“Tuseme hii ndiyo hatima ya utawala wangu?” Alijiuliza Mfalme Ntire akiwa mwenye majonzi makubwa. Akatangaza katika milki yake kuwa yeyote atakayefanikiwa kumuua Jemadari Nyangumi atampa robo ya milki yake.
Wakatoka wanaume wa miraba minne, wakajaribu kupambana na Jemadari Nyangumi lakini wakateketea wote. Jemadari Nyangumi alikuwa anakaribia kabisa kuteka ardhi yote ya Mfalme Ntare.
Akatoka Kadenge kama walivyozoea kumwita. Miguu yake imeangalia kushoto na kulia. Macho yake ni madogo mithili ya macho ya mamba.
Akafika kwa Mfalme akamwambia, “Mtukufu Mfalme, naomba ruhusa yako nikamng’oe huyo nduli.” Mfalme akamjibu akasema, “Mfupa uliomshinda fisi wewe utauweza/” Kadenge akasema, “Nitauweza Mfalme Mtukufu.”
Mfalme akamwambia, “Nakuruhusu uende lakini siwezi kuruhusu jeshi langu kuongozana na wewe maana ni aibu tupu,” Mfalme akasema huku akibinua mdomo. Kadenge akatoka akachukua jiwe lililokuwa katika kombeo lake akamwendea Jemadari Nyangumi. Jemadari alipomwona akacheka, akasema, “Wewe ndiyo nani? Jeshi huna, silaha nazo huna, njoo uone. Nitakuvunjavunja mbavu zako a nyama yako itakuwa chakula cha tai.” akasonya huku akisogea mbele kwa mikogo.
Kadenge akamwangalia, akarusha jiwe lililokuwa katika kombeo lake, likamgonga Jemadari Nyangumi kwenye paji la uso; akaanguka chini puu! Damu zikaanza kumtoka mithili ya maji ya bomba. Mwisho akaaga dunia.
Askari wa chini yake walipoona Jemadari amekufa, wakakimbia. Watu wote katika ufalme wa Ntare wakashangilia, wakambeba Kadenge mpaka kwa Mfalme.
Mfalme akafurahi, akamgawia Kadenge nusu ya ufalme wake, wala siyo robo. Watu wote wakafurahi sana. Mzee mmoja akasikika akisema, “mdharau mwiba mguu huota tende.”
Posted by: MwlMaeda - 08-22-2021, 09:36 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
KUSANYENI KAZI ZANGU
Leo nimewaza mbali, vipi kifo nikihozi,
Nimegutuka akili, niwachie kumbukizi,
Changu kifo kiwasili, niwachie simulizi,
Kusanyeni kazi zangu!
Vile nimetunga sana, beti mashazi mashazi,
Chunguzeni yenye vina, na mizani mabobezi,
Yaharirini kwa kina, hifadhini makavazi,
Kusanyeni kazi zangu!
Mfano ya Mnyapala, yule bwana mbobezi,
Basi siku nikilala, wa milele usingizi,
Fanyeni bila kulala, kutafuta tungo hizi,
Kusanyeni kazi zangu!
Maradhi mengi mwilini, hunijia siku hizi,
Uviko nao jueni, waleta maangamizi,
Heri niwaambieni, na isiwe shitulizi,
Kusanyeni kazi zangu!
Nimekaribia kupanga, miswada jozi kwa jozi,
Kipato kinanizinga, kinipacho pingamizi,
Vile bure ninatunga, tena kuache siwezi,
Kusanyeni kazi zangu!
Nafahamu wasomaji, sio kama hawawezi,
Hao ni kama walaji, na muweni watetezi,
Basi muwe wabebaji, kafanyeni uchambuzi,
Kusanyeni kazi zangu!
Nikikumbuka kaburi, kwacha kutunga siwazi,
Kwanza naongeza ari, hili niliseme wazi,
Nanyi pia mtakiri, ushairi ni mwokozi,
Kusanyeni kazi zangu!
Sikumjua Shabani, pasi kuziona kazi,
Shabani yu kaburini, ameacha simulizi,
Nitaacha kitu gani, mkitie simulizi?
