MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 52 online users.
» 0 Member(s) | 52 Guest(s)

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  BURIANI PROFESA EUPHRASE KEZILAHABI
Posted by: MwlMaeda - 07-24-2021, 07:14 AM - Forum: Wasifu/Tawasifu - No Replies

[Image: euphrase-kezilahabi.jpg]
Kumbe ni kweli kwamba kilichoandikwa kimeandikwa. Wakati ninamlilia mwandishi huyu ambaye amekuwa kioo changu katika fasihi, wakati ninatafuta niandike nini juu yake, nikagundua kwamba kumbe linifanya uhakiki wa kitabu chake cha Nagona.
Labda, nitoe siri ya Kitabu cha Nagona na Mzingile. Hivi ni vitabu viwili vya Profesa Kezilahabi, ambavyo si vitabu vyepesi kuvisoma. Mimi nilivisoma zaidi ya mara tatu bila kufanikiwa kuelewa kilichoandikwa. Nilipokutana na Profesa Mulokozi, nikalalamika, yeye akaniambia vinaeleweka tu. Nikajipa moyo, nikasema kama Profesa Mulokozi, anaamini vitabu hivi vinaeleweka, kwa nini mimi nisivielewe? Ndipo nikaendelea kuvisoma hadi nikafanikiwa kuvielewa na kugundua kwamba hivi ni vitabu viwili tofauti ingawa watu wengi wanafikiri ni kitabu kimoja. Hivyo ninamshukuru sana Profesa Mulokozi, kwa kunipatia moyo wa kuendelea kuvisoma vitabu hivi hadi nikafanikiwa kuvielewa.
Na sioni namna nyingine ya Kumlilia Profesa Kezilahabi, kama kurudia uhakiki wangu wa Nagona. Ninauweka hapa, nikimlilia na kusherehekea maisha yake ambayo yalikuwa kioo cha fasihi katika taifa letu la Tanzania, Afrika na dunia nzima.
Mungu, amlaze mahali pema peponi marehemu Profesa Euphrase Kezilahabi.
UHAKIKI WA KITABU: NAGONA
1. Rekodi za Kibibliografia.
Jina la kitabu kinachohahikiwa hapa ni Nagona, Kimeandikwa na Profesa Euphrase Kezilahabi. Mchapishaji wa kitabu hiki ni Dar es salaam University Press na amekipatia namba ifuatayo katika sekwensia ya vitabu duniani (ISBN): 9976 60 071 2. Kitabu kina kurasa 62 . Na anayekihakiki sasa hivi katika safu hii ni mimi Padri Privatus Karugendo.
II. Utangulizi
Nagona, ni hadithi ya kubuni. Imetungwa kwa mtindo wa uhalisiamazingaombwe. Ni mtindo wa kuandika unaofanana sana ule wa mwandishi Garcia Marquez wa Kolombia, Kyallo Wadi Watimila wa Kenya, Juan Rulfo wa Meksiko, Gunter Grass wa Ujerumani na Said Ahmed Mohamed wa Zanzibar. Waandishi hawa ambao kwa kiasi kikubwa wanatoka mataifa tofauti na lugha tofauti wanaunganishwa na uamuzi wao wa kuandika riwaya kwenye mtindo usiokuwa kawaida.
Kwa kuzingatia kazi hizi za fasihi, twaweza kusema kwamba
waandishi wote hawa wamo kwenye tapo moja kwani wametunga sanaa zao hizi, kusawiri uhalisia kama ulivyo hasa lakini kwa kujumuisha
vipengele vya kimazingaombwe .Masimulizi ya mambo ya kawaida na masimulizi ya matukio yasiyokuwa ya kawaida inakaribiana na Istilahi ya ‘uhalisiamazingaombwe’, ambayo mwanzoni ilitumika kuwahusu
wachoraji katika miaka ya 1920, inatumika kufasili kazi za bunilizi za kinathari za waandishi niliowataja hapo juu na Jorge Luis Borges wa Argentina. Waandishi hawa wanasukanisha uhalisia uliochongwa kwa njia maalum katika ruwaza inayobadilikabadilika daima, huku wakiwakilisha matukio ya kawaida na maelezo ya kina sambamba na vipengee vya kifantasia na kindoto, na kwa kutumia mambo yaliyotokana na visaasili na hekaya.
Nagona, ni riwaya ya kumfanya mtu kutafakari. Ujumbe mzima ni juu ya maisha! Lakini mwandishi anatufanya kutafakari juu ya maisha kwa njia ya uhalisiamazingaombwe. Kwa upande mmoja anatuelezea mambo ya kueleweka kwa hali ya kawaida, na kwa upande mwingine anatuingiza kwenye ndoto na mazingaombwe. Kuna mambo yasiyokuwa ya kawaida. Mfano mtu anakuwa kijana, lakini kuna hali fulani ikimwingia anakuwa mzee! Maana yake ni kwamba hekima na busara vinamfanya mtu kuwa mzee. Mwili unabaki ni wa kijana, lakini roho yake na akili vinakuwa vya mzee!
Nagona ni riwaya inayothibitisha upevu wa falsafa ya Kezilahabi kuhusu dhana ya maisha. Katika riwaya hii, maisha yanasawiriwa katika mtazamo wa dhihaka na kejeli. Ndiyo maana mwandishi anatega kitendawili kwamba waliobahatika kuishi, “…. Walikufa katika rumani. Walikufa wakicheka hali wameshikilia mbavu zao kwa vichomi. Baadhi walikanyagwakanyagwa, wakafa wakicheka. Wengine… walitumbukia katika kisima cha ndoto zao wakafa kwa uwingi wa ndoto walizokunywa…”
Nagona, ni hadithi inayotaka kufanana sana na ile nyingine ya Kezilahabi iitwayo Mzingile. Wachambuzi wengi wamekua wakichambua hadithi hizi kama moja. Lakini kuna tofauti kubwa. Nitaonyesha tofauti hizi kwa kuvichambua vitabu hivi viwili tofauti.
Nagona, ni kitu kinachotafutwa. Wamekitafuta wengi lakini wameshindwa kukipata. Mashujaa wengi wamejitahidi lakini wameshindwa. Nagona, anatafutwa kama mnyama, anawindwa! Na shujaa ni lazima awe na upinde na mshale. Hatimaye Nagona, anajitokeza kama msichana mzuri. Lakini shujaa anayefanikiwa kumpata anashindwa kufanya naye mapenzi. Hatimaye Nagona, anaelekea kuwa ni Hekima, busara, mkombozi au ni Mungu mwenyewe?
“Nagona ni mwanga. Ni kama jua lililopatwa na mwezi. Ukitazama kwa muda mrefu unaweza ukapofuka na usione chochote wakati wote wa uhai wako. Lakini ajabu ni kwamba unavutwa kumtazama bila kinga licha ya hatari zake. Ukishamwona hamu ya kuendelea kumwona haishi. Akitoweka utaendelea kumsaka kila mahali bila woga”
“Nikimwona nitamtambuaje?”
“ Penye mwanga hukosi kupaona. Alipo, uwongo umejitenga, ni yeye peke yake aliyepo pale. Utajikuta umevutwa kuelekea kwake. Lakini hataruhusu umshike awe wako peke yako, maana ni wa kila mtu. Kila mtu anamtambua na ndiyo maana anavuta na anaambaa, sisi tunavutika na tunamwambaa. Hakuna awezaye kuepukana na mvuto wake” (Uk 45).
Mwokozi wa pili ndiye atakaye uokoa ulimwengu. Mwokozi huyu atakuja wakati wa Ungamo kuu au wakati wa Ngoma kuu. Kizee mwenye fimbo, ambaye kwa namna nyingine ndiye kama Mungu mwenyewe, anasababisha vurugu katika ngoma na inatokea maangamizi makubwa. Wanaopona ni pamoja na mhusika mkuu Anayepewa kazi ya kumleta mtoto Nagona, anayezaliwa siku hiyo ya Ngoma Kuu na huyu ndiye analeta ukombozi wa pili!
Kabla ya kufanya uhakiki wa kitabu hiki ningependa kuelezea mazingira yanayokizunguka.
III. Mazingira yanayokizunguka kitabu
Profesa Euphrase Kezilahabi, amezaliwa wakati wa ukoloni. Amesoma shule ya msingi na sekondari wakati wa ukoloni. Amepata elimu ya juu wakati wa uhuru, amekulia kwenye vuguvugu la Azimio la Arusha. Ni wakati ambapo taifa lilitegemea zaidi fikra na uongozi wa Mwalimu. Mawazo mbadala ilionekana kama msaliti. Lakini pia ni wakati ambapo kila maandishi lalichujwa ili kulinda maadili. Kitabu kama Rosa mistika cha Kezilahabi, ambacho kilizungumzia mahusiano ya kimapenzi, kilipigwa marufuku; na labda huu ukawa mwanzo wa Kezilahabi kufikiria kuandika kwa mafumbo. Mpaka mtu agundue kwamba Nagona, inaongelea mapenzi ni hadi karne nyingine. Kezilahabi pia ameshuhudia Azimio la Arusha likitupwa nyuma na kuanzishwa kitu kingine ambacho hakijulikani vizuri.
Nagona, ni hadithi ambayo imetungwa wakati huu wa kuyumba kwa nchi yetu. Mwelekeo ukiwa haujulikani vizuri tunakwenda wapi? Hivyo mtu anaposoma Nagona ambayo iko kwenye mtindo wa uhalisiamazingaombwe, ni lazima kuweka maanani mwandishi anaandika akiwa katika mazingira gani.
Ni wakati ambapo watu walianza kutupilia mbali utamaduni wa Tanzania na kukumbatia utamaduni wa magharibi. Ni wakati ambapo fikra haikutawala tena, fedha ilianza kuzungumza. Rushwa iliota mizizi hadi kwenye chaguzi na watu kuuza huru wao. Ni wakati ambapo wasomi na wenye kutaka kufikiri walionekana kama vichaa.
“Basi hayo ndiyo yalikuwa maktaba ya taifa. Walikata shauri kutupa vitabu vyao vyote huko. Vimeoza na miti imeota juu yake. Waliopata kupita humo wanasema kuna mizungu. Waandishi wanalilia kusomwa wasife” (Uk 5)
Pia tukumbuke kwamba Kezilahabi, amesoma kwenye shule za seminari. Yeye ni Mkatoliki ambaye anaona wazi hasara kubwa waliyoipata wale wote walioziacha dini zao za jadi na kuingia dini mpya za Ukristu na Uislamu. Hili analiongea kwa uangalifu mkubwa na kwa mafumbo ya hapa na pale.:
“Mimi nahubiri habari za Kristo. Wewe unahubiri upagani”
“Wewe ni mcheza ngoma ya twiga nje ya duara. Twiga hawezi kuhimili ngoma yenye vurumai, vurugu, na ghasia katika gharika la hisia na fikra” (Uk 10).
Hapa mwandishi anatuchorea mabishano kati ya babu mwenye imani yake ya jadi na Padri ambaye alikuwa anahubiri neno la Mungu. Na ukweli kwamba imani hizi za kigeni zilileteleza watu waanze kuishi bila kufikri, bila kuhoji: “ Katika mkono mmoja alikuwa amepakatishwa Biblia Takatifu na mwingine Korani Tukufu. Mdomo wake uliwa umefungwa kwa kitambaa cheupe na juu ya kitambaa hiki kwenye mdomo palionekana maandishi yaliyosema “Kimya ni hekima” (Uk 3).
“Watu wa mji huu hawasemi. Anayezungumza katika mji huu ni mmi, na labda mzee mmoja karibu na mto. Sisi sote wawili tunaitwa vichaa katika mji huu. Wanatuona wendawazimu. Wakituona tu wanakimbia” (Uk 5).
Kwa kifupi ni kwamba Mwandishi, aliandika hadithi hii fupi, lakini yenye fikra nzito akiwa kwenye mazingira ya vita, mazingira ya mapambano: Ni kupambana na ukoloni, ukoloni mambo leo, utandawazi, siasa uchwara, dini za kigeni, hadi mtu anapopata Uhuru wa kweli. Nagona ni kujitambua, kujikubali na kuendeleza kizazi. Ndo maana mwisho wa hadithi yake mtoto anazaliwa.
Euphrase Kezilahabi alizaliwa 13 Aprili 1944 huko Namagondo kisiwani Ukerewe kilichopo ndani ya Ziwa Viktoria. Babake Vincent Tilibuzya alikuwa msimamizi wa kijiji na Euphrase alikuwa na ndugu 10 yaani wavulana 5 na wasichana 5. Alisoma shule ya msingi ya Nakasayenge halafu tangu 1957 Seminari ya Kikatoliki ya Nyegezi aliyomaliza mwaka 1966.
1967 alijiandikisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akasoma ualimu na fasihi hadi digrii ya B.A. katika mwaka 1970. Mwaka uleule 1970 akawa mwalimu wa shule ya sekondari Mzumbe (Morogoro) halafu kwenye shule ya sekondari ya Mkwawa (Iringa).
1971 alirudi chuoni Dar es Salaam akawa mhadhiri msaidizi wa chuo alipoandika pia tasinifu ya M.A. kuhusu riwaya za Shaaban Robert, tangu 1974 mhadhiri kamili na 1978 mhadhiri mwandamizi. Akaendelea na masomo ya Ph.D. huko Marekani kwenye Chuo Kikuu cha Wisconsin Madison alipotoa tasinifu yake mwaka 1985 kuhusu “African Philosophy and the Problem of Literary Interpretation”. Sasa ni profesa wa lugha za Kiafrika kwenye Chuo Kikuu cha Botswana.
Euphrase Kezilahabi ni mwandishi ambaye ametoa mchango mkubwa katika fasihi ya Kiswahili. Yeye ndiye anatambuliwa kama mwanzilishi wa ushairi huru (free verse) katika Kiswahili alipoandika Kichomi na baadaye Karibu Ndani.
Kezilahabi anajulikana kwa ushujaa wake wa kujaribu mitindo mipya katika uandishi wake na ukisoma vitabu vyake kama Rosa Mistika, Dunia Uwanja wa Fujo, Kichwamaji, Gamba la Nyoka na Kaptula la Marx utakutana na chembechembe za upya katika nyanja mbalimbali na hasa matumizi ya falsafa.
Baadhi ya maandiko yake ni:
Riwaya:Rosa Mistika (1971),Kichwamaji (1974), Dunia Uwanja wa Fujo (1975),Gamba la Nyoka (1979),Nagona (1987/1990),Mzingile (1991)
Mashairi: Kichomi (1974),Karibu Ndani (1988) Dhifa (hakijatolewa bado).
Tamthiliya: Kaptula la Marx (1978/1999)
Baada ya maelezo haya sasa tuone kitabu chenyewe kwa muhtasari.
IV. Muhtasari wa Kitabu
Kijana shujaa, akiambatana na mashujaa wengine ambao ni Nabii, Mtume, Mfuasi na Mtenzi, wanasafiri kumtafuta Nagona. Hawa walijulikana kama askari wa mwanga. Huyu Nagona, anatafutwa kama paa! Anawindwa. Safari ya kumfikia ni ngumu sana. Mwandishi, ndipo anapoonyesha ukomavu wa uandishi wake. Safari hii ya kumsaka Paa, inakuwa ya karne – ingawa kwa kutafakari kwa kina ni safari ya mtu ndani mwa nafsi yake. Ni safari ya kutafuta ukweli!
Njiani mashujaa wa mwanga wanakumbana na vikwazo vingi. Watu wengi walijaribu kumtafuta Paa huyu bila ya mafanikio. Na wengi walishindwa masharti na kukatwa vichwa. Mashujaa wa mwanga wanaonyeshwa vichwa vilivyokatwa. Pamoja na vitisho vyote, bado walitaka kuendelea kumsaka Paa hadi wampate!
Babu alitoa ushuhuda jinsi ilivyo vigumu kumkamata Nagona: “ Ahaa! Nagona! Kwa muda wote wa uhai wangu alinipiga chenga. Mara nyingi nilimwona kwa mbali. Mara chache sana nilikaribiana naye. Sikupata nafasi ya kumweka mikononi mwangu nilipokuwa karibu naye. Daima alirudi kinyumenyume, nami niliendelea kumfuata nikiongozwa na nguvu fulani. Nilipokuwa mvivu wa kufikiri alinipotea kabisa lakini alitokea tena nilipoanza kufikiri kwa makini. Nawaonea wivu waliopata kumweka mikononi mwao ingawa daima aliwaponyoka. Yote haya shauri ya maluweluwe. Hatuoni tena kilichowekwa wazi. Tumekuwa vichaa kwa kutafuta kilicho wazi na kwa kujaribu kufichua kilicho wazi. Wewe mjukuu wangu nyota yako nzuri. Huenda ukabahatika kumwona na kumshika mikononi mwako” (Uk 44).
Na kweli mashujaa wa mwanga walifanikiwa kuvishinda vikwazo vyote na kumfikia Paa huyo ambaye alikutwa ni msichana mzuri kupindukia. Hata hivyo aliwaponyoka! Ni nani awezaye kumkamata? Babu anaendelea kuelezea kwamba hata ukimkamata, Nagona ni wa watu wote!
Safari ya kumsaka Nagona, inatufunulia mengi: “ Wanaishi kwa matumaini. Wanakula matumaini yao wenyewe ambayo wanasema huzaliana siku hadi siku’
“Hayo matumaini hutoka wapi?”
“Ndotoni”
“Hizo ndoto wanazitoa wapi?”
“Katika kisima cha ndoto ambacho wanasema hakikauki kamwe”
“Hicho kisima kiko wapi?”
“Yeyote afikirie hawezi kukiona”
“Kwa nini?”
“Wanasema fikra hufumba mboni za urazini”
“Hao watu wamekufa au wazima?”
“Kama kufa ni kutokuwepo basi wazima. Zaidi ya hayo maisha tuyajuayo yaweza kuwa ndoto za mtu mmoja mwenye vichwa vingi. Hakuna jibu rahisi” (Uk 6).
Katika safari hii ya kumsaka Nagona, tunafunuliwa pia kizazi kisichopenda kusoma. “ Watu wa mjini waliitupa miswada yangu yote ya kitanzia wakanibakizia komedi. Walipoanza kukaa kimya na kuchekacheka, hata hizo komedi wakazitupa msituni. Walisema kucheka ni ushindi…” (Uk 7).
Safari ya kumsaka Nagona, inapotoka ndotoni, tunafunuliwa viwanda vyetu vingi ambavyo sasa hivi vipo tu havifanyi kazi. Hata hivyo vingine bado vina meneja na walinzi. Meneja wa viwanda visivyofanya kazi bado wanaamini wako kazini na wao ni muhimu sana kwenye viwanda hivyo;
“ Wataalamu gani! Mimi ndiye niliyesimamia mradi wa kujenga kiwanda hiki tangu jiwe la kwanza la msingi hadi mwisho wake. Wao wanajua nini! Na kwa nini Serikali isiniulize mimi matatizo ya kiwanda hiki! Mapendekezo mangapi nimekwisha andika! Yote yalitupwa kapuni! Waambie waondoke”(Uk 22).
Viwanda vimekufa lakini bado vinalindwa. Wanaovilinda wanajua wafanyacho. Wanapoulizwa wanalinda nini wakati viwanda vimekufa, wanajibu: “ Tunalinda maiti asifunuliwe”… “Sisi ni waosha!”… “ Aibu ya maiti aijuaye mwosha”.(Uk22). Ni sawa na kusema la kuvunda lina ubani? Viwanda vimekufa, bado kuna watu wanalinda ili aibu isitoke nje? Hapo kuna maendeleo?
Lakini pia katika safari ya kumsaka Nagona, tunafunuliwa kwamba: “Katika bonde hili kuna imani kuwa ajali ni mwanzo tu wa kitu au wazo jipya. Bila ajali hakuna ambacho kingekuwako. Kuzaliwa kwenu ndiyo ajali kubwa iliyopata kutokea katika uhai wenu. Wakati huo hamkuwa na utashi..” (Uk 23).
Tunaambiwa pia kwamba: “ Hakuna maumivu katika kufa. Kuna masikitiko na huzuni. Masikitiko kwa mali na watu uwaachao nyuma na kwa yale ambayo hukupata nafasi ya kuyatekeleza. Lakini mimi nimeacha mali gani nyuma! Hakuna. Labda maneno yangu. Nimeacha nani nyuma ! Hakuna isipokuwa wewe, baba yako na mama yako. Ninyi nyote mlinielewa vyema na mko imara. Hamtanisaliti. Niliyotaka kutekeleza nimeyatekeleza. Muda nilikuwa nao wa kutosha” (Uk 42).
Babu, ambaye anaonekana kuwa na hekima kubwa katika simulizi hii ya Nagona, anaonyesha wazi wazi kwamba yeye haogopi kufa na wala hana wasi wasi wowote:
Anasema: “Anayeogopa ni yule aliye na tamaa ya kuishi maisha ambayo hajayaishi”
“Maisha ambayo hajayaishi?”
“ Maisha baada ya kifo. Mimi sina tamaa hiyo. Maisha kitu cha ajabu. Nyuma hakuna nyayo na mbele hakuna nyayo, nyayo ziko katikati tu. Kama hujui ulikotoka na hukumbuki, ya nini kutaka kujua uendako!”.
Ndo maana ngoma ni lazima ichezwe katikati mwa duara. Ukicheza nje ya dura wewe uko nje, wewe uko nje maisha. Katikati ni leo, ni maisha ya hapa hapa na wala si ya jana au ya kesho. Ni maisha ya leo ni maisha ya Nagona!
Hadithi inafikia mwisho kwa maangamizi makubwa. Hilo ungamo kuu au ngoma kuu, inaleta vurumai. Watu nakanyagwa na kufa. Hata hivyo kwenye vurumai na vifo hivyo anazaliwa mtoto, tena binti wa kuendeleza kizazi: Binti huyu anapewa jina la Nagona! Inakuwa ni simulizi ya matumaini mapya!
V. TATHIMINI YA KITABU.
Nianze kwa kumpongeza Profesa Kezilahabi, kwa kazi hii nzuri sana aliyoiandika. Kusema kweli hadithi hii inaburudisha na kufikirisha. Ingawa si hadithi ya kueleweka upesi kama Rosa Mistika, bado inaburudisha kwa mtu anayesoma kwa kutafakari.
Ingawa mtindo alioutumia wa uhalisiamazingaombwe, unaonekana kuwa mpya na wengi wanafikiri alijifunza mtindo huu alipokwenda kusoma Amerika, maana ni mtindo unaotumika Amerika ya kusini, bado ukweli unabaki kwamba mtindo huu wa simulizi ni wa Kiafrika. Bibi zetu na babu zetu walikuwa wakitusimulia hadithi za mazimwi na uhalisiamazingaobwe. Simulizi hizi zilitumika kama njia moja ya kujenga maadili, kujiamini na ushujaa.
Ukerewe kama ilivyo kwa Mwanza na Kagera, kuna hadithi za Mungu wa Maji “Mugasha”, Mungu wa misitu “Ilungu”, Mungu wa kilimo na mavuno “Nyakalembe”. Hadithi za miungu hawa zinaelezwa kwa mtindo wa uhalisiamazingaombwe. Hivyo Nagona, si kwamba ni kitu kipya. Labda ni kwa vile tunasahau haraka. Mwandishi anaonyesha tabia hii ya kusahau katika simulizi yake.
Hata hivyo ni ukweli kwamba Waafrika tunapenda miujiza, tunapenda miujiza hadi kuamini kwamba kila kitu kinaweza kutokea kwa miujiza. Tunachoma moto na kuharibu mazingira na bado tunategemea mvua inyeshe! Isiponyesha tunakwenda kwenye nyumba za ibada kuomba mvua inyeshe. Ipo mifano mingi inayoonyesha jinsi Waafrika tunavyopenda miujiza. Hivyo ujumbe mzito kama wa Profesa Kezilahabi, ukipitia kwenye uhalisiamazingaombwe, unaeleweka haraka.
Vitabu vya Nagona na Mzingile vilileta kizaazaa katika Fasihi ya Kiswahili kwa wasomaji pamoja na wahakiki kwani si rahisi kuelewa hasa anazungumzia nini. Inabidi kwanza uwe na uelewa mpana wa matapo makuu ya falsafa za Kimagharibi (mf. Existentialism, Epistemology, Metaphysics, Psychoanalysis, Aesthetics na Phenomenology) na pia falsafa za Kiafrika kama unataka kuelewa cho chote kinazungumziwa katika vitabu hivi.
Kutokana na ugumu wa kueleweka wa vitabu hivi, wahakiki wengi wamemlaumu Kezilahabi kwamba pengine ameuleta mtindo huu wa uandishi katika fasihi ya Kiswahili wakati riwaya ya Kiswahili bado haijakomaa sawasawa. Wahakiki wengine wamefikia hata kumhukumu kwamba pengine ameiua riwaya ya Kiswahili. Ukweli ni kwamba Profesa Kezilahabi, anazifufua riwaya za Kiswahili. Ukoloni, ulifuta simulizi zetu na zilipachikwa majina ua ushenzi na upagani:
“Wewe ndiye kiongozi wa kundi hili la wapagani?”
Babu alimtazama kwa jicho kali. Wazee walimwangalia babu kwa makini wakisubiri neno litakalomtoka.
“Mbona unacheza ngoma yako nje ya duara? Bila njuga hupendezi”.
Padri alimtazama kwa njia iliyoonyesha kutoelewa vizuri. “Nimekuja kukuona wewe”
“Kuhusu?”
“Nimesikia habari za mazungumzo yako. Yanapingana na yangu”
“Mimi si mhubiri. Na mazungumzo yako sijayasikia”
“Na hawa hapa wanafanya nini?”
“Ni askari wa mwanga. Wawindaji”
“Mimi nahubiri habari za Kristo. Wewe unahubiri upagani”
“Wewe ni mcheza ngoma ya twiga nje ya duara. Twiga hawezi kuhimili ngoma yenye vurumai, vurugu, na ghasia katika gharika la hisia na fikra” (Uk 10).
Kutokana na kutoelewa simulizi za Kezilahabi, wahakiki wanafikiri Nagona Na Mzingile ni kitabu kimoja? Ni wazi kuna namna ya kufanana, lakini hivi ni vitabu viwili tofauti. Vinaongelea maisha na umuhimu wa Waafrika kupambana kwa nguvu zote na utandawazi wa kimagharibi unaokuja na kutuvamia. Wale wanaoupinga utandawazi huu, wanaonekana kama vichaa.
Profesa Kezilahabi, amefanikiwa katika Nagona, kuonyesha jinsi maisha ya Waafrika yanavyozunguka ardhi, mito, misitu, wanyama. Haya anayaonyesha vizuri na kwa mtindo wa kutomchosha msomaji. Ameonyesha umuhimu wa Wazee, vijana na wanawake katika jamii zetu.
Lakini hasa ni kuonyesha umuhimu wa Mkombozi wa pili. Anamalizia simulizi lake kwa matumaini mapya. Utafikiri ukombozi huu ni muhimu leo hii; maana kama kuna kipindi cha historia ya taifa letu kilichohitaji Mkombozi wa pili na maisha mapya ni wakati huu tuliomo sasa hivi. Sote tunamhitaji Nagona!
VI. HITIMISHO.
Ni wazi ningependa kuwashauri wasomaji wangu kukinunua kitabu hiki na kukisoma. Pamoja na ukweli kwamba si kitabu chepesi kueleweka kwa uvumilivu mtu anaweza kukisoma na kuelewa. Hata hivyo maisha nayo hayaeleweki haraka; tunapanda milima na mabonde katika maisha na wakati mwingine hatufiki sehemu ya kupumzika na kustarehe.
Na,
Padri Privatus Karugendo.
+255 754 633122

