MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 73 online users.
» 0 Member(s) | 72 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  ODC : MUHADHARA WA KUMI : Kategoria za Kisintaksia na Ushahidi wa Kuwepo Kwazo
Posted by: MwlMaeda - 11-28-2021, 11:45 AM - Forum: Nukuu - No Replies

Muhadhara 10: 
Muhadhara  wa Kumi
 Kategoria za Kisintaksia na Ushahidi wa Kuwepo Kwazo
10.1 Utangulizi
Katika mhadhara uliopita tulipokuwa tunafasili dhana ya sintaksia tulidokeza kuwa sintaksia huchunguza jinsi maneno yanavyopangwa katika tungo. Jambo hili linatuambia kuwa katika lugha kuna maneno. Maneno hayo katika kila lugha hayajakaa kivoloya bali huwa yanahusiana kiasi cha kuweza kuwekwa katika makundi madogo. Akishadidia hoja hii, O’Grady, (1996: 182) anaeleza kuwa Ukweli wa msingi kuhusu maneno katika lugha zote za binadamu ni kwamba yanaweza kuwekwa katika makundi madogo zaidi yajulikanayo kama kategoria za kisintaksia. Kauli hii ya O’Grady inatuingiza katika udadisi wa kutaka kujua maana ya kategoria. Hivyo, tunajiuliza, “Kategoria ni nini?” Kusudi la muhadhara huu ni kujaribu kufasili dhana ya kategoria na kuangalia kama kweli kategoria zipo au la.
Madhumuni ya Muhadhara
Baada ya kusoma muhadhara huu unatarajiwa kuweza:
(i)     Kufafanua dhana ya kategoria
(ii)    Kutaja kategoria za kisintaksia
(iii)  Kueleza ushahidi wa kuwepo kwa kategoria za kileksika
10.2 Dhana ya Kategoria
Kwa mujibu wa Khamisi na Kiango (2002: 9) dhana ya kategoria ilitumiwa na wanasarufi mapokeo kwa namna tofauti na inavyotumiwa na wanasarufi mamboleo. Neno kategoria kama lilivyotumika katika sarufi mapokeo ya akina Aristotle limetokana na neno la Kigiriki na kutafsiriwa kama uarifu (predication). Wao walitumia dhana ya kategoria kuwa ni sifa bainifu, yaani zile sifa zinazoambatana au zinazoambikwa kwenye aina za maneno kama vile idadi, nafsi, kauli, ngeli, njeo, dhamira na uhusika.
Kategoria kwa mtazamo wa kisarufi mamboleo ni jamii, seti, kundi au makundi ya maneno yanayofanya kazi ya kufanana. Aidha, darajia yoyote ya vipashio inayotambuliwa katika uchambuzi wa lugha fulani huitwa kategoria.
Kwa sasa kategoria zipo katika viwango au darajia tatu: kiwango cha neno, kiwango cha kimuundo au kirai na kiwango cha kidhima. Kategoria hizi tatu zinajulikana kwa majina ya:
  • Kategoria za kileksika
  • Kategoria za virai
  • Kategoria za kidhima
10.2.1 Kategoria za Kileksika
Kategoria za kileksika ni kategoria za kiwango cha neno moja moja. Wataalamu mbalimbali wametofautiana katika idadi na istilahi za kategoria hizo. Kuna wanaotaja kategoria nne (tazama O’Grady, 1996: 182), saba (tazama Nkwera, 1978; Kapinga, 1983) na nane (tazama Kihore, 1996). Kategoria za kileksika zilizoainishwa mpaka sasa ni hizi zifuatazo:
Kategoria Mifano
(a) Nomino (N): Masanja, kijana, mtu, kitabu, vumbi, maziwa, utoto, ugonjwa n.k.
(b) Kitenzi (T): tembea, sema, totoa, ugua, kuwa n.k.
© Kivumishi (V): (-)dogo, -eusi, (-)zito, zuri n.k.
(d) Kihusishi (H): cha, katika, la, tena, hadi n.k.
(e) Kielezi (E): kijinga, vizuri, kabisa, sana, hasa, wima n.k.
(f) Kiwakilishi (W): mimi, wao n.k.
(g) Kiunganishi (U): na, lakini, ila, au, ama n.k.
(h) Kibainishi (B): yule, huyu, hawa n.k.
(i) Kiingizi/Kihisishi (K): abe!, naam!, hebu! n.k.
Kama tulivyobainisha kuhitilafiana kwa wataalamu juu ya ukategorishaji wa maneno, O’Grady (1996: 182) anaona kuwa kategoria za kileksika ni (a) mpaka (e) tu na kategoria zinazobaki ni kategoria zisizo za kileksika au ni kategoria za kidhima kwa kuwa maana za vipashio hivyo si rahisi kufasilika au kuelezeka. Aidha, katika kategoria za virai, ni kategoria za (a) mpaka (e) tu ndizo hutokea kama maneno makuu ya virai husika.
Kuna mkanganyiko unaoweza kujitokeza kuwa kuna maneno yanayoweza kuwa katika kategoria zaidi ya moja. Je, ni vigezo gani vinatumika ili kubaini kategoria za maneno? Vigezo vinavyotumika kubaini kategoria za maneno ndizo hutumiwa pia kama ushahidi wa kuwapo kwa kategoria katika lugha.
10.3 Ushahidi wa Kuwapo kwa Kategoria za Kileksika
Ushahidi unaounga mkono kuwapo kwa kategoria za kileksika ni wa kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia na kisemantiki.
10.3.1 Ushahidi wa kifonolojia
Katika ushahidi huu kigezo kinachotumiwa ni mkazo au shadda. Neno moja linakuwa katika kategoria tofauti kutokana na uwekaji wa mkazo. Tutazame mifano ifuatayo:
1) Wafanyakazi wote wamejenga baraBAra
2) Kazi zote zimefanyika baRAbara
3) We need to imPORT new technology
4) We need an IMport of new technology
Katika mifano hiyo hapo juu, neno la mwisho katika sentensi 1) ni nomino na katika sentensi 2) ni kielezi. Katika sentensi 3) neno la nne ni kitenzi na neno hilohilo katika sentensi 4) ni nomino. Maneno ni yaleyale lakini yamekuwa katika kategoria tofauti kutokana na uwekaji wa mkazo mahali tofauti. Kwa hiyo, mkazo unathibitisha kuwapo kwa kategoria za kileksika. Unathibitisha kuwa kuna kategoria mbili za neno moja. Hapa tunaona kuwa kanuni fulani za kifonolojia lazima zijue taarifa za kikategoria kabla ya kutumika. Kwa hiyo, tunahitimisha kwa kusema kwamba lile dai la O’Graddy (1996) la kwamba maneno yamegawanyika katika makundi mbalimbali lina ukweli ndani yake.
10.3.2 Ushahidi wa kimofolojia
Katika ushahidi huu kinachoangaliwa ni uambikatizi. Viambishi fulani vya kisarufi huweza kuambikwa kwenye maneno yaliyo katika kategoria fulani tu na haviwezi kuambikwa kwenye maneno ya kategoria tofauti.
Kwa mfano, O’Graddy (1996) anasema katika lugha ya Kiingereza kiambishi cha wingi –s huambikwa kwenye maneno ya kategoria ya nomino, kiambishi cha njeo iliyopita –ed na cha hali ya kuendelea huambikwa kwenye vitenzi, na viambishi vya ukadirifu -er, -est huambikwa kwenye vivumishi. Vivyo hivyo, katika lugha ya Kiswahili, viambishi vya idadi na ngeli huambikwa katika nomino na vivumishi, viambishi vya njeo, kauli, na usababishi huambikwa katika vitenzi n.k.
10.3.3 Ushahidi wa kisintaksia
Hapa kigezo kinachotumika na ambacho yasemekana ndicho kinachoaminika zaidi (O’Grady, 1996: 184) ni kile cha mtawanyo. Tunaangalia nafasi ambayo maneno yanachukua katika tungo.
Kwa mfano, maneno ya kategoria ya nomino ndiyo yanayoweza kuchukua nafasi iliyo wazi katika utungo ufuatao:
__________ anaweza kuwa mnyama hatari sana.
Simba
Chui
Nyoka n.k.
10.3.4 Ushahidi wa kisemantiki
O’Grady (1996: 183) anasema kuwa kigezo kinachohusika hapa ni maana. Kwa maneno mengine, tunajua kuwa neno fulani liko katika kategoria fulani kutokana na linavyofasiliwa. Kwa mfano:
Nomino: maneno yanayotaja vitu
Vitenzi: maneno yanayotaja vitendo
Vivumishi: maneno ambayo hutaja sifa za nomino
Vielezi: maneno ambayo hueleza namna ambavyo tendo linafanyika
Vihusishi: maneno yanayohusisha
Vibainishi: maneno ambayo huweka vitu bayana
Tutakubaliana sote kuwa kigezo hiki hakiwezi kuwa cha kuaminika sana. Kunaweza kuwa na mapungufu mengi mtu akitumia fasili katika kuchanganua kategoria za maneno. Tuangalie mifano michache ya maneno kutoka lugha ya Kiingereza.
  • “Assasination” linaonyesha hali ya kutenda lakini ni nomino
  • “Fast food” katika neno ambatano hili, neno “fast” linadokeza namna ambavyo chakula kinavyotengenezwa (haraka haraka). Kwa jinsi hii neno fast linaonekana kuwa ni kielezi ilhali ni kivumishi.Aidha, kategoria ya vivumishi inaweza kuwa ngumu kuibainisha ikiwa peke yake kwa sababu Huweza kuwa kiwakilishi.
Kigezo kizuri kinachofaa kutumika katika ushahidi wa kisemantiki ni utata. Utata ndicho kigezo kizuri cha kuonyesha kuwa maneno yana kategoria mbili au zaidi. Utata ni kipengele kinachodhihirisha tafsiri zaidi ya moja. Yaani ni hali ya kipashio kimoja kuwa na maana zaidi ya moja. Upo utata wa kileksia na wa kimuundo. Katika utata wa kileksia, leksimu au neno moja linakuwa na maana zaidi ya moja. Kwa mfano:
Kaa 1. Mnyama wa majini, gegeleka (Nomino)
  1. Kijinga cha moto (Nomino)
  2. Keti (Kitenzi)
Panda 1. Tia mbegu ardhini (Kitenzi)
  1. Jamiiana (Kitenzi)
  2. Kwea (Kitenzi)
  3. Njia iliyogawantika (Nomino)
Katika utata wa kimuundo, tafsiri zaidi ya moja zinaibuka kutokana na jinsi utungo ulivyotungwa. Kwa mfano:
Hali halali
N V: Hali ambayo si haramu; ile inayoturuhusu kufanya jambo fulani
T T: Hawezi kula wala kulala
10.4 Hitimisho
Kutokana na ushahidi wa kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia na kisemantiki, ni dhahiri kuwa maneno hugawika katika makundi mbalimbali madogo zaidi kama ilivyodaiwa na O’Grady (1997).

