SHAIRI: MTUNZI NIMEZALIWA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MTUNZI NIMEZALIWA (/showthread.php?tid=980) |
SHAIRI: MTUNZI NIMEZALIWA - MwlMaeda - 08-21-2021 MTUNZI NIMEZALIWA nimezali mtunzi, Leo ndio kimbukizi, Basi sote tuienzi, wazaliwa na wazazi, Haya ya Mola mapenzi, Mfano hatuelezi, Sasa pigeni miluzi, amezaliwa mtunzi. Nimeona kunyamaza, ningewacha bumbuwazi, Bayana ninaeleza, jambo hili wazi wazi, Miaka nimetimiza, japo wazo sielezi, Sas pigeni milizi, amezaliwa mtunzi. Tumshukuru Jalali, peke yetu hatuwezi, Ijapo Mimi sisali, na kuniacha hawezi, Tangu nikiwa awali, hata macho siangazi, Sasa pigeni milizi, amezaliwa mtunzi. Sasa nimekua jama, nipeni maamukizi, Muache kunisakama, ati mtoto wa juzi, Nimekuwa nimesema, waulizeni Wazazi, Sasa pigeni miluzi, amezaliwa mtunzi. Basi nombeeni heri, zidisheni maombezi, Mungu anipe fahari, ja yakuti na feruzi, Yalo mema na mazuri, anipe huyu Mwenyezi, Sasa pigeni miluzi, amezaliwa mtunzi. Sendi mbele nasimama, pigeni tena miluzi, Kuleni wali kwa nyama, la! Ogeni mchuzi, Mtunzi hapa nakoma, shairi siendelezi, Sasa pigeni miluzi, amezaliwa mtunzi. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |