COURSE TITLE: THEORY AND PRACTICE OF TRANSLATION AND INTERPRETATION II
COURSE CODE: BKS 221
MUDA: SAA 2
MAAGIZO:
JIBU SWALI LA KWANZA NA MENGINE MAWILI
1a) Tofautisha tafsiri na ukalimani (alama 8)
b) Fafanua sifa za mfasiri bora (alama 4)
c) Eleza hatua mbili kuu za kufasiri kwa mashine (alama 4)
d)Onyesha majukumu ya nadharia ya tafsiri (alama 8)
e) Eleza dhana zifuatazo:
i) Nadharia ya kisemantiki (alama 3)
ii) Nadharia ya Usuluhishi (alama 3)
Tafsiri kwa Kiswahili makala A (alama 20)
Tafsiri kwa Kiingereza makala ya B (alama 20)
Jadili nadharia ya mawasiliano katika tafsiri ilivyodokezwa na Peter Newmark. (alama 20)
Onyesha uhusiano wa nadharia ya tafsiri na taaluma nyingine (alama 20)
Makala A
NINA: Jusper, where were you?
JUSPER: Serving the nation.
NINA: How could you desert your brother?
JUSPER: It was an order.
NINA: What order? You take off that thing and go and put on something descent. The others will soon be here.
JUSPER: Is Regina with them?
NINA: Perhaps.
JUSPER: Girlfriend number one; she ought to come.
NINA: She’s far away in the city. Where is your father?
DOGA: (Whispering rather loudly.) Do not detain him. Let him go.
JUSPER: He can’t go; he is dead.
NINA: My son, please go and put on a clean shirt.
JUSPER: A clean shirt? No. Not after the murder.
NINA: What shall we do now? The illness creeps back on him. Jusper , do you know what day today is?
DOGA: Don’t remind him.
JUSPER: Come and see for yourself. (Points at the crack.) Do you see this river, all this water? I threw him in there. Don’t tell me he swam away, because he didn’t. He was dead when I threw him there.
NINA: He thinks he has killed you. Please do something before he spoils the ceremony.
DOGA: I told you to shut that mouth!
JUSPER: Alright, I will shut up. Nobody need know am a murderer. (throws the sticks away.) After all, it was great fun. Now I know how they feel when they do it. Shall I go and confess I did it?
NINA: Yes my son, go and put on a clean shirt and then you can confess.
JUSPER: Do you think they will harm me if I address the rally?
NINA: No, they won’t. Just go and put your shirt first.
JUSPER: Will they put him in a government coffin, do you think?
NINA: Good God, what shall we do?
JUSPER: I will go and recommend a government coffin with many handles so that everybody will help lower him into the grave. (He smiles, stands at attention, salutes, then exits, military style.)
NINA: He has never behaved like this before.
DOGA: His eyes were full of sleep.
NINA: Why did he think he had killed you?
DOGA: It was his brother he thought he had killed. I saw him address the grave as if Adika sat right on top of it. It was both strange and frightening.
Makala B
Kwa muda mrefu, kumejitokeza majaribio yanayolenga katika kuieleza lugha pasina mafanikio makubwa hadi pale ilipoanza kutumika mikabala ya kisayansi. Mikabala ya kisayansi ikawa mihimili na misingi dhabiti ya kuichunguzia lugha. Wataalamu mbalimbali wameeleza maana ya isimu, mathalan Besha(1994)ambaye anaifafanua isimu kama taaluma ambayo inachunguza na kuweka wazi kanuni ambazo ni msingi wa kila lugha. TUKI (1990) wanaeleza kuwa isimu ni sayansi ya lugha. Basi, tunaweza kusema kuwa isimu ni taaluma inayohakiki lugha kisayansi. Isimu ni sayansi ya matamshi,maumbo,miundo,maana na matumizi ya lugha.
Taaluma hii hutumia mtazamo wa kisayansi katika kuichambua lugha kinyume na ilivyokuwa hapo zamani ambapo watafiti waliathiriwa na hisia na mielekeo yao. Taaluma hii hujaribu kujibu maswali mbalimbali kuhusu lugha.Maswali haya ni pamoja na: Lugha ni nini? Lugha hufanyaje kazi? Huwa unajua nini unaposema unajua lugha fulani? Je, lugha ni sifa ya binadamu pekee? Lugha ya binadamu hutofautianaje na mawasiliano ya wanyama? Asili ya lugha ni ipi? Kwa nini kuna lugha nyingi? Lugha hubadilikaje? Watoto hujifunzaje lugha? Je, lugha na lahaja fulani ni rahisi kuliko nyingine? Mtu huandikaje na kuchanganua lugha isiyokuwemo kwenye maandishi?
