaji mali.) Badala ya kutumia matrekta au majembe ya ng’ombe watu wa sehemu nyingi za dunia, hasa Afrika, hutumia viserema. Ukulima wa kiserema ni wa tonge domoni tu, basi. Anayetaka kupata mazao mengi hana budi apate watu wengi wamlimie. Na watu hao wataka kulipwa. Kulipa nako kunapunguza faida. Jambo moja la kufanya ni kupata watumwa. Lakini utumwa mkongwe hauko siku hizi. Na utumwa mamboleo nao unahitaji kiasi fulani cha ijara, sio bure. Hivyo la kufanya ni kuweza kupata watumwa kwa namna nyingine. Hapa ndipo taaluma ya uchawi kama vile ndondocha, mizuka, msukure, na kadhalika hutumika. Vizuu ni watumwa bora zaidi maana hawawezi kugoma’wala kujadili vitu vizuri. Kama asemavyo Dk. Emmanuel Mbogo, wao hulishwa kinyeke na kuridhika.37
Riwaya ya Mirathi ya Hatari inaelezea mkasa uliokitikisa kijiji cha Kitelevadzi na kuashiria mfarakano mkubwa.38 Kisa ni kuwa Mzee Kasembe alikuwa anagombania shamba la watu wengine wawili, yaani Kipedzile na Malipula.39 Ili kujipatia shamba hilo kulihali, Malipula, kwa kutumia radi, aliteketeza familia yote ya Mzee Kasembe isipokuwa Gusto ambaye hakuwa nyumbani.
Kadiri nyenzo za uzalishaji mali zinavyoimarika ndivyo taaluma ya uchawi kwa minajili ya kudhuru kwanza ili kujinufaisha inavyopotea.
Uchawi na Maendeleo
Baada ya mjadala wote uliotangulia suala linabakia: nini nafasi ya uchawi katika maendeleo ya Watanzania na riwaya zao za Kiswahili.
Kwa bahati mbaya, kwa mujibu wa ushahidi uliopo – kama ilivyoonyeshwa katika makala haya – taaluma ya uchawi imetumika zaidi kuibananga badala ya kuiendeleza jamii. Kutokana na taaluma ya uchawi inabidi kwanza mchawi adhuru ili ajinufaishe binafsi. Zaidi ya yote elimu hiyo yote ni kunga inayohifadhiwa kwa misingi ya ubinafsi dhidi ya maendeleo ya jamii kwa jumla.
Kwa kuwa, basi, kazi za sanaa kama vile riwaya hupata taswira yake kutokana na jamii inayohusika, riwaya za Kiswahili mintaarafu ya taaluma hii ya uchawi nazo zimeelezea uovu wa uchawi na hata kulaani kwamba inapasa utokomelee mbali.40
Riwaya Fadhili Msiri wa Naugua inaelezea uadui unaozuka baina ya nchi ya Naugua na Ramali. Katika hadithi hii kijana Kadi alitoka kwao Ramali nchi ya Wachawi, kwenda Naugua. Huko alimpenda mwali mmoja Mwanagele na kutaka kumuoa. Lakini kutokana na mila ya Naugua ilibidi kwanza amgombanie na kijana mwingine Fadhili, ili kupata ushindi wa kumuoa. Katika mashindano hayo Kadi alipigwa na kuumia. Watu wa Ramali wakaja juu na kutaka kuiangamiza Naugua kwa sihiri. Kwa bahati nzuri waganga – Mzee Jala na Bi Kizee Mkunyambi kutoka nchi ya Tiba – walizuia azma ya Waramali kumuua Fadhili, Mwanagele na kuteketeza familia nyingi za Wanaugua.
Mirathi ya Hatari42 nayo inaonyesha namna taaluma ya uchawi ilivyotumiwa kuteketeza watu kwa minajili ya ubinafsi wa mtu au watu wachache.
Lakini, kama ilivyodaiwa awali matumizi mabaya ya taaluma hayafanyi taaluma hiyo nayo kuwa mbaya. Hivyo katika Mirathi ya Hatari Mzee Kazembe aliukumbatia mkono wa mwanawe Gusto na kumuusia:
“Mwanangu, nakuachia kazi kubwa. Ni urithi mkubwa ukiutumia vyema; bali pia ni mirathi ya hatari usipojihadhari nayo.”43 Na hata baadaye wakati Gusto alipokuwa anatawazwa kuwa mchawi usiku kule pangoni, Mzee Mavenge, mmojawapo wa wachawi, alimsisitizia Gusto: “Kama nilivyokueleza yote hii ni elimu ya pekee. Ukufahamu na kuitumia vizuri unaweza kuumiliki ulimwengu. Ni siku hizi tu Wazungu wamekuja na elimu yao ya uongo na kweli wakawapotosha vijana wetu”.44 Kama hoja ni matumizi mabaya Mzee Mavenge alisema: “Hebu sikiliza jinsi wanavyouana! Hebu angalia mavyombo yao ya kivita! Nayo vile utasema yanasaidia kuinua hali ya binadamu!”45
Mijadala hiyo michache katika Mirathiya Hatari inapanua mawazo kuwa hakika taaluma ya uchawi ina sura mbili: ya wema, na ya uovu. Wengi wetu tunaiona ile sura ya uovu tu. Na kwa hivyo waandishi nao wameangukia katika upofu huo. Hili ni kosa kubwa kwa vile linapingana na kweli. Je, sio kweli kwamba kweli itashinda namna tunavyoishi!46
Sifa moja adhimu kwa mwandishi, na hasa msanii wa riwaya na tungo nyingine, ni kuheshimu kweli. Wakati mwingine hana budi kuitafiti na kujua kweli imesimamia wapi maana daima kuna watu ambao kazi yao ni kuipotosha na kuificha kweli.
Taaluma ya uchawi imejificha, dhahiri, lakini imepotoshwa ama kutokana na ukufi wa elimu au kwa kusudi. Kazi ya waandishi ni kutandua utandabui huu hasidi.
Hitimisho
Hoja inatolewa hapa kuiangalia vizuri sura ya pili ya taaluma ya uchawi ili kuutumia kwa maendeleo na hata ulinzi. Kwa mfano, wachawi wanaweza kuruka na kusafiri mbali kwa muda mfupi tena bila ya kuonekana. Wanaweza wakapenya ndani ya nyumba bila ya kuibomoa na kuwataa watu usingiri mzito kwa muda mrefu.47 Wanaweza wakafanya mengi mengine ya manufaa.
Basi nini wajibu wa waandishi wa riwaya katika suala hili la kuitumia taaluma ya uchawi kwa maendeleo?
Kwanza kabisa narejea katika hoja yangu ya awali kuwa moja ya sababu kubwa ya taaluma ya uchawi kutumika vibaya au kwa ubinafsi ni kutokana na kuwa na zana duni za uzalishaji mali, yaani umaskini. Kadiri maendeleo yatakavyoongezeka ndivyo matumizi ya madhara ya uchawi yatakavyopungua. Hata hivyo uchawi unaweza ukaendelea kutumika kwa madhara kwa muda mrefu kutokana na udhaifu wa wanadamu kutapia mali, uwezo, hata anasa tu, pamoja na wivu. Mchawi anaweza kuwa tajiri lakini akaamua kumuua tajiri mwenzake ili aondoe upinzani naye katika biashara.
Iwapo ni hivyo, nini wajibu wa waandishi wa riwaya katika kipindi hiki cha mapito? Ni vigumu kutoa jibu la mkato kwa sababu ileile niliyoigusia awali: kuwa kazi yoyote ya sanaa hupata taswira yake kutokana na jamii inayohusika. Hivyo kadiri uchawi unavyotumika zaidi kwa uovu ndivyo itakuwa muhali kwa waandishi kuuenzi kwa njia ya maendeleo.
Hata hivyo badala ya kuulaani tu uchawi utokomezwe kulihali, waandishi wanaweza kufanya mambo mawili makubwa: kwanza, kuwahamasisha wenye taaluma ya uchawi waifundishe pasi na kificho. Pili, waitumie kwa nia ya maendeleo kama anayoonyesha Ibrahim Hussein katika Kinjeketile48 ambapo wazalendo wa Tanganyika waliazimia kuitumia taaluma ya uchaw kupigana na wakoloni wa Kijerumani.
Tanhihi
1. Hivi karibuni viongozi wa ngazi za juu kabisa hapa nchini wamedai kuwa uchawi ni imani isiyo na msingi.
2. Yusuf, A.A. (1983) The Holy Quran. Translation and Commentary. Al Rajhi Co., Maryland.
3. Agano la Kale, (1980) T.M.P., Tabora.
4. G. Parrinder, Witchcraft, European and African. Faber and Faber, London.
5. J. Middleton, (1963) Witchcraft and Sorcery in East Africa. Praegar, New York.
6. A. Murray, (1963) The Witchcraft ni West Europe, Clarendon Press, Oxford.
7. G. Michael, (1967) The African Witch. London.
8. A. Harwood, (1970) Witchcraft, Sorcery and Social Categories Among the Wasafwa, Orford.
9. A. Scobie, (1965) Murderfor Magic. Cassel, London.
10. E. Arnold, Witchcraft. London, 1969.
11. M. Douglas, (1970) Witchcraft: Confessions and Accusations, Tavistock Publications, London.
12. Parrinder, (m.y.k.) uk. 10
13. A.S. Homby, (1924) Oxford Advanced Learners Dictionary of Current English. Oxford University Press, Oxford, uk. 131.
14. TUKI (1981) Kamusiya Kiswahili Sanifu. Oxford, Dar es Salaam.
15. Parrinder, (m.y.k.) uk. 9. Makabila ya nchi mbalimbali za Afrika yanatajwa kuhusiana na imani hiyo ya uchawi, nayo ni pamoja na Basuto wa Basutoland, siku hizi Botswana, Lorendu wa Afrika Kusini, Yombo na Ibo wa Nigeria, na Azande wa Sudan.
16. k.h.j., 114.
17. Douglas, (m.y.k.) uk. 35. Mfano unaotolewa hapa ni wa tajiri mmoja aliyeitwa Nutters aliyeishi Lancashire, Uingereza, mnamo 1622.
18. Parrinder, (m.y.k.) uk. 9.
19. A.A. Yusuf, (m.y.k.).
20. k.h.j. uk. 45.
21. Agano la Kale, (m.y.k.) uk. 803.
22. Tanzania (1962) Fungu la 19, Sheria ya Ushahidi, Na. 6.
23. Fungu la 27 k.h.j.
24. Pamnder, (m.y.k.), uk. 143.
25. k.h.j., uk. 145.
26. Tanzania (1981) Elias Kigadye na Wenzake, Shauri la Jinai la Rufani Na. 41,1981, Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Dar es Salaam.
27. Douglas, (m.y.k.) uk. 305.
28. k.h.j. uk. 318.
29. k.h.i. uk. 318.
30. k.h.j. uk. 319.
31. k.h.i. uk. 320.
32. k.hJ. uk. 320.
33. TUKI (m.y.k.), uk. 131. Kizuu ni mtu aliyefunikwa kwa mazingaombwe ili kutumika nyumbani kwa uchawi; kijumbe cha uchawi.
34. A. Scobie, (1965) Murder for Magic. Cassel, London, uk. 96.
35. A.K. Armah, (1984) The Healers. Heinemann, Logos.
36. Wakati mwingine watu hutumwa kutafuta sehemu hizo za siri au viungo vya mwanadamu na kuviuza kwa anayevihitaji.
37. E. Mbogo, (1986) “Ngoma ya Mwanamalundi” (Muswada), Dar es Salaam.
38. C.G.M. Mung’ong’o (1977) Mirathi ya Hatari. TPH., Dar es Salaam, uk. 2.
39. k.h.j., uk. 2.
40. k.h.j., uk. 26.
41. A. Kondo, (1975) Fadhili Msiri wa Naugua. TPH, Dar es Salaam.
42. Mung’ong’o, (m.y.k.).
43. k.h.j., uk. 16.
44. k.h.j., uk. 25.
45. k.h.j., uk. 26.
46. S. Robert, (19/65) Masomo Yenye Adili. Nelson, Nairobi.
47. Watu kadha wa kadha, pamoja na viongozi wengine wa nchi hii, wamewahi kujikuta wametolewa nje wakati wa usiku bila ya kujijua, wengine wakiwa uchi wa nyama.
48. E. Hussein, (1969) Kinjeketile. Oxford University Press, Dar es Salaam.

Print this item

  KWA VIPI FASIHI NI SANAA?
Posted by: MwlMaeda - 07-16-2021, 02:37 PM - Forum: Nukuu - No Replies

Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa ambapo mtu hulitumia umbo hilo kueleza yale anayotaka wengine wayafahamu.
i. Matumizi ya mtindo katika kufikisha ujumbe. Mtindo humtofautisha mwanafasihi mmoja na mwingine. Kila mwanafasihi ana mtindo wake. Ufundi unakuja pale ambapo ufundi hutumika katika mtindo ambapo mambo kama, matumizi ya barua, dayolojia, monolojia na matumizi ya nafsi hujumuishwa.
ii. Matumizi ya muundo. Jinsi ambavyo visa hupangiliwa kwa ufundi mkubwa ili kuwezesha kuifikisha kazi ya fasihi kwa walengwa, ndiyo sanaa yenyewe. Maana yake ni kwamba, mwandishi hutumia ubunifu katika kupangilia visa na matukio.
iii. Matumizi ya lugha. Lugha itumikayo katika fasihi ni tofauti na lugha nyingine. Katika lugha ya fasihi kuna matumizi ya tamathali za semi, misemo, nahau na ujenzi wa picha na taswira. Haya yote yanaifanya fasihi iwe sanaa.
iv. Matumizi ya wahusika. Si kutumia wahusika pekee, bali ule uchaguzi mzuri wa wahusika huifanya fasihi iwe sanaa. Mwanafasihi anauwezo wa kuamua anataka wahusika wa aina gani katika kazi yake. Ana uwezo wa kumwacha hai mhusika mpaka mwisho wa kazi yake. Pia, ana uwezo wa kuyakatisha maisha ya mhusika yeyote.
v.  Matumizi ya mandhari. Jinsi mwandishi anavyojenga mandhari yake kwa ubunifu ndiyo huifanya fasihi ikawa sanaa. Kadiri mandhari inavyojengwa na mwandishi ndivyo inavyosaidia kuijenga kazi ya fasihi na kuifanya ieleweke zaidi kwa wasomaji.

  Misingi ya Uhakiki katika Fasihi ya Kiswahili
Posted by: MwlMaeda - 07-16-2021, 12:00 PM - Forum: Nukuu - No Replies

