SHAIRI: NIFUNDISHENI KUTONGOZA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: NIFUNDISHENI KUTONGOZA (/showthread.php?tid=889) |
SHAIRI: NIFUNDISHENI KUTONGOZA - MwlMaeda - 08-18-2021 NIFUNDISHENI KUTONGOZA Kila ninapojaribu, kurusha yangu ndoana, Wala sipati jawabu, nabakia kujikuna, Wenzangu napata tabu, ninakosa wasichana, Nifunzeni kutongoza, nami nimpate wangu. Inanifika aibu, waniita mvulana, Ingawa Mimi shaibu, wa kunilea ndo Sina, Tazama zangu sharubu, hivi zinasokotana, Nifunzeni kutongoza, nami nimpate wangu. Ona haya maajabu, bado sijaitwa bwana, Kila siku najaribu, changu kifua kutuna, Naambulia taabu, nalo jibu la hapana, Nifunzeni kutongoza, nami nimpate wangu. Au niende ghaibu, kwa Wazungu na Wachina, Niipande merikebu, nikamsake kimwana, Jamani nipeni jibu, fahamuni raha Sina, Nifunzeni kutongoza, nami nimpate wangu. Moyo unaleta gubu, ukimbiavyo ujana, Wanicheka mie bubu, eti nashindwa kunena, Ningelikuwa na babu, ngenifunza kwa mapana, Nifunzeni kutongoza, nami nimpate wangu. Kinachonipa ajabu, nisemapo mnaguna, Au nakosa adabu, heshima niwe hakuna? Basi nipeni sababu, mbona mnacheka sana, Nifunzeni kutongoza, nami nimpate wangu. Sasa nimeshika nibu, kwenu ombi kulinena, Ally na Kaka Rajabu, nisaidie kijana, Neno liwe matibabu, hata lisilo na kina, Nifunzeni kutongoza, nami nimpate wangu. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |