Sanaa ni matokeo ya dhana ya mawazo ya msanil ili sanaa lundwe msanil ni lazima awe na dhana kamili kichwani mwake kuhusu sanaa anazokusudla kuunda. Baadhl yasanaazenyemaana ni zileambazo mtazamajl aklzlona anazlelewa mara moja maana yake bila ya kuuliza msanil aeleze alichokusudia alipozitengeneza. Kuna sanaa za alna nylngl. Sanaa zilizo maarufu ni za rangl, za magogo ya mitl, za mawe na za udongo wa mflnyanzi kwa kutaja mlfano mlchache tu.
Sanaaza rangl zlnaweza kuwa nawatu, wanyama wa porini na wa nyumbanl, mlti mikubwa na misitu, nyanda zenye nyasl, milima, majl ya baharl na ya mazlwa makubwa, mazinglra ya mvua na ya ukame, hali ya watu wenye haslra na wenye furaha, desturl na tabia za watu zilizochongwa kwenye magogo ya miti au zilizoundwa katika udongo wa mflnyanzi zinaweza kuwa za watu, wanyama wa mlfugo ya nyumbani au porini au vltu vlsivyo na uhai vya matumizi ya nyumbani kama vitl vya kukalia, flmbo za kutembelea, vitanda vya kulalia, milango ya nyumba, vyungu vya kupikia chakula au kuwekea maji na pombe. Ili sanaa hizi zitokee msanil anahitaji vifaa vya kutumia kama magogo ya miti, mawe au udongo wa mfinyanzl, tezo, patasi, msumeno, nyundo za mlti na za chuma, na vinginevyo.
Msanil lazima awe na ujuzi kamili wa kutumia vyombo hlvi. Akiwa ni mchoraji inambidi atayarishe mahali pa kuchorea sanaa. Kama ni mchongajl ni lazima achague lile gogo ambalo litatosha sanaa yake. Mchongajl anajua kwamba aklchonga sehemu fulani hawezi kuirudishia. Lakini akitumia udongo wa mfinyanzi anaweza kuanza kuumba sanaa yake hatua kwa hatua, akiongeza sehemu zake ndogo ndogo. Hapo akikosea sehemu fulani anaweza kuiondoa na kuirudlshla.
Msanii anajua sanaa zenye manufaa ni zile zilizo na maana katika malsha yake na yale ya wenzake. Ni sanaa zinazoeleza shughuli, mawazo na busara za watu. Ni sanaa zenye hadhi ya tabia za watu ndizo zinazompasa msanli azlfurahle na kujlvunia.
Haiwezekani kabisa msanii kuunda – sanaa zinazoonyesha hali ya maisha ya watu bila kufshi nao. Ni muhimukabisa msanii awe ameelewa matatizo na furaha za maisha ya watu kwa kulshi nao wala sl kusoma vitabu au kusomeshwa shuleni juu ya maisha yawatu hao.
Hata kama msanii ameishi maisha hayo na watu kama ameyadharau kwa njia yoyote hawezi kutengeneza sanaa zinazostahili sifa za watu hao. Msanii halisi ni lazima ajivunie maisha na desturi za watu ndlpo atakapoweza kutengeneza sanaa zitakazofaulu kuonyesha desturi zao bila kukosea.
Sanaa za msanii mashuhuri zinawatia moyo wasanii wenzake kwa kuwatia moyo hatusemi kwamba wanamwiga moja kwa moja ila wanajiuliza’maswali kwamba ikiwa mwenzao ameweza kutengeneza sanaa zinazowashangaza watu wakizitazama kwa nini wao wasiweze kufaulu kama yeye? Kutokana na kujiuliza hivyo watafanya bidii na bila shaka watafanikiwa.
Msanii halisi ana uwezo wa aina mbili, ule wa kuzaliwa na wa pili wa bidii zake. Bila shaka kipaji cha kuzaliwa ni cha maana sana katika maisha ya msanii, lakini bila bidii kipaji hicho hakimfikishi mahali popote. Kipaji cha msanii ni lazima kiende pamoja na ari, bldii na kutoridhika hatua hadi hatua mpaka amefikia ngazi ya juu sana ya maendeleo yake ya usanii.
Tunapotazama historia ya wasanii tunaona kwamba wasanii wameishi pamoja, wakishirikiana kimawazo na kupeana moyo wakati wote wa shughuli zao. Lugha yao ni ya kisanii. Mawazo yao ni ya kuelewana kisanii, kwa hiyo popote walipo wanaishi maishayafurahapamoja.
Ni kweli kabisa kusema ujuzi wa sanaa unaweza kurithiwa na mtoto kutoka kwa baba yake mzazi. Lakini sl kweli kusema kwamba watoto wote wa baba huyo ambaye alikuwa msanii maarufu watakuwa wasanil. Wakati mwlngine hutokea asizae hata mtoto mmoja msanii kama yeye n’a wakati mwingine hutokea miongoni mwa watoto wake sita au saba akatokea mtoto mmoja tu akawa msanii kama baba yake.
Wakati mwingine hutokea sehemu fulani ya nchi, kwa sababu zisizoeleweka, ikawa na wasanii wengi kuliko sehemu zingine za nchi. Na wakati mwingine katika historia ya nchi kabila fulani linaweza kuwa na wasanii wengi maarufu kuliko makabila mengine katika nchi ile ile. Haya ni mambo ambayo sisi binadamu tunaweza kueleza. Na kwa upande wetu tunafurahi tunapopewa baraka ya kuwa na wasanii maarufu katika nchi yetu.
Maanaya Sanaa katika Malsha ya Mtanzania
Sanaa ina maana kubwa na pana katika maisha ya Mtanzania. Sanaa ni kitambulisho cha Mtanzania mahali popote duniani. Sanaa nzuri, iliyo na hadhi ya kusudi la msanii ni ya pekee na haiwezi kuwako nyingine kama hiyo. Sanaa ya namna hiyo ni ya maana kwa msanii na kwa Watanzania wenzake.
Mtanzania akizitembelea nchi za nje na kwa bahati nzuri akiiona sanaa ya Tanzania katika maonyesho ya sanaa za nchi nyingine ataltambua mara moja bila kuambiwa na mtu. Ataanza kulelezea sanaa hlyo na wageni watamsikiliza maelezo yake kwa kuwa ni urlthl wa nchi yake.
Ukitembelea nchini Tanzania na kukutana na wafinyanzi wa vyungu watakushangaza waklkuelezea jinsl wanavyoheshimu mahali wanapochlmba udongo wao. Wafinyanzi hao ambao wanatoka katika kijiji chao, msituni au mlimani au kwenye mtelemko wa maji. Kwa ajili ya kuchimba udongo hapo, vlzazl hata vizazi, shimo huwa kubwa na pana. Waflnyanzl kutoka kijiji kingine, hata wasipoambiwa kwambamahali hapa ni pa wafinyanzl wengine waklpatazama tu watajua pana wenyewe, na hawatapagusa. Hakuna ruhusa mgeni yeyote kutoka Tanzania au nje ya Tanzania kuonyeshwa mahali hapa kwa kuwa udongo unaochimbwa hapa unatumiwa na wafinyanzl wa pale tu kwa kuumbia vitu vyao. Kule Narumu, Kilimanjaro, kuna mahali pa aina hii. Mahali pengine ni Pare ya Kusini. Kwa hiyo ni mahali pa heshima na udongo unaochimbwa pale lazima uwe wa manufaa kwa kuumbiavitu vyenye utashi wa waflnyanzl nawajamii kwaujumla.
Msanii akisha iunda sanaa yake na Ikiwa nzurl, sanaa ya uchoraji, uchongajl au ya udongo wa mfinyanzi, basi wananchi wanaipokea na kujivuniakwa kuwa imetengenezwa na msanii wao. Ni heshima kubwa kwa msanii ikiwa sanaa yake inapokelewa namnahii.
Msingi wa Sanaa Tanzania
Sanaa katika Tanzania zina msingi wa miaka mingi kuliko jambo lingine lolote. Tangu miaka iliyopita babu zetu walikuwa wakitumia sanaa za aina zote kwa kuonyes ha vitendo vya wakati wao.
Wasanii wa wakati huo walituachia maelezo kamili ambayo tunayatumia kujifunza historia ya kaleyababu zetu. Kama wasanii hawa wasingefanya hlvyo leo tusingeweza kujifunza sehemu mojawapo ya historia ya Tanzania. Kwa hiyo inatubidi tuheshimu kazi za wasanii wetu wa kale na kutoa shukrani nyingl kwamba hata enzl hizo zilikuwa na wasanii. Kutokana na elimu hiyo ya wasanii wa kale ni lazima tuelewe kwamba wasanii wa Tanzania ya leo wanajenga msingl wa historiayawatu waTanzaniaya baadaye.
Katika Wilaya ya Kondoa tuna picha za mapangoni zilizochorwa na wasanii wa Tanzania. Sanaa zenye watu na wanyama wa porini zilichorwa miaka mia tano iliyopita. Picha hizi, ambazo tunaweza kuziona leo, zilichorwausoni mwa majabali ya mapango, babu zetu walipokuwawakiishi.
1. Picha ya mtoto wa kike anayechukuliwa ili aolewe.
Kuna sanaa zinazoonyesha maisha ya watu wa wakati huo. Sanaa hiyo hapo juu ina watu watano mwanamke katikati wanaume wawili waliojifunika nyuso upande wa kulia na wanaume wengine wawili wasiojifunika nyuso upande wa kushoto. Wanaume wa upande wa kulia wanamvuta mwanamke ili wampeleke kwao aolewe. Wale wanaume wawili wa upande mwingine wanamzuia mwanamke ambaye ni’ mwanawao asiolewe. Hii sanaa inatufundisha mila za babu zetu za wakati huo. Baada ya wazazi wa pande zote mbili kukubaliana mtoto aolewe na mtoto mwenyewe akikubali kuolewa, siku ya mtoto huyo kuchukuliwa ni lazima nguvu itumike na wale wa nyumbani kwake wamzuie kwa kuonyesha walimpenda mwanawao. Mila hii bado tunayo kila mahali Tanzania.
2. Kongoni aliyepigwa mshale na mwindaji
Katika picha Na. 2 tunamwona Kongoni akiwa na mshale wa mwindaji mwilini mwake. Damu inatiririka kutokamwilini na huku anaumiasana. Kwaupande wa kulia anaonekana mwindajl baada ya kutupa mshale akiwa na upinde mkononi. Picha hii inadhihirisha kwamba sanaa ilikuwa na nafasi kubwa katika maisha yakilasiku tangu enzi za maisha ya mapangoni. Picha Na. 3 nayo ilichorwa kwa madhymuni hayohayo.
3. Faru aliyechorwa kwa kalamu
Wataalamu wa historla ya kale kwa kutumia sanaa hizi wameweza kutupa miaka ya binadamu walivyolshi. Kazi iliyobaki sasa ni kutumia masalia ya vitu vilivyotumiwa kama mifupa, vyungu, ili kuonyesha shughuli nyingine za maisha ya watu wa wakati huo.
Wakati fulani, ambao haujajulikana vizuri, babu zetu walianza kuoridoka mapangom na kuishi porini, wakaanza kujenga nyumba za kuishi kama tujuavyo leo. Wakati huo waliendelea ‘na sanaa zao kwa kupamba kuta na milango ya nyumba zao, viti vya kukalia, ngao, mitungi ya kuwekea maji na pombe.
Kuanzia sanaa za mapangoni za Wilayaya Kondoa na uendelezaji wa vitu vlngl wakati watu walipoishi maisha ya kawaida mpaka leo, ndiyo msingi wa sanaa zetu Tanzania. Msingi huo uko katika milanadesturi za watuwaTanzania.
Matumizi ya Sanaa katika Maisha ya Mtanzania
Katika historia ya watu wa Tanzania hakuna sanaa zilizotengenezwa bila sababu maalum katika maisha ya watu. Tanzania kote bila shaka zamani alikuwako mchoraji aliyetimiza mahitaji ya wanakijiji. Mwanakijiji humwona mganga na kumwarifu kwamba shida itakwisha ikiwa atatengenezewa sanamu ya babu yake ambaye atamshughulikia ili matatizo yake ya maradhi yaishe. Basi mwanakijiji huenda kwa mchongaji na kumwelezea matatizo yake na kumwarifu jinsi alivyotumwa na mganga. Mwanakijiji akiisha mweleza mchongaji humchongea sanamu ambayo inafafana na babu yake kutokana na maelezo aliyopewa. Akimaliza kumchongea humkabidhi mwanakijiji sanamu yababu yake. Sanamu ya babu huyo huchukuliwa na mganga nakuwekwa mahali patambiko.
