MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 44 online users.
» 0 Member(s) | 43 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  SWALI: AINA ZA VIRAI KWA MUJIBU WA MASSAMBA NA WENZAKE
Posted by: MwlMaeda - 06-27-2021, 04:21 PM - Forum: Mitihani - No Replies

SWALI:
Jadili mtazamo wa Massamba na wenzake kuhusiana na aina za virai ukilinganisha na mtazamno wa wanazuoni wengine.
UTANGULIZI
Kirai ni dhana pana na yenye mkanganyiko mkubwa kiasi cha kuwaibua wanazuoni mbalimbali ambao kila mmoja amejitahidi kwa uwezo na uelewa wake kufafanua dhana hii. Kwa mahitaji ya swali hili tutatalii mitazamo ya wataalamu mbalimbali akiwemo Massamba na wenzake katika kufasili dhana hii ya kirai na aina za virai.
KIINI
FASILI YA KIRAI
Kwa kuanza na tuangalie fasili ya kirai kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali Massamba na wenzake (2009), wanasema kuwa kirai ni kipashio cha kimuundo chenye zaidi ya neno moja na ambacho hakina muundo wa kiima kiarifu.
Fasili hii ya Massamba na wenzake inaelekea kutuaminisha kuwa kirai ni lazima kiwe na zaidi ya neno moja. Swali la kujiuliza hapa ni je, neno kuu linalotambulisha aina ya kirai likisimama peke yake haliwakilishi aina husika ya kirai? Ukweli ni kwamba kila neno kuu la kirai lisimamapo pekee huwakilisha aina husika ya kirai hata bila ya kuambatana na kijalizo chochote cha kirai.
Mfano:
Kirai Nomino
Kirai
hiki chaweza kuwa nomino pekee au nomino na kijalizo.
(a) Mtoto mzuri
           KN
(b) Mtoto
        KN
Kihore na wenzake (2007), wanasema kuwa kirai ni kipashio cha kimuundo chenye neno
moja au zaidi lakini bila uhusiano wa kiima kiarifu. Kwao mahusiano ya kiima
kiarifu ni yale yanayoonesha anayetenda jambo na tendo linalotendwa, anayetenda
jambo ni kiima na tendo linalotendwa ni kiarifu.
Mfano:
Mtu mnene/ anachoma nyama.
   Kiima                kiarifu
TUKI, (2011), wanadai kuwa kirai ni kipashio chenye zaidi ya neno moja lakini ambacho hakina muundo wa kiima kiarifu.Maana hii ya TUKI inawiana na ile ya Massamba na wenzake.
Mdee, J.S (2007) anasema kuwa kirai ni neno au kifungu cha maneno chenye neno kuu moja. Kwa mujibu wa Mdee kirai kinaweza kuwa neno moja au kifungu cha maneno. Uhusiano kati ya neno kuu na maneno mengine (vijalizo) ndio hutambulisha na kutofautisha aina ya kirai.
Fasili zote hapo juu zinashadadia mambo ya msingi kuwa kwanza kirai sharti kijikite katika mahusiano baina ya maneno ambapo huwa kuna neno kuu moja linalotawala aina ya kirai, pili neno kuu la kirai huweza kusimama pekee au kuambatana na kijalizo kimoja au zaidi. Hivyo basi kirai kinaweza kusimama kama neno moja au zaidi iwapo tu kuna neno kuu linalotawala na kumiliki maneno mengine.
AINA ZA VIRAI
Kuhusu aina za virai wataalamu pia wametofautiana, tofauti zao zipo hasa katika aina na idadi lakini pia matumizi ya istilahi zao.
Massamba na wenzake (2009) wanatambua aina tano za virai ambazo ni:
·      Virai – nomino
·      Virai – vitenzi
·      Virai – vivumishi
·      Virai – vielezi
·      Virai – viunganishi
Zabron, T.P (2017) yeye anatambua na kutetea aina sita za virai ambazo ni:
·      Kirai – nomino
·      Kirai – kitenzi
·      Kirai – kivumishi
·      Kirai – kielezi
·      Kirai – kihusishi 
·      Kirai – kibainishi
Naye Mdee, J.S (2007) anatambua aina tano za virai ambazo ni kama zifuatazo:
·      Kirai – nomino
·      Kirai – kitenzi
·      Kirai – kivumishi
·      Kirai – kielezi
·      Kirai – kihusishi
Ukichunguza kwa makini miongoni mwa wanazuoni waliorejelewa katika kazi hii utabaini kuwa kuna mfanano juu ya idadi kati ya Massamba na Mdee isipokuwa Zabron ambaye anatambua aina sita. Baada ya uainishaji huo hapa chini tutaonesha tofauti baina yao kwa kurejelea aina wanazotofautiana na misingi ya utofauti huo.
TOFAUTI ZA AINA ZA VIRAI
Kwa kuanza na kundi la Massamba na wenzake, wao hawatambui kirai kihusishi badala yake wanatambua kirai kiunganishi. Kiunganishi kinaelezwa kuwa ni neno linalounganisha pande mbili zenye hadhi sawa kisarufi. Msingi wa tofauti hii ni kutokana na ukweli kwamba maneno yanayotumika kama kiunganishi ndiyo pia hutumika kama kihusishi.
Maneno hayo ni kama vile: Ingawa, Na, Kwa kuwa, Bila, Pasipo, Sembuse, Lakini,
Mfano:
Baba alifika ingawa mama hakumuona
Shule imejengwa na mafundi wameondoka
Wanafunzi walifeli kwa kuwa walimu hawakuwafundisha ipasavyo
Kwa upande wa Mdee, J.S (2007) na Zabron, T.P (2017) wanatambua kirai kihusishi kama aina moja wapo ya virai na hawatambui kirai kiunganishi. Mdee, (ametajwa) anasema kirai kihusishi ni kirai ambacho neno kuu ni kihusishi na Kihusishi ni neno linaloonesha uhusiano baina ya pande mbili zenye hadhi tofauti kisarufi.
Mifano ya maneno yaundayo kirai kihusishi ni kama vile:
Kwa, ya, na, au katika
Mfano:
–       Alienda kwa miguu
–       Atakuja kwa amri yako
–       Anasoma na mama
–       Amelala katika chumba
Kwa upande mwingine Zabron, T.P (2017) yeye pamoja na kutambua kirai kivumishi kama wengine pia ameongeza aina moja zaidi
ijulikanayo kama kirai kibainishi (KB). Anafafanua zaidi kuwa KB ni kirai ambacho neno kuu ni kibainishi. Vivumishi vibainishi vinaundwa na maneno kama vile: wawili, changu, kile, wote, hawa au wangu.
Mfano:
–       Wanafunzi wale pale
–        Kitabu hiki
–       Wachezaji wote hawa
Wapo wanaoona kuwa aina hiyo ya kirai ni sehemu tu ya kirai kivumishi na pengine ndio sababu ya kutoainisha kama aina ya
kirai inayojitegemea.
HITIMISHO
Kwa ujumla dhana ya kirai ni pana na yenye utatanishi mkubwa usioweza kumalizwa kwa urahisi. Ikumbukwe kuwa dhana hii inaukilia zaidi misingi ya kisarufi ya umiliki na utawala wa kategoria za maneno ambapo maneno makuu humiliki na kutawala maneno mengine katika msululu wa kategoria za maneno. Watangulizi katika taaluma hii walianza kwa kuainisha aina tano za maneno makuu ambazo ndizo zilizotumika kama kigezo kikuu cha kuamulia aina ya kirai. Hivi leo mitazamo inazidi kuibuka kutokana na mwamko wa wanazuoni wa kisasa katika kushughulikia dhana hii. Hata kazi hii itabaki kuwa kwego ya kuendelezea mpando wa kitaaluma katika kuifikia kweli ilipo.
MAREJELEO:
Massamba D.P.B na wenzake (2009) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA): Sekondari na vyuo, TUKI, Dar es salaam.
Mdee, J.S (2007) Sarufi ya Kiswahili: Sekondari na Vyuo, DUP, Dar es Salaam.
Kihore Y.M na wenzake (2007) Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA): Sekondari na Vyuo, TUKI, Dar es salaam. TUKI
(2011) Kamusi ya Kiswahili Sanifu.  TUKI, Dar es salaam.
Zabron, T.P (2017) Miundo Msingi ya Sarufi ya Kiswahili. Karljamer Publishers Ltd, DSM.

Print this item

  OSW 121 / OSW 131 : UTANGULIZI WA LUGHA NA ISIMU –JARIBIO KUU MAALUMU —Alhamisi , 05
Posted by: MwlMaeda - 06-27-2021, 04:06 PM - Forum: Mitihani - No Replies

Print this item

  OSW 226: USHAIRI WA KISWAHILI—JARIBIO KUU—-Ijumaa , 10 February 2012
Posted by: MwlMaeda - 06-27-2021, 04:01 PM - Forum: Mitihani - No Replies

Print this item

  TENDI ZA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 06-27-2021, 03:49 PM - Forum: Ushairi - No Replies

.pdf   TASWIRA YA KIFO CHA SHUJAA KATIKA UTENDI.pdf (Size: 148.22 KB / Downloads: 3)

Print this item

  KATEGORIA ZA KILEKSIKA
Posted by: MwlMaeda - 06-27-2021, 03:34 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

Kategoria ya kileksika ndilo kundi la kwanza la kisemantiki ambapo vitu vyote vilivyo katika ulimwengu, vinavyoonekana na visivyoonekana hupewa majina ya kidhahania kimakundi. Makundi hayo si ya ubia bali hutegemea jamii-lugha, utamaduni wao na mazingira yao. Uainishaji wa vitu kimakundi hutokea bila kufahamu, kufikiri au kupanga. Hali ya ufahamu hutokea panapozuka utata.