Print this item

  DHANA YA SILABI, AINA NA MIUNDO YAKE
Posted by: MwlMaeda - 11-28-2021, 11:40 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

DHANA YA SILABI NA AINA ZAKE
Utangulizi
Jumanne, (2014) Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za lugha hutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti.
Feng Shengli, (2003) Silabi ni mpangilio wa fungu la sauti za kutamkwa.
David Crystal, (2003) Silabi ni sauti moja au zaidi inayowakilisha kifungu kimoja cha sauti katika lugha.
Massamba na wenzake, (2004) Silabi ni sehemu ya neno ambayo huweza kutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Maelezo haya yanamaana kwamba maneno ya lugha hutamkwa katika utaratibu wa kufuata silabi.
Kamusi ya Kiswahili sanifu (Toleo la pili, 2004-2005) Inasema kuwa silabi ni sehemu ya neno inayoundwa na konsonanti na irabu au irabu peke yake na kutamkwa kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Kwa mfano, “i” na “ta” katika neno “ita” ni silabi mbili tofauti.
Hivyo basi kwa kuangalia maana zilizotolewa na wataalamu mbalimbali tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa, silabi ni kipashio cha kifonolojia ambacho sauti au fungu la sauti linalojitosheleza kimatamshi, ambacho hutamkwa mara moja na kwa pamoja.
                              AINA ZA SILABI
Kwa mujibu wa Massamba (2004), kuna aina mbili za silabi ambazo ni;
  1. Silabi huru.
  2. Silabi funge.
SILABI HURU
Ni silabi ambazo huishia na irabu. Kwa mfano silabi hizo ni “ka, da, ba, cha na nyingine nyingi. Kimsingi maneno yote ya lugha ya Kiswahili sanifu ambayo yana asili ya kibantu huundwa kwa silabi huru.
Kwa mfano maneno kama vile;
Mama—&ma&ma&.
Baba—&ba&ba&.
Mimina—&mi&mi&na&.
Sukuma—&su&ku&ma&.
Mageuzi—&ma&ge&u&zi&.
Usafiri—&u&sa&fi&&ri&.
                                      SILABI FUNGE
Ni silabi zinazoishia na konsonanti ambapo katika lugha ya Kiswahili ni nadra kuzipata maana lugha hii hutumia silabi huru. Silabi funge zimetokana na maneno yaliyokopwa kutoka lugha nyingine za kigeni. Kwa mfano neno Rais &ra&i&s& ni neno lenye silabi funge kwa sababu linaishia na konsonanti “s”.
                   MIUNDO YA SILABI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
Kwa mujibu wa Kihore (2003), katika lugha ya Kiswahili kuna miundo mbalimbali ya silabi, kwanza kabisa kuna miundo ya silabi zinazotokana na lugha za kibantu ambayo ni kama ifuatavyo;
  1. Muundo wa irabu peke yake. (I).
Mifano;
Ua—&u&a&.
Oa—&o&a&.
Oga—&o&ga&.
Anga—&a&nga&.
Onyesha—&o&nye&sha&.
  1. Muundo wa silabi konsonanti na irabu. (KI).
Mifano;
Kama—&ka&ma&.
Baba—&ba&ba&.
Konsonanti—&ko&nso&na&nti&.
Jema—&je&ma&
Paka—&pa&ka&.
  1. Muundo wa silabi ya konsonanti, kiyeyusho na irabu. (KKI).
Mifano;
Fyeka—&fye&ka&.
Bweka—&bwe&ka&.
Bwawa—&bwa&wa&.
Fyatua—&fya&tu&a&.
Kwako—&kwa&ko&.
  1. Muundo wa silabi ya nazali peke yake.
Mifano;
Nne—&n&ne&.
Nchi—&n&chi&.
Mtu—&m&tu&.
Mti—&m&ti&.
Mkufu—&m&ku&fu&.
Mganga—&m&ga&nga&.
  1. Muundo wa silabi wa konsonanti, konsonanti na irabu. (KKI), katjika muundo huu wa silabi konsonanti ya mwanzo huwa ni vitamkwa nazali [m] na [n].
Mifano;
Ngamia—&nga&mi&a&.
Ndama—&nda&ma&.
Mbuzi—&mbu&zi&.
Mbuga—&mbu&ga&.
  1. Muundo wa silabi wa konsonanti, konsonanti, kiyeyusho na irabu. (KKKI).
Mifano;
Jangwa—&ja&ngwa&.
Ugonjwa—&u&go&njwa&.
Dundwa—&du&ndwa&.
Mbwa—&mbwa&.
Kwa mujibu wa Samwel, M (2009), Miundo ya silabi za Kiswahili zinazotokana na maneno ya lugha za kigeni ni pamoja na;
  • Muundo wa konsonanti, konsonanti na irabu. (KKI), muundo huu ni tofauti na muundo uliotangulia kwani muundo huu unahusisha tu konsonanti zisizokuwa nazali.
Mifano;
Labda (Kiajemi)—&la&bda&.
Stoo (Kiingereza)—&sto&o&.
Sekta (Kiingereza)—&se&kta&.
Daftari (Kiarabu)—&da&fta&ri&.
Kabla (Kiarabu)—&ka&bla&.
  • Muundo wa silabi wa konsonanti, konsonanti, konsonanti na irabu. (KKKI), muundo huu nao unajitokeza katika lugha ya Kiswahili sanifu kutokana na maneno ya mkopo kutoka lugha ya kiingereza.
Mifano;
Springi—&spri&ngi&.
Skrubu—&skru&&bu&.
  • Muundo wa silabi wa konsonanti, irabu na konsonanti. Kuna maneno yenye asili ya kigeni katika lugha ya Kiswahili sanifu ambayo yana silabi funge na yana muundo wa konsonanti, irabu na konsonanti. (KIK).
Mifano;
Maktaba—&mak&ta&ba&.
Muktadha—&muk&ta&dha&.
Bakshishi—&bak&shi&shi&.
Maksi—&mak&si&.
Leksia—&lek&si&a&.
  • Muundo wa silabi ya irabu na konsonanti. (IK).
Mifano;
Oksijeni—&ok&si&je&ni&.
Inspekta—&in&spek&ta&.
  • Muundo wa silabi wa konsonanti, konsonanti, irabu na konsonanti. (KKIK).
Mifano;
Trekta—&trek&ta&.
Inspekta—&in&spek&ta&.
MAREJEO
Crystal D, (2003) A Dictionary of Linguistics and Phonetics: Blackwell.
 Shengli F, (2003) A prosodic grammar of Chinese: University of Kansas.
Kihore Y.M na wenzake (2003) Sarufi maumbo ya Kiswahili sanifu sekondari na vyuo: Dar-es-Salaam
Kamusi ya Kiswahili sanifu (Toleo la pili 2004-2005). Dar es Salaam Tanzania
Massamba na wenzake (2004) Fonolojia ya Kiswahili sanifu (FOKISA) Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Dar es Salaam Tz
Massamba na wenzake (2009) SARUFI MAUMBO YA KISWAHILI SANIFU (SAMAKISA) Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Dar es Salaam Tz
Samwel M. (2009) Kozi tangulizi ya fonolojia na sintaksia ya kiswahili: (DUCE) Dar es Salaam

Print this item

  DHANA YA LAFUDHI
Posted by: MwlMaeda - 11-28-2021, 11:38 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

DHANA YA LAFUDHI
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili sanifu (Toleo la pili 2004-2005) inaeleza kuwa lafudhi ni matamshi ya mzungumzaji yanayotokana na lugha yake ya mwanzo au lugha zinazomzunguka, au ni udhihirishaji wa sauti za lugha unaomtambulisha mtu mmoja au jamii ya watu.
Massamba na wenzake (2009) SAMAKISA, wanasema kuwa lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanayotokana na athari za kimazingira.Mazingira hayo yanaweza kuwa eneo atokalo mtu, mahali aliposomea, kiwango chake cha elimu na tabaka lake la jamii.
          Kimsingi tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa lafudhi ni sifa ya masikizi ambayo humtambulisha mzungumzaji na jiografia yake, uzungumzaji huo huwatofautisha wazungumzaji wa lugha moja katika jamii au mazingira fulani.
Kwa mujibu wa wavuti wa www.shuledirect.co.tz/notes/views/195 wanadai kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha ya pili kwa watumiaji wengi wa Afrika Mashariki kwa hiyo hii inafanya kuwatambua wazungumzaji wa Kiswahili kulingana na makabila yao au maeneo wanakotoka. Kwa mfano hapa Tanzania tunaweza kuwatambua watu wa Mwanza kwa lafudhi yao, pia watu wa Mtwara kwa lafudhi yao.
Kwa mfano;
  1. Usiniretee maswara ya ubaguzi wa kikabira hapa. (Wakurya).
  2. Ukikaa nchale, ukisimama nchale. (Wamakonde).
  3. Wewe unakamuaga mang’ombe tu. (Wasukuma).
  4. Mbona unakuwa kinganganizi, nilishakwambia sikupendi lakini wewe bado unaningangania tu. (Wahaya).
Katika mifano tajwa hapo juu kuanzia mfano wa kwanza mpaka wanne tunaona makosa yanayojitokeza katika baadhi ya tungo wanazozitumia. Kwa mfano katika mfano wa (a) tunaona namna jamii ya Wakurya inavyotumia herufi “r” badala ya “l”, vilevile katika mfano wa pili (b) tunaona namna jamii ya Wamakonde wanavyotumia herufi “n” na “ch” badala ya “m”na “sh”.
          Katika mfano wa tatu © tunaona namna jamii ya Wasukuma wanavyoongeza vitamkwa katika baadhi yamaneno, kwa mfano katika mfano wameongeza vitamkwa “ma” katika neno “ng’ombe” na kitamkwa “ga” katika neno “unakamua”. Pia katika mfano (d) tunaona jinsi jamii ya Wahaya wanavyoshindwa kutamka herufi (ng’) katika tungo zao.
          Lafudhi pia inaweza kujitokeza katika mazingira mbalimbali kama vile;
  1. Kushindwa kutamka baadhi ya herufi au vitamkwa.
  2. kwa mfano kabila la Wanyakyusa hushindwa kutamka herufi “v” na badala yake hutumia herufi “fy” katika tungo zao.
Kwa mfano; fyatu fyimechanika badala ya viatu vimechanika.
Pia Wanyakyusa hutamka “s” badala ya “z”, kwa mfano, mapindusi badala ya mapinduzi, vilevile hutamka herufi “ky” badala ya “ch” kwa mfano, kyiama kya mapindusi badala ya chama cha mapinduzi.
  1. Kabila la wapare hushindwa kutamka herufi “s” na badala yake hutamka herufi “th”. Kwa mfano, Thithi thote ni ndugu badala ya Sisi sote ni ndugu. Wapare pia hushindwa kutamka herufi “z” na badala yake hutamka “dh”. Kwa mfano, Nguo dhao dhote dhimeibiwa badala ya Nguo zao zote zimeibiwa.
  2. Kabila la Waha hushindwa kutamka herufi “n” hasa katika neno kama vile “nne”. Kwa mfano, Mwanafunzi amejibu maswali maine badala ya Mwanafunzi amejibu maswali manne.
  3. Lafudhi inayojitokeza katika mazingira ya kuongeza vitamkwa, kwa mfano,
  4. Katika kabila la Wasukuma hupenda kuongeza vitamkwa “ma” na “ga” katika baadhi ya maneno. Kwa mfano, Mang’ombe mengi badala ya Ng’ombe wengi, Watoto wanapendaga kula badala ya Watoto wanapenda kula.
  • Lafudhi inayojitokeza katika mazingira ya kupoteza au kudondosha baadhi ya vitamkwa. Kwa mfano katika kabila la Wachaga baadhi ya vitamkwa hudondoshwa wakati wa utamkaji wa baadhi ya maneno, kwa mfano Wachaga hudondosha kitamkwa “h” katika neno “hela” na “y” katika neno “yangu”. Kwa mfano, Mangi nipe ela angu aise!
  • Hali ya kupanda na kushuka kwa sauti, lafudhi pia huweza kujitokeza katika mazingira ya kupanda na kushuka kwa sauti hasa kwa wazungumzaji wageni wa lugha ya Kiswahili.
Kwa mfano, Habari zenu
                     Hamjambo wote
Hivyo basi pamoja na kuwa lafudhi inamtambulisha mzungumzaji fulani kuwa anatoka wapi (asili yake), lakini pia lafudhi huweza kuvuruga utaratibu wa lugha sanifu ambapo tunaona kuwa lafudhi inaweza kupoteza maana ya baadhi ya maneno kwa wazungumzaji wa lugha moja, kwa mfano neno “kura” na “kula” pia “mahali” na “mahari” ni maneno ambayo huweza kuleta utata hasa pale yanapotamkwa na jamii ya Wakurya.
MAREJEO
Crystal D, (2003) A Dictionary of Linguistics and Phonetics: Blackwell.
 Shengli F, (2003) A prosodic grammar of Chinese: University of Kansas.
Kihore Y.M na wenzake (2003) Sarufi maumbo ya Kiswahili sanifu sekondari na vyuo: Dar-es-Salaam
Kamusi ya Kiswahili sanifu (Toleo la pili 2004-2005). Dar es Salaam Tanzania
Massamba na wenzake (2004) Fonolojia ya Kiswahili sanifu (FOKISA) Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Dar es Salaam Tz
Massamba na wenzake (2009) SARUFI MAUMBO YA KISWAHILI SANIFU (SAMAKISA) Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Dar es Salaam Tz
Samwel M. (2009) Kozi tangulizi ya fonolojia na sintaksia ya kiswahili: (DUCE) Dar es Salaam

Print this item

  DHIMA KUU YA VIAMBISHI VYA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 11-28-2021, 11:31 AM - Forum: Maswali na majibu - No Replies

SWALI:
Kitezi cha kiswahili Mara nyingi hakiwezi kukaa peke yake kufuatana na viambishi vyenye uamilifu wa aina kadhaa, fafanua kauli hii kwa mifano ya kutosha.
Kiswahili ni lugha ambishi kama zilivyo lugha nyingine za Kibantu. Neno kiambishi lina maana ya kipashio chenye maana ambacho hufungiliwa kwenye mzizi wa neno ili kuletaKiswahili ni lugha ambishaji kama vile zilivyo lugha nyingine za Kibantu. Neno kiambishi lina maana ya kipashio chenye maana ambacho hufungiliwa kwenye mzizi wa neno ili kuleta maana inayokusudiwa. maana inayokusudiwa.
Tofauti na lugha zisizotumia viambishi kwa wingi kama vile Kiingereza ambapo msemaji huhitajika kubadilisha neno zima au kulazimika kutumia maneno mengi kwa nia ya kubadilisha kidogo tu maana iliyobebwa na kitenzi fulani, katika Kiswahili, msemaji hubadilisha tu viambishi katika kitenzi hicho hicho. Hebu tutazame mifano ifuatayo kuthibitisha madai haya. ‘He comes’ {Kiingereza} – ‘huja’ (Kiswahili); ‘He would have come’ (Kiingereza)- ‘Angalikuja’ (Kiswahili); ‘He who comes’ (Kiingereza) – Ajaye (Kiswahili) miongoni mwa mengine.
Lugha ya Kiswahili ina viambishi vya aina mbili ambavyo ni awali na tamati. Viambishi awali huwakilisha dhana tofauti za kisarufi ambazo ni pamoja na nafsi , ngeli, umoja na wingi, nyakati au njeo, urejeshi, mahali, wakati miongoni mwa nyingine. Viambishi tamati navyo huwakilisha mahali, wakati, rai na mnyambuliko.
Nafsi
Katika lugha ya Kiswahili, vambishi vya nafsi hutokea kabla ya mzizi wa neno. Viambishi hivyo ni vya aina sita: nafsi ya kwanza (umoja na wingi) nafsi ya pili (umoja na wingi), nafsi ya tatu ( umoja na wingi). Mifano : Mimi ninaimba wimbo mzuri, Wewe unatoka wapi? Yeye atakuja kesho. Tofauti inayojitokeza baina ya Kiswahili na Kihispania ni kuwa, viambishi vya nafsi vya Kihispania huja mwishoni mwa kitenzi ilhali vile vya Kiswahili hutokea kabla ya mzizi wa kitenzi. Tutaangazia mifano ifuatayo ili kuthibitisha jambo hili. Ninasoma(Kiswahili)- Leo (Kihispania), Unasoma (Kiswahili)- Lees (Kihispania), Tunasoma (Kiswahili)- Leemos (Kihispania). Herufi zilizokolezwa rangi zinawakilisha nafsi katika lugha zote mbili.
Ngeli
Tofauti na ilivyokuwa zamani, ambapo upangaji wa ngeli ulizingatia viambishi awali vya nomino, mtindo mpya unaojulikana kama upatanisho wa kisarufi unazingatia viambishi awali vya vitenzi katika kuziweka nomino katika makundi tofauti. Mifano: Kijiko kimevunjika- Vijiko vimevunjika, Uji umemwagika- Uji umemwagika.
Nyakati/Hali
Kiswahili kina nyakati tatu ambazo ni wakati uliopo, ujao na uliopita , tofauti na Kihispania ambacho kina takriban nyakati kumi na tano na Kiingereza ambacho kina nyakati mbili tu – wakati uliopo na wakati uliopita. Pamoja na nyakati hizo tatu, Kiswahili kina viambishi vya hali ambavyo pia hujulikana kama wakati kadiri ya hali. Hivi ni pamoja na: ki, ka, a, hu, me, ngali na kadhalika. Viambishi vya ( a) huwa havionyeshi wakati maalum wa kutendeka kwa kitendo kifanyavyo kiambishi (na) cha wakati uliopo. Waama, matumizi ya viambishi hivyo huwa hayaonyeshi mwanzo au mwisho wa kutendeka kwa kitendo. Mifano katika sentensi: Mama apika chakula; Wanafunzi hawa wajitahidi ; Tunda laanguka kutoka mtini; Maziwa yamwagika
Urejeshi
Huitwa viambishi vya urejeshi kwa sababu hutuarifu nomino inayorejelewa inapatikana katika ngeli gani. Vinaweza kuja kabla au baada ya mzizi. Vijapo kabla ya mzizi , huitwa ‘o’ rejeshi awali. Vitokeapo baada ya mzizi, huitwa ‘ o’ rejeshi tamati. Mifano: Jambo unalolifanya ni kinyume cha sheria (‘o’ rejeshi awali); Jambo ulifanyalo ni kinyume cha sheria (‘o’ rejeshi tamati). Muundo wa virejeshi hutofautiana kulingana na ngeli.
Mahali
Hivi huwakilisha ngeli ya mahali ya pa-ku-mu. Mifano katika sentensi: Ulipoketi pana siafu, Ulikoketi kuna siafu, Ulimoketi mna siafu. Zaidi ya kiambishi ‘po’ kutumiwa kuwakilisha mahali maalum, kinaweza kuonyesha wakati. Mfano: Utakapokuja utanikuta nikisoma. Hata hivyo, ‘po’ huwa haionyeshi wakati kamili wa kutendeka kwa kitendo hadi pale itakapoandamana na viambishi vingine; ‘napo’- wakati uliopo, ‘takapo’ – wakati ujao, ‘lipo’-wakati uliopita. Mifano katika sentensi: Anapokula hazungumzi; Atakapofika tutamlaki kwa shangwe; Alipomwona alimfanya tambiko la risasi.

Print this item

  ZIJUE KAZI ZA VIAMBISHI
Posted by: MwlMaeda - 11-28-2021, 11:29 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

Viambishi vina dhima kubwa katika sarufi. Katika mada hii tutajadili matumizi mbalimbali ya viambishi Na, Ki, U, Ni, Ji, Ku, Li, na Kwa.
Matumizi ya kiambishi “NA”
“Na” inaweza kutumika kuonesha hali zifuatazo:-
(a) Kuonesha wakati uliopo.
Mfano: -Sisi tunasoma vizuri.
-Jane anakimbia polepole.
(b) Kuonesha urejeshi wa mtendwa.
Mfano: -Yule aliniachia mwenyewe.
-Walinambia ninapendeza.
© Kusaidia kuunda mzizi wa neno.
Mfano: -Nazi imeoza.
-Nani atashinda leo usiku?
-Ugali unanata.
-Watoto walinatana.
(d) Kuonesha nafsi ya kwanza umoja.
Mfano: -Nakuomba urudi nyumbani
-Nakupenda.
-Nakushukuru sana.
(e) Husaidia katika kuonesha kauli za utendaji, yaani ya kutendana.
Mfano; -Wanapendana.
-Walisukumana.
-Walipoonana walishangaana.
Matumizi ya kiambishi “KI”
(a) Hutumika kuonesha ngeli ya KI-VI
Mfano: -Kiti kimevunjika.
-Kikapu kimeibwa.
(b) Hutumika kuonesha wakati ujao hali ya masharti.
Mfano: -Ukiniona tu utapofuka macho.
-Ukimleta tutamgombania.
© Huonyesha urejeshi wa mtendwa.
Mfano: -Tulikiona.
-Alikitupa kitumbua chake.
(d) Katika Nomino za vivumishi “Ki” hukaa mwanzo ili kuonesha hali ya udogo.
Mfano: -Kipaka kinakimbia.
-Kibibi kizee kinaumwa.
-Kitoto kidogo kinacheka.
(e) Kuonesha hali ya udogo katika hali ya dharau au ya kusifu.
Mfano: -Kitoto kipenzi kimekuja.
-Kichungwa kitamu kimeliwa.
-Kitoto kizuri kimezaliwa.
-Kibuyu kibovu kimepotea.
-Kitoto kibaya kimekufa.
(f) Hutumika katika kielezi kuonesha jinsi ya tendo linavyotendeka.
Mfano:-Mwanne anacheza kizee.
-Anakwenda kivivu.
-Walimpiga kizembe.
(g) Mara nyingine “Ki” husaidia katika kuunda mzizi wa neno.
Mfano: -Kisu kimeibwa.
-Kitana kimepotea.
-Kiti kimeharibika.
(h) Kiashirio cha dharau.
Mfano: -Kione.
-Kitazame.
-Kiangalie
Matumizi ya kiambishi “U”
(a) Kubainisha nafsi ya pili umoja.
Mfano: -Ulikula chakula bora?
-Umeniona ninavyopendeza?
-Unasoma sana usiku.
(b) Kuonesha hali ya ushirikishi.
Mfano: -Wewe u mototo wangu.
-Ulikuwa u mdogo.
-Ulikuwa u mwerevu.
© Kuunda mzizi wa neno.
Mfano: -Simba aliua watu sita.
-Sikumuua kwa makusudi.
(d) Hutumika kuonesha urejeshi wa mtendwa.
Mfano: -Wanaupenda.
-Waje wote walioula.
-Ulioupika utaupakua.
(e) Huweza kuonesha hali ya kunominisha.
Mfano: -Ulitaka kufanya Uhodari?
-Umasikini ni hatari.
-Tunahitaji Umoja.
(f) Kuonesha ngeli ya U-ZI, U-YA au U-I
Mfano; -Ugonjwa umeenea………Ngeli ya UYA
Ukuta umevunjika……….Ngeli ya U-ZI
Mgomba umeanguka………Ngeli yU-I
Matumizi ya Kiambishi “Ni”
(a) Hutumika kuonesha nafsi ya kwanza umoja.
Mfano: -Ninasoma vizuri.
-Sikufahamu kama nilimuonea huyu.
-Niambie.
(b) Hutumika kuonesha ushirikishi baina ya vitu viwili.
Mfano: -Kesi ni mkarimu.
-Mimi ni daktari wa meno.
© Hutumika kuonesha urejeshi wa mtendwa.
Mfano: -Alinipiga.
-Atanisukuma.
-Amenionea.
(d) Hutumika kuonesha mahali ikiwa “ni” itatokea mwisho wa nomino.
Mfano: -Nenda Uwanjani.
-Kachungulie chumbani.
Matumizi ya Kiambishi “KU”
(a) Kubainisha wakati uliopita.
Mfano: -Hakusoma.
-Hakuja.
(b) Kubainisha ukanushi.
Mfano: -Hakuona.
-Sikumpiga.
© Kunominisha kitenzi.
Mfano: -Kusoma hakuishi.
-Kusoma kwale kwanichukiza.
(d) Kubainisha urejeshi wa mtendwa.
Mfano: -Alikupiga.
-Atakusomesha.
-Hakukuona.
-Hakukukuna.
(e) Kuonyesha nafsi ya pili tu.
Mfano; -Alikuona.
-Watakuminya.
-Hakukukuta.
(f) Kusaidia kuundia mzizi wa neno au kubeba shina la kitenzi lenye silabi moja.
Mfano: -Yeye alitaka kula.
-Anakunywa chai.
-Maji yamekupwa.
(g) Kubainisha ngeli za majina katika ya “KU”
Mfano; -Kusoma kunafaidisha.
-Kucheza kwako kunanchukiza.
Matumizi ya Kiambishi “LI”
(a) Kuonyesha wakati uliopita.
Mfano: -Mimi nilikimbia.
-Mtoto alikuja.
(b) Kubainisha ngeli ya LI-YA
Mfano: -Jumba limebomoka.
-Gari limeanguka.
© Husaidia katika kuunda mzizi wa neno.
Mfano: -Amelima shamba.
-Atamlisha mtoto.
-Utalipa zote.
(d) Kubainisha urejeshi wa mtendwa.
Mfano: -Amelikimbiza.
-Ataliona.
-Amelipiganisha.
(e) Huonyesha kama kiashirio cha dharau.
Mfano: -Lione.
-Litazame.
-Liangalie.
Matumizi ya “Kwa”
(a) Hutumika kuonesha sababu ya kutokea tendo.
Mfano: -Amejiuzulu kwa uzee wake.
-Ameuliwa kwa ukaidi wake.
-Alimfuata kwa hasira zake.
(b) Hutumika kuonyesha kifaa kilichotumika kutendea tendo.
Mfano: -Alikwenda kwa gari.
-Amekula kwa kijiko.
-Alipigwa kwa rungu.
© Hutumika kuonyesha mahali litokeapo tendo.
Mfano: -Nimetumwa kwa Zainabu.
-Unampeleka kwa nani?
-Ninarudi kwa Mama yangu.
(d) Hutumika kuonyesha mfanano baina ya vitu viwili.
Mfano: -Wataingia wawili kwa wawili.
-Moja kwa moja tutaelekea njia hii.
(e) Hutumika kuonyesha utofauti baina ya vitu viwili.
Mfano: -Ghana ilifungwa mawili kwa moja.
-Wazee kwa vijana washirikiane.
(f) Hutumika kuonyesha hali ya tendo lilivyofanyika.
Mfano: -Anatembea kwa maringo.
-Walimpiga kwa nguvu zao zote.
-Alimfuata kwa ghadhabu kubwa.
Matumizi ya KA
  1. Kiambishi kiwakilishi cha Wakati Usiodhihirika
  2. Mama akamtuma mwanawe aende kuchota maji.
  3. Nikamwuliza anionyeshe sanduku lake.
  4. Katika vitenzi sambamba – kitendo kimoja kinapofanyika baada ya kingine
  5. Alikula akashiba kisha akalala.
  6. Tulifika nyumbani, baba akatuuliza tumewaacha wapi fahali.
  7. Kuagiza au Kuamuru
  8. ‘Kalaleni!’ Mama akawaamuru watoto.
  9. Kamwambie asirudi hapa tena.
  10. Kiishio cha kauli ya kutendeka
  11. Kijana mtundu alipigwa akapigika.
  12. Tulijaribu kufungua mlango lakini haukufunguka.

Print this item

  ATHARI YA VIAMBISHI NYAMBULISHI
Posted by: MwlMaeda - 11-28-2021, 11:23 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

Maana ya Viambishi:
Kutokana na Riro S. Matinde katika kitabu chake cha  Dafina ya Lugha na Nadharia, (2012).  Anasema; “Kiambishi hutokana na neno ambika ambapo kuambika ni kuweka kitu mahali kwa kukiegemeza kwa kingine”.  Hivyo basi anaendelea kusema kuwa; “Viambishi ni vineno vilivyoshikishwa katika mzizi wa kitenzi, kabla na hata baada ya mzizi wa kitenzi hicho”.
Hivyo basi tunaweza kusema kuwa viambishi ni mofimu zinazowekwa mwanzoni au mwishoni mwa kitenzi na kuleta maana fulani.  Pia tunaweza kusema kuwa kiambishi ni silabi inayofungamanishwa na mzizi wa neno, kwa hiyo kiambishi ni Mofimu Tegemezi.
Riro S. Matinde anaendelea kusema kuwa kuna aina mbili za viambishi ambavyo ni:-
(1) Viambishi Awali – hivi ni viambishi ambavyo hutokea mwanzoni mwa Kitenzi (kabla ya mzizi) na huwa vya aina mbalimbali.
(2) Viambishi Tamati – Hivi ni viambishi ambavyo hutokea mwishoni mwa Kitenzi (baada ya mzizi).
Viambishi vya Mnyambuliko:
Vitenzi hunyumbuliwa au kurefushwa kwa kuongezwa viambishi ambavyo hudokeza kauli mbalimbali kati ya Kitenzi na Kiishio.  Viambishi hivi vya mnyambuliko ni viambishi ambavyo hutokea baada ya mzizi wa kitenzi.  Huwa upande wa kulia wa mzizi.  Matinde anaeleza kuwa Viambishi hivi huwa na uamilifu ufuatao:
(a) Kiishio hicho ni kiambishi ambacho hutokea mwishoni mwa Kitenzi, aghalabu {a} hutokea katika vitenzi vinavyotokana na lugha za kibantu ilihali {e}au {i} au {u} hutokea katika vitenzi vyenye asili ya lugha za kigeni, mathalani ingia, ongoza, vua, starehe, ahidi, sahau na vinginevyo vingi.
(b) Virejeshi – virejeshi hutumika kulingana na ngeli za nomino, viambishi hivi hutuelekeza kwa mtenda au mtendwa katika baadhi ya vitenzi.
Kwa mfano:
(i)   Vibaka wasumbuao mjini wmeongezeka mara dufu.
(ii)   Akufukuzaye hakwambii toka.
(iii)   Kimsumbuacho ni urembo wake.
(iv)   Amwambiaye uongo ni bibi yake.
Kwa maana hiyo tunaweza kusema kuwa viambishi vya mnyambuliko wa vitenzi hubadilika Kisintaksia kulingana na mnyambuliko wa vitenzi. Kwani kama inavyojulikana kuwa Sintaksia ni tawi la Isimu linalojishughulisha na maumbo mbalimbali ya maneno.
Kutokana na maelezo hayo hapo juu tunaweza kusema kwamba athari za viambishi vinyambulishi katika kitenzi zinaweza kuonekana katika kauli mbalimbali kama ifuatavyo:
(i)  Kuali ya kutendea.
(ii)  Kauli ya kutendewa .
(iii) Kauli ya kutendana .
(iv)  Kauli ya kutendesha.
(i) Kauli ya kutendea – Kauli hii huonyesha hali ya kumfanyia mtu/kitu jambo fulani, na hapa atahari ya kiambishi huonekana pale ambapo Kitenzi hunyambuliwa au hurefushwa.  Kwa mfano:
  • Soma – som-e-a.
  • Imba – imb-i-a.
  • Cheza – chez-e-a.
  • Osha – osh-e-a
(ii)   Kauli ya kutendewa – Kauli hii huonyesha mtu / kitu kufanyiwa jambo fulani na mtu/kitu mwininge na athari ya kiambishi huonekana kama ifuatavyo:-
  • Weka – wek-ew-a.
  • Lima – Lim-iw-a.
  • Lipa – Lip-iw-a.
  • Beba – beb-ew-a.
(iii) Kauli ya kutendana – Hii ni ile hali ya kumfanya mtu kitendo naye anakufanya hivyo hivyo:
Mfano:
  • Piga – pig-an-a.
  • Pika – piki-a-na.
  • Omba – omb-a-n-a.
  • Fanya – fany-a-n-a.
(iv) Kauli ya kutendesha – Hii ni ile hali ya kumfanya mtu atende jambo Fulani.  Mfano wa athari za vitenzi vinyambulishi katika kauli hii ya kutendesha ni kama ifuatavyo:
  • Andika – andik-ish-a.
  • Lima – lim-ish-a.
  • Cheza – chez-esh-a.
  • Soma – som-esh-a.
Hivyo basi kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa viambishi vinyambulishi vina athari katika vitenzi kwani huonyesha kauli mbalimbali.   Pia ambapo vitenzi huyambuliwa au kurefusha

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO ' USTAARABU'
Posted by: MwlMaeda - 11-28-2021, 11:17 AM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

ETIMOLOJIA YA NENO ' USTAARABU'
Ustaarabu, katika Lugha ya Kiswahili) ni neno lenye maana: 1. 'hali ya mtu kuwa na maendeleo na mwenendo na maadili yanayokubalika katika jamii. 2. Mwenendo mwema unaozingatia heshima na utu wa binaadamu na kukubalika na binadamu wote.
Neno hili (ustaarabu) asili yake ni Kiarabu na huko ni 'isti-iraabu' استعراب' neno litokanalo na kitenzi cha Kiarabu ista-araba استعرب(ameiga silka na mwenendo wa Waarabu, amejishughulisha kusoma Taaluma za Waarabu, Fasihi yao, Historia yao na Maendeleo yao yatokanayo na kukaa katika miji) likiwa na maana ya 'hali ya kuiga silka na mwenendo wa Waarabu, kujishughulisha kusoma Taaluma za Waarabu, Fasihi yao, Historia yao na Maendeleo yao yatokanayo na kukaa katika miji)
Ile maana ya Kiswahili ya neno 'ustaarabu' kwa Kiingereza 'civilization' neno lake katika Lugha ya Kiarabu ni 'hadhwaara حضارة lenye kuhusishwa na maendeleo na mwenendo wa mtu unaotokana na kukaa kwake katika miji; kinyume na Mkazi wa maeneo ya vijijini/jangwani.(Badawiyyu/Bedui).
Hii ina maana neno 'ustaarabu' limechukua maana mpya lilipoingia katika Lugha ya Kiswahili.
Maana nyingine ya neno 'ustaarabu' katika Lugha ya Kiarabu ni: 1. Kuzungumza lugha chafu isiyo staha. 2. Hima ya Wazungu kujishughulisha na kutafiti Utamaduni wa Waarabu, Fasihi Yao, Historia yao, Maisha yao katika maeneo ya mijini na Lugha yao ya Kiarabu na Taaluma zake.
Shukran sana.

Na;
Khamis Mataka
+255 713 603 050

Print this item

  Usarufi wa Tungo
Posted by: MwlMaeda - 11-28-2021, 11:13 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

Usarufi wa Tungo
Mzungumzaji wa Kiswahili atakuwa na matatizo na usarufi1 wa tungo zifuatazo, yaani atakuwa na wasiwasi kuwa kanuni fulani za lugha ya Kiswahili zimevunjwa, na pia atatambua zimevunjwa kwa namna gani.
Quote:
1 usarufi ni sifa ya tungo kutii kanuni za kisarufi za lugha husika. Utosarufi kwa upande mwingine ni ukiukaji wa kanuni za lugha.
(8) Ile mtoto imechana kitabu chake.
(9) Watoto yao na baba wamekuja.
(10) Asha na Mahemba mewakimbia.
Si vigumu kwa mjua Kiswahili kuipa tafsiri sentensi ya (8) kwa sababu kilichokosewa ni upatanisho kati ya nomino kiima na vipashio inavyovitawala2, yaani kionyeshi {ile} na kitenzi {imechana}. Mjua Kiswahili anatambua kuwa tungo kama (8) inaweza kutolewa na mtu anayejifunza Kiswahili kabla hajajizatiti sawasawa katika upatanisbo wa makundi tofauti ya maneno ya Kiswahili. Anaweza kuisahihisha sentensi hiyo hivi:
Quote:
(8a) Yule mtoto amechana kitabu chake.
2 kutawala ni sifa ya kipashio kimoja kusimamia yanayotokea katika kipashio kingine au tungo moja kusunamia kinachotokea katika tungo nyingine.
Lakini tungo ya (9) inaonekana kuwa imevunja kanuni za “juu” zaidi za lugha, na mjua Kiswahili ataikataa moja kwa moja tungo hiyo, ingawaje anaweza kujaribu kuirekebisha isomeke kama:
Quote:
(9a) Watoto wamekuja na baba yao.
Kuna mambo kadhaa ambayo yamemlazimu mjua Kiswahili kuyatengeneza upya ili tungo ya (9) isomeke kama (9a). Kwanza neno yaohaliendi na neno watoto, bali na baba. VUe vile katika Kiswahili, kitenzi (kiarifu) cha sentensi huja baada ya nomino kiima na wala si baada ya kishamirishi. Nafasi ya na pia imebidi ibadilike. Hivyo kilichokosewa hapa ni mfuatano wa vipashio katika sentensi sahihi ya lugha ya Kiswahili.
Utosarufl wa tungo ya (10) hautokani na mfuatano wa maneno katika tungo hiyo, bali unatokana na ukiukaji wa mfuatano wa vipasbio ndani ya neno, kama usahihishaji ufuatao unavyoonyesha:
Quote:
(10a) Asha na Mahemba wamekimbia.
Hapa tunaona kuwa kuna mambo mengi yanaweza kusababisha utosarufi wa tungo kama: (i) upatanishi kati ya maneno yanayojenga sentensi; (ii) mfuatano wa maneno katika sentensi; (iii) mfuatano wa vipashio vinavyojenga neno.
Wakati huo huo, mjua Kiswahili atakubali usarufi wa tungo ifuatayo, hata kama maneno ya tungo hiyo ni mageni kwake:
Quote:
(11) Vile vikarusi vimekota takarani.
Akiangalia tungo hii, mjua Kiswahili anaweza kufikiri kuwa maneno yaliyomo ni ya kisayansi, au kama ameisikia tungo hiyo kutoka kwa watoto wadogo, anaweza akafikiri kuwa ni mchezo wa kitoto. Lakini hawezi kuwa na mashaka juu ya usahihi wa muundo wa tungo hiyo kwa vile anaweza kuihusisba kwa urahisi na tungo nyingine za Kiswahili kama hii ifuatayo:
Quote:
(12) Vile vifaranga vimeanguka majini.
Hii ni kwa sababu vipashio vilivyowekewa italiki katika (12) vinatoa vidokezo muhimu vya sarufi ya Kiswahili.
Pamoja na usarufi wa tungo, mjua lugha yoyote anayo maarifa yanayomwezesha kutofautisha kati ya aina za sentensi katika lugha yake kutegemea ‘kusudio’ la sentensi hiyo. Anajua, kwa mfano, ni tungo zipi ni za kuuliza, na aina za maswali yanoyoweza kuulizwa, pamoja na majibu yanayotegemewa; atajua zipi ni za taarifa, au za kebehi, utani, nk. Kwa mfano, ikiwa mjua Kiswahili ataulizwa (13) atatambua kwa urahisi kuwajibu lake linaweza kuwa (13a) na si (13b):
Quote:
(13) Mtoto yuko wapi?
(13a) Amelala.
(13b) Ndiyo.
Lakini ikiwa ataulizwa (14) atatambua kuwa (14a) haliwezi kuwa jibu ambapo (14b) linaweza kuwa mojawapo ya majibu ya swali hilo:
Quote:
(14) Mtoto amekwishakula?
(14a) Amelala.
(14b) Ndiyo.
Mjua Kiswahili pia anayo maarifa yanayompa utambuzi kuwa tungo zifuatazo hazihitaji kujibiwa kwa maneno, ila pengine kwa vitendo, kwa sababu ni tungo za “utendaji”, yaani zinazomtaka mzungumziwa kutekeleza kususdio la tamko:
Quote:
(15) Tafadhali nipatie maji ya kunywa.
(16) Simba huyo ananguruma, tukimbie!

Print this item

  NENO NI NINI?
Posted by: MwlMaeda - 11-28-2021, 11:11 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