Usiku wa manane yule mganga akisimama mbele ya tambiko, na mwanakijiji akisimama ubavuni mwake kimya, humwita babu yake mwanakijiji na kumwomba aonane na mwanae ili amwombe amsamehe makosa yake ili (yeye au mkewe au mwanawe) mgonjwa apone. Wakati huo huo mganga humkabidhi sehemu fulani za nyama ya kondoo mweusi au mweupe na kuziweka kwenye tambiko mbele yake. Mwishowe wote wawili wanaondoka. Kwa kweli visehemu vya nyama huliwa na wanyamawaporini lakini huaminika kwambayulebabu ndiye aliyevila vile visehemu vya nyama, kwa hiyo alimkubalia mwanaye maombi yake. Huu ni mfano wa kuonyesha jinsi sanaa inavyotumiwa katika maisha ya Mtanzania.
Wamakonde ambao ni wachongaji mashuhuri Tanzania walichongamichongp ya miti yakufunikauso wa mtu ambao ulitiwa umaridadi mzuri ya kupendekeza tangu miaka iliyopita katika historia ndefu ya kabila lao. Uchongaji wa mchongo huu ulifuata umbile la mchezaji kiongozi wa hadithi ya kijadi. Kiongozi huyu ndiye aliyejua kucheza akifuata muziki wa hadithi hiyo. Wachezaji wengine wote walimfuata huyo mchezaji kiongozi. Pia muziki uliopigwa ulikuwa na kikundi kingine pembeni, wakati wapiga muziki waljpokuwa wakifuata muziki wa hadithi. Sanamu ya kuvaa usoni ilichongwa kwa sababu ya michezo, ambayo ilikuwa na sababu kamili. Kama ilivyo katika nchi zote za AfrikaSanamu yausoni (lipiku) Sanaayamsingi, na siku zote ilichongwa ili itumike, siyo itazamwe na kupendezawatazamaj! machoni.
Wasukuma hutumia sanaa za uchoraji kwa madhumuni tofauti kabisakwa kulinganishanayaleya Wamakonde. Wasukuma wana chama chao cha wachezaji wa nyoka. Msukuma akitaka kuwa mwanachama lazima alipe ada kwanza ndipo aingie katika masomo baada ya kula kiapo kwamba atakuwa mwanachama mwaminifu ambaye atafuata mafunzo kwa dhati na kwamba hatatoa siri za chama kwa mtu yeyotenjeyaChamanakwambaakitoasiri njeatakufa. Mafunzo huchukua muda mfupi au mrefu ukitegemea ari na bidii ya mwanachama. Mwanachama mpya anajulishwa kwamba chama kina mafunzo ya aina mbalimbali; ukamataji wa nyoka, matibabu ya watu walioumwa na nyoka, uchoraji wa sanaa kwenye kuta za nyumba za kufundishia na kadhalika. Nyumba za kufundishia zinaweza kuwa vibanda vilivyojengwa na kubomolewa baada ya muda wa mafunzo, au nyumba fulani katika kijiji zilizochaguliwa na chama. Jambo la msingi kuhusu muda wa mafunzo ni kufundisha hadithi. Hadithi ikiisha eleweka mwalimu wa sanaa anafundisha wanachama wapya namna ya kuchagua picha ambazo watachora ili zieleze hadithi waliyojifunza. Picha hizo zitakazochaguliwa zitakuwa zile ambazo zltawezekana kuchorwa na mtazamaji aklzitazama aelewe hadithi yake. Plcha zlkisha eleweka wachoraji huenda porini na kutafuta rangl mbalimbali, nyinglne za maganda ya mltl, majani ya mitl, mbegu na mlzlzl ya mltl. Pla walitafuta gundi ya namna ya utomvu, kutoka miti fulani ambayo wailitumia kwa kushikia rangl kwenye uso wa ukuta. Baada ya mwalimu wa sanaa kumaliza uchoraji wa sanaa za ukutani humkabidhi mwalimu wa mafunzo plcha hizo zaukutani. Mwalimu wa mafunzo hutumia sanaa hizi za ukutani kwa kuwafundisha wanafunzi wake mpaka wamezlelewa, kila moja, na jinsl zilivyotumiwa katika hadlthl na mwalimu wa sanaa na wanafunzl wake. Ili shughuli za uchoraji ziende sawasawa kama zilivyopangwa ni lazima mwalimu wa uchoraji ashirlklane vizuri na mwalimu wa mafunzo. Wakati mwlnglne husaidiana na msaada huu hutiliwa moyo katika mpango mzima wa chama cha wachezaji wa nyoka.
Mafunzo ya elimu ya Sanaa yatolewe pamoja na elimu kwa ujumla katika ngazi mbalimbali za elimu. Hapo hapo ndipo utaratibu wa mafunzo utatengenezwa. Wachongaji watafundishwa kuchonga vitu kutokana na historia, hadithi na mazingira ya nyumbani kwao. Watafundishwa namna nzuri ya kuchagua magogo yatakayofaa kwa michongo yao na vyombo vya asili. Mafunzo kuhusu uchoraji na uumbaji yatazlngatlwa namna hiyo hiyo.
4. Ilandula Igulu.
Shetani wa alfajiri. Mkongojo alioshika unawaka moto na ni alama ya kupata kwa jua. Ana paka wa porini ambaye anamfuata popote aendapo. Picha hii imechorwa na Msukuma kwenye ukuta wa nyumba za mafunzo ya wachezaji wa nyoka.
Ni rahisi kuficha mipango ya chama ya mafunzo ya uchoraji lakini ni vigumu zaidi kuficha mafunzo ya waimbaji na wachezaji. Waimbaji na wachezaji wanapofanya mazoezi yao katika vibanda vyao ni lazima sauti zao zisikike nje ya vibanda hivyo. Hata hivyo wanachama wote hujaribu kwa bldii zao zote kuweka mipango yao yote katika hali ya siri kutoka mwanzo hadi mwisho. Matumizi ya sanaa katika ·michezo ya wanachama wa chama cha wachezaji wa nvoka ni ya juu sana
5. Yahitinde
Yahitinde (Picha Na. 5) ni mchezajl wa nyoka aliyeishi miaka mingi iliyopita. Alijulikana sana kwa mafunzo yake aliyotoakwawanafunzi wapyawachama cha wachezaji wa nyoka. Mafunzo ya mwalimu huyu Msukuma yalihusika na ukamataji wa nyoka.
Uthamlni wa sanaa katika Tanzania ni wa namna mbalimbali kwa kutegemea ni watu gani wanaohusika na mahali walipo.
Watu ambao hawakufundlshwa utaalemu wa uthamini wa sanaa wanaliona jambo hili ni kama miujiza. Hawawezi kuamini kwamba binadamu mwenzake huchora, kuchonga au huumba sanaa ya mtu au mnyama. Kama utaalamu wa namna hiyo upo basl ni wa mtaalamu wa juu ya wataalamu wa kawaida.
Kama watu wanaohusika na uthamini wanaishi sehemu za mwambao, kwa desturi hutilia mkazo uthamini wavitu kamamiti navitu vinginevyo.
Ikiwa watu wanaohusika ni wale waliopata mafunzo ya juu katika somo hili, basi kazi hii huwa rahisi na ya kufurahisha. Kwanza wanaitazama sanaa inayohusika kutokana na msanii aliyeichora sanaa hiyo. Pili wanatazama uhusiano wasanaa hiyo najamii wa msanii. Halafu wanatazama utaalamu wake katika kuchora sanaa hiyo. Kama ni sanaa ya uchoraji wa rangi wanaangalia Jinsi alivyotumia rangi hizo. Kama ni sanaa ya kuchonga mchongaji ametumia gogo lililotosha urefu na upana wa sanaa aliyokusudia kuchonga.
Kwa ujumla sanaa nzuri ya aina yoyote Tanzania hupewa sifa inayostahili. Watu wanaona ujuzi wa sanaani wapekee.Siku hizi kwaajili yamwamko mzuri wa siasa yetu ya “Ujamaa na Kujitegemea” ambayo imeenea nchini kote watu wanaona kazi ya wasanii kuwa ni mfano mzuri wa siasa hii. Pia wanao wasanii na wataalamu ambao wanatangaza sifa nzuri ya nchi yetu. Watalii na wageni kutoka nchi za nje huvutiwa na sanaa nzuri za Tanzania kwa kuwa ndizo zinazoonyesha jinsi watu wa Tanzania wanavyoishi na kuongoza mambo ya nchi yao wenyewe. Sanaa hizi nzuri zinaonyesha shughuli za Watanzania vizuri zaidi kuliko maandishi ya vitabu na kuliko hotuba hata zikiwa nzuri namna gani, kama picha Na. 6 inavyoonyesha. Sababu yake hapa ni kwa kuwa badala ya kutumia lugha ya maneno msanii anatumia jinsi mtazamaji anavyotumia macho ya rohoni mwake na kuona kile kitu ambacho fikra zake zimeona. Tunaweza kusema ni kile kile ambacho macho ya undani wa mtu yameona na hawezi kukieleza kwa maneno ya ulimi wake. Anakiona rohoni mwake kwa bujiweka mahali pa Mtanzania msanii ili aweze kukiona hicho kitu. Labda tunaweza kusema ni utashi ambao Mtanzania, msanii aliouona miongoni mwa jamii yake na akatafsiri kwa njia ya rangi au gogo la mti. Uwezo huu wa tafsiri ya utashi huu wa njia ya sanaa ndio usanii wenyewe na kila msann anao wa peke yake Hakuna msani anayefanana na msann mwingine kwa madhumuni haya Msann mzuri wa namna hn hachon au hachongi au haumbi sanaa mbili zilizo sawa sawa, kila moja ni tofauti na nyingine
6. Mama akisali
Kuhusu utaalamu wa juu wa uthamini wa sanaa mafunzo yake ni magumu. Kwa upande wa mtazamaji asiyekuwa na mafunzo yoyote akitazama sanaa anasema anaipenda, au ni nzuri lakini hawezi kutoa sababu kwa nini anaipenda
Kwa kuwa sanaa ni vitu muhimu katika maishaya watu na wanaishi navyo wakati wote ni jambo la maana kama watu wangefundishwa uthamini wa sanaa hizo. Wakisha pewa mafunzo hayo wangependa sanaa zao zaidi Masomo ya uthamini yanaweza kuendeshwa huko huko vijijini ambako sanaa hutengenezwa, na ingefaa yaende pamoja na mafunzo ya usanaa.
Kuna mitizamo mikuu minne ya kiulimwengu inayojitokeza katika suala la chimbuko la fasihi. Mitazamo hiyo ni kama ifuatayo;
Mtazamo wa kidhanifu
Mtazamo wa kidhanifu wa misingi yake katika kudhani tu kwa hiyo kufuatana na mtazamo huu inaaminika kuwa fasihi na Sanaa kwa ujumla kutoka kwa Mungu kwa hiyo mwanasanaa huipokea ikiwa imekwishapikwa na kuivishwa na Mungu huyo.
Mtazamo wa namna hii ulijitokeza tangu zamani sana wakati wanafalsafa wa mwanzo wa kigiriki na kinenzi kama vile Socrafes Plato na Anstotle,walipoanza kuingia katika ulimwengu wa nadharia ya Sanaa. katika uwanja wa nadharia ya fasihi/Sanaa ya Kiswahili kuna mifano mingi ya wahakiki wa mwanzo waliokuwa na mitazamo sawa naya wanafalsafa hao mfano F.Nkwera (1970), insha yake ya fasihi inadhihirisha uaminifu wake wa mawazo ya kidhanifu kwa kudai “fasihi ni Sanaa ambayo huanzia kwa muumba humfikia mtu katika vipengele mbalimbali -ni hekima ambayo mtu ameshirikishwa apate kumtambua muumba wake”.
Nkwera ameungwa mkono na wahakiki wengine ambao wanasisitiza mtazamo huu kwa kusema
“Mtengenezo ya Sanaa huonekana kuwa ni shughuli ya kiungu yenyekumwiga Mungu ambaye ndiye msanii wa kwanza”
John Ramadhani pia katika makala yake ya fasihi ya Kiswahili anasisitiza kuwa.
“Zaidi ya kwamba fasihi ni hisia vile vile kitendo cha mtu kubaini kazi ya Sanaa ni uigaji wa Mungu ambaye ndiye mfalme wa Sanaa zote”.
Mawazo haya ya akina Nkwera,John Ramadhani na wengine yamejaa mwangwi tu wa mawazo yaliyochakaa ambayo yalikwisha kutajwa na kushughulikiwa na wahakiki wa zamani tuliowataja kwa msimamo huu wa kidhanifu,Sanaa au fasihi havijifinyangwi kwa jitihada za akili za mikono ya mtu bali hupokelewa kutoka katika mikono mbayo mtu hana uwezo wa kuiona.
