Posted by: MwlMaeda - 08-19-2021, 09:02 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU
SEHEMU YA 02
Kwakweli kwa Zamda usiku wa siku ile ulikuwa ni usiku wa Yeye kujikuta kama ni mlinzi wa Nyumbani kwao.Kwasababu hata Usingizi kwake Kwakweli ulikwea mbali sana hata kubembelezeka haubembelezeki kabisa.Akawa anasema Hivi akiwa mda huo kitandani giza kote Yaani mda huo taa zimezimwa.
Ni Kweli Yaani nikiwaangalia wale mashoga zangu Kwakweli hadi wananitamanisha.Angalia huyo Kidawa anavaa saa kali vile nywele anaenda kunyoa hadi Raha Jamani.Huyo Mwantumu naye ndiyo usiseme Yaani namna anavyozitafuna hizo Hela za hao wanaume na kawapanga hadi Raha kwa akili tu.Yaani mtoto mdogo tu vile anawapanga wavulana namna ile.Duuu sijui Jamani na Mimi nijiunge na mawazo ya Hawa mashoga zangu Au mawazo ya mama.Kwanza Hawa ndiyo wakati wao haya mawazo ya mama yeye anaongea hivyo kwa vile ameshapita hiki kipindi cha usichana.Huu ndiyo Wakati wetu bana na sisi wasichana."Lakini anapoendelea kuyachuja maneno ya Hao shoga zake Zamda Lakini na maneno ya mama yako yalimuijia masikioni mwake huku akiwa anavutia picha ya siku ile wakiwa wamekaa jikoni hapo. Zamda akaanza tena kusema hivi ".
Hapana..... Hapana..... Hapana lazima nifuatilie mawazo ya mama yangu.Kwasababu mama yangu Kwakweli Kwa namna alivyoongea siku ile,Kwakweli aliongea kwakuweza kunipatia faida Mimi Au ni kumpatia faida nani zaidi ya Mimi. Embu huu ushetani utoke humu kichwani mwangu kabisaaaaaaa. Sitaki cha mawazo ya Huyo Kidawa wala huyo Mwantumu. Kama ni ushoga bora tuuvunje na kuufutilia mbali kabisaaaaaaa. Wale siyo marafiki wazuri kabisaaaaaaa. Bora nife na umasikini wangu hivi hivi.Yaani nilivyo mdogo hivi na nilivyo mlembwende hivi afu ndiyo nije nipate huo ugonjwa wa UKIMWI nitakuwa mgeni wa nani miyeeeeeeeeeeeee Jamani.Acha nibaki hivi hivi Bali si kuendelea kujiunga na lile Kundi. Yaani lile Kundi wala siyo kundi kabisa Lakusema kila mmoja wapo pale akupatie ushauri."Kwakweli usiku wa Zamda kwa siku ile ulikuwa ni usiku wa Yeye Kuwaza na kuwazua tu.Lakini baada ya kupita mda kidogo Hivi akawa tayari naye Usingizi ukawa umeshampitia na akawa amelala Usingizi uliokuwa ni mzito kwelikweli".
kwakweli kwa usiku ule baada ya Zamda kupitiwa na Usingizi mkali kwelikweli kuna ndoto fulani ilimwijia. Ambapo ndoto Hiyo inaonesha kwamba Zamda yuko sehemu fulani hivi ambayo ni kama mtoni hivi.Eneo hilo nalo kuna watu wako hapo mojawapo wakiwa ni Shoga zake Zamda yaani Kidawa na Mwantumu. Lakini sehemu hiyo inaonesha kwamba Zamda amebeba mtoto ambapo inaonesha kabisa Zamda ameshakuwa vya kutosha haswaaaa.Anaonekana akiwa anamtoto mgongoni wa kike analia kwelikweli huku akawa anasema kwamba hivi
Daaaa Jamani hii ndiyo tabu ya kuwa na mtoto. Yaani wanasumbua kwelikweli."Baada ya Zamda kuzungumza namna hiyo Kidawa na Mwantumu wakiwa wanaonekana wako pembeni Hapo wakawa wamecheka kicheko cha moja kwa moja kilichofanya hadi yule Mtoto kuweza kunyamaza kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa baada ya kusikia sauti zile za shoga zake Zamda.Baada kucheka kwa sekunde kazaa wakaambatanisha na maneno kwaajili ya huyo rafiki yao kwakusema ".
Heheeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!..!!!.Mwanafunzi kapewa tunzo ya ufundishaji bora na Mwalimu kawekwa pembeni."Baada ya wote kuzungumza maneno Yale Zamda anaonekana ameshika ndoo ya kuchotea maji hadi akawa ameiachia na kubaki anawasikiliza hao shoga zake.Kisha Kidawa akawa anaendelea kuyatema hayo maneno kwa huyo Zamda".
Watu na degree zao za kuwa na wanaume wengi hawajapata watoto nashangaa wewe sijui uliweka style gani ikajipenyesha tu.Tulikuambia shoga yetu Lakini wewe ukajifanya pembe la tembo kumbe Hamna chochote. Sikiliza ya wahenga wewe.Ila ndiyo hivyo maji yakishamwagika hayazoleki."Ndoto ile ikawa inaendelea Zamda akawa na sura ya kihuzuni palepale kwa maneno ya huyo Kidawa anavyoyatoa Lakini wala huyo Kidawa hatishiwi na hiyo sura ya kihudhuni ya Zamda.Kidawa anasema".
Ulijifanya eti ooooo Mimi siwezichezewa na Kila mwanaume mwanaume. Mbona huyo mmoja kakuchezea na tayari kakupa mimba na mtoto Huyo. Tena huyo si mtoto wa pili."Hapo ndipo Zamda akashangaa kabisaaaaaaa huku akiwa anaongea kimoyomoyo akisema Hivi".
Hawa wanajuaje kwamba Mimi Nina watoto wawili. Kwasababu hata Hiyo mimba ya kwanza tu sikuwahi kuja hapa.Kujifungua sijajifungulia hapa nyumbani kwetu Mimi nimejifungulia sehemu nyingine tu.wamejuaje Hawa."Kidawa akaendelea na maneno yake ya kumchambua Zamda".
Heheeeeeeeeeeeeeeeeee unashangaa nini Sasa Unajua kwamba hatuelewi kuhusiana na gazeti Lako. Hohoooooooooo umeula wa chuya Zamda Yaaani kama ulikuwa unajipa hayo mawazo yatafutie kifutio kikubwa kabisaaaaaaa uyafute Hayo mawazo.Watu tunajua kuanzia gazeti lilipoanzia hadi lilipoishia na hadi mda huu tuko na wewe hapa.Yaani gazeti Lako limesomeka Kweli Kweli kuliko hata ya magazeti mengine huku kwetu.Kwasababu wewe ulijifanya nyooonyoo mwisho wa siku wajanja wa mjini wakakuonesha shooooshooo na hayo ndiyo matokeo ya shoooshooo zile za kujificha.Pole sana shoga Wetu."Mwantumu naye akaingilia baada ya kuona Kidawa kaishiwa na maneno ya kusema. Ilikuwa hivi ".
Ule uzuri wako uko wapi sasa. Angalia Sasa umeruka mkojo na kwenda kukanyaga mavi Kabisaaaaaaa. Duuuuuuuuuuuu wanuka Mbona. Angalia Sasa afadhali huyo jamaa hata angekuwa na uwezo wa kukuoa kumbe naye shombo tu.Yaani mwanamke ulikuwa unawagoganisha hao wanaume hapa mtaani kwelikweli enzi zako Lakini kwasasa hiyo ndiyo kwishiney kabisaaaaaaa.Yaani kila mwanaume alikuja na style yake ya kukutongoza na waliokuwa wakija walikuwa ni wajanja wa mjini watu na hela zao.Lakini wewe ukawa unajifanya unawapangua yaani unawawekea mgomo baridi tu.Sasa ule mgomo baridi dada sijui kwasasa tusemeje.Labda tusubiri tu kama wahenga walivyosema kwamba Ng'ombe hazeeki maini."Lakini kwa pembeni panaonekana pia kuna Bibi anaonekana naye yuko hapo anawasikiliza huyo Kidawa na Mwantumu wanavyombubujikia maneno ya nguoni kwelikweli. Bibi yule Kwakweli aliyavumilia maneno Yale Lakini ikabidi aingilie mada kwakusema Hivi".