Misingi ya Uhakiki katika Fasihi ya Kiswahili

T.S.Y. Sengo
Madhumuni
Madhumuni ya makala haya ni kujaribu kuitafakari dhana ya uhakiki wa Fasihi ya Kiswahili na misingi inayoitawala na kuisimamia. Katika jaribio hilo, kutafanywa juhudi za kutoa maelezo ya dhana muhimu, kujadili misingi iliyopo na kupendekeza mingine, kudadisi na kueleza nafasi na kazi za mhakiki.
Maelezo
Uhakiki
Uhakiki katika Fasihi ya Kiswahili si taaluma yenye umri mkubwa. Umri wake haufikii hata robo karne. Dhana hii ya uhakiki kwa lugha ya kawaida, ina maana ya “upataji wa hakika au kweli ya jambo; maelezo yanayochambua maandishi kwa kufafanua mambo mbalimbali yaliyomo.”1 Upataji wa hakika au wa kweli ya jambo unahusu ujuzi mkubwa. Ujuzi huu si ule wa kiufundi na kisanii tu bali wa maarifa na hekima. Ajuaye ni yule mwenye uwezo wa kuona tofauti katika vitu vya kufanana na mfanano katika vitu tofauti, imani na itikadi tofauti, mazingira na hali tofauti, dhana na hoja tofauti, kauli na semi tofauti, na juu ya hayo atajua kuwa akiwezacho kujua si kila kitu na kwamba juu ya kila mwenye kujua kuna mjuzi zaidi. Hivyo maana ya uhakiki kuwa ni jitihada ya upataji wa hakika au kweli ya jambo yanazidi kuthibitisha hoja ya wanafalsafa kuwa kuhakiki sharti kukite katika kujua. Uhakiki hauwezekani kufanywa bila ya kuwa kinachohakikiwa kinafahamika ndivyo. Maana haya ndiyo yatakayotawala fikira za makala haya.
Ama kuhusu maana ya pili ya uhakiki kuwa ni “maelezo yanayochambua maandishi kwa kufafanua mambo mbalimbali yaliyomo,” ni dhahiri kuwa ufafanuzi huo sharti ukite pia katika kujua ndaninnje ya hilo jambo linalofafanuliwa, na fani ambayo imelipamba jambo lenyewe. Sharti iwekwe wazi kuwa si kila ufafanuzi ni uhakiki kwani maandishi ya fasihi yana mashiko yake mbali na yale ya maandishi mengine. Na makala haya yanashughulikia uhakiki wa maandishi ya kifasihi ambayo ni kazi zote za kisanaa zitumiazo maneno na viashiria mbalimbali. Na si fasihi yoyote bali Fasihi ya Kiswahili.
Uhakiki ni daraja ya juu ya maelekezo ya kisanii yenye kuwalenga watu wa aina tatu: wasomaji wa kawaida walio majumbani na maskulini, waandishi asilia wa kazi za sanaa, na watu wanaodhaniwa wana macho ya kuona na uwezo wa kutenda na kuyatafakari yasemwayo kwa lengo la kutengeneza. Msomaji hupata mwongozo wa namna bora zaidi za kumuwezesha kuifahamu kazi ya sanaa kutokana na viwango tafauti vya uhakiki tafauti juu ya shairi, ngano, riwaya, tamthiliya, n.k. Mwandishi hupata faraja na hamasa kutokana na uhakiki wa kazi zake, hukua na kukomaa; wachache labda hupata homa na kuingiwa na baridi kazi zao ziwekwapo sawa.
Uhakiki katika jadi za Kiswahili ndicho chuo kikuu cha mafundo makuu. Mathalani, katika maisha ya kila siku, methali huwakumbusha wanajamii: “Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu;” “Mgema ukimsifu tembo hulitia maji,” na “Haambiliki huachwa akaadhirika,” n.k. Hizi ni tahakiki za Idsanaa zinazotawala maisha ya kweli ya mja ya kila siku Uswahilini.
Kama uhaldki ni daraja kuu, ni wazi kwamba manyakanga wa chuo hicho sharti wawe watu wa aina yake. Si kila mfafanuzi wa jambo au mpataji kweli husibu kuwa mhakiki. Ni lazima uhakiki uwe umejikita katika ujuzi wa mtu ambave mzingiro wake wa kimaisha umepanuka na kupevuka na dari lake la akili na fahamu lina kina na kimo kikuu. Na ujuzi huo sharti uwe ujuzi ylio ndiwo kwa namna zote za kuutafutia na kuupatia; sharti uwe ujuzi wa kinadharia; misingi na utendaji kwa upande mmoja, na uwe wa umbuji mkuu kuhusu maisha ya jamii za watu na yao yote kwani fasihi huvielezea vyote vinavyowahusu watu hao na wala haichagui vile vya watu wasio duni wakiwa katika hadhara nyingine. Ama kwa hakika sanaa ya uhakiki ni sanaa kubwa na nzito inayodai umri na ukomavu wa aina yake. Haya hayako tu katika fasihi ya Kiswahili, fasihi ya Tanzania au fasihi ya Afrika tu bali yako katika misingi ya fasihi ya binadamu wowote na popote walipo. Kwa mfano, Thomas Cooke amepata kuandika kuwa “Ukuzaji wa ladha nzuri katika tungo za kishairi ndio ukuzaji pia wa tabia njema.” Kadhalika, “Hapana jingine linaloweza kulishughulisha taifa mbali ya uhimizaji wa waandishi bora.”2 Ni wazi kuwa mawazo haya yanaipa sanaa ya uhakiki nafasi, hadhi na dhima ya namna yake. Kanuni za kitu au jambo zimepewa sifa maalumu hapa ya kwamba zinahusiana sana na ubora wa tabia za watu, jamii na ubora wa yao.
Mhakiki
Mhakild ni msanii aliyekomaa katika nadharia, misingi na utendezi wa taalimu yake. Ni mkomavu wa kuona mengi katika sanaa anayoishughulikia. Tafsiri azitoazo huwa ndizo na zenye kulenga kuwanufaisha wasomaji, msanii wa kazi inayohakikiwa na hadhira kuu, yaani jamii. Ama mhakiki hawi ni “mlimaji” wala “mgongaji” kwani hizo ni ila katika sanaa ya kitaaluma, na si sifa kamwe. “Mlimaji” na “mgongaji” ni mtu atumiaye nguvu za mwili, sana hasira na hisia mfanano. Mhakiki hutumia ufundi, akili na hekima Kamwe mhakiki “halimi” wala “kugonga”.
Kusifu au kulaumu tu si sifa ya mhakiki bali ni haki yake na wajibu pia kuipima kazi kwa vigezo vyake na kusema kweli palipo ndipo. Msanii mstahiki sifa apewe na sababu zitolewe ili sifa hizo ziwe misingi kwa kazi zote nyingine za mithili hiyo.
Ni stahiki ya mhakiki kuitwa mwalimu kwani choyo na inda ya kuwaua wasanii watangulizi au wengine si sifa ya mhakiki kama ilivyo kwa mwalimu azalishaye madaktari, wahandisi na marais. Mhakiki hana gere wala tamaa ya kutaka awe yeye tu na wengine siwo. Na kwa kuwa mwalimu huyu kapevuka vya kutosha, upevu na ukomavu wake humpa hadhi ya mapenzi ya kweli. Ndipo Mtume Muhammad (S.A.W.) alipomfafanua mhakiki kwa maneno yafuatayo: “Ndiye mpenzi pekee yule ambaye atanionyesha udhaifu wangu na kunipa zawadi kwa kufanya hivyo.”3
Hivyo mhakiki ni yule na lazima awe yule ambaye huwa ni mfasiri wa jadi ya jamii anayoiwakilisha. Kazi yake hutegemea athari za muundo wa jamii, hisia, vigezigezi vya vionjo vya mwili, maumbile, wakati, pahala na hali nzima ya kuwepo kwa dunia ya sanaa ya uhakiki. Mwelekeo wake huwa ule wa ndani – nnje na wala si ule wa nnje – ndani. Jadi ya jamii moja huitawala jamii na jamii ikajithaminisha kwayo. Na mhakiki ni mlezi wa jamii yake kwa vile aitakiavyo kheri ya kuendelea zaidi na zaidi katika matengenezo ya vipengele vyote vya maisha ya mja bila ya kuua mlolongo wa jadi ya sanaa wala ya wasanii. Kwa taadhima kubwa, yafaa ikumbukwe kuwa “mhakiki ni mtu na kila mtu ana mipaka yake.”4
Fasihi ya Kiswahili
Kiswahili kwa asili ni lugha ya Waafrika walioishi pwani ya Afrika Mashariki kwa karne na karne. Kiswahili ni Kipwani, ni lugha iliyozaliwa kwa mchanganyiko maalumu wa lugha za Kibantu za jamii za awali ambazo zililazimika kuwasiliana zilipokabiliana baharini au nchi kavu. Kiswahili ni lugha ya muungano wa tamaduni kabla na baada ya majilio ya wageni. Historia hii ya awali iliparaganywa sana na wanasiasa wateule waliojificha katika maziaka ya utaalamu na, au umisionari.
Waarabu walipofika katika upwa wa Afrika Mashariki waliwakuta watu na lugha zao. Kuwaita “watu wa pwani” (sawahil) haikuwa na maana ya kuwa watu hao waliletwa na Waarabu, ama waliwazaa na wanawake weusi wa pwani hiyo. Waliokuja kutoka kwao walibakia kuwa Waarabu, Wamanga, Washihiri, n.k., na vizazi vyao vilivyochanganya damu viliendelea, hadi hivi leo, kuitwa Machotara. Mswahili kabakiza weusi na Uafrika wake.
Hivyo, kanuni za lugha – wiyati na zile za kijamii, zina dalili zenye nguvu kuwa jamii ya Waswahili wa pwani ya Afrika Mashariki isingeishi bila ya lugha kusubiri majilio ya wageni kwa vile ni maumbile ya waja kuwasiliana kwa kutumia lugha. Na kwa fikira za kitumwa ati Kiswahili kilikuwa zao la utumwa, Wazungu waliwatuma Waarabu kushika watumwa Afrika Mashariki, ukanda wa Sudani, Afrika Magharibi na kwingineko. Kwa nini basi Kiswahili kizaliwe na ubwana wa Waarabu waliokuja pwani ya Afrika ya Mashariki tu?
Falsafa nayo inaieleza lugha kuwa ndicho chombo pekee kinachounda na kutumia dhana. Falsafa hii inayoelezea utamaduni wa Kiswahili yaweza pia kuielezea Fasihi ya Kiswahili kwa kuwa ni fasihi iliyojitosheleza na kujikimu kistahiki.
Kwa hiyo, Fasihi ya Kiswahili ni taaluma ya maneno ya kisanii ya Waswahili, ya Wapwani. Makala haya yatakitisha fikira zake katika kweli hii. Hii haina maana kuwa madai ya kisiasa na ya kuhalalisha nafasi za kazi na masilahi ya kimaisha, hayana nafasi. Makala haya yanaheshimu mipaka ya mtumiaji Kiingereza na Mwingereza; mtumiaji Kichina na Mchina; mtumiaji Kinyanyembe na Mnyanyembe; na hali kadhalika Mpogoro aliyejifunza na kukitumia Kiswahili na Mswahili. Hii ni yakini ya kihesabu ambayo haihitaji mizengwe.
Fasihi ya Kiswahili, kwa hali hii ya pili, imekuwa na maana ya kazi za kisanaa zilizowasilishwa kwa Kiswahili. Inawezekana kuwa na fasihi ya Wangoni iliyoandikwa kwa Kiswahili. Sharti ionekane kweli iliyo dhahiri kuwa Ungonini si Uswahilini ingawa miongoni mwa Waswahili, Wangoni nao walikuwemo kama inavyozidi kujidhihirisha kuwa Wangazija wengi wa Visiwa vya Ngazija wana asili ya Umakua, Uyao, Umakonde wa kusini ya Tanganyika na kaskazini ya Msumbiji.
Hali hii ikiwekwa wazi, taaluma hukomaa. Ikionewa kinyaa, taaluma huzorota. Taaluma haitaki kuficha siri. Ndiyo sababu Fasihi ya Kingereza inafahamika kuwa ni Fasihi ya Waingereza na Fasihi kwa Kiingereza ndiyo ile yoyote nyingine iwayo bali hutumia Kingereza ikiwa ndiyo lugha ya mawasiliano. Na wataalamu wasionee haya fasihi zao za Kikwere, Kigogo, Kibondei, Kikerewe, Kipare, Kihehe, n.k., kwani zikipambanishwa na ile ya Kiswahili, kila moja ni fasihi ya hadhi yake na hapana moja iliyo bora kuishinda nyingine katika hali za kawaida.
Wasiwasi wa baadhi ya wanataaluma wa kudhani kuwa Kiswahili kimemeza lugha nyingine hivyo bora nao waiue asili va Kiswahili ili kila mtu awe MswahiB hauna mashiko ya kitaaluma wala ya ukomavu wa kitaalamu. Nao umewafikishia watafiti wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kupendekeza kuwa jina la taasisi hapo baadaye liwe Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili na Lugha nyingine za Tanzania na Afrika; ili lugha, tamaduni na fasihi nyingine nazo zifanyiwe kazi za stahiki zao.
Kinachosemwa katika sehemu hii ya makala ni kuwa Fasihi ya Kiswahili ni Fasihi ya Waswahili na Uswahili wao. Kadhalika, kwa sasa, Fasihi ya Kiswahili ina maana ya Fasihi yoyote itumiayo Kiswahili, kwa mfano kazi za waandishi kama Aniceti Kitereza.5

Misingi
Misingi ni vigezo vikuu na muhimu vya kufanyia kazi. Kwa haja ya makala haya, baadhi ya misingi hiyo ni pamoja na nadharia (za fasihi, jadi, utamaduni, n.k.), ukomavu (wa kitaaluma na kiumri), ukweli na haki, uwezo wa kisanii, mwelekeo, na lengo.
Nadharia
Mhakiki wa kazi za sanaa lazima aelimishwe na ahitimu katika taaluma za nadharia. Kuna siri nyingi muhimu katika nadharia za kila fani. Hivyo mhakiki anawajibika kuzimaizi kwa undani sana nadharia za fasihi anayoishughulikia. Ama ajue kuna sanaa za jadi, taalumaratibu ya sanaa nyingine, k.v., hadithisimulizi, thieta ya jadi (sanaa za maonyesho), methali, nyimbo, vitendawili n.k.; na kwamba kila kimoja cha hivi kina nadharia zake. Ajue kuna nadharia za ushairi kwa jumla na nadharia za ushairi wa Kigogo, ushairi wa Kimasai, ushairi wa Kiingereza, kadhalika ushairi wa Kiswahili. Ajue kuna riwaya, tamthiliya, hadithi fupi, na sanaa za muziki; na kwamba kila kimoja cha hivi kina nadharia zake.
Nadharia ni taalumadhahania ambayo inahitaji uwezo mkubwa wa mtu. Nadharia zina sehemu kubwa sana katika utenzi wa kitu au jambo lolote la maana. Mwalimu Kenneth S. Goldstein amepata kuwaambia wanafunzi wake kuwa: “Bila kupata mafunzo katika nadharia, kuna dalili za wazi kabisa kuwa mkusanyaji (mchunguzi) hatakuwa anajua ni matatizo yepi yanahitaji utatuzi.”6 Katika uhakiki wa fasihi bila kuhitimu katika nadharia, matokeo ni kuwa na watu wanaojitia katika sanaa hiyo ili “kulima” au ‘kugonga” wenzao ili nao wapate majina. Mfano mzuri wa “ugongaji” ni ule wa mtu anayemtaka kila mtu mwingine kuwa kama yeye au kuwa yeye kwa fikira na mwelekeo. F.E.M.K. Senkoro7 hafahamiki anadai nini katika misingi iliyowafanya kina Fr. F. Nkwera kusema “sanaa hutoka kwa Mungu”; au ufafanuzi wa kina John Ramadhani na wenziwe walipodai kipengele kimojawapo cha fasihi kuwa ni hisi, hadi kuthubutu kutumia lugha ambayo kabisa haitumiki katika taaluma kwa kuuita kila mtizamo wa watu hawa “mtizamo uliopotoka,” madai ambayo yanakingana na misingi ya kitaaluma. Kwani angeulizwa: “Wewe ni nani hasa katika fasihi hata uone sisi tumepotoka na wewe hujapotoka?” angepata taabu kutoa jawabu. Kama alivyopata kusema Mohamed Bakari kuwa kulithamini shairi, mara nyingine, inampasa mtu kuwa mwizi wa ulimwengu wa faragha wa mshairi,8 ndivyo iwezavyo kusemwa kuhusu mhakiki na ulimwengu wake wa faragha kimalezi, kiitikadi, kimwelekeo na kitaaluma. Mhakiki ni mtu, na watu ni watu na yao. Haimkiniki wahakiki wote wawe mtu mmoja kwa mawazo, itikadi, mwelekeo, n.k.
Hivyo nadharia ndicho kigezo kikuu cha kumwezesha mhakiki kufanya kazi yake ya kujenga jengo la taaluma juu ya matofali ya watangulizl wake. Anayo haki ya kujenga tofali bora zaidi lakini yu mweledi wa adabu za kutothubutu kubomoa msingi. Umbuji wa lugha yake na uwezo wake wa usanii humpa fursa ya kuziba ufa bila ya kujenga ukuta kwa hekima na maarifa.
Ukomavu
Katika falsafa ya elimu, kuna hoja zihusuzo “mzingiro wa maisha” na “dari ya akili”. Mambo haya mawili huenda na umri, elimu na safari za kuiga mazuri. Umri ukizidi, elimu ikipanuka na safari dhahiriya na dhahniya zikiwa nyingi, mtu hupanua mzingiro wake wa uzoefu katika maisha na kupandisha juu zaidi kimo na kina cha dari yake ya akili. Maisha yanapoanza katika umri wa miaka arubaini, kama mtu keshapitishwa katika mfumo bora wa elimu, kapata kisomo na elimu, hususani huwa mpevu na mkomavu wa mengi. Ukomavu wa kitaaluma utamfanya amheshimu kila mtu na kila kifanywacho na wengine. Huwa yu mweledi na mfahamivu wa mbinu na lugha ya kutumia kurekebisha pale ambapo panastahiki. Huwa yu mtu wa kutoa maoni yake na mara nyingi kukiri kuwa hutafautiana na maoni ya fulani ama fulani kwa sababu za kimsingi kadhaa.
Kwa kuwa yu mtu mzima kiumri, magomvi ya kitoto ya kushikana mashati au kumwagiana mchanga si fakhari tena ya mhakiki. Bali huwa mtu mstahiki wa busara itakiwayo na mwandishi au mtunzi wa kazi ya fasihi, msomaji au msikilizaji wa kazi hiyo, kadhalika na athari ya kazi kwa jamii yake, kwake mwenyewe na kwa wahakiki wenziwe.

Ni dhahiri kuwa mhakiki anahitajika awe mpevu katika nadharia na taaluma kwa jumla, katika misingi ya kitaalamu; na kama ana mwelekeo wa kiutamaduni, kisiasa, kiuchumi, kisanii, n.k., awe pia amekomaa katika hayo. Na msingi wa ukomavu ndio mmojawapo’uliolipa taabu sana bara la Afrika kwa kuwa viongozi wake wengi kwa robo karne ya mwanzo wa uhuru hawakuwa nao. Ukomavu wa kisiasa wataka ukomavu wa kiuchumi, kielimu na kiitikadi ili Mwafrika naye ajihisi kapevuka katika kuchangia ukweli na haki.
Nadharia na ukomavu humfanya mtu aandikapo kuhusu fasihi ya Kigogo aanze na Ugogo wenyewe, Wagogo wenyewe, na misingi inayoutawala utamaduni huo. Huu ni mwelekeo wa ndaninnje. Si kweli na si haki kwa mhakiki wa fasihi ya Kiswahili kutumia nadharia au misingi ya fasihi ya Kiarabu, Kijerumani, Kichina au Kihindi kwa kisingizio cha kuwa fasihi ni fasihi. Mja ni yuleyule popote alipo, lakini fasihi yake ni kizaliwa cha utamaduni wa mazingira yake. Si vibaya kuanza na ndani mwa Mswahili kabla ya kumpambanisha na ndugu yake wa “ubantuni” au “ubinadamuni”. Kwa mfano, undani wa mpwani ni pamoja na athari za bahari na itikadi zote zitawalazo maisha yake; dini yake. Mpwani haoni haya kukiri ana Mwenyezi Mungu mwenye uwezo na nguvu, na kwamba mbele yake, yeye Mswahili si lolote si chochote; kwamba maisha mazima ya mja ni upuuzi, hayana maana ila kwa mtu afanyaye ibada na kazi za kuzalisha na kubadilisha hali ya kiuchumi, kisiasa, kijamaa na kuleta amani miongoni mwa watu. Kucha Mwenyezi Mungu ni adili la maisha, halina kusoma ama kutokusoma. Tambiko, jando, unyago, n.k., ni sehemu ya jadi ambayo hubadilika kidogokidogo kwa athari za wakati, maendeleo, n.k. Na kila kimoja katika hivi kina kanuni za mashiko ambazo mhakiki wa mwelekeo wa ndaninnje sharti aziheshimu.

Makala haya yanadai kuwa kweli isemwe na haki ifanywe kuhusu kazi za fasihi. Mwandishi anayeimba nyimbo za kimapinduzi sharti atazamwe yeye mwenyewe alivyo na anavyoishi. Je, yeye mwenyewe ni mwanamapinduzi anayeyajua mapinduzi? Si mnafiki anayetaka labda kuuza maandishi yake katika soko maalumu? Au katili linalotaka kuua watu kwa jaribio lake la siasa? Jamii ya mwandishi itazamwe jinsi inavyompokea na kumthamini mtu huyo. Nayo ipimwe kama kweli inao uwezo wa kumjua mtu aliye ndiye na mtu asiye ndiye. Je, mwandishi huwachezea shere watu wake kiasi gani? Kama yu avaa kindenga, chatosha kumtia katika uwanamapinduzi? Kama yu avaa baraghashiya, yatosha hiyo kumtia katika kundi la waumini? Elimu yake je? Uwezo wake je? Familia yake je?
Hatua hii huenda ikaonekana imechupa mipaka ya kitaaluma na kuingilia mambo ya Idbinafsi. Mwono huo ni wa kitaaluma ambao umetoka nnje ya tamaduni za Kiafrika. Ni mwono wa nnjendani. Uafrikani na Uswahilioi, mtu huthaminiwa kwa vile alivyo mzimamzima. Na mhakiki anapoitathmini kazi ya fasihi sharti aitazame kweli na haki katika ukamilifu wake.

