Hakuna siku niliyojisikia vibaya kama siku moja nipo nyumbani, kama kawaida yangu nilikua nimelewa chakari, nimejilaza kwenye kochi. Hapo ni baada ya kumtukana mke wangu na kuwaambia wote waende jikoni.
Ilikua ni usiku, lakini baada ya muda njaa ilinibana, nilinyanyuka kwa kuyumbayumba kwenda jikoni ili kudai chakula ambacho mke wangu amepika nikiwa hata sijui pesa katolea wapi kwani asubuhi sikuacha chochote.
Baada ya kufika mlangoni nikiwa kabla sijaupiga teke kama kawaida yangu nilisikia sauti ya mtoto wangu wa miaka minne akimuuliza Mama yake. “Mama eti na sisi Baba yetu anakufa lini?”
Nilistuka, nikasimama na kuanza kusikilzia walikua wanazungumza nini. “Wewe mtoto nyamaza usiseme hivyo ni vibaya, tema mate chini!” Mke wangu alimkemea lakini mtoto hakujali.
“Sasa Mama mbona Dadada amesema Baba yake Juma amekufa, ameenda kwa Mungu na hatarudi tena, kwanini na sisi Baba yetu asiende ili tubaki wenyewe…”
Mtoto aliendelea kuongea, mke wangu alijaribu kumkanya lakini hakusikia aliendelea. Mtoto mwingine mkubwa binti yangu wa miaka kumi yeye alimkatisha kumuelewesha.
“Baba Juma anaenda kwa Mungu kwasababu ni mtu mzuri, Baba yeye hataenda kwa Mungu anaenda kwa shetani, haendi mbinguni….” Alimaliza kumuelewesha mdogo wake, mke wangu alichanganyikiwa zaidi, alijaribu kuwakanya lakini yule mdogo aliendelea…
“Heri Baba hata afe, maana anakupiga wewe kila siku ana sisi kutupiga. Mimi ningekua Rambo ningemuua paaap! Paaa! Pigo moja tu anakufa! Nikiwa mkubwa namuulia mbali” Alionge akwa kujigamba.
Mtoto aliendelea kuongea sasa kwa msisimko. Nilijikuta nasimama wima, pombe zote ziliniishia njaa ilikoma, nilianza kutembea kurudi sebuleni, nilishindwa hata kukaa. Niliingia chumbani na kuanza kujiangalia kwenye kioo.
Nimeyafanya nini maisha yangu. niliwaza nikikumbuka zamani nilivyokua nikitamani kuwa na familia nzuri, kua na mke mzuri na watoto ambao wananipenda.
Lakini sasa mtoto wangu mwenywe, mtoto wa miaka minne alikua anatamani mimi Baba yake kufa! Nilitamani kulia lakini nilijua haitasiadia, niliingia bafuni na kuanza kujitapisha, nilitapika pombe yote, nikaingia kwenye friji nikachukua bia zote na wine.
Nikaenda kuzimwaga kisha nikarudi jikoni, nikafungua mlango kistaarabu nikaumbaia mke wangu sasa nimecha pombe, naomba mnisamehe lakini sasa nimemaua kubadiliaka.
Tangu siku hiyo sijawahi kunywa pombe, kumpiga wala kumtukana mke wangu, nina amani na furaha kuliko kipindi chote. Kumbe manaynyaso niliyokua nikimpa mke wangu yalikua yakiniumiza mimi zaidi kuliko mke wangu.
***MWISHO
Kamwe hakuna furaha ya peke yako, huwezi kufurahi ukiwa mwenyewe, starehe ya peke yako ni starehe ya upweke. Mwanaume unahitaji familia ili uweze kusema unafuraha.
Kama familia yako inalia, mkeo analia basi jua huna furaha. Pia haikufanyi mwanaume kamili, haikufanyi mwanaume zaidi kuwatesa wanao au mke wako, inakufanya mwanaume mpumbavu tu!
Kama wewe ni baba jiulize je kwa unayotenda ipo siku mwanao atayasema haya?
Juma alimtumia meseji mke wake; “Samahani mke wangu sitaweza kuja kukuchukua, nipo Hospitalini hapa Mama amelezwa kapungukiwa damu ndiyo nahangaika watu wa kumuongezea”
Mkewe akajibu; Kwahiyo Mama yako ndiyo umemuona wa muhimu sana kuliko mimi, yaani mimi nipande Bajaji kisa Mama yako anaumwa, si umuache uje unichukue, unakaa huko kwani wewe Daktarai!
Gari yangu mwenyewe kisha unisumbue sababu ya Mama yako! Umesikia gari ya wagonjwa hiyo, ungetaka kumhudumia Mama yako si ungenunua ya kwako!”
Alituma meseji lakini hata kabla ya kujibiwa alipiga simu na kuzidi kutukana. Juma alimuuliza’; Kwahiyo ni muache Mama hapa nije kukuchukua?” Mkewe alimjibu, ndiyo kwani ukimuacha atakufa! Si ushasema yuko hospitalini! Si kuna madaktari huko!
Nitaendaje kwenye sherehe peke yangu kama vile sina mume!” Juma alikata simu na baada ya kama nusu saa hivi alikua nyumbani tayari kumchukua mkewe, kwahasira mke alipanda kwenye gari, walienda mpaka kwenye sherehe.
Sherehe ilianza, huku mke akinywa kwa hasira hakutaka hata kuongea na mumewe. Juma alikaa kimya akiwa na mawazo mengi kila mara akishikilia simu yake. Katika kipindi chote hicho mkewe hakumuuliza hata hali ya Mama.
Sherehe iliisha wote wakaingia kwenye gari kurudi nyumbani. Walilala mpaka asubuhi mkewe akiwa hajamuulizia chochote. Asubuhi walijiandaa kwajaili ya kwenda kazini, wakati wanatoka Juma alimuuliza mke wake.
“Kwahiyo nikupeleke kazini au unakwenda kwanza kumuangalia Mama yako? Hali yake jana ilikua mbaya na sijui kama alipata watu wa kumuongezea damu?” Mkewe alistuka, jicho limemtoka.
“Mama yangu! nani kakuambia Mama yangu anaumwa, mimi mbona niliongea jana nayeye alikua mzima kabisa!” Huku akitabasamu Juma alimjibu.
“Jamani jana si nilikuambia Mama anaumwa hali mbaya kalazwa hospitalini?”
“Uliniambia lakini hukuniambia kama ni Mama yangu!”
“Jamani mke wangu sisi si ni mwili mmoja, sasa niliposema Mama nilikua na haja gani ya kusema Mama yangu au wako, kwamaana ninavyojua Mama yangu Mama yako na Mama yako ni Mama Yangu.
Huku akilia. “Sasa ndiyo ukamuacha Mama hospitalini, kwani kapatwa na nini? Yaani unanaicha na sherehekea kumbe Mama yangu anaumwa!”
“Alipata ajali ya gari jana, akapoteza damu nyingi, sasa hospitalini kulikua hakuna damu ndiyo nikawa natafuta watu wa kumuongezea, sema uliposema niache kuhangaika naye ndiyo nikaacha sasa sijui hali yake inaendeleaje maana alizidiwa sana.
Huku akilia mkewe aliingia kwenye gari kwa kasi akimtaka mumewe aendeshe gari kwa haraka, Juma aliendesha gari taratibu akipitia ofisini kwao kusaini, mkewe alilalamika lakini alimuambia kuwa hawezi acha kusaini kwenda kumuangalia Mama.
Kwa namna alivyokuwa amechanganyikiwa mkewe alishindwa hata kuendesha gari hivyo ilibidi amsubiri mumewe waondoke wote. Njia nzima mkewe alikua akilia, Juma akitabasmu tu.
Mkewe alijua Mama yake alishakufa kwa kukosa damu kwani kwa hali aliyoelezewa alijua kuwa hawezi pona. Alifika na kuwakuta ndugu zake wako nnje, aliwasalimia na kuwauliza hali ya Mama walimuambia aingie kumuona.
Alizidi kuchanganyikiwa akijua Mama yake kashafariki. Alifika na kumkuta Mama yake mzima, alimsalimia na kumuomba msamaha kwa kuchelewa kuja kumuona akisema alikua hajui, Mama yake alimuuliza kwa mshangao.
“Ulikua hujui wakati Mumeo jana alikuwa hapa, Baba wawatu kahangaika sana mpaka kupata watu wa kuniongezea damu, kasumbuka sana jana, mwanangu hapa umepata mume. Asingekua mumeo ningeshakufa kwani madakitari walisema ningekosa damu ningekufa…”
Mke wa Juma alishindwa cha kujibu, hakujua kuwa kumbe Juma hakuacha kutafuta damu alihakikisha Mama yake yuko salama ndiyo akaondoka.
“Sikumuambia Mama, Jana alikua anajisikia vibaya, nadhani presha ilikua inamsumbua nikasema nisimuambie kwani angeweza kuchanganyikiwa. Asubuhi ndiyo nikamuambia baada ya kuona yuko vizuri”.
Naendela vizuri mwanangu, ahsante sana kwa kuhangaika na mimi jana, nilikua hoi sana. Mama yake aliongea huku akitabasmau. Mkewe alinyanyuka, huku akitoa machozi alimkumbatia mumewe na kumuambia nisamehe mume wangu sasa ndiyo nimejua maana ya ndoa ni nini?
Juma alimkumbatia nayeye kwa nguvu na kumuambia. Usijali mke wangu nakupenda sana nilitaka tu ujifunze kuwa mali sio kila kitu, najua umenizidi kipato lakini pesa zinatafutwa na kamwe hela haiwezi kuzidi thamani ya utu.
“Mkeo amefariki Msiba uko hapa nyumbani?” Denis alipokea ujumbe mfupi kwenye simu yake, kuangalia ulitoka kwa Mama yake mzazi. Nguvu zilimuishia, alikua akiongea na mteja ofisini kwake lakini sauti ilikauka.
Bila kujijua alijikuta ananyanyuka na kuanza kutembeatembea ofisini kwake akiwa hajitambui. Wafanyakazi wake walimuuliza bosi vipi lakini hakuwa na jibu la maana la kuwapa.
Akili yake ilikumbuka maneno ambayo alimuambia mkewe asubuhi wakati anaondoka, mkewe alimuambia sukari imeisha na kwa dharau alimjibu “Sasa unaniambia mimi ili nini? Kwani ni lazima unywe chai huko kwenu mlikua mnakunywa chai kila siku??”
Alikumbuka namna usiku wake alivyompiga makofi baada tu ya mboga kuungua alipochelewa kuepua kwani alikua ananyonyesha mtoto wao wa mwisho ambaye yeye mwenyewe ndiyo alimuita amnyonyeshe kwani alikua analia sana.
Alikumbuka namna siku mbili kabla mkewe alisema amechoka kupigwa na kunyanyaswa, anakumbuka namna alivyomjibu kwa dharau kuwa kama amechoka aondoke amuachie watoto wake.
“Ameniachia wanangu!” Alijikuta anaropoka na machozi yalianza kumtoka. Alishindwa hata kutembea hivyo alikaa chini kabisa sakafuni. Wafanyakazi wake walikuja na kumnyanyua na baada ya kumuuliza ndipo alipowaambia mkewe amefariki.
