DHANA YA LAFUDHI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: DHANA YA LAFUDHI (/showthread.php?tid=1594) |
DHANA YA LAFUDHI - MwlMaeda - 11-28-2021 DHANA YA LAFUDHI
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili sanifu (Toleo la pili 2004-2005) inaeleza kuwa lafudhi ni matamshi ya mzungumzaji yanayotokana na lugha yake ya mwanzo au lugha zinazomzunguka, au ni udhihirishaji wa sauti za lugha unaomtambulisha mtu mmoja au jamii ya watu.
Massamba na wenzake (2009) SAMAKISA, wanasema kuwa lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanayotokana na athari za kimazingira.Mazingira hayo yanaweza kuwa eneo atokalo mtu, mahali aliposomea, kiwango chake cha elimu na tabaka lake la jamii.
Kimsingi tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa lafudhi ni sifa ya masikizi ambayo humtambulisha mzungumzaji na jiografia yake, uzungumzaji huo huwatofautisha wazungumzaji wa lugha moja katika jamii au mazingira fulani.
Kwa mujibu wa wavuti wa www.shuledirect.co.tz/notes/views/195 wanadai kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha ya pili kwa watumiaji wengi wa Afrika Mashariki kwa hiyo hii inafanya kuwatambua wazungumzaji wa Kiswahili kulingana na makabila yao au maeneo wanakotoka. Kwa mfano hapa Tanzania tunaweza kuwatambua watu wa Mwanza kwa lafudhi yao, pia watu wa Mtwara kwa lafudhi yao.
Kwa mfano;
Katika mifano tajwa hapo juu kuanzia mfano wa kwanza mpaka wanne tunaona makosa yanayojitokeza katika baadhi ya tungo wanazozitumia. Kwa mfano katika mfano wa (a) tunaona namna jamii ya Wakurya inavyotumia herufi “r” badala ya “l”, vilevile katika mfano wa pili (b) tunaona namna jamii ya Wamakonde wanavyotumia herufi “n” na “ch” badala ya “m”na “sh”.
Katika mfano wa tatu © tunaona namna jamii ya Wasukuma wanavyoongeza vitamkwa katika baadhi yamaneno, kwa mfano katika mfano wameongeza vitamkwa “ma” katika neno “ng’ombe” na kitamkwa “ga” katika neno “unakamua”. Pia katika mfano (d) tunaona jinsi jamii ya Wahaya wanavyoshindwa kutamka herufi (ng’) katika tungo zao.
Lafudhi pia inaweza kujitokeza katika mazingira mbalimbali kama vile;
Kwa mfano; fyatu fyimechanika badala ya viatu vimechanika.
Pia Wanyakyusa hutamka “s” badala ya “z”, kwa mfano, mapindusi badala ya mapinduzi, vilevile hutamka herufi “ky” badala ya “ch” kwa mfano, kyiama kya mapindusi badala ya chama cha mapinduzi.
Kwa mfano, Habari zenu
Hamjambo wote
Hivyo basi pamoja na kuwa lafudhi inamtambulisha mzungumzaji fulani kuwa anatoka wapi (asili yake), lakini pia lafudhi huweza kuvuruga utaratibu wa lugha sanifu ambapo tunaona kuwa lafudhi inaweza kupoteza maana ya baadhi ya maneno kwa wazungumzaji wa lugha moja, kwa mfano neno “kura” na “kula” pia “mahali” na “mahari” ni maneno ambayo huweza kuleta utata hasa pale yanapotamkwa na jamii ya Wakurya.
MAREJEO
Crystal D, (2003) A Dictionary of Linguistics and Phonetics: Blackwell.
Shengli F, (2003) A prosodic grammar of Chinese: University of Kansas.
Kihore Y.M na wenzake (2003) Sarufi maumbo ya Kiswahili sanifu sekondari na vyuo: Dar-es-Salaam
Kamusi ya Kiswahili sanifu (Toleo la pili 2004-2005). Dar es Salaam Tanzania
Massamba na wenzake (2004) Fonolojia ya Kiswahili sanifu (FOKISA) Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Dar es Salaam Tz
Massamba na wenzake (2009) SARUFI MAUMBO YA KISWAHILI SANIFU (SAMAKISA) Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Dar es Salaam Tz
Samwel M. (2009) Kozi tangulizi ya fonolojia na sintaksia ya kiswahili: (DUCE) Dar es Salaam
Wavuti wa www.shuledirect.co.tz/notes.
|