Neno ni dhana tata, utata wake unatokana na kupewa fasili tofauti tofauti kutokana na uwanja linamotumika. Hapa tutachunguza dhana ya neno kwa mapana yake.
MGAWANYO WA KAZI
  • Maana ya neno kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali,
  • Kiini cha utata wa neno,
  • Hitimisho.
Kamusi ya Kiswahili Sanifu (toleo la tatu, 2013:420) wametoa fasili tatu za neno. Fasili ya kwanza “neno” limefasiliwa kama mkusanyiko wa sauti zinazotamkwa au kuandikwa pamoja na kuleta maana. Kisha wakafasili neno kama jambo kubwa  mfano nina “neno” nataka kukupa; ameniletea neno, na katika fasili ya tatu wamefasili neno kama mahubiri, mfano “neno” la Mungu.
Kwa mujibu wa Longman Dictionary (2008:1899) wamefasili neno  kama kipashio cha lugha ambacho mtu anaweza akaelewa iwapo kitakuwa kimesemwa au kuandikwa kama kilivyo. (tafsiri yetu)
Habwe na Karanja (2004:71) wanasema neno ni kipashio cha kiisimu kinachoundwa na mofimu moja au zaidi.
Katamba (1994:38) anasema neno ni kipashio kidogo cha maana katika lugha ambacho kina dhima ya kisarufi. Anaendelea kusema, neno linaweza kusimama peke na kuleta maana bila kupachikwa vipande vingine. Hivyo katika neno “childish” (utoto) linaweza kutenganishwa na kubaki “child” (mtoto) na neno hili likatumika kiupwekeupweke kwa sababu ni neno linalojitegemea. Lakini hatuwezi kutenganisha kipande “ish” kikasimama pekeyake na kuleta maana.
Sisi kama kundi (kwa malengo ya kozi hii) tunaona neno ni kipashio cha lugha kinachoundwa na mofu moja au Zaidi ambayo inaweza kusimama pekeyake na kuleta maana katika lugha mahususi.
Ni kweli dhana ya neno ina utata. Utata huo unasabishwa na vigezo tofautitofauti ambavyo hutumika katika kufasili dhana ya neno na mipaka yake.
Mdee (2010:5) anafafanua njia tatu zinaweza kutumika katika kufasili neno, njia hizo ni kama:- neno kama kipashio huru kisichogawanyika; maana ya neno kiothografia, na neno kama kipashio cha maana. Sisi tumeenda mbali kwa kuongeza fasili nyingine za neno kwa vigezo kama vile kigezo cha kisarufi katika kufasili dhana ya neno na kigezo cha kifonolojia.
Neno kama kipashio huru kisichogawanyika. Fasili hii ya neno ni ya Leonard Bloomfield (1933) inayosema “neno ni umbo dogo kabisa lililo huru”. Fasili hii ina mambo makuu mawili, kwanza neno liwe umbo dogo, pili neno liwe umbo huru. Hapa umbo dogo humaanisha umbo ambalo haliwezi kugawanyika bila kupoteza maana yake. Mfano neno “pasi” huwezi kuligawanya katika “pa” na “si” bila kupoteza maana yake. Hivyo umbo dogo ni lile ambalo linashikilia maana. Kwa upande wa neno kuwa huru ina maanisha umbo hilo lazima liweze kutamkwa pekee bila kutegemea au kuliambisha kwenye neno lingine, haya ni maneno kama vile njoo, lete, jua, n.k.
Tatizo(utata) la kigezo hiki: Ugumu wa kigezo hiki neno linalopewa uzito hapa ni lile katika lugha za mazungumzo pekee. Katika lugha za maandishi tunaweza kuwa na vipande vidogo vya maneno lakini ambavyo vikiwa huru hatuwezi kusema vina maana kwa kuwa huwa havirejelei kitu au hali yoyote ile. Mfano katika lugha ya Kiswahili vipande “na”, “kwa”, “tu”, n.k havina maana vikiwa pekee pekee. Katika lugha ya Kiingeza vipande kama “a”, “the”, “and”, “to”, n.k vivyo hivyo havina maana vikiwa pekee pekee.
Maana ya neno kiothografia. Kigezo hiki huchukulia neno kuwa ni maandishi yanayoacha nafasi mwishoni. Rubanza(2010), anaeleza kwamba neno kiothografia ni mfuatano wa maandishi ambao huacha nafasi tupu mwishoni bila uwepo wa nafasi tupu katikati. Neno hudhiirika linapokuwa katika maandishi tu na lisiwe na nafasi katikati. Mfano; ubao, chaki n.k. Maneno kama Askari kanzu, Bata maji, n.k huchukuliwa kama maneno mawili tofauti. Katika Kiingereza neno kama “cannot”, “blackboard”, n.k huchukuliwa kama neno moja. Maneno kama “washing machine” (mashine ya kufulia) na “White House” (ikilu ya marekani) huchukuliwa kama maneno mawili tofauti.
Matatatizo ya kigezo hiki: Hushidwa kuelezea maneno ambatani, kwao uandikaji wa neno ambatani kwa kutenga au kuacha nafasi katikati huchukulia kuwa ni maneno mawili. Hii sio sahihi kwani maneno ambatani huwa na dhana moja hivyo hutakiwa kuchukuliwa kama neno moja. Pia kigezo hiki hushughuliki tu na lugha ya maandishi na kuipuuza lugha ya mazungumzo ambayo ndiyo hutupatia lugha ya maandishi. Pia zipo kugha nyingine ambazo hazitengi maneno yake katika uandishi, pamoja ya kuwa ndani ya neno moja kunaweza kuwa na dhana nyingi zinazorejelewa. Mfano lugha ya Kigreenland Eskimo neno “uluminippug” maana yake ni “yumo mwanaume ndani ya nyumba yake”.
Dhana ya neno kifonolojia. Kigezo hiki huchukulia neno kuwa ni kipande cha lugha kinachotokana au kujengwa na kipashio kidogo cha kimatamshi. Kufuatana na kigezo hiki kuna vigezo fulani vilivyo wekwa ambavyo hutofautiana kutoka lugha moja na nyingine. Rubanza (ameshatajwa) hueleza kwamba zipo lugha ambazo upo uwezekano wa kulitambua neno kwa kutumia sifa za kimatamshi. Lugha kama hizi ni zile ambazo zina utaratibu wa kuweka mkazo mahali fulani maalumu katika maneno wakati wote. Anaeleza zaidi kwamba sehemu hiyo inaweza kuwa mwanzoni mwa kila silabi ya kwanza ya neno, au silabi ya pili toka mwisho kwa baadhi ya lugha. Kwa mfano chunguza sentensi ifuatayo kutoka katika lugha ya Kingereza; “I didn’t take the test yesterday” Kufutana na utaratibu wa lugha hii sentesi hii ina maneno matatu tu yaliyokolezwa, kwasababu mkazo huwekwa kwenye maneno yenye kubeba maana (content words). Utaratibu huu una vighairi kwa sababu kuna wakati hata yale maneno yasiyobeba maana (grammatical words) hubeba mkazo kwa sababu za kimsisitizo wa neno au maneno husika katika sentensi (prosodic stress) Mfano katika sentensi ilele “I didn’t take the test yesterday” Ikiwa mzungumzaji ataweka mkazo kwenye “I” atakuwa akionyesha msisitizo sio yeye aliyefanya jaribio jana. Ikiwa mzungumzaji ataweka mkazo kwenye “didn’t”atakuwa anasisitiza kuwa yeye hakufanya jaribio jana (labda kafanya jambo jingine). Na ikiwa mzungumzaji ataamua kuweka mkazo kwenye “the” atakuwa akimaanisha kuwa hakufanya jaribio hilo(linalokusudiwa na muulizaji) labda kafanya jaribio lingine tofauti.
Hivyo kwa kutumia kigezo cha mkazo katika maneno tunashindwa kufahamu neno hasa ni lipi. Je vile vipande vya sauti ambayo havibebi maana katika lugha basi navyo ni maneno? Na kama ndio, basi kwa nini lugha hii isivitambue kama ni maneno kamili kiasi cha kubeba mkazo asilia?
Dhana ya neno kwa kigezo cha maana. Kwa mujibu wa Mdee (ameshatajwa) hueleza kwamba neno ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana, hueleza zaidi kwamba neno ni lazima liwe na maana. Mfano; baba – mzazi wa kiume, mama – mzazi wa kike. Kwa hiyo kwa kutumia kigezo hiki neno hutambuliwa kuwa ni kipashio cha kiisimu chenye maana.
Utata wa kigezo hiki: Je, maneno yote ya lugha yana maana ya kisemantiki? Pia kuna maneno mawili au zaidi yenye maana moja, Kwa mfano; mkono wa birika, maana yake mchoyo. Yapo maneno mengine yenye maana zaidi ya moja, mfano; kaa, paa, na kata, maneno haya yakisimama yenyewe huwezi kupata maana moja mpaka yawe katika mahusiano na maneno mengine kwenye sentensi.
Dhana ya neno kisarufi. Kwa mujibu wa Katamba (1993:19) ili neno litambulike lazima liwe katika muktadha wa matumizi. Katamba, anasema neno moja linaweza kuwa na dhima mbalimbali na dhima hiyo itagundulika tu litakapokuwa ndani ya muktadha wa matumizi kwenye sentensi. Anatoa mtano wa neno la kiiingereza “cut” kwamba likiwa kiupweke upweke mtu hawezi kutambua linarejelea nini, pamoja kwamba neno hilo katika lugha ya Kiingereza ni kitenzi yaani “kata” lakini kuna wakati linaweza kutumika kurejelea nomino. Chunguza mifano hii: “I need my cut” na “I have cut my finger”. Ukiichunguza vizuri mifano hii “cut” katika sentensi ya kwanza hurejelea nomino yaani “nahitaji stahiki yangu”(tafsiri yetu)  na “cut” katika sentensi inayofuata hurejelea kitenzi yaani “nimekata kidole changu”(tafsiri yetu). Kigezo hiki pia huenda mbali kwa kufafanua kuwa pia maneno kama; na, tu,si, n.k katika Kiswahili na maneno; and, an, the, on n.k katika Kiingereza nayo hayawezi kutambulika yanarejelea nini lazima yawe katika muktadha wa matumizi ndio tunaweza kusema ni aina gani za maneno au kutambua maana zake.
Udhaifu wa kigezo hiki ni kwamba kuna maneno mengi sana ambayo maana zake hutambulika hata yasipokuwa katika muktadha wa matumizi kwenye sentensi, aya au kifungu cha habari. Maneno haya ni kama vile nomino za mahali kama vile Dar es Salaam, Ulaya, Bukoba n.k; nomono za pekee zinazorejelea majina ya watu kama vileMutashobya, Mwendamseke, Rubanza, n.k. Sasa tunajiuliza kuwa aina hizi za nomino na nyingine nyingi ambazo ni kama hizi je si maneno? Hivyo na kigezo hiki hakijajitosheleza katika kutupatia maana ya “neno” itakayokidhi mahitaji ya taaluma zote.
Tunahitimisha kwa kusema kwamba Pamoja na vigezo mbalimbali vinavyotumika kufasili neno kuonekana ndicho kiini cha ugumu wa fasili ya neno lakini pia tofauti za lugha nazo huchangia kufanya fasili ya neno kuwa ngumu. Hii ni kwa sababu tabia za lugha hutofautiana, kwa sababu neno linaweza kuwa neno katika lugha fulani lakini lisiwe neno katika lugha nyingine. Pia mitazamo tofautitofauti ya wataalamu nayo ni sababu nyingine ya ugumu huo. Hivyo ni muhimu kama wanafunzi wa kozi ya Mofolojia kuelewa vizuri vigezo hivi na kuhusisha mawazo ya wataalamu mbali mbali katika kuijadili dhana ya neno. Hii itatusaidia kutoyaacha maneno ambayo kwa fasili ya Kimofolojia hayaonekani kama ni maneno. Uchanganuzi wa kimofolojia wa maneno hushughulikia pia aina za maneno kama  vihusishi, viunganishi, vihisishi maneno ambayo kwa fasili ya kimofolojia yanaonekana kama si maneno kwa kuwa tu hayana maana hasa pale yanapokuwa pekee pekee bila kuhusishwa na maneno mengine kwenye muktadha wa matumizi.
MAREJELEO.
Bloomfield, L. (1933). Language. Henry Holt: New York.
Habwe, J. na Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Phonex Publisgers: Nairobi
Katamba, F. (1993). Morphology. Mac Millan Press Ltd: London
Katamba, F. (1994). English Words. Routledge: London
Mdee, S. (2010). Nadharia na Historia ya Leksikografia. TUKI: Dar es Salaam
Quirk, L. (2005). Longman Dictionary of Contemporary English. Pearson Longman: New York
Rubanza. (2010). basic Reading. Yaliyoandailwa na Rubanza.
TUKI (2013). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. (Toleo la tatu). Oxford: Dar es Salaam