Uwezo
Uwezo wa kisanii katika uhakiki ni jambo la msingi sana. Mhakiki wa riwaya, kwa mfano, si lazima sana awe mwanariwaya yeye mwenyewe, lakini yafaa awe msomaji wa riwaya nyingi sana. Awe ni mpenzi, mtafiti na mtu wa kuzitafakari riwaya. Awe mjuzi wa vigezo na misingi ya riwaya. Ajue riwaya ni nini, miundo na mitindo mbalimbali, wahusika na matukio mbalimbali, tamathali za usemi ambazo ndizo ziko katika uhalisia wa jamii inayohusika. Kadhalika mhakiki wa tamthiliya au wa mashairi, tenzi, ngonjera, nyimbo, n.k. Kanuni za kila fani ya fasihi sharti zipewe nafasi na haki yake. Uwezo hupatikana kwa ari, mafunzo, ukomavu, uzoefu, na kukubali kuoneshwa njia. Nao hukua kadiri ya mhakiki akuavyo. Kwa mfano, kina Kiango9 wa juzi si sawa tena na wa leo. Na kila mhakiki wa kweli hupigania kukuza uwezo wake siku hadi siku.
Mwelekeo
Baadhi ya wapitiaji au wachambuzi hupenda kuwa na “misimamo” katika kazi zao. Kwa daraja ya mhakiki, kuwa na ndoto hiyo ni hasara. Msimamo huwapo katika mijadala ya kishule au labda ya kisiasa. Na mtu sharti asi-mame alipo ili apiganie upande wake. Mhakiki yeye ni mtoa hoja na sababu. Hoja zake na sababu zake zionyeshwapo zinatafautiana na za wengine, mhakiki mkomavu hujifunza haraka iwapo atatosheka na sababu ya kubadili au kuongezea hoja maoni yake. Kigeugeu cha mhakiki si ila: ni sifa mradi tu aseme wazi kuhusu mabadiliko hayo. Ni dalili ya kukua na kuendelea.
Mwelekeo huathiriwa sana na mazingira, malezi, nadharia, na ukomavu wa mtu. Katika Fasihi ya Kiswahili, mhakiki hana nafasi ya kuelekea kwenye dharau au matusi dhidi ya dini kwani utamaduni wa fasihi hiyo umejikita katika imani nzito ya kuwako kwa Mwenyezi Mungu mmoja, mitume, malaika, n.k. Uyakinifu katika fasihi hiyo ni ule wa asilimia kwa mia wa ki-Mungu-mungu; kweli ambayo haishindani wala kulinganishwa na udhanifu wa kisayansi ambao bado binadamu anaufanyia kazi. Mifano ni kanuni za maumbile na kanuni za matokeo ni yakini isiyotoa. Udhanifu wa “atom” iliyosemwa ni chembe ndogo isiyoweza kubabadilika, leo si “atom” tena, ni “neutron”.
Kinyumenyume cha matumizi haya ya uyakinifu na udhanifu kimekusudiwa kuonyesha kwamba kuna haja ya kuzama zaidi katika mambo kabla wahakiki hawajayapamia.
Na viwe viwavyo, mja katika ukamilifu wake haishi kwa mkate tu. Hivyo mielekeo ya uhakiki isiwakanganye wahakiki hadi wakafika kuparaganyika. Mradi washenzi na waungwana wamo maishani pamoja, watake wasitake, sharti wahakiki washirikiane kwani huo ndiwo mtihani waliopewa. Na wahakiki wa Ki-Marx au Ki-Mao sharti wathamini kazi za wahakiki wenzao ambao fikira zao zimekita kwa “Baba Mtakatifu” au kwa “Muhammad (S.A.W.)” au “Mizimuni”, n.k. Vinginevyo wataulizwa: “Nyinyi ni kina nani kudai haki ya kuwa wahakiki bora kutushinda sisi ati kwa kuwa tunatafautiana mielekeo? Marx na Mao wana ubora gani wa kumshinda Yesu na Muhammad?”
Lengo
Lengo la mhakiki ni kujaribu kutumia uwezo wake kusaidia kuifahamisha kazi anayoihakiki kwa mtu aliyeiandika na kwa msomaji. Katika jaribio hili, mhakiki akiwa mwalimu, atakosoa penye kustahili na kuelekeza penye kustahiki. Sifa za wazi atazisema ili wengine wapate kuziiga pindi waonapo zawafaa. Ila nazo zitaonyeshwa ili mwenye nazo aziache na asiye nazo aziepuke. Mradi lengo la mhakiki litabakia kuyatengeneza mambo yawe na yazidi kuwa mazuri. Huu ni wajibu wao kama anavyodai Abdilatif Abdalla kuwa: “Na itakuwa ni wajibu wao kuyasahihishamakosa yaliyokwisha fanywa.na hao waliotangulia.”10 Na watayafanya hayo kitaaluma na kihaki-liliahi, yaani kikwelikweli na kwa uaminifu mkubwa sana.
Nafasi na Kazi ya Mhakiki wa Fasihi ya Kiswahili
Nafasi
Ni jambo la mantiki kwamba mhakiki ni kiungo cha lazima katika fasihi yoyote iwayo. Haingekuwa kinyume cha hivyo kuwa katika fasihi ya Kiswahili mhakiki hana nafasi, haiyumkiniki. Nafasi yake inahitajika zaidi kwa vile taaluma hii haina umri mkubwa baada ya kuwa imeanza katika miaka ya 1970. Mzee John Ramadhani na Farouk Topan ni miongoni mwa waasisi wa uhakiki katika Fasihi ya Kiswahili. Athari ya kazi zao ndiyo iliyowazaa akina Kiango na Sengo wa siku za uchanga wao, na vijukuu akina Mulokozi na Senkoro; na Mbunda Msokile ambaye kawa mchambuzi mkuu wa vitabu redioni na kwenye magazeti, hasa Kiongozi. Ni wazi kuwa mhakiki bado anahitajika sana na ataendelea kuhitajika sana. Kwani yeye ndiye mwalimu na kiungo cha kazi ya fasihi na jamii iliyokusudiwa kinyume na wazo kwamba “sanaa yaweza kujisemea yenyewe”.11 Yaweza kweli, lakini sanaa hiyo sharti iwe pamoja na usanii wa mhakiki.