Udhaifu, mtazamo huu umepotosha maana halisi kwa kuchanganya Imani na taaluma,pia unajaribu kumtenganisha msanii na jamii yake kwani unatoa nadharia inayomwinua msanii na kufanya aonekane kuwa mtu wa ajabu aliyekaribu na Mungu kuliko watu wengine wa kawaida.
Mtazamo wa kiyakinifu
Kulingana na mtazamo huu Chanzo cha fasihi ni sawa na chanzo cha binadamu wenyewe yaani Binadamu na mazingira yake ndio Alfa na Omega ya fasihi.Iwe kwa kuumbwa au mabadiliko kuanzia chembe hai ambayo imepitia maendeleo kadha ya makuzi hata kufikia mtu binadamu alioanishwa na kazi ili kuyabadili mazingira yake.Katika harakati zake za kujiendeleza kiuchumi kila mara alijaribu hiki na kile alichokiona kinafaa alikiendeleza Zaidi na kukidumisha katika hali hii hadithi(ngano), methali, vitendawili, nyimbo, tenzi(mashairi) n.k vyote hivyo vilitungwa na kusimuliwa kwa madhumuni ya kufunza, kukosoa, kuadhibu, kuchokoza fikra na kuliwaza jamii baada ya kazi.
Sanaa hii ilirithishwa toka kizazi hadi kizazi kwa njia ya masimulizi na binadamu alivyozidi kujiendeleza kisayansi na kiteknolojia akahifadhi taaluma hii katika maandishi.Ndiyo sababu tunasema chanzo cha fasihi ni sawa na chanzo cha binadamu mwenyewe na jinsi binadamu alivyozidi na atakavyozidi ndiyo taaluma hii ilivyokuwa na kuendelea.
Fasihi inatokana na sihiri
Istilahi Sihiri’ ina maana ya Uwezo au nguvu ya kimiujiza inayotumiwa na watu kusababisha matokeo fulani.Watalaam hawa wanadai kuwa chimbuko la fasihi ni haja ya mwanadamu kukabiliana na kujaribu kuyadhibiti mazingira yake. Haja hiyo haikutimilika ipasavyo katika hatua zake za mwanzo za maendeleo ya mwanadamu kwani uwezo wa kisayansi na kiteknolojia wa mwanadamu wa wakati huo bado ulikuwa kiwango cha chini sana.Hivyo Imani au miujiza ilichukua nafasi ya sayansi na ugunduzi.Fasihi ilichimbuka kama chombo cha sihiri hivyo katika kujaribu kuyashinda mazingira,Mfano Wawindaji walichora picha ya mnyama waliyetaka kumuwinda kabla ya kwenda kuwinda,kisha walichoma mkuki au mshale kwa kuamini kuwa kitendo hicho kitatokea kuwa kweli watakapo kwenda kuwinda. Nyimbo walizoimba wakati wa kufanya sihiri hiyo ndiyo fasihi ya mwanzo.
Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba inachangnya dhima na chimbuko kwani kutumika kwa nyimbo au ushairi katika sihiri hakuthibitishi kuwa sihiri ndiyo chimbuko lake.Sihiri ni amali moja tu kati ya amali nyingi za wanadamu wa mwanzo zilizotumia ushairi.
Nadharia ya Mwigo
Wataalam wa nadharia wanadai kuwa Fasihi imetokana na mwigo(Uigaji),Katika nadharia hii inaeleza kuwa mwanadamu alianza kuwa mbunifu kwa kuiga maumbile yaliyomzunguka.Hivyo sanaa za mwanzo mara nyingi zilijaribu kusawiri vitu vilivyomo katika mazingira ,mfano wanyama,ndege,miti,watu.
Nadharia hii ni kale,ilianzisha na wataalamu wa kiyunani na walioieneza zaidi ni Plato (Republic) na Aristotle (Poetics) Plato anahusisha mwigo na dhana ya uungu.Anaeleza kuwa Maumbile na vilivyomo ni mwigo tu wa sanaa ya kiungu.Sanaa ya Mwanadamu (Hususani ushairi) ambayo huiga tu mambo hayo yaliyomo katika maumbile haiwezi kuwa na ukweli au uhalisi wa kuwa inaiga maumbile ambayo na yenyewe yanaiga kazi ya Mungu.Hivyo alishauri aina fulani za ushairi zipigwe marufuku kwa sababu zinapotosha ukweli.
Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba inasisitiza mno uigaji na kusahau suala la ubunifu katika sanaa na fasihi.Kama wasanii wangeig maisha na mazingira tu,sanaa yao ingepwaya sana na haingekuwa tofauti na picha ya fotografia au maelezo ya matendo ya mazingira na matendo ya kila siku ya mwanadamu.
SANAA ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa, umbo ambalo mtu hulitumia kueleza hisi zinazomgusa kwa kutoa kielelezo au vielelezo vyenye dhana maalum.
Kuna aina kuu tatu za sanaa. Kwanza ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa na uzuri wake kuonyeshwa wakati wowote. Hizi ni sanaa za uonyesho.
Nazo ni kama vile uchoraji, uchongaji, ufinyanzi na utarizi.
Sanaa za ghibu hazijitokezi kwenye umbo linaloonekana kwa macho au kushikika bali katika umbo linalogusa hisia. Mifano ni kama vile usairi, uimbaji, upigaji muziki n.k. Uzuri wa sanaa hizi umo katika kuzisikia.
Uzuri wa sanaa za vitendo umo katika umbo la vitendo, na ili kuupata uzuri huu yampasa mtu kutazama vitendo vikifanyika.
Umbo hili linalazimisha kuwepo kwa msanii na mtazamaji wa sanaa mahali pamoja kwa wakati mmoja ama sivyo sanaa haikamiliki.
Hali hii ndiyo iliyosababisha sanaa za vitendo kuitwa sanaa za maonyesho, kwa sababu lazima wakati zinapotendeka awepo mtu wa kuonyeshwa, maana uzuri wake umo katika vitendo vyenyewe.
Kwa hiyo sanaa za maonyesho ni kitendo chochote kinachohitimishwa na dhana inayotendeka, mtendaji, uwanja wa kutendea na watazamaji. Zipo nadharia tatu zinazoelezea chimbuko na asili ya sanaa za maonyesho.
MICHEZO YA KUIGIZA
Sanaa za maonyesho ni michezo ya kuigiza, ama ni michezo inayoonyeshwa kwenye jukwaa lenye pazia na taa nyingi za jadi. Huu ni mtazamo mmojawapo ambao unaaminiwa na baadhi ya wataalamu kwa kuwa unasisitiza kwamba sanaa za maonyesho lazima zichezwe jukwaani, kuwepo na pazia na taa nyingi.