Print this item

  KITABU CHA MWANAFUNZI-DARASA LA SITA
Posted by: MwlMaeda - 07-24-2021, 07:09 AM - Forum: Nukuu - No Replies

.pdf   Kiswahili-darasa-la-6.pdf (Size: 9.82 MB / Downloads: 18)

Print this item

  Kiswahili kina wenyewe, kienee lakini kisitokomee
Posted by: MwlMaeda - 07-24-2021, 06:57 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

[Image: kiswahili.jpg]

Utangulizi
Kama zilivyo lugha nyingi zilizopata bahati ya kuwa kiunganisho baina ya wazungumzaji kutoka makabila na mataifa mengine, Kiswahili nacho kina wenyewe wenye asili nacho na kina watumiaji wa kawaida.
Wenyewe ni watu wa mwambao wa Afrika Mashariki na baadhi ya visiwa vyake ambao, hata kama wana ndimi nyingi, wanakusanywa kwenye tawi moja la lugha hii. Watumiaji wa kawaida wa Kiswahili wametapakaa kote Afrika Mashariki na Kati na hata nje ya bara la Afrika, ambao kwa idadi wao ni wengi zaidi kuliko watu wenyewe wa mwambao wa Afrika Mashariki.
[Image: ghassassni.jpg?w=259&h=259]
Na Mohammed Ghassani
Nalo hilo si jambo la ajabu kwa lugha iliyopata bahati kama ya Kiswahili. Ni kama ilivyo kwa Kiingereza ambacho idadi ya wanaokitumia kwenye shughuli mbalimbali za maisha zilizo na zisizo rasmi inapindukia ya Waingereza wenyewe.
Kwa hivyo, pamoja na kufurahia kuwa Kiswahili kinazidi kuenea kimatumizi kwenye taasisi rasmi ndani na nje ya Afrika Mashariki, huko kusiifanye lugha hii isiyo na mwenyewe. Watumiaji wa lugha hii, ambao si wenye lugha, wasijipe mamlaka ya kuitawala na kuiamulia vipi iwe, itamkwe ama iandikwe kwa kuwa kwao tu kwenye vyombo vya maamuzi.
Kiswahili kina wenyewe, lakini sio kila mtumiaji wa Kiswahili ni Mswahili, kama vile ambavyo si kila mtumiaji wa Kiingereza ni Mwingereza. Nguvu na mamlaka ya lugha vyapaswa kuwa mikononi mwa wenye lugha yao ili wakati ikienea, isiwe inatokomea na kuangamia.
Uwenyewe wa Lugha: Baina ya Umiliki na Uweledi
Hoja yangu hasa ya msingi ni kwamba, kwanza, wako watu wanaojitambua kuwa ni Waswahili kwa kuwa Kiswahili ndiyo lugha yao ya kuzaliwa (na wakati mwengine ya pekee) na Uswahilini ndipo pao na, pili, wako watu wanaoitwa Waswahili ambao wanakitumia Kiswahili katika shughuli zao mbalimbali za maisha, lakini hawana mizizi ya Uswahilini na hii siyo lugha yao ya kwanza na wala ya pekee.
Wako pia waliozaliwa Uswahilini na Waswahili wenyewe lakini Kiswahili si chao tena maana walihama kimwili au kiakili (au kwa vyote viwili) kutoka pale yalipo mapishi yao, na wako ambao wamezaliwa Uswahilini na wazazi wasiokuwa Waswahili, lakini mapishi yao yote yakawa ya Kiswahili na Uswahili ndio utambulisho wao mkuu.
Haya yote yanahusiana na umiliki wa lugha. Lakini kuna masuala muhimu ya uweledi wa lugha (ambalo mizizi yake imo kwenye taaluma) na la mamlaka ya lugha (ambalo mizizi yake ni siasa).
Kwenye la uweledi, kuna kanuni ya msingi ya Kiisimu kuwa “lugha ya kibinaadamu ni mali ya mwanaadamu!” Maana yake ni kuwa mwanaadamu yeyote anaweza kujifunza lugha yoyote na kuitumia kama yake.
Kanuni hii inazingatia nadharia ya lugha kama chombo cha mawasiliano. Kwamba madhali wanaadamu wote wana mfumo sawa wa sauti na kwa kuwa lugha yenyewe ni tanakali za sauti tu, basi mfumo huo wa sauti unaweza kuzipokea na kujizowesha tanakali zozote na za kibinaadamu. Ndio maana kuna watu wanazungumza lugha zaidi ya moja kwa ufasaha na usanifu wa hali ya juu hata kama hawakuzaliwa nazo.
Mfano ni Abdulrazak Gurnah, Mswahili mzawa wa Zanzibar, ambaye mbali ya kuwa bingwa wa riwaya za Kiingereza, pia ni profesa wa Kiingereza na mkurugenzi kwenye idara ya Kiingereza ya Chuo Kikuu cha Kent cha Uingereza. Yaani ni kama mzawa wa Ireland akawa mwandishi bingwa wa riwaya za Kiswahili na akawa mkurugenzi wa Taasisi ya Kiswahili nchini Zanzibar!
Wako wengine kama vile Wole Soyinka na Chinua Achebe wa Nigeria, Ali Mazrui na Ngugi wa Thiong’o wa Kenya, Nuruddin Farah wa Somalia na au Diop Boubacar wa Senegal, ambao nao walijifunza na kuzimudu lugha za kigeni na kuzitumia kwenye kiwango cha juu cha uweledi hadi wenye lugha wenyewe wakawatunuku nishani. Lakini vipi kuhusu mamlaka ya lugha? Je, wao walikuwa na wanazo nguvu kwenye lugha hizo?
Uwenyewe wa Lugha: Baina ya Umiliki na Madaraka
Kama ilivyosemwa hapo juu, suala la uweledi wa lugha linahukumiwa kitaaluma. Lakini inakuwaje pale ambapo pana mfumo ambao taaluma yenyewe inahukumiwa kisiasa? Siasa hapa inamaanisha uwezo wa kufanya maamuzi na nguvu za kuyasimamia maamuzi hayo.
Tunapolijadili suala la mamlaka ya lugha, tukitumia nadharia ya lugha kama alama ya nguvu za kisiasa, tunakikuta Kiswahili kikiwa na bahati mbaya ya kutwaliwa mamlaka yake na wasiokuwa wazaliwa wa lugha hii kwa guo la uweledi wa lugha. Tangu Waswahili walipopoteza mamlaka na nguvu zao za kisiasa katika mwambao wa Afrika Mashariki, wamejikuta wakipoteza pia na mamlaka ya lugha yao.
Mwaka huu nilihudhuria Kongamano la Kiswahili la Bayreuth kusini mwa Ujerumani, ambalo waandaaji waliliita jina la “Pwani na Bara” na miongoni mwa yaliyojitokeza ni mifano ya wanafunzi wa skuli za mwambao kushindwa kwenye mitihani ya somo la Kiswahili, huku wanafunzi wa Bara wakifaulu. Kwa nini iwe hivyo? Miongoni mwa majibu yamo kwenye mamlaka inayoutayarisha mtihani huo na mfumo mzima kwa ujumla. Si mfumo wa Uswahili wala wa Waswahili.
Hapana shaka, sehemu nyengine ya jawabu ni uzembe wa wenyewe wanafunzi wa Mwambao ambao wanalidharau somo la Kiswahili kwa kujiona kuwa tayari ni lugha yao na hivyo hawana haja ya kupoteza muda mwingi kuisoma. Wenzao wanaisoma kama kitu kipya na kuimeza kama wanavyomeza kanuni za Fizikia na Kemia. Kisha wanaitema hivyo hivyo kwenye karatasi ya mtihani.
Sijafanya utafiti wa kina, lakini uzoefu wangu unanipa matokeo kuwa asilimia kubwa ya waliokisomea Kiswahili, ambao hatimaye huwa ndio walimu au viongozi wa taasisi zinazoisimamia lugha hii ndani na nje ya Afrika Mashariki, si Waswahili kutoka Mwambao. Si wale ambao lugha hii ndiyo ya kuzaliwa nao. Si wale ambao wanayajuwa mapishi ya Kiswahili na Uswahili. Hakika wako ambao hata wanawaangalia Waswahili na Uswahili kwa jicho la dharau. Lakini wao ndio waamuzi wa msamiati upi, muundo upi na herufi ipi ni sahihi kwenye Kiswahili.
Hoja ya Ubantu wa Kiswahili imekuwa ikitumiwa vibaya kumaanisha kuwa kila Mbantu ni Mswahili na hivyo ana uweledi, umiliki na mamlaka ya Kiswahili. Huu ni upotoshaji wa hali ya juu lakini unasimamiwa na wenye madaraka ya kisiasa (nguvu na uamuzi).
Nilipiga mfano wa uweledi wa lugha kwa baadhi ya waandishi wa Kiafrika waliozisoma na kuzimudu lugha za kigeni na hata wakapata nishani kwa kuzitumia lugha hizo, lakini umbali wowote waliofika kamwe hawawezi kuziundia lugha hizo misamiati, kanuni wala miongozo ya matumizi yake. Hayo ni mambo yaliyomo mikononi mwa wenye lugha yao.
Hitimisho
Nihitimishe hoja yangu ya uweledi, umiliki na mamlaka ya lugha kwa msisitizo kwamba lugha ni chombo cha kisiasa. Fasili ya siasa inayotumiwa kwenye uchambuzi huu ni ile isemayo kuwa siasa ni uwezo wa kuamua na nguvu za kuyasimamia maamuzi hayo.
Wakoloni, kama vile Wareno, Waingereza, Wafaransa na Wahispania, walitumia lugha zao kutawala na hata baada ya kuondoka kwao kimwili, lugha hizo zilibakia kuendeleza ukoloni mamboleo kwenye makoloni yao makongwe. Upwa wa Bahari ya Hindi mashariki mwa Afrika ulitawaliwa na wengi, wakiwemo hao Wareno na Waingereza, lakini hakuna mtawala aliyefanikiwa kuwalazimisha kuzungumza lugha za wakoloni na badala yake Kiswahili ndicho kikawalazimisha wao kukitumia kwa shughuli zao.
Kwa hivyo, kimsingi Kiswahili ni alama ya dhamira ya kisiasa ya Waswahili wenyewe. Ndio maana mimi ni miongoni mwa wanaojenga hoja kwamba, kama zilivyo lugha nyengine zote kuu ulimwenguni, Kiswahili nacho kilipaswa kuwa na dola lake. Dola linaloamini kwenye Uswahili, Waswahili na Kiswahili.
Ingelikuwa haikupoteza mamlaka yake, labda Zanzibar ingeliendeleza madaraka yake kwenye lugha, si kwa kuwa Kiswahili cha Zanzibar ndicho Kiswahili pekee au kilicho bora zaidi kuliko Viswahili vyengine vinavyozungumzwa na wenyeji wa mwambao wa Afrika Mashariki. La hasha! Ni kwa kuwa Zanzibar ndiyo nchi pekee ambayo asilimia 100 ni Uswahilini.
Lakini Zanzibar ya leo haina uwezo wa kufanya maamuzi kwenye lugha ya Kiswahili na hata inapoyafanya, haina nguvu za kuyasimamia. Inazo taasisi za lugha hiyo kama vile Baraza la Kiswahili na Taasisi ya Kiswahili, lakini kiwango cha nishati, wakati, na rasilimali kinachoekezwa kwenye taasisi hizo hakilingani kabisa na uzito wa lugha hii kuu. Kama ilivyopoteza mamlaka yake kwenye mengine, Zanzibar imepoteza pia kwenye lugha.
Je, hoja yangu hii inapingana na haja ya Kiswahili kutanuka na kusambaa nje ya eneo lake la asili? Hapana. Mimi naona fahari sana kwamba lugha iliyochimbukia udongo mmoja na mimi ndicho sasa chombo cha kuwaunganisha mamilioni ya Waafrika na walimwengu wengine. Moyoni mwangu najisikia faraja sana, mathalan, ninapomsikia Rais Filipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji anazungumza Kiswahili. Husema naye huyu amenyonya ziwa moja nami.
Bali kauli yangu kwenye hili ni hii:
Kienee
Kisambae
Kizagae
Kitandawae
Lakini katu…
Kisiyoyomee
Kisitokomee
Kisipotee!
CHANZO >>>>

Print this item

  UCHAMBUZI WA MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI-MWANDISHI: SHAABAN ROBERT
Posted by: MwlMaeda - 07-23-2021, 08:40 PM - Forum: Nadharia mbalimbali - No Replies

UCHAMBUZI WA KITABU CHA MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI-MWANDISHI: SHAABAN ROBERT

UTANGULIZI
Kitabu cha Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini  ni riwaya iliyoandikwa na Shaaban Robert (1936-1946) yenye insha na mashairi yanayoelezea mambo aliyoyafanya kuanzia umri wa ujana mpaka uzee wake, pamoja na mafanikio mbalimbali aliyoyafikia, changamoto alizokumbana nazo na namna alivyozitatua.
DHAMIRI YA MTUNZI
Kwa mujibu ya kamusi ya Karne ya 21(2011) inafafanua kwamba, dhamiri ni ile azma, kusudio au nia ya kufanya jambo. Katika muktadha wa kifasihi tunaweza kusema dhamiri ni lile lengo au kusudi la mtunzi katika kuitunga kazi yake. Na hii inatuthihirishia kwamba, kila mtunzi husukumwa na jambo fulani (ama zito ama jepesi) katika utunzi wake. Hakuna mtunzi anayetunga kazi yake katika ombwe. Mwandishi yoyote yule hata kama anaandika tungo za kubuni, kwa kawaida huwa amesukumwa na jambo au mambo fulani aliyowahi kusikia, kushuhudia katika fikra zake au katika hali halisi maishani; na fikra hizo hujengwa na mambo fulani ya tajiriba halisi katika maisha halisi.
Hivyo Shaaban Robert katika kitabu chake cha “Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini”suala la msingi lililomsukuma mpaka kuandika kitabu hiki ni kutaka kuweka kumbukumbu nzuri juu ya maisha yake kwa yale yote ambayo aliyafanya akiwa kama mwandishi maarufu wa Afrika Mashariki na Kati, hususani kwa vizazi vijavyo ambavyo havikupata bahati ya kumwona mwandishi huyu, kwa hiyo kwa kupitia kazi yake hii waweze kujifunza mengi na kupata mafanikio katika maisha.
NADHARIA YA UHALISIA
Kwa mujibu wa Ntarangwi (2004) anasema nadharia hii katika upana wake, humaanisha uwakilishi wa uhalisi wa mambo katika fasihi. Nadharia hii ilizuka katika karne ya kumi na tisa hususani kwa lengo la kupinga mkondo wa ulimbwende. Mhalisia huamini katika matokeo ya mambo na ukweli anaouzingatia ni ule unaoweza kuonekana na kuthibitishwa kwa tajirba. Vile vile, wanauhalisia huiamini demokrasia kama hali ya maisha, na malighafi ya kuelezea maisha ya kawaida, ya kadiri na ya kila siku. Hivyo basi uhalisia hujikita katika mambo yaliyopo, tukio mahsusi na matokeo yanayoweza kuthibitika.
Imani ya mhalisia ni kwamba kazi ya fasihi yapaswa kuwaweka wanajamii husika katika ulimwengu wao wa kawaida, wa kweli, na halisi. Hivyo basi hata picha za ulimwengu atakazoumba msanii, zapaswa kudhihirisha hali hiyo.
Mhakiki anayezingatia nadharia hii ya uhalisia, hupembua namna mtunzi alivyodhihirisha uhalisi wa mambo kupitia maudhui aliyoyazingatia na wahusika aliowasawiri. Hivyo basi, mhakiki hutizama jinsi ukweli ulivyodhihirishwa katika juhudi za mtunzi za kuchora hali halisi ya mambo katika wakati maalum. Kwa muhtasari basi msanii anatarajiwa kusawiri wahusika, matukio na mandhari yanayokubalika na kuaminika katika jamii ya wakati wake. Ufahamu wa mazingira na maisha anayoyalenga mtunzi ni nguzo muhimu kwa mhakiki wa kihalisia. Shida inayoletwa na nadharia hii ni kuchukulia kwamba uhalisi na maana yake hauna utata wowote katika jamii yoyote, ni kwamba unachukulia kuwa watu wote katika jamii hiyo wanaona uhalisi mmoja na kuwa na fasili sawa kuhusu maisha yao.
Haki na uaminifu; Shaaban Robert anaona kuwa uaminifu na kutenda haki ni nuru ya maisha bora kwa mwanadamu hapo baadaye. Dhamira hii inajidhihirisha katika insha yake ya Umri uk.2 anasema, “Milango ya nyuma ya kuifikia bahati ilikuwa mingi lakini haikunishawishi hata kidogo”. Suala hili linahusisha hata katika jamii zetu za leo, kwani watu wengi hutumia milango ya nyuma katika kufikia mafanikio. Kwa mfano; kwa kutoa rushwa, ufisadi nk.
Dhuluma na uonevu; Shaaban Robert anaeleza kuwa dhuluma na uonevu vimekuwa ni vipingamizi vikubwa katika mafanikio ya mtu ya kila siku, kwa mfano kama vile kunyimwa jambo fulani au kukandamizwa kwa sababu fulani ni ukuta katika maendeleo binafsi na ya jamii kwa ujumla. Jambo hili linajibainisha katika uk.1 “Mara kwa mara niliposimama wima kuiendea niliteleza nikaanguka chini. Nilipotaka kunyoosha mkono kuishika yalitokea mazuio ambayo sikuyatazamia au nilifungiwa milango ya mbele nisionane nayo”.
Vilevile katika insha ya Mwandishi S. Robert ameonesha ni kwa namna gani alivyodhulumiwa katika uchapaji wa kazi zake. Kwa mfano, uk.78 anasema; “Kwa kazi yangu iliyoweza kuleta sh.25000/- kwa vitabu 5000/- katika mwaka 1954 sikupewa hata pesa moja ya shaba kwa muda wa miaka kadhaa…sikupata kitu kwa kazi yangu iliyoleta karibu sh.15000/- kwa vitabu 5000/- katika mwaka 1958”. Pia anaonesha ni kwa namna gani alivyozidi kudhulumiwa na hata wale ambao walichukua madaraka baadaye. Mfano; uk.79 “Nilikuwa mtumishi wa bure na mtu wa chini kuliko pembe nyeusi yoyote iliyopata kuwako katika ulimwengu huu. Kwa nani? Kwa wale waliofadhiliwa na waliotajirishwa na waliotumikiwa na waliofunzwa na kazi zangu”
Katika jamii yetu ya leo hususani Tanzania tunaona mambo haya yamekithiri sana. Hivyo basi, ili jamii iweze kuondokana na hali hii ni lazima iungane pamoja na kupinga dhuluma na uonevu. Pia kwa kuzingatia haki ya mwandishi S. Robert anasema; uk.80 “Mwandishi si mtu wa ajabu awezae kuishi kwa kula hewa na kunywa ukungu. Ni mtu wa desturi ambaye kama watu wengine wa desturi, hafarijiwi na hasara”.
Ugumu wa soko la vitabu; Mwandishi ameonesha ugumu wa suala hili pale alipofungua duka la vitabu lakini watu hawakuhamasika kununua vitabu hivyo, hali hii ilitokana watu wengi kutokujua kusoma na kutokana na utamaduni wa jamii hiyo katika suala zima la usomaji wa vitabu kwani hawakujua thamani yake, kama asemavyo; uk.110 “Walikuwa katika tarehe yaujinga wa kujua kuwa mazoea ya kusoma yalikamilisha utu wetu katika dunia. Hawakufahamu kwamba katika vitabu ndimo ghala za utamaduni wa elimu zilimopatikana”. Hali hii inahalisika sana katika jamii ya leo kwani watu wengi wanajua kusoma lakini hawana utamaduni wa kusoma hivyo husababisha soko la vitabu kuwa gumu.
Uzalendo; Suala hili limeoneshwa na S. Robert jinsi gani alivyokuwa mzalendo kwa nchi yake (Tanganyika) katika kupinga mifumo yote ya kiutawala wa kikoloni ambaye ilimdharau mwafrika hususani katika kipengele hiki cha kisiasa, kuwa mwafrika hawezi kufanya chochote. Mfano uk.75 “Mwafrika aliweza kufanya nini? Alikuwa mtu gani mbele ya watu?” hali hii ilimfanya Shaaban Robert kujitoa muhanga katika kushiriki misafara mbalimbali ya kisiasa ili kuhamasisha maendeleo ya mwafrika, japokuwa gharama zote za safari hiyo zilikuwa juu yake. Na hii ilitokana na hali ya uzalendo iliyojaa kifuani mwake, kama asemavyo katika uk.74“Sikuwa na kago juu ya ari hii. Alivyokuwa kila mtu ndivyo nilivyokuwa mimi vilevile. Nilitekwa na uzalendo kama alivyotekwa mtu yoyote mwingine. Sikupenda kuwa mgeni katika nchi ya asili na uzazi wangu”.
Hivyo basi suala hili la uzalendo linahalisika katika jamii ya sasa, kwani watu mbalimbali huingia katika siasa na kutetea maslahi ya haki zao ili kujipatia maendeleo hivyo mwandishi anaitaka jamii ya sasa kujitoa muhanga katika kupingana na utawala mbovu uliojaa dharau kwa wale wanaowaongoza.
Kifo na maisha; Haya ni mambo yaliyomo ndani ya jamii, kama binadamu tunapaswa kuyapokea, kuyakubali na pia kuangalia ni kwa namna gani tutakabiliana nayo. Shaaban Robert anaeleza ugumu wa maisha ya upweke na ukiwa na jinsi alivyoyakabili baada ya kufiwa na mkewe Amina. Uk.4 “…mauti yake ya mapema yalikuwa ni msiba na hasara kubwa kwangu.”Lakini Shaaban Robert anatuonesha kwamba pamoja na matatizo hayo jamii inapaswa kuwa na moyo wa uvumilivu kwani upo wakati mwingine mzuri ujao.
Mapenzi ya dhati; Shaaban Robert anaonesha mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa mkewe baada ya kifo. Mfano katika uk.3 anasema, “…tokeo hili lilikuwa pigo kubwa sana kwangu na msiba katika nyumba nzima. Marehemu huyu alikuwa johari ya maisha yangu, tegemeo na mshauri mwema”.
Vilevile alionesha mapenzi ya dhati kwa kuwajali wanae ambao nao walikuwa na upweke wa kumkosa mama yao, alionesha upendo mkubwa kwao kwa kutoacha mwanya wa kujisikia wakiwa. Mfano aliwapatia elimu; uk.5 anasema, “…niliwapenda kwa mapenzi sawa kama baba na mama, nikawatunza kama mboni za macho yangu”. Shaaban Robert anaiasa jamii kuwa suala la kulea watoto baada ya kifo cha mzazi mmoja si la mama tu, bali hata baba kama mzazi anapaswa kuwalea watoto walioachwa tena kwa mapenzi yote ya baba na mama, hivyo si budi jamii kubadilika katika hili.
Nafasi ya mwanamke; Mwandishi Shaaban Robert anamuona mwanamke kama kiungo muhimu sana katika safari hii ya maisha, anamchukulia katika nafasi mbalimbali kama ifuatavyo:
·        Mwanamke kama tegemeo na mshauri mwema. Mfano; uk.3 “…marehemu huyu alikuwa jahari ya maisha yangu, tegemeo na mshauri mwema”.
·        Pia anamuona mwanamke kama mtu mwenye ushirikiano na asiye mvivu. Mfano; uk.3 “…alinisaidia katika mambo mengi wakati wa maisha yetu pamoja ambayo yangalinishinda kuyatenda mimi peke yangu”. Pia hata katika isha ya Idara ya Utawala Shaaban Robert anaeleza uhodari na uchapakazi wa mke wa Mudir. Mfano; uk. 61 “bibi huyu alikuwa hodari na mcheshi sana”
·        Vilevile anaona mwanamke kama mlezi muhimu sana. Kwa mfano; uk.5 “…nilisikitishwa mno kwa ukosefu wa malezi ya mama yao lakini nilikuwa sina uwezo wa kumwita arudi duniani tena”.
·        Shaaban Robert anamuona mwanamke kama pambo na faraja katika maisha ya ndoa. Anasema katika uk.3 “Sura yake ilikuwa jamali kwa kimo cha kadirio, uso wake ulikuwa mviringo wa yai, nywele nyeusi za kushuka, paji pana, nyusi za upinde, macho mazuri yaliyokuwa na tazamo juu ya kila kitu, kope za kitana, masikio ya kindo yasiyopitwa na sauti ndogo, meno ya mwanya…”
·        Mwanamke pia ameoneshwa kama mtu mpole na mwenye heshima. Jambo hili Shaaban Robert ameliweka wazi makusudi ili jamii iweze kuiga na kubadilika kwani wanawake wengi sasa wamepungukiwa na hilo. Mfano; uk.37 “Mke huyu wa pili alikuwa mpole, mwenye madaha na heshima, alikuwa na sura ya haya ambayo ilichuana na utawa kama uso kwa kioo”.
Kufanya kazi kwa bidii; Kwa kiasi kikubwa Shaaban Robert ameonesha mfano hai katika utendaji bora wa kazi akiwa kazini, kwani alikuwa ni mtu wa kujituma na vilevile alikuwa ni kiongozi mzuri na mwenye kupenda kushirikiana na wafanyakazi wenzake. Amelibainisha hili kama nyenzo kuu na muhimu sana katika kazi wakati wote, kwani kupitia nyezo hii kuna manufaa mengi sana kama vile kupendwa na watu, kupandishwa cheo na hata kuaminiwa sana ndani ya jamii. Jambo ambalo jamii ya leo yapaswa kuiga. Mfano; uk.41 “Niliaminiwa sana hata kuliko nilivyotazamia. Mapendeleo niliyotendewa yalikuwa mengi sana”. Pia hata katika uk.40 “Nilitenda yote yaliyokuwa katika uwezo wangu kutimiza wajibu”. Pia hata katika Insha ya Idara ya Utawala makarani walikuwa ni wachapakazi.
Utu wema, urafiki na uhusiano mzuri na watu; Jambo hili Shaaban Robert ameliona kama nguzo muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu yoyote. Anasihi kuwa maisha ya uadui ni maisha mabaya yasiyo na furaha, hakutaka uadui, kumkwaza mtu, aliishi kwa wema na kujenga urafiki daima. Na hivi ndivyo inavyopaswa kuwa kwa mwanadamu yoyote yule kuenenda, kwani hayo huleta maendeleo binafsi na ya jamii kwa ujumla. Mfano; uk.39 “…miguu yangu ilikuwa tayari kwenda kutafuta urafiki…maisha ya uadui kila upande ni mazito kwa mtu yeyote”.
Utii na unyenyekevu; Shaaban Robert ameonesha hali ya utii na unyenyekevu kwa wakuu wake wa kazi na hata wafanyakazi wenzake. Mara zote alijidunisha na kujishusha ilihali akiacha watu waseme juu ya uzuri na ubora wake. Mfano; uk.43 alipopandishwa cheo alisema, “Kisha moyo ulinikua kwa kuona kuwa kazi yangu ilikuwa imehesabiwa na kuonekana thamani yake, wakati mimi mwenyewe nilikuwa nimeidunisha”. Uk.45 “Sifa ilikuwa kubwa kuliko niliyotenda, nikainama chini kwa haya; na huzuni ilikuwa kubwa vilevile moyo ukanilemea”. Shaaban Robert anatuonesha kwamba suala hili aliliona tangu hapo mwanzo na ndiyo maana anaifundisha jamii kuwa yapaswa kutenda vivyo hivyo ili iwe taa ya kuangaza na sabuni ya kung’arisha maisha yao.
Suala la mirathi; Mwandishi Shaaban Robert anatuonesha ugumu uliopo katika suala zima la ugawanyaji wa mirathi. Suala hili linahalisika hata katika maisha yetu ya sasa tunaona jinsi ndugu wanavyopingana na hata kuchukiana kwa sababu ya mirathi. Kutokana na hali hii Shabaan Robert hajasita kutuonesha umuhimu wa kuacha wasia juu ya ugawanyaji wa mali. Kwa mfano; uk. 48 “Choyo cha warithi mbalimbali kilifanya magawanyo kuwa magumu ajabu”
Ubaguzi wa rangi na matabaka; Enzi za ukoloni kulikuwa na ubaguzi wa rangi wa watu weupe na weusi katika mambo mbalimbali ya kijamii, mfano; kusalimiana kwa kushikana mikono, vyombo vya usafiri vilikuwa katika madaraja, daraja la kwanza walikuwa watu weupe (wazungu) wakati daraja la tatu walikuwa watu weusi (waafrika).
Vilevile hata sehemu za malazi zilikuwa katika misingi ya kiubaguzi. Shaaban Robert alilionesha hili katika uk.50 “Karibu ningalilala nje Korogwe kwa ukosefu wa malazi ya abiria waafrika”. Pia uk.52 “Huyo alikuwa ni mzungu, hakuwa tayari kushikana mikono na mimi”.
Pia hata katika Insha ya Msuso uk.105 anasema; “Mtu yoyote aliyekuwa si mweupe katika Afrika kusini hakuwa na ustahili, dhamani wala heshima ya uanadamu. Aliweza kutendewa ukatili wowote ambao haukuwezekana kujaribiwa hata kwa wanyama wa porini bila ya lawama katika nchi nyingine za ulimwengini.” ya mambo haya leo hii yapo hata katika jamii yetu japo yanajidhihirisha kwa namna nyingine. Leo ubaguzi kati ya matajiri na masikini, wenye vyeo na wasionavyo ni mkubwa sana.
Wema na ubaya; Mwandishi huyu ameonesha nguvu kubwa ya wema juu ya ubaya, anasema palipo na wema ubaya hushindwa na kutupwa kabisa. Mfano; uk.51 anasema kwamba, “Idadi ya watu wema ni kubwa siku zote kuliko jumla ya watu wabaya”. Katika jamii yetu ya leo wema upo lakini bado unamezwa na ubaya kwa kiasi kikubwa kutokana na woga, uroho wa madaraka, ubabe wa baadhi ya watu, nk. Ila Shaaban Robert anaipa jamii suluhu ya ubaya kuwa yatupasa kuwa wema.
Dharau; Suala la kudharauliwa kwa waafrika lilioneshwa wazi na wazungu pamoja na wahindi. Hii ni pale ambapo hata kama mwaafrika angekuwa na cheo cha juu kuliko mzungu bado mzungu angeheshimiwa sana kuliko mwaafrika huyo. Shaaban Robert katika utumishi wake alilionja hili na lilimpa mfadhaiko mkubwa sana. Mfano; uk.54 anasema, “Nilikuwa ni radhi kuwekwa chini ya wakubwa wangu lakini niliona dharau wadogo kuwekwa juu yangu”. Uhalisia wa jambo hili ndani ya jamii yetu ya leo lipo katika sehemu mbalimbali za kazi, kwani watu wanaangalia undugu, urafiki na mahusiano mengine ambayo hayana hadhi yoyote katika cheo fulani.
Dhamira nyingine zilizojitokeza katika kazi hii zipo katika insha mbalimbali, kwa mfano Insha ya “Naondoka Mpwapwa” kuna dhamira ya umuhimu wa elimu kwa watoto wa kike, ujasiri na tamaa ya mali. Masuala haya ni masuala ambayo yapo katika jamii yetu ya sasa, hivyo ni vyema jamii ichukue mazuri yote na kuacha mabaya kama vile tamaa ya mali.
Pia katika Insha ya “Idara ya Utawala” dhamira ambayo imejitokeza ni suala zima la utawala, ambapo mwandishi anatueleza ni kwa namna gani viongozi wanavyotakiwa kuwajibika katika nafasi zao za kazi. Kwa mfano; uk.61 mwandishi amemuonesha Mudir na masaidizi wake jinsi walivyokuwa wakiwajibika.
vilevile katika Insha ya “Nilikuwa Mshairi” kuna dhamira ya umuhimu wa ushairi. S. Robert anaonesha ni kwa namna gani ushairi ulivyo muhimu, kwani huweza kutunza kumbukumbu na uhai wa mwandishi. Mfano; uk.64 “Mauti huua mwili wa mwandishi ukawa vumbi tupu kaburini lakini mchoro alioandika wakati wa maisha yake hudumisha uhai wa jina lake duniani milele”.
Kipengele kingine cha Maudhui ni Mgogoro;Ni hali ya kutokuelewana baina ya pande mbili yaani mtu na mtu, mtu na kikundi au mtu mwenyewe na nafsi yake.Migogoro mbalimbali imeweza kujitokeza ambapo tunaweza kuigawa katika vipengele vifuatavyo; Mgogoro wa nafsi,Mgogoro wa kiuchumi,Mgogoro wa kijamii na Mgogoro wa kiuchumi.
Katika mgogoro wa nafsi tunamwona Shaaban Robert akionesha hali ya kujiuliza juu ya maisha mazuri yakoje na je afanye nini ili awe na jina zuri duniani. Mfano; uk.2 “Ukosefu wa jina zuri ni ukiwa mkubwa duniani. Jambo hili sikulipenda.” Suluhisho la mgogoro huu; Shaaban Robert aliamua kufanyakazi kwa bidii na kuwa mtu mwema.
Mgogoro mwingine wa nafsi unajitokeza kwa S. Robert  kwamba ni kwa vipi angepata mke aliye na sifa kama za Amina! (mke wake wa kwanza ambaye ni marehemu). Anasema uk.37“Nilikuwa na marafiki na wenye huruma kadha wa kadha lakini, kati yao palikuwa hapana mtu niliyeweza kumwita mke. Nafasi yake ilikuwa haina mtu nyumbani”. Suluhisho la mgogoro huu, alimpata mke wa pili aliyekuwa na sifa alizozihitaji.
Pia kuna mgogoro wa kijamii ambapo umetokea pale Shaaban Robert alipodharauliwa kuhusu cheo chake. Hii ilijitokeza pale ambapo S. Robert hakutendewa haki kazini kwake, kwani badala ya kuwekwa wa kwanza katika orodha ya mshahara kutokana na cheo chake aliwekwa mwishoni kwa kuwa tu yeye alikuwa ni mwaafrika. Suluhisho la mgogoro huu Shaaban Robert aliamua kuandika barua kwa mkuu lakini barua hiyo haikufanyiwa kazi. Basi S. Robert aliamua kuvumilia. Uk.55 “Katika ulimwengu watu wengine walikuwa wamepatwa na madhila kuliko yaliyonipata mimi wakavumilia. Mimi nilikuwa ni nani nisivumilie?”
Mgogoro mwingine wa kijamii ni kati ya S. Robert na ndugu wa mke wake. Chanzo cha mgogoro huu ni uchoyo wa baadhi ya warithi wa mirathi. Suluhisho lake ni pale S. Robert alipowapa uhuru wa kuchagua sehemu waliyotaka na zile zilizoachwa kuwa zake na watoto wake. Uk.48 “Basi nilitoa shauri kuwa isipokuwa mimi na watoto wangu kila mrithi alikuwa na idhini ya kuchagua sehemu yake katika shamba apendalo, na sehemu zisizochaguliwa itakuwa haki ya watoto na mimi. Shauri hili lilisuluhisha mambo kama uchawi”.
Pia mgogoro wa kijamii mwingine ni kati ya S. Robert na msimamizi wa safari, chanzo cha mgogoro huu ni ubaguzi au dharau, hii ilijionesha pale ambapo S. Robert alipoambiwa kushuka katika lori la daraja la pili ili kuwapisha wahindi wanne wakati yeye alistahili kuwa katika hilo gari kutokana na yeye alistahili kuwa mfanyakazi wa serikali. Suluhisho la mgogoro huo S. Robert na watoto wake aliwapisha na kushuka. “Msimamizi wa safari, mhindi vilevile, hakuona mtu mwingine wa kushuka ila mimi”.
Katika mgogoro wa kiuchumi tunamwona Shaabani Robert akilalamika namna alivyodhurumiwa pesa za manunuzi ya vitabu vyake,uk 78 anasema “Kwa kazi yangu iliyoweza kuleta sh 25000/= kwa vitabu 5000 katika mwaka 1954 sikupewa hata pesa moja ya shaba kwa muda wa miaka kadhaa….sikupata kitu kwa kazi yangu iliyoleta karibu sh 15000/= kwa vitabu 5000 katika mwaka 1958.Suluhisho la mgogoro huu ni kwamba Shaabani Robert alizidi kuwa mvumilivu pasipo kuvunjika moyo katika kazi yake ya uandishi uk 79 anasema…..sijavunjika moyo,tena ningali nayo bado furaha katika uandishi kama alivyo bi-arusi kwa mpenzi wake.Katika maisha baadhi husumbuka na wengine hucheka.
Ujumbe; mwandishi S. Robert ametoa ujumbe wa aina tofauti tofauti kwa lengo la kuiasa na kuionya jamii ili iweze kubadilika na kufikia maendeleo yenye kuleta tija kwa mtu binafsi, jamii na taifa kwa ujumla.
·        Kufanya kazi kwa bidii ni msingi mzuri katika maisha. Mfano S. Robert alifanya kazi kwa bidii na ndio maana alifanikiwa katika maisha yake yote na hivyo kujijengea jina zuri.
·        Jambo la msingi na bora katika maisha ni kutokata tamaa, hata kama tunashindwa kupata mafanikio makubwa ni bora kupata kidogo kuliko kukosa kabisa. S. Robert anasema kuwa; uk 2. “Jaribu dogo la wema ni bora kuliko kubwa la ubaya”.
·        Utu wema ni matendo mazuri. Shaaban Robert anatuasa tuwe na matendo mema, matendo mema yaoneshwe nyakati zote. Mfano; mahusiano mema na marafiki, kauli nzuri kwa watu nk.
·        Haki na uaminifu katika maisha humfanya mtu aheshimike na kukubalika wakati wote.
·        Shaaban Robert anatuasa kuwa na mapenzi ya dhati katika maisha kwani hutufanya kuishi vyema.
·        Suala la kumtegemea Mungu katika kila jambo ni muhimu, na kitu kizuri kinatoka kwa Mungu. Mfano; mke mwema au mume mwema.
·        Suala la malezi ni la watu wote wawili na sio suala la mmoja. Hivyo hakuna budi baba na mama kushiriki kikamilifu katika malezi hasahasa baba.
·        Hakuna haja ya kujilimbikizia madaraka na majukumu kwani maisha ya duniani ni ya mpito.
·        Uandishi ni silaha muhimu katika utunzaji wa kumbukumbu za kihistoria.
·        Nafasi ya elimu itolewe kwa watu wote.
·        Ni vema kuwa wavumilivu katika kufanikisha jambo Fulani.
Falsafa ya mtunzi; Shaaban Robert anaamini kuwa mtu hupendwa na kukubalika kwa watu kutokana na matendo yake mazuri kama vile, kauli njema, ufanyaji kazi kwa bidii, utii na unyenyekevu, msamaha, uvumilivu na kuwa na moyo wa kujitoa. Anasema; “Wema hushinda ubaya na haki ya mtu haipotei”.
Mtazamo; Mtazamo wa S. Robert ni wa kimapinduzi anaona kuwa kufanya kazi kwa bidii huleta maendeleo.
Msimamo; Shaaban Robert ameonesha msimamo wa aina mbili kwanza msimamo wa kidhanifu ambao umetokana na imani yake aliyoishikilia kwamba Mungu ndiye tegemeo. Na anatudhihirishia kwamba mtu akimtegemea Mungu atafanikiwa. Pili ameonesha msimamo wa kiuyakinifu kwani anaeleze kuwa, mtu anayefanya kazi kwa bidii na mwenye ushirikiano na maadili mema ndiye hujitengenezea jina zuri katika jamii. Na hii inajidhihirisha wazi katika Maisha yake ya kabla na baada ya miaka hamsini na ndiyo maana mpaka leo anakumbukwa.
Baada ya kuangalia maudhui katika insha mbalimbali sasa tuangalie umbo la ndani na la nje katika ushairi. Hapa tutachambua mashairi pamoja tenzi. Kwa kuanza na shairi la “Amina” katika umbo la ndani (maudhui) kwa kutumia nadharia ileile ya Uhalisia.
Mwandishi S. Robert ameonesha dhamira mbalimbali kama ifuatavyo:
Mapenzi ya dhati na ndoa; Shaaban Robert anaeleza mapenzi yake ya dhati kwa Amina (marehemu) anaona kwamba Mungu ndiye anayefunga na kufungua mapenzi. Mfano; katika ubeti wa 2 uk.4 anasema;   2.
“Nilitaka unyanyuke, kwa kukuombea dua,
 Sikupenda ushindike, maradhi kukuchukua,
Ila kwa rehema yake, Mungu amekuchagua,
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua”
Dini na imani kwa Mungu: Shaaban Robert anaamini uwepo wa Mungu ndio maana katika ubeti wa 2 anamwombea mke wake dua kwa Mungu ili ayashinde maradhi. Anaamini kuwa Mungu hashindwi na kitu lakini kwa mapenzi yake ameamua kumchukua.
Maadili mema na maonyo: hali hii imejidhihirisha pale Shaaban Robert alipokuwa anawaasa watoto wake katika utenzi wa Hati na Adili, juu ya kuwa na maadili mema. Anataja mambo kama adabu na utii, utu wema, umuhimu wa mwanamke kujitunza, kujali wakati, umuhimu wa elimu, kuepuka fitina, kumcha Mungu, kuwaheshimu wazazi, mapenzi ya dhati katika ndoa, kuepuka uvivu, kutii mamlaka, kutunza ahadi nk. mfano katika ubeti wa 34. Anaelezea uvumilivu katika maisha ya ndoa.   34.
“Na mume msishindane,
Wala msinuniane,
Jitahidi mpatane,
Ndiyo maisha ya ndoa”
Pia katika ubeti wa 36 anaelezea usafi na kutunza mazingira;
36. “Nyumba yako inadhifu,
Kwa kufagia uchafu
Kila mdudu dhaifu
Asipate pa kukaa”
Maana ya kifasihi ya ubeti huu ni kwamba, mwanamke anapaswa kutunza mwili, moyo na akili yake ili visije vikaingiliwa na mawazo machafu/fikra potofu ambazo zitadhoofisha mahusiano/mapatano katika ndoa au familia yake.
Umuhimu wa elimu: katika ubeti wa 31, uk 10. Shaaban Robert anaonesha jinsi gani elimu ilivyomuhimu katika maisha. Anasema;   .
31.  “Elimu kitu kizuri,
Kuwa nayo ni fahari,
 Sababu humshauri,
Mtu la kutumia”.
Heshima kwa wazazi: ili kuishi maisha mema na yenye baraka, Shaaban Robert anawaasa Hati na Adili wawaheshimu wazazi na wala wasioneshe dharau ili wapate taadhima. Mfano katika ubeti wa 36.uk.26 anasema;
36. “Tatu baba na mama,
Wataka taadhima,
Na kila lililojema,
Ukiweza watendee”.
Vivyo hivyo hata katika jamii yetu ya leo tunaona jinsi gani watoto na vijana wengi wanavyo wadharau wazazi wao na hata watu waliowazidi umri. Hivyo basi si budi jamii kubadilika kwani heshima ni kitu muhimu sana katika maisha.
Ujane: Shaabani Robert anaonesha athari za kuondokewa na mume au mke na pia umuhimu wa mke na mume. Mfano; ubeti. 13:1 “Dunia mume na mke, kwa watu hata wanyama”
Vilevile anaonesha umuhimu wa kuwa pamoja kati ya mume na mke. Mfano; ubeti 3:3 “Adamu pasipo mke, Mungu hakuona vyema”,
Katika uhalisi suala la ujane lipo na halikwepeki ni kitu ambacho kinaumiza sana iwapo mmoja anaondokewa na mwezi wake.
Umuhimu wa ndoa;  katika shairi la Ndoa ni Jambo la Suna Shaabani Robert anasisitiza kwamba katika dini ya kiislamu ndoa ni kitu muhimu sana katika maisha ya duniani, hivyo anawahamasisha vijana waoe kwani ndoa ni jambo la kheri na ni suna kutoka kwa Mtume. Pia anawahamasisha vijana waache zinaa. Ubeti 8:2 “Huko kubibirishana, ni haramu vitabuni”,
Ubaya wa unafiki; hii inajitokeza katika shairi la “Ndumakuwili” mwandishi anaonesha ubaya wa mtu mnafiki na jinsi alivyo kwani si rahisi kumtambua kama anavyosema katika ubeti 2.
2. Hujivika pande zote, mkapa akavikika,
Litengezwalo lolote, hangui huridhika,
La sharia au tete, lisemwalo hutosheka,
Ndumakuwili si mwema, hujidhuru nafsia.
Hata katika jamii yetu ya leo watu kama hao wapo, hivyo mwandishi anaiasa jamii kuachana na tabia ya ndumakuwili kwani hukwamisha maendeleo.
Umuhimu wa shukrani; katika shairi la “Namshukuru” mwandishi anatufundisha kwamba katika maisha tunapaswa kuwa watu wenye shukrani kwa Mungu katika kila jambo. Mfano, ubeti.10 uk 104.
“Namshukuru Manani, mwenye uwezo arifu,
Hafi maji baharini, mzawa kufa kwa sefu,
Mambo yake yanafani, kila akiyasarifu,
Alhamdulillahi, namshukuru Latifu”.
Nafasi ya mwanamke: Shaaban Robert hakuacha kujadili suala la mwanamke katika jamii. Hili linajidhihirisha kwenye utenzi wa “HATI”, anamuasa binti yake kuwa awe mtii, msafi, mpishi bora, mvumilivu katika ndoa nk. mfano katika ubeti wa 33.uk.10 anasema;
33. “Upishi mwema kujua
       Na mume kumridhia
      Neno analokwambia,
     Kwako itakuwa taa”.
Ujumbe; katika mashairi yake mwandishi S.Robert ametoa ujumbe huhimu sana katika kuiasa jamii kama ifuatavyo:
·        Maisha ya kumtegemea Mungu ni yenye fanaka.
·        Jamii yapaswa kuzingatia elimu kwani ni mwanga wa maisha.
·        Ili vijana wafanikiwe katika maisha wanapaswa kuwa na utii na adabu.
·        Tuwe makini katika katika maneno tutamkayo yasiwe na athari mbaya kwa jamii, kama matusi, kunena uongo nk.
·        Kupekuwa uvivu na kufanya kazi kwa bidii ni silaha ya maendeleo.
Baada ya kuangalia umbo la ndani katika ushairi sasa tuangalie umbo la nje katika ushairi. Kwa kutumia nadharia ya Umuundo-mpya.
Nadhari ya Umuundo-mpya ni zao la nadharia ya Umuundo. Nadharia hii inatumia neno Umuundo-mpya kuonyesha mtizamo wa kimuundo katika fasihi ambao ulitokea baada ya ukinzani wa nadharia ya Umuundo. Japo dhana hii haiwezi kupewa maana moja maalum, imehusishwa na maendeleo kutoka au katika kazi za Derrida (1973, 1976), Lacan (1977), Kristeva (1981, 1984, 1986), Althusser (1971) na Foucault (1978, 1979a na b, 1981, 1986). Kazi hizi nazo zilichangiwa na kazi za Ferdinand de Saussure na Emile Benveniste (kuhusu isimu-jamii ya umuundo). Nadharia hii ya Umuundo-mpya hujikita zaidi katika kusisitiza kuwa maana inaweza kubadilika kulingana na miktadha husika. Kwa mfano. Maana ya neno tajiri hutofautiana katika lugha mbalimbali na hata kati ya miundo tofauti ya lugha moja, na hutegemea matumizi na muktadha wa matumizi hayo. Ndipo sasa hapana maana moja ya neno au fungu la maneno.
Kulingana na nadharia hii basi, neno ‘mama’ kwa mfano, huwa halina maana ya kindani inayotokana na lugha husika bali huwa na maana za kijamii zilizotokana na lugha hiyo na ambazo zinakinzana na kubadilika kulingana na mazingira na kipindi cha kihistoria.
Kwa kuanza na kipengele cha mtindo:
Mtindo; kwa mujibu wa Senkoro (2011), “Mtindo katika kazi ya fasihi ni ile namna ambavyo msanii hutunga kazi yake na huipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni au kawaida za zilizofuatwa kama ni zilizopo (za kimapokeo) au ni za kipekee”.
Kwa ujumla mtindo uliotumiwa na mwandishi ni wa kipekee kabisa kwani ameweza kuchanganya insha,mashairi pamoja na tenzi ambazo kwa ujumla huelezea maisha yake S.Robert hususani katika insha, na katika mashairi na tenzi kuna majonzi, mawaidha, maonyo na maadili.
Katika kipengele cha mashairi mtindo uliotumika ni wa kimapokeo kwa sababu amezingatia urari wa vina na mizani, urari wa mishororo, kibwagizo na utoshelevu katika kila beti. Mfano ubeti wa 2 katika shairi la “Amina” anasema;
2. “Nilitaka unyanyuke, kwa kukuombea dua,
      Sikupenda ushindike, maradhi kukuchukua,
      Ila kwa rehema yake, Mungu amekuchagua,
     Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua”
Muundo; kwa mujibu Senkoro (kashatajwa), “muundo hutokana na umbo na mpango wa kazi ya fasihi; kwa hiyo hapa ndipo tutapata katika ushairi wa Kiswahili, mashairi yenye miundo mbalimbali iainishwayo na idadi ya mistari (vipande/mishororo) katika kila ubeti, mathalani mashairi ya uwili, utatu, unne” nk.
 Muundo uliotumika katika mashairi yote na tenzi zote ni muundo wa tarbia yaani mistari minne katika kila beti. Mfano, shairi la Amina ubeti.1 uk.4
Anima umejitenga, kufa umetangulia,
Kama ua umefunga, baada ya kuchanua,
Nakuombea mwanga peponi kukubaliwa,
Mapenzi tuliyofunga hapana wa kufungua.
Vilevile hata katika “UTENZI HATI” na “UTENZI WA ADILI” mwandishi ametumia muundo wa tarbia (mistari minne). Mfano; utenzi wa ADILI uk.
Kijana lete kalamu,
Nina habari muhimu,
Napenda uifahamu,
Dadayo kasha zamuye,
Matumizi ya lugha; mwandishi ametumia lugha fasaha na inayoeleweka na wote hasa katika upande wa insha, lakini katika upande wa ushairi kwa kiasi fulani ametumia msamiati wa lugha ya kiarabu. Mfano katika shairi la “Namshukuru” kuna maneno kama vile, Illahi, Alhamdulillahi, Latifu, rakadha, ashrafu, nk. Vilevile ametumia tamathali za semi kama vile:
Tashbiha: shairi la “Amina” ubeti wa 1:2 uk.4 “Kama ua umefunga baada ya kuchanua”. Neno “kama” ni tashbiha inayotumika kulinganisha vitu viwili.
Vilevile hata katika “UTENZI WA HATI” uk.7 ubeti wa 7:4 tunaona tashbiha zikijitokeza. Anasema, “Nakupenda kama Hidaya” na ubeti wa 6:3 anasema, “Tunza kama sahibu” pia uk.7 ubeti wa 5:3 “Itunze kama fedha”
Takriri: urudiaji wa neno, sentensi au kifungu cha maneo ili kusisitiza jambo. ubeti wa 1:3 na 4 “Nakuombea mwanga, peponi kukubaliwa” pia ubeti wa 4:3 “Nawe wangu penzi, peponiutaingia”. Neno “peponi” limerudiwa ili kuonesha msisitizo kwamba baada ya maisha haya kuna maisha mengine peponi (mbinguni). Pia uk.6 ubeti wa 5:2 “Nijaze kadha wa kadha”, vilevile katika “UTENZI WA HATI” neno “hati” limejitokeza mara nyingi mfano, ubeti wa 1, 2, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 17, 18, 19… pia neno binti katika ubeti wa 1, 92, 93, 94, 95.
Ritifaa: Ngure (2003:128) ni kitu kisicho na uhai kama vile maiti huwa kinasemeshwa kana kwamba nafsi yake ingali hai. Mfano; katika shairi la Amina S.Robert anaongea na marehemu Amina kana kwamba yu hai. Hii imejidhihirisha katika shairi zima. Mfano; ubeti wa 4 na 5
Tashihisi: kukipa kitu kisicho hai uwezo wa kutenda. Mfano; ubeti wa 6:2;3 uk.5 anasema,
“Vumbi tena likiunga, roho likirudishiwa,
Mauti yakijitenga, mapenzi yatarejea”,
Pia katika UTENZI WA HATI uk.7 ubeti wa 6:1 anasema, “Dunia ina aibu”. Hapa dunia inapewa sifa ya ubinadamu ya kuona aibu. Vilevile uk.8 ubeti wa 17:3 anasema,
“Sauti yendavyo mbio”. Hapa napo sauti inapewa uwezo wa kukimbia kama kitu chenye uhai. Pia uk.27 ubeti wa 43:2 “Viungo vyake husema”. Viungo mbalimbali vya mwili vinapewa uwezo wa kusema kama binadamu.
Sitiari: kitu kupewa jina la kitu kingine. Hii ni katika “UTENZI WA HATI” uk.13 ubeti wa 50:3 anasema, “Mtu mwongo ni msongo”. Mtu mwongo anafananishwa na mtu asiyechezwa unyago/asiyefundwa. Pia hata katika uk.17 ubeti wa 81:1 chungo inafananishwa na kitu kilichooza. Anasema, “Chongo mbaya ni uvundo”, vilevile uk.26 ubeti wa 37:3 baba anafananishwa na mbegu. “Baba yako ni mbegu”, uk.15 ubeti wa 64:1 mama anafananishwa na kitu cheupe, kitu safi. Anasema “Mke ni nguo nyeupe”,
Jazanda (matumizi ya picha na ishara). Ubeti wa 1. Katika shairi la Amina Mwandishi anasema;
            “Amina umejitenga, kufa umetangulia,
             Kama ua umefunga, baada ya kuchanua”,
Hapa anafanisha kifo cha Amina na jinsi ua linavyonyauka.
Pia hata katika shairi la ndoa, mwandishi ametumia neno kunguru akimaanisha wale watu wasio tulia katika ndoa zao.
Taashira: maana inayotajwa si ile inayomaanishwa. Mfano uk.7 ubeti wa 6:1 katika “UTENZI WA HATI” anasema “Dunia ina aibu” pia uk.16 ubeti wa 73:1 na 74:1 anasema “Tumbo la rutuba”, “Tumbo hili la dhahabu”. Mwandishi anaposema “tumbo la rutuba” ni dhahiri kuwa anamaanisha tumbo la uzazi la mwanamke. Pia anaposema “tumbo hili la dhahabu”anamaanisha tumbo lenye thamani na la pekee wengine hawana.
Misemo: ni kauli fupifupi zenye ujumbe mzito. Kwa mfano: uk.9 ubeti wa 20:1 “Dunia ni Mvurugo” yaani inamaanisha kuwa duniani kuna mabaya na mazuri, hivyo tunapawa kuwa waangalifu. Pia uk.6 ubeti wa 5:1, “Ulimwengu una adha” pia uk.13 ubeti wa 54:1 “Ulimi wa pilipili”
Methali: uk.9 ubeti wa 22:2 “Cheche huzaa moto” yaani kitu kidogo chaweza kuleta madhara makubwa. Pia uk10 ubeti wa 28:1 “Dunia mali ya roho” pia katika shairi la “UJANE” uk. 82 ubeti wa 4:1 “Ujane neno la feli, kugombana watu wema”,
Taswira: katika “UTENZI WA HATI” uk.26 kuna taswira ya “hereni”. Hapa mwandishi anamfananisha hati na pambo la sikioni, anaona kuwa binti yake akizingatia hayo atafanikiwa maishani. Pia kuna taswira ya “pilipili” (kitu kichungu) ubeti wa 54. “UTENZI WA HATI”anamuasa mwanae asiwe na ulimi kama wa pilipili bali awe na kauli ya upole na faraja siku zote.
Jina la kitabu; “Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini”. Jina hili linasadifu kabisa yaliyomo katika kitabu, kwani, kazi yake yote mwandishi ameigawa katika sehemu kuu mbili sehemu ya kwanza ni Maisha yangu na sehemu ya pili ni Baada ya Miaka Hamsini. Vilevile katika kuelezea maisha yake ameelezea kwa mtindo wa insha, mashairi na utenzi. Na katika kila kichwa cha insha, shairi na utenzi vimesadifu kabisa yaliyomo ndani yake.
Kufaulu kwa mwandishi; Mwandishi amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, kwani mambo aliyoyandika yana halisika katika maisha yetu ya kila siku.
Kutokufaulu kwa mwandishi; Mwandishi ameelezea mambo mengi kwa kufuata imani ya dini ya kiislamu na kusahau kwamba anaowaandikia ni mchanganyiko wa imani tofauti tofauti. Pia amejikita zaidi katika mambo dhahania kama vile Mungu. Vilevile hata lugha aliyoitumia kwa kiasi fulani ina msamiati wa kiarabu hasa katika ushairi, hivyo inawawia vigumu kuelewa wale wasiojua lugha ya kiarabu.
Hitimisho; Sisi kama wachambuzi wa kazi hii tunamwona S. Robert kama kivuli kinachoishi, kwani mambo mengi aliyoyaeleza bado yapo katika jamii ya leo na kazi yake bado inamashiko na itaendelea kuwa na mashiko hata kwa vizazi vijavyo.

