Fasihi simulizi ya kiafrika ina aina mbalimbali za nyimbo kulingana na matukio:
Nyimbo: Nyimbo ni kila kinachoimbwa. Kipera(aina) hiki kimegawanyika katika vijipera vifuatavyo ambavyo ni, tumbuizo, bembea, kongozi, nyimbo za dini, wawe, tenzi, tendi, mbolezi, kimai, nyiso, nyimbo za vita, nyimbo za uwindaji, nyimbo za taifa, nyimbo za watoto na nyimbo za kazi.
Tumbuizo: hizi ni nyimbo za furaha ziimbwazo kuwafurahisha watu kwenye matukio mbalimbali kama vile ngomani au harusini. Bembea; hizi ni nyimbo za kubembeleza watoto. Kigezo kilichotumika hapa ni kigezo cha kidhima ambapo hulenga kubembeleza watoto.
Kongozi:hizi ni nyimbo za kuaga mwaka.
Nyimbo za dini:hizi ni nyimbo zinazoimbwa kwa lengo la kumsifu Mungu au miungu.
Wawe:hizi ni nyimbo za kilimo; huuimbwa wakati wa kulima.
Tenzi:hizi ni nyimbo ndefu za kimasimulizi au mawaidha.
Tendi:hizi ni nyimbo ndefu za masimulizi juu ya matendo ya mashujaa, wahusika wa tendi ni watu wenye historia za matendo ya kishujaa.
Mbolezi:hizi ni nyimbo za kilio au maombolezo.
Kimai:hizi ni nyimbo zihusuzo shughuli za baharini.
Nyiso:hizi ni nyimbo za jandoni.
Nyimbo za vita:hizi ni nyimbo ziimbwazo na askari wakati wa vita..
Nyimbo za watoto:hizi ni nyimbo waimbazo watoto wakati wa michezo yao.
Nyimbo za uwindaji:hizi ni nyimbo ambazo huimbwa na makundi ya wawindaji wakati wa shughuli au sherehe zao.
Nyimbo za Taifa:hizi ni nyimbo za kusifia Taifa au kabila.
Nyimbo za kazi:hizi ni nyimbo zinazoimbwa katika shughuli mbalimbali kama vile, kulima, kutwanga, kusuka, uvuvi, uashi, useremala na kadhalika
Maghani: Maghani ni istilahi inayotumiwa kuelezea aina ya ushairi ambao hutolewa kwa kalima au maneno badala ya kuimbwa.Kipera(aina) hiki kina vijipera vitatu ambavyo ni maghani ya kawaida,sifonamaghani masimulizi.Maghani ya kawaidani kundi ambalo tunaweza kuingiza fani mbalimbali za ushahiri simulizi kama vile ushairi wa mapenzi, siasa, maombolezo, kazi, dini ilimradi unaghanwa katika namna ya uwasilishwaji wake.
Sifo:hizi ni tungo za kusifu ambazo husifu watu, wanyama na mimea. Baadhi ya sifo huwa zinakashifu au kukejeli. Sifo huwa na aina muhimu kama vile vivugo (majigambo),pembezinatondozi.
Kivugo:hili ni ghani la kujisifia, hutungwa na kughanwa na muhusika mwenyewe.
Tondozi:hizi ni tungo za kusifu watu, wanyama au vitu.
Ghani masimulizi:hizi ni ghani ambazo hutambwa ili kusimulia hadithi, historia au tukio fulani. Ghani masimulizi ina aina vinne ambavyo ni rara, ngano, sifo na tendi.
Rara ni hadithi fupi nyepesi ya kishairi yenye visa za kusisimua; rara huimbwa au kughanwa ikiambatana na ala za muziki.
Ngano:hizi ni hadithi za mapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu katika kuelezea au kuonya kuhusu maisha.Ngano huwa ghani masimulizi inapowasilishwa pamoja na ala ya muziki.
Sifo:hizi ni tungo za kusifu: sifo huwa ghani masimulizi inapoingiza muziki katika utondozi wake, lugha iliyotumika ni lugha ya kishairi.
Tendi:hizi ni ghani ndefu za masimulizi juu ya matendo ya mashujaa yenye uzito kijamii au kitaifa.