Nadharia hii inatuaminisha kuwa sanaa za maonyesho ni tamthilia tu, jambo ambalo linaleta shaka kidogo.
Tamthilia ni utanzu ulioletwa na Wakoloni kwa hiyo, kuamini nadharia hii ni sawa na kusema kuwa hakuna sanaa za maonyesho zenye asili ya hapa Afrika Mashariki.
Ni sawa na kusema kuwa kabla ya ujio wa Wakoloni sisi tulikuwa hatuna sanaa zetu wenyewe. Wazo hili si kweli na ni potoshi. (Mhando & Balisidya 1976).
Mtazamo huu unatokana na fasili ya sanaa za maonyesho inayodai kuwa sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa za mchezo, mchezaji, uwanja wa kuchezea na watazamaji.
Dosari kubwa katika ufafanuzi huu imo katika neno mchezo (play). Neno hili lina maana duni likilinganishwa na hali na umuhimu wa sanaa za maonyesho zenye asili ya Kiafrika.
Tukichukua kwa mfano unyago, jando, kusalia mizimu au masimulizi ya hadithi, ambayo ni mifano ya sanaa za maonyesho zenye asili ya Kiafrika, tunakuta zile sifa zote zipo.
Isipokuwa tunajua kuwa shughuli zote hizi si mchezo na umuhimu wazo hauruhusu hata kidogo kuingiza neno mchezo. Shughuli hizi zina maana muhimu ambayo inahusu maisha ya binadamu katika jamii yake.
Ni shughuli zinazobeba wazo maalum lenye lengo la kujenga utu wa mwanajamii na kubainisha taratibu za maisha yake. Basi vipi tuseme shughuli hizi zina sifa ya mchezo?
Wazungu wanaridhika na neno hili kwa sababu sanaa za maonyesho za utamaduni wao aghalabu zinafanywa kwa masihara tu.
Sanaa za maonyesho zao zaidi ni kwa madhumuni ya kujiburudisha au pengine kutafuta kipato.
Lakini kila aina ya sanaa za maonyesho ya Kiafrika ina dhana fulani ndani yake, kwa mfano kuhusu maana ya maisha, utekelezaji wa madaraka ya kiutu uzima, ushujaa, maadili au mafunzo ya historia ya jamii.
Kwa hiyo basi sanaa za maonyesho za Kiafrika ni dhana zilizo kwenye umbo linalotendeka na katu si mchezo. Kutokana na utamaduni wa Kiafrika, tunaweza kusema kuwa sanaa za maonyesho ni dhana inayotendeka.
Na ili dhana hii itendeke anahitajika mtu wa kuitenda. Mtendaji huyu huhutaji uwanja wa kutendea hiyo dhana na wakati akiitenda wanakuwapo watazamaji.
VICHEKESHO
Wakati Mkoloni alituletea sanaa ya maonyesho ya kikwao, sisi tulishiriki katika tamthilia za Shakespeare kama washiriki au watazamaji tu.
Tamthilia hizi hazikuwa na maana yoyote kwetu kutokana na kuwa zilibeba na ziliongelea utamaduni wa Kizungu. Tulifurahishwa na vile vitendo vilivyofanywa kwenye jukwaa katika tamthilia hizi na hivyo vitendo hivi vilituchekesha tu.
Basi jambo kubwa kwa Mwafrika ikawa ni vile vichekesho na hivyo kudhani kuwa jambo muhimu katika tamthilia ni kule kuchekesha kwake.
MAIGIZO
Wazo hili limetokana na tafsiri mbovu ya neno “play” ambalo lina maana ya mchezo wa kuigiza. Inawezekana aliyetafsiri neno hili alifuata nadharia za zamani sana za drama, ambapo ilidhaniwa kuwa uigizaji (imitation) ndio kiini cha drama.
Hata hivyo nadharia hii ilitupiliwa mbali kwa vile haikudhihirisha kiini hasa cha drama. Wengi wamepotoshwa na wazo kuwa uigizaji ndio kiini cha sanaa za maonyesho kama vile neno michezo ya kuigiza linavyoonyesha.
Hivyo, hata katika kutazama sanaa za maonyesho za asili wengi wamekuwa wakitazama iwapo kuna uigizaji.
Na hapa wengi wanakwama kwani katika unyago, jando, kusalia miungu n.k hakuna uigizaji bali wanaoshiriki wanashika nafasi fulani fulani. Hivyo ni bora kutumia neno tamthilia pale tunaporejelea “play.”
Ingawa zote ni sanaa za maonyesho, zina misingi tofauti kutokana na tofauti za utamaduni wa jamii husika.
Dhana ya fasihi simulizi imekuwa ikijadiliwa kwa miongo mingi na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo:- Mulokozi, anafafanua kwamba, Fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi. Hapa anamaanisha fasihi simulizi ni tukio ambalo hufungamana na muktadha fulani ya kijamii wenye kutawaliwa na fanani hadhira, fani inayotendwa, tukio, mahali na wakati.
Wamitila, (2003) anasema kuwa, fasihi simulizi ni sanaa ya lugha inayotungwa na kubuniwa kwa mdomo bila kutumia maandishi. Aidha fasihi simulizi ni tukio linalofungamana na muktadha fulani wa kijamii na mwingiliano wa fanani, hadhira, fani inayotendwa, tukio, mahali na wakati.
OKpewho, I (1992) anasema, kuwa fasihi simulizi humaanisha fasihi itolewayo kwa neno la mdomo. Hapa anaungana na Balisidya kuwa pasipo mdomo, fasihi simulizi haikamatiki.
Baada ya kufafanua dhana ya fasihi simulizi kulingana na wataalamu mbalimbali, sasa tuijadili dhana ya sanaa za maonyesho.
Penina Muhando na Ndyanao Balisidya (1976) wanajadili kwa kina sana dhana ya sanaa za maonyesho. Mjadala wao umejikita sana katika swala lisemalo kuwa “sanaa za maonyesho ni nini?
Kutokana na swali hilo wanasema kuwa, utapata majibu mbalimbali lakini mara nyingi majibu yatakuwa kama haya yafuatayo:
– Sanaa za maonyesho ni michezo ya kuigiza
– Sanaa za maoanyesho ni michezo ionyeshwayo kwenye jukwaa lenye pazia na mataa mengi ya rangi.
-Sanaa za maonyesho ni michezo ya Shakespeare kama vile Mabepari wa Venisi.