Kazi
Mwanafunzi wangu A.G.N.M. Gibbe, katika makala yake ya “Dhima ya Mhakiki”12 amesema ya kutosha. Kiasi kikubwa kaathirika na nyimbo, mavazi, hamasa na hata fakhari za uwanamapinduzi ambao ulishika sana Afrika Mashariki na Kati katika miaka 1965/80. Katika Tanzania, uwanamapinduzi uliofasiriwa na vijana wasomi ulihusu sana jitihada za kina Mao za kukana uunguungu na kuhimiza uunguwatu. Wachina baada ya Mao wamerudisha imani zao kwa Mwenyezi Mungu na wanamapinduzi wa Tanzania waliendelea kwenda kuabudu siku za Jumapili, na walio wakaidi sana hawakuacha kumtaja Mungu waliposhikwa na gego au malaria. Wengine wengi walibakia na Mwenyezi Mungu wao mmoja na mkweli daima. Hii haina maana kuwa hapajakuweko wanamapinduzi wa kweli ambao tamaa zao, sala zao na juhudi zao ni kuyatendea haki, kweli na kazi maisha ya jamii zao ili mabadiliko ya hali katika elimu, uchumi, siasa (ukweli, upole, uammifu n.k,), na vipengele vyote vya maisha ya kila siku yawe yakidhihirika kwa kila mwananchi, na pasiwe mmoja akawa anadai hadiya za kuwa mbele ya wenziwe. Hivyo basi baadhi ya kazi za mhakiki ni pamoja na:
Quote:
(i) Kuchambua na kuweka wazi funzo ambalo linatolewa na kazi ya asihi.
(ii) Kuchambua na kufafanua picha za kisanii zilizotumika katika kazi ya fasihi.
(iii) Kumshauri mwandishi ili afanye kazi bora zaidi.
(iv) Kumuelekeza msomaji ili apate faida zaidi kuliko yale ambayo angeweza kuyapata bila ya dira ya mhakiki.
(v) Kuhimiza na kushirikisha fikira za kihakiki katika kazi za fasihi.
(vi) Kuweka, kubakiza, na kukuza kiwango cha utunzi na usomaji wa kazi za fasihi.
(vii) Kuonyesha kuwa kwa kila kizuri kuna kizuri zaidi na hapana kizuri kisicho dosari.
(viii) Kutafiti na kuweka sawa nadharia za fasihi teule.
(ix) Kusema kweli ipasayo kuhusu tamaduni na falsafa zinazotawala fasihi.
(x) Kuheshimu na kuthamini kazi za waandishi kwa kuzifanyia haki, n.k.
Maoni
Makala haya kwa jumla yamejaribu kupendekeza mambo kadhaa yanayomhusu mhakiki. Mwandishi wa awali wa kazi za fasihi hakupewa nafasi sana. Kiwango cha mapitio na uchambuzi wa kazi za fasihi, ambacho kimekuwako tangu fani hii ilipoanza katika fasihi ya Kiswahili, kimesemwa hakitoshelezi sifa za kiwango cha uhakiki. Ni maoni ya mwandishi wa makala haya kuwa mhakiki wa fani ya fasihi sharti awe amesoma siyo nadharia na kazi kadhaa za fasihi tu bali pia sharti awe amehitimu katika taaluma za falsafa ya fasihi, falsafa ya sanaa kwa jumla, na katika nadharia za uhakiki na uzoefu wa utendezi wa kazi hiyo.
Kazi, karibu zote zilizochapishwa, zinahusu uchambuzi wa kazi za fasihi ambazo zinasomwa maskulini. Hivyo lengo kuu ni kujaribu kuzieleza na kuzifahamisha kazi hizo kwa wanafunzi na kwa walimu wao. Mwalimu John Ramadhani, Mwalimu Farouk M. Topan, baadaye akina Saifu Kiango, na kufuatiwa na kina Mwalimu Mwarabu Mponda, Mwalimu M. Mulokozi na F. Senkoro – wote hawa wamezielekeza kazi zao kwa wanafunzi na walimu wao, iwe ni shuleni, vyuoni au vyuo vikuu. Kwa mawazo yaliyokusudiwa karatasini humu, wote hao wamekuwa wakifanya kazi za uchambuzi, ufafanuzi, usaili, upitizi, na sanaa za ualimu.
Uhakiki wataka kiwango cha juu zaidi cha uandishi wa kazi za fasihi, k.v., Siku ya Watenzi Wote, Kusadikika, Mashetani, Jogoo Kijijini, na mifano ya hizo; ukomavu wa hali ya juu katika taaluma, nadharia, falsafa, maisha na uwezo wa kupima na kuamua haki. Lengo liwe ni kuzihakiki kazi hizo kwa ajili ya wahakiki wapevu ili nao wazihakiki kwa upevu huo.
Hitimisho
Makala yamejaribu kujadili dhana na misingi ya uhakiki wa fasihi ya Kiswahili. Fasihi hii ni ya upwa wa pwani ya Afrika Mashariki, na ina umri mkubwa na athari nyingi za maingiliano ya jamii. Hivyo mhakiki wa kazi zote za fasihi hii sharti aujue na kwa kiasi kizuri authamini utamaduni wake ambao ni pamoja na dini za jamii, itikadi na imani zao, falsafa na mielekeo yao, kanuni na ada zao, ushenzi na uungwana wao, n.k.
Makala yamehimiza utafiti katika fasihi ya Kiswahili na fasihi za Kimakonde, Kirangi, Kiziguwa, Kikae, Kitumbatu, n.k., ili uhakiki uwe unapiga ndipo.
Fasihi ya Kiswahili, kwa maana ya fasihi ya Kigogo kwa lugha ya Kiswahili, au fasihi ya Kimbulu kwa lugha ya Kiswahili, ina nafasi kubwa katika malezi na elimu ya taifa hili. Muhimu, mhakiki lazima aseme ni fasihi ya watu fulani anayoishughulikia.
Mwisho wa yote, makala yamesema kuwa uhakiki ni usanii mpevu sana unaohitaji kula chumvi nyingi katika mengi. Nao umejikita katika kweli na haki, na usafi wa nia. Na kwa mapendekezo yaliyotolewa, kuna matumaini kuwa taaluma hii itakuzwa na kukomazwa.
Tanbihi
1. TUKI (1981) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press, Dar es Salaam, uk. 196.
2. Terry Eagleton (1984) The Function of Criticism. London, uk. 14 (tafsiri yangu).
3. Mtume Muhammad (S.A.W.) Katika Kauli zake thabiti za Hadithi za kuaminika.
4. A.G.N.M. Gibbe (1978) “Dhima ya Mhakiki” katika Mulika 12. TUKI, Dar es Salaam, uk. 5.
5. M.M. Mulokozi na D.P.B. Massamba (wh.) (1984) Kiswahili 51/1 & 51/2. TUKI, Dar es Salaam, uk. xi.
6. Kenneth S. Goldstein (1964) A Guide for Field Workers in Folklore. Folklore Associates. Pennesvlvania Inc., uk. 17.
7. F.E.M.K. Senkoro (1982) Fasihi. Press and Publicity Centre, Dar es Salaam, uk. i.
8. Mohamed Bakari (1981) “Swahili Islamic Literature and Westem Literary Critics”. Unpublished paper presented at the Conference of the Nile Valley Countries. IAAS – University of Khartoum, uk. 15.
9. S.D. Kiango na T.S.Y. Sengo (1973) Hisi Zetu, TUKI Dar es Salaam; Ndimi Zetu (1974) Longman, Tanzania Ltd., Dar es Salaam.
10. Abdilatif Abdalla (1975) “Utangulizi” katika T.S.Y. Sengo. Shaaban Robert. Longman Tanzania Ltd., Dar es Salaam, uk. xxv.
11. Eagleton,k.h.j., uk. 42.
12. Gibbe,k.h.j., kur. 2-8.

Print this item

  NYIMBO ZA FASIHI SIMULIZI
Posted by: MwlMaeda - 07-16-2021, 08:12 AM - Forum: Ushairi - No Replies

Fasihi simulizi ya kiafrika ina aina mbalimbali za nyimbo kulingana na matukio:
Nyimbo: Nyimbo ni kila kinachoimbwa. Kipera(aina) hiki kimegawanyika katika vijipera vifuatavyo ambavyo ni, tumbuizo, bembea, kongozi, nyimbo za dini, wawe, tenzi, tendi, mbolezi, kimai, nyiso, nyimbo za vita, nyimbo za uwindaji, nyimbo za taifa, nyimbo za watoto na nyimbo za kazi.
Tumbuizo: hizi ni nyimbo za furaha ziimbwazo kuwafurahisha watu kwenye matukio mbalimbali kama vile ngomani au harusini. Bembea; hizi ni nyimbo za kubembeleza watoto. Kigezo kilichotumika hapa ni kigezo cha kidhima ambapo hulenga kubembeleza watoto.
Kongozi:hizi ni nyimbo za kuaga mwaka.
Nyimbo za dini:hizi ni nyimbo zinazoimbwa kwa lengo la kumsifu Mungu au miungu.
Wawe:hizi ni nyimbo za kilimo; huuimbwa wakati wa kulima.
Tenzi:hizi ni nyimbo ndefu za kimasimulizi au mawaidha.
Tendi:hizi ni nyimbo ndefu za masimulizi juu ya matendo ya mashujaa, wahusika wa tendi ni watu wenye historia za matendo ya kishujaa.
Mbolezi:hizi ni nyimbo za kilio au maombolezo.
Kimai:hizi ni nyimbo zihusuzo shughuli za baharini.
Nyiso:hizi ni nyimbo za jandoni.
Nyimbo za vita:hizi ni nyimbo ziimbwazo na askari wakati wa vita..
Nyimbo za watoto:hizi ni nyimbo waimbazo watoto wakati wa michezo yao.
Nyimbo za uwindaji:hizi ni nyimbo ambazo huimbwa na makundi ya wawindaji wakati wa shughuli au sherehe zao.
Nyimbo za Taifa:hizi ni nyimbo za kusifia Taifa au kabila.
Nyimbo za kazi:hizi ni nyimbo zinazoimbwa katika shughuli mbalimbali kama vile, kulima, kutwanga, kusuka, uvuvi, uashi, useremala na kadhalika
Maghani: Maghani ni istilahi inayotumiwa kuelezea aina ya ushairi ambao hutolewa kwa kalima au maneno badala ya kuimbwa.Kipera(aina) hiki kina vijipera vitatu ambavyo ni maghani ya kawaida,sifonamaghani masimulizi.Maghani ya kawaidani kundi ambalo tunaweza kuingiza fani mbalimbali za ushahiri simulizi kama vile ushairi wa mapenzi, siasa, maombolezo, kazi, dini ilimradi unaghanwa katika namna ya uwasilishwaji wake.
Sifo:hizi ni tungo za kusifu ambazo husifu watu, wanyama na mimea. Baadhi ya sifo huwa zinakashifu au kukejeli. Sifo huwa na aina muhimu kama vile vivugo (majigambo),pembezinatondozi.
Kivugo:hili ni ghani la kujisifia, hutungwa na kughanwa na muhusika mwenyewe.
Tondozi:hizi ni tungo za kusifu watu, wanyama au vitu.
Ghani masimulizi:hizi ni ghani ambazo hutambwa ili kusimulia hadithi, historia au tukio fulani. Ghani masimulizi ina aina vinne ambavyo ni rara, ngano, sifo na tendi.
Rara ni hadithi fupi nyepesi ya kishairi yenye visa za kusisimua; rara huimbwa au kughanwa ikiambatana na ala za muziki.
Ngano:hizi ni hadithi za mapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu katika kuelezea au kuonya kuhusu maisha.Ngano huwa ghani masimulizi inapowasilishwa pamoja na ala ya muziki.
Sifo:hizi ni tungo za kusifu: sifo huwa ghani masimulizi inapoingiza muziki katika utondozi wake, lugha iliyotumika ni lugha ya kishairi.
Tendi:hizi ni ghani ndefu za masimulizi juu ya matendo ya mashujaa yenye uzito kijamii au kitaifa.

Print this item

  Utungaji Wa Kazi Za Kifasihi
Posted by: MwlMaeda - 07-16-2021, 08:03 AM - Forum: Uandishi/Utungaji - No Replies

Kazi za fasihi simulizi hazikutokea tu, zilitungwa. Mtu fulani alikaa na akatunga kazi fulani ambayo inajulikana katika jamii. Katika mada hii utajifunza kanuni mbalimbli zinazohusika na utunzi wa kazi za fasihi simulizi. Pia utapata fursa ya kujifunza jinsi ya kutunga kazi mbalimbali za fasihi simulizi kama vile ngonjera, methali , nahau, vitendawili na kazi nyingine. Utajifunza pia kanuni zinazoongoza utunzi wa kila kazi ya fasihi simulizi.

Mashairi
 
Kanuni za Utungaji wa Mashairi
Uandishi wa kubuni unamtaka mtunzi atumie milango yake ya fahamu kinagaubaga. Kuna milango ya fahamu mitano ambayo ni pamoja na: kuona, kunusa, kusikia, kuhisi, na kuonja.
  • Kuona: je, mhusika unayemfikiria kichwani mwako unamwonaje? Umbo lake ni la kuvutia au kuchusha? Je, macho yake yakoje – je ni ya golori au la? Ni makubwa au madogo? Je, ni mlemavu wa macho?
  • Kunusa: pua zako zinakufanya usikie harufu gani? Je, ni harufu mbaya au nzuri? Je, ni uvundo au marashi? Je, mhusika wako ananuka kikwapa au uturi? Je, ananuka mdomo?
  • Kuhisi: je, unapokaa karibu naye unajihisi nini? Je, unapata mhemko wowote au huhisi chochote? Je, akikupapasa mwilini mwako unajisikia nini? Akikugusa bega unajisikia nini?
  • Kuonja: je, ukiweka kitu hicho mdomoni unaonjaje – ni chungu au tamu? Je, ina pilipili au masala? Je, kuna chumvi au sukari? Je, kitu hicho kina ukakasi au uchachu?
  • Kusikia: je, sauti unayoisikia ikoje? Inamtoa nyoka pangoni? Inakufanya ukose usingizi? Je, ni sauti nzuri au mbaya? Ni nyororo au nzito? Kama ni sauti ya muziki – je, iko chini au juu (kelele)?
Uzoefu wa Mwandishi
Uzoefu ni hali ya kukaa au kujishughulisha na jambo au kitu kwa muda mrefu. Mwandishi ana uzoefu (uzoevu) wa kukabiliana na maisha kwa kiasi gani? Je, ni matatizo gani ambayo umekutana nayo katika maisha yako? Je, ni mafanikio gani umekutana nayo katika maisha yako? Kwa mfano, katika ajali ya MV Spice (2011) kuna baadhi ya watu waliokolewa na magodoro ya Tanzania? Magodoro haya yana nailoni na je kama yasingekuwa na nailoni? Uzoevu/uzoefu wako ukoje?
Uchunguzi/utafiti
Uchunguzi unapaswa ufanywe na mwandishi ili aweze kuandika jambo au tukio bila kuongopa. Kwa kufanya udanganyifu, mwandishi atapoteza imani yake kwa wasomaji wa kazi zake.
Uchunguzi ili ufahamu au ujue mtu, mnyama, mdudu na kadhalika – anatembeaje, anakulaje, analalaje, anaishije, anachekaje, analiaje, anazaaje, anahusianaje na wenzane na mazingira yake? Haya ni maswali muhimu katika kumwezesha mtunzi kufanya utafiti wa kina ili ajue kitu anachotaka kukiandika akiandikaje na akiwasilishaje ili aweze kuikamata hadhira(walengwa) yake.
Mwandishi baada ya kuzingatia mambo haya sasa anaweza kuanza kutunga kazi yake. Hapa sisi tutajikita zaidi katika utunzi wa mashairi. Kabala hatujaenda katika hatua ya utunzi ni muhimu kujua dhana ya shairi kwa ujumla wake, na baada ya hapo tutakuwa tumekwisha pata maarifa yakutosha juu ya mashairi ambayo yatatuwezesha kutunga mashairi.
Dhana ya shairi
Shairi ni kipande cha maandishi kilichopangwa kwa utaratibu katika mistari. Sauti za silabi hufanana zikiwa kati au mwisho mwa mstari. Maandishi hayo yakisomwa huleta ujumbe na hisia fulani ya kimaisha.
Mpango wa maneno ya shairi, ambao huweza kuimbwa hutoa picha wazi, maana halisi na burudani ya kimuziki. Nyimbo nyingi za makabila zimepangiliwa kishairi ijapokuwa hazikuandikwa.
Mashairi yana umbo ambalo huonekana kwa mpangilio wa sauti na idadi ya maneno katika mistari. Umbo hili hutofautisha shairi na tenzi. Kuna mambo kadhaa yanayotakiwa kufahamika kuhusu shairi, nayo ni:
Beti – Kifungu kimoja cha shairi ambacho kina uzani sawa.
Vina – Ni mwisho wa mistari ambayo huwa na silabi zenye sauti ileile mwishoni mwa sentensi.
Mizani – Ni idadi zilizo sawa za silabi katika kila mstari, ubeti hadi ubeti.
Kituo – Huu ni mstari wa mwisho wa ubeti. Kuna vituo za aina tatu:Kituo cha bahari – ni mstari unaotoka mwanzo hadi mwisho bila kubadilika katika kila ubeti;Kituo cha kimalizio – ni kituo ambacho mstari wa mwisho maneno yake hubadilika ubeti hadi ubeti;Kituo nusu bahari – ni mstari wa mwisho ambao maneno yake nusu hubadilika na nusu hubaki kama ulivyo ubeti hadi ubeti.
Katika mashairi (ya kimapokeo), kila mstari lazima uwe umekamilika na ubeti uwe na maana kamili.

Vipengele za fani katika mashairi
Vipengele za fani katika shairi ni pamoja na:
Jina / anwani
Mandhari
Wahusika
Muundo –tathnia, tathlitha, tarbia, tathamisa, sabilia n.k
Mtindo – pindu, msisitizo, beti kubadilishana vina, kurudiwa kipande kizima cha mstari wa mwisho kikiwa ni chanzo cha ubeti unaofuatia.

Vipengele za Maudhui kati mashairi
Vipengele za maudhui ni pamoja na: migogoro, ujumbe, falsafa, msimamo, mtazamo, na dhamira za mwandishi.Matumizi ya ushairi ni pamoja na: kuomboleza, kubembeleza, kuliwaza, kufundisha, kuburudisha, kukosoa, na kadharika.
Baada ya hapa sasa unaweza kuanza kutunga shairi lako la kwanza.
Kuigiza Ngonjera
Katika kuigiza ngonjera muigizaji hana budi kuzingatia fani yenye kanuni zifuatazo; mtindo wa mashairi ya kimapokeo, muundo wa mashairi ya kimapokeo wenye mizani, vina, vipande, mishororo na beti, kuteua mandhari kutegemeana na mada, kuwepo kwa wahusika wawili au zaidi au makundi mawili au zaidi na matumizi ya lugha ya kishairi.
  1. Maigizo
  2. Kanuni za Utungaji wa Maigizo
Maigizo ni tendo la kuiga sura, tabia, matendo na mazungumzo ya watu au viumbe wengine yaani kuiga jinsi walivyoumbwa, wanavyotembea, wanavyovaa, wanavyosema n.

Hatua za kutunga maigizo
Kuchagua wazo, tendo, visa au tukio la kuigizwa:Ni lazima jambo hilo liwe na uzito, umuhimu au athari fulani katika jamii. Matukio hubainika kutokana na utafiti. Matukio yanayoweza kuwa kiini cha kutungiwa maigizo ni kama vile matumizi mabaya ya simu za mkononi, mitindo ya mavazi, madhara ya uganga wa kienyeji, madhara ya UKIMWI n.k.
  • Kuchagua muktadha au mahali pa kutendeka kwa jambo:Muktadha waweza kuwa ofisini, shuleni, kijijini, mjini, barabarani, kwenye daladala n.k
  • Kuamua mtindo wa kuwasilisha jambo la kuigizwa:Hapa mtunzi anaweza kutumia fumbo, vichekesho, historia, tanzia n.k. Inashauriwa mtunzi kuchanganya mbinu ili kuongeza mvuto.
  • Kupanga hoja kuu zinazojenga maudhui ya igizo:Maudhui hujikita katika migogoro au mivutano. Suluhisho la mivutano hupatikana pale migogoro inapofikia kilele. Kwa mfano jamabazi sugu anapokamatwa.
  • Kuweka mpangilio wa maonyesho:Maonyesho hujumuisha vitendo na hoja zinazokamilisha sehemu inayobeba aina moja au zaidi ya maudhui. Sehemu kadhaa nazo hukaa zikajenga kitendo ambacho hubeba jambo mojawapo muhimu. Katika migawanyo hii yapasa mtunzi atunge kauli na vitendo vinavyoandamana navyo.
  • Kubuni wahusika na kuweka aina au idadi yao kulingana na matukio:Mtunzi anashauriwa kutumia wahusika wanaohitilafiana. Kwa mfano wazee, vijana, wanawake, wanaume, wanene, wafupi n.k. Mtunzi akishawateua anaweza kuwatungia kauli na zamu za matendo katika sehemu mbalimbali.
  • Ni muhimu pia kwa mtunzi kuwaumba wahusika wake na kuamua maleba yao:Uamuzi huu yapasa ufanywe kwa kuzingatia mazingira. Kwa mfano siku hizi sio lazima wahusika wazee kuvaa ngozi, kutumia mkongojo na kuvuta mtemba.
    Urefu wa maigizo ni suala la kuamliwa kutegemea tukio
Kutunga maelezo kuhusu mandhari:Maumbile ya wahusika na vitendo zao, ni muhimu kuelezwa katika mabano.
Kuandika maigizo na kuhariri:Ni muhimu kutumia lugha ya kimazungumzo inayovutia, yenye kuleta taharuki na yenye utamu unaoeleza maadili kwa mnato.

