SHAIRI LA KUMUENZI HAJI GORA HAJI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Watunzi wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=17) +--- Thread: SHAIRI LA KUMUENZI HAJI GORA HAJI (/showthread.php?tid=3) |
SHAIRI LA KUMUENZI HAJI GORA HAJI - MwlMaeda - 06-14-2021 Tangao la nuru yako, limezunguka bahari Kimbunga kwenye maeko, kimetulia shuwari Yamepita maandiko, kwa kalamu ya kahari Umekwisha mzunguko, kuishi kwenye sayari Lala salama habibi, kipenzi cha washairi Andiko la maajabu, labubujika bongoni Ni andiko la dhahabu, si la kusoma chuoni Ni tunu yake Wahabu, hidaya yenye thamani Alitunukiwa babu, Gora pomoni moyoni Lala salama habibi, kipenzi mwanafasihi Unaishi vitabuni, umelala mioyoni Maisha ya hali duni, uliishi duniani Ni duni tulivyodhani, ila duni ya thamani Naamini kwa Manani, maisha yako peponi Lala salama habibi, kipenzi mwanachuoni Nikuzungumze vipi, hata niishe kalima Niziseme mara ngapi, sifa kwa yako heshima Nikazitafute wapi, hadithi za kukusema Yatosha japo makapi, bora niweke khatima Lala salama habibi, kipenzi cha kila mtu Ali Hilal Zanzibar. 13.6.2021 |