MALIKA "MWANAKUPONA ALIYEFANIKIWA KUKATA RUFAA YA KIFO "
Na.
HEMED KIVUYO
"Wangu muhibaka sikuhizi sikuoni,tangu kuondoka moyo upo msibani,sijui hakika ilokuudhi Ni Nini,naomba tamka unijuze kwa yakini ,Mimi nakutaka Wewee,nakupenda weweee"
Ni baadhi ya mashairi yaliyopo katika wimbo wa Malika yaani Taarab. Malika Ni Nani,yupo wapi ,na kwanini kafanikiwa kukata rufaa ya kifo?
AISHA ABDULY MAARUFU KWAJINA JINA LA MALIKA . Ni mzaliwa wa Kismayuu Somalia .
Kumuelezea bi Malika yahitaji wigo mpana mno,lakini nitakufafanulieni kwa ufupi.
Malika Ni Mwimbaji hodari wa Taarab zenye kulalamikia Mapenzi ,na hata kushajihisha Mapenzi,Nk.
Nakosa lugha ya kumwelezea Mwanakupona huyu ambaye haishi kunitoa matozi kila nisikiapo sauti yake kupitia tungo zake ,Hana kifani.
Siwezi kuelezea sauti yake kupitia maandishi yangu,labda nikusihi usikize tungo zake.
Malika ameimba nyimbo nyingi mno za Taarab,baadhi ya ametunga na kuimba na baadhi ametungiwa na kuimba yeye mwenyewe .
Katika upeo wa mato yangu,bi Malika Ni Mwanamke mwenye sauti yenye kutibu maradhi yangu Mengi mno . "Napohisi uchovu sauti ya Malika imekuwa Nguvu kwangu,napodhihakiwa ,sauti ya Malika imekuwa tiba kwangu" Mwenyezimungu azidi kumpa Umri .
Baadhi ya Tungo zake maarufu Ni "WAPEWAPE VIDONGE VYAO" ZABIBU,YALAITI,NDUGU WAFAZA,NINGEULALIA MTO,STAKI STAKI,MWANAWAJINI
MR.MAHMOUD NK.
Hali ya usalama Nchini Somalia imekuwa hamkani kwa muda mrefu,Malika aliiacha Nchi yake kutokana na machafuko hayo na kuweka Kambi kwa muda mfupi Tanzania Kisha Mambasa Nchini Kenya .
Wakati Aliitwa Aisha Abduly jina lake halisi
Alipokelewa Kenya kwa shangwe na kuishi vyema,kutokana na Sauti yake si tu yakumtoa nyoka pangoni Bali hata Mamba MTO rufiji,Wakenya walimpa jina la Malika .
Na wakati anakaribia kuondoka Kenya akawaimbia " Metembea Nchi nyingi,lakini Kenya kufika kwangu ndiyo namba wani,siwati kuwakumbuka nyumbani kwetu kirudi" tawaombea wadudi"
Alitunga pia wimbo kuomba Vita simame Nchini Somalia na warejee Kama zamani.
"Ni Nchi yangu Somalia,nilozaliwa nikalelewa na maisha nikayajua,leo yamekuwa hayaa mola atatunusuru,Leo yamejiri haya"
Kama ilivyokuwa kwa Siti Bint Saad,hakukosa wasompenda. Baadhi walimwita majina mabaya Malika nakumtaka arejee kwao..
Akawajibu kwa Wimbo ,Wimbo uliitwa staki staki na baadhi ya mashairi yalisema hivi
"Staki staki stakiii japo kuwa sinachangu Mimi kunyanyaswa staaakii..staki stakii stakii japo Ni mnyonge Mimi kuonewa staakii"
Wimbo huu ulipendwa hata na maadui zake kwakua mwiba wa samaki humchoma hata mnunuzi.
Wimbo Zabibu pia ulikuwa maarufu Sana,na wengine hudhani uliimbwa na Bi Kidude laa hasha!
"Hiyo yako si Zabibu Ni tunda lililo na sumu,mempa mwenye imani roho ilomtulia,hiyo siyo kazi yangu Mimi kwenda uchawini ninaye mpenzi wangu wewe nikuroge Nini , huyu tenaa!!!!
Kuna wimbo uliitwa halohalo. Kulitokea kisa kimoja kwa Alhanisa Malika kupigiwa simu na mtu asiyemfahamu,akimsihi mtu huyu kujitambulisha lakini wapiii!
Malika akatunga wimbo "haloo haloo jina lake alifitaa hajulikani Ni nanii haloo haloo".
NINGEULALIA MTO.Wimbo huu mpaka hii leo umekuwa miongoni mwa nyimbo zenye kunitibu "kwa wakubwa na watoto wakubwa pambano mwao,kuna Mengi ya uzito,yangu hayawi nishanii..NINGEULALIA mtooo ningeulaliaa mto".
Jina la Malika lilikuwa maarufu mno Afrika na Ulaya,kila akitaka kurejea Somalia Basi Hali ya machafuko ilipamba Moto.