Kusanyeni kazi zangu!
Mfano leo ajali, ikasimama pumzi,
Msilie nyie bali, yafanyeni maongezi,
Tangu tungo ya awali, kusanyeni msisizi,
Kusanyeni kazi zangu!
Bai bai nasimama, shairi siendelezi,
Shikeni niliyosema, muhimu habari hizi,
Fanyeni bila kukoma, ruhusa siwakatazi,
Kusanyeni kazi zangu!
MTUNZI NIMEZALIWA
nimezali mtunzi, Leo ndio kimbukizi,
Basi sote tuienzi, wazaliwa na wazazi,
Haya ya Mola mapenzi, Mfano hatuelezi,
Sasa pigeni miluzi, amezaliwa mtunzi.
Nimeona kunyamaza, ningewacha bumbuwazi,
Bayana ninaeleza, jambo hili wazi wazi,
Miaka nimetimiza, japo wazo sielezi,
Sas pigeni milizi, amezaliwa mtunzi.
Tumshukuru Jalali, peke yetu hatuwezi,
Ijapo Mimi sisali, na kuniacha hawezi,
Tangu nikiwa awali, hata macho siangazi,
Sasa pigeni milizi, amezaliwa mtunzi.
Sasa nimekua jama, nipeni maamukizi,
Muache kunisakama, ati mtoto wa juzi,
Nimekuwa nimesema, waulizeni Wazazi,
Sasa pigeni miluzi, amezaliwa mtunzi.
Basi nombeeni heri, zidisheni maombezi,
Mungu anipe fahari, ja yakuti na feruzi,
Yalo mema na mazuri, anipe huyu Mwenyezi,
Sasa pigeni miluzi, amezaliwa mtunzi.
Sendi mbele nasimama, pigeni tena miluzi,
Kuleni wali kwa nyama, la! Ogeni
mchuzi,
Mtunzi hapa nakoma, shairi siendelezi,
Sasa pigeni miluzi, amezaliwa mtunzi.
“LAZIMA afe! Lazima afe!” Komandoo Mlasi Kasanura Bamba alirudia tena kujiapiza. Damu ilikuwa imetapakaa sakafuni chumba kizima. Maiti kumi zisizo na vichwa zilikuwa mbele ya macho yake na nyingine zilikuwa zimetapakaa hovyo nje. Grand Kapakacha alikuwa bado kajificha nyuma ya mlango bunduki mkononi ,jambia kiunoni. Ni operesheni kabambe kweli kweli. Je, mambo haya yakoje? Ungana na mwandishi katika riwaya hii ya kusisimua.
BAADA ya kuona yule dereva hazinduki na bado damu zikiendelea kumtiririka masikioni, Grand K. hofu ilimwingia akadhani tayari ameishaua! “Balaa gani tena hili jamani la asubuhi asubuhi “, alilalama Grand K. kichini chini huku akimkodolea macho yule dereva pale chini. Akatimka mbio haraka na kuwaita wale walinzi wake wa nyumba waje kumsaidia. “Hajafa huyu, bado mzima! Amezirai tu!” alisema yule mlinzi Mzee ambaye muda mfupi uliopita alipata kisanga cha kupigwa na kutemewa makohozi na Grand K. kwa kosa la kulala usingizi juu ya magunia. “Sasa nyie endeleeni tu kumpa huduma ya kwanza, mimi nawahi mjini kwenye shughuli zangu nimeishachelewa sana!” aliagiza Grand K huku akiingia ndani ya gari na dereva mwingine.
Grand K na huyo dereva mwingine sasa walichoma mafuta kuelekea mjini huku dereva huyo akiwa amegubikwa na hofu moyoni kwa kuamini kwamba ipo siku na yeye yanaweza kummkuta kama hayo yaliyomkuta mwenzake aliyezimia leo.
“Leo utanipitisha kwanza kwa Bwana Ziro, kisha kwa yule Mhindi wangu, halafu utanipeleka pale Kisutu Chef’s Pride nikapate Yoga, sawa?… Baada ya hapo nitakwambia tena twende wapi”, Grand K. alimweleza dereva katika namna ya kuamuru. Tangu hapo ikawa sasa ni amri tu, “kata kushoto…..kata kulia!…..simama!….rudi nyuma kwanza!…..ingia kushoto…….mbele kidogo….!!” Na yule dereva akabakia kutii amri na kuitikia tu “Sawa Mzee!…..sawa bosi!….”
