SHAIRI: NIKAZIKWE LIPARAMBA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: NIKAZIKWE LIPARAMBA (/showthread.php?tid=37) |
SHAIRI: NIKAZIKWE LIPARAMBA - MwlMaeda - 06-16-2021 Johari kijiji hiki, Mithiliyo siiwezi, Hata ningepewa laki, Na kukihizi siwezi, Ingawa hakisifiki, Chafanana na feruzi, Nasema yenye mithaki, Sifa majazi majazi. Kingine mimi sitaki, Nikaanzisha makazi, Na wala sijaafiki, Kuna tamu ya malazi, Hainiishi ashiki, Kuhama huko siwezi, Sifa kimetamalaki, Kwa siku hata miezi. Ni kifa hamniziki, Ila ni hapa azizi, Na kaburini sishuki, Shikeni habari hizi, Bora kunitaalaki, Niwapayo maongozi, Isiwe afanaleki! Niwaache bumbuwazi. Penginepo sipataki, Kamwe huko sijilazi, Ila ni kijiji hiki, Kwa mama yangu mzazi, Nasema siteremki, Kumbukeni maongozi, Kwengine haunifiki, Wa milele usingizi. Walipolala rafiki, Pia na mama mzazi, Bibi naye hafufuki, Na kumuhama siwezi, Nuru Mbunda hukumbuki, Kipenzi changu lazizi, Mbali nao sijiweki, Kwengine hamunilazi. Ni faradhi kufariki, Kushinda kifo siwezi, Nikikumbuka rafiki, Sipungukiwi machozi, Mwadhani sihuzuniki, Mkaona sijilizi, Kinauma kitu hiki, Ndio mana sinyamazi. Mwengine hamkumbuki, Emiliana azizi, Pia ni wangu rafiki, Wa Ntanga yake makazi, Aliumwa hatibiki, Hapo kifo akahozi Sikitaki kitu hiki, Kukifanya kumbukizi. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Nyasa-Ruvuma 0753738704 |