MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: SICHELEI KUFA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: SICHELEI KUFA
#1
Mimi sichelei kufa, kudura yake Manani,
Kufa budi nitakufa, mchana ama jioni,
Hufa visivyo na ufa, sembuse aliye duni!
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.

Kama kufa ni maafa, naona bwana huponi,
Kiumbe hana sarifa, mauti yamo milini,
Nikifa hupati mafa, furaha yako nini?
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.

Ikiwa kufa kashifa, si peke yangu ufuni,
Ikiwa neno la dhifa, sina mfundo moyoni,
Iwapo kufa sharafa, sifi ninangoja nini?
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.

Hufa watu wenye sifa, na mafao duniani,
Wapenzi wake latifa, kama Mitume wa dini,
Hufa walaji wa mofa, na walao biriani,
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.

Kafa Tumwa Mustafa, patabaki kitu gani?
Maneno yako kifafa, hayana fikira ndani,
Si maneno ya wadhifa, mfano wa punguani,
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.

Ebu niambie kaifa, nguvu huletwa na nini?
Siyo yangu taarifa, maneno yenu shetani,
Na nyinyi mwataka sifa, nayo haipatikani,
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.

Uchache wa maarifa, ama kasoro kichwani,
Ni neno la takilifa, kwa hukumu na maoni;
Ndoa haina hilafa, ni sheria ni kanuni,
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.

Ndoa kitu ashrafa, utumwa wajia nini?
Ndoa jambo mzofafa, huwaje umajinuni!
Ndoa ni lulu nadhifa, nimehuni kitu gani?
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.

© Shaaban Robert – Kielelezo cha Fasili

Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)