07-17-2021, 06:53 PM
Fasihi na tanzu nyingine za sanaa kama uchongaji, ususi, utarizi, muziki, ufumaji, uchoraji, ufinyanzi na maonyesho vinatofautiana kwa kiasi kikubwa kama ilivyoorodheshwa katika hoja hizi:
- Kazi za fasihi hutumia lugha.
- Kazi za fasihi hutumia wahusika.
- Kazi za fasihi hutumia mandhari.
- Kazi za fasihi huwa na utendaji ambao hujitokeza zaidi katika fasihi simulizi, ambapo, fanani na hadhira yake hutenda.
- Kazi za fasihi zina fani na maudhui.
- Huwa na uwanja maalumu wa kutendea
- Hukutanisha fanani na hadhira ana kwa ana
- Huweza kubadilika kulingana na wakati na mazingira mfano fasihi simulizi
Mwl Maeda