Walimchukua mpaka kwenye gari na safari ya kurejea nyumbani ilianza, walifika nyumbani, kila kitu kilikua kimya, nyumba ilikua imefungwa na hakukua na mtu.
Denis alizidi kuchanganyikiwa zaidi asijue nini cha kufanya ndipo alipokumbuka kuwa Mama yake alimuambia msiba uko nyumbani hivyo alidhani kuwa ni nyumbani kwao.
*****
Safari nyingine ilianza, Denis alikua na mawazo, hayakuwa mawazo tu ya kufiwa bali ya aibu. Pamoja na kumiliki kampuni kubwa akiajiri watu ziadi ya kumi lakini mkewe alimnyanyasa na kumtesa kama kinyago, mbali na kumpiga lakini alikua hamhudumii vizuri.
“Atakua amefia kwa Mama wakati amenda kuomba hela ya matumizi…” Aliwaza kwani mara nyingi alipokuwa akimnyima pesa Mama yake mzazi ndiyo alikua akimsaidia na ndiyo alizuia mara nyingi mkewe asiondoke.
Alifika mpaka nyumbani kwao, kweli kulikua na msiba, maturubai yalishawekwa, watu walishaanza kupika na watu walishaanza kujaa taratibu. Alijitahidi kushuka kwenye gari na kuanza kutembea kuelekea nyumbani.
Watu walikua wakimsalimia na kumpa pole, aliipokea kwa aibu huku akiwaza ni kitu gani kiliwasukuma wazazi wake kufanyia msiba pale na ni nini kilikua kimesababisha mauti ya mkewe.
“Ameumwa sana muacheni apumzike..” Ilikua ni sauti ya Baba yake ikimuambia jirani yao mmoja. Hapo ndipo alichanganyikiwa zaidi akiwaza ni kwa namna gani mkewe alikua anaumwa bila yeye kujua.
Lakini alikumbuka ni mara kibao mkewe alimuambia anaumwa lakini alidharau na ni mara nyingi Mama yake alimsema kuhusu kutokumsikiliza mkewe na mara nyingi tu Mama yake aliongozana na mkewe hospitalini.
Yeye kwake yote hayo hakujali, kila mke alipomuambia anaumwa yeye alidai haki yake ya ndoa, alizidi kumpiga na alianza kukumbuka namna ambavyo alimpiga mpaka kulazwa lakini bado hakujali.
Aliwaza labda ndiyo ilikua sababu ya kifo chake. “Au alikua anaumwa kimyakimya hasemi akaja kusema nyumbani..” Alitembea mpaka kufika ndani, alikaa na kusalimiana na ndugu wengine ambao nao walikua wanampa pole kwa msiba.
Alizipokea huku akijaribu kujizuia machozi yasitoke. Mara mtoto wake wapili wa miaka minne alikuja. Alikua akilia akimtaka Mama yake watu wakimuambia asubiri Mama yake anakuja.
Mtoto alimkimbilia Dennis na kuanza kulia namtaka Mama namtaka Mama. Denis alichaganyikiwa kwani hakuwa na jibu la kumpa, hakujua amumbie nini kuhusu Mama yake.
Mara mtoto mwingine mkubwa kidogo wa miaka saba alikuja, alikua amembeba mtoto wao mdogo mchanga wa miezi sita. Alimfuata Baba yake na kumuuliza Baba Mama yuko wapi Jack anataka kunyonya.
Hapo ndipo aliishiwa nguvu kabisa, maneno yake ya “Ondoka niachie wanangu yalizunguka kichwani kwake” Aliwaangalia wanae na kusema kweli nimeachiwa, umeniweza Juddy mke wangu.
Alijikuta anaanza kulia kama mtoto kitu ambacho kiliwafanya na wanae wote kulilia. Denis alichanganyikiwa, kila mtu aliyekua anakuja alienda kumpa pole, nguvu zilimuishia alikata tamaa, na majuto ya hali ya juu, kila tendo baya alilokua akimfanyia mkewe lilimjia kichwani.
****
“Mama Jose njoo umnyonyeshe mtoto analia muda mrefu..” Ilikua ni sauti ya Mama yake, Denis alistuka na kunyanyuka kuangalia, Mama Jose ni mkewe na hakujua ni kwanini Mama yake alikua anamuambia aje kumnyonyesha mtoto wakati alishafariki dunia.
Kabla hajasema chochote Mama yake aliingia “Ohhh umekuja, nikajua utakuja baadaye kazi zimekubana, mkeo alisema hupatikani kwenye simu.”
Denis alizidi kuchanganyikiwa, alibaki na mshangao. Mara mkewe aliingia, hapo ndipo alichanganyikiwa zaidi, alistuka kama vile ameona mzimu, kidogo amdondoshe mtoto aliyekua amempakata.
“Vipi Baba Jose…” Mkewe alimuuliza, namna alivyokua akimuangalia haikua kawaida. “Uko hai mke wangu?” Alijikuta anauliza. “Ndiyo kwani vipi ulitaka nife?” Mkewe alijibu kwa kebehi kidogo kwani alijua ni madharau ya mumewe.
“Lakini Mama..” Denis aliongea kwa kushangaa huku akimuangalia Mama yake. Mama yake alitabasamua na kumuambia, aliyekufa ni Bibi yako si ndiyo anakuitaga mume wangu.
Wewe mbona kila siku ukipiga simu unaulizia mke wangu hajambo. Denis alipumua kwa nguvu huku akikaa chini, mkewe alichukua mtoto kwenda kumnyonyesha. Denis alimfuata huko huko chumbani, alipiga magoti mbele yake na kusema.
