SHAIRI: NALIA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: NALIA (/showthread.php?tid=40) |
SHAIRI: NALIA - MwlMaeda - 06-16-2021 NALIA Nyachani nitabaruku, Kwake Ilahi Mwenyezi Nami niavye shauku, ngawa n-jaa majozi Walau niseme haku, imhusuyo mzazi Umetawafu mpenzi, nalia ingawa haku. Nalia ingawa haku, e baba yangu mzazi Umauti ukupiku, ubana zako pumzi Mwana mkiwa ruzuku, mruzukuji Azizi Umetawafu mpenzi, nalia ingawa haku. Nalia ingawa haku, npigwa ni bumbuwazi Ja aliyeroa kuku, n-nywea sili siwazi Shuwari haipo huku, na kimbunga kimesizi Umetawafu mpenzi, nalia ingawa haku. Nalia ingawa haku, mbee zako simulizi Nkwitapo marufuku, hupo hunambia njozi Baba kama ipo siku, ningekwita ubarizi Umetawafu mpenzi, nalia ingawa haku. Nalia ingawa haku, mbele tena sitogezi Haja haambiwa peku, bovu liso matumizi Nimeikubali haku, hii kwetu ni farazi Umetawafu mpenzi, nalia ingawa haku. Mtunzi Pandu Haji Gora Chumbuni |