– Sanaa za maonyesho ni vichekesho
– Sanaa za maonyesho ni maigizo yanayochekesha au kufurahisha na mengineyo yanayofanana na hayo.
Kwa kufuata majibu haya huenda tukafikiria kuwa sanaa za maonyesho ni tamthilia (michezo ya kuigiza) tu yaani ni kitendo chochote chenye sifa nne ambazo ni mchezo, mchezaji, uwanja wa kuchezea na watazamaji. Kwa upande mwingine tunaelewa kuwa tamthiliya ni aina ya sanaa iliyoletwa kwetu kutoka nchi za kimagharibi wakati wa ukoloni ambapo walileta drama na tamthiliya za Shakespeare, sisi tukazipenda na tukazionyesha na kuziendeleza mpaka kufikia hatua ya kuandika tamthiliya za Kiafrika kwa lugha za Kiafrika kuhusu maisha ya jamii ya Kiafrika.
Hivyo basi, iwapo tutafikiria kuwa sanaa za maonyesho ni tamthiliya tu, basi ni kusema kuwa kabla ya mkoloni kutuletea tamthiliya tulikuwa hatuna sanaa za maonyesho za kijadi.
Wazo hili ni potofu sana kwani tunazo sanaa za maoneysho zenye asili ya hapa hapa Afrika. Hii ni kwa sababu tunasema kuwa sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa za mchezo, mchezaji, uwanja wa kuchezea na watazamaji kama vile jando, unyago, kusalia mizimu au masimulizi ya hadithi.
Dosari kubwa katika ufafanuzi huu imo katika neno mchezo (play) lenye maana duni sana likilianganishwa na umuhimu wa sanaa za maonyesho zenye asili ya Afrika. Tukichukua kwa mfano; jando, unyago, kusalia mizimu au masimulizi ya hadithi ambayo ni mifano ya sanaa za maonyesho zenye sifa zote nne. Isipokuwa tunajua kuwa shughuli zote hizi siyo michezo na umuhimu wao hauruhusu hata kidogo, kuingiza neno mchezo kwa kuwa zina maana muhimu ambayo inahusu maisha ya binadamu katika jamii yake.
Katika jamii ya Kiafrika ambayo utamaduni wake ulikuwa haujaingiliwa na utamaduni wa nchi za kigeni, ilikuwa na aina nyingi sana za sanaa za maonyesho. Kwa kuwa jamii hizo zilikuwa zimegawanyika katika makabila mengi, kila kabila lilikuwa na aina zake za sanaa za maonyesho. Lakini kwa ujumla wake sanaa za maonyesho za asili zinaweza kugawanywa kwenye makunmdi makubwa matano kwama vile sherehe, ngoma, masimulizi ya hadithi, kusalia miungu na majigambo. Sanaa hizi za maonyesho za kijadi zinazoingia kwenye kundi moja zaweza kitofautiana hapa na pale kimtindo lakini kimsingi huwa ziko sawa.
Hivyo basi baada ya kuifafanua kwa kina dhana ya sanaa za maonyesho pamoja na asili yake, zifuazo ni hoja zinazoelezae ni jinsi gani sanaa za kimagharibi zilivyoathiri sanaaa za maonyesho za Kiafrika na fasihi simulizi kwa ujumla.
Sanaa za maonyesho za kimagharibi zilizifanya sanaa za maonyesho za Kiafrika kujikita katika dhana za vichekesho yaani ni maigizo yanayochekesha tu (drama), Kwa kuwa tangu awali sanaa za maonyesho za Kiafrika zilikuwa na umuhimu wake katika jamii husika, lakini wakati wa mkoloni walileta sanaa za maonyesho za kikwao yaani drama sisi (Waafrika) tulishiriki kama washiriki au watazamaji tu, mfano Waafrika walichukulia kule kushiriki kwao ni kama kujiburudisha au kujifurahisha tu. Walifurahishwa na vile vitendo vilivyofanywa kwenye jukwaa na katika kufurahi walichekeshwa pia. Basi ikawa jambo linalojitokeza kwenye tamthiliya hizi ni kule kuchekesha na walidhani kuchekesha ndiyo madhumuni ya tamthiliya.
Watu wa magharibi ndio waliotufanya tufikiri hivyo kwa sababu hawakutambua ama kwa makusudi ama kwa kutoelewa Waafrika walikuwa na sanaa zao za asili. Walituletea drama kama vile wanatuletea sanaa mpya ambayo aina yake haikuwapo hapa Afrika. Mwafrika kwa kuwa aliendelea kujua kuwa sanaa za maonyesho ni tamthiliya (drama). Baadaye Waafrika walipanua dhana hizo na kuja na tamthiliya mpya katika hali ya vichekesho. Utunzi wa vichekesho ulijikita katika misingi ya kitamthiliya iliyozungumzia zaidi mazingira ya Kiafrika.
Kutothamini sanaa za maonesho za kiafrika, wakoloni kutotambua ama kwa makusudi kwamba kuna sanaa za maonesho za Kiafrika hata kama walifahamau walipuuza wakatupilia mbali sanaa za maonesho za Kiafrika wakaingiza drama kama sanaa mpya na mkazo ukatiliwa zaidi katika sanaa hiyo mpya. Mfano kupitia dini na elimu ya watu wa magharibi iliwafanya Waafrika kuanza kudharau sanaa zao za jadi na kuanza kuingiza sanaa za kigeni shuleni na ibada za kigeni. Kufuatia vitendo vyote vya sanaa za maonyesho.
Wageni wa magharibi walitumia mbinu mbalimbali kufuta na kuondoa vitendo mbalimbali vya jadi na tamaduni za Kiafrika ambavyo ndivyo vilivyobeba sanaa za Kiafrika kama vile jando na unyago, kutambikia mizimu, ngoma za jadi nk. ambavyo vitendo hivi viliitwa vya kishenzi. Njia walizotumia ni kuingiza dini na elimu za kimagharibi.
Sanaa za maonesho zilionekana kama maigizo, (plays) wazo hili limesababishwa na tafsiri mbovu ya neno “play” ambalo limefasiriwa kuwa mchezo wa kuigiza kuita [play] mchezo wa kuigiza ni kosa linalotokana na aidha kutokuelewa kiini cha drama ama aliyetoa tafsiri hii alikuwa amefuata nadharia za zamani sana za drama ambapo walidhani uigizaji (imitation) ndiyo kiiini cha drama, hivyo basi dhana hii kuwa sanaa za maonesho ni maigizo imezifanya sanaa za jadi za Kiafrika kupoteza maana.