“Samahani mke wangu nilikua sijajua thamani yako mpaka leo. Yaani leo ndiyo nilichanganyikiwa, nilijua umekufa na tayari nilishaona maisha hayawezekani bila wewe. Naahidi nitabadilika nitakua mume mwema na kamwe sikunyanyasi tena.
Mama yake ambaye alisimama mlangoni alitingisha kichwa na kucheka. Huku akisema “Unavyoringa uachiwe watoto kila siku unajua uchungu wa kulea wewe au unataka uachiwe ili uje kunitupia wanao hapa nianze kulea wajukuu!”
Hakusubiri hata jibu aliondoka akimuacha mwanae akiendelea kuomba msamaha akiwa haamini kuwa mkewe yuko hai. Siku ile ndiyo ilikua siku ya Mabadiliko ya Denis hakuwahi kumpiga wala kumnyanyasa tena mkewe.
INASIKITISHA JAMANI SOMA HII!
Baba na mama baada ya kurudi kazini pamoja wakakuta BARUA iko mezani SEBULENI ikisema…. “Baba na mama, ni matumaini yangu kuwa mtasoma ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka
juu ya meza, naomba msishtuke mana ni mambo ya kawaida kwenye maisha tunayoishi, najua mtaumia kwa vile bado nasoma na ndo nipo kidato cha kwanza…” Napenda kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii barua sipo nyumbani, nimetoroka mana nimegundua nina uwezo wa kujitegemea kwa sababu mi ni kijana mwenyewe umri wa miaka 14 na ninajua kipi chema na kipi kibaya. Tangu mwezi mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano na binti mmoja aliyeitwa Rachel, mwenye umri wa miaka 27 na kwa sasa ndo naishi naye kwenye chumba alichopanga. Nilipokuwa nyumbani sikuwa napata hela za kutosha ila sasa nimeanza kushika noti za shilingi 10,000… Msichana niliyenaye ni mzuri sana wa umbo na ninampenda sana, amenifundisha njia za kutafuta hela. Amenipangia kazi ya kuuza madawa ya kulevya na yeye ikifika usiku
anaenda kuuza mwili wake, basi kila siku tunapata hela ya kutosha, huyu mchumba wangu ni msichana mwenye bidii, kwa siku analala masaa 6 tu maana mwanaume yeyote akija lazima awe naye chumbani kwa muda wa masaa 3. Msiwe na hofu, nipo salama kabisa na nimeamua kumwoa Rachel mana ni kila kitu kwangu. Pia amenunua gari la kubebea mbao kwahiyo biashara inaenda vizuri, Rachel ameenda kupima afya na amekutwa na upungufu wa kinga mwilini,mara nyingi namridhisha anapotaka kitu flani, iwe kufanya
naye mazoezi ya viungo au kufanya naye mapenzi, si mnajua unapokuwa na mgonjwa unakuwa naye karibu, ila mi pia sijihisi vizuri mana kila saa nakohoa tu na sina uhakika kama nimeathirika. Tumepanga baada ya miaka miwili tutawatembelea, nadhani mpaka miaka miwili iishe atakuwa ameshajifungua, na ni furaha yangu mtamwona mjukuu wenu. Wazazi wangu sina la kuongeza kwaherini Mungu akipenda tutaonana.
NB: “Baba na mama, mi nipo chumbani kwangu najisomea, mnachokisoma ni home work ya mwalimu wa kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi ya kusisimua, naomba muiangaliekama kuna
makosa
Alimpenda mno mke wake, alijitahidi kumpa mkewe kila kitu kilochopo ndani ya uwezo wake, lakini mke wake hakuwa akiridhika na ku appriciate. Ingawa hakuwa tajiri lakini alijitahidi mno ku share kile alichonacho.
Kila alipomnunulia nguo mkewe, jibu pekee alilolipata lilikuwa ni kwamba alikuwa akikamilisha jukumu lake kama mume. Mkewe hakuwahi kutoa shukrani hata mara moja.
Mwanaume angemnunulia nguo mkewe lakini mkewe alikuwa akimjibu kwamba nguo ni ya bei ya chini na quality yake ni ndogo. Mume angetabasamu na kumwambia mkewe kwamba “siku moja nitakapokuwa tajiri nitakununulia vitu vyote vya gharama unavyovitaka” kwa sasa naomba nivumilie tu mke wangu!
Mke hakuwa akimpigia simu mume wake labda tu pale alipokuwa akihitaji kitu au pesa kutoka kwa mumewe, na kama asipokamilishiwa ombi lake ilikuwa ni ugomvi kwa siku kadhaa.
Jioni moja, mume alirudi kutoka kazini, alileta nyumbani kilogramu moja ya nyama, kwa furaha tele alitegemea kumsuprise mkewe. Alifika nyumbani na kumuona mkewe na akamuonyesha ile kilo ya nyama! Mkewe kwa dharau akamwambia ” eh na ndio unajiita mwanaume? Unafikiri kurudi nyumbani na kilo moja ya nyama bila viungo, mafuta ya kupikia wala mbogamboga ndio kutakufanya uonekane kidume? Bora ungeacha tu! Huna msaada wowote hapa.
Kisha akaenda kuitupa ile nyama jalalani, mume alijisikia vibaya sana lakini hakuchoka kuendelea kumpenda mkewe. Aliendelea kufanyiwa vituko mbalimbali lakini hakuteteleka juu ya mapenzi kwa mkewe na familia yake.
Siku moja mume alipatwa na maumivu ya mguu wa kushoto, baadae uvimbe ukatokea katika mguu na ukawa ukikua siku baada ya siku.
