MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  

Password
  





Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 185 online users.
» 0 Member(s) | 183 Guest(s)
Bing, Facebook

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

 
  FASIHI YA KISWAHILI NADHARIA NA UHAKIKI
Posted by: MwlMaeda - 06-16-2021, 01:42 PM - Forum: Nukuu - No Replies


.pdf   FASIHI YA KISWAHILI NADHARIA NA UHAKIKI.pdf (Size: 616.27 KB / Downloads: 5)

Print this item

  FASIHI SIMULIZI
Posted by: MwlMaeda - 06-16-2021, 01:40 PM - Forum: Nukuu - No Replies


.pdf   FASIHI SIMULIZI.pdf (Size: 511.33 KB / Downloads: 3)

Print this item

  FASIHI SIMULIZI KWA KINA
Posted by: MwlMaeda - 06-16-2021, 01:36 PM - Forum: Nukuu - No Replies


.pdf   FASIHI SIMULIZI KWA KINA.pdf (Size: 685.15 KB / Downloads: 10)

Print this item

  MBINU ZA KUFUNDISHIA LUGHA
Posted by: MwlMaeda - 06-16-2021, 01:32 PM - Forum: Nukuu - No Replies


.pdf   MBINU ZA KUFUNDISHIA LUGHA.pdf (Size: 232.47 KB / Downloads: 2)

Print this item

  SARUFI NA SINTAKSIA YA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 06-16-2021, 01:23 PM - Forum: Nukuu - No Replies


.pdf   OSW 221 SARUFI NA SINTAKSIA NUKUU (2021).pdf (Size: 735.44 KB / Downloads: 8)

Print this item

  SHAIRI: NAWAKUMBUSHA TU
Posted by: MwlMaeda - 06-16-2021, 11:41 AM - Forum: Ushairi - No Replies

1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...

"KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI".
??????

Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake, leo twatambua nini maana yake

Nawakumbusha tu
??

SHAMBA SHAMBA SHAMBA
?????????????

Print this item

  SHAIRI: NALIA
Posted by: MwlMaeda - 06-16-2021, 07:54 AM - Forum: Ushairi - No Replies

NALIA

Nyachani nitabaruku, Kwake Ilahi Mwenyezi
Nami niavye shauku, ngawa n-jaa majozi
Walau niseme haku, imhusuyo mzazi
Umetawafu mpenzi, nalia ingawa haku.

Nalia ingawa haku, e baba yangu mzazi
Umauti ukupiku, ubana zako pumzi
Mwana mkiwa ruzuku, mruzukuji Azizi
Umetawafu mpenzi, nalia ingawa haku.

Nalia ingawa haku, npigwa ni bumbuwazi
Ja aliyeroa kuku, n-nywea sili siwazi
Shuwari haipo huku, na kimbunga kimesizi
Umetawafu mpenzi, nalia ingawa haku.

Nalia ingawa haku, mbee zako simulizi
Nkwitapo marufuku, hupo hunambia njozi
Baba kama ipo siku, ningekwita ubarizi
Umetawafu mpenzi, nalia ingawa haku.

Nalia ingawa haku, mbele tena sitogezi
Haja haambiwa peku, bovu liso matumizi
Nimeikubali haku, hii kwetu ni farazi
Umetawafu mpenzi, nalia ingawa haku.


Mtunzi
Pandu Haji Gora
Chumbuni

Print this item

  UHUSIANO WA TAFSIRI NA TAALUMA NYINGINEZO
Posted by: MwlMaeda - 06-16-2021, 07:27 AM - Forum: Tafsiri na Ukalimani - No Replies