Eeeeeeee tuuuuuuuuuuu "Akatema mate ikiashiria kwamba amechukizwa na maneno Yale.Akawa anasema Hivi."Nyiye watoto Nyiye kama wewe ni kuku usimcheke mwenzako akiwa anachinjwa Kwasababu na wewe utapita kwenye hicho hicho kisu.Yawezekana kwanza mchinjaji wa kuku wa kwanza tena alikuwa na roho nzuri. Lakini ikaja kwako ambaye ni kuku wa pili akaja mchinjaji ambaye ni Hana huruma katika Maisha yake.kwanza anaanza kukuchinja na Kisu kibutuuuuuu.Wajukuu zangu msitukane mamba kabla hamja vuka mto.Mnanisikia.....Hivi nyiye mnamtukana mkunga angali mu wazazi mwaja.Afadhali huyu mwenzenu anajua Ana watoto wawili na anajua anakizazi kulikoni nyiye wanasheitwani wakubwa nyiye mliofanya mapenzi kuliko hata wazazi wenu afu mnajisifia kabisa Yaani nyiye ambao kila kona za mtaa wa Kwanza, wa pili,watatu,wanne na hata watano na kuendelea zinawajua.Afadhali mwezenu ni mwanamama kwasasa anajulikana kwamba ana sherehe yake duniani lakini je kwa nyiye mnasherehe gani duniani?.Au siki hizi kuna siku ya makahaba duniani.Labda kama itakuwa imeanzishwa hivi karibuni.Yaani mnaongea kwa kujitapa kabisa na midomo yenu kama kunguru wa pwani kwa wale wala urojo.Nyiye wakati Hamjijui hata kama mna vizazi.Etiiiii kabisaaaaaaa mnajitapa wataalamu wa kuruka fimbo ikitaka kuangusha mate meupe mazito.Wakati mate hayo meupe umeyameza na baadaye ukanywa maji malaini na magumu mengine ya mviringo tayari yakawa yametoa hayo mate meupe ya fimbo ambayo ilikuwa nyeusi Au nyeupe. Nyiyeeeee wajukuu zangu laiti mngejua mama zenu walivyolia siku ile ya kujifungua Basi mngempa pongezi huyu mwanadada mnayemzonga hapa kwamba Ana watoto wawili hata umri wa kufikia watoto wawili haujafika.Yawezekana wewe unayemwambia mwezako kwamba jamaa yake ananuka shombo.Afadhali huyo anajua ananuka shombo ila ni mchumba wake halali iko siku tu maisha yanaweza kumbadilikia na kujikuta shombo zimeenza Kunukia marashi kama hamjaanza kumfuatilia huyo mme wake ili muweze kumchuna vizuri.Sasa kulikoni nyiye ambao mnasema kwamba mna mabahasha wenu huko huko mtaani,mjini Kumbe waume wa watu.Nyoooooooooo....Shwaiiini nyiye hamjui cha mtu mavi.Embu ondokeni hapa hata sitaki kuwaona hapa machoni mwangu.Wanakulaaniwa nyiye.Yaaani mnavyoongea mtafikiri mnajua hata litakalotokea kesho kumbe hata litakalotokea baada sekunde chache zijazo hamjui.
Baada Bibi yule kuwafukuza pale na Zamda naye akaamua kujitwisha ndoa yake na kisha ndoto Hiyo inaonesha Kwamba Zamda Anaonekana anamuaga Bibi yule japokuwa hamjui kabisaa.
Ndoto ile ikawa imeishia pale na Hapo hapo tayari Zamda akawa ameshituka na akatoka kitandani pale kisha akaenda sehemu taa ile ya kuwaka kwa kuchajishwa na nguvu ya jua.Kufika pale mezani akawa amewasha taa ile na akawa amerudi kukaa kitandani pale akiwa amekaa kitako huku akiwa kajifunika shuka lake la bluu.Lakini huku anaonekana anahema kwelikweli kwa ndoto ile aliyokuwa akiiota.Mda huo ikiwa ni usiku wa manani Kabisa Huko nje pamenyamaza kimyaaaaaa na kutulia tuliiiiiiii Yaani hata ukiangusha Sindano Kwakweli unaweza kusikia mlio wa Sauti yake.Kisha akaanza kuongea peke yake
Mama Yangu ndoto gani hii mungu wangu embu niepushie hili balaa nililoliota Lahaula eeeeeeeee mbona kama sielewi. Yaani Nina watoto wawili alafu Mwantumu na Kidawa hawana mtoto hata wakusingiziwa tu.Eeee mungu weeeeeeee niepushie mbali kabisaaaaaaa hili balaa.Yaani kabisa nimepewa mimba na mtu ambaye hata maisha kwake hayafai.Sasa hii ndoto inamaanisha nini."Mda huo anavyoongea hivyo akawa hata anajisahau yuko ndani ambapo chumba kinachofuatia hapo ni chumba ambacho wanalala baba na mama Zamda. Kwahiyo Baba Zamda akawa anasikilizia sauti ile kwa mbali sana ndipo akaja akajua kwamba sauti ile inatoka hapo ndani kwa Zamda. Baada ya baba Zamda kutambua hivyo ndipo akawa anamuamsha mama Zamda kwakusema Hivi ".
Mke wangu.....mke wangu embu inuka."Baba Zamda akiwa anaongea kwa sauti ya chinichini.Mama Zamda akiwa anaonekana yuko katika Bahari ya Usingizi mzito kwelikweli.Akawa ameitika kwakusema Hivi".
Mmmmmh nini mme wangu usiku huu?.
Wewe inuka ndipo utajua ninini usiku huu.
Lakini Jamani mme wangu ."Baada ya kuamka mda huo Zamda bado anaongea huko chumbani kwake. Kisha baba Zamda akawa anamwambia hivi mama Zamda".
Sasa hivi ni kama saa nane na midakika hivi Lakini huko chumbani kwa Zamda huko nasikia sauti kabisaaaaaaa ya mtu akiongea na taa hiyo iko imewashawa."Kisha mama akarukia Mada kwakusema Hivi".
Sidhani kweli.
Hudhani Kitu gani wewe inawezekana huyo Zamda kaingiza mwanaume huko ndani.
Hapana haiwezekani mme wangu Zamda hawezi kufanya hivyo.
Embu mke wangu nenda kamuangalie inawezekana ni janga limemkuta huko alafu sisi tunaanza kujibunia tu hapa.Nenda kamuangalie Neenda."Nakweli mda huo Mama Zamda Anaonekana anainuka Haraka Haraka ili kwenda kumuangalia huyo Zamda.
Siku iliyofuatia ilikuwa ni siku ya Jumamosi Hivi ambapo siku hiyo kwa Zamda na shoga zake huwa hawaendi shuleni. Lakini Zamda ,Mwantumu na Kidawa huwa wanaishi mtaa mmoja.Basi siku Hiyo walienda Kabisa Nyumbani kwa akina Zamda .Ambapo mama na Zamda huwa naye anajishughulisha na shughuli za kijungu Jiko tu huko mjini Kwahiyo kwanzia asubuhi hadi Jioni huwa hapatikani nyumbani na hata baba Zamda pia anajishughulisha na vishughuli vidogovidogo tu huko mjini.
Basi wakiwa wamekaa hapo nje maongezi yao yalikuwa hivi.
Maamuzi ni ya kawaida tu.Kwakweli Kidawa na Mwantumu huo ushauri wenu sidhani kama utanifaa."Kisha Kidawa akasema Hivi ".
Yaani tuseme Jana tulifanya kazi bureeeee Kabisaaaaaaa. Umeona sisi kwamba ushauri wetu wala haufai kuandikika. haya."Mwantumu naye akasema Hivi".
Sawa Basi wewe fuata huo wa mama yako na wewe hujui sijui na mama yako naye kipindi kama hiki alikuwaje."Zamda akawajibu Hivi".
Sawasawa haina shida acha tu nibaki mjinga mjinga tu Hivi Hivi.
Baada ya Kidawa na Mwantumu kuona kwamba huyo Zamda haelekei katika mstari wao wakawa wameamua kuondoka nyumbani kwao.
Lakini baada ya miezi kuzidi kwenda zaidi na tabia za Zamda kidogo nazo uvumilivu ulianza kufikia ukingoni. Ambapo kipindi hicho bado kama mwezi mmoja wafanye Mtihani wa Taifa wa kidato cha pili.
Siku hiyo ikiwa ni mishale ya saa sita za Usiku sehemu fulani katika club fulani Hivi iliyoko katikati ya jiji Mda huo Kidawa na Mwantumu wakiwa nao wanaingia ili watafute eneo maalumu la kujikita.Lakini kwa mbali Kidawa anaona kama vile sura ya Zamda ila haamini ni kama ni Zamda kweli au kama vile ni changa la la macho.Kwahiyo wakaamua wanyooshe njia moja kwa moja hadi hapo wanapomuona huyo Zamda baada ya Kidawa kumshitua Mwantumu kwamba kama ile sura wanaijua.
Kidawa na Mwantumu Kwakweli walivyovaa ni mithili ya wanadada wanaotaka kwenda kuigiza nyimbo fulani ya mahadhi ya kimagharibi.Huyo Mwantumu kutokana na kaurefu fulani alikojaaliwa ndiyo haswaa akawa anaonekana kama vile mzungu ukichanganya na weupe wake Fulani hivi. Kavaa kinguo ambacho kimefunika huko Nyumba tu Lakini huku Mbele ya uke wake kama vile kimetobolewa tobolewa Fulani hivi na kikiwa ni kifupi Kweli Kweli. Kiatu cha bei ghali.