Alienda hospitalini na akakutwa alikuwa na kansa, hakuwa na pesa za kutosha za matibabu ya kansa. Japo alikuwa mgonjwa ila alijitahidi kuhudumia familia yake.
Miaka miwili baadae hali ilizidi kuwa mbaya, mpaka akapelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. Alifanyiwa operation na mguu ukaondolewa baada ya kuwa umeathiriwa vibaya na kansa. Lakini kwa bahati mbaya walikuwa wamechelewa, ugonjwa ulikua umesha athiri na maeneo mengine mengi ya mwili.
Alimwita mkewe na kumwambia “NITUNZIE WANANGU” najihisi mwili udhaifu, roho inataka kunichomoka, maumivu hayaniishi, nafikiri siwezi kuishi tena! Siku zote nitakuwa na wewe kiroho! Mwenyezi Mungu akubariki na ninakupenda sana mke wangu!
Alivuta pumzi yake ya mwisho na kufariki. Mkewe na watoto wake pamoja na ndugu na marafiki waliomboleza msiba ule na wakazika!
Miezi mitatu baadae mkewe alikuwa ameinamia kaburi la mumewe akitamka maneno haya kwa uchungu mwingi!
“Mume wangu mpenzi! Ulifanya kila uwezalo kunihudumia, ulinijali vema na kunipa kile kilichokuwa ndani ya uwezo wako. Ila mimi nilichokulipa ni migogoro na ugomvi usiokwisha. Sikutambua umuhimu wako! Nimeuona sasa hivi ulivyoondoka na kuniachia watoto!
Sasa nimekua mimi ndio wa kuwatafutia chakula watoto, kuwalipia ada, mavazi na kila kitu! Sio siri ulikuwa wa muhimu sana
Nakumbuka siku ile nilivyotupa jalalani ile kilo ya nyama, lakini sasa sijui hata kilo moja ya nyama naipata wapi.
Wema hufa mapema! Najuta mume wangu, mume ambae kila nilipokuudhi hukuonesha kukasirika bali ulitabasamu. Najua unanisikiliza nakuomba sana unisamehe. Wote tumekumbuka uwepo wako. Mwanao Diana kila siku anauliza utarudi lini?
Hautatutoka akilin mwetu mpaka pale tutakapoungana na wewe huko uliko. Mwenyezi Mungu akulaze mahala pema peponi.
MUHIMU:
*Siku zote kubali kile ulichopewa bila kujalisha ni kidogo ama kikubwa.
*Mapenzi sio ni nini tulicho nacho, au ni utajiri gani tulionao ila mapenz ni ku share kile kidogo tulicho nacho
*Ushawahi kuchukua muda wako na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kile alichokubariki nacho? Kama hujawahi kufanya hivyo ni bora ufanye sasa!
Shukuru Mungu kwa alichokupa, kitunze kidumu. usije ukajikuta ukipoteza almasi wakati upo busy ukikusanya mawe.
Posted by: MwlMaeda - 08-21-2021, 10:21 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
Kijana mmoja alisafiri kwa meli na rafiki zake, wakiwa katikati ya safari yao meli ilianza kuzama. Watu wengi pamoja na rafiki wa yule kijana walikufa maji wakati wanajaribu kujiokoa kwa kuogelea, lakini yule kijana alifanikiwa kushika ubao ulioelea majini akaanza kuelea nao, maji yalimpeleka hadi kisiwa cha mbali sana ambako hakukuwa na watu wala wanyama isipokuwa wadudu tu! Alifika ufukweni amechoka sana na asiyeamini tukio lililotokea, akaishi huko kwa kula matunda. Aliweza kujenga ka-kibanda kwa shida sana maana hakuwa na shoka wala panga, hatimaye akaanza maisha mapya.
Aliishi muda mrefu kisiwani na tayari alishazoea mazingira yale ya shida japo shida haizoeleki. Mara zote nyakati za jioni aliwasha moto kwa kupekecha vijiti. Siku moja kama kawaida yake aliwasha moto nje karibu na kibanda chake, aliota moto muda mrefu hatimaye akapitiwa na usingizi. Alilala hapo hapo hadi usiku wa manane aliposhtushwa na joto kali lisilo la kawaida. Kumbe moto ulishika nyasi za kibanda chake na kibanda chote kikaungua moto.Alilia sana na kumlaani sana Mungu kwa mateso hayo akisema “Hivi Mungu nimekukosea nini mpaka unitese hivi? Pamoja na shida zote hizi bado unaniongezea shida nyingine, umeteketeza makazi yangu ilhali nimejenga kwa shida, Hukuridhika kunitenga mbali na familia yangu nilipoishi kwa raha? Hukuridhika kuwaua rafiki zangu wote baharini? Kwanini Mungu umekuwa mkatili hivi? Bora nife tuu maana nimeshachoshwa na hizi shida!” akaendelea kulalamika na kumlaani Mungu hadi kukapambazuka.
Ilipofika asubuhi aliiona meli ikija kwa mbali kuelekea alipo, alishangaa maana hakuna meli yoyote inayoweza kwenda kisiwa kile labda kama imepotea njia. Meli ilipofika ufukweni yule kijana akaifuata, alienda moja kwa moja hadi kwa kapteni.Kapteni akamwambia “tuliona moto mkali sana usiku tukahisi ni meli inawaka moto tukasema tuje ili tutoe msaada..kwa kweli tumetembea masaa mengi sana hadi kufika hapa, mshukuru Mungu maana ametumia moto kutuleta hapa” yule kijana kusikia hivyo alilia sana, akajilaumu kwa jinsi alivyo mnung’unikia Mungu. Akaelewa kuwa Mungu ana njia nyingi za kuleta msaada kwa mtu. Akapiga magoti akatubu huku akimshukuru Mungu. Safari ya kurudi nyumbani ikaanza.