MAREJEO:
Mdee, J.S. na wenzake (2011). Kamusi ya Karne ya 21. (toleo la pili) Longhorn Publishers (K) Ltd. Nairobi.
Ngure, A. (2003). Fasihi Simulizi kwa Shule za Sekondari. Phoenix Publisher. Nairobi.
Ntarangwi, M. ( 2004). Uhakiki wa Kazi za Fasihi. Augustana College, Rock Island, IL 61201
Robert, S. (1991). Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini. Mkuki na Nyota Publishers. Dar es Salaam.
Senkoro, F.E.M.K. (2011) Fasihi. KAUTTU Limited. Dar es Salaam.

Print this item

  NADHARIYA YA UHALISIYA KATIKA Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini
Posted by: MwlMaeda - 07-23-2021, 08:33 PM - Forum: Nadharia mbalimbali - No Replies

Kitabu cha Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini  ni riwaya iliyoandikwa na Shaaban Robert (1936-1946) yenye insha na mashairi yanayoelezea mambo aliyoyafanya kuanzia umri wa ujana mpaka uzee wake, pamoja na mafanikio mbalimbali aliyoyafikia, changamoto alizokumbana nazo na namna alivyozitatua.
 
DHAMIRI YA MTUNZI
Kwa mujibu ya kamusi ya Karne ya 21(2011) inafafanua kwamba, dhamiri ni ile azma, kusudio au nia ya kufanya jambo. Katika muktadha wa kifasihi tunaweza kusema dhamiri ni lile lengo au kusudi la mtunzi katika kuitunga kazi yake. Na hii inatuthihirishia kwamba, kila mtunzi husukumwa na jambo fulani (ama zito ama jepesi) katika utunzi wake. Hakuna mtunzi anayetunga kazi yake katika ombwe. Mwandishi yoyote yule hata kama anaandika tungo za kubuni, kwa kawaida huwa amesukumwa na jambo au mambo fulani aliyowahi kusikia, kushuhudia katika fikra zake au katika hali halisi maishani; na fikra hizo hujengwa na mambo fulani ya tajiriba halisi katika maisha halisi.
[url=https://www.blogger.com/null][/url]Hivyo Shaaban Robert katika kitabu chake cha “Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini”suala la msingi lililomsukuma mpaka kuandika kitabu hiki ni kutaka kuweka kumbukumbu nzuri juu ya maisha yake kwa yale yote ambayo aliyafanya akiwa kama mwandishi maarufu wa Afrika Mashariki na Kati, hususani kwa vizazi vijavyo ambavyo havikupata bahati ya kumwona mwandishi huyu, kwa hiyo kwa kupitia kazi yake hii waweze kujifunza mengi na kupata mafanikio katika maisha.
 