Baada ya mwendo mfupi hivi walifika nyumbani kwa Bwana Ziro, rafiki mkubwa wa Grand K. wanayeshirikiana katika biashara na miradi yake mbalimbali. Grand K. na Bwana Ziro ni marafiki vipenzi kwelikweli tena wa kufa na kuzikana. Siri zake zote Grand K. ni za Bwana Ziro na za Bwana Ziro zote ni za Grand K. Hakuna litakalomgusa mmoja halafu mwingine lisimguse. Walikuwa ni kama chuma na sumaku au pacha wawili.
Bwana Ziro yeye anaishi Mwenge jijini lakini maskani yake makubwa ni kwenye kituo cha Tax cha Mnazi Mmoja pale barabara ya Lumumba jijini ambapo mara nyingi hupenda kushinda pale akipiga soga , kucheza bao au drafti na wazee wa pale.
Baada ya kufika nyumbani kwa Bwana Ziro, Grand K. aliteremka na kuingia ndani. “Ooohooh….. Paka Mweusiumefika!”, alitania Bwana Ziro huku akitabasamu kwa furaha baada ya kumwona Grand K. “….Ohooh….Paka Mwanga haujambo?” alirudishia Grand K. kwa utani huku nae akicheka pia. Wenyewe Grand K. na Bwana Ziro wamezoea kuitana kwa majina hayo ya kimafumbo kila wanapowasiliana ili kuwatambua maadui zao au watu wasiowataka katika mambo yao. Basi wao na kundi lao zima la uharamia husalimiana kwa ishara hizo hizo kila wanapo wasiliana katika simu. Hapo kwa Bwana Ziro walizungumza kimya kimya kwa muda halafu mara Grand K. akaaga. “Nakutakia bravo rafiki yangu, Paka Mweusi hakosi nyama!”, alimalizia Bwana Ziro kumwambia Grand K. ambaye alikuwa akichapulisha mwendo kuelekea nje alikomwacha dereva na gari.
*************
BAADA ya kutoka kwa Bwana Ziro, sasa walielekea kwa yule Mhindi Bw. Somji Patel ambaye anaishi Upanga Mtaa wa Mathurada. Gari lilikata kona na kupinda upande wa kushoto wa barabara ya Morogoro likaingia barabara ya Umoja wa Mataifa. Halafu likapinda tena kona karibu na msikiti wa Tambaza likaingia kulia kwenye barabara moja ndogo ya lami. Liliongoza mbele kidogo likapinda kona kushoto na kusimama katika jumba moja kubwa la kifahari lililozungushiwa ukuta na mitambo maalum ya kuzuia wezi.
Dereva alipiga hodi mara tatu mara wakaona lango kubwa la kuingilia magari linafunguliwa na mtu mmoja mweusi wa makamo hivi ambaye bila shaka alionekana kuwa mmoja wa walinzi wa Bwana Somji.
“Vipi huyu bwana tumemkuta?” aliuliza Grand K. huku akiteremka kutoka garini. Kabla hata yule mlinzi hajajibu mara wakasikia sauti ya Somji mwenyewe ikijibu kwa furaha kutokea mlango wa ndani “Ohoo Bwana K. iko nakuja! Karibu muzuri dugu yangu.” Na mara Somji mwenyewe alitokea akiwa tumbo wazi. “Welcome my friend… Kuja kwa ndani”, Somji alimkaribisha Grand K. huku wote wawili wakiongozana kuelekea Sitting-Room.
Ni nadra sana kumuona Somji akitoka mwenyewe kuja kumpokea mgeni nje isipokuwa kwa wageni wake maalum kama Grand K. Mara nyingi Bwana Somji hungojea wageni waingie wenyewe ndani baada ya kutoa idhini kwa walinzi wawaruhusu kupita kama ni wageni wa maana. Ama kwa wageni wengine wa hali za chini basi hawaruhusiwi japo kukanyaga kizingiti cha mlango. Majibu yao yote hupatiwa hapo hapo mlangoni kupitia kwa wale walinzi. Lakini sio Grand K. Yeye akifika hapo Bwana Somji humchangamkia na kumnyenyekea utadhani yeye Somji ni mtumwa wa Grand K.
