Welcome, Guest |
You have to register before you can post on our site.
|
Online Users |
There are currently 62 online users. » 0 Member(s) | 61 Guest(s) Bing
|
Latest Threads |
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
|
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
|
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
|
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
|
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
|
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403
|
|
|
SIMULIZI : KAKA HUKO ULIPO TUNAOMBA UTUSAMEHE, PUMZIKA KWA AMANI SASA! |
Posted by: MwlMaeda - 08-20-2021, 07:59 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
|
|
“Baba Karanga za Diamond! Baba nataka Karanga za Diamond!” Huu ni ule wakati ambao unasimama kwenye foleni na unatamani hata kuwasha gari na kusukuma magari yaliyo mbele yako. Ilikuwa ni jioni nimetoka kuwachukua wanangu shule na mtoto wangu mdogo wa mwisho alianza kupiga kelele za kutaka karanga. Pembeni yangu kulikuwa na kijana, au niseme mtoto kashikilia Karanga za Diamond kazizungusha shingoni anauza.
Alikuwa akipita kila gari kuuza, kwa kawaida sipendi kushusha vioo kwenye gari lakini kutokana na kelele nilijua na ile foleni angeanza kulia, nilimdekeza sana hivyo sikutaka alie kwa kitu cha Shilingi elfu moja. Nilishusha Kioo cha gari na kumuita yule kijana. “Karanga bei gani?” Nilimuuliza, “Moja mia tatu, tatu buku, aliongea huku akinioneshe kama anataka nikate. “Naomba za elfu tatu.” Niliongea huku nikimkabidhi noti ya Shilingi elfu kumi.
“Shikamoo Baba Mdogo…” Ilikuwa ni salamu yake wakati anaipokea ile pesa, nilishituka kidogo na kunyanyua uso wangu kumuangalia. Sikuwa namfahamu, hivyo nilidhani ni salamu tu za vijana kwa kuwa nilinunua Karanga nyingi. “Umenisahau? Mimi Peter, Peter Jackson…” Sasa aliongea akionesha kuwa ananifahamu kabisa, alitaja jina la Marehemu Kaka yangu. Nilijikuta nakodoa macho kumuangalia vizuri.
Nilishituka kwani mbele yangu ni kama alikuwa amesimama Jackson, sura yake kipindi tunaenda kuteka maji kule Kijijini Iringa ilinijia. Hapo ndipo nilikumbuka, yule alikuwa ni mtoto wa Marahemu Kaka yangu, ndiyo najua mnashangaa, mimi niko kwenye Gari nauziwa Karanga na mtoto wa Marehemu Kaka yangu, mnadhani labda ni Kaka wa jirani. Hapana, ni Kaka yangu, tena si tumbo moja tu, hapana yeye ndiyo aliniachia ziwa.
Najua mnashangaa mnajiuliza labda alitutenga tangu zamani. Hapana yeye ndiyo alinisomesha mpaka kumaliza chuo kikuu. Wakati huo yeye akifanya kazi nzuri tu kama Mkatoika kampuni moja, baada ya kuishi maisha ya shida kipindi cha utotoni na yeye kusoma kwa bidii na kufanikiwa kutoka kimaisha hakutusahau ndugu zake. Mpaka anafariki miaka mitatu iliyopita alihakikisha kuwa wote tunasoma na sikusoma tu bali alitutaftia kazi nzuri.
“Wewe unafanya nini huko Barabarani wewe si ulikuwa shule?” Niliuliza kwa aibu, nilitaka kumfokea lakini nilikumbuka tangu mazishi ya Kaka yangu na kugaiwa kwa mirathi sikugeuka nyuma. Sio mimi tu hata ndugu zangu wengine, kila mmoja alikuwa na familia yake hivyo kila mtu alikuwa bize na maisha yake. Baada ya wazazi wetu wote kufariki Kaka yetu yule ndiyo alikuwa akituunganisha hivyo, yeye alipotangulia kila mmoja lishika hamsini zake.
“Niliacha Baba, sasa hivi niko nafanya biashara…” Aliongea kwa uchangamfu kabisa. Nakumbuka wakati Baba yake akifariki alikuwa akisoma kidato cha kwanza Nairobi na moja ya sehemu za Mirathi ilikuwa ni kwa ajili ya kutunza watoto ikiwa ni pamoja na kuwasomesha. “Nishikie nikuombee chenji hapo kwa mwenzangu…” Aliongea huku akimuita kijana mwingine aliyekuwa pembeni yake na kumuomba chenji, mimi bado nilikuwa nimeduwaa.
Bado nilikuwa nawaza ni nini kilikuwa kimetokea mimi niko kwenye gari nina maisha mazuri wakati mtoto wa Kaka yangu anauza karanga, mchafu mchafu kachakaa na anaonekana kuchoka. Lakini hakua na makuu, wala hakutaka kuniomba chochote, alinipa chenchi yangu. “Msalimie Mama mdogo Baba, sisi ni wazima… Mama anakusalimia…”
Aliongea na kuondoka, huwezi amini nilimuangalia mpaka anapotelea bila kuweza kunyanyua mdomo kumuita. Machozi yalikua yananitoka bila kujua. “Nimefanya nini?” Nilijiuliza bila majibu. Nilikuja kustuliwa na honi za magari mengine wakiniambia kuwa niondoke kwani nawachelewesha. “Baba unaumwa? Mbona unalia?” Mwanangu mkubwa aliniuliza lakini sikua na jibu.
Nilifika nyumbani na kumuuliza mke wangu kama anawasiliana na mke mwenzake, mke wa marehemu kaka yangu. Hakua akiwasiliana naye, alikua hata hajui anaishi wapi? Nilishindwa kukaa ndani, niliamua kwenda kumtafuta, nilifika kwenye nyumba yao, kufika ndipo nilikumbuka kuwa ile nyumba ilikua ni ya shirika ambayo Kaka yangu alipewa hivyo baada ya kufariki waliondolewa na alikua anaishi mtu mwingine.
Nikakumbuka kuna sehemu Kaka alikua anajenga, nilienda nyumba ilikua haijakamilika, alikua anajenga nyumba kubwa ya ghorofa. Nilifika na kukutana na watoto wengine wa Kaka, walikua wakicheza nnje ya lile ghorofa kubwa ambalo lilikua kama Gofu. Wao walikua wadogo hata hawakunitambua, lakini mimi niliwakumbuka. Walinisalimia niliwaulizia Mama yao wakaniambia ametoka, sikua na haraka nilitaka kumsubiri kwani hata hakua na namba za simu.
Nilikaa pale mpaka kwenye saa moja hivi za usiku. Peter ndiyo alikuja na kuniona, alishangaa kuniona pale na kunisalimia, alinikaribisha ndani. Alionekana kuchoka sana lakini alijitahidi kutabasamu, alishakua kijana anaelewa. Nilimuulizia alipo Mama yake na kama atachelewa. “Nyie si mngempeleka kumuona Mama! Mnamchelewesha Baba mdogo au hamjui ana kazi zake huko za kufanya!” Aliwafokea kidogo, nilimuambia haina shida ndipo akaniambia alipo Mama yake.
Hakukua mbali sana, tuliingia kwenye Gari na kuanza safari, ndani alinichangamkia, aliniulizia kuhusu wanangu, kuhusu Shangazi zake, kuhusu Baba zake wadogo wengine na watu wengi wa familia. Alikua akimjua kila mtu lakini kwa bahati mbaya sisi ni kama tulikua tumewasahau. Mimi na ndugu zangu tulikua tukikutana mara kwa mara lakini hata mara moja tulikua hatujawahi kuwazungumzia lakini yeye ambaye hata alikua hatujui vizuri anaulizia tunaendeleaje.
Nilifika alipokua shemeji yangu, nilimuona kakaa Barabarani, karai la ndizi na kibatari kiko mbele yake. “Mama kuna mgeni wako…” Alimuita Mama yake ambaye alishtuka kuniona. Nilimuona yule shemeji yetu ambaye alikua anatupikia mara kwa mara tukienda kumsalimia. Alikua kachoka, kakonda imebaki sura tu, alijitahidi kutasabasamu, alichangamka, alijitahidi kuonyesha kama hana shida yoyote lakini shida zilijionyesha.
Tulisalimiana, aliona aibu hata kunishika mkono akihisi atanichafua. Nilimuomba turudi nyumbani naye hakubisha, nilifika mpaka kwake ndipo nikagundua kuwa walikua wakiishi katika gofu, hata milango lilikua halina zaidi ya shuka lililotundikwa kama mlango. Kweli niliumia, aliniletea kiti nikakaa, kila nikifumbua macho nilimuona Marehemu Kaka yangu kasimama ananisuta.
Nilihisi kama ananiambia “Kweli nyie ndiyo wa kuwafanyia hivi wanangu, nyie niliowaamini nikawasomesha! Hivi kweli mke wangu ambaye nilimkataza kufanya kazi awe Mama wa nyumbani nyie nikawatafutia kazi ndiyo analea wanangu nyie na kazi nzuri hata kuwasomesha hamuwezi?” Nilishindwa kuvumilia nilimuuliza shemeji yangu nini kimetokea akaniambia, maisha.
Baada ya kupata mirathi alitegemea kuendelea kuwasomesha watoto, alitumia tumia akijua ni pesa nyingi lakini matumizi yalikua makubwa, anashtuka zishakatika nusu hapo ndipo akaamua afungue biashara, kwakua hakua na uzoefu alitapeliwa mara mbili na kupoteza kila kitu. Nilisikitika na kumuambia kwanini hakuja kuomba msaada alinikumbusha alishanipigia simu mara zaidi ya kumi zote namuambia nitamtafuta nitamtafuta.
Nilikumbuka mara ya mwisho alikuja ofisini kuniambia kuhusu ada ya watoto nikampa elfu kumi. Sikua na chakuongea zaidi nilijua sisi ndiyo tumemuangusha, Kaka yangu hakumuandaa kubeba majukumu kama yale. Alimfanya Mama wa nyumbani, alimkataza hata kutoka ndani, kila kitu alikua ananunuliwa, Kaka alikua na wivu na mara nyingi akitoka alikua anapigwa na kweli tulikua tunamuona Kaka yuko sawa na shemeji anakosea.
Hata katika mali hakua akimshirikisha zaidi ya sisi ndugu zake, hata ndugu wa shemeji alikua hawasaidii na kila mara alisema hana pesa. Niliona aibu kuendelea kuuliza, nilimuambia anyanyuke tunaondoka pale na kuanzia siku ile nitamsaidia kulea familia kwani ni jukumu letu wale ni wenetu. Sikutaka waendelee kulala pale niliwachukua na kuondoka nao. Sasa hivi watoto wamerudi shule na shemeji nimemfungulia biashara.
Nyumba nimepata watu wa kuimalizia wanataka kufungua ofisi hivyo naamini mpaka mwezi wa nane mwaka huu wataanza kuchukua kodi kidogo kidogo. Nimeandika kisa changu ili kumuomba msamaha Kaka yangu kwa kushindwa kulea familia yake na kuwaambia wanaume wenzangu kuwa hata kama una mali kiasi gani hakikisha unamuandaa mkeo kuhudumia wanao kwani ndugu wana familia zao na ukiondoka watakusahau, nawaambia kwa sababu sisi tulisahau pamoja na kusaidiwa sana.
***MWISHO.
Najua watu wengi hatuwazi kuhusu kifo lakini kipo. Je, mwanaume umemuandaa mke wako kubeba majukumu ya kuhudumia wanao au unategemea ndugu na wewe mwanamke Je, umejiandaa kubeba majukumu au unasubiri yakufike kwanza?
|
|
|
Masimulizi ya Alfu Lela U Lela |
Posted by: MwlMaeda - 08-20-2021, 07:50 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
|
|
Masimulizi ya Alfu Lela U Lela
UTANGULIZI
Hakika asasi za hadithi za ALFU LELA U LELA ni Asia hasa Arabuni, Bara Hindi, na Ajemi. Asasi hii inasemekana imetoka katika kitabu kimoja cha Ki-Persia cha hadithi za majini kiitwacho Hazar Afsanah (Visa Elfu Moja) kilichotafsiriwa Kiarabu katika mwaka 850. Wanazuoni wa sasa waliotafiti zaidi juu ya hadithi hizi wanasema kuwa chanzo hasa cha ALFU LELA U LELA ni Bara Hindi na Persia. Walakini, wasimulizi wa nchi mbalimbali wa hadithi hizi, kila walipozisimulia, waliongezea hadithi na visa vingi vya kikwao mpaka zikaongezeka idadi na kuwa vitabu chungu nzima!
Hadithi hizi zipendwazo sana na walimwengu na zilizotafsiriwa kwa lugha nyingi, zimeletwa Ulaya, kwa mara ya kwanza, na Mfaransa Antoine Galland (1646-1715) aliyekuwa na taaluma ya mambo ya Kiarabu na aliyesafiri sana Mashariki ya Kati nyakati hizo; halafu zikatafsiriwa kwa Kijerumani mwaka 1865 na Gustav Weil, mtaalam wa Mashariki ya Kati.
Ijapokuwa hadithi hizi zilitafsiriwa kwa Kiingereza, kwa mara ya kwanza (1706-8) na mtu asiyejulikana, tafsiri kamili kwa lugha ya Kiingereza ya vitabu ilifanywa na John Payne (1882-4). Walakini, tafsiri iliyopendwa zaidi ni ile ya Sir Richard Burton ya vitabu 10 ya mwaka 1885-6.
Kwa Kiswahili, hadithi hizi, ambazo zilitoweka baada ya Uhuru, zilitafsiriwa na Edwin W. Brenn katika mwaka 1928 chini ya uongozi, ufupishaji, na uhariri wa Mmisionari F. Johnson. Wao walizifupisha na wakazibadili (kwa mfano safari ya saba na ya mwisho ya Sindbad) kwa sababu zisizojulikana.
Mimi, katika vitabu hivi vipya nimetoa tafsiri mpya kutoka katika vitabu vya lugha mbalimbali bila kuzihariri wala kuzifupisha isipokuwa sehemu fulani fulani tu ambazo nimeona huenda zikaeleweka vibaya.
Kwa kuwa hadithi hizi ni za asili ya Kiarabu, kwenye fahrisi nimejaribu, kadiri nilivyoweza, kutumia maneno fulani fulani ya asili ya Kiarabu kama yaandikwavyo au yatamkwavyo kwa lugha hiyo na kama yalivyotumiwa katika tafsiri nyingi. Walakini, maneno hayo nimeyaeleza kwa Kiswahili kama yajulikanavyo na yalivyoandikwa katika kamusi ya Kiswahili Sanifu.
Sina budi kusisitiza humu kuwa kabla Wareno, wazungu wa kwanza kukanyaga mwambao wa Afrika Mashariki mnamo mwaka 1498 chini ya uongozi wa nahodha Vasco da Gama wakivinjari Afrika kutafuta njia ya kuelekea Bara Hindi, Waswahili, toka enzi na enzi, waliingiliana na wafanyabiashara na mabaharia kutoka Ajemi (Persia), Arabuni na Bara Hindi. Kuna ushahidi kamili wa kihistoria unaothibitisha pia kuwa hata Wachina na Wa-Indonesia wa kale walifika mwambao wa Afrika Mashariki kuitwako Uswahilini. Hivyo basi, ngano, visa, na hadithi nyingi za Kiswahili zilizosimuliwa na Waswahili toka enzi za kale, kuna nyingi zilizoathiriwa na nchi hizo na kuna za asili ya nchi hizo ambazo, baada ya miaka nenda, mwisho zikawa za Kiswahili. Kwa hiyo, kuzikana au kuzifutilia mbali ni kinyume cha kanuni za fasihi. Haiwezekani, kwa mfano, kwa sababu fulani fulani, ngano, hadithi au visa vya Kizulu, Kirusi au Kijapani, vikabadilishwa na kudai kuwa ni vya Kiingereza, Kiarabu au Kichina! Fasihi ikiwa ni nzuri, hutasfiriwa kwa lugha nyingi za dunia kwa manufaa ya walimwengu. Lakini fasihi hiyo hubaki ya asasi yake. Hivyo basi, nimeona ni kkheri picha za tafsiri hii mpya ya ALFU LELA U LELA ziwe za kiasili kama zilivyochapishwa katika matoleo ya kwanza ya lugha mbalimbali kwani Shahrazad au Sindbad hawakuwa wa asili ya Kiafrika!
Kwa kumalizia, naishukuru famila yangu na binti yangu kwa uvumilivu wao wa kuukabili upweke walioukabili nilipokuwa nikitumia wakati wangu mwingi kuzitafsiri hadithi hizi ofisini, wakati ambao wangefurahi kuwa nami! Namshukuru pia Salehe Awadh Mazrui wa E-PLUS Duesseldorf, Ujerumani, kwa utaalam na msaada wake wa ki-kompyuta ulionifaa sana, kwani kila kompyuta yangu ilipokwama, yeye, bila kusita, alitoka Dusseldorft kuja upesi Cologne kulitatua tatizuo! Namshukuru pia Lutz Diegner kwa msaada wake wa kunifafanulia kwa Kiswahili maana ya maneno magumu ya Kijerumani. Shukran za dhati nazitoa kwa sahibu yangu, mshairi mashuhuri Abdilatiff Abdalla ambaye sasa ni mhadhiri wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Leipzig, Ujerumani kwa kuupitia mswada huu, kwa ushauri wake, na kwa kuiandika Dibaji ya vitabu hivi. Kwa kumalizia, tafsiri hii isingewezekana kama si nafasi na msaada wa hali na mali niliopewa na Taasisi ya Lugha za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Cologne, Ujerumani.