NADHARIA YA UHALISIA
Kwa mujibu wa Ntarangwi (2004) anasema nadharia hii katika upana wake, humaanisha uwakilishi wa uhalisi wa mambo katika fasihi. Nadharia hii ilizuka katika karne ya kumi na tisa hususani kwa lengo la kupinga mkondo wa ulimbwende. Mhalisia huamini katika matokeo ya mambo na ukweli anaouzingatia ni ule unaoweza kuonekana na kuthibitishwa kwa tajirba. Vile vile, wanauhalisia huiamini demokrasia kama hali ya maisha, na malighafi ya kuelezea maisha ya kawaida, ya kadiri na ya kila siku. Hivyo basi uhalisia hujikita katika mambo yaliyopo, tukio mahsusi na matokeo yanayoweza kuthibitika.
Imani ya mhalisia ni kwamba kazi ya fasihi yapaswa kuwaweka wanajamii husika katika ulimwengu wao wa kawaida, wa kweli, na halisi. Hivyo basi hata picha za ulimwengu atakazoumba msanii, zapaswa kudhihirisha hali hiyo.
Mhakiki anayezingatia nadharia hii ya uhalisia, hupembua namna mtunzi alivyodhihirisha uhalisi wa mambo kupitia maudhui aliyoyazingatia na wahusika aliowasawiri. Hivyo basi, mhakiki hutizama jinsi ukweli ulivyodhihirishwa katika juhudi za mtunzi za kuchora hali halisi ya mambo katika wakati maalum. Kwa muhtasari basi msanii anatarajiwa kusawiri wahusika, matukio na mandhari yanayokubalika na kuaminika katika jamii ya wakati wake. Ufahamu wa mazingira na maisha anayoyalenga mtunzi ni nguzo muhimu kwa mhakiki wa kihalisia. Shida inayoletwa na nadharia hii ni kuchukulia kwamba uhalisi na maana yake hauna utata wowote katika jamii yoyote, ni kwamba unachukulia kuwa watu wote katika jamii hiyo wanaona uhalisi mmoja na kuwa na fasili sawa kuhusu maisha yao.
Haki na uaminifu; Shaaban Robert anaona kuwa uaminifu na kutenda haki ni nuru ya maisha bora kwa mwanadamu hapo baadaye. Dhamira hii inajidhihirisha katika insha yake ya Umri uk.2 anasema, “Milango ya nyuma ya kuifikia bahati ilikuwa mingi lakini haikunishawishi hata kidogo”. Suala hili linahusisha hata katika jamii zetu za leo, kwani watu wengi hutumia milango ya nyuma katika kufikia mafanikio. Kwa mfano; kwa kutoa rushwa, ufisadi nk.
Dhuluma na uonevu; Shaaban Robert anaeleza kuwa dhuluma na uonevu vimekuwa ni vipingamizi vikubwa katika mafanikio ya mtu ya kila siku, kwa mfano kama vile kunyimwa jambo fulani au kukandamizwa kwa sababu fulani ni ukuta katika maendeleo binafsi na ya jamii kwa ujumla. Jambo hili linajibainisha katika uk.1 “Mara kwa mara niliposimama wima kuiendea niliteleza nikaanguka chini. Nilipotaka kunyoosha mkono kuishika yalitokea mazuio ambayo sikuyatazamia au nilifungiwa milango ya mbele nisionane nayo”.
Vilevile katika insha ya Mwandishi S. Robert ameonesha ni kwa namna gani alivyodhulumiwa katika uchapaji wa kazi zake. Kwa mfano, uk.78 anasema; “Kwa kazi yangu iliyoweza kuleta sh.25000/- kwa vitabu 5000/- katika mwaka 1954 sikupewa hata pesa moja ya shaba kwa muda wa miaka kadhaa…sikupata kitu kwa kazi yangu iliyoleta karibu sh.15000/- kwa vitabu 5000/- katika mwaka 1958”. Pia anaonesha ni kwa namna gani alivyozidi kudhulumiwa na hata wale ambao walichukua madaraka baadaye. Mfano; uk.79 “Nilikuwa mtumishi wa bure na mtu wa chini kuliko pembe nyeusi yoyote iliyopata kuwako katika ulimwengu huu. Kwa nani? Kwa wale waliofadhiliwa na waliotajirishwa na waliotumikiwa na waliofunzwa na kazi zangu”
Katika jamii yetu ya leo hususani Tanzania tunaona mambo haya yamekithiri sana. Hivyo basi, ili jamii iweze kuondokana na hali hii ni lazima iungane pamoja na kupinga dhuluma na uonevu. Pia kwa kuzingatia haki ya mwandishi S. Robert anasema; uk.80 “Mwandishi si mtu wa ajabu awezae kuishi kwa kula hewa na kunywa ukungu. Ni mtu wa desturi ambaye kama watu wengine wa desturi, hafarijiwi na hasara”.
Ugumu wa soko la vitabu; Mwandishi ameonesha ugumu wa suala hili pale alipofungua duka la vitabu lakini watu hawakuhamasika kununua vitabu hivyo, hali hii ilitokana watu wengi kutokujua kusoma na kutokana na utamaduni wa jamii hiyo katika suala zima la usomaji wa vitabu kwani hawakujua thamani yake, kama asemavyo; uk.110 “Walikuwa katika tarehe yaujinga wa kujua kuwa mazoea ya kusoma yalikamilisha utu wetu katika dunia. Hawakufahamu kwamba katika vitabu ndimo ghala za utamaduni wa elimu zilimopatikana”. Hali hii inahalisika sana katika jamii ya leo kwani watu wengi wanajua kusoma lakini hawana utamaduni wa kusoma hivyo husababisha soko la vitabu kuwa gumu.
Uzalendo; Suala hili limeoneshwa na S. Robert jinsi gani alivyokuwa mzalendo kwa nchi yake (Tanganyika) katika kupinga mifumo yote ya kiutawala wa kikoloni ambaye ilimdharau mwafrika hususani katika kipengele hiki cha kisiasa, kuwa mwafrika hawezi kufanya chochote. Mfano uk.75 “Mwafrika aliweza kufanya nini? Alikuwa mtu gani mbele ya watu?” hali hii ilimfanya Shaaban Robert kujitoa muhanga katika kushiriki misafara mbalimbali ya kisiasa ili kuhamasisha maendeleo ya mwafrika, japokuwa gharama zote za safari hiyo zilikuwa juu yake. Na hii ilitokana na hali ya uzalendo iliyojaa kifuani mwake, kama asemavyo katika uk.74“Sikuwa na kago juu ya ari hii. Alivyokuwa kila mtu ndivyo nilivyokuwa mimi vilevile. Nilitekwa na uzalendo kama alivyotekwa mtu yoyote mwingine. Sikupenda kuwa mgeni katika nchi ya asili na uzazi wangu”.
Hivyo basi suala hili la uzalendo linahalisika katika jamii ya sasa, kwani watu mbalimbali huingia katika siasa na kutetea maslahi ya haki zao ili kujipatia maendeleo hivyo mwandishi anaitaka jamii ya sasa kujitoa muhanga katika kupingana na utawala mbovu uliojaa dharau kwa wale wanaowaongoza.
Kifo na maisha; Haya ni mambo yaliyomo ndani ya jamii, kama binadamu tunapaswa kuyapokea, kuyakubali na pia kuangalia ni kwa namna gani tutakabiliana nayo. Shaaban Robert anaeleza ugumu wa maisha ya upweke na ukiwa na jinsi alivyoyakabili baada ya kufiwa na mkewe Amina. Uk.4 “…mauti yake ya mapema yalikuwa ni msiba na hasara kubwa kwangu.”Lakini Shaaban Robert anatuonesha kwamba pamoja na matatizo hayo jamii inapaswa kuwa na moyo wa uvumilivu kwani upo wakati mwingine mzuri ujao.
Mapenzi ya dhati; Shaaban Robert anaonesha mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa mkewe baada ya kifo. Mfano katika uk.3 anasema, “…tokeo hili lilikuwa pigo kubwa sana kwangu na msiba katika nyumba nzima. Marehemu huyu alikuwa johari ya maisha yangu, tegemeo na mshauri mwema”.
Vilevile alionesha mapenzi ya dhati kwa kuwajali wanae ambao nao walikuwa na upweke wa kumkosa mama yao, alionesha upendo mkubwa kwao kwa kutoacha mwanya wa kujisikia wakiwa. Mfano aliwapatia elimu; uk.5 anasema, “…niliwapenda kwa mapenzi sawa kama baba na mama, nikawatunza kama mboni za macho yangu”. Shaaban Robert anaiasa jamii kuwa suala la kulea watoto baada ya kifo cha mzazi mmoja si la mama tu, bali hata baba kama mzazi anapaswa kuwalea watoto walioachwa tena kwa mapenzi yote ya baba na mama, hivyo si budi jamii kubadilika katika hili.
Nafasi ya mwanamke; Mwandishi Shaaban Robert anamuona mwanamke kama kiungo muhimu sana katika safari hii ya maisha, anamchukulia katika nafasi mbalimbali kama ifuatavyo:
·         Mwanamke kama tegemeo na mshauri mwema. Mfano; uk.3 “…marehemu huyu alikuwa jahari ya maisha yangu, tegemeo na mshauri mwema”.
·         Pia anamuona mwanamke kama mtu mwenye ushirikiano na asiye mvivu. Mfano; uk.3 “…alinisaidia katika mambo mengi wakati wa maisha yetu pamoja ambayo yangalinishinda kuyatenda mimi peke yangu”. Pia hata katika isha ya Idara ya Utawala Shaaban Robert anaeleza uhodari na uchapakazi wa mke wa Mudir. Mfano; uk. 61 “bibi huyu alikuwa hodari na mcheshi sana”
·         Vilevile anaona mwanamke kama mlezi muhimu sana. Kwa mfano; uk.5 “…nilisikitishwa mno kwa ukosefu wa malezi ya mama yao lakini nilikuwa sina uwezo wa kumwita arudi duniani tena”.
·         Shaaban Robert anamuona mwanamke kama pambo na faraja katika maisha ya ndoa. Anasema katika uk.3 “Sura yake ilikuwa jamali kwa kimo cha kadirio, uso wake ulikuwa mviringo wa yai, nywele nyeusi za kushuka, paji pana, nyusi za upinde, macho mazuri yaliyokuwa na tazamo juu ya kila kitu, kope za kitana, masikio ya kindo yasiyopitwa na sauti ndogo, meno ya mwanya…”
·         Mwanamke pia ameoneshwa kama mtu mpole na mwenye heshima. Jambo hili Shaaban Robert ameliweka wazi makusudi ili jamii iweze kuiga na kubadilika kwani wanawake wengi sasa wamepungukiwa na hilo. Mfano; uk.37 “Mke huyu wa pili alikuwa mpole, mwenye madaha na heshima, alikuwa na sura ya haya ambayo ilichuana na utawa kama uso kwa kioo”.
Kufanya kazi kwa bidii; Kwa kiasi kikubwa Shaaban Robert ameonesha mfano hai katika utendaji bora wa kazi akiwa kazini, kwani alikuwa ni mtu wa kujituma na vilevile alikuwa ni kiongozi mzuri na mwenye kupenda kushirikiana na wafanyakazi wenzake. Amelibainisha hili kama nyenzo kuu na muhimu sana katika kazi wakati wote, kwani kupitia nyezo hii kuna manufaa mengi sana kama vile kupendwa na watu, kupandishwa cheo na hata kuaminiwa sana ndani ya jamii. Jambo ambalo jamii ya leo yapaswa kuiga. Mfano; uk.41 “Niliaminiwa sana hata kuliko nilivyotazamia. Mapendeleo niliyotendewa yalikuwa mengi sana”. Pia hata katika uk.40 “Nilitenda yote yaliyokuwa katika uwezo wangu kutimiza wajibu”. Pia hata katika Insha ya Idara ya Utawala makarani walikuwa ni wachapakazi.
Utu wema, urafiki na uhusiano mzuri na watu; Jambo hili Shaaban Robert ameliona kama nguzo muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu yoyote. Anasihi kuwa maisha ya uadui ni maisha mabaya yasiyo na furaha, hakutaka uadui, kumkwaza mtu, aliishi kwa wema na kujenga urafiki daima. Na hivi ndivyo inavyopaswa kuwa kwa mwanadamu yoyote yule kuenenda, kwani hayo huleta maendeleo binafsi na ya jamii kwa ujumla. Mfano; uk.39 “…miguu yangu ilikuwa tayari kwenda kutafuta urafiki…maisha ya uadui kila upande ni mazito kwa mtu yeyote”.
Utii na unyenyekevu; Shaaban Robert ameonesha hali ya utii na unyenyekevu kwa wakuu wake wa kazi na hata wafanyakazi wenzake. Mara zote alijidunisha na kujishusha ilihali akiacha watu waseme juu ya uzuri na ubora wake. Mfano; uk.43 alipopandishwa cheo alisema, “Kisha moyo ulinikua kwa kuona kuwa kazi yangu ilikuwa imehesabiwa na kuonekana thamani yake, wakati mimi mwenyewe nilikuwa nimeidunisha”. Uk.45 “Sifa ilikuwa kubwa kuliko niliyotenda, nikainama chini kwa haya; na huzuni ilikuwa kubwa vilevile moyo ukanilemea”. Shaaban Robert anatuonesha kwamba suala hili aliliona tangu hapo mwanzo na ndiyo maana anaifundisha jamii kuwa yapaswa kutenda vivyo hivyo ili iwe taa ya kuangaza na sabuni ya kung’arisha maisha yao.
Suala la mirathi; Mwandishi Shaaban Robert anatuonesha ugumu uliopo katika suala zima la ugawanyaji wa mirathi. Suala hili linahalisika hata katika maisha yetu ya sasa tunaona jinsi ndugu wanavyopingana na hata kuchukiana kwa sababu ya mirathi. Kutokana na hali hii Shabaan Robert hajasita kutuonesha umuhimu wa kuacha wasia juu ya ugawanyaji wa mali. Kwa mfano; uk. 48 “Choyo cha warithi mbalimbali kilifanya magawanyo kuwa magumu ajabu”
Ubaguzi wa rangi na matabaka; Enzi za ukoloni kulikuwa na ubaguzi wa rangi wa watu weupe na weusi katika mambo mbalimbali ya kijamii, mfano; kusalimiana kwa kushikana mikono, vyombo vya usafiri vilikuwa katika madaraja, daraja la kwanza walikuwa watu weupe (wazungu) wakati daraja la tatu walikuwa watu weusi (waafrika).
Vilevile hata sehemu za malazi zilikuwa katika misingi ya kiubaguzi. Shaaban Robert alilionesha hili katika uk.50 “Karibu ningalilala nje Korogwe kwa ukosefu wa malazi ya abiria waafrika”. Pia uk.52 “Huyo alikuwa ni mzungu, hakuwa tayari kushikana mikono na mimi”.
Pia hata katika Insha ya Msuso uk.105 anasema; “Mtu yoyote aliyekuwa si mweupe katika Afrika kusini hakuwa na ustahili, dhamani wala heshima ya uanadamu. Aliweza kutendewa ukatili wowote ambao haukuwezekana kujaribiwa hata kwa wanyama wa porini bila ya lawama katika nchi nyingine za ulimwengini.” ya  Mambo haya leo hii yapo hata katika jamii yetu japo yanajidhihirisha kwa namna nyingine. Leo ubaguzi kati ya matajiri na masikini, wenye vyeo na wasionavyo ni mkubwa sana.
Wema na ubaya; Mwandishi huyu ameonesha nguvu kubwa ya wema juu ya ubaya, anasema palipo na wema ubaya hushindwa na kutupwa kabisa. Mfano; uk.51 anasema kwamba, “Idadi ya watu wema ni kubwa siku zote kuliko jumla ya watu wabaya”. Katika jamii yetu ya leo wema upo lakini bado unamezwa na ubaya kwa kiasi kikubwa kutokana na woga, uroho wa madaraka, ubabe wa baadhi ya watu, nk. Ila Shaaban Robert anaipa jamii suluhu ya ubaya kuwa yatupasa kuwa wema.
Dharau; Suala la kudharauliwa kwa waafrika lilioneshwa wazi na wazungu pamoja na wahindi. Hii ni pale ambapo hata kama mwaafrika angekuwa na cheo cha juu kuliko mzungu bado mzungu angeheshimiwa sana kuliko mwaafrika huyo. Shaaban Robert katika utumishi wake alilionja hili na lilimpa mfadhaiko mkubwa sana. Mfano; uk.54 anasema, “Nilikuwa ni radhi kuwekwa chini ya wakubwa wangu lakini niliona dharau wadogo kuwekwa juu yangu”. Uhalisia wa jambo hili ndani ya jamii yetu ya leo lipo katika sehemu mbalimbali za kazi, kwani watu wanaangalia undugu, urafiki na mahusiano mengine ambayo hayana hadhi yoyote katika cheo fulani.
Dhamira nyingine zilizojitokeza katika kazi hii zipo katika insha mbalimbali, kwa mfano Insha ya “Naondoka Mpwapwa” kuna dhamira ya umuhimu wa elimu kwa watoto wa kike, ujasiri na tamaa ya mali. Masuala haya ni masuala ambayo yapo katika jamii yetu ya sasa, hivyo ni vyema jamii ichukue mazuri yote na kuacha mabaya kama vile tamaa ya mali.
Pia katika Insha ya “Idara ya Utawala” dhamira ambayo imejitokeza ni suala zima la utawala, ambapo mwandishi anatueleza ni kwa namna gani viongozi wanavyotakiwa kuwajibika katika nafasi zao za kazi. Kwa mfano; uk.61 mwandishi amemuonesha Mudir na masaidizi wake jinsi walivyokuwa wakiwajibika.
vilevile katika Insha ya “Nilikuwa Mshairi” kuna dhamira ya umuhimu wa ushairi. S. Robert anaonesha ni kwa namna gani ushairi ulivyo muhimu, kwani huweza kutunza kumbukumbu na uhai wa mwandishi. Mfano; uk.64 “Mauti huua mwili wa mwandishi ukawa vumbi tupu kaburini lakini mchoro alioandika wakati wa maisha yake hudumisha uhai wa jina lake duniani milele”.
Kipengele kingine cha Maudhui ni Mgogoro;Ni hali ya kutokuelewana baina ya pande mbili yaani mtu na mtu, mtu na kikundi au mtu mwenyewe na nafsi yake.Migogoro mbalimbali imeweza kujitokeza ambapo tunaweza kuigawa katika vipengele vifuatavyo; Mgogoro wa nafsi,Mgogoro wa kiuchumi,Mgogoro wa kijamii na Mgogoro wa kiuchumi.
Katika mgogoro wa nafsi tunamwona Shaaban Robert akionesha hali ya kujiuliza juu ya maisha mazuri yakoje na je afanye nini ili awe na jina zuri duniani. Mfano; uk.2 “Ukosefu wa jina zuri ni ukiwa mkubwa duniani. Jambo hili sikulipenda”. Suluhisho la mgogoro huu; Shaaban Robert aliamua kufanyakazi kwa bidii na kuwa mtu mwema.
Mgogoro mwingine wa nafsi unajitokeza kwa S. Robert  kwamba ni kwa vipi angepata mke aliye na sifa kama za Amina! (mke wake wa kwanza ambaye ni marehemu). Anasema uk.37“Nilikuwa na marafiki na wenye huruma kadha wa kadha lakini, kati yao palikuwa hapana mtu niliyeweza kumwita mke. Nafasi yake ilikuwa haina mtu nyumbani”. Suluhisho la mgogoro huu, alimpata mke wa pili aliyekuwa na sifa alizozihitaji.
Pia kuna mgogoro wa kijamii ambapo umetokea pale Shaaban Robert alipodharauliwa kuhusu cheo chake. Hii ilijitokeza pale ambapo S. Robert hakutendewa haki kazini kwake, kwani badala ya kuwekwa wa kwanza katika orodha ya mshahara kutokana na cheo chake aliwekwa mwishoni kwa kuwa tu yeye alikuwa ni mwaafrika. Suluhisho la mgogoro huu Shaaban Robert aliamua kuandika barua kwa mkuu lakini barua hiyo haikufanyiwa kazi. Basi S. Robert aliamua kuvumilia. Uk.55 “Katika ulimwengu watu wengine walikuwa wamepatwa na madhila kuliko yaliyonipata mimi wakavumilia. Mimi nilikuwa ni nani nisivumilie?”
Mgogoro mwingine wa kijamii ni kati ya S. Robert na ndugu wa mke wake. Chanzo cha mgogoro huu ni uchoyo wa baadhi ya warithi wa mirathi. Suluhisho lake ni pale S. Robert alipowapa uhuru wa kuchagua sehemu waliyotaka na zile zilizoachwa kuwa zake na watoto wake. Uk.48 “Basi nilitoa shauri kuwa isipokuwa mimi na watoto wangu kila mrithi alikuwa na idhini ya kuchagua sehemu yake katika shamba apendalo, na sehemu zisizochaguliwa itakuwa haki ya watoto na mimi. Shauri hili lilisuluhisha mambo kama uchawi”.
Pia mgogoro wa kijamii mwingine ni kati ya S. Robert na msimamizi wa safari, chanzo cha mgogoro huu ni ubaguzi au dharau, hii ilijionesha pale ambapo S. Robert alipoambiwa kushuka katika lori la daraja la pili ili kuwapisha wahindi wanne wakati yeye alistahili kuwa katika hilo gari kutokana na yeye alistahili kuwa mfanyakazi wa serikali. Suluhisho la mgogoro huo S. Robert na watoto wake aliwapisha na kushuka. “Msimamizi wa safari, mhindi vilevile, hakuona mtu mwingine wa kushuka ila mimi”.
Katika mgogoro wa kiuchumi tunamwona Shaabani Robert akilalamika namna alivyodhurumiwa pesa za manunuzi ya vitabu vyake,uk 78 anasema “Kwa kazi yangu iliyoweza kuleta sh 25000/= kwa vitabu 5000 katika mwaka 1954 sikupewa hata pesa moja ya shaba kwa muda wa miaka kadhaa….sikupata kitu kwa kazi yangu iliyoleta karibu sh 15000/= kwa vitabu 5000 katika mwaka 1958.Suluhisho la mgogoro huu ni kwamba Shaabani Robert alizidi kuwa mvumilivu pasipo kuvunjika moyo katika kazi yake ya uandishi uk 79 anasema…..sijavunjika moyo,tena ningali nayo bado furaha katika uandishi kama alivyo bi-arusi kwa mpenzi wake.Katika maisha baadhi husumbuka na wengine hucheka.
Ujumbe; mwandishi S. Robert ametoa ujumbe wa aina tofauti tofauti kwa lengo la kuiasa na kuionya jamii ili iweze kubadilika na kufikia maendeleo yenye kuleta tija kwa mtu binafsi, jamii na taifa kwa ujumla.
·         Kufanya kazi kwa bidii ni msingi mzuri katika maisha. Mfano S. Robert alifanya kazi kwa bidii na ndio maana alifanikiwa katika maisha yake yote na hivyo kujijengea jina zuri.
·         Jambo la msingi na bora katika maisha ni kutokata tamaa, hata kama tunashindwa kupata mafanikio makubwa ni bora kupata kidogo kuliko kukosa kabisa. S. Robert anasema kuwa; uk 2. “Jaribu dogo la wema ni bora kuliko kubwa la ubaya”.
·         Utu wema ni matendo mazuri. Shaaban Robert anatuasa tuwe na matendo mema, matendo mema yaoneshwe nyakati zote. Mfano; mahusiano mema na marafiki, kauli nzuri kwa watu nk.
·         Haki na uaminifu katika maisha humfanya mtu aheshimike na kukubalika wakati wote.
·         Shaaban Robert anatuasa kuwa na mapenzi ya dhati katika maisha kwani hutufanya kuishi vyema.
·         Suala la kumtegemea Mungu katika kila jambo ni muhimu, na kitu kizuri kinatoka kwa Mungu. Mfano; mke mwema au mume mwema.
·         Suala la malezi ni la watu wote wawili na sio suala la mmoja. Hivyo hakuna budi baba na mama kushiriki kikamilifu katika malezi hasahasa baba.
·         Hakuna haja ya kujilimbikizia madaraka na majukumu kwani maisha ya duniani ni ya mpito.
·         Uandishi ni silaha muhimu katika utunzaji wa kumbukumbu za kihistoria.
·         Nafasi ya elimu itolewe kwa watu wote.
·         Ni vema kuwa wavumilivu katika kufanikisha jambo Fulani.
Falsafa ya mtunzi; Shaaban Robert anaamini kuwa mtu hupendwa na kukubalika kwa watu kutokana na matendo yake mazuri kama vile, kauli njema, ufanyaji kazi kwa bidii, utii na unyenyekevu, msamaha, uvumilivu na kuwa na moyo wa kujitoa. Anasema; “Wema hushinda ubaya na haki ya mtu haipotei”.
Mtazamo; Mtazamo wa S. Robert ni wa kimapinduzi anaona kuwa kufanya kazi kwa bidii huleta maendeleo.
Msimamo; Shaaban Robert ameonesha msimamo wa aina mbili kwanza msimamo wa kidhanifu ambao umetokana na imani yake aliyoishikilia kwamba Mungu ndiye tegemeo. Na anatudhihirishia kwamba mtu akimtegemea Mungu atafanikiwa. Pili ameonesha msimamo wa kiuyakinifu kwani anaeleze kuwa, mtu anayefanya kazi kwa bidii na mwenye ushirikiano na maadili mema ndiye hujitengenezea jina zuri katika jamii. Na hii inajidhihirisha wazi katika Maisha yake ya kabla na baada ya miaka hamsini na ndiyo maana mpaka leo anakumbukwa.
Baada ya kuangalia maudhui katika insha mbalimbali sasa tuangalie umbo la ndani na la nje katika ushairi. Hapa tutachambua mashairi pamoja tenzi. Kwa kuanza na shairi la “Amina” katika umbo la ndani (maudhui) kwa kutumia nadharia ileile ya Uhalisia.
Mwandishi S. Robert ameonesha dhamira mbalimbali kama ifuatavyo:
Mapenzi ya dhati na ndoa; Shaaban Robert anaeleza mapenzi yake ya dhati kwa Amina (marehemu) anaona kwamba Mungu ndiye anayefunga na kufungua mapenzi. Mfano; katika ubeti wa 2 uk.4 anasema;   2.
                                             “Nilitaka unyanyuke, kwa kukuombea dua,
                                               Sikupenda ushindike, maradhi kukuchukua,
                                     Ila kwa rehema yake, Mungu amekuchagua,
                                   Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua”
Dini na imani kwa Mungu: Shaaban Robert anaamini uwepo wa Mungu ndio maana katika ubeti wa 2 anamwombea mke wake dua kwa Mungu ili ayashinde maradhi. Anaamini kuwa Mungu hashindwi na kitu lakini kwa mapenzi yake ameamua kumchukua.
Maadili mema na maonyo: hali hii imejidhihirisha pale Shaaban Robert alipokuwa anawaasa watoto wake katika utenzi wa Hati na Adili, juu ya kuwa na maadili mema. Anataja mambo kama adabu na utii, utu wema, umuhimu wa mwanamke kujitunza, kujali wakati, umuhimu wa elimu, kuepuka fitina, kumcha Mungu, kuwaheshimu wazazi, mapenzi ya dhati katika ndoa, kuepuka uvivu, kutii mamlaka, kutunza ahadi nk. mfano katika ubeti wa 34. Anaelezea uvumilivu katika maisha ya ndoa.
                                                  34.  “Na mume msishindane,
     Wala msinuniane,
    Jitahidi mpatane,
   Ndiyo maisha ya ndoa”