Rosch (1975) anaziita kategoria hizi za kisemantiki kategoria tambuzi. Kategoria hizi hupangwa na watumiaji wa lugha kutegemea tajiriba zao, imani na mazoea ya  jamii au kundi fulani la kijamii, na jinsi wanavyouona ulimwengu wao bila shaka itadhihirika kutokana na kategoria tofauti tofauti za kisemantiki. Kila kategoria huwa na kielelezo chenye sifa mahususi, na chochote kinachokiuka sifa za kundi hubainika kimaelezo na kuwekwa katika kundi lingine.
Kwa mfano, kasuku anaweza kutumika kama kielelezo cha ndege ilhali popo ambaye ana sifa za ndege vilevile hutofautishwa na ndege kwa vile baadhi ya sifa zake ni tofauti na zile za ndege wengine.
Mbinu nyingine ya uainishaji ni ile iliyotumiwa na Voegelin (2006) na inazigawa kategoria za kisemantiki kwa matapo manne. Matapo hayo ni pamoja na 1) sura ya nchi pamoja na vitu na viumbe vilivyomo, 2) tabia na shughuli za watu, 3) shughuli za kiakili pamoja na hisia, jazba na maadili na, 4) watu na mahusiano kati yao. Katika kujumlisha matapo haya ya kusemantiki, Voegelin (Aprili 2006) katika makala ya AIATSIS anayaita makundi ya kisemantiki ambayo ni pamoja na nomino, vivumishi, vitenzi, na mengineyo anuwai yanayotoa maana msingi za dhana mbalimbali. Kategoria za kisemantiki zimerejelewa kama kategoria za kisintaksia na na kisemantiki na Bennet (2000).
Mbinu nyingine inayotumiwa kuainisha kategoria za kileksika ni ile inayoyagawa maneno ya lugha kwa makundi mawili makuu. Makundi hayo ni maneno makuu na maneno ya kimatumizi. Kundi la kwanza lina maneno mengi mno, na kila neno huwa na sura mbalimbali kutegemea jinsi linavyobainika kiuamilifu katika tungo.
Sura hizo zinatokana na uambishaji wa maneno hayo. Kundi la pili lina maneno machache, na maneno hayo huwa hayabadilikibadiliki (Crystal, 2003).
Maneno katika lugha hugawanywa katika sehemu mbalimbali kutegemea matumizi yayo katika upatanisho wa kisarufi.

Migao hiyo ndiyo huitwa aina za maneno. Kila lugha ina maneno mengi yanayotumika katika mawasiliano ya kawaida na yale yanayotumika katika miktadha na taaluma maalum, na uianishaji huo hutegemea maana au semantiki, maumbo ya maneno hayo au mofolojia yao pamoja na uamilifu wa maneno hayo kwenye tungo, (Kapinga, 1983; Mgullu, 1999).
Nyanja za kileksika ndizo huorodheshwa kwenye makamusi ya lugha na maana za kila neno kuelezewa. Pamoja na maana msingi ya neno, matumizi yake pia huelezwa pamoja na jinsi neno hilo hubainika kimatumizi. Kando na matumizi yake, maneno huelezwa kama ni ya umoja au wingi, miktadha yanamotumika pamoja na makundi yao. Katika ufundishaji wa sarufi, maana msingi za maneno husisitizwa pamoja na taratibu za upanganji wa maneno hayo kenye tungo ili maana ziweze kufasiriwa kwa urahisi.
Kategoria za kileskika zimeelezwa kama aina za maneno katika lugha za Kiswahili na Ekegusii (Whiteley, 1956 ; Massamba na wenzake, 1999 ; Habwe na Karanja 2004). Katika lugha ya Kiswahili maneno yameainishwa kwa makundi manane  makuu ambayo ni nomino, viwakilishi, vivumishi, vitenzi, vielezi, viunganishi, vihusishi na vihisishi. Majina ya makundi hayo yanatokana na uamilifu wayo katika sintaksia. Katika lugha ya Ekegusii makundi yaliyotambuliwa na Whiteley (1956) ni pamoja na nomino, viwakilishi, vivumishi, vitenzi, vielezi, viunganishi, vihusishi na vihisishi. Taratibu hizi za uainishaji wa maneno katika lugha hizi mbili unaelekea kushabihiana kwa sababu lugha hizi zote ni za Kibantu na muundo wake wa kisintaksia unashabihiana sana.
Utafiti huu utachunguza kategoria mbili za kileksika ambazo ni nomino na vitenzi. Nomino ni maneno yanayotajia vitu, watu, hali na mahali. Kuna aina mbalimbali za nomino, (Mgullu, 1999 ; Habwe na Karanja 2004). Katika lugha za Kiswahili na Ekegusii, nomino zina mshabaha mkubwa kimaana na kiothografia, hasa ikizingatiwa kuwa hizi zote ni lugha za Kibantu.
Mifano ya nomino ni :
Kiswahili         Ekegusii
Mtu                 Omonto
Nyumba          enyomba
Utamu              obwansu
Kuku               engoko
Maji                 amache
Munyu             omonyo
Maneno haya yana maana mahususi zinazoeleweka yanapoelezwa bila miktadha ya kimazungumzo. Tofauti na maana msingi za maneno haya, neno linapowekwa kwenye muktadha kimazungumzo linapata maana nyingine, kwa mfano:
3. Mainye n’achete enyomba yaye. Mainye anaipenda nyumba yake. Kando na maana msingi ya nyumba, nomino hiyo inapata maana nyingine ambayo inadhihirika kiusemi kwamba: Mainye anaipenda familia yake Mazungumzo yanaliwezesha neno ‘nyumba’ kusimba maana nyingine tofauti na uwazi na hivyo kuzua umaanisho wa familia.
Vitenzi ni maneno yanayoeleza mambo yanayotendeka. Massamba (2004) anaeleza kitenzi kama ‘Kipashio kinachotoa taarifa kuhusu tendo linalofanyika, lililofanyika au litakalofanyika.’ Lugha zote zina maneno ya kutajia vitendo. Lugha za Kiswahili na Ekegusii zina vitenzi vingi ambavyo hubainisha mlingano wa kimuundo.
Mifano ya vitenzi katika lugha hizi ni:
Kiswahili         Ekegusii
Amka              booka
Funga              sieka
Toka                sooka
Angalia             rigereria
Lala                  raara
Maana msingi za vitenzi hivi katika lugha hizi ni mahususi. Hata hivyo, kimazungumzo vitenzi hivi huweza kupata maana nyingine tofauti na maana za kileksika, na maana hizo zinaweza kufikiwa na msikilizaji kwa kutumia mbinu ya ufaafu katika miktadha maalum, kwa mfano, mtu akisema;
4. Tom nere osieka
    Tom ndiye alifunga
Uwazi wa kauli hii ni kwamba Tom ndiye alifunga (pengine mlango) lakini umaanisho wake katika mazungumzo ukawa unaelekea kwenye ile hali ya kuwa wa mwisho katika mashindano fulani. Washiriki wa mazungumzo haya ni lazima wawe katika hali sawa ya kimawazo ili kupata maana ya kile kilichomaanishwa ingawa hakikusemwa kwa kutumia mbinu za uhusiano.

Print this item

  VIGEZO VINAVYOSABABISHA UGUMU WA KUJIFUNZA LUGHA YA PILI
Posted by: MwlMaeda - 06-27-2021, 03:01 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

Vigezo vinavyosababisha ugumu wa kujifunza lugha ya pili
Hivyo vipengele vitano vinavyojitokeza kurahisisha kujifunza lugha-mama huwa vigumu
kupatikana katika kujifunza lugha ya pili, yaani mazingira, muda, walimu,
mwingiliano na lugha nyingine, uhusiano na wengine.
Mwingiliano wa lugha-mama na lugha ya pili ni kigezo kikubwa sana. Mwanafunzi wa makabila
mbalimbali wanashindwa kukimudu Kiswahili kutokana na athari za lugha-mama zao.
Kuna matatizo ya:
(a) Kuchanganya sauti au kubadili sauti k.m. chai (wanyakyusa) kyai
(b) Kuondoa sauti k.m. halafu (wahaya) alafu
© Kuongeza sauti k.m. mtu (wajaluo) mutu
(d) Kubadili sauti k.m. thelathini (wasambaa) selasini
Kila mtoto mwenye akili timamu anamudu vizuri sana lugha-mama yake. Lakini inapofika lugha ya pili panajitokeza matatizo mengi. Tutawezaje kupunguza matatizo hayo?
Kwanza, kujitahidi kufuata kanuni zile za kujifunza lugha ya kwanza zinazowezekana k.m. kusikiliza na kuzungumza kutangulie; kisha kusoma na kuandika.
Pili, ufundishaji ya lugha ya pili pia uwe katika mazingira halisi. Mwalimu ujitahidi kutengeneza mazingira halisi na kutumia mifano dhahiri. Kama vitu dhahiri kama nyoka, waziri n.k. haviwezi kuletwa darasani basi picha na michoro dhahiri itumike.
Tatu, mwalimu utoe mazoezi mengi na ya mara kwa mara. Mazoezi hayo yatajumuisha stadi zote za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika.
Nne, katika kufanikisha kujifunza lugha ya pili, itabidi kuwa na marudio ya mara kwa mar. hii itasaidia kujenga uzoefu na hivyo kuimarisha uzingatiaji.

Print this item

  Harakati Zinazohusu Swala la Wanawake Katika Tanzania
Posted by: MwlMaeda - 06-27-2021, 02:43 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

.pdf   Harakati Zinazohusu Swala la Wanawake Katika Tanzania.pdf (Size: 270.94 KB / Downloads: 0)

Print this item

  SIKU 100 ZA MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA MCHANGO WAKE KATIKA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 06-27-2021, 02:33 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

SIKU 100 ZA MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA MCHANGO WAKE KATIKA MAENDELEO YA KISWAHILI UCHAMBUZI WA MASUALA 11 MUHIMU YAHUSUYO LUGHA ADHIMU NA AUSHI YA KISWAHILI

Anaandika PhD Dkt.Ahmad Sovu

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kazi iendelee.

Tunaendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuazima pumzi yake. Amina.

Wapenzi wasomaji wa makala zetu mnamo tarehe 19/03/2021 Rais wetu Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan aliapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Rais wa awamu ya 6 kufuatia kutawafu kwa Rais wa awamu ya 5 Dkt.John Pombe Magufuli tarehe 17/03/2021.

Mheshimiwa Rais Samia ametimiza siku 100 ambako kilele chake kitakuwa siku ya Jumatatu.

Makala haya yamekusudia kuonesha mchango wa Rais Samia na serikali yake kwa kipindi cha siku 100 kuhusu lugha ya Kiswahili.

1 Historia fupi kwa nini siku 100?

Ili kujenga ufahamu wa pamoja, tupitie historia fupi ya siku 100 katika nchi mbalimbali kama ilivyofafanuliwa katika makala ya Ndugu Abbas Mwalimu-Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia ambaye yeye amezungumzia siku 100 za Rais Samia kwa mnasaba au kwa jicho la Diplomasia.

Anafafanua na tuna mnukuu hapa:

Kimsingi asili ya siku 100 zilianza kutazamwa kuanzia mwaka 1933 wakati huo Rais Franklin Delano Roosevelt  alipoapishwa kuwa Rais wa 32 wa Marekani tarehe 4 Machi, 1933 katika kipindi ambacho kulikuwa na mdororo mkubwa wa uchumi nchini  Marekani na duniani kwa ujumla

Rais Roosevelt alifanya mabadiliko makubwa na ya haraka ya kisera katika mfumo wa uchumi na jamii ili kukabiliana na hali hiyo ya mdororo

Rais Roosevelt alihakikisha ndani ya miezi mitatu ya mwanzo Serikali yake inapeleka miswada mingi ya mabadiliko ya sheria mbalimbali Bunge la Congress ili kupambana na mdororo huo

Serikali ya Rais Roosevelt ilifanikiwa kuidhinisha miswada 76 iliyolenga kukabiliana na mdororo  kuwa sheria ndani ya siku 100 na hivyo kuchukuliwa kama mafanikio katika kipindi kifupi cha kuwepo madarakani.

Rais Roosevelt maarufu kama FDR alijiwekea utaratibu wa kuzungumza na wananchi moja kwa moja kupitia redio na kuwaeleza namna alivyokuwa akikabiliana na tatizo hilo na hivyo kuondoa wasiwasi kwa wananchi

Tangu kufariki kwake tarehe 12 Aprili, 1945 siku 100 zimekuwa zikichukuliwa kama kipimo cha namna gani Rais wa Marekani atakabiliana na changamoto zilizojitokeza kwa wakati huo na namna gani ataonesha mwanga wa mafanikio

Utaratibu huu umerithiwa na nchi nyingi duniani ikiwamo Tanzania ambapo hadi Jumatatu itakuwa kilele cha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kutimiza siku hizo

Baada ya kupata ufahamu huo. Ufuatao ni mchango wa Rais Samia na serikali yake katika maendeleo ya Kiswahili kama ifuatavyo:

2 Katika Elimu

Katika hotuba yake baada ya kuwaapisha makatibu wakuu na viongozi mbalimbali wa serikali aliwataka viongozi wanaosimamia sekta ya elimu kutafakari juu ya kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika elimu. Alisema:

...Lakini pamoja na kuangalia suala zima la Historia yetu na kutumia lugha yetu ya Kiswahili kwenye elimu, sasa hivi eeeh nchi za Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki Kiswahili ni somo katika selabasi zao. Lakini na sie wenye Kiswahili bado ni somo kwenye selabasi yetu. Sasa tunavyosema tunakuza Kiswahili...sijui liangalieni vizuri. Ni mawazo kutoka kwangu liangalieni vizuri...msije mkasema Rais kasema nasema tuliangalie

Ukitazama maelezo haya ni dhahiri Mheshimiwa Rais aliwataka wadau wa elimu na viongozi wanaosimamia masuala ya elimu kuwa na tafakuri juu ya matumizi ya Kiswahili katika elimu.
Hatua hii kwa namna moja ni kama imeanza kuchukuliwa hatua. Ambapo hivi karibuni tumeshuhudia taasisi ya elimu ikifanya mijadala na wadau kuhusu mifumo bora uendeshaji wa elimu nchini. Wadau wa Kiswahili na wataalamu wengine bila shaka wametoa na wanaendelea kutoa maoni yao juu ya Kiswahili kutumika kufundishia.

3. Kuwatia moyo Wabunge wa Kenya kuhusu matumizi ya Kiswahili
Mnamo tarehe 05/05/2021 alilihutubia Bunge la Kenya. Katika hotuba yake pamoja na mambo mengine aliwaeleza Wabunge hao kuwa yeye ni mfuatiliaji mzuri sana wa Bunge hilo. Katika ufuatiliaji wake hufurahishwa sana na matumizi ya Kiswahili cha Kenya ambacho kina vionjo mbalimbali. Anasema:

Kiswahili chenu kina vionjo vingi, kuna vionjo vingi ambavyo peke yake ni burudani tosha kusikiliza(vicheko) anaendelea kusema:

nilikuwa namsikiliza Mheshimiwa Spika anavyoshindwa kutaja namba za miaka (vicheko) kwa Kiswahili lakini inafurahisha kwamba mliishatunga kanuni za Bunge na mkamualika Mheshimiwa Job Ndugai kuja kuzindua kanuni zile tarehe 31 Oktoba 2019. Hii inatia moyo kuwa tuko pamoja  na kweli mnataka kutumia Kiswahili lakini hatua kwa hatua...Rai yangu kwenu ni kuwaomba msaidie kuleta uhusiano wetu

Maelezo haya ya Mheshimiwa Rais Samia  yanatia moyo Wakenya na kuzidi kuzungumza Kiswahili zaidi na kwamba kukifahamu ni hatua kwa hatua.

Ziara ya Mheshimiwa Rais pamoja na masuala mengine muhimu ya kitaifa bado hakuacha kuhimiza matumizi ya Kiswahili.

4 katika uga wa sheria

Katika kikao kazi kilichofanyika tarehe 27/Mei/2021 Mheshimiwa Profesa Paramagamba Kabudi, waziri wa sheria na katiba alipokutana na  wakurugenzi wa Idara na vitengo vya sheria na Wizara zote za serikali mjini Dodoma.
Pamoja na mambo mengine kikao kililenga kufanya tathimini ya zoezi la kutafsiri sheria mbalimbali mbalimbali katika lugha ya Kiswahili. Mheshimiwa Kabudi alisema:

Maamuzi yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano na sita ya kutumia Kiswahili kwenye sekta ya sheria si kwamba Watanzania hawajui Kiingereza, isipokuwa Kiswahili ni lugha ya Taifa letu, ni utambulisho wa Taifa letu na ni utambulisho wa utu wetu

Maelezo haya ya Prof.Kabudi yanaonesha namna Rais Samia Suluhu kazi imeendelea katika suala la matumizi ya lugha kwenye uga wa sheria na mahakama.

Katika  hatua nyingine, Mheshimiwa Geofrey Pinda naibu Waziri wa sheria na katiba, katika mkutano wa wadau kujadili mchango wa matumizi ya Kiswahili katika upatikanaji haki kwa wananchi. Alisema:

...na sasa tumeamua kwa makusudi mahakama na Baraza la ardhi yote lazima yatumie Kiswahili katika kutatua migogoro ile ambayo ilikuwapo katika jamii...

Mheshimiwa Pinda alisisitiza kuwa matumizi ya Kiswahili katika uga wa sheria na mahakama kuwa ndio tunarudi kwenye Uhuru wa kweli.
Hapa tunaona namna ndani ya siku hizi 100 za Mheshimiwa Rais Samia  zinaendeleza kazi ya kukuza na kuendeleza Kiswahili katika uga wa sheria na mahakama.

5 Kiswahili chazidi kupaa katika Jumuiya ya SADC na Umoja wa Afrika

Ndani ya siku 100 za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Kiswahili  kimezidi kukua na kutamalaki katika anga za kimataifa. Kupitia kwa Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Balozi Leberata Mulamula, katika siku ya Umoja wa Afrika (Africa Day) kwenye kikao na mabalozi  alisema:

Lugha ya Kiswahili yachaguliwa kuwa lugha rasmi katika mikutano ya umoja wa nchi za Afrika

Mheshimiwa Balozi Mulamula alisisitiza kuwa Kiswahili ni lugha inayotumika katika anga hizo ukilinganisha na lugha nyingine za Kiafrika.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa waziri wa fedha na uchumi Daktari Mwigulu Nchemba kwa niaba ya nchi alitetea kwa hoja kuntu matumizi ya kuboreshwa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (KAKAMA) badala ya kufutwa kama ilivyokuwa imependekezwa na Mtaalamu mshauri.

  Mheshimiwa Mwigulu alisema:

Tunatetea Kiswahili kama kielelezo cha Afrika Mashariki na tume hii ambayo imesimamia hicho Kiswahili. Tunaiona ni taasisi muhimu sana ambayo baadae inatakiwa hata iweze kuunganisha hizi nchi zetu, yaani Kiswahili kiweze kufika kwenye kila taasisi zingine pamoja na huko kwenye Idara za elimu ambayo tunasema...

Hapa inadhihirika  namna ambavyo wateule wa Mheshimiwa Rais Samia wakisimama imara katika kupigania Matumizi ya Kiswahili na utamaduni wetu.

Hii ni kufuatia maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia  mwenyewe pale alipolihutubia Bunge
la 12 tarehe 22 Aprili, 2021 alisisitiza:

Jambo la kwanza na muhimu kabisa tutakalolipa kipaumbele kwenye miaka hii mitano ni kuendelea kulinda na KUDUMISHA TUNU ZA TAIFA letu, yaani Amani, Umoja na Mshikamano, Uhuru wa nchi yetu, Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar pamoja na Muungano wetu. Kama mnavyofahamu, amani na umoja ni msingi mkuu wa maendeleo katika Taifa lolote. Hivyo basi, nawasihi sana Watanzania wenzangu
tushirikiane kwa pamoja katika kulinda tunu hizi

Moja ya tunu zetu kama Taifa  ni lugha yetu adhimu ya Kiswahili.