Cologne, Ujerumani
Juni,2 003
SULTAN SHAHRIYAR NA SULTAN SHAHZA-MAN
HAPO KALE paliondokea Sultani mmoja wa Kisassanid aliyekuwa na enzi kubwa sana iliyoenea toka Bara Hindi mpaka Uchina. Jeshi lake kubwa lenye nguvu, liliweza kuishinda na kuiteka kila nchi ya jirani mpaka sifa za utawala wa Sultani huyo zikaenea kila pembe ya dunia. Alipofariki, akaacha wana wawili waliokuwa mashujaa na hodari wa kupanda farasi, hasa mkubwa aliyeitwa Shahriyar aliyerithi kiti cha enzi cha baba yake. Yeye alifuata nyayo za baba yake mpaka raia zake wote wakampenda. Mdogo wake aliyeitwa Shahzaman akawa Sultani wa nchi ya Samarkand.
Basi ndugu wawili hawa wakendelea kutawala nchi zao kwa furaha na kwa haki kwa muda wa miaka ishirini mpaka siku moja Sultani Shahriyar akaingiwa na hamu ya kutaka kumwona mdogo wake. Basi akamwamuru Waziri wake Mkuu aende Samarkand akamwalike Shahzaman.
Baada ya safari ndefu ya siku nyingi katika jangwa, mbuga na nyika, Waziri Mkuu akawasili katika mji mkuu wa Samarkand. Bila kuchelewa akafikishwa mbele ya Sultan Shahzaman aliyefu- rahi sana kupokea salamu na ujumbe kutoka kwa kaka yake; na yeye, bila kuchelewa, akatoa amri safari ya kumzuru kaka yake itayarishwe. Matayarisho yalipokamilika, Shahzaman akatanguliza msafara wake wa ngamia na farasi ulioshehenzwa vyakula na za- wadi za kila namna ukiongozwa na watumishi na wajakazi wake wa kumhudumia wakati wa safari yake ndefu. Kabla hajaondoka, walakini, akamchagua Waziri wake Mkuu amshikie madaraka yake mpaka atakapojaaliwa kurudi.
Usiku Sultani Shahzaman akakumbuka amesahau zawaidi muhimu aliyodhamiria kumpelekea kaka yake. Basi bila kuonekana na mtu, akatoka hemani mwake, akarejea kwenye kasri lake. Alipo- ingia ndani, la haula! akamkuta mkewe amekumbatiwa kimapenzi na mtumwa wake mmoja! Kuona vile, akapigwa na butaa; haku- weza kuamini yale aliyoyashuhudia pale penye sofa! Akafikiri,
“Kama kitendo kama hiki kinaweza kutokea wakati sijafika mbali, iblisi huyu atafanya nini nitakapokuwa mbali?” Hapo akafuta up- anga wake, akawaua wote wawili pale pale.
Aliporejea kwenye kambi, akaamuru msafara uendelee. Akaendelea na safari yake kwa huzuni na majonzi mengi mapaka akafika mji mkuu wa kaka yake.
Sultan Shahriyar aliposikia mdogo wake anawasili, akatoka kwa furaha na kwa shangwe astahiliyo Sultani kwenda kumlaki mdogo wake. Alipomwona, akamkubatia, akamkaribisha jijini mwake lililojiandaa kumpokea mikono miwili.
Lakini wakati Sultan Shahriyar alipokuwa akimfurahisha na kumtumbuiza mdogo wake, mawazo ya Sultan Shahzaman yakawa yako kwa yule mkewe na vile vitendo vyake vya ufisadi alivyokuwa akivifanya pale sofani.
Ijapokuwa alikuwa na huzuni na majonzi mengi hivyo, hakuna yeyote aliyejua wala aliyemweleza mkasa ule. Lakini Sultan Shahriyar alitambua kuwa kuna lililokuwa likimkera mdogo wake lakini hakutaka kuuliza. Alifikiri labda ni mambo ya utawala wa nchi au kuondoka kwake ndiko labda kulikokuwa kukimtia wasiwasi. Basi baada ya siku chache Sultan Shahriyar akaona ni kkheri amwa- like mdogo wake waende wakawinde ili apate kumliwaza; lakini Shahzaman akajibu kuwa anaumwa na hawezi kwenda kokote. Hapo Sultan Shahriyar aende peke yake.
Wakati Shahzaman alipokuwa ameketi peke yake karibu na dirisha la chumba chake lililoelekea bustanini huku akiwaza juu ya yale masaibu yaliyompata, mara mlango mmoja ukafunguka na wajakazi ishirini wakiongozana na watumwa ishirini wakatokea. Katikati yao alikuwemo malkia, mke wa kaka yake, ambaye uzuri wake ulikuwa hauna kifani. Wote arobaini wakelekea moja kwa moja mpaka penye chemchemi ya maji iliyokuwa ikitiririka. Hapo wakvua nguo, wakakaa majanini. Mara malkia akaita, “Masud, njoo utekeleze kazi yako!”
Mara pandikizi la mtumwa likatokea ambalo, mara tu lilipofika, likamkumbatia malkia na kufanya naye mapenzi pale bustanini! Wale watumwa wengine nao, hali kadhalika, wakawa wanazini na wale wajakazi. Wakaendelea na mapenzi yao mpaka kulipoanza kuchwa na wakati wa Sultani kurejea kutoka mawin- doni ulipokaribia.
Shahzaman alipoona vile, akafikiri, “Wallahi, mkasa ulioni- pata mimi si mkubwa kama huu ninaoushuhudia hapa!”
Hapo ile huzuni aliyokuwa nayo ikamtoka, akaanza kula na kunywa kwani toka alipowasili kwa kaka yake chakula kilikuwa hakimshuki rohoni.
Sultan Shahriyar aliporejea, akashangaa kumwona mdogo wake amebadilika na sasa yumo katika hali nyingine kabisa.
“Imekuwaje, ndugu yangu,” Sultan Shahriyar akahoji kwa mshangao, “kuwa nilipoondoka ulikuwa dhaifu uliyepauka uso na sasa unaonekana mwenye siha nzuri hivi?”
“Mintaarafu siha yangu sasa na unyonge niliokuwa nao awali,” akajibu Shahzaman, “nitakusimulia sababu lakini sithubutu hata kidogo kukufunulia sababu zilizoleta mabadiliko hayo; lakini jua kuwa, baada ya kupokea mwaliko wako, nilianza safari ya kuja huku. Kwa kuwa nilisahau lile jiwe la tunu nililokupa zawadi, ili- nibidi nirejee nyumbani nikalichukue.”
Nilipoingia ndani, nikamkuta mke wangu amekumbatiwa na mmoja wa watumwa wangu wamelala kwenye sofa wakifanya mapenzi! Unaweza kukisia jinsi nilivyohisi! Ghadhabu zilizoni- panda zilinifanya niwaue paho hapo wote wawli; halafu nikarejea kwenye msafara, nikaendelea na safari ya kuja huku wakati moyo wangu umejaa huzuni na majonzi.”
Aliposikia maneno hayo, Sultan Shahriyar akamsihi mdogo wake amweleze na ile sehemu iliyobaki. Shahzaman, baada ya kusita na kulazimishwa, akawa hana budi kumweleza kaka yake yote aliyoyashuhudia pale bustanini.
Akipigwa na mshangao na kupandwa na ghadhabu, Sultan
Shahriyar akasema: “Siamini hayo unayoyasema mpaka niyashuhu- dia mwenyewe kwa macho yangu!”
“Kama ni hivyo,” akapendekeza Sultan Shahzaman, “basi tangaza unakwenda tena kuwinda halafu rudi upesi uje hapa ujifiche nami, nawe utayashuhudia yale niliyoyashuhudia.”
Basi siku ya pili Sultan Shahriyar akatangaza madhumuni yake ya kwenda tena kuwinda. Hapo kundi lake la kuwinda likatoka mjini huku limebeba matumizi ya Sultani wakati akiwa mawindoni.
Baada ya kubaki kidogo kambini kule mawindoni, Sultan Shahriyar akatoa amri kwa watumishi wake kuwa wasimruhusu yeyote kuingia hemani mwake; halafu akajibadili kwa kuvaa mavazi mengine, akatoka bila kuonekana na mtu yeyote, akarejea hadi kwake alikomkuta mdogo wake akimsubiri.
Basi wote wawili wakajibanza karibu na lile dirisha lililoele- kea bustanini. Mara malkia na wajakazi walewale wakatokea tena wakifuatwa nyuma na watumwa walewale. Walipofika bustanini, wakayatenda yaleyale waliyoyatenda siku ile ya kwanza!
Kuona vile, Sultan Shahriyar akapigwa na bumbuazi na mshangao mkubwa sana. Akamgeukia mdogo wake, akamwambia, “Ndugu yangu mpenzi, tuuache ufalme na tutokomee ulimwen- guni tukatafute kama tutawapata waliokumbana na mikasa kama yetu.”
Baada ya Shahzaman kukubali, wakatoka kwa siri, wakasafiri kwa masiku mpaka siku moja wakafika pwani penye ufukwe mmoja mzuri mweupe wa bahari ukingoni pake pameota majani mazuri yaliyoptiwa na chemchemi ya maji safi baridi. Hapo wakashuka juu ya farasi zao, wakatawadha, wakasali sala ya adhuhuri.
Wakati walipokuwa wamepumzika kwenye kivuli cha mti mmoja mkubwa uliokuwa ukingoni wakila chakula chao cha mchana, mara bahari ikachafuka, ikaanza kutoa mapovu na maw- imbi yakaanza kupanda juu. Ghafla pale baharini pakazuka jabali refu ajabu!
Lo! kuona vile wale ndugu wawili wakapigwa na mshangao; haraka wakapanda juu ya ule mti! Walipokuwa juu, wakatazama baharini, wakaona kumbe lilikuwa si jabali bali ni jini lililobeba kasha kubwa kichwani!
Lile jini likatoka mle baharini, likaelekea pale mtini wal- ipokuwa wale ndugu wawili. Baada ya kukaa chini, likafungua lile kasha, likatoa sanduku alilolifungua. Mle sandukuni makatoka msichana mmoja mzuri kama nini!
“Mwanamwali mzuri, mtoto wa watu niliyemnyakua kwao usiku wa arusi yake,” likasema lile jini, “nataka kupumzika hapa kidogo.”
Baada ya kutamka maneno hayo, lile jini likaweka kichwa chake juu ya paja la yule msichana, na mara likachotwa na usingizi likalala fofofo pale kivulini!
Katika kutazama kwake huko na huko, yule msichana akanyanyua macho juu kule mtini; mara akawaona wale ndugu wawili. Kuwaona tu, akawaashiria washuke wasiogope; lakini wale Masultani wakamsihi ayasalimishe maisha yao.
“Kama hamtashuka,” akasema yule msichana, “nitaliamsha hili jini na bila shaka yoyote litawaadhibu vikali.”
Waliposhuka, msichana akawaambia, “Mkitaka usalama wenu, ni lazima mfanye mapenzi nami sasa hivi tena papa hapa!”
Sultan Shahriyar na Sultan Shahzaman wakakataa katakata lakini yule msichana akasisitiza kwa hasira, “Kama hamtafanya nitakavyo, nitaliamsha jini sasa hivi!”
Baada ya kuwalazimisha kufanya alivyotaka, wale ndugu wawili wakabaki naye kwa muda alioutaka yule msichana, halafu akatoa kijaluba kibindoni mwake, akakifungua, akatoa pete tisini na nane zilizotungwa kwa uzi wa hariri, akasema huku akitabasamu kwa maringo, “Mnaona, wote wenye pete hizi wamelala nami wakati hili jini li haadhir, limelala kama mfu, na nyinyi ni lazima mnipe pete zenu sasa hivi!” Wakampa.
“Jini hili,” akaendelea yule msichana, “limeniteka nyara usiku wa arusi yangu; likanifungia sandukuni kisha likalitia sanduku ndani ya kasha kubwa hili mnaloliona ambalo hulifunga kwa kufuli saba, halafu hulizamisha katika lindi la bahari kuu ili eti nilindike! Ani- takapo, kama leo, hunitoa. Laiti lingejua hila za wanawake!”
Sultan Shahriyar na Sultan Shahzaman kusikia maneno yale, wakastaajabu sana, wakaambiana, “Kama kitendo kama hiki linaweza kutendewa jini lenye nguvu kama hili sembuse siye! hakika mikasa iliyotupata sisi haiwezi kulinganishwa na nusu ya vitendo vya msichana huyu!”
Basi bila kukawia wakarejea makwao. Mara tu alipoingia ka- tika kasri lake, Sultan Shahriyar akaamuru malkia na wale watumwa wake wote wakatwe vichwa.
Basi toka siku hiyo Sultan Shahriyar akawa hana imani tena na wanawake; ikawa kila siku ni kumwoa mwanamwari mzuri na kumwua asubuhi ya pili. Akaendelea kufanya hivyo kwa muda wa miaka mitatu mapaka msiba mkubwa ukaenea kote mjini na ukamkumba takriban kila aliyekuwa na binti mzuri mle jijini; wengi wakalihama jiji kwa kuwakhofia mabinti zao.
Kazi hii ya kuhuzunisha ya kumtafutia Sultan mwanamwari alifanyiwa na Waziri Mkuu mpaka ikafikia siku ambayo Waziri Mkuu alishindwa kumpatia Sultani mwanamwari wa kumwoa; akarejea kwake akiwa na wasiwasi na woga wa ghadhabu za Sultani.
Waziri Mkuu alikuwa na mabinti wawili; mkubwa aliitwa Shahrazad na mdogo aliitwa Dunyazad. Shahrazad alikuwa si mzuri wa sura tu bali pia alikuwa mwenye akili, busara, na ujuzi wa kila elimu ya falme za kale. Alizidurusu na kuzihitimu vizuri mpaka akawa aalim wa mambo mengi. Siku ile akamwona baba yake ni mnyonge mwenye wasiwasi mwingi; akamwuliza lililokuwa likim- kera. Waziri Mkuu akamweleza yale yaliyokuwa moyoni mwake.
Ndipo Shahrazad akasema, “Baba, niache mimi niolewe na Sultani; yatakuwa mawili: kufa au kuokoa maisha ya wasichana wenzangu waangamiao vibaya kila siku.”
Ijapokuwa Waziri Mkuu alifanya juu chini kumshawishi binti yake aache kusudio lake, hakufuzu, kwani Shahrazad aling’ang’ania tu akubaliwe kuolewa na Sultani.
“Kumbuka yaliyompata punda katika kisa hiki kifuatacho,” akaonya Waziri Mkuu; ndipo akamsimuliwa Shahrazad
KISA CHA PUNDA, FAHALI NA MKULIMA
HAPO kale, akaanza Waziri Mkuu, paliondokea mkulima mmoja tajiri aliyekuwa na kundi la wanyma wa kila namna na aliyejaaliwa kujua lugha zao. Hakuna aliyejua siri hiyo kwani ali- yemfundisha alimwonya asiitoe ama sivyo atakufa!
Basi katika banda moja mkulima huyo aliwaweka wanyama wawili: punda ampandaye aendapo safarini, na fahali amlimiaye shamba lake. Ikawa kila jioni, baada ya kazi, fahali humwendea punda aliyewekwa mahali pazuri penye nafaka nyingi na maji safi ya kutosha, ili aongee naye.
Kwa kuwa yule mkulima hakuwa na safari nyingi, ikawa kazi ya yule punda ni kula na kupumzika tu mle bandani wakati mwenzake fahali anababuka kwa kazi ngumu ya kukokota jembe zito kule shambani!
Siku moja yule mkulima alimsikia fahali wake akimwambia punda, “Bahati ilioje hiyo uliyo nayo mwenzangu! Mimi humenyeka kutwa shambani ilhali wewe mwenzangu wapumzika kutwa humu bandani ukilishwa na ukinyweshwa vizuri bila hata kupandwa na bwana wetu!”
Punda akamwambia fahali, “Tumia akili, rafiki yangu; bila kutumia akili mambo hayaendi. Kwa hiyo, nakushauri ufanye hivi: kesho utakapotiwa hatamu kwa madhumuni ya kupelekwa shamba, jibwage chini ujifanye mgonjwa! Usinyanyuke hata kama watakutandika mijeledi mia! Ukinyanyuka, jibwage tena chini; na watakapokurudisha hapa na kukuletea nyasi, susa kabisa kuzila! Fanya hivyo kwa muda wa siku mbili tatu upate kupumzika!”
Mfanyakazi alipompeleka shamba asubuhi ya pili, yule fahali akajifanya mgonjwa wa kufa! Na aliporudishwa bandani na kuletewa nyasi, akafuata ushauri wa mwenzake punda. Ndipo mkulima akamwambia mfanyakazi wake, “Leo mwache fahali apumzike, mchukue punda akafanye kazi yake!”
Jioni, baada ya kufanyishwa kazi kweli kweli, yule punda akarudishwa bandani yu hoi taabani! Alipoingia ndani, yule fahali akamshukuru punda kwa ule ushauri wake mwema uliomfaa sana; lakini punda hakujibu kitu ila alijuta kimoyomoyo kwa kumshauri haraka mwenzake bila kufikiri matokeo yake yatakuwaje!