Pia katika ubeti wa 36 anaelezea usafi na kutunza mazingira;
36. “Nyumba yako inadhifu,
        Kwa kufagia uchafu
                                          Kila mdudu dhaifu
                                         Asipate pa kukaa”

Maana ya kifasihi ya ubeti huu ni kwamba, mwanamke anapaswa kutunza mwili, moyo na akili yake ili visije vikaingiliwa na mawazo machafu/fikra potofu ambazo zitadhoofisha mahusiano/mapatano katika ndoa au familia yake.
Umuhimu wa elimu: katika ubeti wa 31, uk 10. Shaaban Robert anaonesha jinsi gani elimu ilivyomuhimu katika maisha. Anasema;   .
                                                                31.  “Elimu kitu kizuri,
                                                                           Kuwa nayo ni fahari,
                                                                          Sababu humshauri,
                                                                          Mtu la kutumia”.
Heshima kwa wazazi: ili kuishi maisha mema na yenye baraka, Shaaban Robert anawaasa Hati na Adili wawaheshimu wazazi na wala wasioneshe dharau ili wapate taadhima. Mfano katika ubeti wa 36.uk.26 anasema;
36. “Tatu baba na mama,
                                                                  Wataka taadhima,
                                                                  Na kila lililojema,
                                                                  Ukiweza watendee”.
Vivyo hivyo hata katika jamii yetu ya leo tunaona jinsi gani watoto na vijana wengi wanavyo wadharau wazazi wao na hata watu waliowazidi umri. Hivyo basi si budi jamii kubadilika kwani heshima ni kitu muhimu sana katika maisha.
Ujane: Shaabani Robert anaonesha athari za kuondokewa na mume au mke na pia umuhimu wa mke na mume. Mfano;
                                 ubeti. 13:1
                                    Dunia mume na mke, kwa watu hata wanyama,
Vilevile anaonesha umuhimu wa kuwa pamoja kati ya mume na mke. Mfano;
                                       ubeti 3:3
“Adamu pasipo mke, Mungu hakuona vyema”,
Katika uhalisi suala la ujane lipo na halikwepeki ni kitu ambacho kinaumiza sana iwapo mmoja anaondokewa na mwezi wake.
Umuhimu wa ndoa;  katika shairi la Ndoa ni Jambo la Suna Shaabani Robert anasisitiza kwamba katika dini ya kiislamu ndoa ni kitu muhimu sana katika maisha ya duniani, hivyo anawahamasisha vijana waoe kwani ndoa ni jambo la kheri na ni suna kutoka kwa Mtume. Pia anawahamasisha vijana waache zinaa. Ubeti 8:2 “Huko kubibirishana, ni haramu vitabuni”,
Ubaya wa unafiki; hii inajitokeza katika shairi la “Ndumakuwili” mwandishi anaonesha ubaya wa mtu mnafiki na jinsi alivyo kwani si rahisi kumtambua kama anavyosema katika ubeti 2.
2. Hujivika pande zote, mkapa akavikika,
    Litengezwalo lolote, hangui huridhika,
    La sharia au tete, lisemwalo hutosheka,
    Ndumakuwili si mwema, hujidhuru nafsia.
Hata katika jamii yetu ya leo watu kama hao wapo, hivyo mwandishi anaiasa jamii kuachana na tabia ya ndumakuwili kwani hukwamisha maendeleo.
Umuhimu wa shukrani; katika shairi la “Namshukuru” mwandishi anatufundisha kwamba katika maisha tunapaswa kuwa watu wenye shukrani kwa Mungu katika kila jambo. Mfano, ubeti.10 uk 104. “Namshukuru Manani, mwenye uwezo arifu,
                            Hafi maji baharini, mzawa kufa kwa sefu,
                           Mambo yake yanafani, kila akiyasarifu,
                           Alhamdulillahi, namshukuru Latifu”.
Nafasi ya mwanamke: Shaaban Robert hakuacha kujadili suala la mwanamke katika jamii. Hili linajidhihirisha kwenye utenzi wa “HATI”, anamuasa binti yake kuwa awe mtii, msafi, mpishi bora, mvumilivu katika ndoa nk. mfano katika ubeti wa 33.uk.10 anasema;
33. “Upishi mwema kujua
                                                    Na mume kumridhia
                                                   Neno analokwambia,
                                                   Kwako itakuwa taa”.
Ujumbe; katika mashairi yake mwandishi S.Robert ametoa ujumbe huhimu sana katika kuiasa jamii kama ifuatavyo:
·         Maisha ya kumtegemea Mungu ni yenye fanaka.
·         Jamii yapaswa kuzingatia elimu kwani ni mwanga wa maisha.
·         Ili vijana wafanikiwe katika maisha wanapaswa kuwa na utii na adabu.
·         Tuwe makini katika katika maneno tutamkayo yasiwe na athari mbaya kwa jamii, kama matusi, kunena uongo nk.
·         Kupekuwa uvivu na kufanya kazi kwa bidii ni silaha ya maendeleo.
Baada ya kuangalia umbo la ndani katika ushairi sasa tuangalie umbo la nje katika ushairi. Kwa kutumia nadharia ya Umuundo-mpya.
Nadhari ya Umuundo-mpya ni zao la nadharia ya Umuundo. Nadharia hii inatumia neno Umuundo-mpya kuonyesha mtizamo wa kimuundo katika fasihi ambao ulitokea baada ya ukinzani wa nadharia ya Umuundo. Japo dhana hii haiwezi kupewa maana moja maalum, imehusishwa na maendeleo kutoka au katika kazi za Derrida (1973, 1976), Lacan (1977), Kristeva (1981, 1984, 1986), Althusser (1971) na Foucault (1978, 1979a na b, 1981, 1986). Kazi hizi nazo zilichangiwa na kazi za Ferdinand de Saussure na Emile Benveniste (kuhusu isimu-jamii ya umuundo). Nadharia hii ya Umuundo-mpya hujikita zaidi katika kusisitiza kuwa maana inaweza kubadilika kulingana na miktadha husika. Kwa mfano. Maana ya neno tajiri hutofautiana katika lugha mbalimbali na hata kati ya miundo tofauti ya lugha moja, na hutegemea matumizi na muktadha wa matumizi hayo. Ndipo sasa hapana maana moja ya neno au fungu la maneno.
Kulingana na nadharia hii basi, neno ‘mama’ kwa mfano, huwa halina maana ya kindani inayotokana na lugha husika bali huwa na maana za kijamii zilizotokana na lugha hiyo na ambazo zinakinzana na kubadilika kulingana na mazingira na kipindi cha kihistoria.
Kwa kuanza na kipengele cha mtindo:
Mtindo; kwa mujibu wa Senkoro (2011), “Mtindo katika kazi ya fasihi ni ile namna ambavyo msanii hutunga kazi yake na huipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni au kawaida za zilizofuatwa kama ni zilizopo (za kimapokeo) au ni za kipekee”.
Kwa ujumla mtindo uliotumiwa na mwandishi ni wa kipekee kabisa kwani ameweza kuchanganya insha,mashairi pamoja na tenzi ambazo kwa ujumla huelezea maisha yake S.Robert hususani katika insha, na katika mashairi na tenzi kuna majonzi, mawaidha, maonyo na maadili.
Katika kipengele cha mashairi mtindo uliotumika ni wa kimapokeo kwa sababu amezingatia urari wa vina na mizani, urari wa mishororo, kibwagizo na utoshelevu katika kila beti. Mfano ubeti wa 2 katika shairi la “Amina” anasema;
        2.  “Nilitaka unyanyuke, kwa kukuombea dua,
                                               Sikupenda ushindike, maradhi kukuchukua,
                                     Ila kwa rehema yake, Mungu amekuchagua,
                                     Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua”
Muundo; kwa mujibu Senkoro (kashatajwa), “muundo hutokana na umbo na mpango wa kazi ya fasihi; kwa hiyo hapa ndipo tutapata katika ushairi wa Kiswahili, mashairi yenye miundo mbalimbali iainishwayo na idadi ya mistari (vipande/mishororo) katika kila ubeti, mathalani mashairi ya uwili, utatu, unne” nk.
 Muundo uliotumika katika mashairi yote na tenzi zote ni muundo wa tarbia yaani mistari minne katika kila beti. Mfano, shairi la Amina ubeti.1 uk.4
1.      Anima umejitenga, kufa umetangulia,
     Kama ua umefunga, baada ya kuchanua,
     Nakuombea mwanga peponi kukubaliwa,
Mapenzi tuliyofunga hapana wa kufungua.
Vilevile hata katika “UTENZI HATI” na “UTENZI WA ADILI” mwandishi ametumia muundo wa tarbia (mistari minne). Mfano; utenzi wa ADILI uk.
Kijana lete kalamu,
Nina habari muhimu,
Napenda uifahamu,
Dadayo kasha zamuye,
Matumizi ya lugha; mwandishi ametumia lugha fasaha na inayoeleweka na wote hasa katika upande wa insha, lakini katika upande wa ushairi kwa kiasi fulani ametumia msamiati wa lugha ya kiarabu. Mfano katika shairi la “Namshukuru” kuna maneno kama vile, Illahi, Alhamdulillahi, Latifu, rakadha, ashrafu, nk. Vilevile ametumia tamathali za semi kama vile:
Tashbiha: shairi la “Amina” ubeti wa 1:2 uk.4 “Kama ua umefunga baada ya kuchanua”. Neno “kama” ni tashbiha inayotumika kulinganisha vitu viwili.
Vilevile hata katika “UTENZI WA HATI” uk.7 ubeti wa 7:4 tunaona tashbiha zikijitokeza. Anasema, “Nakupenda kama Hidaya” na ubeti wa 6:3 anasema, “Tunza kama sahibu” pia uk.7 ubeti wa 5:3 “Itunze kama fedha”
Takriri: urudiaji wa neno, sentensi au kifungu cha maneo ili kusisitiza jambo. ubeti wa 1:3 na 4 “Nakuombea mwanga, peponi kukubaliwa” pia ubeti wa 4:3 “Nawe wangu penzi, peponiutaingia”. Neno “peponi” limerudiwa ili kuonesha msisitizo kwamba baada ya maisha haya kuna maisha mengine peponi (mbinguni). Pia uk.6 ubeti wa 5:2 “Nijaze kadha wa kadha”, vilevile katika “UTENZI WA HATI” neno “hati” limejitokeza mara nyingi mfano, ubeti wa 1, 2, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 17, 18, 19… pia neno binti katika ubeti wa 1, 92, 93, 94, 95.
Ritifaa: Ngure (2003:128) ni kitu kisicho na uhai kama vile maiti huwa kinasemeshwa kana kwamba nafsi yake ingali hai. Mfano; katika shairi la Amina S.Robert anaongea na marehemu Amina kana kwamba yu hai. Hii imejidhihirisha katika shairi zima. Mfano; ubeti wa 4 na 5
Tashihisi: kukipa kitu kisicho hai uwezo wa kutenda. Mfano; ubeti wa 6:2;3 uk.5 anasema,
“Vumbi tena likiunga, roho likirudishiwa,
Mauti yakijitenga, mapenzi yatarejea”,
Pia katika UTENZI WA HATI uk.7 ubeti wa 6:1 anasema, “Dunia ina aibu”. Hapa dunia inapewa sifa ya ubinadamu ya kuona aibu. Vilevile uk.8 ubeti wa 17:3 anasema,
“Sauti yendavyo mbio”. Hapa napo sauti inapewa uwezo wa kukimbia kama kitu chenye uhai. Pia uk.27 ubeti wa 43:2 “Viungo vyake husema”. Viungo mbalimbali vya mwili vinapewa uwezo wa kusema kama binadamu.
Sitiari: kitu kupewa jina la kitu kingine. Hii ni katika “UTENZI WA HATI” uk.13 ubeti wa 50:3 anasema, “Mtu mwongo ni msongo”. Mtu mwongo anafananishwa na mtu asiyechezwa unyago/asiyefundwa. Pia hata katika uk.17 ubeti wa 81:1 chungo inafananishwa na kitu kilichooza. Anasema, “Chongo mbaya ni uvundo”, vilevile uk.26 ubeti wa 37:3 baba anafananishwa na mbegu. “Baba yako ni mbegu”, uk.15 ubeti wa 64:1 mama anafananishwa na kitu cheupe, kitu safi. Anasema “Mke ni nguo nyeupe”,
Jazanda (matumizi ya picha na ishara). Ubeti wa 1. Katika shairi la Amina Mwandishi anasema;
            “Amina umejitenga, kufa umetangulia,
             Kama ua umefunga, baada ya kuchanua”,
Hapa anafanisha kifo cha Amina na jinsi ua linavyonyauka.
Pia hata katika shairi la ndoa, mwandishi ametumia neno kunguru akimaanisha wale watu wasio tulia katika ndoa zao.
Taashira: maana inayotajwa si ile inayomaanishwa. Mfano uk.7 ubeti wa 6:1 katika “UTENZI WA HATI” anasema “Dunia ina aibu” pia uk.16 ubeti wa 73:1 na 74:1 anasema “Tumbo la rutuba”, “Tumbo hili la dhahabu”. Mwandishi anaposema “tumbo la rutuba” ni dhahiri kuwa anamaanisha tumbo la uzazi la mwanamke. Pia anaposema “tumbo hili la dhahabu”anamaanisha tumbo lenye thamani na la pekee wengine hawana.
Misemo: ni kauli fupifupi zenye ujumbe mzito. Kwa mfano: uk.9 ubeti wa 20:1 “Dunia ni Mvurugo” yaani inamaanisha kuwa duniani kuna mabaya na mazuri, hivyo tunapawa kuwa waangalifu. Pia uk.6 ubeti wa 5:1, “Ulimwengu una adha” pia uk.13 ubeti wa 54:1 “Ulimi wa pilipili”
Methali: uk.9 ubeti wa 22:2 “Cheche huzaa moto” yaani kitu kidogo chaweza kuleta madhara makubwa. Pia uk10 ubeti wa 28:1 “Dunia mali ya roho” pia katika shairi la “UJANE” uk. 82 ubeti wa 4:1 “Ujane neno la feli, kugombana watu wema”,
Taswira: katika “UTENZI WA HATI” uk.26 kuna taswira ya “hereni”. Hapa mwandishi anamfananisha hati na pambo la sikioni, anaona kuwa binti yake akizingatia hayo atafanikiwa maishani. Pia kuna taswira ya “pilipili” (kitu kichungu) ubeti wa 54. “UTENZI WA HATI”anamuasa mwanae asiwe na ulimi kama wa pilipili bali awe na kauli ya upole na faraja siku zote.
Jina la kitabu; “Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini”. Jina hili linasadifu kabisa yaliyomo katika kitabu, kwani, kazi yake yote mwandishi ameigawa katika sehemu kuu mbili sehemu ya kwanza ni Maisha yangu na sehemu ya pili ni Baada ya Miaka Hamsini. Vilevile katika kuelezea maisha yake ameelezea kwa mtindo wa insha, mashairi na utenzi. Na katika kila kichwa cha insha, shairi na utenzi vimesadifu kabisa yaliyomo ndani yake.
Kufaulu kwa mwandishi; Mwandishi amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, kwani mambo aliyoyandika yana halisika katika maisha yetu ya kila siku.
Kutokufaulu kwa mwandishi; Mwandishi ameelezea mambo mengi kwa kufuata imani ya dini ya kiislamu na kusahau kwamba anaowaandikia ni mchanganyiko wa imani tofauti tofauti. Pia amejikita zaidi katika mambo dhahania kama vile Mungu. Vilevile hata lugha aliyoitumia kwa kiasi fulani ina msamiati wa kiarabu hasa katika ushairi, hivyo inawawia vigumu kuelewa wale wasiojua lugha ya kiarabu.
Hitimisho; Sisi kama wachambuzi wa kazi hii tunamwona S. Robert kama kivuli kinachoishi, kwani mambo mengi aliyoyaeleza bado yapo katika jamii ya leo na kazi yake bado inamashiko na itaendelea kuwa na mashiko hata kwa vizazi vijavyo.

MAREJEO:
Mdee, J.S. na wenzake (2011). Kamusi ya Karne ya 21. (toleo la pili) Longhorn Publishers (K) Ltd. Nairobi.
Ngure, A. (2003). Fasihi Simulizi kwa Shule za Sekondari. Phoenix Publisher. Nairobi.
Ntarangwi, M. ( 2004). Uhakiki wa Kazi za Fasihi. Augustana College, Rock Island, IL 61201
Robert, S. (1991). Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini. Mkuki na Nyota Publishers. Dar es Salaam.
Senkoro, F.E.M.K. (2011) Fasihi. KAUTTU Limited. Dar es Salaam.

