UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Uandishi/Utungaji (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=12) +--- Thread: UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI (/showthread.php?tid=578) |
UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI - MwlMaeda - 07-16-2021
Kazi za fasihi andishi ni sanaa, yaani zinahitaji ubunifu wa mwandishi ili ziwe katika mwonekanao huo wa kisanaa. Fasihi andishi hutumia lugha na wala sio lugha tu bali lugha ya kisanaa, kama tulivyokwishaona katika mada zilizotangulia kwamba lugha ni kipengele muhimu sana katika fasihi. Ili kazi ya kifasihi ya msanii husika iwe nzuri na ya kuvutia, masanii hana budi kuwa na ubunifu wa hali ya juu katika kutumia lugha.
Msanii awe na uwezo wa kupangilia maneno, kuteua maneno katika hali ya ujumi lakini pia yakiwa yamebeba ujumbe unaoigusa hadhira(walengwa) yake. Kwa maana hii mwandshi wa kazi za kifasihi, iwe riwaya au tamthilia ni lazima azingatie sana lugha, kwani lugha ndio nyenzo kuu ya usanaa wa fasihi kwa ujumla.
Kuna hatua kadhaa za kuzingatia wakati wa kuandika kazi ya kisanaa, hatua hizo ni kama zifuatazo:
Hadithi ni masimulizi ya kubuni yaliyoandikwa kinathari inaweza kuwa na wahusika wengi, matukio mengi na mandhari mapana (inategemena na aina ya hadithi, iwapo ni hadithi fupi wahusika wake huwa ni wachache na pia matukio ni machache, mandhari yake pia ni finyu). Kuna aina zifuatazo za hadithi kulingana na kigezo cha urefu au maudhui. Kwa kigezo cha urefu kuna Hadithi Fupi na Riwaya. Kutokana na maudhui kuna Riwaya Dhati na Riwaya Pendwa.
Riwaya dhati ni zile zinazozungumzia masuala muhimu ya kijamii, kama vile uonevu wa tabaka la chini, rushwa, uongozi mbovu n.k
Riwaya pendwa ni hadithi zenye lengo la kuburudisha, kutokana na usimuliaji wake uliojaa taharuki na fantasia. Mambo yanayosimuliwa katika riwaya hizi ni yale yanayogusa hisia za watu kwa urahisi kama vile mapenzi, mauaji, ujasusi n.k.
Mikondo(aina) ya uandishi wa hadithi
Mkondo wa hadithi ni mwelekeo ambao mwandishi anaufuata katika utunzi wa kazi yake. Mikondo(aina) ya utunzi wa hadithi ni pamoja na hii ifuatayo:
Mkondo wa kiwasifu; mkondo(aina) huu huhusisha hadithi zote zinazosimulia maisha ya watu. Ni riwaya ambayo inasimulia maisha ya mtu toka alipozaliwa hadi wakati huo.
Mkondo(aina) wa kitawasifu; hadithi zinazofuata mkundo huu ni zile zinazosimulia maisha ya mtu binafsi yaani mwandishi mwenyewe. Kwa mfano riwaya ya “maisha yangu baada ya Miaka hamsini”. (S.Robert)
Mkondo(aina) wa kihistoria; hadithi katika mkondo(aina) huu zinahusu matukio ya kweli ya kihistoria yaliyotokea. Kwa mfano riwaya ya “Uhuru wa Watumwa”
Mkondo(aina) wa kipelelezi; hizi ni hadithi zinazozungumzia upelelezi wa uhalifu fulani kama vile ujambazi, wizi, rushwa, mauaji n.k.
Mkondo(aina) wa kimapenzi; katika mkondo(aina) huu zinaingia riwaya zote zinazozungumzia masuala ya mapenzi.
2. Utungaji wa hadithi fupi
Kama tulivyokwisha ona hapo nyuma sifa za hadithi fupi, basi katika utungaji wake mambo yafuatayo ni sharti yazingatiwe:
|