Posted by: MwlMaeda - 08-19-2021, 09:01 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU
MWANDISHI: Saidi Kaita
SEHEMU YA 01
Ni saa moja Jioni mda huo wakionekana mama na mwanaye aitwaye Zamda.Sehemu waliyokaa ilikuwa ni Jikoni wakiwa wanafanya Maandilizi ya chakula cha usiku.Jikoni hapo chakula ambacho kilikuwa kimebandika na kufunikiwa haki ilikuwa ni wali ambao ndio ulikuwa umedhamiriwa kuliwa usiku ule..Zamda kwa umri wake ndiyo ulikuwa ni umri wa tayari kufikia kuvunja ungo.Tangu akiwa mdogo ni mwana ambaye Kwakweli ambaye amejaaliwa uzuri ambao Kwakweli ni mungu amemjaalia.Basi mda huo mama Zamda akawa na maongezi kidogo na mwanaye Wakati wakiwa wanangojea wali uweze kuiva.Mda huo Mama Zamda akiwa amekalia kiti aina kigoda naye Zamda akiwa amekalia kigoda. Taa iliyokuwa ikiwapatia mwanga hapo jikoni ilikuwa ni taa ya kuchajisha kwa kutumia mwanga wa jua Yaani Solar Power.Hivyo basi mazungumzo yalikuwa yanajikita sana katika suala la huyo Zamda kuvunja ungo.Kwahiyo mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo.
Mwanangu Zamda ndiyo hivyo umeshakua. Utoto umekutoka na kwasasa umeingia kwenye usichana.Ambapo utoto huo ulikuwepo ni Kwasababu ya ukuzi wa mola namna ulivyo. Na kwasasa ndiyo Hivyo umeshakuwa katika makuzi mengine tena Yaani baada kuvunja ungo.Kuvunja ungo ndiyo mwanzo wa kuanza kuweza kujielewa Sasa ni tabia gani wewe kama msichana utakayokuwa nayo.Kwakweli mwangu kati ya watoto wangu ambao wananikosha roho yangu ambao kwaujumla nawategemea watakuja kniondoa katika haya maisha mabovu tunayoyaishi ni wewe.Najua iko siku na mimi ntaitwa mama mke na mtu ambaye anamiliki migari hiyooo.Yote hiyo ni kwasababu tu ya wewe mwanangu Zamda.Kwakweki mwanangu kwa uzuri umejaaliwa hadi natamani ningekuwa na hela ningeeajiri hata askari awe anakulinda tu na huyo askari awe ni askari wa kike mwenye nguvu ya kukulinda kwelikweli.Ila tatizo ndilo hilo sasa sisi mahoehae mungu ndicho alichotujaalia.Sawa Uzuri ndiyo huo umejaaliwa mwanangu ila Sasa Angalia Miluzi mingi humchanganya Mbwa. ""Zamda akiwa anamsikiliza kwa makini mama yake ilibidi amuulize swali kidogo kwa msemo ambao ameusikia kutoka kwa Mama yake.Alimuuliza hivi""
Mama Unamaanisha nini unaposema Miluzi mingi humchanganya Mbwa?."Alimuuliza kwa sauti ya chini iliyojaa aibu fulani kwa heshima anayompa mama yake.Mama akawa anamjibu kama ifuatavyo ".
Aaaaa....mwanangu japokuwa waswahili husema kwamba usimwambie mtu maana ya kitu fulani maana baada ya kumwambia maana hiyo tu atakuona hauna maana yoyote. Lakini kwa wewe kwa vile ni mwanangu hivyo basi nakupenda na pia nakutakia Maisha ambayo Kwakweli hata nikifa usiku wa leo hii maneno yangu haya yatakuwa yakisikika masikioni mwako.Macho yako yatakuwa yanavuta taswira ya namna tulivyokaa na taa yetu hapa.Nimesema kwamba Miluzi mingi humchanganya Mbwa mwanagu nikiwa namaanisha Kwamba"mda huo mama Zamda akawa amemgusa Zamda kwa Mkono wake wa kulia na Zamda akawa ametikisa kichwa chake akimaanisha ameetikia kisha mama Zamda akaendelea kusema Hivi".Siku zote mbwa anapokutana na watu katika njia aliyopita na njia hiyo ikawa ni njia ambayo imejaa watu wengi kila mtu anahulka yake.Basi wanaweza kila mtu akaanza kupiga mluzi wake kwa namna na madhumuni yake.Kuna ambao watapiga Miluzi kama vile wakipuliza Nai ,Wengine ndiyo hivyo kama sauti za chura wakiwa kati urojo wa maji asubuhi Au usiku ile wanatoa sauti zake.Lakini kuna wengine Nai watapiga hata makelele tu hata kama hawawezi kupuliza huo Mluzi.Lakini Mbwa Huyo mda huo Yeye hata jua kwamba haya ni makelele Au laa Bali atajua ni Miluzi ya watu wanaomtamani kumpiga .Basi mda huo Miluzi ile hupenya moja kwa moja hadi ndani ya masikio yake na kujikuta mbwa huyo anashindwa ni wapi pakuelekea.kinachomkuta hapo anaenda huku anarudi kule na huku tena mwisho wa siku kizunguzungu kinaweza hata kumpata.Basi hapo kumpiga Mbwa huyo ni kiurahisi sana...Sasa tena sana na kujikuta kaumia tayari."Zamda ikambidi aulize swali kwakuona maelezo ambayo mama yake anampa Kwakweli kama yana ukakasi kwake kidogo. Alimuuliza hivi ".
Sawa mama kidogo kama nakuelewa ila panaponishinda kuelewa ni kwamba kuna uhusiano gani kati ya Miluzi mingi humchanganya Mbwa na kuhusiana na Mimi kuvunja ungo?.Kwasababu... Sababu nahisi kama vile kidogo hapo sijakupata vizuri.Yaani nahisi ni kama Unataka kufananisha Biskuti na mkate ....mhhh sielewi mama Hapo.
Ni Kweli ni vigumu kuweza kunielewa kwa Haraka Bali yatakikana tafakuri kidogo ambapo Tafakuri hizo zitasindikizwa na maelekezo yangu ambayo nataka nikupatie.Ni kwamba mwanangu huyo Mbwa nimekutolea mfano wewe hapo japokuwa si kwamba wewe ni mbwa kweli."Zamda akacheka kwa sauti yake ya madaha kisha Mama Zamda akawa anaendelea na maongezi.""Yaani wewe kwasasa utakuwa ni mtu ambaye Kweli ukipita katika kundi fulani la wavulana kila mtu ataanza kukutamani na si kukupenda na siku zote mwanaume huanza kumtamani msichana na ndipo kama ni kumpenda ndipo ataanza kumpenda baada ya kukutana nae Mara kadhaa hivi.Sijui kama wanisikiiliza mwanangu kwa umakini?."Mda huo anapomuuliza hivyo akawa amemsogezea uso wake huku Mkono wake wa kulia tena akiwa anamshika Zamda kwa kuonesha usisitizaji fulani kwa mada anayoizungumzia. Zamda akasema Hivi"".
Mama nakusikiliza kwa makini Sana.
Hayaa nisikilize kwelikweli kwa makini.Mwanangu hii ndiyo dunia ya kipindi ya kizazi cha nyoka. Kwahiyo upitapo sehemu ambayo patakuwa na kundi la wavulana kila mvulana anaweza kukumezea mate tu na baada ya mda kila mtu ataanza Sasa kukutafuta kwa mda wake na hapo Sasa kila mtu huja na mluzi wake.Atafanya afanyavyo hadi mwisho wa siku utajikuta mluzi ule umekuchang'anya na kuanza kuukubali kwa asilimia mia moja kabisaaaaaaa na hata asilimia elfu moja inawezekana.Lakini baada ya hapo tena kesho pakikucha wataanza kuhadisiana huko magengeni utashangaa na mapema mwingine tena anakuja anaaza kukupulizia mluzi weeeeeeee kwa namna yake mwisho wa siku unaanza kuona Au unaanza kufananisha mluzi wa kwanza na mluzi wa pili upi umezidi.Kifuatacho kwa tamaa zako utajikuta waangukia kwenye mluzi wa pili.Hivyo hivyo mwisho wa siku unajikuta Miluzi imezidi na baada ya hapo wote waliokuwa wakikupigia Miluzi wakishajua wewe Ndiyo tayari huna muelekeo Kwasababu kule ukipigiwa Mluzi na mtu fulani waenda tu.Hapo Sasa wajikuta gazeti linachanika na wanunuzi na wasomaji hawana tena mda na hilo gazeti Ambalo lilikuwa likibamba Kweli Kweli likisema kwamba Zamda mashaalah Yaani hapo Ndiyo wewe sasa mwanangu hapo unakuta kila kona hawana hamu na wewe.Kwaujumla gazeti likishalowana hapo Kwakweli hata kama lilikuwa na mataarifa ya udaku chungu mzima wala hakuna anakayeanza kwenda kujihangaisha kununua vipande vya gazeti Hilo lililochanika kwa mvua iliyolinyeshea gazeti Hilo. Sijui kama wanipata Mwanangu?.
Fuuuuuuuuuuuuuuuuuu."Zamda akahema utafikiri kajitua mzigo fulani ambao ni mzito kwelikweli kwa maneno machache mama yake anayompatia Kisha akasema Hivi ". Kwahiyo mama Kwasababu mama Kwahiyo kukua Shida Tena?.
Mwanangu Hilo ni Jambo Ambalo Kwakweli linalohiitaji kalamu ya kupigia msitari kabisa mmoja mnyoofu kabisaaaaaaa.Kukua nako ni mungu katujaalia sisi waja wake ili tuwe tunakuwa ni maelezo ya vipindi mbalimbali. Yaani kuna kipindi ulikuwa na mwaka sifuri hadi ukifikia miaka mitano,baada Hapo ukafikia hadi miaka kumi na Sasa hadi leo hii Angalia umri wako.Kila kipindi cha umri wako kinakuwa na matukio ambayo yanawezakuwa mengine ni ya kufurahisha Au ya kuhuzunisha. Alafu mwanangu ukichanganya na huu umasikini tuliokuwa nao Kwakweli hapa nyumbani usijeukakufanya mwanangu kuanza kutaka kupata Hela za kujiremba kwakuuza mwili wako.
Sawasawa mama sitofanya hivyo nakuahidi.
Yaani mwanangu kwa hatua uliyofikia hii Kwakweli ni hatua ambayo kwa Mimi naona kama ni hatua ya kuhitaji kutumia akili sana.Kwasababu mwanangu kwasasa ndiyo upo hicho kidato cha pili na hao wanaume nao siku hizi wanawapenda wasichana ambao ni wanafunzi Kweli Kweli. Unashangaa dereva tax kajitokeza huyu sijui wa gari fulani kajitokeza sasa hapo Utakuja kujuta pindi wameshakujua namna mwili wako ulivyo hapo hawatokuwa na hamu na mwingine. Mwanangu sura yako isijeikakufanya unaharibu maisha yako.Kwasababu kwa dunia ya Sasa Jamani kuna magonjwa mengi sana ambayo Kwakweli ukilipata tu hilo gonjwa na ujue kabisaaaaaaa Wewe maisha yako hapo yameshaanza utata tena utata mkubwa sana na mwisho wa siku hadi utashangaa na hadi Ndugu wanakutenga.
Ugonjwa gani huo mama ambao hata ndugu wanafikia kujitenga?.
Ohooooo!!!?. Mwanangu watakutenga na watakutenga kweli kweli na mwisho wa siku majungu tu huko mtaani.Ugonjwa huo moja ya ugonjwa ambao ni mbaya kabisaaaaaaa ni huu Ugonjwa wa UKIMWI Yaani mwanangu hapo ukifikia Yaani ni bora hata kupata mimba itajulikana ni namna gani ya kuitoa Au laa ila kwa Hilo gonjwa hapo Kwakweli ni hadi kufa kwako.Kwahiyo ndiyo maana nakuasa sana tangia mwanzoni kwamba mwanangu usitamani Hela ya mtu kwakutegemea kwamba mwili wako ndiyo duka kwamba una bidhaa adimu Sana Lahashaa.Kwasababu mwisho wa siku kama ni bidhaa watanunua na watakuja kuanza kuona kwamba bidhaa zako zimeshapitwa na Wakati tayari.
Sawa mama nimekusikiliza kwa makini sana nanikuahidi mama kuwa sintokuangusha.
Sawasawa ila Chamsingi kama ni maneno yangu nimeshayaongea mda huu hata nikifa leo usiku najua kuna maneno kabisaaaaaaa nilimwachia mwanangu.Basi Sawa embu tufanye kuaandaa Mambo ya chakula naona kama chakula tayari.Kwasababu huyo Baba yako anarudi mda si mrefu kutoka huko msikitini.."mda huo mama Zamda akiwa anaonekana akiwa anakiepua chakula kilichoko jikoni kwakutaka kujua kama kipo tayari"".
Basi ikiwa ni siku iliyofuatia mwanadada Zamda akiwa na rafiki zake wawili ambao Kwakweli huwa anapendana nao kwelikweli. Hao ndiyo marafiki zake wa shuleni.mda huo wakionekana wakiwa ndiyo wanatoka shuleni wakiwa wamevalia sare zao za shule kwa siketi walizokuwa wamevaa ni za rangi ya bluu na mashati kola zao zikiwa zinaonekana ni nyeupe na masweta yakiwa ni ya bluu na chini wakiwa wamevaa viatu vya mwisho saa sita.Basi mda huo nao wakiwa wanaelekea Nyumbani maongezi ya hapa na pale hawayakosi ikiwa ni pamoja na utani ambao Kwakweli uliwafanya wenyewe wawe wanafika nyumbani kwa Haraka sana.Basi mda huo rafiki zake hao mmoja anaitwa Mwantumu na mwingine anaitwa kidawa.Basi mda huo aliyekuwa ameshika Jahazi la kuongea alikuwa ni Zamda. Maongezi yao yalikuwa hivi.
Yaani Kidawa duuu Jana mama kaongea na Mimi kwelikweli hadi nikawa nahisi kweli Sasa kukua shida sijui ni sawasawa na kujitwisha Zigo la chawa Yaani hapo lazima kujikuna kila kona."Mda huo anaongea hivyo hadi akawa anashika kiuno chake ili ainogeshe stori vizuri. Kisha kidogo Kidawa akawa anaingilia mada akiwa anasema ".
Huyo mama yako alikuambia nini Hiyo Jana?."Wote mwendo wakiwa wanatembea mwendo wa Bi Arusi kisha huku Zamda akawa anasema Hivi".
Yaani shoga WANGU huyo mama kanichachia kweli kweli kuhusiana na Mimi kuvunja ungo. Yaani Hayo maneno ya kiutu ukubwa alivyokuwa akiniambia Yaani sijui tu nisemeje."Mwantumu akawa amedakia mada na kisha akamuuliza Zamda hivi".
Heee Zamda maneno gani tena Hayo ya kiutu ukubwa wasema .Embu tuambie.
Nakwambia oooo anasema kwamba nijitunze sana kwamba si kila mwanaume akija kunitongoza nimkubalie mwisho wa siku watakuja kuniona kama kopo la maziwa ukishakunywa kopo Hilo thamani yake inashuka kabisaaaaaaa.." kisha Kidawa akarukia maneno ya Zamda kwakusema Hivi ".
Wala hamna cha wakukutema wala nini.Mtoto umejaaliwa umbo Hilo .....mmh..eti....mmh afu wataka kuishi maisha ya kimaskini kwa ubaya gani ulio nao.kuna wenzako wamejaaliwa sura tu Lakini huko nyuma wala.embu check wewe kila mahali Mtoto mashaallah."Kidawa anavyoongea huku kashika kiunio na mwendo kuupunguza ili ampe Zamda vizuri maneno".Yaani kama ndiyo mama yangu ile mwanzoni aliongea Kweli Kweli Kuhusu Mimi kuvunja ungo kuvunja ungo. Wacha weeeee....hayo maneno nakwambia aliyokuwa akinipa utafikiri niko kwenye kicheni part vile kumbe ni mama." mwantumu naye akaunga Mkono kuhusiana na Ushauri wa Kidawa kwa Zamda kwakusema Hivi ".
Kweli Kidawa Mimi mwenyewe mama yangu ananijua nilivyo Yaani Kwaujumla tunajuana naye yaani kila mtu analijua daftari la mwenzake.Mama ile mwanzoni tu Ndiyo Hivyo aliniambiaga tu Mwantumu umeshakuwa karibu ukubwani yanini maneno mengi kama vile wahutubia dunia."Wote walicheka kwa maneno anayoyaongea huyo Mwantumu kwakugonga mikono huku kicheko wakiwa wamenogesha Kwakweli kama vile watu wakubwa kumbe visima vyao ndiyo vimeanzwa kuogelewa na visima vingine ndiyo vinaanza kutafutiwa ni namna gani ya kwenda kuviogelea baada ya kujua ni kisima cha maji ya moto Au ya baridi.Kisha Zamda naye akaamua la kusema".
Mmh....jamani shoga zangu mnavyonitamanisha Yaani ....Yaani sijui nifanyaje tu."Kidawa akarukia mada kwakusema Hivi".