Siku ya pili mfanyakazi akaja tena, akamchukua punda, akaenda akamfanyisha tena kazi kutwa mpaka jioni. Aliporudishwa hoi, yule fahali akamshukuru tena mwenzake.
“Laiti nisingemshauri!” Punda akajuta kimoyomoyo; hapo akamgeukia mwenzake akamwambia, “Sahib yangu, nilipokuwa nikirudi, nilimsikia bwana wetu akimwambia mfanyakazi: ‘kama fahali hakupona, kesho mpeleke machinjoni akachinjwe!’ Kwa kuwa u rafiki yangu mpenzi, nimeona ni kkheri nikuarifu mapema upate kujua mambo yalivyo!“”
Fahali kusikia vile, akamshukuru tena mwenzake, akamwam- bia, “Kesho nitajitolea mwenyewe kwenda kazini!”
Asubuhi ya pili mkulima na mkewe wakenda kule bandani kumwangalia fahali huku wakiongozana na mfanyakazi. Wal- ipofika, wakamwona fahali anatimka mbio mle bandani huku akitoa mashuzi kuthibitisha kuwa yu mzimwa wa kigongo! Hapo mkulima akaanguka kicheko akacheka sana!
“Una cheka nini, mume wangu?” Akataka kujua mkewe. Mume akamjibu, “Linalonichekesha halifai kuambiwa mtu; si wewe wala si mwingine.”
Mke akashikilia lazima aambiwe; mume akakataa katakata mpaka kule nyumbani kwao kukawa hakuna tena furaha isipokuwa bughudha, manung’uniko na kununa kwa mke aliyedai sharti aam- biwe lililomchekesha mumewe siku ile.
Alipoona hali ya nyumbani mwake imekuwa mbaya, siku moja mume akamwambia mkewe, “Nitilie maji nikaoge nivae nguo tohara nisali ndipo nitakapokuambia kile kilichonichekesha siku ile; lakini ujue kuwa mimi si mumeo tena maana nikikuambia, nitakufa!”
Mke asijali; mradi atimiziwe lile alilolitaka. Basi akafanya kama vile alivyoambiwa na mumewe.
Alipokwisha sali, mume akamwambia mkewe, “Kwanza nakwenda kuwaaga wazee wangu, ndugu zangu, na jamaa zangu. Nitakaporudi, nitakuambia kilichonichekesha siku ile.”
Wakati alipokuwa akielekea kwa wazazi wake, njiani mkulima akamkuta jogoo wake amewakusanya makoo hamsini akiwabe- beza huku wote wakiwa katika hali ya furaha na ya maridhawa. Lakini mbwa wake aliyekuwa karibu na aliyekuwa amejikunyata kwa huzuni na majonzi, akamwambia jogoo, “Mbona mwenzetu huna huzuni?”
“Kwa nini niwe na huzuni?” Jogoo akataka kujua. “Unacheka na kufurahi na makoo wako ilhali unajua kuwa bwana wetu atakufa leo; huna hata huruma?” Akasema mbwa kwa huzuni.
“Nini kitakachomwua bwana wetu? Mbona namwona yu mzima wa kigongo tena anaonekana ana afya nzuri?” Akauliza tena jogoo.
“Sababu,” akajibu mbwa, “ni mkewe ashikiliaye kuambiwa neno ambalo bwana wetu akimwambia, atakufa!”
Jogoo kusikia vile akasema, “Basi bwana wetu ndiye mjinga wa mwisho! Hebu nitazame mimi; nina makoo hamsini wanitiio wote kwani nawafurahisha na nawaridhisha vilivyo bila tatizo lolote ilhali bwana wetu ana mke mmoja tu amsumbuaye na kumwumiza kichwa kutwa kucha! Kama mkewe hasikii maneno yake, basi aende dukani akanunue hainzarani amtandike mikwaju mpaka mke ashike adabu na akome kuulizauliza mambo yasiyomhusu!”
Yule bwana kusikia maneno ya jogoo, akaenda zake moja kwa moja mpaka dukani, akanunua bakora nyembamba ya mtobwe, akarudi nayo nyumbani kwake. Alipoingia ndani, akamwita mkewe chumbani. Alipokuwa ndani, akaubana mlango vizuri, akamtandika mkewe bakora za kutosha mpaka mke akakoma kuzaliwa! Mke akataka kujua sababu ya kupigwa vile; ndipo mumewe akamjibu, “Lililonichekesha siku ile na ulilialo sikuzote ndilo hili; na kama unataka zaidi sema!”
“Toba ya Rabbi!” akalia mke kwa maumivu makali huku akipiga mayowe, “Nimekoma, mume wangu, wala sitaki tena kulijua lile lililokuchekesha siku ile!”
* * *
BAADA YA Waziri Mkuu kusimulia kisa hiki, Shahrazad akasema, “Hakuna chochote kitakachonibadili nia katika jitihada yangu niliyoikusudia kuitekeleza.”
Basi Waziri Mkuu ikawa hana budi kumpamba bintiye kwa lebasi za hariri na vito vya tunu kabla hajampeleka kwa Sultani. Lakini kabla hajaondoka, Shahrazad akamwambia Dunyazad, “Mdogo wangu, nitakapopelekwa kwa Sultani, nitakuagiza uje. Usiku, kabla hakujapambazuka, uniamshe, useme, ‘Dada yangu, tafadhali nakusihi unisimulie moja ya hadithi zako tamu za kusi- simua ili nipate kuipitisha sehemu iliyobaki ya usiku huu tutaka- okuwa pamoja kwa mara ya mwisho.’ Halafu nitakusimulia visa ambavyo, Inshaallah, natumaini vitakuwa ni chanzo cha mwisho wa msiba uukabilio umati wa mji huu.”
Basi Waziri akamchukua Shahrazad mpaka kwa Sultani. Sultan Shahriyar alipoufunua ushungi wa Shahrazad, akastaajabu sana kuona uzuri wake usio kifani.
Basi usiku wa manane, baada ya starehe na maburudiko, Shahrazad akamwambia Sultani kwa unyenyekevu, “Ewe Seyyid yangu, nina mdogo wangu nimpendaye kuliko mboni za macho yangu; nataka kumuaga kabla hakuja kucha. Nakusihi niidhinie aje niagane naye kwa mara ya mwisho.”
Mara ileile Sultani akatoa amri Dunyazad akaletwe. Alipofika, akamkumbatia dada yake na kabla hakujapambazuka, akasema, “Dada yangu mpenzi, tafadhali nakusihi unisimulie moja ya hadithi zako nzuri ili tuipitishe sehemu ya usiku huu tutakaokuwa pamoja kwa mara ya mwisho.”
Hapo Shahrazad akamgeukia Sultan Shahriyar, akasema, “Itakuwa ni furaha kwangu iwapo Sultani ataniridhia.”
Sultani, ambaye hakuwa na usingizi wakati ule, akakubali na kumsikiliza Shahrazad akasimulia
KISA CHA MBILIKIMO MWENYE KINUNDU
KATIKA jiji la Basrah, akaanza Shahrazad, paliishi mshona nguo mmoja aliyefanikiwa sana katika kazi yake na aliyependa sana mambo ya starehe, anasa na mzaha. Ilikuwa ni desturi yake jioni
Sultan Shahriyar, Shahrazad na Dunyazad
kwenda na mkewe nje matembezini kujistarehesha. Jioni moja, wakati walipokuwa wakirejea kutoka katika starehe zao, njiani wakakutana na mbilikimo mmoja mwenye kinundu aliyekuwa akiwatumbuiza watu. Kwa kuwa alikuwa na nishai ya divai, yule mbilikimo akawa anapiga dumbak na kuimba kwa furaha. Mshonan- guo na mkewe walifurahishwa sana na vitendo vya yule mbilikimo; wakamwalika kwao ili usiku ule awe mgeni wao.
Walipowasili nyumbani, mshona nguo akaenda haraka sokoni, akanunua samaki mkubwa wa kuchoma, mikate ya kiajemi, zaituni, ndimu, na vitamutamu vya kumalizia maakuli.
Aliporudi navyo, wote watatu wakaketi, wakawa wanakula kile chakula. Kwa kuwa mke wa mshona nguo alikuwa ni mcheshi na mpenda mzaha, akamtilia yule mbilikimo kipande kikubwa cha samaki mdomoni, akamlazimisha akimeze. Kwa bahati mbaya, kile kipande cha samaki kilikuwa na mwiba mkali uliojificha. Yule mbi- likimo alipokimeza, ule mwiba ukamsakama kooni asipate pumzi, akaanguka chini. Walipomkagua, wakastaajabu kuona amekufa!
La Haula! Mshonanguo kuona vile, akanyanyua mikono juu, akaomboleza: “Hakuna mwenye nguvu na mwenye uwezo isipokuwa Mwenyezi Mungu aliyemwacha mtu huyu kufa kwetu ghafla namna hii!”
“Kilio chako hakitatusaidia kitu chochote,” akasema mkewe, “iliyobaki ni kutafuta njia ya kujisalimisha na maiti huyu!”
“Tutafanya nini?” Akauliza mshona nguo huku akitetemeka
Mshonanguo akagutuka kumwona mbilikimo amekufa! kwa khofu.
“Nyanyuka upesi!” Akatamka mkewe, “tutamfunika shuka na kumbeba nje usiku huu huu wakati mimi nikiongoza njia nikilia, ‘mwanangu ni mgonjwa, maskini mwanangu ni mgonjwa! Nani atatuelekeza kwa mganga?’”
Mshona nguo akalikubali shauri la mkewe; wakamfunika shuka yule mbilikimo, mshona nguo akambeba wakati mkewe akiongoza njia akiomboleza: “Maskini mwanangu ana ndui! Nani atamtibu ugonjwa huu alionao?”
Watu waliowaona na waliosikia maombolezo ya yule mwa- namke, wakawakwepa huku wakinong’onezana: “Msiwasogelee, wana ugonjwa mbaya wa kuambukiza!”
Basi mshona nguo na mkewe wakaendelea kumbeba yule mbilikimo huku wakiuliza nyumba ya mganga mpaka wakaifikia nyumba ya mganga mmoja Myahudi, wakaubisha mlango. Ulipo- funguliwa na mjakazi, mke wa mshona nguo akamweleza yule mjakazi, “Mpelekee bwana wako fedha hizi umwambie tafad- hali tunamsihi ashuke upesi chini aje amwangalie mwenzetu aliye mgonjwa sana.”
Mjakazi alipokwenda kumwita bwana wake, mke wa mshona nguo akamwambia mumewe: “Tumwache maiti hapa tutowekee upesi!”
Akisaidiana na mke wake, mshona nguo akamsimamisha wima yule mbilikimo, akamwegemeza kwenye ngazi, halafu waka- toka mle haraka, wakatoweka.
Kule juu mganga Myahudi kuona zile fedha, akashuka haraka. Wakati alipokuwa akishuka ngazi gizani, akampiga kumbo yule mbilikimo aliyeegemezwa pale ukutani, akamwangusha chini. Mganga kumtazama, akashtuka kumwona amekata roho. Akafikiri yeye ndiye aliyemwua kwa kumpiga kumbo. Lo masalale! Yule Myahudi akaomboleza kwa kutaja majina ya mitume Musa, Harun, Ezra na Joshua bin Nun!
Baada ya kufikiri kidogo, akambeba yule mbilikimo mpaka juu kwa mkewe, akamweleza yaliyotokea.
“Usisimame hapo kama nguzo!” Akafoka mkewe. “Kama maiti huyu atakutwa hapa asubuhi, ujue tutaangamia! Tumbebe haraka mpaka darini tukamtupe chini kwenye nyumba ya jirani yetu Mwislamu.”
Jirani yao alikuwa Mwislamu mtumishi katika jiko la Mfalme ambako alikuwa na tabia ya kuchelewa kurudi usiku. Nyumba yake iliyokuwa mbali na kwa Mfalme, siku zote waliingia paka waliofuata mapanya waliofuata jibini na nafaka zilizojaa mle; na usiku mbwa walikuwa na tabia ya kuingia jikoni mwake kula makombo.
Basi yule Myahudi na mkewe wakambeba yule mbilikimo, wakapanda naye juu ya dari yao, wakamshusha ndani ya nyumba ya jirani yao Mwislamu, wakamsimamisha kwenye ukuta wa jikoni,
halafu wakatoweka mara moja bila kuonekana na mtu.
Baada ya muda, yule Mwislamu, mtumishi wa Mfalme, usiku akarejea kwake, akaufungua mlango, akawasha mshumaa. Kuona umbile la mtu lililoegemea ukutani jikoni mwake, akagutuka, akatamka kwa hamaki: “Kumbe anayekula jibini na nyama humu jikoni mwangu si paka, si mapanya, wala si majibwa bali ni wewe! Kumbe nimeua bure takriban paka na mbwa wote wa mtaa huu bila kumshuku mtu! Basi leo utanitambua!”
Hapo akanyakua rungu lililokuwa karibu, akampiga nalo yule mbilikimo kifuani, akaanguka chini. Kuona hainuki, yule mtumishi akaingiwa na wasiwasi. Alipomwinamia, akapiga kelele: “Hakuna mwenye nguvu na mwenye uwezo isipokuwa Allah! Mungu ailaani jibini, nyama, na usiku huu uliokuleta hapa kwangu na mkono wangu ukawa ndio sababu ya kifo chako!”
Na alipoona aliyemwua ana kinundu, yule Mwislamu aka- ongeza: “Lahaula! Kuwa na kinundu haikutosha ukaongeza na wizi juu! O Allah, nirehemu kwa kitendo changu kiovu!”
Usiku ulikuwa ukianza kutoweka polepole na mapambazuko yalikuwa yakikaribia wakati yule mtumishi alipombeba yule mbi- likimo akatoka naye nyumbani mwake. Akaelekea naye moja kwa moja mpaka sokoni. Wakati huo barabara zote zilikuwa tupu hazina watu. Alipofika sokoni, akaendelea na mzigo wake mpaka kwenye duka moja. Hapo akamwegemeza yule mbilikimo kweye ukuta wa lile duka, akatoweka zake!
Baada ya muda, Mkristo mmoja, ambaye alikuwa ni mhasibu wa Mfalme, akapita pale akielekea kwenye hamamu ya jiji. Kwa kuwa alikunywa divai nyingi usiku ule, akawa anayumbayumba huku na huko akijisemea: “Mwisho wa dunia umewadia!”
Alipokaribia pale pa yule mbilikimo, akasimama, akaanza kukojoa bila kumwona yule mbilikimo aliyeegemezwa pale. Ilitukia kuwa mapema jioni iliyotangulia yule Mkristo aliwahi kunyang’anywa kilemba chake na ikambidi anunue kingine.
Basi alipokuwa akikojowa, mara akamwona yule mbilikimo,akafikiri ni mwizi anayemvizia anayetaka kumnyang’anya tena kilemba chake kipya! Mkristo akamrukia yule mbilikimo, akamkaba roho, akamwangusha chini huku akimtwanga magumi na kupiga makelele ya kumwita mlinzi wa pale sokoni.
Mlinzi alipofika, akamwona Mkristo amemkalia yule mbi- likimo kifuani huku akimpiga.
“Nyanyuka na wacha kumpiga Mwislamu” Akafoka yule mlinzi; na alipomwona yule mbilikimo amekufa, mlinzi akapiga mayowe ya mshangao akiita: “Jamani njooni! Jambo baya sana limetokea! Mkristo amemwua Muumini!”
Majuto mjukuu! Kuona yale aliyoyafanya, yule Mkristo akaanza kumwomba Yesu na Maria na kujuta kwa ulevi aliounywa usiku ule.
Yule mlinzi akamkamata yule Mkristo, akamtia pingu, akampeleka moja kwa moja mpaka nyumbani kwa hakimu mkuu wa jiji.
Asubuhi aliposimuliwa yaliyotokea, hakimu akatoa amri yule Mkristo anyogwe. Hapo mnadi akapiga mbiu ya mgambo, akatangaza mabarabarani kosa la yule Mkristo na mahali ataka- ponyongewa kesho.
Wakati wa kunyongwa ulipowadia, halaiki ya watu ikajiku- sanya katikati ya jiji kwenye uwanja mkubwa kuja kushuhudia kunyongwa kwa Mkristo. Baada ya muda, mnyongaji akatokea huku hakimu mwenyewe akiwa haadhir. Mnyongaji akamtia yule Mkristo kitanzi shingoni, akawa anasubiri amri kutoka kwa hakimu.
Mara yule Mwislamu, mtumishi wa Mfalme, akajitokeza mbele ya ule umati wa watu huku akipiga makelele: “Tafadhali usimnyonge! Muuaji si yeye bali ni mimi! Mimi ndiye mwenye hatia niliyemuua yule mbilikimo!”
Hakimu kusikia maneno yale, akamhoji: “Kwa nini umemuua?”
“Mauaji yake yametokea,” akajibu Mwislamu, “wakati niliporejea nyumbani kwangu jana usiku. Nilimkuta jikoni mwangu, nikampiga rungu, akaanguka chini, akakata roho. Kwa kuwa nili- ogopa, nikambeba mpaka sokoni. Hivyo, ni mimi ndiye niliyemuua Mwislamu mwenzangu. Basi mimi ndiye nistahiliye kunyongwa si huyu Mkristo. Sitaki roho ya Mkristo itolewe kwa kosa nililolifanya mimi.”
