MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 1… - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SIMULIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 1… - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48)
+---- Thread: SIMULIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 1… (/showthread.php?tid=935)



SIMULIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 1… - MwlMaeda - 08-20-2021

…SEHEMU YA 1…
Mpuzu Yahimana,kijana wa Kiafrika, alipanda ukuta mkubwa uliojengwa kwa mawe, huku akiwa makini asionekane na askari wa kizungu walioizunguka ngome yote ya kikoloni kudumisha ulinzi.Moyo wake ulikosa furaha, macho yake yalitamani kuona sura ya mtoto mrembo wa kizungu kwa mara nyingine tena tangu siku iliyopita. Uvumilivu ulimzidi nguvu, hisia za mapenzi zikamuandama, licha ya ngozi nyeusi aliyokuwa nayo, aliapa kumpata mtoto wa gavana Richald Roben kwa gharama yoyote ile …
“Sijui anajua kiswahili?lakini nitamfundisha, ngoja nichungulie, labda nitamuona tena angalau moyo wangu upate faraja …”!Mpuzu Yahimana aliongea, mikono yake miwili ilikamatilia kwa nguvu mawe ya ukuta imara wa ngome ya kikoloni, moyo wake haukua na hofu juu ya kifo na kunyongwa kikatili iwapo akikamatwa, moyo wake ulimuwaza Angel Richald, mtoto wa kipekee wa gavana wa Kiingereza katika nchi ya Goshani. Mpuzu aliendelea kukwea ukuta, huku kila mara akiangaza mashariki, kutazama kama jua linachomoza, lakini aliambulia wingu la ukungu lililosababishwa na baridi kali majira ya asubuhi.
“Jua lisipochomoza!mtoto wa gavana hatatoka kuota jua sababu ya baridi, lakini inabidi niendelee kupanda juu, muda sahihi ni huu, walinzi wanaamini hakuna Muafrika anayejiamini na kuvuka ukuta huu mkubwa, tena majira haya,bila kujua yupo Muafrika hodari Mpuzu Yahimana, mjukuu wa Yahimana kiongozi mkuu wa Manamba katika koloni hili la Waingereza miaka ishirini iliyopita “,Mpuzu aliongea, kichwa na mwili wake ukitoa mvuke, kutokana na baridi kali ya asubuhi.
Mpuzu alikua tayali kuteseka,kuumia na kufa,sababu ya penzi
.Hatimaye safari ilifika Ukingoni, majumba ya Kizungu yalianza kuonekana,Mpuzu akiwa umbali wa futi hamsini kutoka chini.Tabasamu likaipamba sura yake kufika mwisho wa ukuta, jua nalo lilichomoza ,katika wakati sahihi ambao Mpuzu aliutarajia.
“Ewala! jana alikuwa amekaaa pale kwenye zulia, bila shaka hata leo atakaa pale kuota jua, eee mizimu ya mababu nisaidieni nitimize lengo langu, nitoke salama mahala hapa ………”,Mpuzu aliongea huku akiomba ulinzi wa mizimu ya mababu imlinde, kwani ilikuwa ni kosa la jinai kwa Muafrika yoyote yule kukanyaga ngome ya kikoloni, makazi ya wazungu, waarabu pamoja na wahindi.
…………………………………
The great Fort (Ngome kubwa);
Siku tatu zimepita tangu akanyage Afrika,awali alifikili ni bala tajiri kama Ulaya, kinyume na matarajio yake, Afrika ilijaa mashamba makubwa ya mikonge, mashamba yaliyomilikiwa na wazungu, huku Waafrika wakifanyishwa kazi kwa nguvu na kulipwa senti moja tu kwa masaa kumi na mbili shambani.
Hamu ya kutaka kujua koloni walilotawala wazazi wake ilimwishia, akiwa na siku moja tu, alitaka kuondoka Goshani na kurudi Uingereza.
“Subili mwanangu, wait two weeks to come, i will take you back to British (subili wiki mbili zijazo, nitakurudisha Uingereza) “,ni maneno ambayo Angel aliambiwa, kila alipozungumzia swala la yeye kurudi Uingereza mbele ya baba yake.
Ghafla wazo la yeye kurudi Uingereza likatoweka, fikra mpya zikatawala kichwa chake, moyo wa Angel ukazama katika penzi la kijana wa Kiafrika, kijana Mpuzu Yahimana aliyeingia ngome ya Kikoloni siku iliyopita akiwa na manamba wenzake, wakiwa wameleta mazao ya katani kwenye ghala la kuhifadhia mazao, kabla ya kusafirishwa kwa meli kupelekwa Uingereza.
Usiku hakula chakula, hakuna mtu angemshirikisha tatizo lake akamsaidia, tofauti na kawaida yake, alilala mapema kupumzisha kichwa chake,kichwa kilichojaa mawazo mengi, kwani aliwaza na kuwazua namna ya kuwa karibu na kijana yule wa kiafrika, na mahali pa kumpata bila majibu yoyote yale. Kutokana na badiliko la ghafla, gavana Richald Robeni alifikili mwanae anaumwa kumbe sivyo.
Asubuhi na mapema, jua lilichomoza, Kama kawaida yake, Angel alitoka nje ili aweze kuota jua. Alitoka nje, huku kichwa chake kikitafakali namna ya kumdanganya baba yake, ampatie ruhusa ya kutembelea makazi ya Waafrika, suala ambalo lilikuwa ni gumu mithili ya chatu kummeza tembo.