TAFSIRI ni taaluma ya lugha ambayo imefuata ukalimani baada ya ugunduzi wa maandishi. Tafsiri ni uhawilishaji wa maana iliyo katika matini ya lugha chanzi kwa njia ya kuweka maana inayolingana katika matini ya lugha lengwa.
Kwa hivyo ni shughuli au jaribio la uhawilishaji wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja hadi nyingine.
Kwa ujumla, fasili hizi zote zinaonyesha kuwa tafsiri hufanyika katika maandishi. Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa tafsiri ni shughuli ya uhawilishaji wa maana, mawazo, dhana au ujumbe ulio katika maandishi kutoka lugha chanzi na kuweka badala yake maana, ujumbe, mawazo au dhana inayolingana na ile ya lugha chanzi katika lugha lengwa.
Ikiwa taaluma ya lugha, tafsiri ina majukumu kadhaa ya kushughulikia. Pamoja na majukumu hayo ni kutolea matangazo, mfano katika utalii, brosha n.k. Ni njia ya mawasiliano baina ya watu wanaozungumza lugha tofauti na ni wenzo wa kueneza utamaduni hasa ikizingatiwa jinsi dini za kigeni kama vile ukristo na uislamu zilivyoingizwa nchini kwa njia ya tafsiri na ukalimani.
Tafsiri ni wenzo wa kukuza fasihi, mfano hadithi ya Alfu Lela Ulela (siku elfu moja), Treasure Island (Kisiwa Chenye Hazina), Robinson Krusoe na Kisiwa Chake, Mabepari wa Venisi n.k. waandishi waliweza kuiga mbinu za uandishi na hivyo kuwa na fasihi bora.
Aidha, tafsiri ni wenzo muhimu wa kujifunza lugha ya kigeni na kujifunza miundo na maumbo ya lugha fulani. Kwa mfano watu wanaofanya utafiti kuhusu lugha fulani hutumia tafsiri kama njia ya kuelezea lugha hizo. Tafsiri humwezesha mtu kujiajiri (kama chanzo cha ajira).
Mfasiri anapofanya kazi ya kufasiri anapata pesa na hivyo hizo pesa humsaidia katika maisha yake ya kila siku. Pia ni kama njia ya kukuza lugha kwa kuwa msamiati mwingi huingia katika lugha lengwa na hivyo kuitajirisha.
Sifa za mfasiri
Ili mtu kuitwa mtafsiri anatikwa awe anamudu vizuri sarufi za lugha zote mbili anazofanyia kazi. Anastahili awe na ufahamu wa kutosha kuhusu utamaduni wa lugha chanzi, awe ni mtumiaji mzuri wa kamusi na marejeo mengine muhimu.
Aidha, anastahili kuwa na uwezo mkubwa wa kuandika katika lugha chanzi na angalau awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
Kuna mambo muhimu ambayo mtafsiri anatakiwa kuyazingatia katika kutafsiri matini. Mtafsiri atalazimika kusoma matini yote kabla hajaanza kutafsiri. Anapaswa kufanya hivyo ili aweze kuelewa kinachozungumzwa – ujumbe uliomo. Aweze kuandaa marejeleo muhimu anayohitaji kama vile kamusi, vitabu n.k. ili vimfae katika jitihada za kubaini aina ya matini pamoja na matatizo yanayojitokeza katika matini husika na kuweza kuyatatua matatizo hayo.
Kuna uwezekano wa kuwapo kwa matatizo ya kitahajia katika tungo ambazo hazijakamilika.
Mtafsiri anastahili kuigawa kazi katika vipande kama ni ndefu au inashughulikiwa na watu wengi.
Ingawa hivyo, kuna mwingiliano mkubwa kati ya tafsiri na taaluma nyinginezo kama hizi zifuatazo:
Semantiki
Hii ni taaluma inayohusiana na maana. Katika tafsiri tunazingatia maana ya lugha chanzi ili isitofautiane na maana ya lugha lengwa. Muktadha pia sharti uzingatiwe katika kupata maana.
Isimujamii
Huangalia jamii inavyoathiri lugha na lugha inavyoathiri jamii. Katika taaluma ya tafsiri, tamaduni, mila, itikadi na desturi za jamii husika huzingatiwa.
Mfano unapokutana na maneno ya kitamaduni katika tafsiri kama vile salamu, vyakula n.k hapa inabidi utamaduni wa lugha husika uzingatiwe.
Isimu Linganishi
Katika tafsiri, tunalinganisha lugha moja na nyingine ili kuelewa miundo na maumbo kati ya lugha chanzi na lugha lengwa. Kwa hivyo isimu linganishi huchukua nafasi yake hapa.
Elimu mitindo
Kuna uainishaji wa mitindo ya lugha na muktadha wa matumizi yake katika tafsiri, kitu ambacho kipo pia katika taaluma ya elimu mitindo.
Uhakiki wa matini
Kabla mtafsiri hajaanza kutafsiri matini, ni lazima ahakiki matini chanzi kwa lengo la kubaini upungufu unaojitokeza ili kujua namna ya kuweza kukabiliana nao.
Mantiki
Hii ni taaluma inayohusu ukweli na usahihi katika kauli au matini fulani. Taaluma hii humsaidia mtafsiri kubaini usahihi na mantiki iliyopo katika lugha chanzi.
Falsafa
Ni taaluma inayosisitiza kutafuta maana za maneno kutokana na matumizi halisi katika matini. Hii humsaidia mtafsiri kujua falsafa ya matini husika na hatimaye kuelewa maana yake.