Print this item

  VIPENGELE VYA ISIMUJAMII VINAVYOCHANGIA KATIKA URASMI WA LUGHA
Posted by: MwlMaeda - 11-28-2021, 11:04 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

KATIKA kuchunguza lugha, wanaisimu hutumia misingi ya kisayansi kama zifanyavyo sayansi nyingine. Maswala katika isimu huelezwa kwa udhahiri usio na utata wowote. Hoja huelezwa bila kuleta vuguvugu lolote la kimaana.
Habwe na Karanja, (2003) wanaeleza kuwa utaratibu na uwazi ni dhana zinazokaribiana sana. Bila kuwa na uwazi ni vigumu kuwa na utaratibu na kinyume chake.
Utaratibu ni kufanya jambo kwa mpangilio mzuri wenye kubainika na aghalabu unaweza kuhusisha wakati, idadi, umuhimu na hata ukubwa.
Katika kushughulikia na kuelewa lugha mwanaisimu hujikuta akiwa na kazi ya kutimiza majukumu ya kueleza maana na asili ya lugha, kuchambua muundo wa lugha, kueleza uhusiano kati ya lugha na asasi nyingine za mwanadamu na kuibua nadharia mbalimbali za lugha.
Hizi ndizo sifa bainifu ambazo kwa mara nyingi hutuelekeza katika uwezo wa kutofautisha lugha zinazotumika katika kudumisha mawasiliano ya kila siku miongoni mwa wanajamii.
Umilisi (langue) ni ujuzi alionao mjua lugha kuhusu lugha yake. Ni ujuzi alio nao mjua lugha ambao upo katika ubongo wake. Ujuzi huo huhusu kanuni zinazotawala lugha hiyo husika.
Ujuzi huu humwezesha kutambua sentensi sahihi, zisizo sahihi na kupambanua sententi zenye utata. Ujuzi huo humwezeha kupuuza makosa ya kiutendaji katika mazungumzo kama vile kuteleza kwa ulimi, kukatisha sentensi n.k.(Rubanza, 2003).
Utendaji (parole) ni kile asemacho mjua lugha katika muktadha wa mawasiliano ikiwa ni pamoja na makosa ya kiutendaji ya bahati mbaya na yale ya kukusudiwa. Vilevile tunaweza kusema ni udhihirikaji wa ujuzi wa lugha alionao mjua lugha.
Uamilifu au utumizi (functionalism) ni elimu inayohusu muundo wa lugha kwa kurejelea kazi zake za kijamii katika mawasiliano.
Inamchukulia mtu binafsi kama kiumbe-jamii na kuchunguza namna anavyojifunza lugha na kuitumia katika mawasiliano na wanajamii wenzake.
Urasmi (formalism) ni elimu ya maumbo dhahania ya lugha na mahusiano yake ya ndani. Huzingatia maumbo ya lugha kama uthibitisho wa kimalimwengu bila kuzingatia namna jamii inavyowasiliana.
Uelezi ni mtazamo ambao huelezea ukweli wa lugha jinsi ilivyo na inavyotumika na jamiilugha husika. Na siyo namna inavyotakiwa kutumika.
Isimu elezi haiweki kanuni ngumu au sheria ngumu zozote zinazotokana na mawazo ya mtu juu ya lugha fulani bali huelezea lugha kwa kuangalia namna lugha hiyo inavyojidhihirisha yenyewe.
Huelezea sheria na kanuni ambazo mzungumzaji mzawa ameziweka kichwani na zinazoakisi uwezo wake wa lugha. Kwa kifupi, haielezi wala kuagiza namna mtu anavyotakiwa kutumia lugha bali namna lugha ilivyo na inavyotumika na wamilisi wa lugha hiyo.
Uelekezi ni mtazamo unaojaribu kuweka kanuni za usahihi wa namna watu wanavyotakiwa kutumia lugha.
Katika misingi hii, lugha rasmi hutumika pakubwa tunapokuwa waangalifu zaidi katika mazungumzo yetu.
Kadri uangalifu unavyozidi kudhihirika katika mazungumzo fulani ndivyo yanavyopata nafasi kubwa zaidi kutambuliwa kuwa rasmi. Mfumo rasmi wa lugha huzingatia matumizi ya mseto wa sentensi changamano na sahili zenye kuwasilisha maana kamilifu.
Kwa mujibu wa Joos (1961), lugha rasmi haina madakizo au mapambo na aghalabu inahusishwa na kujitambulisha kwa wageni. Hujiepusha na urudiaji isipokuwa tu pale ambapo msisitizo unahitajika. Katika kukwepa udondoshaji, lugha rasmi huzingatia kanuni zote za kisarufi na usahihi.
Lugha rasmi ni aina ya mawasiliano yanayotumika katika mazungumzo na maandishi yaliyo rasmi kama vile kwenye mazingira ya afisini, mahakamani, uwasilishaji wa maazimio, maagizo, miongozo, nyaraka muhimu za kiserikali, hati za idara mbalimbali, matangazo ya kisheria au makala ya kitaaluma.
Katika matumizi ya lugha hii, usahili na ukweli wa mambo yanayojadiliwa ni kigezo muhimu sana kuzingatiwa. Mfumo wa lugha unaotumika katika matini ya kisheria kwa mfano, ni ule unaosisitiza kabisa usahili wa lugha ili kujaribu kuzuia ufafanuzi unaogongana na sheria hizo.
Aidha, mawasiliano katika shughuli rasmi hayafanywi ovyo tu bila ya kufuata mpangilio maalum wa matukio. Badala yake, huzingatia mtiririko maalum unaokusudia kuleta ukamilifu wa maana.
Lugha huhusisha matumizi ya zana za kiisimu zinazofanana au kulingana katika kuelezea mambo. Mathalan, tuandikapo barua za kiafisi, aghalabu tunajikuta tukitumia ‘klishe’ zilezile zilizokwisha kushamiri katika mawasiliano mengi ya namna hii. Fomu za kujazwa na wahusika ni mfano mzuri zaidi.
Mazungumzo yoyote rasmi hupangwa kabla ya kuwasilishwa ili kuepuka uradidi na urejeshi mwingi. Ni mpangilio huu wa hali ya juu ndio unaoipa lugha hii jina lake.
Kuna matumizi ya istilahi maalum zinazohusu masuala ya afisini au kidiplomasia. Aidha, vyeo au nyadhifa za wahusika mbalimbali hutajwa. Huzingatia uwazi kwa kuepuka matumizi ya misimu, nahau, mafumbo au lahaja.
Kwa ujumla, lugha rasmi ni namna ya mawasiliano katika nyanja za utawala, uendeshaji wa uongozi pamoja na masuala ya kisheria. Mawasiliano haya yanaweza kutekelezwa ama kwa njia ya maandishi au mazungumzo.
Matumizi ya viungo au miondoko ya mwili pia ni mbinu ya mawasiliano iliyo na viwango vyake vya urasmi.
Kwa mfano, katika mahojiano kwa minajili ya kutafuta ajira, matumizi fulani ya viungo vya mwili yanaweza kumdhihirisha msailiwa kama asiyependezwa na kazi hiyo, asiye mwaminifu, aliye na mtazamo hasi, asiye msikivu au aliye na wasiwasi au kiasi fulani cha aibu.
Matumizi ya lugha rasmi aghalabu hutegemea matukio, wakati, idadi ya walengwa, uhusiano baina ya mzungumzaji au mwandishi na hadhira yake pamoja na uwezekano wa habari kuwa  za kibinafsi au kwa ajili ya umma.

Print this item