Print this item

  NADHARIA YA UPOKEZI (MWITIKO WA MSOMAJI)
Posted by: MwlMaeda - 07-23-2021, 08:29 PM - Forum: Nadharia mbalimbali - No Replies

MAANA YA NADHARIA

(Williady, 2013), Nadharia ni maelezo yakinifu kuhusu kitu, tajiriba, mahalifa au upumbavu na mafanikio au maangamizi yanayochomoza katika jamii. Hivyo nadharia hufungamana na mambo mbalimbali ya jamii kama vile mbinu, maarifa, tasinifu, mikabala na mienendo mbalimbali ya jamii.
1. NADHARIA YA UPOKEZI (MWITIKO WA MSOMAJI)
Nadharia ya Upokezi (mwitiko wa msomaji) ambayo husisitiza nguvu ya msomaji. Nadharia ya Upokezi (Reception Theory) iliasisiwa na wahakiki wa waasisi wa Kijerumani mwishoni  mwa miaka ya 1960.Miongoni mwa waasisi wa nadharia hii ni Robert C. Holub,Hans Robert  Jauss na Wolfagang Isser.Katika kitabu chake Reception Theory (1984), Holub anaelezea nadharia ya Upokezi  kuwa ni Mabadiko ya jumla ya umakinikiaji kutoka kwa mwandishi na kazi yake kwenda kwa matini na msomaji”
Nadharia ya upokezi inaakisi mabadiliko ya mbinu katika historia ya fasihi na ilizingatiwa kama jibu kwa jamii,wanazuoni na maendeleo ya fasihi huko Uerumani Magharibi  mwishoni mwa miaka ya 1960.Kwa mujibu wa Holub, nadharia ya Upokezi ulikuwa ni njia ya Kimapnduzi kwa wahakiki wa kisasa.
Waitifaki wa nadharia hii wanashiilia msimamo kuwa kazi ya fasihi hupata maana baada ya matini na msomaji kuadhiriana.Msomaji au mpokeaji ndiye huipa maana kazi ya fasih.
Kwani huiona na kuilinganisha na uzoefu wake wa maisha. Kielelezo hiki kipya cha uhakiki hutilia maanani dhima ya msomaji.Hans Robert Jauss katika makala yake “The change in the Paradigm of Literary Scholarship” (1926) ambaye anachukuliwa kama mmoja wa mihimili ya nadharia hii ya Upokezi anaelezea umuhimu wa kuielezea kazi ya Fasihi.Isser anaiona kazi ya Fasihi kama kitu au tukio lililo nje ya muktadha na historia.
Anasema kuwa ili kazi ya fasihi ieleweke ni lazima ushiriki  wa msomaji uoane au upatane na maana inayojitokeza katika kazi ya Fasihi.
Kwa hiyo basi , nadharia ya Upokezi hufasili Fasihi kama mchakato wa namna msomaji na wanavyoathiriana.Uzoefu wa maisha wa msomaji unaweza kutoa tafsiri tofauti kwa kazi ya fasihi kutoka msomaji mmoja na mwingine.
2.NADHARIA YA  ONTOLOJIA YA KIBANTU.
Nadharia ya Ontolojia ya Kibantu. Kuna wataalamu mbalimbali waliozungumzia nadharia hii. Kwa jumla, wataalamu hawa wameeleza maana ya Ontolojia kuwa ni mtazamo unaohusu kuwepo kwa kitu katika dunia na kuangalia vitu katika uhasilia wake (Nicholaus 2011).
Ontolojia inaweza kutazamwa kwa namna tatu: kama taaluma, kama falsafa na kama nadharia. Hivyo kwa kuwa utafiti huu ulichunguza “Mabadiliko ya kiuandishi kutoka kanuni za Ki-Aristotle kwenda kanuni za jadi ya Ki-Afrika”, kipengele cha Ontolojia ya Kibantu kinachoweza kutumika katika kazi za fasihi, tuliona ni vyema kutumia Ontolojia kama nadharia katika utafiti huu, kwani imewezesha utafiti huu kufikia malengo yake, pia ilihusiana na mada iliyoshugulikiwa.
Kimsingi kuna mitazamo minne kuhusu Ontolojia ya Kibantu. Mitazamo hiyo ni, ule wa falsafa ya kisiasa (Itikadi ya kisiasa), mtazamo au falsafa ya Kihikimati (Sagacty), wanafalsafa waliojikita katika kurekodi imani katika utamaduni wa mwafrika (Ethnofilosofia), na falsafa ya Kiuweledi.
Wanaitikadi wa kisiasa walichunguza masuala ya undugu wa kifamilia, ujamaa na kujitegemea ndani ya Afrika. Wanasiasa hao ni Julius Nyerere, Leopold Senghor na Kwame Nkurumah. Lengo lao lilikuwa ni kutaka kutafuta uhuru wa kweli kwa waafrika ili kurudisha heshima kwa mwafrika kama ingewezekana.
Mtazamo wa Kihikimati umejikita katika masuala ya uhuru, hekima na desturi za watu. Waanzilishi wa mtazamo huu wameshawishika kwamba falsafa ya kiafrika haiangalii vitu vyote vinavyohusu kazi. Lengo lao walitaka kuonesha kwamba ujinga sio hali ya kifalsafa na ujinga upo kwa kila jamii, ujinga wa mwenzako waweza kuwa uhuru kwake. Waanzilishi wa falsafa hii ni Odera H. Oruka na Marcel Griaule’s.Marcel Griaule’s alifanya mazungumzo na Oyotemmeli kiongozi wa kabila la Wadogoni na matokeo yake walipata falsafa ya kidini ya wadogoni.
Ethnofilosofia hujishughulisha na ukusanyaji wa mitazamo ya kiulimwengu kutoka katika tamaduni mbalimbali za waafrika. Hii imejikita katika masuala ya imani, masimulizi na misemo ya watu. Muunganiko huo umeunganishwa na Paulin Hountondji.  Wengine waliojihusisha na falsafa ya kiafrika katika mtazamo huu ni Placid Tempels, Leopald Senghor, John Mbiti na Alex Kagame. Hivyo, mtazamo huu umejikita zaidi katika masuala ya mila, desturi na imani za jamii.
Falsafa ya Kiuweledi imejikita katika uchambuzi na ufafanuzi wa ukweli. Zaidi inajihusisha na uhakiki, na hoja ndizo sifa za msingi kwao. Waanzilishi wa falsafa hii ni Paulina Hountondji, Kwasi Waredu, Odera Oruka na Peter Bodunrin. Wanasema kuwa falsafa ya kibantu kwa sasa inaitwa Metafilosofia, na imejikita katika kuangalia maudhui ya msingi. Wao wanahoji kwamba falsafa ya Afrika ni ipi?
Roberto (1996) anasema Ontolojiani nadharia inayohusu kuwapo, yaani ni nadharia inayoangalia yaliyokuwepo na yale ambayo hayakuwepo, halisi na yasiyo halisi, tegemezi na vinavyojitegemea.
Parrinder (1969) anasema kuwa nadharia ya kibantu inahusisha mwafrika na imani yake. Hujumuisha maisha, mazingira pamoja na fikra zake. Pia anasema kuwa mawazo ya mwafrika hujengwa katika misingi ya nguvu mbalimbali ambazoni Mungu, binadamu, wanyama, mimea na kadhalika.
Wataalamu wengine waliozungumzia nadharia ya Ontolojioa ni: Husserl (1913), Tugendhat (1928), Wolff (1928), Gruber’s (1993), Bolzano (1996), Guariono (1998), Wamitila (2008) na Cocchiarella (2007).
Kwa jumla, wataalamu hawa wameeleza mengi juu ya nadharia hii, jambo lililosisitizwa sanana wataalamu wengi waliojadili nadharia hii ni kuhusu uchaguzi wa Ontolojia nzuri na namna ya kutumia nadharia hii. Wanasema Ontolojia nzuri ni ile inayohusisha njia za Kisayansi na kutupatia njia chache na rahisi ambazo zitaelezea mambo mbalimbali katika ulimwengu. Pia nadharia hii inatukuza sana Ubantu na kumuona mwafrika kama kiumbe bora mwenye uwezo wa kubuni na kusimamia mambo yake kwa usahihi. Mbali na kutumia Ubantu (U-Afrika), nadharia hii inaeleza mambo kadhaa ambayo ni sehemu ya ufahari kwa waafrika, mambo hayo ni pamoja na dhana ya familia pana, kuamini uzazi kuwa ndio njia ya uzima wa milele, yenye kuhashiria umuhimu wa binadamu, na Ugumba ni laana na utupu kwa binadamu, kuabudu katika Mungu na miungu na kuheshimu Wahenga. Pia huhusisha na imani kuhusu uchawi, na sihiri, na ndani yake kuna masuala ya uganga. Pia umri kwa waafrika una nafasi kubwa sana katika jamii na unabeba hekima za mtu.
3.UJUMI (AESTHETICS)

Ujumi ni nini?
Ujumi ni tawi la falsafa linaloshughulika na uzuri, ubaya, ladha, n.k.
 AU
Ujumi ni elimu ya sheria na kanuni za sanaa.
Neno ujumi kwa kiingereza linajulikana kama “Aesthetics”. Neno hili limetoholewa kutoka katika lugha ya kigiriki “Ais  –  thesis”, likiwa na maana ya “Hisia” (Feelings), hasa hisia za akilini (Mental perception).
Alexander Gottlieb Baumgarten (mjerumani) ni miongoni mwa wanafalsafa yalioshungulikia kwa kina juu ya falsafa hii ya Ujumi. Baumgarten alidokoa baadhi ya mawazo fasaha kutoka kwa Leibniz. Leibniz alizungumzia mambo makubwa mawili amabayo ni LOGOS na ETHOS.

LOGOS, ni mantiki itokanayo na neno la maharifa au sababu ipelekeayo uwelewa mpya au kuyachekecha mawazo makuukuu na kupata neno lenye kuchukua mkondo mpya.
 
ETHOS, ni desturi ama mguso, tabia ama kaida Fulani ndani ya jamii ambazo hufanya matakwa yahusuyo jamii Fulani tu.
 
Baumgarten, alikiendeleza kipengele cha mguso na hisia na neno “Aesthetics” likaanzishwa.
 
Kabla falsafa mpya ya Aesthetics haijachukua kasi yake, hapo awali masuala ya hisia yaliwekwa chini ya nadharia ya hisia za akili (mental perception). Dhana ya ujumi ilitoka kwenye nadharia ya hisia za akili katika karne ya 18 na kuitwa “Falsafa ya uzuri” au “Falsafa ya sanaa” au yote mawili kwa pamoja.  Baadaye ujumi uliachana na falsafa na kuwa tawi linalojitegemea la elimu.
 
Kabla ya Baumgarten, ushairi na sanaa kwa ujumla ilijadiliwa kitaalamu katika kapumoja. Hii inamaana kwamba ushairi haukutofautishwa na muziki au uchoraji ama ususi, vyote vilielezwa kwa pamoja.
Baumgarten akaigawa dhana hii katika maeneo mawili ambayo ni uzuri na sanaa.

1.       UZURI (The good or the truth).

Uzuri ni ukamilifu wa hisia za akili unaoleta kulitazama jambo au mambo Fulani katika mtazamo chanya, haijalishi, kwani mwingine anaweza kulichukulia jambo hilo kimtazamo hasi lakini mtazamo wake hauondoi uzuri wa chanya kwa atazamaye chanya.

2.       SANAA

Sanaa ni ufundi wa kuunda jambo. Twaweza kuueleza uzuri kupitia sanaa. Sanaa yaweza kuupambanua uzuri kwa viwango vya juu zaidi kuliko jambo lolote lile.

4. NADHARIA YA UFEMINISTI ( Mtazamo wa kike)
(Williady, 2015) Nadharia hii inahistoria ndefu duniani, ikimaanisha ni moja ya nadharia zilizopata kutokea miongo mingi iliyopita. chanzo cha kuibuka kwa nadharia hii ni vuguvugu la kutaka kufuta kabisa uonevu wa mwanaume kwa mwanamk. nadharia hii inadai kuwa chimbuko lauonevu na ukandamizaji unaofanywa na wanaume kwa wanawake ni uroho wa mwanaume katika kumtawala mwanamke. Kwaufupi, ajaenda kuu ya ufeministi na mafeministi ni kumaliza kabisa utawala wa mwanaume kwa mwanamke.
moja ya wadau waliochangia sana kuendelea kwa nadharia hii kwa kasi ni Adrew Dworkin. Mwaka 1976, akiwa katika mji mkuu wa Uingereza, London, alitoa mapendekezo makali katika kukomesha utawala wa mwanaume kwa mwanamke, Dworkin anasema: Ili kufanikisha, tunahitaji kubomoa kabisa muundo wa mihimili ya utamaduni wa jamii kama vile sanaa, kanisa, sheria, kaya zinazodhibitiwa na baba, jamii na taswira zote za asasi, mila, desturi ambazo zinamwona mwanamke kuwa mtu ovyo.
WATAALAMU MBALIMBALI WALIVYOZUNGUMZIA MAANA YA UFEMINISTI
Nadharia ya Ufeministi imefasiliwa na wataalamu mbalimbali kama vile:
Wamitila (2003:253), hii ni nadharia ambayo imewekewa msingi na msukumo mkubwa pamoja na nia ya kupigania ukombozi wa mwanamke kutokana na pingu za kiutamaduni, kidini, kijamii, kisiasa na kiuchumi. Hii ni nadharia ambayo inasaili na kudadisi itikadi ya kiume ambayo imekuwepo katika jamii kwa kipindi kirefu. Kudadisi pia fasiri za kiume za fasihi pamoja na mikabala ya kiubabedume.
Ntarangwi (2004:45), ni nadharia ambayo inajaribu kukiuka mitazamo ya kiume ambayo yaelekea inatumiwa sana katika jamii.
Mukobwa M. nadharia ya ufeministi imetokana na mkondo na harakati za kutetea haki za wanawake ulimwenguni na imejikita katika imani ya usawa wa kijinsia, kijamii, kisiasa na kiuchumi.
(Williady, 2015) Ninadharia iliyojaribu kuvunja mwiko wa mfumo dume hapa dunia kwa kuanzisha mapambano ya usawa wa kijinsia, bilashaka majaribio haya bado hayajafanikiwa.
Kwa jumla, nadharia ya ufeministi ni nadharia iliyojikita katika kupinga ukandamizaji wa mwanamke katika jamii hususan katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni.
KUIBUKA KWA UFEMINISTI NA HARAKATI ZA KUIENDELEZA NADHARIA HII
Uhakiki wa kifeministi ulishika kasi miaka ya 1960 na kuendelea kukua na kuishia kuwa muhimu katika miaka ya hivi karibuni. Zipo kazi kadhaa zilizoandikwa kabla na kulimulika suala hili kwa namna moja ama nyingine. Kazi kuu mbili zinazorejelewa hapa ni A Room of One’s Own ya Virginia Woolf na A virdiction of the Right of women ya Mery Wollsto Necraft.
Hata hivyo, kazi iliyoishia kuwa na mchango mkubwa katika kuuweka msingi wa uhakiki wa ufeministi ni kazi maarufu ya mwandishi wa Kifaransa, Simone de Beauvoir iitwayo, The Second sex, 1952 katika kitabu hiki, mwandishi huyu anachukuwa mkabala wa kiharakati kwa kushambulia na kukosoa baadhi ya asasi zinazochangia katika kumdhalilisha au kumdunisha mwanamke. Asasi kuu anazozishambulia ni ndoa, dini na utamaduni.
Nadharia ya ufeministi ilichimbuka huko Marekani katika harakati za kukomesha biashara ya utumwa mwaka 1830. Wanawake wakaanzisha harakati za kupigania haki za mwanamke.
Wamitila (2006:160-161) na Ntarangwi (2004:52-56) wamebainisha malengo mbalimbali ya ufeministi.
Ni kweli kwamba kuna baadhi ya malengo ya ufeministi yanakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika lakini baadhi ya malengo hayo yanasawiri maisha halisi ya mwanamke wa kiafrika kama ifuatavyo:
Kubainisha umuhimu wa mwanamke, kutokana na mwanamke kukulia katika jamii zenye mfumodume. Umuhimu wake haukuonekana, ndiyo maana ikaanzishwa nadharia ya ufeministi ambayo yenyewe iligundua umuhimu wa mwanamke katika jamii. Umuhimu wake upo katika Nyanja zote za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni. Mfano, katika nyanja ya kisiasa mwanamke anaweza kuwa kiongozi bora na mwenye ushauri. Hili linajidhihirisha katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ (1994). Mwandishi anathibitisha hili anaposema:
“Tunayo karibu miaka ishirini ya uhuru! Lini tutampata mwanamke wa kwanza awe waziri atakaye husishwa na maamuzi yatakayoongoza nchi yetu huko tuendako? Kumbe nguvu walizonazo wakina mama, uwezo wao wa kupambana, na kujihusisha kwao bila kutegemea kupata faida yoyote ni mambo ambayo hayahitaji tena kuthibitishwa. Wanawake wamewainua wanaume wengi kwenye ngazi za juu.” (uk.82)
Katika nyanja ya kijamii, mwanamke ni mlezi wa familia. Mfano, Ramatulayi anailea familia yake kwani ameweza kulipa bili ya maji, umeme bila hata kumtegemea mwanaume. Mfano, mwandishi anasema:
“Licha ya mzigo niliokuwa nao tangu zamani, nikaubeba na ule uliokuwa wa Modu. Ununuzi wa vyakula muhimu ulinishughulisha kila mwisho wa mwezi. Nilihakikisha kwamba sikuwa na upungufu wa nyanya au mafuta, viazi mviringo na vitunguu wakati ambapo vyakula hivi viliadimika sokoni… Nilikuwa mwangalifu kuzilipa bili za maji na umeme pindi zilipofika.” (uk.69)
Lengo hili la ufeministi linakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika, kwa kuwa mwanamke wa Kiafrika anaonekana hana umuhimu katika jamii, pia anaonekana kuwa dhaifu ambaye hawezi kuiendesha familia yake bila msaada wa mwanaume hii ni kutokana na jamii nyingi kuendeshwa na mfumodume.
Kuorodhesha kuwa kihistoria wanawake wamekuwa ni tegemezi na wasaidizi wa wanaume, ni kweli kihistoria wanawake wamekuwa wategemezi na wasaidizi wa wanaume. Mfano katika tamthiliya ya Nguzo Mama iliyoandikwa na Penina Muhando (2007) tunaona mhusika BI MOJA alivyokuwa akimtegemea mume wake na kutaka anunuliwe kanga. Mwandishi anasema:
“BI MOJA: (kwa Shaabani): Kama ulijua kufika sasa hivi nipe hela ya kanga bwana meli meli hii hainikosi leo utanipa hela hizo kanga nikakate. Mwezi wa tatu huu kanga sizijui.
Shaabani: Nimekuambia mimi hela sina. Sasa unataka nikaibe?”(uk.31-32)
 Ni kweli kwamba mwanamke wa kiafrika amekuwa tegemezi katika jamii, kwani humtegemea mwanaume katika mambo mbalimbali ya kifamilia. Kwa mfano kutafuta au kununua mahitaji ya nyumbani kama vile chakula, mavazi yake na watoto wake au kulea watoto wake.
Kuondoa ukandamizaji wa mwanamke kutokana na pingu za kiutamaduni, kijamii, kidini, kisiasa na kiuchumi. Jamii nyingi za Kiafrika zimejengeka katika mfumodume, hivyo basi jamii zinamkandamiza mwanamke kutokana na pingu hizo. Katika kulithibitisha hili waandishi wa kazi za fasihi nao hawakuwa nyuma kulizungumzia katika kazi zao na lengo ni kuondoa mfumodume uliojengeka muda mrefu katika jamii.
Kwa upande wa kiutamaduni mwanamke ameonekana kukandamizwa kwa kuonekana hana mamlaka hata ya kurithi mali za mumewe au zake mwenyewe, badala yake hata akifiwa na mumuwe anapigwa, anafukuzwa na kudhalilishwa. Penina Muhando anayathibitisha haya katika tamthiliya yake ya Nguzo Mama kwa kumtumia BI SABA pale anaposema:
            “Akalia Bi Saba tena akalia
            Hana wa kumsaidia
            Mumewe kafa nduguze wakaja juu
            Pesa wamechukua senti tano haikubaki
Vyombo na nguo zote wakagawana
            Roho ilimpasuka Bi Saba kuwaona hao ndugu
            Walivyogombania mali wasiyoichuma…
Sasa juu ya yote haya wamerudi kufagia
Hata ufagio wamebeba
            Na lawama kumtupia eti pesa kazificha.” (uk.39)
Pia mwanamke anaonekana anajishughulisha na kazi mbalimbali za kujiletea maendeleo yake binafsi lakini anarudishwa nyuma kwa kukandamizwa na mwanaume. Penina Muhando anayathibitisha haya kwa kumtumia BI PILI ambaye alikuwa anapika pombe ili kujikwamua katika hali ngumu ya maisha lakini mumewe SUDI alizichukua hela zote alizokuwa alizozipata. Kwa mfano, mwandishi anasema:
            “BI MSIMULIZI: Upishi wa pombe balaa ulimzushia
                                    Visa na mikasa Bi pili havikumuishia
                                    Pesa alizipata kutokana na hiyo pombe
                                    Lakini visa vya pombe hiyo pesa hazikufidia”
            SUDI:              (kwa Bi Pili) Nani kalewa? Umeninywesha wewe?
                                    Wee!hawara zako ndiyo wamekutia jeuri unaninyima pesa.
                                    Toa pesa sasa hivi (Anampiga) Bi Pili anakimbia huku akilia.”          (uk.16)
Vilevile, mwanamke alikuwa anakandamizwa kwa kulazimishwa kurithiwa na kaka au ndugu wa mume pindi anapofiwa na mumewe. Mwandishi analithibitisha hili katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii pale anaposema:           
            “Tamsiri, zitapike hizo ndoto zako za kutaka kuniposa.
            Umeshakaa nazo kwa siku arobaini. Kamwe sitokuwa mkeo.”(uk.81)
Kwa upande wa kisiasa, mwanamke amekuwa akikandamizwa kwa kuonekana hawezi kuwa kiongozi bora wa kuiongoza nchi ndio maana hata nafasi za wanawake zilikuwa chache huko bungeni. Katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ mwandishi anayadhihirisha haya kwa kumtumia Ramatoulayi ambaye akilalamika kuhusu ukandamizwaji wa wanawake huko bungeni pale anaposema:
“Wanawake wanne, Dauda, wanne miongoni mwa wabunge mia moja uwiano gani huu wa kimzaha! Wala hakuna uwakilishaji wa kimkoa” (uk.81)
Kwa upande wa kijamii, mwanamke amekuwa akikandamizwa kwa kupigwa na mumewe bila sababu zozote za msingi. Hili linajidhihirisha katika riwaya ya Rosa Mistika iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi (1988) kwa kumtumia mhusika Zakaria ambaye alikuwa anampiga mkewe bila sababu. Mwandishi anasema:
“Regina tangu aolewe hakuwa na raha! Alikuwa akisumbuliwa na kuteswa na mumewe kwa kosa lisilokuwa lake. Katika kijiji chote cha Namagondo hapakuwa na mwanamke aliyekuwa akipigwa karibu kila juma kama Regina. Wanawake wengi kijijini walijiuliza kwa nini hakutaka kumuacha bwana wake. wengine walimuonea huruma, wengi lakini walimuona mjinga.” (uk.3)
Pi, mwanamke alikuwa anakandamizwa kwa kuonekana kuwa yeye ndiye mwenye majukumu ya malezi, kwa hiyo hata watoto wakiharibika anayelaumiwa ni mwanamke. Euphrase Kezilahabi analithibitisha hilo pale anaposema:
“Lete hiyo barua iko wapi? Pamoja na shilingi ulizopewa unafikiri sisi hapa maskini. Rosa alipigwa tena na tena. Makofi yalikwenda mfululizo hata damu zikamtoka puani na mdomoni. Baba nihurumie sitarudia tena… Zakaria hakujali alichukua fimbo na kuongozana na bintiye mpaka chumba cha watoto hali akinguluma lazima unioneshe barua hiyo unataka kuniletea umalaya wa mama yako hapa.” (Uk.7)
Vilevile, mtoto wa kike alikuwa anaonekana hana thamani katika jamii, na watoto wa kiume ndio waliopewa kipaumbele. Euphrase Kezilahabi anathibitisha haya katika riwaya ya Rosa Mistika kwa kumtumia Zakaria ambaye kabla ya kumpata mtoto wa kiume alikuwa anamnyanyasa sana mke wake lakini baada ya kujifungua mtoto wa kiume manyanyaso yaliisha na alimpenda sana mkewe. Mwandishi anasema:
“Zakaria alirudi nyumbani siku hiyo. Alikuwa amekwisha pata habari hizo njiani. Alimbeba mtoto. Alimpa pongezi mke wake. Regina sasa mji huu umekuwa wako. Asante Regina alijibu akitabasamu, alijiona anauwezo wa kuzungumza.” (uk.24)
Lengo hili linakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika, kwani mwanamke hatakiwi kurithi mali yoyote pindi wazazi wake wanapofariki au mumewe anapofariki. Pia mwanamke kushindwa kupewa nafasi ya kutoa maamuzi yoyote katika masuala ya kiukoo. Kwa upande wa dini mwanamke anakandamizwa na kuonekana dhaifu hivyo kutokuwa na nafasi ya kuongoza waamini. Mfano, dini ya Kiislamu na baadhi ya madhehebu ya Kikristo.
Lengo lingine ni kuzitambua na kuzibainisha dhamira kuu katika kazi zilizoandikwa na wanawake. Dhamira kuu ni dhamira inayomsukuma mwandishi katika kuandika kazi ya fasihi. Baadhi ya waandishi wanawake wameonesha dhamira kuu katika kazi zao kama ifuatavyo:
Nguzo Mama iliyoandikwa na Penina Muhando (2007) imebeba dhamira kuu ambayo ni ukombozi wa mwanamke. Ukombozi huo upo katika nyanja mbalimbali kama vile kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa. Mfano, mwandishi ameonesha wanawake wanavyojishughulisha katika kuinua uchumi wao, kwani walikuwa wakiuza vitambaa na kupika pombe. Mwandishi anathibitisha haya kwa kusema:
“BI TANO: Yaani mnasema mimi mvivu siyo nimezunguka mji mzima na zigo hilo halafu mnaniambia mimi mvivu. Nawaambia watu hawataki kununua au mnataka niwagawie bure.”
BI NANE: Lakini kwa nini wakatae kununua hivi, mbona vile vya mwanzo walivinunua? (uk.16).
Vilevile, Katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ (1994) suala la ukombozi wa mwanamke limejitokeza kama dhamira kuu. Ukombozi huu umejikita katika nyanja za kisiasa, kiutamaduni, kijamii na kiuchumi.
Mfano, katika nyanja ya kijamii, mwandishi ameonesha jinsi ya kumkomboa mwanamke kielimu, pale anaposema:
“…Shangazi Nabu anampeleka Nabu mdogo katika shule ya Kifaransa huko. Huko Nabu alijifunza aina mbalimbali za mapishi, matumizi ya pasi na zana za kutumia na kumenyea…” (uk.39)
Lengo hili linakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika, kwa kuwa tangu mwanzo wanawake walikuwa hawaruhusiwi kuwa viongozi, badala yake wanaume ndio waliochukuwa jukumu hilo la uongozi katika jamii. Pia, wanawake hawakuruhusiwa kupata elimu wakitegemezwa katika majukumu ya nyumbani na kuandaliwa kwenda kuolewa na kuja kuwa walezi wa familia.
Kuichunguza historia ya kifasihi ya jadi ya kike na kuwamulika waandishi wa kike waliotambua hali za wanawake na ambao wanaweza kuchukuliwa kama vielelezo kwa wasomaji wao. Hapo awali kazi mbalimbali za kifasihi za jadi za kike zilielezwa na waandishi wa kiume. Lakini nadharia hii imemulika waandishi wa kike wanaotambua hali mbalimbali na wameamua kuandika kazi mbalimbali ambazo zinaelezea matatizo ya wanawake. Mfano, katika tamthiliya ya Nguzo Mama mwandishi anaelezea jinsi wanawake wanavyonyanyaswa na kuachiwa majukumu ya kulea familia, kuchukuliwa mali zilizoachwa na waume zao baada ya kufariki. Mfano, mwandishi anasema:
“…Haa! Shemeji mmerudi kuchukua hata kitanda! Hata sufuria! Nitalala wapi na nitapikia wapi jamani!” (uk.39)
SUDI: Haya nipe pesa ulizokwisha kupata.
BI PILI: Hee! Kwa nini nikupe?
            SUDI: Leta pesa upesi kabla sijakukong’ota.” (uk.13)
Mariama Bâ naye ni kielelezo kwani ameelezea matatizo mbalimbali yanayowakumba wanawake na namna wanavyokabiliana na matatizo hayo. Mfano mwandishi anasema:
“… Ramatulayi, Acha nisikilize mimi zaidi; Redio ya Kankan ilinifahamisha kwamba ulikataa kuolewa na Tamsiri. Ni kweli? Ndio.”  (uk.87)
 Mwandishi anaonesha jinsi mhusika Ramatulayi alivyojitambua na kukataa kurithiwa na Tamsiri, pia anamkataa Dauda ambaye alitaka kumrithi baada ya kufiwa na mume wake.
Kupitia lengo hili tunaona wanaufeministi wameongelea kuhusu wanawake tu ambao ni vielelezo katika kazi za fasihi, lakini wapo wanaume ambao wamezungumzia masuala mbalimbali yanayowahusu wanawake. Mfano, Shaaban Robert aliyeandika Wasifu wa Siti Binti Saad.
Kudhihirisha kuwa kuna sifa fulani za kike na uzoefu fulani wa kike katika uwazaji, hisia, kutathmini, kujiangalia na kuuangalia ulimwengu wao wa nje. Uzoefu fulani wa kike unajitokeza katika uwazaji na jinsi wanavyousawiri uhalisi. Kazi ambazo zinamsawiri mwanamke kwa njia chanya, mfano ni riwaya ya Kiwasifu ya Shaaban Robert Wasifu wa Siti Binti Saad.  Kuna mashairi kadhaa aliyoyatunga mwandishi ambayo yanaendeleza suala hili la uchanya wa wanawake katika jamii. Mfano wa usawiri wa wahusika linathibitishwa pale mwandishi anaposema:
            “Siti binti Saad,
Ulikuwa mtu lini,
Ulitoka shamba,
Na kaniki mbili chini,
Kama si sauti,
Ungekula nini?” (uk.22)
Hisia: mfano, katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii kupitia mhusika Daba alivyomwambia mama yake kuhusu Benetuu. Mwandishi anasema:
“Hasira ya Daba iliongezeka zaidi jinsi alivyozidi kuichambua hali ilivyokuwa. “Mama! Vunja ndoa yako! Achana naye mtu huyu hajatuheshimu, si wewe wala si mimi… sitaki kukuona unagombania mwanaume na mwanamke mwenye umri sawa na mimi.” (uk.52)
Lengo hili la wanaufeministi, linaendana na hali halisi ya wanawake wa Kiafrika, kwa kuwa mawazo ya mwanamke jinsi anavyojiwazia yeye mwenyewe au kuwawazia wanawake wenzake hutofautiana . vilevile, hisia za mwanamke zinaweza kudhihirika katika maandishi na kuonesha jinsi wanavyowaza katika hali ya kawaida.
HITIMISHO
Lengo la nadharia ya ufeministi lilikuwa ni kuondoa unyanyasaji wa kijinsia hasa kwa mwanamke. Hivyo basi, malengo ya ufeministi yalijikita katika kumnasua mwanamke kutoka katika pingu za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii. Malengo haya ndiyo yanayoleta ukinzani wa maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika. Hali hii imeleta mabadiliko katika maisha ya wanawake wa kiafrika, kama vile kutaka haki ya elimu, kumiliki mali, kurithi mali, kutaka nafasi za uongozi, pia kuwa na maamuzi ya kifamilia au kiukoo, katika kupingana na pingu za maisha.
Nadharia ya Uhemenitiki
Uhemenitiki ni taaluma inayohusiana na uelewaji na kutafsiri matini. Chimbuko la nadharia hii ni katika uchambuzi wa falsafa katika matini za kidini, hususani dini ya Kikristo. Waasisi wanaohusishwa na chimbuko la nadharia hii ni kama vile Friedrich Schleiermacher (1768-1834),Wilhem Dilthey (1833-1911) na Martin Heidegger (1889-1976).
 