6 Kuongeza vifaa vya Kisasa vya mafunzo ya ukalimani kwa vitendo na matumizi ya TEHAMA katika ukuzaji wa Kiswahili

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kupitia Naibu Waziri wa Habar, sanaa na michezo, , Mheshimiwa Pauline Gekul alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Singida Mjini Mheshimiwa Mussa Simai alilotaka kujua mpango wa serikali kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa bidhaa ya kimataifa ili kuendelea kukuza utamaduni wetu duniani.

Mheshimiwa Gekul alijibu:
Tayari tunao Mpango wa kufundisha Kiswahili kwa wageni kupitia Balozi zetu nje ya nchi na serikali imeboresha na kuimarisha mafunzo ya stadi za kufundisha Kiswahili kwa wageni. Pamoja na kutoa machapisho ya Kiswahili rahisi kwa wataalamu wetu

Majibu haya ya Mheshimiwa Naibu Waziri yalikuja kudhihirishwa katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Wizara hiyo Ndugu Mheshimiwa Innocent Bashungwa.
Ambapo Mheshimiwa Waziri alisisitiza jambo hili litakwenda sanjari na uongezaji wa vituo vya Kiswahili katika Balozi mbalimbali za Tanzania zilizoko katika nchi mbalimbali duniani.

Katika hili napenda pia kumpa Kongole sana Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini Mheshimiwa Batilda Swila na Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini China Mheshimiwa Balozi Mbelwa Kairuki na pia ubalozi Qatar kwa mchango wao katika kueneza Kiswahili katika Balozi zao. ?? ndani ya siku hizi 100  ubalozi wa Korea kusini ulifanya Kongamano kubwa la mtandaoni la Kiswahili ambalo lilikuwa zuri sana na lilijumuisha wapenzi wa Kiswahili kutoka pande zote za dunia. Katika Kongamano hili tulishuhudia vijana Wa Kikorea wakiimba nyimbo za uzalendo za Tanzania. Kongoleni sana Mabalozi wetu.

7 Kiswahili chapenya kuwa lugha ya ADPA

Katika kipindi cha siku 100 za Mheshimiwa Rais Samia Kiswahili kimebahatikiwa kupenya na kuwa lugha katika Jumuiya hiyo ya wachimba Almasi Afrika, yaani African Diamond Producers Association ambayo ina jumla ya nchi wanachama 19.

Alipokuwa akizungumza na wanahabari mnamo tarehe 8/4/2021 Waziri wa Madini Mheshimiwa Doto Biteko alisema:

la pili tumekubaliana kwamba, Kiswahili na chenyewe iwe moja ya lugha za mawasiliano katika umoja wetu wa ADPA. Kabla ya leo (yaani siku hiyo) lugha zilizokuwa zinatumika kwenye ADPA ni Kiingereza, Kifaransa pamoja na Kireno leo tumeongeza lugha ya Kiswahili na chenyewe kiweze kutumika katika umoja wa nchi zinazozalisha Almasi hapa Afrika

Kwa lugha ya vijana niliyoisikia hivi karibuni wanasema Mama anaendelea kuupiga mwingi katika lugha ya Kiswahili??

8 Kuongeza msamiati wa kilahaja katika lugha ya Kiswahili

Ndani ya siku hizi 100 za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani alitumia Kiswahili cha lahaja ya kikae (Kimakunduchi) katika hotuba yake alipokuwa anaongea na viongozi wa dini jijini Dodoma mnamo tarehe 18/4/2021. Mheshimiwa Rais alisema:

...Inasikitisha sana kwamba watu wanapiga ngoma mitandaoni lakini ngoma ile inachezwa Bungeni na inachezwa kwa kudemka vizuri sana, mnademka vizuri sana...kulinganisha watu na sio ajenda za kitaifa...

Mheshimiwa Rais Samia anatumia neno demka ambalo maana yake ni kucheza ngoma kwa madaha, matao au maringo  alitumia neno hili pale alipokuwa akiwakumbusha Waheshimiwa Wabunge kujikita kwenye mijadala yenye afya na tija kwa Taifa.
Mheshimiwa Rais Samia anatutambulishia msamiati mpya masikioni mwa Watanzania wengi na sasa tunaanza kuufahamu na kuutumia katika miktadha mbalimbali ya matumizi.

9 Matumizi ya misemo na kaulimbiu mbalimbali ya Kiswahili

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ndani ya siku hizi 100 za utawala wake mbali ya kutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasaha na usanifu, amekuwa akiunda na kutumia misemo mbalimbali ya Kiswahili ambayo husaidia kunogesha hotuba zake na kuhakikisha malengo aliyoyakusudia yanafikiwa.

Tutazame kwa muhtasari misemo hiyo na uchambuzi wake mfupi.

i) Kazi iendelee
Kaulimbiu ya kazi iendelee mwandishi wa makala haya aliwahi kuifafanua kwa kina katika moja ya makala zake zilizohusu hotuba ya Mheshimiwa Rais Samia aliyoitoa Bungeni. Kwa ambao hawakupata nafasi ya kusoma makala hayo nawasihi waisome kwani imeeleza kwa muhtasari namna falsafa hiyo inavyoweka msingi wa namna utawala wake utakavyokuwa.

Kwa ufupi sana falsafa ya kazi iendelee inahimiza na kutaka Watanzania waendelee kuchapa kazi. Kumbuka Mheshimiwa Rais Samia amechukua nafasi ya hayati Magufuli ambaye kaulimbiu yake ilikuwa ni hapa kazi tu ndani ya siku 100 mama Samia anatupatia kaulimbiu mpya inayochagiza kuendeleza mambo yote mazuri ya hayati JPM na kuhimiza kazi iendelee.

ii) Aitambulisha salamu mpya

Mheshimiwa Rais Samia katika kuichagiza kaulimbiu ya kazi iendelee anaitambulisha salamu mpya ya Kiswahili pale aliposema:

leo nina salamu mpya nikisema nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnatakiwa kujibu kazi iendelee

Salamu hii ya Kiswahili imekuwa adhimu inayotumiwa katika hafla mbalimbali za serikali na hata za kijamii.
Mwandishi Majid Mswahili katika makala yake inayohusu Falsafa katika salamu hii alisema:
salamu hii ni zaidi ya salamu kwani inaondoa tofauti zetu za makabila, rangi, dini na hata umaeneo
Hivi ndivyo ambavyo Kiswahili kinavyoweza kutumika kuimarisha umoja, mshikamano na mwenendo bora wa Taifa.

iii) Zege halilali

Msemo mwingine aloutumia Mheshimiwa Rais Samia ni msemo huu wa zege halilali. Msemo huu ni maarufu sana katika shughuli za ujenzi. Katika shughuli za ujenzi mafundi waashi wanapokoroga zege iwe kwa mashine au kwa mikono shurti lile zege limwagwe wakati huohuo, vinginevyo likiachwa litaganda na halitakuwa na maana wala tija.

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatumia lugha ya zege halilali kwa lengo la kuhimiza kaulimbiu yake kuwa kazi lazima ziendeleee na hakuna kulala.
Hivi ndivyo ambavyo, unawaona wateule mbalimbali wa Mheshimiwa Rais wakiendeleza kazi hizo ndani ya siku hizi 100.

iv. ukinizingua nitakuzingua

Mheshimiwa Rais Samia ametumia msemo huu unatumiwa zaidi na rika la vijana. Alibainisha wazi kuwa msemo huu hutumiwa zaidi na Mheshimiwa Waziri kijana na machachari Mheshimiwa Juma Aweso anapotekeleza majukumu yake. Katika kile ambacho ni kuitazama hadhira yake kuwa ni ya viongozi. Wengi katika viongozi hao ni vijana anatumia msemo huu ambao unasadifu muktadha huo pale aliposema:

Wewe ni kijana na mimi ni Mama, ukinizingua na mini nakuzingua

Zingua kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili ni kubabaisha mtu, sumbua mtu au kutesa. Mheshimiwa Rais Samia anawasisitiza viongozi wake kuwa wakimbabaisha naye atawababaisha japo ni Mama. Haya yanadhihirika ndani ya siku 100 ambapo baadhi ya viongozi waliomzingua Mama tayari kishawazingua.

v) Nyumba uliyoizoea kuihama ina tabu

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika mkutano Mkuu maalumu wa Chama cha Mapinduzi Dodoma, alitumia msemo huu katika kushadidia kauli za Ndugu Lazaro Nyalandu alipokuwa akifafanua namna alivyoishi kwa tabu katika Chama alichokuwa amehamia cha CHADEMA  huko awali kabla ya kurudi nyumbani CCM.
Mheshimiwa Rais Samia alisema:

Kule Zanzibar kuna mshairi aliimba nyumba uliyoizoea kuihama ina tabu (shangwe). Ni kazi kweli kuihama nyumba uliyoizoea...na wanaume wanajua hilo...

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu anaitumia lugha katika muktadha mwafaka kabisa. Wimbo aliounukuu kipande hiko unaitwa Dunia ina fisadi ni katika  taarabu asilia. Ambapo unaanza katika beti hiyo wale walionikamia nawaambia waziwazi x2...nyumba uliyoizoea kuihama ina kazi
Maudhui ya shairi hili ni mapana lakini katika makala haya hatujakusudia kulidadavua kwa kina. Msisitizo wetu ni kuonesha ndani ya siku hizi 100 anavyotumia lugha ya Kiswahili katika muktadha sahihi na kushajiisha suala alilolikusudia.

10 Kuendelea kutumia Kiswahili katika hafla mbalimbali za serikali

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu mbali ya umahiri na ulumbi wa kulumba Kiswahili alioruzukiwa na Mola, ndani ya siku 100 za utawala wake ameendelea kutumia lugha ya Kiswahili katika hotuba zake. Amefanya hivyo akiwa ndani ya nchi na hata nje ya nchi, awe na ugeni wa ndani au wa nje haya ni maendeleo makubwa sana kwa lugha yetu ya Kiswahili.