FUNDISHO: Wakati mwingine Kuna mambo mabaya huwa yanatokea katika maisha yetu yanayotufanya tuone kama Mungu ametusahau. Tunamnung’unikia na kumlaumu Mungu bila kujua kuwa Mungu ana njia nyingi sana kutuletea msaada. Njia za Mungu huwa zinaonekana kama ujinga fulani, lakini kiukweli ujinga wa Mungu ndiyo akili kubwa ya mwisho ya mwanadamu. Tunasahau kuwa mabaya tunayokutana nayo yanafanya kazi kwa Manufaa ya hatma zetu. Unaweza fukuzwa kazi usijue kumbe ndio unaelekea katika kazi bora zaidi, unaweza kuachwa na mtu uliyempenda sana ukadhani ndiyo mwisho wa maisha kumbe Mungu amekuandalia mtu mwingine mwenye mapenzi ya dhati mtakayefikia malengo ya kujenga familia, unaweza kukataliwa na kutengwa na ndugu kumbe Mungu amekuandalia watu-baki watakaofanikisha ufikie malengo yako pasipo masimango ya ndugu, hata rafiki wanaweza kukusaliti kumbe Mungu amewaondoa makusudi ili kukuepusha na mabaya waliyoyapanga juu yako. Sasa usimlaumu Mungu ukadhani anakuzidishia matatizo, hapo anatafuta njia ya kuyaondoa hayo matatizo.
Mshukuru Mungu kwa Kila Jambo, kwakuwa hajawahi kukuwazia mabaya. Anakuwazia mema sikuzote.
Posted by: MwlMaeda - 08-21-2021, 10:16 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
MUHTASARI WA MAKALA
Uchambuzi wa makala ya mwandishi Jan Vansina. Hapo Zamani za kale: Mapokeo Simulizi kama historia ya Afrika
Mwandishi anaanza kwa kumnukuu Mbope Luis wa Kongo anayesema “ vitabu vyetu vipo kichwani mwetu”.
Makala imejaribu kuelezea historia ya masimulizi jadi yaliyokuwa yanapatikana Afrika. Mwandishi aanatofautisha jadi za namna mbili kwa kutumia jamii za Kiafrika na za Ulaya. Anasema kuwa tofauti na Ulaya ambako kusoma na kuandika vilikuwa kama kielelezo cha ustaarabu, jamii za Kiafrika kabla ya kuja ukoloni zilijitosheleza na kujieleza kwa kutumia mapokeo simulizi. Mwandishi anasisitiza kuwa nafasi na dhima ya mapokeo simulizi barani Afrika iliendelea kustawi hata baada ya kuingia kwa ustaarabu wa kusoma na kuandika, kwa maneno mengine Vansina anakiri kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya jadi ya mapokeo simulizi na jadi ya maandishi. Katika kulithibitisha hili anamtumia Profesa Willam A. Brown ambaye aliikuta barua huko masino ( Mali ) ambayo maudhui yake yalielezwa kwa kurejelea mambo mbalimbali. Yaliyokuwa yamesahaulika lakini yalikumbukwa kutokana na barua hiyo, barua hiyo ilikuwa kama chombo cha kutunza kumbukumbu hizo ili kurithisha desturi hizo.
Muundo, mfumo na dhima ya mapokeo simulizi ya jamii hubadilika kutokana na maingiliano yanayotokea katika jamii ambayo husababishwa na mabadiliko ya kuachwa kwa vitu muhimu katika wakati maalum na hatua za mabadiliko hayo huitwa muundo wa usahaulifu “structural amnesia” kwa kuwa masimulizi jadi ya jamii, utamaduni ulirithishwa kwa mawasiliano ya ana kwa ana na kubadilisha maudhui, kila jamii ilieleza; imani, maadili, mawazo na mtazamo wake katika fasihi.
Levis Straus anazungumzia muundo ndani wa mazungumzo, anasema kila kinachozungumzwa kina muundo kama huo, ila hujidhihirisha zaidi katika masimulizi. Muundo huu unahusisha msukumo, mtiririko wa maonesho, kujenga kilele kimoja au zaidi, usambamba, uradidi na kubadilika kwa onesho na hivi vyote lazima vichanganuliwe kabla.
Pia anasema athari yake katika maudhui yanaweza kuonekana na mtu yeyote anayechanganua maana ya ishara “ taswira za tendi” au taswira maarufu katika historia.
Katika nukuu ya Levis Straus na wanaantropolojia waliofuata walisema masimulizi mengi yalikuwa ya kitalii.
Kila tarihi ilieleza muundo halisi wa ishara za msingi zinazoeleza sio vitu vyenye thamani tu vilipendwa na jamii ya watu kiundani lakini pia utendaji wa kifikra wa binadamu, fikra za mwanadamu hazina budi kuwa na ushirikiano wa kifikra kabla ya kuelewa na kuwasiliana.
KUSUDI LA MWANDISHI
Kusudi la mwandishi katika kuandika makala hii ni kutaka kuthibitisha kuwa Afrika kulikuwa hakuna masimulizi, mfano ngano, tendi, misemo, hadithi (masimulizi).
NAMNA ALIVYOPANGA KUSHUGHULIKIA
Alishughulikia suala hili kwa kupitia tafiti za wataalamu wengine ambao tayari walikuwa wameshafanya utafiti kuhusu mapokeo simulizi, mfano alimtumia Ernest Bernheim, ambaye katika utafiti wake alidondoa nyimbo, ngano, na saga, hekaya, masimulizi mafupi, misemo na methali.