Aliendelea kuishi Kenya akiendelea kuimba Taarab ambayo nakiri huyu Mwanakupona wa ajabu ameletwa na Allah kwa kazi hiyo.
Alikutana na misukosuko kiasi Cha kutunga wimbo na kuuita misukosuko,hakuacha kitu Mwanakupona huyu .
Alitumia fasihi kuelezea umri wa kuoa na kuolewa,rejea wimbo "shebe nampenda shebe nampenda ntakula nishibe.
Malika ambaye alikoma kurejea Somalia kwasababu za dhahiri aliendelea kuomba Dunia iiisaidie Somalia irudi Kama zamani na warejee nyumbani.
Mwanamama huyu amekuwa maarufu Duniani,na miaka mingi iliyopita alipata makazi ya Kudumu Michigan Marekani anapoishi mpaka sasa.
Manju wa Mazuki Masou Masoud takribani miaka5 iliyopita alifanya naye mahojiano kupitia Radio Tanzania Sasa TBC.
Niliposkia mahojiano hayo nilihamaki Sana na dhahiri hayakuwa mahojiano ya simu Bali Ni ana kwa ana.
Nilidokezwa kuwa alikuja Dar es salaam kuhudhuria Harusi maeneo ya Kariakoo.
Kisha alirejea Marekani.Manju wa Mazuki Masou Masoud usirejee Tena dhambi hii yakutokunijuza ujio wa Bila Malika hata ukisikia yupo Kenya unijuze nimfuate angalau nimshike mkono tu .
Huyu ndiye Aisha Abduly maarufu Malika . Ambaye haotokufa fofofo Bali ataendelea kuishi kupitia tungo zake ambazo zitaishi dahari na DAHARI .
Malika amefanikiwa kukata rufaa ya kifo kwakuweka alama ya Taarab Duniani,wakati ambapo sura yake itakapotoweka Duniani ,sauti na tungo zake zitaendelea kutamalaki chini ya Jua .
Fasihi na tanzu nyingine za sanaa kama uchongaji, ususi, utarizi, muziki, ufumaji, uchoraji, ufinyanzi na maonyesho vinatofautiana kwa kiasi kikubwa kama ilivyoorodheshwa katika hoja hizi:
Kazi za fasihi hutumia lugha.
Kazi za fasihi hutumia wahusika.
Kazi za fasihi hutumia mandhari.
Kazi za fasihi huwa na utendaji ambao hujitokeza zaidi katika fasihi simulizi, ambapo, fanani na hadhira yake hutenda.
Kazi za fasihi zina fani na maudhui.
Huwa na uwanja maalumu wa kutendea
Hukutanisha fanani na hadhira ana kwa ana
Huweza kubadilika kulingana na wakati na mazingira mfano fasihi simulizi
Nyanya umeleta shida, kipi tulichokukwaza
Kila soko we ndo mada, watu wakuzungumza
Umetoweka kwa muda, na bei ukajikweza
Tunakukumbuka nyanya, tafadhali shuka bei.
Nyanya moja hadi jero, utadhani Coca-Cola
Unasakwa ngarenaro, bongo hadi ilemela
Waumiza wapogoro, chaga na kila kabila
Tunakukumbuka nyanya, tafadhali shuka bei.
Nakumbuka enzi zako, nyanya kumi mia mbili
Tukaangua vicheko, ukioza hatujali
Leo sasa zamu yako, umetupiga kabali
Tunakukumbuka nyanya, tafadhali shuka bei.
Kweli tulikudharau, tukakutupa jaani
Kumbe we hukusahau, ukayaweka moyoni
Leo umepanda dau, ndio tunakuthamini
Tunakukumbuka nyanya, tafadhali shuka bei.
Hatuli tena michuzi, tumebaki kulumanga
Zimekosa bei nazi, hunogi tena mpunga
Metunyima usingizi,vitambi vinatuchenga
Tunakukumbuka nyanya, tafadhali shuka bei.
Kukukata kachumbari, hakuna wa kuthubutu
Walala kwa matajiri, hutaki kurudi kwetu
Umekuwa mashuhuri, na hutukumbuki katu
Tunakukumbuka nyanya, tafadhali shuka bei.
Rafikizo bilinganya, kitunguu na karoti
Hawajui Cha kufanya, mbona umewasaliti
Na adui yako panya, kakumisi Sana eti
Tunakukumbuka nyanya, tafadhali shuka bei.
Lile chuzi shatashata, tulilomezea mate
Limekuwa pwatapwata, mradi tonge lipite
Kwa manji tunakukuta, na nyumbani kwa dangote
Tunakukumbuka nyanya, tafadhali shuka bei.
Ewe nyanya shuka bei, ili tuheme wanyonge
Kwa michuzi tujidai, yasitukwame matonge
Mama lishe wapo hoi, yanadorora magenge
Tunakukumbuka nyanya, tafadhali shuka beiii…!