UTANZU WA NOVELA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi andishi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=7) +---- Forum: Riwaya (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=52) +---- Thread: UTANZU WA NOVELA (/showthread.php?tid=1039) |
UTANZU WA NOVELA - MwlMaeda - 08-27-2021 Ni utanzu ulio katikati ya riwaya na hadithi fupi. Huu ni utanzu wa kinathari ambao hutambulishwa kwa kiufinyu au ukosefu wa mgogoro au mgogoro finyu na ufinyu wa kimaudhui. Tofauti kuu kati ya novela na hadithi fupi ni kwamba hadithi fupi aghalabu hujihusisha na kitushi/ tukio moja kuu japo huwepo migogoro kadhaa.Mojawapo ya sifa bainifu za novela ni kujikita kubainisha tukio hali au mgogoro mmoja pekee. Huo mgogoro mmoja aghalabu huibua taharuki ambayo huishia mahali pa mgeuko (turningpoint). Tofauti kuu baina ya riwaya na novela ni kwamba novela huwa na msuko (ploti) mmoja ambao hauruhusu
utokaji nje sana. Yaani mwandishi hana uhuru wa kuacha kisa kikuu anachokisimulia na kuanzisha kingine katika novela hiyo moja. Kwa upande wa wahusika, novela kwa kawaida hujifunga kwenye wahusika wachache ambapo sifa za ndani au za kisaikolojia hazielezwi.
Mifano ya Novela katika Faishi ya Kiswahili ni kama ifuatavyo:
|