Pia alimtumia Profesa William A. Brown kwa kutumia barua yake ambayo aliikuta huko Masino ( Mali) iliyokuwa na maudhui mengi kuhusu Afrika.
Baada ya hapo aliamua kufanya tafiti yeye mwenyewe ili aweze kuziba pengo la wale wataalamu wengine na kuweza kulinganisha kile walichokipata wataalamu waliopita na kile alichokipata yeye kuhusu mapokeo simulizi ya Kiafrika.
JINSI ALIVYOPATA DATA
Aliangalia masimulizi ya Warundi na Warwanda na kuona kuwa masimulizi ya waburundi yalikuwa mafupi kwa sababu yanatolewa katika mkusanyiko usiokuwa rasmi lakini masimulizi ya Warwanda yalikuwa katika mchanganyiko yaani marefu na mafupi.
Pia waliangalia nyaraka zilizoandikwa, makumbusho sanaa halisi, malighafi ya tamaduni na habari ya Wanaismu. Japokuwa data zote hizi isipokuwa ile ya matini iliyoandikwa na zilikuwa zimesomwa na wataalamu wengine.
Zilizoandikwa katika Afrika zilifanywa na wageni ambao hawakuelewa shughuli za jamii na tamaduni walizoshughulikia. Aligundua kuwa nyaraka za zamani zilikuwa na ukweli zaidi, mfano kwa kutumia barua aliyoikuta Masino ( Mali ) na kwa kuangalia masimulizi ya Warwanda na Waburundi.
DATA HIZO ZILIKUWAJE?
Jan Vansina anasema jamii nyingi za Afrika Kusini mwa jangwa la sahara zilitumia mapokeo simulizi kwa muda mrefu, japokuwa zilitumia maandishi kwa kiasi kidogo, hivyo zilitawaliwa na jadi ya kimasimulizi. Kila kitu kilichohusu maisha yao, ikiwemo historia yao kilihifadhiwa katika masimulizi hayo. Hivyo mwanahistoria yeyote mwenye nia ya kutaka kuifahamu historia ya Wafrika hana budi kutambua kuwa mhimili mkuu wa historia ya jamii hiyo ni mapokeo simulizi.
Kwa upande wa Tanzania maeneo mengi ya kati, mapokeo simulizi yalikuwa chanzo kikuu cha historian a maarifa mpaka miaka ya 1880, ambapo historia ya falme za Kongo zilikuwa zimebadilishwa kuwa katika maandishi.
Hayo mapokeo simulizi yalitumika katika siasa ya kijamii, kiuchumi, dini, misafara mbalimbali na shughuli za kiutamaduni.
Data hizo pia zilionyesha mwingiliano wa matini katika mapokeo simulizi, kuhusu hili Vansina anasema suala la mwingiliano matini huhusisha ujitokezaji wa vipengele vya nyimbo za kidini, methali, ngano, katika mapokeo simulizi kama masimulizi ya kijadi yaliwekwa katika mpangilio ( tarihi za matukio mbalimbali ).
Kwa upande mwingine Vansina anafafanua kuwa nyimbo maarufu katika baadhi ya jamii ziliimbwa kwa kurudiwa mara nyingi na zingine kwa nadra. Kwa mfano katika familia za kifalme miongoni mwa jamii za Bushoong ya Kasai (Kongo) nyimbo hizo ziliimbwa kipindi cha kumsimika mfalme. Huko Afrika Magharibi miongoni mwa jamii ya Wadogoni nyimbo hizo ziliimbwa katika shughuli za kidini na kijamii kama vile matambiko na sherehe za kijadi. Katika jamii hii, nyimbo mashuhuri zilizohusu matambiko na sherehe za kijadi zilisimuliwa kwa jamii nzima hasa mara moja kila baada ya miaka sita.
HITIMISHO LAKE
Kutokana na utafiti wake alioufanya kwa kutumia data mbalimbali, alihitimisha kwa kusema kuwa Afrika kuna jadi ambazo zimetokana na masimulizi.
UFAWAFU WA MAKALA
Kila jamii ina umuhimu wake hata kama inatimiza kwa kiasi kidogo mambo mazuri au malengo au dhima yake inaweza kubadilika kipindi cha urithishwaji kwa sababu jamii imebadilika, tathmini ya kuharibika ambayo hutokana na msukumo katika jamii wakati mwingine ni vigumu kukadiria.
Kuna uhusiano mkubwa kati ya mapokeo simulizi na maandishi, katika kuthibitisha hili anamtumia Profesa William A. Brown aliyeikuta barua Masino ( Mali ) ambayo maudhui yake yalielezwa kwa kurejelea mambo mbalimbali yaliyosababishwa lakini yalikumbukwa kutokana na barua hiyo.
Jadi nyingi za Kiafrika ni za kimasimulizi zikifungamana na nyimbo na mashairi lakini haziangukii katika aina ya jadi za Ulaya. Pia kimuundo zipo kama masimulizi, ndefu kuliko zilivyo hadithi zingine.
Maelezo hayo yana mchango mkubwa kwani yanadhihirisha kuwa Afrika kulikuwa na tendi ambazo zilikuwa katika umbo la masimulizi na kishairi.
MAPENDEKEZO
Mwandishi alipokuwa akisema jadi zimetokana na masimulizi hususani ushairi. Je huo ushairi ulikuaje? (ushairi ulikuwa unafuata kanuni au lah!) kwa hiyo utafiti ufanyike zaidi ili kujua huu ushairi ulikuaje.
Kama hizo jadi zilikuwa katika usimulizi, usimulizi huo ulikuwa ni rasmi au sio rasmi? Tunapendekeza mwandishi afafanue kuwa jadi zimetokana na usimulizi gani haswa, kwa hiyo tafiti ziendelee kufanyika.