Aliposikia hayo, hakimu akamwachia yule Mkristo, akamwa- muru mnyogaji amtie kitanzi yule Mwislamu aliyekiri kosa lake.
Mnyongaji akamwongoza yule Mwislamu, akaelekea naye mpaka kwenye kitanzi. Alipokitundika shingoni mwake, mara yule mganga Myahudi akajitokeza hadharani akipiga kelele: “Ngoja, usimnyonge! Huyo Mwislamu hana kosa bali mimi ndiye niliye- muua huyo mbilikimo mwenye kinundu!”
Yule Myahudi naye akaeleza jinsi alivyomuua mbilikimo halafu akaongeza. “Je, dhambi yangu ya kuua mtu haitoshi? Ni lazima mwingine auawe kwa kosa nililolifanya mimi?”
Kusikia vile, hakimu akatoa amri yule Myahudi anyongwe badala ya yule Mwislamu. Lakini kitanzi kilipotiwa shingoni mwa Myahudi, mara mshona nguo naye akajitokeza mbele, akakapiga kelele: “Jamani, msimnyonge Myahudi! Hakuna yeyote aliyemuua mbilikimo isipokuwa mimi!”
Na yeye naye akaueleza ule umati uliohudhuria pale jinsi alivyomuua yule mbilikimo mwenye kinundu.
Hakimu kusikia vile akastaajabishwa sana na kisa cha yule mbilikimo mwenye kinundu, akatamka: “Kisa hiki kinastahili kuandikwa.” Hapo akatoa amri yule Myahudi aachiliwe na badala yake anyongwe yule mshona nguo.
“Inavyoonekana,” akalalamika mnyongaji, “leo jua litakuchwa bila yeyote kunyongwa!”
Ilitukia kuwa yule mbilikimo mwenye kinundu alikuwa mcheshi na mfurahishaji kipenzi wa Mfalme. Alipoona mcheshi wake hajafika kwenye kasri lake usiku kucha na asubuhi ya pili, Mfalme akatoa amri akatafutwe. Waliotumwa wakarudi, wakamwarifu Mflame kifo cha mbilikimo wake na jinsi kila mmoja wa wale watu alivyokiri kosa la kumuua.
“Nenda haraka kwa hakimu ukawalete mbele yangu wote hao waliokiri hilo kosa.” Akaamuru Mfalme.
Mjumbe akatoka haraka, akaelekea kule ambako mnyongaji alikuwa tayari kukikaza kitanzi shingoni mwa mshona nguo.
“Ngoja! Ngoja! Usimnyonge!” Akapiga kelele yule mjumbe wa Mfalme huku akijipenyeza katika ile halaiki ya watu iliyo- hudhuria pale. Kabla mnyongaji hajakivuta kitazi, yule mjumbe akamwarifu hakimu amri ya Mfalme. Hakimu naye, bila kuchelewa, akawapeleka wote kwa Mfalme: mshona nguo, Mriskto, Myahudi, Mwislamu mtumishi wa Mfalme, na ile maiti ya yule mbilikimo mwenye kinundu.
Wote walipofikishwa mbele ya Mfalme, wakajiangusha ki- fudifudi chini, wakaibusu sakafu, halafu kila mmoja wao akaanza kueleza yaliyompata.
Mfalme akastaajabu sana, akaamuru kile kisa kiandikwe kwa wino wa dhahabu. Halafu akawauliza wote waliokuwa haadhir: “Je, mmepata kusikia kisa cha ajabu kama hiki cha huyu mbilikimo mwenye kinundu?”
Yule Mkristo aliyehusika na kile kisa cha mbilikimo mwenye kindundu akawa wa kwanza kujitokeza mbele, akamsimulia Mfalme na waliokuwa hadhirina kisa kifuatacho:-
KISA CHA MKRISTO
“Seyyid yangu,” akaanza yule Mkristo, “mimi si mwenyeji wa hapa bali ni mwenyeji wa Misri na muumini wa madhehebu ya kikoptiki. Nimekuja hapa kuleta bidhaa mbalimbali kutoka kwetu kwa madhumuni ya kufanya biashara. Baba yangu alikuwa dalali mkubwa aliyejulikana sana. Alipofariki, nikaendelea na kazi yake.
|
|
|
HADITHI YA SADIKI NA SIKIRI (CHITEMO) |
Posted by: MwlMaeda - 08-20-2021, 07:45 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
|
|
Sadiki ni mtoto anayeishi karibu na Ujiji. Anaye ndugu yake aitwaye Sikiri. Sadiki na Sikiri husoma katika shule ya Businde.
Sadiki anafanya kazi zote kwa bidii. Lakini Sikiri ni mtoto mbaya kwa sababu ni mvivu, kaidi, tena hana adabu.
Siku moja wakati wa livu baba yao aliwaamsha mapema sana. Akasema, “Sadiki, chuukua hii shilingi. Nenda sokoni ukanunue samaki.
Na wewe Sikiri, nenda kisimani ukateke maji.” Wote wawili wakaenda. Sadiki alinunua samaki, akarudi nyumbani haraka.
Lakini Sikiri alichelewa. Baba yake akamngoja mpaka akachoka.
Baba akatoka kwa hasira kumfuata Sikiri kule kisimani. Alipofika alimkuta anachezea maji.
Anayateka na kuyamwaga juu ya jiwe. Baba yake akamwuliza, “Unafanya nini Sikiri? Mbona unacheza tu? Teka maji, twende nyumbani.” Sikiri akateka maji, wakarudi nyumbani.
Walipofika nyumbani walimkuta mama amekwisha tayarisha uji. Wakanywa.
Walipomaliza, baba yao akawaambia, “Twendeni tukapalilie bustani ya mboga. Mama atabaki hapa nyumbani. Atalisha kuku na kusafisha nyumba. Baadaye atatayarisha chakula.”
Kule katika bustani kulipandwa mchicha, maharagwe, vitunguu na nyanya. Magugu na manyasi yaliota kwa wingi. Sadiki, Sikiri na baba yao walipalilia kwa uangalifu ili wasiharibu mimea ya mazao.
Sikiri hakupenda kazi. Kwa hiyo alitoroka akaenda kichakani. Kule kichakani alitafuta matunda mwitu. Sikiri alikuwa mtoto mvivu kweli. Hakutaka kufanya kazi kwa bidii. Sadiki na baba yake waliporudi nyumbani, akawafuata.
Walipofika nyumbani chakula kilikuwa tayari. Sikiri alikuwa wa kwanza kunawa mikono na kuanza kula. Siku ile mama alipika ugali na samaki alionunua Sadiki. Walipokwisha kula, baba alimwita Sikiri akamwuliza, “kwa nini leo alitoroka?” Sikiri alinyamaza tu. Sakiri alikuwa mtoto mkaidi. Baba akamwambia, “Kesho utakwenda kupalilia bustani. Usipokwenda hutapata chakula.”
Siku iliyofuata Sikiri alikataa kwenda bustanini, alitoroka. Sadiki na baba yake walikwenda kupalilia peke yao. Jioni waliporudi, baba alimwuliza mama, “Sikiri amekwenda wapi?” Mama akajibu, “Mimi leo sijamwona nyumbani. Sijui amekwenda wapi.” Kumbe, siku ile asubuhi Sikiri alipanda basi kwenda mjini Kigoma. Huko njiani aliulizawa nauli . Sikiri hakuwa na pesa hata kidogo. Dereva akamtelemsha pale pale. Akaachwa peke yake. Sikiri alilia sana .
Mwisho akaanza kusema kwa uchungu:-
Sikiri mimi maskini,
Uvivu wangu nyumbani,
Ukiwa huu njiani,
Nakufa hapa kwa nini?
Sadiki sasa ashiba,
Chakula kingi kwa baba,
Nirudi tena kwa baba,
Nakufa hapa kwa nini?
Sikiri alirudi nyumbani. Alikuwa amechoka sana. Alipofika nyumbani aliomba radhi. akamwambia baba na mama.
Naomba radhi nimekosa,
Nitakuwa mtoto mwema sasa,
Shambani tena sitakosa,
Baba na mama nisameheni .
Nitalima kama Sadiki,
Nitalima wala sichoki,
Na nyumbani tena sitoki
Baba na mama nisameheni.
Baba hakumpiga Sikiri. Alimsamehe.
Sikiri akabadili tabia yake, akawa anawasaidia wazee wake. Kila alipotumwa alikwenda upesi. Mama yake alifurahi, akamwambia, “Siku hizi wewe ni mtoto mwema kama Sadiki. Mtoto mtii hupendwa na wazazi wake. Tena hupendwa na watu wote kijijini. Endelea kuwa mtoto mwema na mtii.
|
|
|
SIMULIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 1… |
Posted by: MwlMaeda - 08-20-2021, 07:35 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
|
|
…SEHEMU YA 1…
Mpuzu Yahimana,kijana wa Kiafrika, alipanda ukuta mkubwa uliojengwa kwa mawe, huku akiwa makini asionekane na askari wa kizungu walioizunguka ngome yote ya kikoloni kudumisha ulinzi.Moyo wake ulikosa furaha, macho yake yalitamani kuona sura ya mtoto mrembo wa kizungu kwa mara nyingine tena tangu siku iliyopita. Uvumilivu ulimzidi nguvu, hisia za mapenzi zikamuandama, licha ya ngozi nyeusi aliyokuwa nayo, aliapa kumpata mtoto wa gavana Richald Roben kwa gharama yoyote ile …
“Sijui anajua kiswahili?lakini nitamfundisha, ngoja nichungulie, labda nitamuona tena angalau moyo wangu upate faraja …”!Mpuzu Yahimana aliongea, mikono yake miwili ilikamatilia kwa nguvu mawe ya ukuta imara wa ngome ya kikoloni, moyo wake haukua na hofu juu ya kifo na kunyongwa kikatili iwapo akikamatwa, moyo wake ulimuwaza Angel Richald, mtoto wa kipekee wa gavana wa Kiingereza katika nchi ya Goshani. Mpuzu aliendelea kukwea ukuta, huku kila mara akiangaza mashariki, kutazama kama jua linachomoza, lakini aliambulia wingu la ukungu lililosababishwa na baridi kali majira ya asubuhi.
“Jua lisipochomoza!mtoto wa gavana hatatoka kuota jua sababu ya baridi, lakini inabidi niendelee kupanda juu, muda sahihi ni huu, walinzi wanaamini hakuna Muafrika anayejiamini na kuvuka ukuta huu mkubwa, tena majira haya,bila kujua yupo Muafrika hodari Mpuzu Yahimana, mjukuu wa Yahimana kiongozi mkuu wa Manamba katika koloni hili la Waingereza miaka ishirini iliyopita “,Mpuzu aliongea, kichwa na mwili wake ukitoa mvuke, kutokana na baridi kali ya asubuhi.
Mpuzu alikua tayali kuteseka,kuumia na kufa,sababu ya penzi
.Hatimaye safari ilifika Ukingoni, majumba ya Kizungu yalianza kuonekana,Mpuzu akiwa umbali wa futi hamsini kutoka chini.Tabasamu likaipamba sura yake kufika mwisho wa ukuta, jua nalo lilichomoza ,katika wakati sahihi ambao Mpuzu aliutarajia.
“Ewala! jana alikuwa amekaaa pale kwenye zulia, bila shaka hata leo atakaa pale kuota jua, eee mizimu ya mababu nisaidieni nitimize lengo langu, nitoke salama mahala hapa ………”,Mpuzu aliongea huku akiomba ulinzi wa mizimu ya mababu imlinde, kwani ilikuwa ni kosa la jinai kwa Muafrika yoyote yule kukanyaga ngome ya kikoloni, makazi ya wazungu, waarabu pamoja na wahindi.
…………………………………
The great Fort (Ngome kubwa);
Siku tatu zimepita tangu akanyage Afrika,awali alifikili ni bala tajiri kama Ulaya, kinyume na matarajio yake, Afrika ilijaa mashamba makubwa ya mikonge, mashamba yaliyomilikiwa na wazungu, huku Waafrika wakifanyishwa kazi kwa nguvu na kulipwa senti moja tu kwa masaa kumi na mbili shambani.
Hamu ya kutaka kujua koloni walilotawala wazazi wake ilimwishia, akiwa na siku moja tu, alitaka kuondoka Goshani na kurudi Uingereza.
“Subili mwanangu, wait two weeks to come, i will take you back to British (subili wiki mbili zijazo, nitakurudisha Uingereza) “,ni maneno ambayo Angel aliambiwa, kila alipozungumzia swala la yeye kurudi Uingereza mbele ya baba yake.
Ghafla wazo la yeye kurudi Uingereza likatoweka, fikra mpya zikatawala kichwa chake, moyo wa Angel ukazama katika penzi la kijana wa Kiafrika, kijana Mpuzu Yahimana aliyeingia ngome ya Kikoloni siku iliyopita akiwa na manamba wenzake, wakiwa wameleta mazao ya katani kwenye ghala la kuhifadhia mazao, kabla ya kusafirishwa kwa meli kupelekwa Uingereza.
Usiku hakula chakula, hakuna mtu angemshirikisha tatizo lake akamsaidia, tofauti na kawaida yake, alilala mapema kupumzisha kichwa chake,kichwa kilichojaa mawazo mengi, kwani aliwaza na kuwazua namna ya kuwa karibu na kijana yule wa kiafrika, na mahali pa kumpata bila majibu yoyote yale. Kutokana na badiliko la ghafla, gavana Richald Robeni alifikili mwanae anaumwa kumbe sivyo.
Asubuhi na mapema, jua lilichomoza, Kama kawaida yake, Angel alitoka nje ili aweze kuota jua. Alitoka nje, huku kichwa chake kikitafakali namna ya kumdanganya baba yake, ampatie ruhusa ya kutembelea makazi ya Waafrika, suala ambalo lilikuwa ni gumu mithili ya chatu kummeza tembo.
“,Fliiiiii ,fliiiii ………”,mlio kama filimbi ulisikika, Angel akiwa ameketi kwenye Zulia akiota jua alitazama huku na kule, hakuona chochote kile …
“,What is this? Oooh nothing!”,(Hii ni nini?, ooh hakuna kitu), Angel alizungumza peke yake baada ya kusikia mlio wa filimbi, alipogeuka huku na kule hakuona kitu chochote, akaendelea kuota jua.
“Fliiiii, Fliiiii ……”,filimbi ilisikika tena, Angel akageuka kwa mara nyingine, hakuamini alichokiona, kijana wa kiafrika aliyemkosesha usingizi alikuwa juu ya ukuta akimchungulia, uvumilivu wa mapenzi ukamshinda, hofu ya Mpuzu kudondoka chini ikamuandama Angel, bila kutambua kuwa Mpuzu alikuwa kijana hodari zaidi ya anavyofikilia.
“,Come down please, your not safe over there, you can die ……”,(Njoo chini tafadhali, hauko salama mahala hapo, unaweza kufa), “Kwa lugha ya kizungu Angel alizungumza, lakini Mpuzu hakuelewa chochote kile, jambo ambalo lilipelekea askari wa kizungu kushtuka, kwani Angel alionekana akiongeea na mtu fulani juu ya ukuta na kuhatarisha usalama wake……
“,Paaaaa! paaaa! paaa………”,risasi zilifyatuliwa juu ya ukuta alipokuwa Mpuzu,Mpuzu alimrushia cheni Angel, cheni ambayo Angel aliipokea kwa ustadi mkubwa bila askari yoyote yule wa kikoloni kugundua, huku akiitazama na kuishangaa zawadi ile.
“Paaap! paaaa! ……”,askari wa kikoloni waliendelea kumshambulia Mpuzu bila kumtambua vizuri sura yake ,kwani alikua mbali kabisa juu ya ukuta.
“,Aaaaaaa! “,Mpuzu alitoa ukelele, akalalamika kwa uchungu.
“,Puuuuuh! “,kishindo kilisikika upande wa pili, Mpuzu alidondoka chini ,baada ya kuachia mikono yake miwili, wakati wa kukwepa risasi kuikomboa nafsi yake.
“,Zungukeni, zungukeni upande wa pili,! aletwe hapa, stupid boy! “,askari mmoja wa kikoloni, aliwaamrisha na kuwatawanya wenzake kutoka nje ya ngome kubwa(the great fort), kwenda kumkamata Mpuzu Yahimana.
“,I hate you, I hate you! if you kill him, i will also kill you ………”,(nawachukia, nawachukia!, kama mtamuua na mimi nitawaua ),Angel alifoka kwa hasira na kukimbilia ndani, hakuna aliyejali kelele zake, askari wa kikoloni walipishana kukamata silaha kwenda kumtafuta Muafrika aliyekanyaga ngome yao maarufu kama ngome kubwa (the great fort) na kuichafua.
Mpuzu Yahimana alinyanyuka kwa shida huku akiugulia maumivu, hakuwa tayali kukamatwa na askari wa kikoloni, njia pekee ya kuepuka kifo ni kukimbilia msituni. Safari ya kutokomea mafichoni ilianza haraka haraka ,kabla hawajamkalibia.
…………………………………
Makazi duni; (Slums area)
Magari ya kikoloni yaliingia kwa fujo katika makazi ya Waafrika, askari wa kikoloni walibeba silaha pamoja na mijeledi mikononi, huku sura zao zikikunjamana kwa hasira.