Huyu ndiye Mama Samia Suluhu Hassan ambaye hata kabla ya kupata wadhifa huu wa Urais, pale alipokuwa makamu wa Rais alikuwa mstari wa mbele katika kukuza Kiswahili na kwa kweli kazi imeendelea katika kipindi hiki cha siku 100 tangu awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Heko na kongole sana Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza lugha yetu ya Kiswahili.??

11 Matarajio
Mintarafu ya mafanikio haya ndani ya siku hizi 100, wapenzi na wadau wa Kiswahili tuna matarajio mbalimbali katika awamu ya 6

1.Kiswahili kuendelea kuwa lugha muhimu katika kuimarisha na kuchochea maendeleo ya nchi hususan dhana ya Diplomasia ya uchumi.

2.Kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishia katika ngazi zote za elimu.

3.Kuendelea kuhimiza matumizi ya Kiswahili fasaha na sanifu kwa umma.

4. Kuendelea kuifanya lugha ya Kiswahili bidhaa lugha itakayoingiza fedha.

Hizi ndizo siku 100 za utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan na mchango wake katika maendeleo ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Nawashukuru wataalamu mbalimbali wa Kiswahili kwa maoni yao katika kuboresha zaidi makala haya.

Tuendelee kumtia shime Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wetu wote ambao wanaendeleza tunu ya lugha yetu ya Kiswahili ndani ya Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania. Kiswahili ni nyenzo ya uchumi, uti wa mgongo wa Taifa letu na utambulisho wetu. Bidhaa ya kujidaia na kutambia ulimwenguni kote.

0713400079
Mhadhiri
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-Kigamboni

Print this item

  Wanawake Wakulima
Posted by: MwlMaeda - 06-27-2021, 02:24 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

.pdf   Wanawake Wakulima.pdf (Size: 208.93 KB / Downloads: 0)

Print this item

  MBINU/NJIA ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI/LUGHA YA PILI
Posted by: MwlMaeda - 06-27-2021, 12:46 PM - Forum: Kiswahili kwa wageni - No Replies

MBINU ZA UFUNDISHAJI LUGHA YA PILI/KIGENI

Suala la ufundishaji lilianza miaka mingi tangu muingiliano wa jamii lugha tofauti karne nyingi zilizopita. Jamii moja na nyingine walianza kukubaliana na kukubalinana na lugha ngeni ili wawasiliane nao, na kuibuia haja ya kufundisha lugha ya kigeni. Ufundishaji lugha ya kigeni kitaaluma ilianza karne ya 19 na karne ya 20 ilikomaa sana. Lakini katika kipindi hk chote ufundishaji lgh za kigeni umekuwa ukibadilika kutokana na mabdiliko ya wanafunzi na nadharia za kiisimu na nadharia katika elimu kama taaluma. Hata hivyo ufundishaji lgh za kigeni unazidi kukomaa kutokana namaendeleo ya sayansi na teknolojia, hali hii imeibua mbinu za ufundishaji wa lugha za kigeni.
Mbinu za ufundishaji ni njia za ufundishaji zilizokitwa katika kanuni na miongozo maalumu
  1. Mbinu ya sarufi- tafsiri.
  2. Mbinu ya moja kwa moja.
  3. Mbinu ya usikilizaji.(audialingualism)
  4. Mbinu ya mwitiko kamili wa kivitendo
  5. Mbinu ya utambuzi (cognitive
  6. Mbinu ya ujifunzaji kijumuiya
  7. Mbinu yaupendekezi
  8. Mbinu ya kimawasiliano.
                                                           MBINU YA SARUFI- TAFSIRI.
Hii ni mbinu ya kimapoke kwa kuwa ilianza na ilitawala ufundishaji hata lugha zilizokufa. Hadi sasa inatumika kufundishia watu wengi.
SIFA ZA MBINU HII
  1. Lgh ya utunzi ndiyo inatumika kufundishia
  2. Wanafunzi hupewa orodha za kanuni ya kisarufi ili wakariri (kupewa maneno ya kigeni).
  3. Stadi zinazopewa mkazo ni kusoma na kuandika tu. Mkazo kidogo au hakuna mkazo katika utamkaji wa sauti. Vitabu vilivyoandika kwa ajili ya kufundishia lgh kwa kutumia mbinu hii kwa kiasi kikubwa hufafanua kanuni za kisarufi na kasha kutoa mazoezi mengi ya kutafsiri .
                     MBINU YA MOJA KWA MOJA.
Huzingatiaufundishaji msingi wa uasilia wa lugha. Yaani kumudu lgh ya kigeni kama lugha mama yake. Mbinu hii iliibuka kutokana na kutambua kuwa kutambua lugha ni kuzungumza zaidikuliko kuiandika
SIFA ZA MBINU HII
  1. Lugha lengwa tu ndiyo inayotumika, inachukuliwa kuwa lugha ya kwanza ni chanzo cha makosa katika kujifunza lugha ya pili.
  2. Stadi ya mazungumzo hutawala katika mbinu hii.
  3. Stadi ya kuandika haiwekewi uzito.
MBINU YA USIKILIZAJI.(AUDIALINGUALISM)
Ilijikita katika mbinu ya usikilizaji. Waasisi wa mbinu hii ni wana utabia kama vile Bloomfield 1942, walikabidhiwa mhutasari wa ufundishaji lgh za kigene marekeni na kueleza kuwa kujifunza lugha ni kama kujifunza tabia Fulani ambao wao huona kuwa kujifunza lugha ni kurudiarudia mara kwa mara . lengo la kufundisha lugha ni kuzungumza ni kumwezesha kuzungumza na kukabiliana nayo ana kwa ana kwa kiasi Fulani
SIFA
  1. Kukariri mazungumzo na kufanya mazoezi kuepuka kasoro katika uzungumzaji.
  2. Stadi za lugha hupangiliwa kuanzia stadi ya kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika
  3. Hutumia lugha ya kigeni tu kama lugha ya kufundishia/lugha ya pili. Ufundishaji wa ruwaza wa miundo ya lugha uwe wa kurudiarudia.
  4. Hakuna uelezwaji wa sarufi
  5. Msamiati hujifunzwa kutokana namuktadha
  6. Kuna matumizi ya vinasa sauti kama vile cd,video
  7. Msisitizo upo katika utamkaji
  8. Baada ya mwitiko sahihi hutolewa uimarisho/tuzo.
MBINU YA UTAMBUZI
Iliibuka miaka ya 1970 kama mwitiko wa uhakiki ni mbinu rekebishi ya mbinu 2 zilizotamgulia. Watetezi wa mbinu hii ni wanasaikolojia na wanaisimu tambuzi
SIFA ZA MBINU HII
  1. Inatilia mkazo kumpa mwanafunzi uwezo wa kuelewa mfumo wa lugha ya kigeni, kasha kumpa uhuru wa kuweza kujifunza peke yake kwa kutumia msingi aliopewa mbinu hii hupinga kujifunza lugha, baada ya mwanafunzi kupewa mbinu za ujifunzaji mazoezi na msingi mwanafunzi huachiwa huru na kumuachia ajifunze mwenyewe kwa kutumia mbinu zake. Noam Chomsky anaunga mkono mbinu hii. Vitabu vilivyoandikwa kufundishia lugha ya kigeni humsaidia mwanafunzi kutambua misingi ya kisarufi na ufaham na utungajiwa kubuni na kujieleza.
MBINU YA MWITIKO KAMILI WA KIVITENDO
Hii ni mbinu ambayo hitwa pia mkabala asilia wa kujifunza lugha. Mbinu hii iliasisiwa na wanaisimu saikolojia kama James Asher 1969, mbinu hii inalenga utumiaji wa stadi moja ili kuimarisha stadi nyingine.
SIFA
  1. Mwanafunzi humsikiliza na kumtazama mwalimu akitamka amri na kuzitekeleza moja kwa moja na baada ya hapo mwalimu hurudia kila amri na kumtaka mwanafunzi atekeleze baadae mwanafinzi hutekeleza mwenyewe.
  2. Inasisitiza kuwa katika kujifunza lugha ya pili kwa kutumia vitenzi vilivyo katika kauli ya kuamru kama ilivyo kwa watoto wadogo wanapojifunza lugha mama. Mfano mama taka uji.
MBINU YA UJIFUNZAJI LUGHA KIJUMUIYA
Hujulikana pia kama mbinu ya ujifunzaji kwa ushauri. Ni mbinu iliyobuniwa na Charles A na Curran 1976. Ni wana saikolojia bingwa wa masuala ya ushauri na uelekezi. Katika mbinu hii mwanafunzi huzingwatiwa katika mbinu mbili, kwa upande mmoja hisia zake kama binadamu, hupewa nafasi ya kujieleza na kupewa ujuzi wa lugha kwa kiwango kinachotakiwa
SIFA ZA MBINU HII
  1. Mwanafunzi ndiye egemeo la ujifunzaji lugha. Dhima ya mwalimu ni kushauri tu na kuchochea ujifunzaji uendelee, uhusiano baina ya mwalimu na mwanafunzi ni sawa na mshauri na mteja.
  2. Mwanafunzi huchagua wanachotaka kujifunza na kuambiana kwa lugha yao. Mwalimu ambaye ni mshauri huwatafsiria namna ya kukisema katika lugha ya kigeni na wanafunzi hukisema kwa lugha ya kigeni na kukirudiarudia, mchakato huu huendelea katika mada mbalimbali na mazungumzo huhifadhiwa kwa matumizi ya baadae. Katika upande wa hisia za kibianadamu : wanafunzi hupewa nafasi za kukisema kwa kutumia lugha za kigeni. Dai kubwa la mbinu hii ni kuwa lugha ni watu , lugha ni watu kwa kukabiliana pia lugha ni watu kadri ya mahitaji na miitiko yao. Hivyo wanafunzi huwa jumuiya na hujifunza kupitia jumuiya hiyo.
  3. Katika kutumia mbinu hii hakuna mhitasari wala kitabu kinachotumika kufundishia.
                                                         MBINU YA UPENDEKEZI
Mwasisi wake ni Gorge lozanov 1979. Kwa mujibu wa mbinu hii mazingira bora
                                                         SIFA ZA MBINU HII
  1. Darasa hutengenezwa na kuwa mahara pa kuvutia sana kukaa. Wanafunzi wakae kwa muduara katika vikundi vidogo vidogo na kuwe na michoro mziki, picha. Masomo huangwa katika mada kumi na ufundishwaji hupewa masaa manne kila siku kwa siku 6 katika wiki. Wanafunzi hupewa orodha ya msamiati ili kukariri. Mbinu mbalimbali hutumika ikiwa ni pamoja na uigaji, maswali na majibu, uigizaji n.k. vitabu viulivyoandikwa katika mbinu hii husheheni vielelezo mbalimbali ili kumvutia mwanafunzi katika kujifunza. Lengo la mbinu hii ni kupata umilisi wa mazungumzo yaani maneno 230 katika siku 30.