Baada ya kuingia ndani ya jumba hilo kubwa la kifahari lenye vyumba lukuki ndani, Somji na Grand K. walikwenda moja kwa moja hadi Sitting Room ambapo mke wa Somji alikuja kumlaki mgeni huyo maalum na kuwaletea vinywaji. Mara Somji akamtaka mkewe awapishe pale sebuleni yeye na Grand K. kwamba wana mazungumzo ya faragha. Mke wa Somji akawapisha pasi na tabu wakabaki wawili hao peke yao hapo ukumbini.
Bwana Somji ni mshirika mkubwa wa biashara na kikundi cha kina Grand K. ambacho yeye Grand K. na wenzie akina Bwana Ziro walikipa jina la “G-12 Operation”. Kikundi ambacho shughuli zake halisi hazijulikani.Hakuna anayezijua isipokuwa wenyewe akina Bwana Ziro. Basi Grand K. na Somji walizungumza kwa sauti ya chinichini ya kunong’ona pale sebuleni juu ya mambo yao fulani ya siri. Halafu wakaonekana kama vile wanabishana juu ya kitu fulani hivi kila mmoja akipinga maelezo ya mwenzake. “Pana bana, mimi iko mpa veve natosha bana”, alionekana kulalamika yule Mhindi. “Somji unaniangusha bwana rafiki yangu”, alijibu Grand K. huku akionekana kumbembeleza Somji kitu fulani. Miongoni mwa mambo waliyokuwa wakiyajadili hapo sebuleni kumbe ni pamoja na mauzo ya jumba moja la kifahari ambalo Grand K. amemuuzia Somji. Jumba hilo lililoko kule Kinondoni Shamba jijini ni mali ya urithi iliyokuwa ya marehemu kaka yake Grand K. aitwae Kasanura Bamba. Bwana Kasanura Bamba aliuawa miezi mitatu iliyopita kwa kupigwa risasi ya kichwani na mtu mmoja asiyejulikana. Lakini baadae wengi walimshuku huyo huyo Grand K. kwamba ndio aliyehusika na mauaji ya kaka yake huyo kama si yeye mwenyewe aliyemuua. Grand K. na kaka yake huyo Bw. Kasanura Bamba ni baba mmoja mama mmoja. Yeye Grand K. au Grand Kapakacha, jina lake halisi ni Kapakacha bin Bamba na huyo kaka yake ni Kasanura bin Bamba. Wote walizaliwa huko huko kwao Nkasi mkoani Rukwa. Hivyo baada ya kumuua kaka yake, Grand K. aliichukua nyumba hiyo ya urithi wa watoto wa Mzee Kasanura Bamba na kuiuza kwa Bw. Somji Patel. Sasa leo ndio alikuwa amefuata malipo ya nyumba hiyo hapo kwa Bwana Somji.
Baada ya kushindwa kuafikiana bei na Somji, Grand K. aliamua kumpigia simu rafikiye kipenzi Bwana Ziro ili kumtaka ushauri. “Hallow!”, Grand K. aliinua mkono wa simu na kuita pale sebuleni kwa Somji. “Hallow! PAKA Mweusi?”, aliita Grand K. katika simu. “Hallow PAKA Mwanga?”, ilijibu sauti ya upande wa pili ambayo bila shaka ilikuwa ni ya Bwana Ziro. Mara sauti hiyo ya upande wa pili ikaita tena, “PAKA shume?”. Sauti ya Grand K. nayo ikajibu, “Hakosi nyama!… Nani mchawi ?”. “Mbwa Koko!“, ilijibu sauti ya Bwana Ziro huku akicheka kwa sauti kubwa kwelikweli mle ndani ya simu. Somji alibaki kaduwaa tu akijionea malimwengu akabaki kamkodolea macho Grand K. pale kwenye simu.