HOJA NZITO
1. Uasili wa kijadi unaweza kuwa wa namna mbalimbali, kwanza kwa kushuhudia matukio, pia kutoka katika maandishi, mfano ngano ubunifu wa matukio ya kihistoria au shughuli za kifasihi, visa vya kubuni pamoja na vya kuiba.
2. Afrika kuna tendi ambazo zimetokana na masimulizi ya kijadi.
3. kuna uhusiano mkubwa kati ya masimulizi jadi na maandishi.
4. Nyaraka zilizoandikwa katika Afrika zilifanywa na wageni ambao hawakuelewa shughuli za jamii na tamaduni waliyoshughulikia.
5. kila jadi ina umuhimu wake hata kama itatimiza kwa kiasi kidogo mambo mazuri au maadili.
6. muingiliano matini katika masimulizi jadi ni jambo ambalo haliepukiki mfano; nyimbo za kidini, methali, ngano, yaliwekwa katika mpangilio (tarihi ) za matukio.
HOJA TETE
Jadi za ulaya zina muundo rahisi lakini zina mpaka rasmi na ni za kawaida katika ubora.
JAMBO MUHIMU KATIKA MAPOKEO SIMULIZI YA KIFRIKA
Mapokeo simulizi yamekuwa yakitumika na yanatumika zaidi na zaidi katika historia ya Afrika. Mtiririko huu ni ushahidi katika makala za kihistoria za Kiafrika. Tangu mwanzo mwa mwaka 1960 makala zilikuwa na angalau kipengele kimoja kwa mwaka kilichokuwa kikizungumzia mapokeo simulizi, katika vipindi vyote vitatu vya karibuni vya historia ya Afrika Mashariki vimekuwa vikielezea Mapokeo simulizi kati ya mwaka 1500-1850, hasa sehemu za kati ya Tanzania.
Utaratibu wa kukusanya mapokeo simulizi unapatikana kwa kufuata utaratibu wa kutafuta tamaduni za kifamilia au hata kwa kuona, kuhesabu matukioa kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Kwa mfano, katika kipindi cha ukoloni tukio kama vile vita vya majimaji (1905-1907) Afrika Mashariki. Hali kama hii pia ilipatikana huko Afrika ya kati na maeneo ya Sudan.Jitihada za kukusanya na kuhifadhi data za kimapokeo simulizi zinadhihirika pia huko Jamhuri ya Niger ambapo tunafahamishwa kuwa kuliandaliwa eneo maalumu kwa ukusanyaji na utunzaji wa sanaa jadiyya. Swali ambalo mwandishi anajiuliza ni kuwa pamoja na kuwepo kwa jitihada za kutosha katika kukusanya na kuhifadhi data za mapokeo simulizi hakuna haja ya kujiuliza maswali kuwa Mapokeo simuliz yanaweza kutumika kama chanzo cha taarifa za kihistoria?. Anaendeleza mjadala kwa kusema kuwa haja ya kujiuliza ipo kwani suala hili linategemea namna ya ukusanyaji na uchanganuzi wa data.
Hadithi ya Yesu Kristo – Kiswahili, Tanzania lugha / The Story of Jesus – Swahili, Tanzania Language
Kuna baadhi ya watu kwa sababu tu ya kasumba zao hawataki kuamini kuwa Kiswahili si lugha ya kubeza na inastahili kupewa hadhi ya kuwa lugha ya kufundishia katika nchi zetu za Afrika. Matumizi ya lugha hii kutafsiria kazi mbalimbali, kutumiwa katika mitandao ya kijamii na kufunzwa kwa lugha hii katika vyuo vya nje ni ushahidi wa wazi juu ya kuimarika kwa lugha hii.
Posted by: MwlMaeda - 08-21-2021, 10:02 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
Nimeambiwa msemo huu wahenga waliupata katika kisa kimoja cha zama za kale.
Wanasema kulikuwa na msitu jirani na kijiji, ndani ya msitu kulikuwa na miti mingi sana. Ilitokea kuwa katika msitu ule, kulikuwa na miti inapishana sana kwa uzuri, na kati yao ulikuwepo ule ambao ni mzuri sana!
Mtema kuni (Mtemakuni maana yake ni Mkatakuni) alienda katika msitu ule katika shughuli zake za kila siku za kukata kuni!
Alipofika jirani na ule mti mzuri, huku akiwa na shoka mkononi, ule mti zuri sana ulikuwa jirani na mti mbaya sana!
Katika hali ya kufedhehesha (kwa nyodo na maringo) ule mti mzuri sana ukawa unamcheka na kumdhihaki ule mti mbaya, kwamba hauna mvuto na ndio maana kuanzia mbali kabisa, Mtemakuni amaonyesha kuvutiwa na (yeye) Mti mzuri! Huku Mtemakuni akizidi kuusogelea mti mzuri, mti mbaya sana ukajifariji kwa kumwambia mti mzuri basi subiri “utakiona cha mtema kuni”
Kilichofuata ni kweli, Mtema kuni aliukata na kuucharanga Mti mzuri sana kiasi cha kuugeuza kuni za kumfaa kubeba na kuondoka nazo, huku akiuacha ule mti mbaya salama salmini pale msituni!
Yakawa ni majuto kwa Mti mzuri na furaha kwa Mti mbaya!
Hivo ndio nilivyopokea kisa cha “mtema kuni”
UJUMBE WAKE KWA JAMII
??
1. Mliobarikiwa uzuri punguzeni maringo na nyodo!
2. Usijutie ubaya wa maumbile yako, Mungu ana maana kubwa sana kukuumba hivyo!