8/04/2014

                                                   MBINU YA KIMAWASILIANO
Mbinu hii iliibuka katika miaka ya 1980 na iliendelea kukubalika katika nchi nyingi duniani kama njia bora ya kufundishia lugha ya pili. Kuibuka kwake kulichochewa na hali ya kutegemeana miongoni mwa nchi za bara la ulaya hasa kiuchumi na soko la dunia kati ya nchi hizo, kama taaluma mbinu hii chimbuko lake lilitokea siku nyingi hata kabla ya 1980, wapo wanaisimu waamirifu kama vile Firth 1968, Halliday 1973 na mwanaisimu jamii Hyrmes 1972, walikuwa na mawazo kuwa lugha ni mawasiliano, wanasema “msingi wa mbinu hii ni mwanafunzi ndilo eneo la mafinzo na kwamba kujifunza lugha ni kujifunzakuwasiliana. Hawa wanatofautiana na Noam chomscky kuwa anayedai kuwa kujua lugha ni kujua umilisi wa mfumo nakanuni na hivyo kuitumia sahihi.
Hivyo tangu siku ya kwanza jitihada za mawasiliano lazima zifanyike katika ujifunzaji na ufundishaji, madhumuni ya mbinu hii n kukuza stadi zote za lgh ambazo hutumika katika mawasiliano.

Maana ya mbinu ya kimawasiliano:-
Ni mbinu iliyokitwa kwa mwanafunzi, hutoa mwanya kwa mwanafunzi si katika umilisi wa sarufi bali pia katika stadi za jamii yaani nini cha kusema, namna ya kusema, lini aseme na wapi aseme ili kuridhika na kile anachohitaji kila siku.
Lengo kuu la mbinu hii ni kumfanya mwanafi=nzi apate umilisi wa mawasiliano na mwalimu kazi yake ni kumwezesha mwanafunzi kupata umilisi wa mawasiliano, na umilisi ni pamoja na
  1. Umilisi wa kisarufi
  2. Umilisi wa uneni
  3. Umilisi wa kiufundi, kv alama za kiuakfishi like koma, nukta nk
  4. Umilisi wa kiisimu jamii. Kv namna ya kusema, wapi nk.
                               MISINGI YA MBINU YA UFUNDISHAJI LUGHA KIMAWASILIANO
  1. Namna ya kutumia lugha
  2. Uamiliaji asilia wa lugha kuwa mwanafunzi ajifunze lugha katika muktadha halisi na wenye uasilia
  3. Ufundishaji uhusishwe na hali halisi ya maisha, ili mwanafunzi aelewe uasilia wa maisha
  4. Lugha ifindishwe kama stadi, lugha isifundishwe kama somo, katika mbinu hii mwal awafanye wanafunzi wake wazungumze ili kujua hali halisi. Hivyoikubalike kuwa lugha ni stadi
  5. Ukuzaji uwezo wa kuwasiliana, katika mawasiliano kuna stadi ndogo 4 ambazo zinapaswa kukuzwa kwa mwanafunzi ili aweze kuwasiliana ambazo ni
(a)    Kuzungumza
(b)   Kusikiliza
©    Kusoma
(d)   Kuandika

SIFA ZA MBINU YA KIMAWASILIANO
  1. Sifa kuu ni mawasiliano, inasisitiza mawasiliano lugha inatumika kwa mawasiliano, hivyo mbinu hii husisitiza mawasiliano katika kufundisha lugha. Husisitiza hali halisi ya maisha na mawasiliano katika muktadha hivyo ujumbe unaoelezwa katika mawasiliano huwa katika muundo wa kidhima.
  2. Inamlenga mwanafunzi kwa sababu kazi ya mwalimu ni mwezeshaji tu, anawezesha kisha anaruhusu mwanafunzi kujifunza mwenyewe.
  3. Muktadha wa kijamii, mbinuhii husisistiza mawasiliano ya kijamii na miktadha halisi, hivyo mwanafunzi hujifunza lugha kwa sababu muktadha wa kijamii hutengenezwa.
  4. Uwezo wa kuzungumza, mbinu hii huwasaidia wanafunzi uwezo wa kuzungumza kitu ambacho ni muhimu katika maisha.
  5. Lugha lengwa hujifunzwa kama lugha ya kwanza katika mbinu hii.
  6. Mbinu hii hukuza stadi za lugha kv, kusikiliza na kuzungumza, kusoma kuandika

                                                           MAHITIMISHO
  1. Mbinu hii haihitajiki kupuuzwa kwa sababu hihitaji mawasiliano ya kila siku.
  2. Utumizi wa lugha wa kila siku ndio msingi wa lugha ya pili na siyo lugha ilivyo katika maandishi, kitendo cha kujifunza lgh kwa kimazingira huitwa
  3. Kama ilivyo ujifunzaji wa mfumo zalishi ni muhimu pia kujifunza raghibaya wanafunzi na kuwapa kiwango Fulani cha kujiamini, mwl awape fursa ya kutumia kile walichojifunza katika mazingira halisi.
  4. Kama uzuri wa mzungumzaji mzawa “ni uzuri huo huo anatakiwa aupate mzungumzaji wa lugha ya pili/asiye mzawa. Vitu vya kuandaa: matini ziwe bora ili mjifunzaji kumudu lugha anayojifunza.
  5. Ni muhimu kwa matini kuwa rahisi ili wanafunzi wasitumia muda mrefu kupata dhana ya matini hiyo, katika hali halisi wanapokutana na matini za namna hii wanachanganya hivyo wapewe muda wa kutosha na mazoezi ya kutosha pia.
  6. Matini hizi zipo si kwa ajili ya kusoma tu bali pia katika kuibua lugha itakavyotumiaka darasani na kuongeza marifa zaidi
  7. Urefu matini sharti ziwe fupi.

UGUMU KATIKA MBINU YA MAWASILIANO
Husababishwa na muktadha ambao lugha hiyo inafundishwa unatakiwa kujua kuwa
  1. Unafundisha akina nani?
  2. Wanajifunzia wapi kwa wazawa au ugenini?
  3. Kwanini wanajifunza?
Hivyo muktadha wa ufundishaji uzingatie mambo makuu manne
  1. Umri mfano watoto, vijana au watu wazima
  2. Viwango, unafundisha katika kiwango gani
  3. Ueledi wao, ueledi wao/kazi zao
  4. Muktadha wa kijamii,
UMRI
(a)    Ufundishaji wa watoto
Inaaminika kuwa watoto hujifunza lugha kirahisi kuliko watu wazima, hujifunza bila kujua jitihada wnazofanya katika kujifunza lugha. Utafiti unaonyesha kuwa waqtu wazima wanaweza kuwa wazuri katika baadhi ya maeneo, wanaweza kurunza misamiati mingi kuliko watoto. Wanaweza kutumia michakato mifupi katika kujifunza michakato ya kisarufi na kiisimu wakati watu wazima wakiwa darasani wana uwezo wa juu wa kujifunza haraka. Hivyo wakati watoto huzungumza katika mzingira halisi bila shida watu wazima wanapata shida. Watoto darasani wanaweza kupata ugumu katika kujifunza lugha ya pili kwa sababu ya tofauti binafsi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa ambazi zio katika ufundishaji wa lugha ya pili. Ili kuwa na ufundishajiwa wenye mafanikio unatakiwa kuwa na stadi maalumu tofauti na zile za watu wazima.

MAMBO MATANO YA KUZINGATIA KUFUNDISHA WATOTO.
  1. Kukuza uwezo wa kufikiri, watoto hujifunza kwa kujikita katika viti au mambo aambayo ni ya papo kwa papo katika matumizi ya lugha. Mambo ya kufanya unapokuwa darasani ili kukuza uwezo wa kufikiri wa watoto:
(a)    Usifafanue sarufi kama ilivyo,
(b)   Dhana za sarufi zifundishwe kwa kutumia ruwaza, mf: nilijifunza kisw, ulijifunza kisw, alijifunza kisw. Tulijifunza kisw-, mlijifunza kisw-
Baadhi ya dhana ngumu zirudiwerudiwe.