Print this item

  Karibu sana
Posted by: MwlMaeda - 06-16-2021, 07:14 AM - Forum: My Forum - No Replies

Natumia fursa hii kukukaribisha katika jukwaa hili linalounganisha wadau wa lugha ya Kiswahili popote walipo ulimwenguni. Karibu uchapishe makala zako na kushiriki katika mijadala inayoibuliwa na wadau wa lugha adhimu ya Kiswahili.



Lugha yetu, Fahari yetu

Print this item

  SHAIRI: NIKAZIKWE LIPARAMBA
Posted by: MwlMaeda - 06-16-2021, 06:02 AM - Forum: Ushairi - No Replies

Johari kijiji hiki,
Mithiliyo siiwezi,
Hata ningepewa laki,
Na kukihizi siwezi,
Ingawa hakisifiki,
Chafanana na feruzi,
Nasema yenye mithaki,
Sifa majazi majazi.

Kingine mimi sitaki,
Nikaanzisha makazi,
Na wala sijaafiki,
Kuna tamu ya malazi,
Hainiishi ashiki,
Kuhama huko siwezi,
Sifa kimetamalaki,
Kwa siku hata miezi.

Ni kifa hamniziki,
Ila ni hapa azizi,
Na kaburini sishuki,
Shikeni habari hizi,
Bora kunitaalaki,
Niwapayo maongozi,
Isiwe afanaleki!
Niwaache bumbuwazi.

Penginepo sipataki,
Kamwe huko sijilazi,
Ila ni kijiji hiki,
Kwa mama yangu mzazi,
Nasema siteremki,
Kumbukeni maongozi,
Kwengine haunifiki,
Wa milele usingizi.

Walipolala rafiki,
Pia na mama mzazi,
Bibi naye hafufuki,
Na kumuhama siwezi,
Nuru Mbunda hukumbuki,
Kipenzi changu lazizi,
Mbali nao sijiweki,
Kwengine hamunilazi.

Ni faradhi kufariki,
Kushinda kifo siwezi,
Nikikumbuka rafiki,
Sipungukiwi machozi,
Mwadhani sihuzuniki,
Mkaona sijilizi,
Kinauma kitu hiki,
Ndio mana sinyamazi.

Mwengine hamkumbuki,
Emiliana azizi,
Pia ni wangu rafiki,
Wa Ntanga yake makazi,
Aliumwa hatibiki,
Hapo kifo akahozi
Sikitaki kitu hiki,
Kukifanya kumbukizi.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Nyasa-Ruvuma
0753738704

Print this item