Wataalamu ambao wanashughulikia haya masuala kuhusu lugha huitwa wanaisimu. Mwanaisimu ni mtu anayechunguza lugha kisayansi kwani ana ujuzi wa kanuni zinazoitawala lugha. Mwanaisimu huichanganua na kuieleza lugha kwa kurejelea matukio ya kiisimu kama vile mfumo wa irabu na muundo wa vitenzi vilivyoko katika lugha. Labda swali tunaloweza kujiuliza hapa ni: je malengo ya isimu ni yepi? Suala hili linashughulikiwa katika sehemu inayofuata.
KAMUSINI tunaangazia namna baadhi ya Wanahabari wanavyobananga lugha ya Kiswahili. Kwanza ifahamike dhahiri kuwa lengo la makala haya ni kuchagiza matumizi ya Kiswahili sanifu ikiwa ni pamoja na kusahihisha makosa ya matumizi ya Lugha na hasa yanayofanywa na Wanahabari wa vyombo vyote.
Kwa nini kwa wanahabari ? Ni kwa sababu vyombo vya habari vina nguvu kubwa ya ushawishi ndani ya jamii. Kwa hiyo, vinaweza kuwa mwalimu mzuri au mbaya kwa jamii ndani ya muda mfupi.
Kwa hiyo, makala ya Kamusi hayana chuki na chombo chochote chenye kutumia Kiswahili. Hata hivyo, wapo Wanahabari kwa makusudi au kwa ujinga wanafanya makosa lukuki wanapotekeleza majukumu yao.
Inashangaza kuona namna Watangazi/ Waandishi wa vyombo vya Idhaa za Kiswahili walivyo weledi wa Kiingereza wakati Kiswahili ndiyo lugha ya kupashia habari hawana ujuzi nacho au wanakibeza tu kwa makusudi. Hivyo wanatumikia Kiswahili kilichochapwaa kabisa.
Baadhi ya Wanahabari machale hudhani kuwa ikiwa watasema Kiingereza katika vipindi vyao basi wataonekana wana akili au wana ujuzi mkubwa juu ya kazi zao. Hiki ni kinyumbe cha mambo.
Uchunguzi uliofanywa na makala ya KAMUSI umebaini kuwa Waswahili wengi wanafuatilia vyombo vya habari vya nje vya Idhaa za Kiswahili kama BBC, DW, VoA kwa kuvitaja vichache. Ingawa navyo havipo salama sana katika usanifu wa lugha lakini vyombo hivyo vya nje vinaonesha bidii za wazi kwa kutumia Kiswahili Fasaha.
Ufasaha wao lugha hasa uteuzi bora wa msamiati katika matangazo yao huwafanya Waswahili wengi kufuatilia matangazo ya vyombo hivyo kwa raghba kubwa.
Hata hivyo , hapa nyumbani vipo vyombo vya habari vituamiavyo lugha kwa ufasaha kiasi na kujipambanua kwa kipekee. Baadhi ya vyombo hivyo ni runinga ya Imani- Morogoro na redio Imani ya huko huko, ITV/ Redio One ya Dar es Salaam, TBC taifa, Azamtv/ U FM ya Dar es Salaam.
Hata hivyo, vyombo vilivyotajwa hapo juu bado vina changamoto za lugha lakini kama ilivyosemwa vyombo hivyo vina nafuu kwa kiasi fulani ikilinganishwa na vingi visivyokuwa katika orodha hiyo.
Aidha, vipo vyombo vya habari vya ovyo/ hovyo sana kwa matumizi ya Lugha ya Kiswahili. Hivi ni vile uongozi na watangazaji wake hawaoni soni wala hawajali kuhusu lugha ya Kiswahili. Wao wanaamua kutumia neno lolote tu, katika muktadha wowote , namna yoyote na kivyovyote. Vyombo hivi ni hovyo sana na ni vingi hapa Afrika Mashariki.
Bila shaka wafuatiliaji wa makala haya ya KAMUSI wanaweza kuviorodhesha hapo chini kimoja baada ya kingine. ( Tunaomba uorodheshe vyombo vya ovyo/ hovyo katika mutumizi usanifu ya Kiswahili unavyovijua wewe).
KAMUSI ilifanya uchunguzi zaidi wa uwandani kuhusu sababu za vyombo vya habari kubananga lugha kwa kiasi kikubwa. Baadhi ya sababu ya ubanangaji huo ni pamoja na : Mosi, baadhi ya vyombo hivyo kuwaajiri machale badala ya Wanahabari, pili, Uongozi wa vyombo hivyo kutoweka mkazo katika lugha ya Kiswahili, tatu, vyombo vingi vya nyumbani kutokuwa na kamusi ,
Sababu nyingine ni pamoja na : nne, vyombo karibu vyote kutokuwa na wataalam wa Kiswahili katika madawati ya Habari na vyumba vya habari, tano, Baraza la Kiswahili la Taifa ( BAKITA) kutokuwa na meno makali ya kutoa adhabu kwa wabanangaji wanaotajwa, sita , watangazaji kuwa ushamba , kasumba , kukosa uzalendo na uchache wa mawazo ya Kimajumui wa Kiafrika.