“Mtu yote itoke kwenye slum! sisi tafuta pumbavu moja kuja ingia kwa ngome yetu this morning! “,askari mmoja wa kikoloni alizungumza, akiwa amevalia shati jeupe, pamoja na kaptula, mguuni alivalia viatu vyeusi vilivyong’arishwa na rangi nyeusi,kiunoni alivaa mkanda, mkanda uliounganishwa mpaka mabegani, sare kamili ya jeshi la kikoloni!
“Every family should get out of their slums!, if any member of your family is missing, you will be in trouble all of you ……”,(Kila familia inapaswa kutoka nje ya kibanda chao,kama mtu yoyote katika familia anakosekana,nyote mtakua kwenye matatizo), “askari mwingine alifoka kwa kizungu,huku akitumia mjeledi wake kutoa Waafrika katika vibanda vyao vilivyoezekwa kwa nyasi.
Familia zilipanga mistari,kisha wakubwa kwa wadogo wakachapwa viboko, baada ya mtu mmoja kukosekana. Huku wakihimizwa kutaja mtu aliyekosekana, kwani hakuna manamba wowote waliokuwa tayali wameelekea katika mashamba ya wakoloni.
Kisu cha moto kikachemshwa, wazee wote walitakiwa kukatwa vidole, huku dawa ikiwa ni kumtaja mtu aliyekosekana …
“Mpuzu Yahimana, mwanangu hayupo! msiwahukumu wasio na hatia! “,baba yake Mpuzu alizungumza na kupiga magoti mbele ya askari, pamoja na viongozi wa kikoloni, bila kutegemea, askari walimkamata yeye pamoja na familia yake,walifungwa kamba, kisha wakapakiwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa gerezani …
…ITAENDELEA …
Usikose riwaya hii ya kusisimua,je nini mwisho wa penzi la Mpuzu na Angel kwenye vikwazo vingi vya Ubaguzi na ukatili kutoka kwa Wakoloni …
Mtunzi; Hakika Jonathan
0629905923
|
|
|
SIMULLIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 10… |
Posted by: MwlMaeda - 08-20-2021, 07:31 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
|
|
…SEHEMU YA 10…
Msitu wa mikoko;
Mlio ya magari ulisikika, mwangwi ukasikika na kupenya sehemu zote za msitu wa Mikoko, Mpuzu akapanda juu kabisa ya mti wa ubuyu, alitaka kudhibitisha kama sauti zilizosikika zilikua za magari ya kikoloni,akiwa juu ya mti wa ubuyu, aliona msafara wa magari ya wazungu mia moja, kilomita takribani tano kutoka msituni, akashuka haraka juu ya mti, kuwapatia taarifa Waafrika wenzake.
“,Wanakuja, sio muda mrefu watakua mahali hapa,nazani wanawake na wazee wako mahali salama kwa sasa, lakini wanapaswa kutulia kimya, wasipige kelele, vijana kumi wenye silaha pandeni juu ya mti huu wa ubuyu, wengine pandeni kwenye miti mingine karibu na mitego ilipotegwa ……”,Mpuzu Yahimana aliongea, Angel alikuwa pembeni yake,vijana kumi wakapanda juu ya mti mkubwa wenye urefu wa futi mia moja kwenda juu, mti uliojaa matawi na kuficha Waafrika, wanawake, wazee pamoja na watoto.
Vijana na wanaume wa kiafrika wenye nguvu, wakapanda kwenye miti karibu kabisa na mitego waliyotega, kwa ajili ya mashambulizi. “,Unaenda wapi? baki utakufa, si salama tunapoelekea, “Mpuzu alimfokea dada yake Mwamvua, aliyetaka kuongozana nao, kwenda kupambana, mkononi hakuwa na silaha nyingi zaidi ya panga kubwa katika mkono wake wa kulia.
“,Siwezi kufa kirahisi,hata nikifa,nitakuwa nimekufa kishujaa,naenda kupigania uhuru wa nchi yangu…”,Mwamvua akiwa na nyuso isiyo na tabasamu wala furaha aliongea,alidhamiria kupambana kufa na kupona kupata uhuru wa nchi yake, haijalishi alikuwa na umri kiasi gani.
“,Let her go with us, she know how to fight, anajua kupigana, alipiga white people kule kwa great fort ,muache aende na sisi…”,Angel alimtetea wifi yake mtarajiwa, alishuhudia kwa mara ya kwanza Mwamvua alivyowatia adabu askari wa kizungu katika ngome ya wakoloni,siku mbili zilizopita,tangu siku hiyo alimuheshimu Mwamvua, msichana mdogo mwenye umri wa miaka kumi na tatu tu.
“,Sawa, twende, lakini kuwa makini, maana hujapona vizuri majeraha yako……”,Mpuzu aliongea, akamruhusu mdogo wake kuongozana naye, wote wakakwea miti,wakiwa na silaha za jadi isipokuwa Angel peke yake aliyekuwa na bastola mkononi, bastola aliyotoka nayo katika ngome ya wakoloni.
…………………………………
Jenerali Agustino Darwini aliongoza msafara, kundi la pili la askari mia tatu wa kikoloni,wakafuata njia ndogo iliyopita mkono wa kulia wa kibao chenye jina la msitu,wakaanza kuingia katikati ya msitu.Wakijiamini kwani silaha za Waafrika,silaha za jadi, hazikuwa na uwezo wa kufua dafu mbele ya silaha za wazungu, bunduki pamoja na miripuko ya mabomu.
“,Chochote kitakachotokea mbele ya macho yako,just kill, ua kuyakomboa maisha yako, bila hivyo jeshi lote litapata adhabu kutoka kwa gavana, hakikisha unarudi na kichwa cha Muafrika katika ngome kubwa……”,jenerali wa kikoloni, Agustino Darwin aliongea kwa kiswahili safi kabisa, akiwa mbele kabisa ya askari mia tatu wa kundi lake, macho yake yaliangaza mbele pamoja na msituni, akasahau kuangalia chini pamoja na juu ya miti, mahali walipojificha Waafrika.
Safari ilipamba moto,kundi la jenerali Agustino likaingia katikati ya msitu, macho yao yaliangaza mbele, pamoja na kona zote za msitu, wakapuuzia kuangalia juu ya miti, waliamini Waafrika wangejificha vichakani, mahali salama na vigumu kuonekana, kinyume kabisa na fikra zao, vijana hodari wa Kiafrika walikua juu ya miti ,wakiwaona vizuri askari wa kikoloni,wakijipanga namna ya kuwashambulia, wakawasubili wasogelee mitego yao, ili wawashambulie vizuri.
“,ooooh, help me!, help me!, nisaidieni ,…”,
“,Paaaa, paaaa, paaa …”,
“,Hel…p…me. …,nak…ufa ” ,
kelele zilisikika, jenerali Agustino alipiga kelele kuomba msaada,alijikwaa kwenye mtego wa kamba bila kutegemea, mguu wake ukaburuzwa na kamba mita kadhaa, askari wake wakashambulia bila mafanikio, gogo kubwa lilitoka juu ya mti na kutua katika tumbo la jenerali Agustino Darwin, damu nzito ikatoka mdomoni, mapuani na masikioni, jenerali wa askari wa kikoloni akafa palepale. Askari wake wakabaki wamepigwa na butwaa, kundi lote la askari wa kizungu wakashusha silaha zao mikononi mwao, wakausogelea mwili wa kamanda wao kuuchunguza. Wakiwa hawa amini kile kilichotokea.
“,Amekufa …”,
“,Yes, tayali amekufa, bastard Africans! “,
“,What this, wametuua sana,hii ni dharau, we must show them respect …”,
“,Foolish Africans, wapumbavu kabisa,tukiwakamata,there is no mercy…”,
Kundi la pili la askari wa kikoloni,kundi ambalo liliongozwa na jenerali Agustino Darwin,waliuzunguka mwili wa kiongozi wao,bila tahadhari yoyote,huyu alisema hili,yule akasema lile,bila kutambua uwepo wa maadui zao juu ya miti.
“,Pyuuu,pyuuu,pyuuu…”,
“,Yalaaa,am dying,nakufaa…”,
“,Pyuuu,pyuuu…”,
“,Aaaaaaah…”,
“,Run,run,kimbia,take your guns,shoot them,washambulie……”,
Ghafla kundi la askari wa kikoloni wakashambuliwa,zaidi ya askari kumi wakafa papo hapo,wengine wakafarakana,wakakimbilia msituni,kila mtu njia yake,hawakutambua mahali mishale iliweza kutokea,hawakufahamu mahali walipojificha maadui zao,ghafla mashambulizi yakasimama ,msitu ukawa kimya,kelele na vilio vya wakoloni ndivyo viliutawala msitu.
Askari wa kikoloni takribani ishirini walikimbilia mbele baada ya kushambuliwa, huku macho yao yakiwa bize kuangaza mbele yao, bunduki zao zilikuwa mikononi tayali kwa ajili ya kushambulia adui yoyote yule, hawakujua mahali walipokuwa wanakimbilia kama kulitegwa mitego, pia kulikuwa na askari wa Kiafrika wakiwa wamejiandaa kwa ajili ya kufanya mashambulizi.
“,Go, go, songa mbele, usiogope,be strong …”,
“,don’t worry boss, tutakamata watu nyeusi yote …”,
“„Let’s move, kimbia, songa mbele …”,
Kundi la askari ishirini lilitangulia mbele, likawaacha wenzao nyuma, baada ya kushambuliwa, wengine wakauawa na wengine kutokomea msituni kuyaokoa maisha yao, baada ya kushikwa na taharuki mara tu baada ya kushambuliwa. Kundi likasonga mbele, kila mmoja akimtia moyo mwenzake, walijiamini, waliiamini rangi yao, wakawadharau Waafrika, waliamini lazima watalipiza kisasi na kuwakamata Waafrika,na kuwapatia adhabu kali ikiwemo kunyongwa na kazi ngumu za shambani bila chakula wala maji.
“,yalaaaa, fu…ck…you, foolish Afric…ans,naku…faa …”,
“,don’t move, msije, sima…m…a …”,
“,Puuuu …”,
“,Yalaa…aa, you ki…lled
us (mmetuua) “,
Ghafla askari mmoja aliyekuwa mbele akatumbukia ndani ya shimo, baada ya kukanyaga mtego, akapiga kelele huku akitukana matusi ya kila aina,mwingine tena akatumbukia shimoni, akapiga kelele, akawaonya wenzake wasimame mahali walipo, hawakusikia, wakasogea mbele bunduki zao zikiwa mikononi, walitaka kuwakomboa wenzao waliotumbukia shimoni, wakajikuta wanakanyaga mahali pasipo stahili, kundi lote la watu kumi na nane waliokuwa wamebakia wakatumbukia shimoni, wakapiga kelele za maumivu, visu vilivyokuwa vimetegwa shimoni vikawachoma choma,mwingine kifuani, mwingine tumboni, wakafa palepale, ukimya ukatawala tena ndani ya msitu.
…………………………………
Gavana Richald Robeni, mke wake malikia Magreth, askari mia tatu pamoja na baadhi ya viongozi wa kikoloni walipita upande mwingine wa msitu, upande wa kushoto ambao haukuwa na mitego yoyote iliyotegwa, isitoshe Waafrika hawakujificha katika upande huo wa msitu.
Gavana na kundi lake walisonga mbele, walikuwa makini sana, waliangaza pembe zote za msitu kwa umakini wa hali ya juu, silaha zilikua mikononi mwao, macho yao yaliangaza mita mia moja mbele, juu na chini, kushoto na kulia. Laiti kama wangepita upande wa kulia, mahali walipo jificha Waafrika,kwa umakini walio nao,bila shaka wasingepata madhara makubwa, pengine wangetambua mahali walipo jificha maadui zao.
“,Yala…aa, nakuf…aa, fuck you,……”,
“,paaa, paaa, paaa! “,
Ghafla gavana alisimamisha msafara, alisikia kelele na milio ya risasi upande wa pili wa msitu, hakuona haja ya kuendelea kusonga mbele.
“,let’s go back!,twendeni upande wa pili wa msitu, huko ndiko kuna maadui,”
“,listen, listen, they are shouting, wanapiga kelele mingi huko, wanashambuliana …”,
“,My daughter jamani,let them not kill my daughter, wasimuue mwanangu ……”,
Kundi lote liligeuka nyuma, kila mmoja alisema neno lake, baba yake Angel Richald Robeni aliwahofia askari wake kuuawa, mama yake Angel alihofu mwanae kuuawa, baada ya kusikia milio ya risasi na kelele za vilio, wote wakaanza kurudi nyuma wakikimbia, upande wa pili wa msitu.
…ITAENDELEA …
Usikose vita ya msituni,Waafrika na wakoloni wazungu, Itakuwaje?, usikose sehemu ijayo …
|
|
|
SIMULLIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 11… |
Posted by: MwlMaeda - 08-20-2021, 07:24 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
|
|
…SEHEMU YA 11…
Msitu wa mikoko;
Mpuzu Yahimana aliongoza mashambulizi,waliwashambulia kwa mishale askari wa kikoloni, walipojaribu kuwasaidia wenzao waliojeruhiwa na mitego iliyotegwa na Waafrika, askari wa kikoloni hawakutambua mahali adui zao walipojificha, ilibidi wakimbilie vichakani, kila mtu njia yake, kuziokoa nafsi zao …
“,Tushukeni chini, tuwafuate porini, wengine wakusanye bunduki za maadui tuliowaua,tuzihifadhi mahali salama,maana vita haiishi leo wala kesho……”,Mpuzu aliongea, wote wakakubaliana naye,wakateremka juu ya miti, askari takribani therathini, akiwemo Angel Richald pamoja na Mwamvua.
“,Tufanye haraka, maadui bila Shaka na wao wanatutafuta, “Mwamvua aliongea.
“,Kweli kabisa, kweli kabisa, tufanye haraka! “,mzee Nyamigo aliongea kwa mkazo, akitikisa kichwa,akashika tawi la mti, akaning’inia kama nyani, akaruka chini…
dakika tatu zilitumika,kundi moja la askari lilikuwa chini, wakaanza kuokota silaha,kutoka kwa Wazungu waliouawa baada ya kutumbukia shimoni, huku wengine wakishambuliwa na mishale,waliendelea kukusanya bunduki, wakawasachi mifukoni, wakawanyanganya mabomu waliyokuwa wameweka katika mifuko yao, Mpuzu alikuwa bize akiangalia kila kona ya msitu, akichunguza usalama, wenzake wakiwa wanakusanya silaha kutoka kwa wazungu waliopoteza maisha.
…………………………………
Kundi la pili la Waafrika, kundi ambalo liliongozwa na Ishimwe, walimaliza kushambulia, waliua askari wa kizungu wengi sana, zaidi ya hamsini, huku kiongozi wao wa kizungu, jenerali Agustino Darwin akiuawa vibaya na gogo ambalo lilitegwa na kumpiga tumboni.
“,Leo kapatikana, roho yake mbaya, imesababisha afe kifo kibaya, ona sasa …!”,Ishimwe aliongea,akiwa pamoja na kundi lake la askari therathini, wakiutazama mwili wa kamanda wa kikoloni, jenerali mkatili ambaye aliwachukia sana Waafrika.
“,Puuuu, puuuu … “,..
“,Muache,ameshakufa! “,
“,Wacha nimtie adabu! “,
“,Achana naye,tayali ameshakua mzoga ……”,.
“,Pumbafu sanaa, ngozi nyekundu kama nyanya, harafu unajifanya mjanja, leo umepatikana! “,
Mpuzu alimshika kijana mwenzake, aliyekuwa na hasira kupita kiasi, licha ya Agustino Darwin kupigwa na gogo tumboni,akakata roho, lakini kijana huyu alikuwa bado ana hasira naye, alimpiga ngumi tumboni, akimtukana matusi ya kila aina, alichoshwa na ukatili wa jenerali huyu aliokuwa akiwafanyia.
“,Wengine okoteni silaha tuondoke, watatushambulia,wameingia vichakani,…”,
“,tushamaliza, ”
“,kama mmemaliza, turudini nyuma tukaonane na wenzetu! “,
“,Sawa, sawa …”,
Walimaliza kuokota bunduki za wazungu, wakarudi nyuma,kuonana na wenzao, kundi la Mpuzu.Macho yao yaliangaza mita hamsini mbele, hamsini nyuma, kulia na kushoto, walikuwa makini wasije wakashambuliwa na askari wa kikoloni waliokimbilia vichakani, walipo washambulia awali na kuwazidi nguvu.
…………………………………
Makundi yote mawili, makundi ya askari wa Kiafrika, yalikutana pamoja, wakiwa na machale, walijadiriana namna ya kuendeleza mapambano dhidi ya wazungu,ili kupigania uhuru wao …
“,Wameingia vichakani, tuwafuate! “,
“,Hapana, huko sio salama, tutakufa! “,
“,Kweli, mahali salama kwa mashambulizi, ni juu ya miti, turudini huko, wakija maeneo haya tuwashambulie !”,
“,Wazo zuri, tufanye hivyo! “!