Print this item

  UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI
Posted by: MwlMaeda - 07-16-2021, 07:31 AM - Forum: Uandishi/Utungaji - No Replies

  1. Utungaji wa Hadithi
  2. Mikondo(aina) ya Hadithi
Kazi za fasihi andishi ni sanaa, yaani zinahitaji ubunifu wa mwandishi ili ziwe katika mwonekanao huo wa kisanaa. Fasihi andishi hutumia lugha na wala sio lugha tu bali lugha ya kisanaa, kama tulivyokwishaona katika mada zilizotangulia kwamba lugha ni kipengele muhimu sana katika fasihi. Ili kazi ya kifasihi ya msanii husika iwe nzuri na ya kuvutia, masanii hana budi kuwa na ubunifu wa hali ya juu katika kutumia lugha.
Msanii awe na uwezo wa kupangilia maneno, kuteua maneno katika hali ya ujumi lakini pia yakiwa yamebeba ujumbe unaoigusa hadhira(walengwa) yake. Kwa maana hii mwandshi wa kazi za kifasihi, iwe riwaya au tamthilia ni lazima azingatie sana lugha, kwani lugha ndio nyenzo kuu ya usanaa wa fasihi kwa ujumla.
Kuna hatua kadhaa za kuzingatia wakati wa kuandika kazi ya kisanaa, hatua hizo ni kama zifuatazo:
  • Kuwa na kisa/wazo unalotaka kuliandikia:Katika jamii kuna mambo mengi sana yanayotendeka, msanii anaweza kupata wazo la kiubunifu kutokana na mambo hayo yanayotendeka katika jamii. Kama tujuavyo fasihi andishi kazi yake ni kuonesha yale yanayotendeka katika jamii, kwa hiyo msanii anaweza kutumia fursa hiyo ili kuweka wazi mambo yanayoendelea katika jamii. Kwa mfano mwandishi naweza kutunga kazi ya kibunifu kuhusu, ufisadi, umasikini, mapenzi, ndoa, maisha yake mwenyewe, ushirikina, jambo lolote analoliamini katika maisha (falsafa yake). Kwa hiyo hatua ya kwanza kwa msanii kabala ya kuandika ni kuelewa vizuri jambo analotaka kuandikia. Pia katika hatua hii msanii anaweza kubuni jina la hadithi yake, pia hii inaweza kumsaidia katika upangaji wa visa na matukio ya hadithi yake.
  • Kuchagua umbo la kazi ya fasihi: Msanii akishapata wazo la kuandika, sasa inambidi achague jinsi atakavyoliwasilisha wazo lake hilo. Yaani anaweza kuchagua endapo aandike hadithi fupi, riwaya au tamthiliya, au ushairi au utenzi. Sasa uchaguzi wa umbo la kazi ya fasihi unategemeana na uwezo wa msanii katika aina hizo, kuna mwingine anapenda tamthiliya lakini kuandika riwaya hawezi, kuna mwingine anaona kuandika ushairi ni rahisi na kuna mwingine hawezi. Kwa hiyo ubunifu wa msanii utadhihirika katika uaina ule anaoumudu vizuri zaidi.
  • Kubaini hadhira(walengwa): Mwandishi kujua yule anayemwandikia ni suala la msingi sana. Hadhira(walengwa) ipo ya watu wa aina mbalimbali, watoto, watu wazima, wasomi, wenye elimu ndogo, wakulima, wanasiasa n.k. Sasa mwandishi akishabaini hadhira(walengwa) anayoindikia itamsaidia kuteua lugha ya kuandikia, kwa mfano kama ni watoto, hatutegemei mwandishi kutumia lugha ngumu, misemo na nahau nyingi.
  • Kubuni wahusika na mandhari: Mwandshi baada ya kujua kazi yake inahusu nini sasa inambidi abuni wahusika wa hadithi yake. Wahusika wanaweza kuwa ni watu, wanyama, mimea, mazimwi, malaika n.k. Pia ni lazima abaini mazingira ambamo visa vyote za hadithi na matukio yatakapofanyika. Mandhari yanaweza kuwa baharini, kijijini, mjini, mbinguni, kuzimu n.k
  • Kupanga msuko wa visa na matukio:Msuko wa visa na matukio ni muhimu sana katika usimulizi wa hadithi. Sasa kama mwandishi amaeamua kuwasilisha kazi yake kwa njia ama ya hadithi fupi au riwaya au tamthiliya ni vema ajue namna visa na matukio vitakavyopangwa. Katika kufanya hivi maswali yafuatayo ni muongozo mzuri katika kupangilia ploti: Hadithi yangu itaanzaje? Mgogoro utaanzaje? Ni kati ya nani na nani? Je, kilele cha mgogoro ni nini? Je, ni mhusika mkuu kubakwa na kuambukizwa VVU? Hadithi yangu inaishaje? Je mhusika mkuu ashindwe? Atorokee nje ya nchi? Afungwe? Abadilike Au maadui ndio wafungwe au wafe? Au wabadilike?
  • Kuanza kuandika: Sasa baada ya kupitia hatua hizo zote, mwandishi sasa anaweza kuanza kuandika. Mchakato wa kuandika hua ni mrefu na mwandishi anaweza kujikuta anafuta mara nyingi kile alichokiandika, hii ni kutokana na kwamba mambo mengi ya kuandika huwa yanakuja wakati mwandishi ameanza kuandika kazi husika. Hata hvyo sio vibaya kufanya hivi, hii pia inasaidi kuwa na zao bora la fasihi.
 
  1.  hadithi
Hadithi ni masimulizi ya kubuni yaliyoandikwa kinathari inaweza kuwa na wahusika wengi, matukio mengi na mandhari mapana (inategemena na aina ya hadithi, iwapo ni hadithi fupi wahusika wake huwa ni wachache na pia matukio ni machache, mandhari yake pia ni finyu). Kuna aina zifuatazo za hadithi kulingana na kigezo cha urefu au maudhui. Kwa kigezo cha urefu kuna Hadithi Fupi na Riwaya. Kutokana na maudhui kuna Riwaya Dhati na Riwaya Pendwa.
Riwaya dhati ni zile zinazozungumzia masuala muhimu ya kijamii, kama vile uonevu wa tabaka la chini, rushwa, uongozi mbovu n.k
Riwaya pendwa ni hadithi zenye lengo la kuburudisha, kutokana na usimuliaji wake uliojaa taharuki na fantasia. Mambo yanayosimuliwa katika riwaya hizi ni yale yanayogusa hisia za watu kwa urahisi kama vile mapenzi, mauaji, ujasusi n.k.
Mikondo(aina) ya uandishi wa hadithi
Mkondo wa hadithi ni mwelekeo ambao mwandishi anaufuata katika utunzi wa kazi yake. Mikondo(aina) ya utunzi wa hadithi ni pamoja na hii ifuatayo:
Mkondo wa kiwasifu; mkondo(aina) huu huhusisha hadithi zote zinazosimulia maisha ya watu. Ni riwaya ambayo inasimulia maisha ya mtu toka alipozaliwa hadi wakati huo.
Mkondo(aina) wa kitawasifu; hadithi zinazofuata mkundo huu ni zile zinazosimulia maisha ya mtu binafsi yaani mwandishi mwenyewe. Kwa mfano riwaya ya “maisha yangu baada ya Miaka hamsini”. (S.Robert)
Mkondo(aina) wa kihistoria; hadithi katika mkondo(aina) huu zinahusu matukio ya kweli ya kihistoria yaliyotokea. Kwa mfano riwaya ya “Uhuru wa Watumwa”
Mkondo(aina) wa kipelelezi; hizi ni hadithi zinazozungumzia upelelezi wa uhalifu fulani kama vile ujambazi, wizi, rushwa, mauaji n.k.
Mkondo(aina) wa kimapenzi; katika mkondo(aina) huu zinaingia riwaya zote zinazozungumzia masuala ya mapenzi.
     2. Utungaji wa hadithi fupi
Kama tulivyokwisha ona hapo nyuma sifa za hadithi fupi, basi katika utungaji wake mambo yafuatayo ni sharti yazingatiwe:
  • Hadithi fupi inakuwa na mhusika mkuu mmoja ambaye anajitokeza sana kuliko wahusika wengine.
  • Idadi ya wahusika ni ndogo ukilinganisha na wahusika wa kwenye riwaya.
  • Mandhari ya hadithi fupi si mapana kama ilivyo katika riwaya
  • Hadithi fupi inakuwa inaongelea dhamira kuu moja tu ambayo inaonekana toka mwanzo hadi mwisho wa hadithi

Print this item

  UTUNGAJI WA TAMTHILIYA
Posted by: MwlMaeda - 07-16-2021, 07:20 AM - Forum: Uandishi/Utungaji - No Replies

.pdf   Dhima ya Tamthiliya.pdf (Size: 67.2 KB / Downloads: 4)

Print this item

  Karibu sana
Posted by: MwlMaeda - 07-16-2021, 07:09 AM - Forum: Kidato cha tano na sita - No Replies

Jukwaa hili linahusu maarifa ya ngazi ya sekondari kwa kidato cha tano na sita. Utapata nukuu, mitihani na maswali na majibu.

Print this item

  Karibu sana
Posted by: MwlMaeda - 07-16-2021, 07:08 AM - Forum: Kidato cha nne - No Replies

Jukwaa hili linahusu maarifa ya ngazi ya sekondari kwa kidato cha nne. Utapata nukuu, mitihani na maswali na majibu.

Print this item