Heeeee wewe nawe ufanyeje wakati kitu kinajulikana hiki ni jambo moja tu la kufanya. "Akiwa anaongea huku akimgusa Zamda".wewe Pale shuleni vile viwalimu usivione tu pale tunavila Hela zao kwelikweli.Wewe unakaje kizembezembe hivyo Wakati una bidhaa asili japokuwa kila msichana anayo Lakini utofauti kwa mwanzoni lazima uwepo."Zamda akamuuliza Kidawa swali hili".
Zamda hilo ndilo swali kweli. Haya tulia nikujibu kama ifuatavyo. Zamda wewe jiangalie umbo lako kwanza lilivyo afu unasema tawalipa nini.unajifanya unaenda ofisini Lakini huku unatarget zako.afu Sasa haya masketi marefu usiyavaevae sana utakuwa hata hauonekani kama umekuwa shoga wangu. Mbona maisha simple tu.kweli Nyumbani kwetu hawawezikunipa hata hiyo Hela ya bagia afu tena nishindwe kujiongeza Mimi mwenyewe hapa msichana niliyekuwa.Wewe hata huoni tu Zamda sisi na wewe hatufanani wewe uko vizuri kwa umbo ila hauvai vizuri Lakini japokuwa na sisi hatujajaaliwa sana kama wewe Lakini twavaa kisister duuu kwa Sana. Badilika wewe umeshakuwa shoga wangu."Mwantumu naye akaamua kuchangia mada anaongea huku kasimama kajishika kiuno huku akimkodolea macho huyo Zamda.Ilikuwa hivi."
Mimi nikwambie kitu Zamda ushawahi kusikia watu Wanasema kwamba ujana maji ya moto?."Zamda akaitikia kwa kusema ."
Ndiyo nishawahi kusikia ila maana yake halisi sijaipata na sielewi vizuri sana."Kisha Mwantumu akasema Hivi ".
Ahaaaaa kumbe hujui maana yake Basi ndiyo maana unakuwa kama ni mgumu hivi kwenye kuelewa tunachokupanga Hapa. iko hivi tusemapo ujana maji ya moto kwamba kwa umri huu ulionao shoga wangu huu ndiyo umri wakusema kwamba una maji ya moto. Sasa ngojea hayo maji yaje kuwa ya vuguvugu Au baridi haswaaaa Sasa utakuja kujikuta wanaume na wewe ni kama msikiti na mbwa watakavyokuwa wanapita mbali kabisaaaaaaa. Ila kwasasa damu yako bado ni damu ya moto Basi patakuwa ni kama kidonda na nzi haviachani.Tumia ulichojaaliwa wewe."Kisha Zamda ikabidi naye awajibu kwa madaha kwakusema Hivi".
Afu nyiye mashoga zangu msijemkawa mnanisifia tu umbo umbo tu kumbe hata sina nije nianze kujisikia kumbe wala Sina."Mwantumu na Kidawa walicheka kwakusema".
Heheeeeeeeeeeeeeeeeee " Kisha Kidawa akaongea jambo baada ya kucheka kicheko kitamu kwel kweli hadi wanagonga na shoga yake Mwantumu ". Amakweli kuna mtu unamkuta analalia kitanda cha Kamba na kunguni wanamsumbua Lakini hapo chini ya ardhi yake kuna dhahabu za kutosha. wasamaria wema wanakuambia unadhabu hapo Lakini bado tu hujiamini. Nini Sasa Wakati sisi Ndiyo wataalamu tunajua kwamba vitu kama hivi vya kwako mjini vinauza Kweli Kweli. Nenda na Wakati weeeeee shoga wangu ushakuwa. Yaani Sasa hivi hata ukiwa unamsalimia kijana ukishamuona anaharufu ya vihela vihela Basi tumia ujanja wa kumsalimia na si kila kijana wa kiume anasalimiwa kama unavyomsalimu mama yako Au baba yako.Msalimie kwa mtego.Shoga WANGU Angalia utakuwa unalala njaa na unavaa manguo ya kishamba Shamba tu hapa kumbe kuna Mali unatembea nayo kweli kweli. Kwahiyo shoga yangu Eee Mimi sikundanganyi Kwakweli umejaaliwa Kwahiyo utumie mwili wako vizuri sana hadi utakupatia Fedha.Wewe Zamda mwanzoni Mimi siulikuwa unanionaga navaa manguo Yaani utafikiri naenda kupalilia mahindi afu utafikiri Yaani sijui kama mtu fulani ambaye ni kama kichaa tu.Nikaja kulitambua Hilo jambo kumbe hapa mjini akili na uswahili unahitaji ukishakuwa.Nibaada ya kukalishwa na wataalamu ambao ni maprofessional wamichuno kwa wakaka wale ambao nao wanajifanya fanya kwamba wanahela alafu hawajui namna ya kuzitumia.Yaani baada ya kupita kama wiki moja tu Hivi shoga yangu mbona Hadi maprofessional wamichuno kwa wakaka walinipa saluti. Sasa ndiyo nakushangaa Wewe Hapa. Isijeikiwa tunapigia mbuzi gitaa hapa."Mwantumu naye akamwambia hivi ".
Shoga wangu nikwambie tu kitu sisi ni rafiki zako wakaribu kweli kweli. Kwahiyo unaoona tunakusifia hatukusifii kiunafikinafiki tu hapa. Hapa mjini wewe."Kisha Zamda akawajibu hivi".
Haya shoga zangu acha Mimi niende Nyumbani huyo mama atakuwa ananisubiri kwelikweli niende mtoni.
Hayaaa shogàaaa "Wakajibu kwa pamoja Yaani Kidawa na Mwantumu".
Kwakweli usiku wa siku ile kwa Zamda hata hakusoma Bali akawa anakesha tu akiwa anayachuja mawazo Yaani afuate mawazo ya mama ambayo anajua uchungu wa mwana kwa namna alivyomzaa ai afuate Ushauri wa mashoga zake ambao ni Zamda na Mwantumu.
Posted by: MwlMaeda - 08-19-2021, 08:56 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
…SEHEMU YA 15…
Msitu wa mikoko:7:00am
Msafara wa magari hamsini ya kikoloni uliwasili msitu wa mikoko, gari la kwanza likiwa na jenerali wa jeshi la kichina aliyeitwa Liang Xung,alikuwa ameketi viti vya nyuma, ndani ya gari,mbele yake alikuwa ameketi gavana Richald Robeni, pamoja na mlinzi wake ambaye alikuwa akiendesha gari.
“,Tumefika, msitu ndiyo huu! “,mlinzi wa gavana Richald Robeni aliongea, akasimamisha gari lake,akageuza shingo nyuma,palepale akapigwa na risasi, akafa palepale.
“,Mikono juu! “,gavana wa kichina aliongea, alikuwa amemnyoshea bastola kichwani gavana wa kiingereza, Richald Robeni na yeye alipitia mafunzo ya kijeshi, akataka kuchukua bastola yake lakini alionekana.
“,Nitakumaliza kama nilivyomfanya mwenzako, usisubutu kuweka mikono yako mfukoni! “,jenerali wa kichina aliongea, akamtoa nje, akiwa amempiga roba na kumuwekea bastola kichwani.
“,Wamemkamata gavana yetu, wanataka kufanya mapinduzi na kuchukua koloni letu,tupambane, lets fight ……”,jeshi la waingereza walisikia mlio wa risasi ndani ya gari lililokuwa na gavana wao, wakashuka kwenye magari yao, kabla hawajalisogelea gari, gavana wao akatoka nje akiwa chini ya ulinzi, wakakasilika, makundi yote mawili yakanyosheana silaha,jeshi la kichina pamoja na jeshi la wenyeji ambao ni wazungu wa kiingereza.
“,Mkifanya lolote nammaliza kiongozi wenu! “,kiongozi wa kichina alizungumza, akaamua kubadili mbinu, jeshi la waingereza walikuwa ni wengi, akaamua kuchukua utawala mapema sana kabla ya kwenda kupigana na Waafrika.
“,Put downs your guns! (Wekeni silaha zenu chini …)”,jenerali Liang Xung aliongea, jeshi la waingereza wakagoma kuweka silaha chini, kwa sasa makundi yote yalikuwa yametengana, jeshi la waingereza walikuwa wamesimama upande wa kusini, wakati jeshi la wachina wakiwa wamesimama upande wa kaskazini.
“,Put down your guns , mnataka niuwawe! “,gavana Richald Robeni akafanya kosa lingine tena, likaugharimu utawala wake, alitoa amli, vijana wake wakaitii kwa shingo upande, wakaweka silaha zao chini, askari takribani kumi wa kichina wakakusanya silaha zote za waingereza, wakaziweka upande wao.
“,Fireeee them, waueee! “,jenerali wa kichina alitoa amli kwa jeshi lake, alikuwa katili kama gavana wake.