Kwa hiyo kutokanan na dhana hii ya kuwa sanaa za maonesho ni maigizo (plays) inazinyima hadhi sanaa jadi za kiafrika zenye umuhimu katika jamii husika.
Kuingizwa utamaduni wa kimagharibi; Waafrika walikuwa na utamaduni wao ambao unaendana na matendo yanayoonesha sanaa za maonesho na fasihi ya Kiafrika matendo hayo ni kama jando unyago, kusalia mizimu maleba, ngoma masimulizi ya hadithi na majigambo. Kutokana na kuingia na kukua kwa tamaduni za kigeni Waafrika waliacha kuteketeza sanaa zao za Kiafrika na kuiga sanaa za kimagharibi ambazo zilitawaliwa na tamaduni za kimagharibi.
Athari katika utendaji, kukua kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia ya kimagharibi kuliathiri utendaji wa sanaa za maonesho na fasihi simulizi kwa ujumla kutokana na maendeleo hayo, fasihi simulizi ya Kiafrika ilipopoteza dhana ya utendaji ambao ndio uhai/uti wa mgongo wa fasihi simulizi na sanaa za maonesho.
Ingawa fasihi ya kimagharibi ina athari katika sanaa za maonesho za Kiafrika, pia imeweza kutoa mchango mkubwa katika sanaa zetu.
Nchi za kimagharibi zimeweza kutoa mchango mkubwa katika kukuza sanaa za maonesho na fasihi simulizi ya Kiafrika:
Walisaidia katika uchambuzi wa tamthiliya, Uchambuzi wa tamthiliya kwa kutumia mbinu za kiaristotle na shake spear ilichangia kukuza sanaa za maonesho za kiafrika hasa katika kipengele cha utendaji kwani Anstotle anasema tamthiliya lazima ziwe na sehemu ya kutendea na pawepo na mapazia, taa nk. Hivyo, ilipelekea watunzi wa sanaa za maonesho za Kiafrika hasa tamithiliya kuongeza utendaji wake, mfano tamthiliya ya orodha imefuata mfumo huohuo wa uandishi.
Waafrika kuanza kuandika tamthilia zao; Ushiriki wa Waafrika katika Tamthilia za Sharkespear iliwafanya waanze kuandika tamthiliya zinazozungumzia mandhari ya Kitanzania. Watanzania walishiriki katika tamthiliya ambazo Watanzania hawakuwa wanazielewa kwa hivyo wakajaribu kutunga vijitamthilia vidogovidogo kufuatana na misingi ya Kizungu lakini vilivyoongelea jamii ya Mtanzania ya wakati ule. Hivyo uwezo wa Watanzania (Waafrika kuweza kuandika vijitamthiliya vidogo vidogo ni- mchango kutoka kwa watu wa magharibi kwani waliweza kutumia misingi ya kimagharibi. Aina ya tamthiliya hiyo iliitwa/ilijulikana kama “VICHEKESHO”, vichekesho vilishamiri sana hasa kati ya watoto wa shule ambao bila ya uongozi wa walimu wa kigeni walitunga vichekesho na kuvionesha mfano wa vichekesho “Mshamba wa Mji, “Bwana tajiri na mtumishi wake” au “mshamba wa siagi”
Wageni walisaidia katika uhifadhi wa sanaa za maonesho na fasihi kwa ujumla, hii inamaana Waafrika waliandika tamthiliya zao tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambao zilihifadhiwa kichwani lakini kutokana na Elimu waliyoipata kutokea kwa mkoloni waliweza kuandika au kutunga vichekesho mbalimbali na kuvihifadhi katika, santuri (CD) na maandishi, mfano “mshamba wa siagi” na “mwafrika mwenye elimu” ambapo hii inaonesha mchango wa watu wa magharibi katika kukuza sanaa za maonesho fasihi simulizi kwa ujumla.
Walichangia katika kukomaza sanaa za maonesho na fasihi kwa jumla, Waafrika kuanza kuchapa vitabu, kuanzia mwaka 1961 vitabu mbalimbali viliandikwa vya tamthiliya ambavyo vilizungumzia mambo mbalimbali ya mifumo ya mwanadamu kama uchumi; kijamii; na kisiasa ambapo awali havikuzungumiziwa katika vijitamthilia vidogo vidogo vilivyo lenga kuchekesha na kutoa ujumbe fulani. Hivyo mabadiliko kutoka kuandika vichekesho hadi kuandika mambo ya kijamii yahusuyo Afrika. Mfano; KINJEKITILE, ALIYEONJA PEPO, WAKATI UKUTA, HATIA, TAMBUENI HAKI ZETU.” Kazi hizi ziliandikwa baada ya mwaka 1965.
Waafrika kuanza kuandika kwa ngonjera za Kiswahili; nchi za magharibi zilichangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza sanaa za maonesho na fasihi simulizi kwa ujumla, kwani, kutokana na mambo mbalimbali, yaliyofanywa na nchi za magharibi kama kuwashirikisha Waafrika ambao baadaye waliweza kuandika tamthiliya na ngonjera mbalimbali. Mfano katika miaka 1967 wakati wa kipindi cha Azimio la Arusha ngonjera nyingi katika kipindi hiki zilizungumzia mfumo ya maisha kisiasa, kiuchumi, na kijamii ambapo kazi nyingi ziliandikwa zilizozungumzia juu ya Azimio la Arusha.
Pamoja na athari mbalimbali zilizosababishwa na watu wa magharibi katika sanaa ya maonyesho na fasihi simulizi ya Kiafrika kwa ujumla. Nchi za magharibi zimeweza kuchangia kwa kiasi fulani katika kukua kwa fasihi simulizi na sanaa ya maonesho ya Kiafrika.
Hivyo basi, pamoja na athari na mchango wa nchi za magharibi katika sanaa ya maonesho na fasihi simulizi kwa ujumla imekabiliwa na changamoto mbalimbali kama mipangilio mibaya katika kupanga muda wa kuandaa na kuonesha sanaa hizo, uhaba wa fedha za kuendeshea shughuli zinazohusiana na sanaa ya maonesho na fasihi kwa ujumla pia uchache wa wataalam wanaohusika na fasihi simulizi ya Kiafrika na sanaa ya maonesho kwa ujumla.
MAREJEO
Mhando, P na N. Balisidya; (1976 ). Fasihi na Sanaa za Maonesho. Tanzania Publishing: Dar-es-Salaam.
Wamitila, W. K. (2003). Kichocheo Cha Fasihi Simulizi na Andishi.