“,Jamani, sikieni, hamsikii sauti za miguu, kuna watu wanakuja …”,
“,Harry up, let’s go back, tupande juu ya miti …”,
“,Hata mimi nasikia,wanakuja! “,
Kundi lote la takribani askari sabini, walipanda tena juu ya miti,baada ya kijana mmoja wa Kiafrika kusogeza sikio lake juu ya ardhi, karibu na udongo, akasikia ardhi ikitetemeka kwa mbali, bila shaka kuna watu walikuwa njiani wanakuja, tena wakikimbia, Angel Richald, mpenzi wake Mpuzu, mtoto wa gavana Richald Robeni, hata yeye alikuwa akichezwa na machale, akawahimiza wenzake, wakapanda juu ya miti haraka sana, ndani ya sekunde kumi, wote walikuwa juu ya miti, mikononi walishika upinde na mishale, huku bunduki walizowanyanganya wazungu wakiwa wamezikusanya pamoja, na kuziweka mahali salama juu ya mti, Angel alichukua bunduki moja aina ya smg, pamoja na baadhi ya mabomu madogo takribani matano, silaha zote za kizungu alijua namna ya kuzitumia, mafunzo aliyoyapata katika jeshi la Uingereza, aje kurithi mikoba ya baba yake, miaka kumi ijayo.
“,Shiii, silence please, they are coming, wanakuja! “,
“,Yeah wanakuja,kaeni tayali kwa ajili ya kushambulia,”
“,Sawa, sawa. …”,
Angel Richald, aliwasisitiza wenzake kuwa makini, kujiandaa kwa ajili ya mashambulizi, bunduki yake aliishikilia ipasavyo, jicho lake la kushoto alikuwa amelifumba, jicho lake la kulia lilitazama darubini, na kumuweka adui kwenye targeti, huku kidole kimoja cha mkono wake, kikijiandaa kwa ajili ya kuvuta taiga ili kuruhusu risasi kumiminika na kuteketeza maadui.
…………………………………
Malikia Magreth alikuwa mbele, mume wake, gavana Richald Robeni alifuatia, kisha kundi la askari wa kikoloni wakafuata, nyuma ya gavana Richald Robeni.Msururu ulikuwa mrefu, kutokana na wingi wao, wote walikimbia kwa kufuata njia ndogo, nyembamba, iliyokuwa ikiingia katikati mwa msitu, upande wa kulia.
“,What!, they have killed him, wamemuua Darwin! “,
“,Wamemuua kwa mtego,shit! Africans are bastard, we will kill you too, tutawaua ……”,
Wakiwa wanakimbia, ghafla mama yake Angel, malikia Magreth alifunga breki, alikutana na mwili wa kiongozi wao wa jeshi, walipoangaza upande wa pili, askari wengi wa kikoloni walikuwa wamepoteza maisha, wakavua kofia zao, jasho jembamba likawatoka, walichoka,
“,Who are you, wewe ni nani? “,
“,Colonial soldiers, askari wa kikoloni, don’t shoot us, msitushambulie …”,
Ghafla, malikia Magreth machale yalimcheza, alihisi majani ya vichaka yakicheza cheza, akanyosha bastola yake vichakani, kundi lote la askari wa kikoloni wakanyosha silaha zao kuelekea sehemu hiyo ya vichaka, askari takribani ishirini, askari wenzao wakajitokeza, huku wakionekana kuchoka sana.
“,Tulishambuliwa, wengine wakauawa, hatujui maadui walitokea upande gani, tumetoka vichakani kuwatafuta hatujawaona, ”
“,Tuondokeni, tusonge mbele …”,
“,But why this!, kwanini silaha zao hazipo mahali hapa?…”,
“,Enemies have taken them, maadui watakua wamechukua silaha zao, they want to fight us with guns, wanataka watuue kwa bunduki, they can’t kill us , tuondoke …”,
Walimaliza kujibizana wakiwa na huzuni, wakavaa kofia zao, wakakamata bunduki zao, wakaanza kusonga mbele, kufuata barabara.Macho yao yalikuwa makini, kuangaza kila kona wasije wakashambuliwa, mioyo yao ilianza kujawa na uoga, tofauti na awali, kwa sasa Waafrika walikua hatari sana, wenye mioyo ya ukatili kwa askari yoyote yule wa kikoloni, walikuwa hawana budi kuwa makini, kuepuka kifo.Walikimbia mita chache tu, baada ya dakika tano tu, wakashtuka tena ghafla, walikutana na maiti nyingine za wenzao waliouawa kikatili, ishirini ndani ya shimo, wakiwa wamechomwa na mapanga sehemu mbalimbali, baada kunaswa na mtego wa shimo, wengine walipigwa na mishale …
“,Shit! We are finished, wametega mitego kila kona, we have to be careful …”,
“,Why,hizi people nyeusi imekuwa katili sana, kama pata him or her, we are going to eat them, lazima kula nyama zao! “,
Walifoka, kila mmoja aliongea neno lake, gavana Richald Robeni pamoja na mke wake walishika vichwa vyao kwa huzuni, askari wao walikuwa wameuawa kikatili, wakaanza kuondoka tena, malikia Magreth, mke wake gavana, aliwaza tu kuhusu usalama wa mwanae, alitaka kufanya kila njia, asije akauawa na jeshi la kikoloni, kwani walikuwa na hasira sana baada ya wenzao kuuawa.
“,Lets move on, tusonge mbele …”,
“,Yes boss, let’s go to look for this stupid race, …”,
Gavana Richald Robeni alilihimiza jeshi lake kutokukata tamaa, mke wake akasimama, akaanza kusonga mbele, gavana akafuatia, kisha kundi lote la askari wa kikoloni wakafuata kwa nyuma,dakika mbili zilipita, dakika tatu zikapita,walikuwa njiani wakikimbia kusonga mbele
“,Paaaaa! “,
“,I’ m…dying, nakufa…aa ……”,
“,My mother!, mamaaa!, don’t die,aim sorry mom…”,
Ghafla risasi ilisikika, ikapenya katika kichwa cha malikia Magreth, ubongo wake ukasambaratika, Angel Richald ndiye aliyekuwa ameshika bunduki, akiwa juu ya mti, alifyatua risasi bila kujua kuwa kiongozi wa kundi, alikuwa ni mwanamke, tena mama yake mzazi, ukelele wa uchungu ukasikika, akakata roho palepale, Angel alipiga kelele za huzuni bila kutegemea,hakutegemea kumuua mama yake,mikono yake ilikufa ganzi, mwili ukakosa nguvu, akaachia bunduki yake aina ya smg, ikadondoka chini, askari wa kikoloni walipandwa na hasira, akiwemo baba yake mzazi na Angel, gavana Richald Robeni, hakutegemea kama mwanae alikuwa msaliti kiasi kile, akamuua mpaka mama yake mzazi, jeshi lote la kikoloni walisikia kelele za Angel, wakatambua mahali risasi ilipotekea ,waliinua silaha zao juu kwa pamoja, kushambulia mti mkubwa ambao Angel pamoja na askari wengine wa Kiafrika walikuwa wamejificha …
…ITAENDELEA …
Je, nini kitaendelea? Angel, msichana mrembo aliyejiunga na Waafrika kuwasaidia kupigania uhuru wao, kamuua mama yake bila kutegemea, mama yake akiwa msitari wa mbele kuingia msituni ili adhibiti askari wa kikoloni wasimuue mwanae, usikose sehemu ijayo, R. I.P Queen Magreth …
|
|
|
SIMULLIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 12… |
Posted by: MwlMaeda - 08-20-2021, 07:19 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
|
|
…SEHEMU YA 12…
Msitu wa mikoko
Angel Richald alikuwa hana silaha yoyote ile,moyo wake ulikuwa na maumivu makali baada ya kumuua mama yake mzazi kwa mikono yake mwenyewe,nguvu zikamuishia, akajikuta ameiachia bunduki yake bila kupenda.Mpuzu Yahimana, mpenzi wake Angel, alihuzunika kwa kile kilichotokea, japo alikuwa vitani kupigania uhuru wa Mwaafrika, lakini hakuwahi kufikiria kuwaua wazazi wa Angel, viongozi wa serikali ya kikoloni, gavana Richald Robeni, pamoja na mke wake malikia Magreth hata siku moja, jeshi la kikoloni walizinyosha silaha zao juu ya mti, mahali risasi ilipotokea na kumuua malikia Magreth, mahali kilio cha Angel kilikuwa kinasikika…
“,Shoot them, kill all of them including my daughter, she has killed her mother, she has killed my wife ……”,( wapigeni na risasi, waueni wote akiwemo binti yangu, amemuua mama yake, amemuua mke wangu …)
Gavana Richald Robeni alitoa amri, akiwa amenyoosha silaha yake, akijiandaa kuvuta taiga ya bunduki yake, kuruhusu risasi,vijana wake, askari takribani mia moja hamsini waliosalia, wakajiandaa kuvuta taiga,kulishambulia jeshi la watu weusi waliokuwa wakidai uhuru wao kwa kuingia vitani.
“,Papaaa!paaa!paaa paaaa……”,jeshi la askari wa kikoloni walishambulia.
“,wafyatueni na mishale,lukeni,tokeni juu ya miti,tukimbilie vichakani……”,Mpuzu Yahimana aliwahimiza vijana wake,washuke juu ya mti kuzikoa nafsi zao,silaha zao za jadi zisingefua dafu mbele ya risasi za moto za askari wa kikoloni.
“,papaaa,paapaa…”,askari wa kikoloni waliendelea kushambulia,wakiutekeza mti mkubwa wa ubuyu,matawi na majani ya miti yakateketezwa,yakadondoka chini na kuwalaani wazungu.
“,Yalaaa,nakufaaa,uwiiii!,Mrungu turongole(Mungu tusaidie),tunakufaa……”Kelele za machungu zilisikika,mashujaa wa Kiafrika walipiga kelele za maumivu, risasi zilipenya katika miili yao,wengine tumboni,wengine kichwani,Ishimwe alimanusura apigwe risasi,lakini alimuona mlengaji aliyekuwa amemuweka kwenye tageti,akaruka upande wa pili wa mti,risasi ikamkosa,askari wa kikoloni akaikoki tena amshambulie Ishimwe,alichelewa sana,Ishimwe aliuvuta upinde wake mpaka mwisho,akaufyatua,mshale ukatoboa jicho la askari yule wa kikoloni,ukatokea upande wa pili wa kichwa chake,akafa palepale.Ishimwe akadaka tawi la mti,akaruka chini,akatokomea vuchakani,mahali walipoelekea wenzake walioruka juu ya mti kabla yake…
Angel aliiona bunduki ya baba yake ikielekea upande wake,bila shaka baba yake alitaka kumuua,akaangalia upande wa pili,askari wa kikoloni takribani kumi walijiandaa kumshambulia,hakuwa na hofu yoyote ile,aliona bora afe kuliko kubaki duniani,moyo wake ulimsuta,alijiona ana hatia kubwa kwa kumuua mama yake,hakuona haja ya kukimbia kama walivyofanya Waafrika,walioruka huku na kule,kuelekea mafichoni,katika vichaka virefu msituni.Mpuzu aliwashambulia askari wa kikoloni kwa mishale,yote ikaenda pembeni,hakuua askari hata mmoja,alipogeuka upande wa pili,akamuona mpenzi wake anataka kushambuliwa,alikuwa hajielewi kabisa,akamvuta,Angel akadondokea kifuani kwake,akamkumbatia,mkono wake wa kushoto ulimshika Angel kwa nguvu,mkono wake wa pili ukakamata tawi la mti,huku risasi zikiwakosa kosa,zikipita juu ya vichwa vyao kwa fujo,Mpuzu Yahimana akaruka chini,wakakimbila msituni,huku Angel akilia kilio cha kwikwi,walipogeuka nyuma,walishuhudia maiti nyingi za Waafrika,zikidondoka juu ya mti,wakahuzunika,wakapiga moyo konde,wakasonga mbele na kutokomea vichakani…
“,Kufa,kufa,poor race,i hate you,……”,askari mmoja wa kikoloni,alifoka kwa hasira,akipiga mateke maiti za askari wa Kiafrika,ambao walikuwa bado wakihangaika kukata roho,alizungusha vichwa vyao,akawamalizia,aliwachukia sana Waafrika.
“,Lets follow them,tuingie kwa vichaka kuwatafuta…”,askari mmoja aliongea,akawahimiza wenzake kusonga mbele,kuwafuata Waafrika mahali walipokimbilia.
“,Stop!,don’t follow them,wacha fuata jinga hizi,let’s go back,turudi kwa great fort,we have to add more soldiers,askari yangu kufa nyingi sana……”,gavana Richald Robeni aliwazuia vijana wake kusonga mbele, askari wake wengi sana walikuwa wamepoteza maisha, jeshi lake lilikuwa limepungua, alitaka kurudi katika ngome yao kuongeza nguvu, askari wake wakatii amri yake, wakanyenyua mwili wa malikia wao kwa heshima, wakaupigia saluti, wakaanza safari ya kurudi katika ngome yao, wakiwa na majonzi makubwa …
…………………………………
Wanawake wa Kiafrika, wazee,watoto,pamoja na askari kumi waliokuwa pamoja nao kudumisha ulinzi,wakiwa juu ya mti wa ubuyu, mti uliokuwa umbali wa takribani mita kumi na eneo la vita, walisikia sauti za risasi, kelele za vilio na machungu zikipenya katika masikio yao, machozi ya huzuni yakawatoka, wakaa kimya, bila kutikisika juu ya mti, huku kila mmoja akiomba kwa mizimu, ndugu zao washinde na kurejea salama …
“,Twendeni tukawasaidie, twendeni ……”,askari mmoja, kati ya askari kumi waliokuwa juu ya mti, wakiwalinda wanawake, wazee na watoto, aliongea, alikuwa na shauku ya kutaka kutoa msaada kwa wenzake.
“,Hapana, hatujui wako mahali gani, tunaweza kushuka chini na kushambuliwa, isitoshe, kundi hili kubwa la Waafrika takribani wote, tuna waacha na nani? “,askari wa pili ,askari wa Kiafrika alimjibu mwenzake, akauliza tena swali.
“,Kweli kabisa, tuombe Mungu tu …”,askari wa tatu, akakubaliana na mwenzake, akaunga mkono, hawakua na haja ya kushuka chini ya mti wao wa maficho, wakatupilia mbali mawazo hayo, ghafla ukimya ukatawala tena msituni kwa mara nyingine tena …
…………………………………
Ngome kubwa :3;20pm
Magari kumi tu ndiyo yalirejea, magari ya askari wa kikoloni waliobakia, maiti zote ziliachwa msituni, zilikuwa nyingi sana, wakaziacha, wakiahidi kuzichukua watakaporejea msituni, wakiwa na kundi kubwa zaidi
Askari mia moja na hamsini tu ndio walirudi salama,wakiwa na mioyo iliyojaa huzuni, simanzi, pamoja na hasira juuu ya Waafrika.
“,Wamerudi, they are back! but why, ziko chache sana, zimekufa, they are killed ……”,
“,Hahahaaaa ……”,
Kundi la kwanza, kundi lililoenda kuwatafuta Waafrika katika majumba yao, makazi duni, wakawakosa na kushindwa kuwakamata, kisha wakawekwa rumande kwa amri ya gavana, waliongea kwa kejeli, wakacheka kwa dharau, walifurahi sana wenzao kurudi mikono mitupu,jeshi likiwa limepungua, askari wenzao wakiwa wameuawa kikatili …
“,Vizuri sana Africans, very good!very good! penda nyinyi sana ……”,
“,Hahaaa, haaaa, haaa …”,
Wakiwa wamesimama kwenye nondo za magereza yao, nondo ambazo ziliwawezesha kuona kila kitu kilichokuwa kinaendelea nje, waliwazomea, wakawakejeli askari wenzao, waliorudi wakiwa na nyuso za huzuni, huku baadhi wakiwa wamebeba mwili wa malikia wao, maneno ya kejeli na matusi yalipenya katika masikio ya gavana,akachukia, hasira zikampanda,askari wote waliokuwa pamoja naye wakachukia,sura zao zikakunjamana kwa hasira…
“,Firee them, I say fire them, kill them, uwa jinga yote ……,hypocrite people ……”,gavana Richald Robeni uvumilivu ulimshinda, akanyanyua bunduki yake, akaikoki, akavuta taiga, askari wake, askari waliokuwa pamoja naye, wakatii amri yake, wakageuka mahali yalipokuwa magereza ya wazungu, wakakoki bunduki zao, wakavuta taiga na kuanza kumimina risasi.