“,Paaaa,papapa,paaaa,paaaa! !”,jeshi la waingereza walishambuliwa na risasi,wakafa kama nzige, hawakuwa na uwezo wa kujitetea, walijuta kusalamisha silaha zao.
“,Paaaaaa! “,gavana Richald Robeni na yeye akasambaratishwa ubongo wake, akafa palepale.
“,Yeeeeee! Goshani is our kingdom!(Goshani ni ufalme wetu) “,askari wa kichina walishangilia,koloni la nchi ya Goshani lilikuwa mikononi mwao,vita iliyokuwa imebakia ilikuwa dhidi ya jeshi la Waafrika, vita ambayo waliiona ni rahisi kuliko vita yoyote ile ambayo walikuwa wamepigana,jenerali wao alikuwa amesimama mbele, msururu mrefu wa askari ukamfuata kwa nyuma, macho yao yalitazama mita mia moja mbele, kulia, kushoto na juu ya miti, walikuwa makini sana tofauti na jeshi la waingereza.
Msitu ulikuwa mnene, ulijaa vichaka kila kona, ulitisha, jenerali Liang Xung machale yakamcheza,akaogopa kutangulia mbele,akatanguliza vijana wake kumi, yeye akakaa katikati, msafara ukaendelea.
…………………………………
Jeshi la Waafrika walishtuka usingizini, milio ya risasi iliwashtua sana, kila mmoja akachukua bunduki yake, akaikoki, akajiandaa kufanya shambulio.
Umbali wa mita kadhaa walianza kusikia kelele za watu, Angel akasogeza sikio lake juu ya ardhi, ardhi ilikuwa inatetemeka,wote wakatazama juu, makundi ya ndege yalikuwa yanahama kutoka mwanzo wa msitu, kuja katikati ya msitu.
“,Wanakujaa, jiandaenii, nikitoa amri, shambulia adui! “,Angel aliongea, baada ya dakika tano,jeshi la kichina lilikuwa mbele yao, sare zao zilikuwa na rangi nyeupe pamoja na madoa mekundu, walifanana kwa kila kitu,jeshi la Waafrika wakapigwa na butwaa, askari waliokuwa mbele yao hawakutambua walitokea wapi.
“,Yaaaaala…aa, nakufa…aa …”,
“,Paaa,paaa,paaa!”,
Askari wa kichina waliokuwa wametangulia mbele walidumbukia ndani ya shimo la mtego,wakachomwa chomwa na miti iliyochongoka ndani ya shimo,wakafa palepale,walikuwa askari kumi,jeshi la kichina wakapiga risasi hovyo,waafrika wakalala chini,alimanusura ziwapate vichakani.
“,Ni mtego! wamekufa kikatili, shiit! “,jenerali alishangaa sana, kama si machale kumcheza na kurudi nyuma, angekuwa miongoni mwa askari waliopoteza maisha.
“,Let’s go on, tuendelee na safari but you have to be careful, muwe makini sana! “,jenerali Liang Xung aliongea,msafara ukaendelea, yeye akiwa amesimama katikati, walipiga hatu mbili tu,shambulio lingine likafanyika.
“,Puuuuuu! “,askari mmoja aliyekuwa ametangulia mbele alijikwaa kwenye kamba ya mtego akajitupa mweleka, gogo likatoka juu na kumpiga tumboni, damu zikamtoka mapuani, mdomoni na masikioni, alikufa palepale. Jeshi la kichina likaogopa, likarudi nyuma, wote wakaogopa kusonga mbele.
“,Songa mbelee, tumewauaa askari wa kingereza pamoja na gavana wao, hawa weusi ndiyo watushindee?, let’s move on, songa mbelee! “,jenerali wa kichina aliwafokea vijana wake, kila mmoja aliogopa kutangulia mbele, Angel alikasirika sana, baada ya kusikia baba yake ameuawa, japo hakuelewana na baba yake, lakini alikuwa bado anampendaa.
“,Fireeee them,fireee, piga risasi, shambuliaaa! “,alitoa amli kwa hasira, akarusha bomu lake dogo ambalo lilikuwa mkononi mwake
“,Puuuuuu ,puuu”,lililipuka na kuuwa askari wa kichina kumi na tano, miili yao ikiwa imekatika vibaya sana, kila kiungo mahala pake.
“,Paaaaa, paaaa, paaaa, paaa! “,Waafrika walifanya shambulio la ghafla,wakaua askari hamsini wa kichina, wakabaki askari thelathini na tano, wakafyatua tena risasi zikagoma, risasi zilikuwa zimeisha kwenye magazini za bunduki zao, hapo ndipo mwisho wao ulikuwa umefika, walikuwa hawana silaha nyingine yoyote, isipokuwa Ishimwe aliyekuwa na upinde wake pembeni, akauchukua na kuanza kufyatua.
“,Pyuuuuu! “,Ishimwe alifyatua mshale, alimanusura umpige shingoni jenerali wa kichina, akatazama mahali mshale ulipotokea, akapiga risasi hovyo, askari wote waliobakia wakasambaratisha vichaka na risasi,vikawaka moto.
“,Puuu, puuuuu! “,mlipuko ulisikika, askari wa kichina walilusha mabomu mawili vichakani, Angel akapigwa na bomu, akafa palepale, Mwamvua akafa palepale, Ishimwe na Mpuzu wakajisalamisha, wakanyosha mikono juu, walikuwa wamebaki wawili tu, machozi yaliwatoka,ndugu zao walikuwa wamekufa kikatili,walipigwa na bomu, kila kiungo kilikuwa mahali pake.
“,bhanetuuu bhafwaaa, bhanetuuu bhafwaaa, bhagabho bhachuu bhafwaaa! “,(watoto zetu wamekufaa, waume zetu wamekufaaa! “,Waafrika, wanawake, wazee na watoto waliokuwa juu ya miti walilia, jeshi la kichina likasikia kelele zao juu ya mti mkubwa wa ubuyu, askari wakapanda juu ya mti, wakawatoa Waafrika wote, wote wakawekwa chini ya ulinzi,safari ya kutoka msituni ikaanza,Waafrika wakiwa na majonzi,kwa sasa walikuwa chini ya uongozi wa Wachina.
…………………………………
Gavana Hwang lee alifika nchini Goshani ,alifurahishwa na taarifa za ushindi,jeshi lake lilimchukia,aliwatesa na kuwaua askari wake mara kwa mara,kwa kosa dogo tu,walimpania muda mrefu kumuua.
“,Paaaaaa,paaa!”,risasi mbili zilifyatuliwa, moja ilimpiga gavana,nyingine akapigwa kichwani mlinzi wake ,wote wakiwa wanashuka kwenye helikopta kuikanyaga ngome kubwa(great fort), ardhi ya nchi ya Goshani
“,Yeeeeee!aim your governer,now and onwards!”,(mimi ni gavana wenu,sasa na kuendelea)”, jenerali Liang Xung alipiga kelele za shangwe,alikuwa amekamilisha mauaji,askari wake wakamkimbilia na kumnyenyua,walimpenda sana,akawa gavana mpya wa Goshani pamoja na Gano,yaani ni kisasi juu ya kisasi.
…MWISHO…
Mpuzu na Ishimwe walipatiwa vyeo jeshini,baadaye wakapigania uhuru,wakashinda,Mpuzu akawa raisi,Ishimwe akawa waziri mkuu,wote walikuwa wazee,Gavana Liang Xung alizaa na mwanamke wa Kiafrika,wakapata Mtoto anaitwa Yuan Liang,Wachina walipofukuzwa Goshani,akarudi china na kuacha mtoto pamoja na mke wake,Yuan liang akawa yatima,soma Yuan Liang ujue mengi zaidii!
HADITHI HII NI MALI YA HAKIKA JONATHAN,PAKUA HAKIKA JINATHAN APP PLAYSTORE,AU TEMBELEA www.hakikajonathan.co.tz kwa burudani motomoto
Posted by: MwlMaeda - 08-19-2021, 07:37 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
Pazia la maisha yake muda wote lilikuwa wazi kila aliyepita aliyaona maisha yake, maisha ambayo hayakuwa na usiku wala mchana, kwake hakika alijiona yeye si wa thamani zaidi na zaidi alisema kuwa bora angelifariki angali mdogo labda asingelikumbana na shida zote zile zilizomkumba sasa tofauti na umri wake aliofikia, sasa alipata kuwa na takribani miaka 19 hakuwa na imani kwamba atafika aendapo kwani safari yake ya maisha muda wote aligandwa na kutembea na umaskini kama kivuli cha umbo lake la mwili. Muda wote alitembea nao hakika hapakuwa na mzani unaoweza kupima uzito wa matatizo yake, siku zote kwenye maisha yake alikuwa anasubiri ile kauli ya kulala hali ya kuwa ni maskini na kuamka akiwa tajiri ifike kwake na kila alipojaribu kujitua mzigo uliomwelemea alishindwa kwani mzigo alioubeba ulikuwa mzito sana na hakika hapakuwa na wa kumsaidia kumtua mzigo ule.