“,Fliiiiii ,fliiiii ………”,mlio kama filimbi ulisikika, Angel akiwa ameketi kwenye Zulia akiota jua alitazama huku na kule, hakuona chochote kile …
“,What is this? Oooh nothing!”,(Hii ni nini?, ooh hakuna kitu), Angel alizungumza peke yake baada ya kusikia mlio wa filimbi, alipogeuka huku na kule hakuona kitu chochote, akaendelea kuota jua.
“Fliiiii, Fliiiii ……”,filimbi ilisikika tena, Angel akageuka kwa mara nyingine, hakuamini alichokiona, kijana wa kiafrika aliyemkosesha usingizi alikuwa juu ya ukuta akimchungulia, uvumilivu wa mapenzi ukamshinda, hofu ya Mpuzu kudondoka chini ikamuandama Angel, bila kutambua kuwa Mpuzu alikuwa kijana hodari zaidi ya anavyofikilia.
“,Come down please, your not safe over there, you can die ……”,(Njoo chini tafadhali, hauko salama mahala hapo, unaweza kufa), “Kwa lugha ya kizungu Angel alizungumza, lakini Mpuzu hakuelewa chochote kile, jambo ambalo lilipelekea askari wa kizungu kushtuka, kwani Angel alionekana akiongeea na mtu fulani juu ya ukuta na kuhatarisha usalama wake……
“,Paaaaa! paaaa! paaa………”,risasi zilifyatuliwa juu ya ukuta alipokuwa Mpuzu,Mpuzu alimrushia cheni Angel, cheni ambayo Angel aliipokea kwa ustadi mkubwa bila askari yoyote yule wa kikoloni kugundua, huku akiitazama na kuishangaa zawadi ile.
“Paaap! paaaa! ……”,askari wa kikoloni waliendelea kumshambulia Mpuzu bila kumtambua vizuri sura yake ,kwani alikua mbali kabisa juu ya ukuta.
“,Aaaaaaa! “,Mpuzu alitoa ukelele, akalalamika kwa uchungu.
“,Puuuuuh! “,kishindo kilisikika upande wa pili, Mpuzu alidondoka chini ,baada ya kuachia mikono yake miwili, wakati wa kukwepa risasi kuikomboa nafsi yake.
“,Zungukeni, zungukeni upande wa pili,! aletwe hapa, stupid boy! “,askari mmoja wa kikoloni, aliwaamrisha na kuwatawanya wenzake kutoka nje ya ngome kubwa(the great fort), kwenda kumkamata Mpuzu Yahimana.
“,I hate you, I hate you! if you kill him, i will also kill you ………”,(nawachukia, nawachukia!, kama mtamuua na mimi nitawaua ),Angel alifoka kwa hasira na kukimbilia ndani, hakuna aliyejali kelele zake, askari wa kikoloni walipishana kukamata silaha kwenda kumtafuta Muafrika aliyekanyaga ngome yao maarufu kama ngome kubwa (the great fort) na kuichafua.
Mpuzu Yahimana alinyanyuka kwa shida huku akiugulia maumivu, hakuwa tayali kukamatwa na askari wa kikoloni, njia pekee ya kuepuka kifo ni kukimbilia msituni. Safari ya kutokomea mafichoni ilianza haraka haraka ,kabla hawajamkalibia.
…………………………………
Makazi duni; (Slums area)
Magari ya kikoloni yaliingia kwa fujo katika makazi ya Waafrika, askari wa kikoloni walibeba silaha pamoja na mijeledi mikononi, huku sura zao zikikunjamana kwa hasira.
“Mtu yote itoke kwenye slum! sisi tafuta pumbavu moja kuja ingia kwa ngome yetu this morning! “,askari mmoja wa kikoloni alizungumza, akiwa amevalia shati jeupe, pamoja na kaptula, mguuni alivalia viatu vyeusi vilivyong’arishwa na rangi nyeusi,kiunoni alivaa mkanda, mkanda uliounganishwa mpaka mabegani, sare kamili ya jeshi la kikoloni!
“Every family should get out of their slums!, if any member of your family is missing, you will be in trouble all of you ……”,(Kila familia inapaswa kutoka nje ya kibanda chao,kama mtu yoyote katika familia anakosekana,nyote mtakua kwenye matatizo), “askari mwingine alifoka kwa kizungu,huku akitumia mjeledi wake kutoa Waafrika katika vibanda vyao vilivyoezekwa kwa nyasi.
Familia zilipanga mistari,kisha wakubwa kwa wadogo wakachapwa viboko, baada ya mtu mmoja kukosekana. Huku wakihimizwa kutaja mtu aliyekosekana, kwani hakuna manamba wowote waliokuwa tayali wameelekea katika mashamba ya wakoloni.
Kisu cha moto kikachemshwa, wazee wote walitakiwa kukatwa vidole, huku dawa ikiwa ni kumtaja mtu aliyekosekana …
“Mpuzu Yahimana, mwanangu hayupo! msiwahukumu wasio na hatia! “,baba yake Mpuzu alizungumza na kupiga magoti mbele ya askari, pamoja na viongozi wa kikoloni, bila kutegemea, askari walimkamata yeye pamoja na familia yake,walifungwa kamba, kisha wakapakiwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa gerezani …
…ITAENDELEA …
Usikose riwaya hii ya kusisimua,je nini mwisho wa penzi la Mpuzu na Angel kwenye vikwazo vingi vya Ubaguzi na ukatili kutoka kwa Wakoloni …
 
Mtunzi; Hakika Jonathan
0629905923