“,Paaaa, paaa, paaaa! ”
“,Aaaaa…ah, you have kill…ed us, mmetu…u…a, ”
“,paaaah, paaaah “,
“,Aaa…a…ah “,
Vilio vilisikika, askari wa kikoloni waliokuwa wamefungwa gerezani walikufa kama nzige,wakapiga kelele za maumivu, hakuna aliyesikia vilio vyao, ndani ya dakika tano tu, wote walikuwa wamepoteza maisha, ukimya ukatawala tena katika ngome ya wakoloni …
…………………………………
“,Let’s stop here, mimi choka sana, ”
“,Au ngoja nikubebe “,
“,No, no, hata wewe you have to rest, unapaswa kupumzika…”,
“,Mimi nashauri tupumzike, japo tumebaki wapambanaji arobaini tu, wengine wote wamekufa ……”,
“,Yes,wamekufa,by using this local guns,upinde na mishale, we can’t win the battle,hatuwezi kushinda kabisa, akili ikitulia, machungu ikipungua kwa moyo wangu, fundisha nyie kutumia guns, no way! I have killed my mum, I didn’t expect that, sikutegemea kabisa, I can’t go back,nikirejea kwa baba I will die, we have to win, tunapaswa kushinda,ili kuwakomboa na mimi jikomboa mwenyewe! “,,„Angel alipiga moyo konde, akajivika roho ya paka, akakubaliana na hali halisi, hakuwa na mama tena, baba yake hakumuhitaji tena, walikuwa maadui kwa sasa, hakua na jinsi zaidi ya kuungana na Waafrika kupigania uhuru kufa na kupona, hakua na jinsi kupigania maisha yake, bila hivyo baba yake pamoja na askari wake wa kikoloni watamuua, alipaswa kuwaua kabla hawajamuua …
…ITAENDELEA …
Wazungu kwa wazungu waeuana ndani ya ngome yao, Angel kadhamiria kusahau kila kitu kuhusu wazazi wake pamoja na rangi yake, nini kitaendelea? Usikose sehemu zijazo …
|
|
|
SIMULLIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 13… |
Posted by: MwlMaeda - 08-20-2021, 07:13 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
|
|
…SEHEMU YA 13…
The great fort (ngome kubwa)
Gavana Richald Robeni alikuwa ameketi katika sebure yake, ndani ya kasri lake kubwa la kifahari, uso wake ulikuwa na huzuni,alikuwa amepoteza watu muhimu katika maisha yake, mke wake alipoteza maisha mbele ya macho yake,baada ya kupigwa risasi na Angel, mtoto wao kipenzi ambaye kwa sasa alikuwa ni adui wake mkubwa.
“,Africans must pay!, lazima walipe kifo cha mke wangu, nitamuua Angel kwa mikono yangu mwenyewe ……”,Richald Robeni aliongea,akiwa amejipumzisha, mara baada ya kumzika mke wake, alichukua simu yake kubwa ya mkonga, akapiga simu.
“,Hallow! “,upande wa pili wa simu ulijibu.
“,Aim Richald Roben, gavana ya Goshani, i need your help, nyie kama jirani yangu, mimi huku pigana na Africans, zimeua askari yangu nyingi sana pamoja na mke yangu,nahitaji msaada yenu, one hundred soldiers inatosha sana …”,gavana aliomba msaada kwa majirani zake,kisiwa cha Gano kilichopatikana bahari ya hindi, kisiwa cha waswahili ambacho kiliongozwa na wakoloni wa kichina.
“,Oooh,pole sana,wewe rafiki yangu sana, kila siku unaniuzia pembe za ndovu na mkonge, lazima nikusaidie, nusu saa ijayo jeshi langu litafika katika koloni lako……”,gavana wa kisiwa cha Gano aliyejulikana kwa jina la Hwang Lee aliongea,kisha akakata simu.
Angalau gavana Richald Robeni aliweza kupata faraja, akatabasamu kwa mara nyingine tena, tabasamu ambalo lilificha siri nyingi za uchungu na majonzi.Nusu saa ijayo alitegemea kupokea askari wa kichina mia moja, watakao muongezea nguvu kwenye vita dhidi ya waafrika ambao walitaka uhuru wao,jambo ambalo lilikuwa ni gumu kama samaki kuishi nchi kavu.
…………………………………
Angel Richald, mtoto wa gavana, aliamua kusahau kila kitu kilichokuwa kimetokea, alikuwa amejitoa kwa moyo mmoja kumsaidia mpenzi wake Mpuzu pamoja na jeshi lake, waweze kupata ushindi dhidi ya Waafrika.
“,Kila mtu ajaribu kulenga shabaha,mti ambao nimeuwekea jani la njano,hakikisha mkononi umeshika bunduki, kama ambayo ninayo mimi ……”,Angel aliongea, akanyoosha juu bunduki yake ya smg kila mmoja akaiona,kisha akaikamata vizuri,aweze kuendelea na somo lake.
“,Hii inaitwa magazini,hii ni taiga,hii ni darubini yako,pakia magazini, shika kwa nguvu bunduki yako,hakikisha umeibana kwa nguvu kwenye kwapa lako,kisha tazama darubini,mlenge adui yako,then vuta taiga,shoot him,mpige adui!”,Angel Richald aliendelea kutoa mafunzo yake kwa vitendo,baada ya kutoa maelezo marefu, alikaa vizuri, akafanya kama alivyowaelekeza, wote wakiwa wanamtazama, akavuta taiga na kuruhusu risasi.
“,Paaaaa, paaaa, paaaaa! “,alifyatua risasi tatu, akausambaratisha katikati mti mkubwa wa ubuyu uliokuwa umbali wa mita mia mbili, kutoka eneo la kulengea shabaha.
“,Is it clear?, mmenielewa vizuri? “,Angel aliuliza.
“,Ndiyo tumekuelewa! “,jeshi la waafrika liliitikia, jeshi ambalo lilibakiwa na askari arobaini tu,likiwa limechanganyikana na vijana, wazee wenye nguvu, mdogo wake Mpuzu aliyeitwa Mwamvua pamoja na Angel mwenyewe.
“,Kama mmenielewa ,ngoja tujaribu kufanya shambulio, fateni amri yangu …”,Catherine aliongea, akasimama vizuri, akajiandaa kutoa amri,akiwa mtaalamu pekee wa silaha za kizungu katika jeshi la Waafrika,alitambua kuwa silaha za jadi zisingewafikisha mbali katika vita.
“,Pakia magazini, ikoki bunduki yako,lenga shabaha ya adui wako kwa kutumia darubini,fireeee them, fyatua risasi ……”,Angel alitoa amri, kisha akaruhusu shambulio.
“,Paaaa, paaaa, paaaa, paaa………”,risasi zilisikika,jeshi la Waafrika lilifanya kama lilivyoelekezwa,walishambulia miti waliyoelekezwa, mahali kulipowekwa alama, miti yote ikapasuliwa, Angel akayaziba masikio yake, mlio ulisikika ulikuwa mkubwa, ukasindikizwa na sauti za mwangwi msituni.
“,Yeeeeeee, ngwaluna, gwaluna, “(tumeweza, tumeweza) “,walishangilia kwa furaha, wakitumia lugha yao ya asili, wakaluka kwa furaha kama masai wa kule Monduli mkoani Arusha, nchini Tanzania.
“,Haya sasa, that is over! suala hilo kwisha kabisaa, this is another thing, hiki ni kitu kingine tunapaswa kujifunza,ni rahisi kutumia, sio kama bunduki ……”,Angel aliongea, akachukua mabomu mawili aliyoyakuta katika moja ya maiti za askari wa kizungu, akawaonyesha juu.
“,What is this? “,Angel aliuliza kwa lugha ya kizungu, kwa muda sasa walikuwa wamekaa naye, alikuwa amefahamu maneno mengi ya kiswahili, wao pia walikuwa wamejifunza maneno mengi ya kizungu.
“,bomu! “,
“,Mlipuko, “,
“,Risasi! “,
“,kibuyu! “,
“,Hicho ni kibuyuu! “,
Kila mtu alitamka neno lake, watu wa mwanzoni walipatia, wengine wakakosea kidogo, lakini watu wawili wa mwisho walikosea na kutaja vitu vya ajabu, Angel akajikuta anacheka, kwa sasa alikuwa na furaha, alijiona mmoja kati ya waafrika, alianza kusahau kuhusu kifo cha mama yake aliyemuuwa kwa mikono yake mwenyewe.
“,Hili ni bomu dogo, linauwezo wa kuuwa watu takribani ishirini kwa wakati mmoja, hii hapa ni pini, ukiichomoa kwa kuivuta kisha ukawarushia maadui zako, utakua umemaliza kila kitu, litalipuka na kuwaua, ndio silaha pekee inayoua vibaya! “,Angel aliongea kwa kiswahili safi kilicho nyooka, alianza kuongea kiswahili kizuri cha wazawa,kama vile alikuwa amezaliwa Afrika mashariki.
“,Oneni kwa makini navyofanya!, “Angel aliongea tena, jeshi lake likawa makini kumsikiliza, kwa sasa walimuamini, wakaheshimu mawazo yake, Angel alichomoa pini, kisha akalitupa bomu mita mia moja katikati ya msitu.
“,Puuuu, puuuuu! “,mlipuko ulisikika, miti ilipasuliwa mingine ikadondoka chini, vumbi zito likatimka,waafrika wote wakabaki midomo wazi, walikuwa hawatambui nguvu za silaha za wazungu.
“,Chakula, chakula, muda wa chakula,iyeeeee! iyeeee!, muda wa chakula ……”,la mgambo lililia, mmoja kati ya vijana wenye nguvu alipiga kelele, akiwa ameongozana na wenzake sita, walilejea kutoka msituni kufuata chakula,walikuwa na mikungu mitano ya ndizi pamoja na maembe. Jeshi la waafrika wakaahirisha shughuli zao, mafunzo yao yalikuwa yamekamilika, wakaenda kuwapokea ndizi, ndizi zingine zikapelekwa juu ya mti mkubwa wa ubuyu, maficho ya waafrika wote, ndani ya mti huu kulikuwa na matawi pamoja na mapango ambayo yalitumika kama maficho wakati wote wa vita.
“,we have to be careful, tuwe makini kabisa, muda wowote watarudi, kama sio leo basi kesho asubuhi, “Angel aliongea, akatazama juu angani, yalikuwa ni majira ya jioni, jua lilikuwa limeanza kuzama.
“,Usjali mke wangu, muda wowote tuko tayali kupambana ,ulinzi uko salama kabisa…”,Mpuzu aliongea, akamuondoa shaka mpenzi wake wa kizungu aliyemfanya ajiamini na kuanzisha vita hii ya kupigania uhuru, kwa sasa alikuwa amekamatilia bunduki yake iliyojaa risasi.
“,Wifi usjali, nipo kwa ajili yako …”,Mwamvua, mdogo wake Mpuzu aliongea, akaikoki bunduki yake, akamuhakikishia usalama.
“,Hahaaa, lakini tuwe makini sana, wale ni askari wazoefu na wamepitia mafunzo mbalimbali ya kijeshi, kwahiyo wanatuzidi askari, silaha pamoja na udhoefu, cha muhimu ukiua, hakikisha silaha yake unaichukua ……”,Angel aliongea.
“,Usjali shemeji, mimi nipo kwa ajili ya ulinzi na kutoboa matumbo yao kwa mishale, kwa yoyote yule atakayeisogelea kambi yetu …”,Ishimwe rafiki yake Mpuzu aliongea, akiwa ameshika silaha zote mbili, bunduki pamoja na upinde wake, aliupenda sana, hakuwa tayali kuuacha.
“„Sawa nimewaelewa, “Angel aliongea,wakakumbatiana, kwa sasa walipendana sana.
…………………………………
Gavana Richald Robeni alishtuka, akanyenyuka sebureni kwake, akatoka nje, alikuwa amesikia sauti ya risasi, nje ya ngome yao, baada ya dakika tano, mlipuko wa bomu ukasikika, nje ya ngome yao, moshi mzito ukaanza kuelekea angani, aliuona vizuri sana…
“,What is that? (ile ni nini) “,aliuliza kwa kizungu.
“,ni mlipuko, pamoja na risasi kutoka katika msitu wa mikoko …”,mmoja kati ya askari wa kikoloni aliongea, gavana akatafakari, kisha akatikisa kichwa, alikumbuka jambo fulani, akatambua chanzo cha mlipuko huo.
“,Ndiyo maana askari wetu waliouawa hatujawakuta na bunduki yetu, bunduki yote imechukuliwa na African, but they won’t win this battle, hawatatushindaa! “,gavana alifoka kwa hasira, kisha akarudi zake ndani, akijiandaa kwa vita siku inayofuata.
…ITAENDELEA …
|
|
|
SIMULLIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 14… |
Posted by: MwlMaeda - 08-20-2021, 07:07 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
|
|
…SEHEMU YA 14…
Ngome kubwa :6:20pm
Gavana Richald Robeni aliingia tena ndani kasri lake,alipotaka kuketi kwenye viti vyake,ghafla akasikia muungurumo wa helikopta, muungurumo ulikuwa mkubwa sana, bila shaka zilikuwa helikopta zaidi ya moja, akatoka nje haraka sana, akatazama juu ya anga la ngome yake, akatabasamu, helikopta tano zenye rangi nyeupe iliyopambwa na bendera za kichina,ziliwasili katika ngome yake, alifurahi sana, bila kutambua kuwa alikuwa amejichimbia kaburi yeye mwenyewe.
“,Welcome, karibuni sana kwenye makazi yetu …”,gavana alitoka nje ya kasri lake, akasogea mpaka kwenye kiwanja chao cha ndege, akawapokea askari wapya, akasalimiana na kiongozi wa jeshi hili wakapigiana saluti za heshima.
“,Asante, samahani sana kwa kuchelewa …”,kiongozi wa jeshi la kichina aliongea, akaomba samahani,mkononi alikuwa ameshika fimbo yake ya kijeshi, akiipiga piga mkononi.
“,Ondoeni shaka kabisa,hamjachelewa, kesho asubuhi na mapema tutaelekea vitani, “gavana aliongea.
“,Ok, can you give me the map of that forest? “,(sawa, unaweza kunipatia ramani ya huo msitu? “,kiongozi wa jeshi la kichina aliuliza, alitaka kuijua ramani, awapangie majukumu vijana wake. Gavana alijishika shika na mikono yake, akapekua mifuko ya nyuma ya suruali yake, hakuona ramani, akapekua mifuko ya shati lake, akaipata ramani katika mfuko upande wa kushoto, akampatia jenerali yule, wakashikana tena mikono, kila mmoja akachukua hamsini zake, gavana alirudi katika kasri lake, kiongozi wa jeshi la kichina akaongozana na vijana wake, mpaka kwenye vyumba vyao vya wageni.
…………………………………
Gano :Nusu saa iliyopita
Hwang lee alitabasamu,muda ambao aliusubili kwa hamu ulikuwa umewadia, alitamani sana kumiliki koloni la nchi ya Goshani, nchi ambayo ilijaa utajiri wa kila aina, madini, pembe za ndovu, ardhi yenye rutuba pamoja na nguvu kazi ya kutosha.
“,Lazima niwe mtawala wa Goshani,this is the only chance I was waiting for, lazima nitawale Goshani, lazima! “,Hwang lee aliongea yeye mwenyewe, ndani ya ofisi yake, akanyanyua simu ya mkonga, akapiga, baada ya dakika mbili, akakata simu, alikuwa amemaliza kufanya mazungumzo na mtu aliyekuwa anamuhitaji.
“,Ngo ngo, ngo ngo! “,mlango wa ofisi ya gavana wa kichina uligongwa, gavana katili aliyependa kutawala kila kona za dunia, huku akitumia jeshi lake kueneza utawala wake.
“,Get in!, ingia ndani ,mlango uko wazi …”,Hwang lee aliongea,mlango ukafunguliwa,kisha ukafungwa tena, mtu aliyekuwa amempigia simu alikuwa amesimama kwa heshima mbele yake, fimbo yake akiwa ameiweka na kuibana kwenye kwapa lake, akapiga saluti ya kijeshi.
“,Goshani wanapigana vita, waafrika they need to be free, wanataka uhuru wao, tumepigiwa simu na gavana Richald tukatoe msaada, muda mrefu tulitamani kumilika koloni hili, sasa muda umefika, chukua askari mia moja, nenda huko, fanya mbinu yoyote ile, gavana Richald auwawe, halafu uwa na hao waafrika walioanzisha vita! “,gavana Hwang lee alitoa maelekezo.
“,Sawa mkuu, nimekuelewa, kila kitu kitakwenda sawa,usiwe na shaka! “,jenerali na kiongozi wa jeshi la kichina aliongea, akapiga saluti, kisha akaondoka zake, tarumbeta kubwa ya kijeshi ikapigwa, katika ngome ya gavana, askari wote wakakusanyika..
“,Tunaenda kwenye vita ya dharula,Goshani inapigana vita, koloni la Waingereza na waafrika, tunaenda kutoa msaada, na kuliweka koloni hili katika himaya yetu!,nahitaji askari mia moja tu wa kuondoka nao”,kiongozi wa jeshi la kikoloni alitoa maelekezo kwa jeshi lake, vijana wake wakaluka juu kwa shangwe, walipenda sana kupigana vitaa.
“,Iyeeeeee, “zilikuwa ni shangwe za kufurahia vita, askari mia moja wakaingia katika helikopta zao za kivita, bunduki zao zikiwa mikononi, baada ya dakika tano helikopta ikapaa angani,ikaiacha ardhi ya kisiwa cha Gano, ikaelekea bara,nchini Goshani, nchi zote zikipatikana Afrika ya mashariki.
…………………………………
Msitu wa mikoko :8:00
Jeshi la Waafrika lenye askari arobaini tu kwa sasa, hawakulala, waliendelea kujiandaa na mapambano,walitega mitego kama kawaida yao, walichimba shimo lingine katikati ya barabara nyembamba iliyoingia msituni, ndani ya shimo wakaweka miti iliyochongoka kama mikuki, kisha juu ya shimo wakaweka fito dhaifu zenye uwezo wa kukatika, wakatandaza nyasi, wakaweka udongo juu yake,wakasambaza, haikuwa rahisi kuutambua mtego huu,barabara ilisawazishwa vizuri kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu kutofautisha mahali penye mtego na pasipokuwa na mtego.
“,Vuta juu hilo gogo,lazima liwauee tena kama nzige …”,mzee Nyamigo aliongea,Mpuzu akiwa juu ya mti akalivuta vizuri gogo, juu ya mti, usawa wa barabara, gogo ambalo liliunganishwa na kamba mpaka barabarani, kisha kamba ikafukiwa, yoyote yule ambaye angepita barabarani kizembe na kujikwaa kwenye kamba, kamba ingefyatua mtego, gogo likamuangukia na kumuua palepale.
” ,Yes, well done, tumemaliza, kwa sasa tusikae kwenye miti, wameshajua mahali tulipojificha mwanzoni, watu ishirini wakae katika vichaka upande wa kushoto, wengine ishirini wakae vichakani upande wa kulia “,Angel Richald aliongea, hakuna aliyemuelewa, wote wakabaki wanamtazama, walikuwa hawajui kusoma, kuhesabu wala kuandika.
Mwamvua akaifanya kazi hiyo, alikuwa mtundu sana, siku zote alipenda kujifunza, alifahamu kila kitu mpaka lugha ya kizungu, bila hata kwenda shuleni, alijifunza kupitia wakoloni alioishi nao, alikalili kila kitu walichokifanya ambacho aliona kitamsaidia ,baada ya kumaliza kuwahesabu askari wa kiafrika, na yeye akakaa katika kundi moja lenye watu kumi na tisa,kisha wakaingia vichakani, pembeni ya barabara, wakajificha,kusubili vita…
…………………………………
Ngome kubwa :9:30pm
Kikao cha siri kiliendelea ndani ya vyumba vya wageni,askari wa kichina walipanga mipango yao ya siri kumuua gavana Richald Robeni, kisha waweze kuwa watawala wa Goshani.
“,Sisi tuna askari mia moja tu, wao wako wengi, japo hawazidi mia mbili, mimi nitaenda na gavana, katika gari moja, nitamteka na kumfunga kamba,mlinzi wake nitamuua, hana uwezo wa kupambana na mimi, kisha jeshi la Waingereza, tutawaambia watii amri zetu, kwenye vita na Waafrika,ili kuyaokoa maisha ya kiongozi wao, mtaenda vitani mkirudi mahali mlipotuacha, nikiwa nimemuweka mateka gavana, mtakuta nimemuua,akiwa ndani ya gari, bila wao kujua kama amekufa,nitawaambia waweke silaha chini kumpata gavana wao,wataweka silaha chini, kisha tutawashambulia kwa risasi, mchezo utaishia hapo! “,jenerali wa kichina alitoa maelekezo na mpango wake wa kufanya shambulio, wote wakamuunga mkono. Baada ya kikao, kila mmoja akajipumzisha kitandani, akiisubili kwa hamu asubuhi, siku inayofuata.
.……ITAENDELEA …
|
|
|
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 34 |
Posted by: MwlMaeda - 08-19-2021, 04:24 PM - Forum: Hadithi
- No Replies
|
|
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU
SEHEMU YA 34
Basi kama kawaida yake Zamda siyo mtu wa kujikweza sana.Aliamua kufungua kioo na Kisha akafunga mlango na Kuanza Kutoka Kwenye Gari Hilo lililokuwa ni gari aina Discover 3
Kwahiyo Zamda akiwa amevaa dera lake lililokuwa limemkaa Kweli Kweli kutokana pia na mwili wake namna ulivyo kichwani kajifunga kitambaa cha kuonesha ustara wake.Lakini Zamda akawa amemwambia yule mfanyakazi wake ambaye alikuwa na watoto wa Zamda ambapo yule mfanyakazi anaitwa Hilda.Zamda akamwambia Hilda Hivi.
Hilda usishuke na watoto,
Sawasawa mama.
Kaa nao hapo Hapo.
Sawasawa mama.
Tulia kwanza Mimi niongee na huyu mtu .
Sawasawa mama.
Nakweli Hilda akawa amekaa na wale Watoto wa Zamda Yaani Glady,Rubai na Gift ambapo Gift ndiyo yule mtoto wa pili wa Zamda.
Zamda Alishuka na kwenda kwa Huyo mtu huku akiwa anaangalia sura ya mtu huyo kwakuivutia kumbukumbu za mbali kabisaaaaaaa.Alifika kisha Zamda akamsalimia Mwanadada huyo kwakusema Hivi.
Mambo vipi Dada?.
Safi.Zamda ni wewe kabisaaaaaaa.
Ndiyo, ila mbona Mimi sikukumbuki vizuri?.
Daaa Kwakweli Zamda huwezikunikumbuka Kwasababu mwili wangu wa kipindi hicho siyo kama huu nilionao kabisaaaaaaa. Yaaani nimekuwa kama Mtoto.
Hapana. Ila ni vyema ukaniambia jina lako kwanza Ndiyo hata naweza kukukumbuka vizuri.
Mimi ni rafiki yako tulisomaga shule ya sekondary ya Ngata.
Ngata!!!??.
Ndiyo.Mimi ni Kidawa.
"Zamda alishangaa sana kwakusema"Haaaaaaaa.Kidawa ni Kweli kabisaaaaaaa ni Wewe.
Kweli ni Mimi.
" Walikumbatiana kweli kweli Zamda na Kidawa Kwasababu Kipindi hicho walikuwa ni marafiki wakubwa sana japokuwa waliwahi kugombana kidogo walipokuwa shule sekondary ya Ngata wakiwa na shoga yao mkubwa mwingine ambaye ni Mwantumu .Kwakweli hadi machozi yaliwatoka wote. Kisha Zamda akaendelea kusema hivi ".
Kidawa siamini kama ni wewe kabisaaaaaaa. Mbona umeisha Hivyo Jamani Yaani umekuwa kama mtoto Yaani sijui Ana miaka Kumi na Tano.
Zamda Yaani ni maisha tu shoga wangu.
Kwahiyo Ngata uliondokaga kitambo sana?.
Ndiyo mda Sana tena sana .
Daaaa Sasa hapa mjini Kidawa unajishughulisha na nini?.
Ndiyo Kama unavyoona hili beseni hapa ni la kwangu nauza matunda.
Daaaaaaa Kidawa kweli kweli kabisaaaaaaa?.!
Ni kweli.
Vipi kuhusiana na yule rafiki yetu mwingine yuleeeee.
Unamzungumzia Mwantumu siyo?.
Duuuuuuuuuuuu, kwa Mwantumu Kwakweli.
Kwani yuko wapi Yeye ?.
Aaaaa Kwakweli Zamda kuhusiana na Mwantumu ni Stori ndefu Sana.
Kivipi iwe stori ndefu Tena.
AAA kwa ujumla Mwantumu si Mwantumu tena kwasasa.
Bali ni nani.
Ni marehemu.
" Zamda alishtuka sana Kwakweli kwakuweza kusikia maneno Yale ya Kidawa kuhusiana na Mwantumu. Kisha Zamda akasema Hivi'.Marehemu!!!???.
Ndiyo maana Yake Zamda, Mwantumu alishafariki kitambo sana.
Kweli kabisaaaaaaa.
Ndiyo Ukweli huo kuhusiana na Mwantumu.
Amakweli udongo haushibi.
Na haushibi kweli.
Sasa nini kilisababisha hadi kifo chake?.
Alikuwa anaumwa sana.
Anaumwa sana.
Ndiyo.Yaani aliumwa sana kipindi kile ulivyopotea tu pale mtaani kwetu na Yeye akawa ameanza kuumwa.
Nini haswaa kilikuwa kinamsumbua.
Daaaaaaa, ni ugonjwa mkubwa Sana.
Ugonjwa mkubwa kivipi Kidawa?.
Ni huu Ugonjwa wa kisasa.
Ugonjwa wa kisasa!!??.
Ndiyo.
Ni ugonjwa gani huo wa kisasa?
UKIMWI.
"Zamda akawa ameshituka na kusema hivi"UKIMWI kabisaaaaaaa.
Ndiyo maana Yake Zamda.
Daaa mungu msaidie rafiki yangu Kwakweli huko aliko.Kwahiyo Kidawa Sasa unaishi wapi kwasasa?.
Huko mwisho wa jiji kabisaaaaaaa hukooo.
Mwisho wa jiji Unamaanisha Horima kabisaaaaaaa kule.
Ndiyo.
Haaaaa mbona mbali sana Sasa kule unakuja na nini hadi huku?.
Kwa miguu tu.
Haaaaa kwa miguu kabisaaaaaaa.
Ndiyo Zamda Sasa nitafanyaje.Kwasababu niseme nipande gari nitamaliza Hela na unaweza kukuta Hayo matunda yasinunuliwe hata kidogo huko Kwenye gari.
Daaaaaaa sawa Shoga Wangu wa kitambo embu nipatie namba zako.
Sina hata simu kabisaaaaaaa .
Kabisaaaaaaa huna Simu Kidawa!!??.
Kweli Zamda sina simu.
Duuuuuuuuuuuu Sasa tutakutanaje hapa Mjini kwa style hiyo.
Tutakuna tu Zamda.
Sawasawa. Embu shika Basi hii Hela Kidogo hii itakusaidia kwa mambo madogo madogo Hivi."Zamda alimpatia Kidawa shilingi laki moja ya Kinani. Kisha Kidawa akasema Hivi".
Shukrani sana Zamda, Yaani shukurani kubwa Sana.
Sawasawa haina shida.
Ubarikiwe sana Zamda.
Inshaallah.
Basi acha Mimi nirudi nimekuja hapa chapu.
sawasawa Zamda uzidi kubarikiwa sana.
Basi mda huo Zamda akawa amemuaga huo Kidawa na Kisha Zamda akawa amerudi zake huko kwenye gari lake.
Kwakweli Kidawa roho ilimuuma sana kwa kuweza kumuona Zamda akiwa anaendesha gari tena la bei ghali namna hiyo Kabisa.
Ni miaka kumi na tano imepita tangu Zamda na Zaidu kuoana.Yaani kuanza kuitana mke na mume.Kwakweli ndoa yao ilizidi kukoa moto sana na kuwa nzuri yenye utulivu mzuri kwelikweli kama utajiri wao amabo walikuwa nao.
Ambapo kwa Zaidu tayari naye aliweza kusoma hadi kuja kufanikisha kumaliza shahada yake ya Kwanza na ya pili yaani akawa ana masters yaani shahada ya udhamili ambayo ilikuwa ni shahada ya udhamili ya Fasihi katika chuo kikuu kilichokuwa kikijulikana kwa jina la University of Literature (U.L), yaani Chuo kikuu cha Fasihi ambacho kilikuwa kinapatikana hapo hapo katika jiji kuu la Kinani.
Zaidu kutokana na ustadi wake wa Fasihi aliweza kupewa nafasi katika chuo kikuu hicho cha Fasihi cha Kinani.Ambapo nafasi aliyokuwa amepewa ni nafasi ya Muhadhiri Msaidizi katika chuo kikuu cha Fasihi.
Heshima ya cheo hicho alipewa ni baada ya kuweza kushinda tunzo takribani Saba katika mashindano mbalimbai ya kitaaluma. Ukianza na mashindano ambayo makubwa kabisa aliyafanya na kushinda tuzo ya dunia ya uandishi wa hadithi za kufikirika na zisizo za kufikirika.
Kwahiyo Bibiye Zamda hadi kipindi hicho alifanikisha kuwa na Watoto wanne.Watoto hao ambao ni Glady akiwa ndiyo wa kwanza kutoka kwa marehemu Tito na wa pili ni huyo Gift ambaye ni wa marehemu Tito pia,mtoto wa tatu ambaye ni Rubai na Ndiyo Mtoto wa kwanza kwa Kijana Zaidu na wa nne na wa mwisho ni Aisha. Kwahiyo Zaidu kwa watoto wake kabisa akawa anao wawili wakike na wa kiume.
Lakini Kwakweli Watoto wote aliishi nao na kuonesha moyo mzuri kwao kama vile wote ni wa kwake.Huyo Glady na Gift wote waliona kabisaa Zaidu Ndiyo Baba yao.Wote aliwapeleka Katika shule zenye kufundisha vizuri sana na zenye rekodi nzuri sana za ufaulu katika Taifa la Kinani.
Basi ikiwa siku hiyo ikiwa ni Siku ya jumapili mishale ya saa nane mchana. Siku hiyo Jeni alihudhuria katika chakula cha mchana huko Nyumbani kwa Zaidu. Kipindi hicho tayari Zamda ukimuangalia siyo yule Kabisa. Yaani mwili umekuwa mkubwa Kweli Kweli na kuzidi kuonesha sura ya kiutuukubwa Zaidi.Zaidu naye ndiyo hivyo mzee wa Nyumba naye kama kawaida amejaaliwa mwili ambao si wa kuzeeka baki kwa namna ndefu na mstachi unavyoonekana tayari utajua kwamba huyu mtu ni mkubwa kiumri.Jeni Naye kama kawaida yake aliweza kung'ang'ania mjini tu.Yote hiyo ni baada ya mchumba wake ambaye alikuwa ni polisi alikuja kufariki ni baada ya siku hiyo mchumba wake alikuwa ameenda katika malindo yake huko Walikuwa na polisi wenzake wengine.Ambapo walikutana na Kikundi kibaya sana Yaani kilikuwa na nguvu sana na kuweza kuuliwa askari watatu mojawapo akiwa ni mchumba wa Jeni na wengine wakawa wamefanikiwa kukimbia ndipo wakaenda kutoa taarifa huko kazini kwao.
Kwahiyo kwa siku hiyo Kwakweli ilikiwa ni siku maalumu sana kwa wakutani hap watatu Yaani Zamda, Zaidu na Jeni.Wakiwa wamekaa katika Jumba la kifahari la Zaidu.
Mda huo wakiwa katika kila mtu na kiti chake meza hapo inaonekana ina chakula cha kutosha Kabisa na matunda ya aina mbalimbali. Basi mda huo Zaidu akiwa amevaa suruali yake ya bluu Hivi na tisheti nyeusi, Zamda kama kawaida yake Bibiye wa madera,Mda huo akiwa amevaa dera lililokuwa na rangi nyekundu na njano na liliyokuwa limechorwachorwa maua ya love.Jeni naye suruali nyeusi na tisheti nyekundu. Basi mda huo Zaidu akiwa ameshika kikombe akinywa juice huku akisema Hivi.
Unajua Jeni Natumai kwasasa ni miaka kama vile Kumi na Tano hivi Tangu Mimi na Zamda ambaye Ndiye mke wangu kuoana.
Ndiyo ndiyo Zaidu.
Aaaaaaa Zamda mke Wangu.
"Zamda aliitika kwa madaha Kweli Kweli huku akiwa na Glass iliyokuwa na juice tele.Alisema Hivi".Beee mume Wangu.
Najua Unajua kabisaaaaaaa kwamba Jeni ndiyo chanzo cha sisi hadi kuitana hapa mke na mume.
Ni kweli mume wangu hilo nalijua sana tena sana.Ndiyo maana huwa Nasema Jamani Jeni umenifungulia vizuri sana njia ya maisha yangu.Kwahiyo nipende kusema tu shukurani sana sina hata kingine cha kukulipa.
Aaaaaa shukurani pia kwako wewe kwkaunifanya na Mimi hadi kuwa hapa.
Sawasawa.
" Zaidu akasema Hivi ".Kwakweli Jeni Mimi ni shukurani aisseeee Sijui nikupatie Shukrani ngapi Jamani. Kwasababu ni mengi ambayo umenifanyia kwaajili ya faida yangu.
Sawasawa Zaidu. Pia Zaidu hata Mimi Kwakweli niseme tu Kwakweli ni shukurani nyingi sana za kukupa wewe Kwasababu kwa wewe ndiye kama mtu ambaye unaniweka mjini na hadi mda huu Mimi kuitwa eti Boss wa salon zote ziitwazo Jeni Hair Salon hapa mjini. Unajua siamini kabisaaaaaaa.
Aaaaa unajua Jeni niseme tu kwamba sisi wote katika msafara huu hadi leo hii tuko hapa kila mtu hapa ana msaada wake mkubwa sana kwa mwenzake.
" Zamda akasema Hivi "Ni Kweli mume wangu.Kwasababu maisha yetu yalikuwa ni ya kama duara vile.Yaani huyu kamsaidia yule na yule kamsaidia Huyu Basi Yaani ni full misaada tu kabisaaaaaaa.
Ni Kweli mke wangu.
Basi wote mda huo Kwakweli Walikuwa na Furaha sana kwa marafiki hao watatu ambao kwamba kila mtu anaonekana Kweli amemsaidia mwenzake kwa namna yoyote ile Au njia yoyote ile.
Hapa Sasa ndiyo pale pakujua kwamba saa nyingine katika Maisha Kwakweli unaweza kulia sana Ukisema kwamba maisha ni magumu sana na unaanza kuamua kukata tamaa na kutokana na hali uliyo nayo.Hapana si vyema kukata tamaa angali u mzima.Yaani roho ikiwa bado inadunda kamwe haifai kukata tamaa Kabisaaaaaaa.
Kuna mda machozi yatakutoka sana hadi mda mwingine unatokwa na macho ya damu Lakini bado tu hakuna kukata yamaaa.
Tukumbuke tu maisha ni Safari ndefu ambayo Kwakweli Safari hiyo huwa na Vituo vingi sana.
TAMATI
MWISHO.
FACEBOOK PAGE: saidikaitastories.com
LINK:https://www.facebook.com/kaitastory/
MAWASILIANO: 0783372139
E-MAILaidikaita7@gmail.co
|
|
|
|