Kila aliyekutana naye alimhisi kuwa yeye ni chizi au kichaa fulani maana nywele zake zilikuwa sawia kabisa na rangi ya udongo ulio mwekundu tena zilizosokotana na kukamatana kama mkanda uliofungwa barabara kwenye suruali. Machozi kwenye mashavu yake yalizoea kuchirizika na mara zote alikuwa akijiuliza maswali mengi sana na kufikiria juu yaje, ina maana Mungu amenisahau kabisa? Na kama hajajisahau juu yangu je lini ataninolea kisu changu name nianze kula nyama kama ilivyo kwa wengine. Kwa hakika alikosa jibu. Mara zote alikuwa akikumbuka ile siku alipojiwa na mtu ambaye alizungumza kwa sauti ya chini kabisa na kumwambia siku moja lazima ubadili maisha yako na baadaye yule mtu akatoweka, kauli hii hupoza vidonda vya moyo wake na husimamisha machozi ambayo mara zote yalizoea kutiririka mashavuni mwkae. Mtu huyu hakuwa hohe hahe bali ni zaidi ya hohe hahe katika maisha yake, hakuwahi kuwaona wazazi wake kwani walikuwa hawaonekani tena kwenye kioo.
Jua lilipozama kutokana na mawazo aliyokuwa nayo usingizi ulimchukua lakini siku moja aliamini kuwa ataacha kurusha mawe na kuangua matunda yaliyo juu kabisa ya mti na ataanza kula matunda yadondokayo bila ya kutumia nguvu nyingi hatimaye Mungu akamuangazia nuru kwenye maisha yake, je ni nani aliyemfanya akumbuke kauli ile aliyoambiwa na na yule mtu ambaye kwa muda mchache alimpotea na kumfanya aamini kumbe kuna wakati virefu vinaweza kuonekana vifupi hapo ndipo maisha yake yalipojichochea kuni na kuanza kuiva kabisa. Hakika penye nia pana njia maisha yake yalikuwa mazuri kabisa alimiliki nyumba yake na maisha yake aliyatamani yale maisha.
Siku moja alipokuwa safarini alifikiri mengi sana na kujiuliza kwanini Mungu amemzawadia maisha mazuri kama yale na kwanini sio wengine, maswali yale yalikuwa hayana majibu kamili kama yale ya kujiuliza kuwa kuku na yai kipi ni cha kwanza kuja duniani. Hakika hakupata jibu hatimaye akajikuta akitabasamu kwa muda mfupi mara ghafla honi ilisikika kwa ukulele mkali na ikamfanya aamke na kuinuka pale alipokuwa kwani ilikuwa ni njia ya magari na hata watembea kwa miguu, alipojiinua pale alipo ndipo maswali mengi yakaanza kumjia kichwani mwake akaanza kujiuliza kwanini Mungu aliamua kumfikirisha ndoto kama ile pale alipokuwa usingizini, basi hueda nikawa najutia juu ya umaskini wangu lakini siku ambayo Mungu ataamua kunipa utajiri vivyo hivyo nitajutia juu ya utajiri wangu.
Ewe Mungu asante kwa hiki ulichonipa maana kwa hikihiki kidogo kinaweza kikawa kikubwa atakaponiweka na watu wenye shida zaidi yangu na nimeamini kuwa siwezi kufikiria kufungua mlango wa sebuleni ikiwa nimefungiwa chumbani, kwa hiyo ni lazima nianze kufikiria kufungua mlango wa chumbani na baadaye ndipo nifikirie kuhusu mlango wa sebuleni ili niweze kujitoa hapa nilipo.
Posted by: MwlMaeda - 08-19-2021, 07:20 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
Mbwa aliambiwa: Utalinda nyumba za watu, utakuwa rafiki bora wa mwanadamu, utakula makombo atakayokuachia, na utapewa umri wa miaka 30.
Mbwa akasema: Miaka 30 ni mingi, nataka miaka 15 tu. Akapewa.
Kima aliambiwa: Utarukaruka kutoka tawi hili kwenda lingine. Utakuwa na kazi ya kuwahadaa na kuwachekesha watu. Utaishi miaka 20.
Kima akasema: Miaka 20 ni mingi nataka miaka 10 tu. Akapewa.
Punda aliambiwa: Utafanya kazi kuanzia mawio mpaka machweo na kubeba mizigo mizito mgongoni mwako. Utakula shayri, hutokuwa na akili, na utapewa umri wa miaka 50.
Punda akasema: Nimekubali kuwa punda, lakini miaka 50 ni mingi sana, nataka miaka 20 tu. Akapewa.
Mwanadamu aliambiwa: Wewe utakuwa kiumbe mwenye akili zaidi duniani, utaitumia akili yako kuwaongoza viumbe wengine, utaishi maisha mazuri ili kuiendeleza dunia, na utapewa umri wa miaka 20. Mwanadamu uwa hatosheki kabisa. Hivyo basi….!
Mwanadamu akasema: Niwe mtu wa kuishi miaka ishirini tu? Hiyo ni michache mno. Nataka ile miaka 30 aliyoikataa punda, ile 15 aliyoikataa mbwa, ile 10 aliyoikataa kima. Akapewa.
Tangu wakati huo mwanadamu huishi miaka 20 kama mtu, kisha huoa au kuolewa. Baada ya hapo anaishi miaka 30 kama punda, akifanya kazi kuanzia mawio mpaka machweo na kubeba mizigo mizito mgongoni mwake.
Watoto wake wanapokuwa wakubwa anaishi miaka 15 kama mbwa akilinda nyumba, kufunga milango na kuzima umeme na kula chakula kidogo au makombo anayoachiwa na watoto wake.
Anapozeeka na kustaafu anaishi miaka 10 kama kima. Anahama kutoka nyumba hii kwenda nyingine, na kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine. Anatengeneza uongo na visa ili kuwachekesha wajukuu zake.
Hivyo kila hatua anayopiga mwanadamu inampa majukumu na sifa Fulani. Usifanye mambo ya vijana kama umeshazeeka na usifanye mambo ya wazee ungali kijana.
Posted by: MwlMaeda - 08-19-2021, 07:14 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
Katika upekuzi wangu jana nikawa nimekifuma kitabu hiki na mwisho nikakutana na hadithi hii ungana nami kuisoma inatoka katika kitabu cha 6 Tujifunnze Lugha Yetu!
Zamani za ukoloni, palitokea Mzungu mmoja. Mzungu huyo hakuwa mtu mwema. Alikuwa mkali na mkatili sana. Kwa ajili ya ukatili wake watu walimwita mkoloni. Wananchi wote walimchukia sana popote pale alipokwenda.
Mzungu huyo alikuwa Bwana Shamba. Alikuwa na bakora iliyokuwa imetengenezwa kwa mkwaju. Kila alipokwenda kukagua mashamba, alikuwa na bakora hiyo mkononi. Alipendelea sana kuitwa “Bwana Mkubwa”. Mkolono huyo alifurahia sana kupiga watu. Aliwapiga watu waliposhindwa kupalilia mashamba. Aliwapiga pamba yao ilipokuwa chafu. Aliwapa taabu sana.
Katika kijiji cha Kwachaga, Wilaya ya Handeni, alikuwapo mzee mmoja aliyeitwa Kibanga. Mzee huyu alikuwa mwenye nguvu, hodari na shujaa. Alikuwa fundi wa mieleka. Ingawa alikuwa mwenye nguvu, alikuwa mpole. Hivyo watu wa Kwachaga walimpenda na kumtegemea kuwaongoza vitani.
Siku moja yule Mzungu alifika Kwachaga kukagua mashamba ya mihogo. Jumbe pamoja naye wakatembelea mashamba. Kwa bahati mbaya mwaka ule haukuwa na mvua ya kutosha. Kwa hiyo mihogo haikustawi. Kila wakati yule Mzungu alipotazama mashamba alitikisa kichwa na kufoka. Mwisho akamwagiza Jumbe kuitisha mkutano wa watu wote wa kijiji. Waliporudi kijijini Jumbe akapiga mbiu. Watu wote wakakusanyika. Walipofika tu, yule Mkoloni akaanza kuwatukana, akawaambia, “Ninyi watu weusi ni wavivu sana. Hamfanyi kazi sawa sawa. Mashamba yenu ni mabaya sana”. Jumbe akataka kumjibu ili kumweleza kwa nini mihogo haikustawi. Kabla hajamweleza yule Mzungu alimrukia na kumpiga kofi. Kisha akasema, “Sitaki kujibiwa na wewe, mvivu wa wavivu”. Watu wote wakakaa kimya. Hakuna aliyeweza kufanya kitu.
Kibanga akajitokeza, akasimama. Akamtazama yule Mkoloni kwa dharau sana. Kisha akamwuliza, “Kutuita sisi wavivu ndiyo nini? Na kumpiga Jumbe wetu mbele yetu, maana yake nini?”
Kabla ya kumaliza kusema, Mkoloni aliamka kitini kwa hasira , akataka kumpiga Kibanga. Alishika bakora yake mkononi. Akasema, “Nitakuadhibu vibaya kima we! Unajifanya kuwa shujaa? Huwezi kucheza na bwana mkubwa. Nitakupiga, kisha utakwenga jela miezi sita.” Lakini Mkoloni hakuwahi kumwadhibu Kibanga. Aliadhibiwa yeye. Kabla ya kumfikia, Kibanga alimpiga chenga. Kisha akamrukia, akamnyang’anya bakora yake. Akaitupa, ikaokotwa na vijana, wakaificha.
Kibanga alimshika yule Mzungu akamwambia. “Wewe umezoea kutoa amri kila siku, lakini leo utashika adabu, mbwa wee!” Papo hapo alimnyanyua juu na kumbwaga chini, puu! Yule Mkolono akaumia sana. Kabla ya kuamka, Kibanga alimwinua tena na kumbwaga chini kama furushi la pamba. Akamkalia.
Hapo yule Mkoloni akawa hana la kufanya. Bila ya bakora alikuwa hana nguvu. Akaomba radhi akilia, “Samahani! Naumia! Nihurumie! Sitafanya tena hivyo.” Kibanga alimjibu kwa dharau, “Sikuachi mbwa wee! Leo utakiona cha mtema kuni! Ulijiona una nguvu. Leo nitakutengeneza.”
Wazee wakamshika Kibanga na kumwomba asimpige tena. Akamwacha. Kwa shida yule Mkoloni akajikokota kwenda hemani. Alikuwa amejaa vumbi huku damu zikimtoka. Wazee wengine wakamfuata nyuma. Walinyamaza kimya, wakimhurumia. lakini vijana walifurahi sana.
Baadaye waliimba wimbo wa kumsifu Kibanga.
Jioni yule Mkoloni aliomba radhi kwa wazee. Mzee mmoja akasimama na kumwambia, “Umefanya vizuri kuomba radhi, nasi tunaipokea. Lakini tangu leo usijivunie ubwana. Jivunie utu. Ninyi wakoloni mna kiburi. Mnatudharau. Kama ungetuuliza tungekuambia kwa nini mihogo haikustawi. Haya yote yamekupata kwa sababu ya kiburi chako. Katika nchi hii tunaamini kuwa kiburi si maungwana”.
Baada ya hapo wazee wakamsamehe, lakini hawakumpa bakora yake. Ikabaki nyumbani kwa Jumbe. Yule Mkoloni akaondoka. Tangu siku hiyo hakufika tena Kwachaga. Kila mara alipokutana na watu aliyakumbuka maneno ya yule mzee, “Kiburi si maungwana”.
Siku hizi kijiji cha Kwachaga kina maendeleo mazuri ya kilimo na mifugo. Maendeleo yote yamepatikana kwa sababu ya uongozi bora wa Serikali ya wananchi.
Kilio, kilio, kilio kwa kijana wa leo, Afrika! Wakati vijana wengine wanapoombwa kujiunga na jeshi ili kujenga na kulinda nchi yao, siyo kwangu. Kwangu naburutwa msituni, kujiunga na jeshi kuendeleza vita ya wenyewe kwa wenyewe. Napigana na ndugu zangu ndani ya taifa moja ili matumbo machache yafaidi almasi, dhahabu, mafuta na maliasili nyingine. Naingizwa katika vita isiyo na maana yoyote kwangu.
Nikitaka kutafuta elimu, hakuna madarasa. Upepo umeezua paa la nyasi la shule yetu! Nikibahatika kupata kaelimu kadogo; chini ya mti, nazuiwa kufikiri zaidi. Naambiwa kuwa, Afrika hakuna kufikiri! Mtu mweusi hana fikra ila mtu mweupe ndiye mwenye fikra. Natakiwa nifuate fikra zake!
Nikitaka ajira, naambiwa uzoefu miaka mitano au kumi na zaidi. Uzoefu nitaupata wapi? Nikitamani kujiajiri mazingira hayaniruhusu: Umasikini, umasikini tena umasikini umenikumbatia! Nikijiunga na siasa, wimbo maarufu kote ulimwenguni ni demokrasia.
Demokrasia ina mizengwe, umajimbo, ukabila, udini, ubabe, rushwa, ubabaishaji, yutapeli na kushindana bila kukubali kushindwa. Siasa barani kwetu ni kiini macho na matokeo yake ni ‘demoghasia’ isababishayo vifo. Ubinafsi umejaa! Kujipitishia marupurupu kibao! Ubaguzi! Majigambo! Dharau…..!
Nikitaka kusema, naambiwa mjinga, Nikidai haki, naambiwa madai yangu ni ya kijinga. Nalazimishwa kuandika barua ya kuomba msamaha na kuahidi kuwa sitadai haki tena! Nalazimishwa kuwa bubu. Kijana msomi nanyimwa uhuru wa kutoa mawazo yangu mbele ya jumuiya yangu. Kijana msomi nafungwa mdomo. Kijana msomi kukaa na kunyamaza kimya ni usaliti. Usaliti kwa jamii ya walipa kodi ambao pesa zao zimenisomesha hadi kuitwa msomi. Kijana msomi, kutofikiri ni dhambi nyekundu pyuuu!- isiyosameheka. Msomi kutofikiri ni kifo cha kifikra kwangu mimi kijana wa
Kiafrika. Chochote ninachotaka kufanya kinanikatisha tamaa. Nikiwa ‘deiwaka’ mpiga debe, kila siku nitaamkia korokoroni! Nikitaka kujiburudisha na gongo au viroba – ni kifo cha ajabu. Nikibugia unga – kwangu ni kifo cha mende wekundu! Nikijiingiza kwenye ukahaba, natozwa kodi ya maendeleo!
Nikitaka kuwa “changudoa”, UKIMWI unaniwinda kama mamba awindavyo viumbe baharini! Sasa nifanye nini? Balaa kubwa kwangu! Nikiamua kuokoka, wokovu hauonekani. Nimebaki njia panda. Mchungaji amekuwa mwongo, katu hasemi ukweli. Ananilaghai kuwa wokovu upo karibu kuingia badala ya kuniambia kweli wokovu umekwishatoweka. Naambiwa kuwa nijiwekee hazina mbinguni ambako kutu na wadudu hawataharibu mali yangu…Huu ni utapeli.
Ingekuwa vizuri kama ningeelezwa wazi jiwekee akiba tumboni mwa sheikh au tumboni mwa mchungaji au tumboni mwa padre! Naambiwa kuwa toeni ulichonacho utabarikiwa badala ya kuambiwa kuwa kitayabariki matumbo ya wachache! Nakumbuka wakati mama yangu alipokuwa mwalimu katika shule ya msingi ya Mabonde Kuinama, aliniambia kwamba, urithi wa utamaduniwetu ni mila na desturi za Afrika. Lakini siku hizi sivyo. Siku hizi naambiwa kuwa urithi wa kizazi kipya ni bia aina ya “Safari Larger”.
Kijana wa sasa naangalia wizi wanaofanyiwa watu maskini lakini sisemi chochote. Najinyamazia kimya. Wizi umo makanisani, misikitini, Ikulu, mahakamani na hata bungeni. Lengo ni kuwanyanyasa, kuwadhulumu, kuwaonea, kuwanyonya na kuwadhalilisha wanyonge. Hakika kunyamaza kwangu ni usaliti. Nimeitambua nafsi yangu. Naahidi kupambana hadi kufa na kupona.
Inanifika aibu, waniita mvulana,
Ingawa Mimi shaibu, wa kunilea ndo Sina,
Tazama zangu sharubu, hivi zinasokotana,
Nifunzeni kutongoza, nami nimpate wangu.
Ona haya maajabu, bado sijaitwa bwana,
Kila siku najaribu, changu kifua kutuna,
Naambulia taabu, nalo jibu la hapana,
Nifunzeni kutongoza, nami nimpate wangu.
Au niende ghaibu, kwa Wazungu na Wachina,
Niipande merikebu, nikamsake kimwana,
Jamani nipeni jibu, fahamuni raha Sina,
Nifunzeni kutongoza, nami nimpate wangu.
Moyo unaleta gubu, ukimbiavyo ujana,
Wanicheka mie bubu, eti nashindwa kunena,
Ningelikuwa na babu, ngenifunza kwa mapana,
Nifunzeni kutongoza, nami nimpate wangu.
Sasa nimeshika nibu, kwenu ombi kulinena,
Ally na Kaka Rajabu, nisaidie kijana,
Neno liwe matibabu, hata lisilo na kina,
Nifunzeni kutongoza, nami nimpate wangu.