Mathalani, baadhi ya Wanahabari wanaohusikika wakieleza kwa mfano, ,( i) Watu wawili wameweza kufa, (ii) Timu ya Yanga imeweza kufungwa katika mchezo wa mwisho ligi mabao mawili na Azam.Haya ni baadhi tu ya makosa.
Yaani mwanadamu aliyetoka nyumbani kwake kwa azama ya kutarazaki kwa mkosi tu akagongwa na motokali kisha kupoteza maisha. Ati mtu huyo anatajwa kuwa ameweza kufa kama vile mtu huyo alikuwa akitafuta kufa na amefanikiwa kufa huko.
Na huo mfano wa pili, kwanza haupendezi masikioni mwa Yanga wenyewe lakini si kweli kwamba yanga iliingia uwanjani ili kupoteza mchezo ule dhidi ya kikosi cha Azam. Basi tu Mipango si matumizi na mchezo wenyewe umechezwa wakati watu wakiwa na swaumu! Shubamiti!
KAMUSI inatoa wito kwa jamii ya Wanahabari kujitahidi kukifahamu vema Kiswahili na kukitumia kwa ufasaha. Makala ya KAMUSI ipo tayari kusaidia wanahabari katika kujifunza lugha Kwa nadharia na vitendo. Chombo chochote chenye utashi na lugha kinaweza kuwasiliana na uongozi wa kamusi ili kushirikiana katika kutoa mafunzo ya kunoa ubongo ili kujijengea uwezo wa matumizi sanifu ya Kiswahili chanana.
” Lugha ndiyo Utambulisho wa Utamaduni wa mtu, Fikra sahihi hufumbatwa na lugha sahihi”
Majid Mswahili #Bwanakamusi
Mchambuzi wa Lugha, Fasihi , Fasaha ya Kiswahili.
Usithubutu Kupitwa na Makala haya ya KAMUSI. ( Imahaririwa tahajia)
Tuandikie: majidkiswahili@gmail.com Au +255 715 83 84 80.
KAMUSI imeletwa kwenu kwa hisani ya Utu- Tanzania na Culture Link Africa Ltd na Kamusi Pevu ya Kiswahili
KAMUSINI LEO tunaendelea kusaidia kutoa uelewa kuhusu maneno ya Kiswahili.
Baadhi ya maneno yanayotumika vibaya
1. Mbele/Mbeleni
Neno mbele linaweza kuwa na maana ya siku au tarehe za usoni. Mfano: Tarehe ya uchaguzi imesogezwa mbele.
Mbele pia ina maana ya usoni mwa kitu au mtu, kama vile mbele ya macho, mbele ya watu. Lakini neno ‘mbele’ likiongezewa kipashio ‘ni’ na kuwa ‘mbeleni’, basi kwa silka na adabu za Waswahili neno hilo hugeuka kuwa tusi, lenye maana ya sehemu za siri za mwanamke. Hivyo, maneno mawili haya si vibadala, kila moja lina maana yake.
2. Husika
Sifa moja ya vitenzi vya Kiswahili ni kuchukua viambishi vya mtenda, wakati na mtendwa. Vipashio hivyo vina dhima, maana na matumizi maalumu vinapotumika, kama vile kubadilisha nafsi ya mtenda na mtendwa, ngeli, kuonesha umoja na wingi na wakati wa kutokea kwa tendo. Kwa mfano:
mtu – a_nayekusika – watu wa_naohusika
gari – i_nayohusika – gari zi_lizohusika
kazi – i_takayohusika – kazi zi_takazohusika
Kutumia neno husika bila kuliambatanisha na vipashio vyake vya mtenda, mtendwa na wakati ni kukiuka taratibu za sarufi ya lugha zilizokubalika bila ya kuwa na sababu za msingi.
3. Mrabaha
Baadhi ya watumiaji wa lugha ya Kiswahili kwa kutojua au kutokuwa makini wanalitamka neno hili kwa kuzibadilisha nafasi za silabi ‘ba’ na ‘ha’ na kulitamka #mrahaba, yaani linazalisha neno jipya ambalo hata halimo katika lugha.
Makala haya ya KAMUSI inakushajiisheni wafuatiliaje wa nakala haya hasa wanahabari kumanikia usanifu wa lugha ya kutangazia habari zao.
#Usithubutu Kupitwa na Makala ya Kamusi.
KAMUSI imeletwa kwenu kwa hisani ya BAKIZA #KamusiLaKiswahiliFasaha na #Tamthiliya ya NjeNdani.
Majid Mswahili
#Bwanakamusi.
Mchambuzi wa Lugha, Fasihi na Fasaha ya Kiswahili.
Tuandikie : majidkiswahili@gmail.com Au + 255 715 838480