  1. Muda wa utayari, hii ni tofauti ya watoto na watu wazima wao huwa na mda mfupi, kazi ya mwl ni kuweka mvuto wa lugha na lifurahishe ili kuonyesha uhalisia. Ni muhimu kuelewa nini maana ya utayari, zingatia yafuatayo:
(a)    Andaa mazoezi ya kuvutia
(b)   Wape aina mabalumbali za mazoezi kuwaandaa
©    Mwl ahuishe , ahaishe na aasilishe kuhusu somo lenyewe, zingatia kuwa mwl ni lazima awe mtendaji kutengeneza utayari wa watoto.
(d)   Ucheshi huwafanya watoto wajifunze.
(e)   Hakikisha unapata udadisi, uchunguzi wa watoto ili kujua mwelekeo wao.
  1. Milango ya fahamu, watoto wanapaswa kutumia milango yote ya fahamu inayochangamushwa, kazi ya mwl ni kujitahidi kuchangamsha hii milango ya fahamu hadi zaidi ya macho na maskio. Mambo ya kufanya
(a)    Fanya michezo hii hupanua milango yao ya fahamu
(b)   Kazi mradi ndogondogo ili kuwafanya wajifunze
©    Misaada ya ufahamu , mf: maua yana harufu gani?
(d)   Tumia lugha ya ishara, n I muhimu kwa sababu watoto wataangalia kwa makini na kutambua lugha.
  1. Athari, haya ni mabo ambayo ni vizuizi katika ujifunzaji lugha. Watoto wana udhaifu kuliko watu wazima, namna ya kuondoa athari za lugha
(a)    Thibiti darasa kutomcheka mtu darasani,
(b)   Uwe mkweli katika kuwajenga,
©    Hakikisha wanashiriki mazungumzo kadri inavyowezekana, wape nafasi kujaribu kufanya kitu kwa kila mmoja.

  1. Uasilia, umaana wa lugha, watoto huingalia lugha mpya kama inaweza kutumika papo kwa papo. Hawajisikii ikiwa lugha haina manufaa kwao mfano lugha isoyo ya asili na isiyo na maana. Kipi cha kufanya:
(a)    usitumie lugha rasmi sana,
(b)   lugha ihusianishwe na mazingira kama vile mazingira, matukio, uhusika mf: motto ahusike kamapolisi, daktari nk.
©    Mbinu ya kuanza na kitu kizima itumike usianze na vipande vipande, weka mkazo katika stadi mablimbali kama kusoma, kusikiliza, kusoma na kuandika
b. ufundishaji watu wazima
watu wazima wanaweza kufundishika kwa urahisi, kiwango chao cha aibu kinaweza kuwa kikubwa hata zaidi ya watoto lakini wao hujiamini. Kuna mambo matano ya kuzingatia katika kufundisha watu wazima.
  1. Kukuza uwezo wa kufikiri, watu wazima wana uwezo wa kutumia data mbalimbali na kanuni, kuwa mwangalifu kufundisha udhahania katika matumizi ya lugha.
  1. Muda wa utayari, watu wazima wana uwezo wa kuwa na utayari kwa muda mrefu hata kama somo haliwavutii,. Lakini kanuni ya kuwapa mazoezi kanuni ni ile ile.
  1. Milango ya fahamu, itumike pia japokuwa watu wazima huongozwa na hisia zaidi.
  1. Athari, jitahidi kuondoa athari zinazotokea katika ujifunzaji na ufundishaji lugha.
  1. Uasilia na umaana wa lugha. Watu wazima wana uwezo wa kufikiri dhana dhahania za lugha na dhana zisizo asilia zinaweza kutumika katika ujifunzaji.
USIMAMIZI WA DARASA LA WATU WAZIMA
  1. MWl uoneshe heshima na nidhamu ili wasijenge dhana ya kuchukia somo au kuwa na mwelekeo hasi wa somo hilo,
  2. Mwl asiwachukulie watu wazima kama watoto
  3. Mwl awape uhuru wa kufanya wanapokuwa katika mazingira yao wanapokuwa nje ya darasa
  4. Mwl asiwafundishe watu wazima nidhamu kama vile watoto
  5. Wachukulie kuwa ni watu wazima hivyo wanaweza kufanya mambo kiutu uzima.

VIWANGO VYA WANAFUNZI
Ufundishaji wa lugha za kigeni huwa katika viwango vitati
(a)    Kiwango cha awali
(b)   Kiwango cha kati
©    Kiwango cha juu

Ufundishajiwa kiwango cha awali
Wanafunzi hawana maarifa kuhusu hiyo lugha hivyo mwl ni mwezeshaji wao katika malengo yao, mwl anapaswakutoa zawadi ili kuwafanya wanafunzi kuweka umakini,
Mambo kumi ya kuzingatia
  1. Mchakato wa ukuzaji akili kwa wanafunzi, wanafunzi washiriki kurudiarudia maneno aktika siku zile za mwanzo. Mwl asichanganyikiwe na wanafunzi kutopata mabadiliko katika kipindi kifupi maana ni lugha ngeni kwao, siku za mwanzo wapatie mazoenzi madogomadogo mf: waweze kutaja majina yao na wanakokaa. Mazoezi yalenge kuwakuza uelewa.
  2. Kazi ya mwl. Mwanafunzi hutegemea mwl katika kila kitu kuhusiana na lugha, kazi za vikundi zitumike katika kujijengea uelewa. Mf picha.
  3. Unenaji wa mwl, mwl aongee kwa sauti ya kutosha, mwl atumie misamiati rahisi kabisa na sarufi rahisi kabisa.
Mwl atumie lugha ya kwanza mara chache sana, si vizuri uwaruhusu wanafunzi kutumia lugha zao za kwanza mara kwa mara. Mwl atumie lugha ya kwanza kwa manufaa ya : kuelezea hoja za sarufi 2. Kuonyesha maneno yaloyowachanganyaau kwenye maneno ya kiutamaduni
  1. Hakikisha lugha inayotumika ni lugha inayotua inafuata kanuni za kimawasiliano hivyo ionyeshe uasilia waa lugha isiwe lugha rasmi sana kwa wako katika hatua za awali mf: salamu na utambulisho, mwl hakikisha kuwa ufundishaji   ni rahisi na mfupi. Mwl usiwakatishe tama wanafunzi wako bali wape muda kujifunza.
  2. Ufasaha na usahihi, ufasaha ni muhimu katika hatua hii hakikisha unakuwa katika semi fupifupi mana ni muhimu kuhimizauzungumzaji , usahihi utiliwe mkazo katika sarufi za lugha. Ni muhimu kuangal;ia mahitaji ya wanafunzi katika kuzungumza bila kukosolewa katika kuzungumza. Wape mazoezi ya kisarufi na kifonolojia.
  3. Ubunifu wa wanafunzi, lengo la kujifunza lugha ni kujenga uelewa na kuzalisha kitu kipya ili kuweka ubunifu na utoaji. Katika kiwango cha awali wanafunzi wanaweza kuwa wabunifu kwa kiwango Fulani usitegemee ubunifu mkubwa sana katika lugha.
  4. Mbinu, mbinu rahisi zitumike, anzisha maswali unayoyamiliki yakifuatiwa na maswali ya wanafunzi, pia mbinu ya makundi ni mbinu nzuri sana.
  5. Malengo ya mzungumzaji na msikilizaji, kazi yake ni uasilia wa mawasiliano hakikisha usikilizaji na uzuungumzaji una maana ya mawasiliano.
  6. Malengo ya usomaji na uandishi, katika kiwango cha awali mada ya kusoma na kuandika inatakiwa iwe fupi inayokidhi matakwa ya wahusika kama vile matangazo, kazi ya kuandika inapaswa kuwa ya kuorodhesha.
  7. Sarufi, inatahusisha vitenzi rahisi, viwakilishi vya nafsi .toa lugha lugha ianyieleweka. mbinu ya kuambukiza sarufi inafaa katika kufundisha sarufi na kuambukiza ruwazA
KIWANGO CHA KATI
Ni mambo yale yale ya kiwango cha awali
  1. Mchakato wa ukuzaji akili kwa wanafunzi, wanafunzi washiriki kurudiarudia maneno aktika siku zile za mwanzo. Mwl asichanganyikiwe na wanafunzi kutopata mabadiliko katika kipindi kifupi maana ni lugha ngeni kwao, siku za mwanzo wapatie mazoenzi madogomadogo mf: waweze kutaja majina yao na wanakokaa. Mazoezi yalenge kuwakuza uelewa.
  2. Kazi ya mwl. Mwanafunzi hutegemea mwl katika kila kitu kuhusiana na lugha, kazi za vikundi zitumike katika kujijengea uelewa. Mf picha.
  3. Unenaji wa mwl, mwl aongee kwa sauti ya kutosha, mwl atumie misamiati rahisi kabisa na sarufi rahisi kabisa.
Mwl atumie lugha ya kwanza mara chache sana, si vizuri uwaruhusu wanafunzi kutumia lugha zao za kwanza mara kwa mara. Mwl atumie lugha ya kwanza kwa manufaa ya : kuelezea hoja za sarufi 2. Kuonyesha maneno yaloyowachanganyaau kwenye maneno ya kiutamaduni
  1. Hakikisha lugha inayotumika ni lugha inayotua inafuata kanuni za kimawasiliano hivyo ionyeshe uasilia waa lugha isiwe lugha rasmi sana kwa wako katika hatua za awali mf: salamu na utambulisho, mwl hakikisha kuwa ufundishaji   ni rahisi na mfupi. Mwl usiwakatishe tama wanafunzi wako bali wape muda kujifunza.
  2. Ufasaha na usahihi, ufasaha ni muhimu katika hatua hii hakikisha unakuwa katika semi fupifupi mana ni muhimu kuhimizauzungumzaji , usahihi utiliwe mkazo katika sarufi za lugha. Ni muhimu kuangal;ia mahitaji ya wanafunzi katika kuzungumza bila kukosolewa katika kuzungumza. Wape mazoezi ya kisarufi na kifonolojia.
  3. Ubunifu wa wanafunzi, lengo la kujifunza lugha ni kujenga uelewa na kuzalisha kitu kipya ili kuweka ubunifu na utoaji. Katika kiwango cha awali wanafunzi wanaweza kuwa wabunifu kwa kiwango Fulani usitegemee ubunifu mkubwa sana katika lugha.
  4. Mbinu, mbinu rahisi zitumike, anzisha maswali unayoyamiliki yakifuatiwa na maswali ya wanafunzi, pia mbinu ya makundi ni mbinu nzuri sana.
  5. Malengo ya mzungumzaji na msikilizaji, kazi yake ni uasilia wa mawasiliano hakikisha usikilizaji na uzuungumzaji una maana ya mawasiliano.
  6. Malengo ya usomaji na uandishi, katika kiwango cha awali mada ya kusoma na kuandika inatakiwa iwe fupi inayokidhi matakwa ya wahusika kama vile matangazo, kazi ya kuandika inapaswa kuwa ya kuorodhesha.
  7. Sarufi, inatahusisha vitenzi rahisi, viwakilishi vya nafsi .toa lugha lugha ianyieleweka. mbinu ya kuambukiza sarufi inafaa katika kufundisha sarufi na kuambukiza ruwaza.
KIWANGO CHA JUU

MUKTADHA WA KIJAMII
Upo katika namna 2
  1. Kijamii na kisiasa na
  2. Kitaasisi
MUKTADHA WA KIJAMII NA KISIASA
Baadhi ya mambo ya kijamii na kisiasa ni pamoja na usahihi na kufaa
Rejesta na mitindo
Semi zinazokubalika katika jamii
Usanifu wa lugha katika kabila na kitaifa
Sera ya lugha katika taifa
Lahaja ya lugha
Katika kipengele hiki tunaangalia muktadha wa kisw kama lugha ya 2 na katika lugha ya kigeni. Unapofikiria muktadha wa lugha ya 2 na lugha ya kigeni fikiri pia nn kinatokea nje ya darasa wanafunzi wanapotoka darasani.
MUKTADHA WA UJIFUNZAJI WA LUGHA YA PILI
Lugha lengwa ya darasani hupatika nje ya darasa. Wanafunzi huweza kuwasiliana kwa lugha yao nje ya darasa. Mfano: Kiswahili Tanzania , kiingereza marekani
–          Lugha ya kigeni muktadha wa ujifunzaji wake (lugha lengwa inayofundishwa|) haipatikani nje ya darasa, wanafunzi huwa na msamiati wa darasani tu. Mfano: kiingereza Tanzania , japan, ujeruman . pia Kiswahili ni lugha ya kigen nchini marekeni, china nk. Njia za ufundishaji katika muktadha wa lugha ya pili ni tofauti na ule
MUKTADHA WA KISWAHILI KAMA LUGHA YA PILI
Mwalimu unapofundisha lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili fanya yafuatayo:
  1. Wape kazi nyingi za nyumbani zenye uzungumzaji mahususi ili wayaone yanayotokea mtaani na walinganishe.
  2. Wahimize wanafunze kufanya mazoezi na wazawa
  3. Kusanya makala na magazeti
  4. Wahimize kupata mrejesho sahihi kutoka kwa wazawa.
  5. Wasisistize wanafunzi kutunza kumbukumbu sahihi walizojifunza darasani.
  6. Weka mpango wa kutembelea nyanjani (field trips)
  7. Kuwepo kwa ushirikiano wa wazawa wa lugha. Karibisha hata wazawa darasani
UFUNDISHAJI WA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI
Kunakuwepo na shida katika ufundishaji wa kisw kama lugha ya kigeni kwa kuwa nje ya darasa kunakuwepo na lugha isiyopatikana nje ya darasa.
Muda wa kujifunza ni mdogo katika lugha.
MAMBO YA KUFANYA (MWALIMU)
  1. Mwalimu atumie uasilia wa lugha na mbinu shirikishi.
  2. Hakikisha unatoa motisha mara kwa mara kila utoapo zoezi ili kuwahamasisha wanafunzi.
  3. Wasaidie sana wanafunzi wako ili waone umhimu wa lugha hiyo.
  4. Wape majaribio ya kufanya kazi na usisitize kuyafanya.
  5. Toa fursa za ziada darasani kama radio, tv, magazeti, vitabu, makala nk.
  6. Fanya michezo ya uigizaji na usumuliaji
  7. Leta wazawa waje kuzungumza nao
  8. Weka mbinu za nje kuzitumia nje ya darasa
  9. Unda klabu za lugha.
  1. Ueledi wao
Hapa tunaangalia je ni wanadiplomasia, wanataaluma, wamisionari nk.

MADA YA 4: UTAYARISHAJI WA MUHTASARI (SYLABUS) NA VIFAA VYA KUFUNDISHIA
  1. Utayarishaji wa syalabus katika ufundishaji wa Kiswahili
Syllabus ni muhatasari wa mada zinazokwenda kufundishwa katika kiwango Fulani cha elimu
Mambo ya kuzingatia katika kuandaa syabus
(a)    Malengo ya kozi
(b)   Mada zizingatie uelewa wa wanafunzi kwa kila kiwango: mf, kiwango cha juu, chini au kati
©    Mada zizingatie muktadha wa wanafunzi
(d)   Izingatie uelewa wa wanafunzi, izingatie uelewa wa awali wa wanafunzi.
(e)   Izingatie matakwa na mahitaji ya wanafunzi na jamii kwa ujumla.
(f)     Izingatie muda katika ufundishaji wa kila kiwango.
VIPENGELE
  1. Malengo ya jumla ya kufundisha Kiswahili kwa wageni.
  2. Matokeo ya ujifunzaji
  3. Mada zitakazofundishwa kwa kiwango Fulani
  4. Mbinu za kufundishia mada
  5. Vifaa/zana zitakazotumika katika ufundishaji na ujifunzaji wa lugha.
  1. UTAYARISHAJI WA VITABU VYA KUFUNDISHIA KISWAHILI KWA WAGENI.
(a)    Ni muhimu kuzingatia mtiririko mzuri wa mada / masomo kuanzia somo moja hadi jingine kuanzia rahisi kwenda ngumu. Kuna vipengele vine vya kuazingatia katika uandaaji wa kitabu cha kitabu cha Kiswahili kwa wageni
(i)                  Kurasa za utangulizi, yatolewe maelezo ya utangulizi juu ya historia fupi ya lugha ile ili kusaidia mwanafunzi kujua hali na hadhi ya Kiswahili nchini Tanzania ,
pia sauti za lugha na matamshi lazima zionyeshwe katika utangulizi. Maneno ya lugha mama ya mwnafunzi yatumike kutafsiri maneno ya kigeni kumfanya mwanafunzi kutambua sauti ambazo haziko katika lugha yake.
(ii)                Kurasa zenyewe, Masomo yenyewe yaonyeshe mtiririko wa mada zenyewe
(iii)               Kurasa za mwisho,
(a)    Orodha ya misiamia na semi zilizotumika katika kitabu hicho zionyeshwe na zipangwe kialfabeti kurahisisha uapatikanaji wa msamiati. Ni vizuri orodha hiyo iwe na tafsiri katika lugha ya wanafunzi. Pia kunafaa kuwe na orodha mbili za maneno, maneno ya kigeni na maneno ya lugha mama, lengo la orodha hizo mbili ni kuipa nafasi lugha ya wanafunzi kujifunza lugha ya kigeni. Pia kurasa za mwisho zioneshe majedwali kuonesha sarufi ya lugha inayofundishwa kusaidia upatikanaji wa maneno yaliyo sahihi
  1. UTAYARISHAJI WA SOMO LENYEWE
Mambo ya kufanya
  1. Somo liwe na lengo mahususi kumsaidia mwanafunzi kuwasiliana, mada idokeze nn mwanafunzi atajifunza aweze kuwasiliana na wazawa wa lugha.
  2. Somo liwe na msamiati na sarufi ambavyo vinavyokidhi mahitaji wa mwanafunzi.
Msamiati udhihirike kutokana na mada yenyewe, sarufi imhamasishe mwanafunzi kutaka kuzungumza na si kujua kanuni tu.
  1. Somo lionyeshe lugha inavyozungumzwa na wazungumzaji.
  2. Somo liwe na vielelezo vya mazingira halisi na taarifa muhimu za kiutamaduni wa lugha ambayo mwanafunzi anajifunza. Pia aelezwe kuwa salamu yaweza kuwa fupi au ndefu. Mf: shikamoo: hutolewa na mdogo kwa mkubwa. Kifamilia si mme mke na watoto tu bali hata ndugu wa karibu wa lugha hiyo.
  3. Somo liambatane na vielezo kama vitu halisi kama picha, vielelezo,nyimbo, matangazo magazeti, ramani hasa katika hatua ya kwanza. Nk. Lengo la vielelezo ni kumuingiza mwanafunzi ndani ya lugha, utamaduni wa lugha ili aweze kujieleza.
  4. Kila somo liwe na mazoezi halisi wa stadi za lugha mazoezi hayo yatokane na matini au vielelezo vilivyoandamana na masomo hayo. Mazoezi yamwezeshe mwanafunzi kupata umahiri wa uamilifu wa lugha na kukuza mawasiliano. Baada ya kila somo lielezwe mwanafunzi akafanye nn baada ya somo.
UWASILISHAJI WA DARASANI 22/04/2014 KIPINDI CHA JIONI
Swali: Jadili mbinu ya mawasiliano inavyoweza kutumiwa na mwalimu katika kufundisha Kiswahili kwa wageni.
Richard 1996
Mbinu hii ilikuwa katika bara la ulaya na kupelekea kuongezeka kwa wahamiaji na hivyo kukawa na mahitaji makubwa ya wanafunzi wa lugha za kigeni.
Misingi ya ufundishaji
  1. Kujikita katika uwezo wa kuwasiliana katika lugha wanayofundishwa wanafunzi na usijikite katika sarufi ya lugha.
  2. Wanafunzi wapewe nafasi ya kuzungumza kile wanachokijua kuhusu lugha kwa kutumia uwezo wao.
  3. Mwalimu awe mvumilivu pale wanafunzi wanapokuwa wamekosea kwa sababu hawana misingi ya lugha hiyo.
  4. Ufundishaji lugha uzingatie misingi halisi ya maisha
  5. Umilisi wa mawasiliano kwa kutofautisha wapi pakutumia lugha rasmi na wapi pasipo pa kutumia lugha rasmi. Chanzo>>>>>

Print this item