 Msingi mkubwa wa nadharia ya Uhemenitiki ni imani ya kwamba matendo ya binadamu yanaathiriwa kwa njia  mbalimbali na asasi tofauti zilizoko katika mazingira yake. Msingi huo unatupeleka katika dhana ya kuibua umuhimu wa kuelewa njia au mbinu za uelewaji wa maana za matini. Madai ya msingi ya nadharia ya Uhemenitiki yanahusisha dhana mbalimbali kama vile duara la kihemenitiki, utukuzaji pamoja na ile ya ufufuaji wa kisarufi, kisaikolojia na kimuktadha (Senkoro, 1987; Wamitila, 2002 katika Ponera, 2010).
 
Akizungumzia suala la Mviringo au Duara la Kihemenitiki, Senkoro (1989:9) anasema:
“…katika usomaji kuna mviringo wa kihemenitikiambao humfanya msomaji aende mbele na nyuma, kushoto na kulia mwa yale yaongelewayo katika kaziya fasihi.Hadhira huwa wanabashiri na kuhusisha mambowanayoyapitia maishani mwao”.

Kulingana na nadharia hii ya Uhemenitiki huwa kuna ugumu wa kuwepo kwa uwiano kati ya malengo na maana asilia ya mtunzi dhidi ya uelewaji wa maana aipatayo msomaji. Uelewaji wa maana kwa msomaji huhusisha kuyajua mambo mbalimbali yaliyomzunguka mtunzi wakati au kabla ya kuitunga kazi husika. Ni vigumu kuelewa malengo na maana asilia ya mtunzi iwapo msomaji au mhakiki hatahusisha mambo hayo. Kwa kufanya hivyo, ndipo msomaji atakuwa amelitalii duara la kihemenitiki. (Ponera, 2010).

Dhana ya Utukuzaji  katika nadharia ya Uhemenitiki inamaanisha jumla ya makisio mbalimbali ambayo msomaji au mhakiki wa kazi ya fasihi huwa nayo punde aishikapo kazi yoyote ya kifasihi. Makisio hayo  hujengwa akilini mwa msomaji kulingana na misingi mbalimbali kama vile anwani yake (jina na picha ya kitabu), kiwango cha usomi, utamaduni, upeo wa uelewa, pamoja na ulinganisho wa kazi zozote zilizotungwa na watunzi wengine zinazofanana na hiyo (Wamitila, 2002).
 
Wamitila (2002:193) anafafanua kuwa dhana ya Ufufuaji, hususani ule wa kisaikilojia iliasisiwa na Dilthey (1833-1911).  Alisisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa msomaji au mhakiki kufufua muktadha asilia wa kazi inayohusika na kujaribu kujiweka katika muktadha huo ili aweze kuipata maana asilia ya matini. Kwa mujibu wa mawazo yake, kazi mbalimbali za kifasihi zinaweza kuwa na maana mbalimbali kwa wasomaji mbalimbali. Aidha, dhana ya ufufuaji inasisitiza kuwa ili kuielewa na kuitafsiri maana ya matini lazima msomaji au mhakiki azame katika kuuelewa mtindo. Hapa neno ‘mtindo’ limetumika kumaanisha muktadha wote wa mfumo wa maneno na sentensi zilizotumika katika matini.
 
Dhana hizi zinazobeba madai ya msingi ya nadharia ya Uhemenitiki zinahusiana kwa kiasi kikubwa. Gadamer (1960) ambaye amenukuliwa na Senkoro, (1987:7) anasema:
 
 “Taaluma ya Uhemenitiki hujihusisha na utafutaji wa maana ya kazi ya fasihi
                kwa kuuliza maswali muhimu manne:
                i. Ni nini maana ya fasihi?
                ii. Je, maana hii inahusianaje na kusudi la mwandishi?
                iii. Je, tunaweza kuzielewa kazi za fasihi za tamaduni na historia tofauti na zetu?
                iv. Je, ni rahisi kupata uelewaji wa ndani wa kazi ya fasihi au huu hutegemea
                      mazingira na historia ya hadhira ihusikayo?”.

Kuyajibu maswali haya kulihusisha kwa pamoja dhana za Duara la Kihemenitiki, Ufufuaji na Utukuzaji ambazo zinaunda madai ya msingi ya nadharia hii. Misingi ya nadharia hii ilitumika katika kuendesha utafiti uliofanywa unaohusu vipengele vya msingi vya kiufafanuzi. Misingi hiyo ni ile iliyomo katika dhana tatu muhimu zilizomo katika nadharia hii ambazo ni Duara la Kihemenitiki, Ufufuaji na Utukuzaji.

Hivyo, taswira zinazojitokeza katika ushairi wa Kaluta Amri Abedi zilichunguzwa kwa kuhusianishwa na vipengele vingine vya kimaisha kama vile matukio ya kihistoria yaliyojiri kabla au wakati wa utunzi, tabia na mwenendo halisi wa Sheikh Kaluta Amri Abedi mwenyewe, hali halisi ya maisha tangu kipindi cha baada ya kazi husika kutungwa hadi sasa, na jiografia ya alipokuwa mtunzi (duara la Kihemenitiki). Aidha, uchunguzi ulihusisha fikra binafsi za mtafiti kuhusiana na lugha na taswira mbalimbali zijitokezazo katika Diwani ya Amri (Utukuzaji). Vilevile uchambuzi wa data ulizingatia mtindo mahsusi ambao Kaluta Amri Abedi aliutumia katika utunzi kwa kuulinganisha na matumizi ya lugha ya wakati huo (Ufufuaji).

Print this item

  NADHARIA YA UHUSIANO: DHANA YA PROPOSISHENI (2)
Posted by: MwlMaeda - 07-23-2021, 08:20 PM - Forum: Nadharia mbalimbali - No Replies

DHANA YA PROPOSISHENI

Katie Wales (2001),
anasema kuwa proposisheni ni neno lililoazimwa kutoka kwa elimu ya falsafa.
Maana kiproposisheni katika kauli au sentensi ndio ya kimsingi akilini na
wakati huohuo maana katika proposisheni ni ya kidhahania ambayo huhusisha kiima
na kiarifu. Proposisheni hufanana na vitendo usemi vya kauli. Hulingana
kisarufi na sentensi arifu ambayo huwa na kiima na kiarifu. Hata hivyo, kuna
tofauti baina ya viwango tofauti vya sarufi na maana. Kama vile, sentensi
katika kauli tendaji na katika kauli tendwa zaweza kueleza proposisheni ambayo
yaonekana kuwa moja hata kama zina kiima na kiarifu tofauti.
Kwa mfano:
Mpira
ulichezwa na watoto.
Watoto
waliucheza mpira.
Vilevile, proposisheni
yaweza kuwa na maana zaidi ya moja, kama ina utata. Kwa mfano:
Joy
amepigia Judy mpira.
Maelezo katika mfano , yana maana kuwa labda Joy alimpiga Judy kwa sababu ya Mpira au pengine
alimpigia mpira ili wacheze pamoja, vilevile huenda ikawa Joy aliupiga mpira
kwa niaba ya Judy. Hivyo basi, proposisheni katika sentensi hii tabainika kama
msemaji ataeleza bayana maana aliyoikusudia katika kutamka kauli hii.
Kulingana na Halliday
(1985), proposisheni hukubaliwa au kukataliwa. Hii ina maana kuwa kama ni ya
ukweli ambao unaweza kuthibitika, basi itabidi washiriki katika mazungumzo
kuikubali na kuamini jambo lililomo katika proposisheni hiyo. Kwingineko, kama
itakuwa haina ukweli ambao unaweza kuthibiti, basi washiriki katika mazungumzo
wataikataa na kutoiamini kuwa ya kweli. Hivyo basi, ni lazima proposisheni
ithibitiwe katika misingi ya kweli au uongo.
Kwa mfano:  ‘Nchi ya
Kenya ni huru.’
Proposisheni katika
kauli hii itakubalika kwa sababu ni jambo lililo wazi na kila mtu anafahamu
kuwa ni nchi yetu ilijinyakulia uhuru na kujikomboa kutoka kwa utawala wa
wakoloni
Larson (1984:89 -197),
anasema kuwa proposisheni ni mkusanyiko wa dhana katika kundi la watu ambalo
huwasiliana. Hivi anamaanisha kuwa Proposisheni hutegemea uhusiano uliopo baina
ya dhana zilizomo.
Kwa mfano:  John,
Peter, alimpiga.
Kama John ndiye
aliyetenda kitendo cha kumpiga Peter, basi proposisheni itakuwa: John alimpiga Peter. Vivyo hivyo, Kama
Peter ndiye aliyetenda kitendo cha kumpiga John, basi proposisheni itakuwa: Peter alimpiga John. Muundo wa
semantiki katika proposisheni waweza kuonyeshwa kwa njia zifuatazo
tunazoziangazia hapa chini.
Kwa mfano: Proposisheni
katika
1) Mtenda -.John … kitendo : kumpiga… mwathiriwa :
Peter
2) Mtenda : Peter … kitendo : kumpiga … mwathiriwa :
Joh
M fuatano wa maneno
katika sarufi utabainisha ni nani aliyempiga mwingine. Proposisheni yaweza
kuzua maana kadha.
Kwa mfano:
1) John aiimpiga Peter.
2) Peter alipigwa na
John.
3) Kupigwa kwa Peter
kulifanywa na John.
4) Peter ndiye alipigwa
na John.
5) John ambaye aiimpiga
Peter.
Kuna proposisheni za
matukio ambazo hubainishwa kwa dhana ambazo huwakilishwa na maneno tofauti.
Kama vile:
[Image: SAM_1544.JPG]
Sentensi hiyo hapo juu
kwanza itachanganuliwa kwa kutambua dhana ambazo huwakilishwa na maneno
tofauti. Kisha, sentensi hii ya kisarufi kuelezwa kama proposisheni ambapo
matukio yatakuwa msingi wa proposisheni hizo. Hivyo basi, matukio hayo
yatakuwa; kuharibu na kupanga.
Proposisheni zitakuwa: Mtu aliharibu mji
                                       Mtu
alipanga vyema.
Proposisheni huelezwa
kwa kujumlisha wahusika. Nomino Mtu
imetumika katika proposisheni hizi kuwakilisha mtenda ambaye alitenda kitendo.
Kwa mfano:  “John
alikataa ahadi ya Peter.’
Matukio basi ni kukataa na ahadi kisha Wahusika ni John
na Peter.
Hivyo basi, John
alikataa naye Peter alikuwa ameahidi kufanya kitu fulani na Peter aliahidi
kabla ya John kukataa. Hatimaye tunafahamu kuwa tukio la kuahidi lilifanyika
kabla ya tukio la kukataa.
Proposisheni ndicho
kitengo kidogo zaidi katika mawasiliano. Dhana moja hutokea pamoja na dhana
zingine ili kuwepo na mawasiliano yenye maana. Kila tukio huwakilisha proposisheni.
Kwa mfano: “Joy aliruka ukuta,
alikimbia na kutumbukia ndani ya ziwa’.
Sentensi hizi zina
proposisheni tatu ambazo ni:
1) Joy aliruka ukuta.
2)
Joy alikimbia.
3)
Joy alitumbukia ziwani.
Matini chanzi katika
lugha yoyote yaweza kuwa proposisheni. Kwa mfano:
1) Lugha chanzi: Kutotii husababisha kuteseka sana.
      Proposisheni: Mtu hukosa kutii.
                              Mtu huteseka.
2) Lugha chanzi: Sifa hiyo ilipokelewa vyema na Maria.
     Proposisheni: Mtu alimsifu Maria.
                           Maria aliitikia vyema.
3) Lugha chanzi: Watu wanaofikiria kuwania kiti cha Urais,
wataanzisha kampeni zao hivi
                               karibuni.
Proposisheni: Kuna watu wanaolifikiria tendo.
                       Wanataka kuwa Rais.
                      Watafanya kampeni hivi karibuni.
Tukio laweza kuwa; tendo, tajriba au mfanyiko.
Kwa mfano:  Tendo:
Wavulana walikimbia.
                                  Paul alikula.
                       Tajriba: Maria
alisikiaJilimbi.
                                     John aliona ng ‘ombe.
                     Mfanyiko: Barafu iliyeyuka.
                                        Paka alikufa.
Kuna proposisheni za
hali ambazo kitu au matokeo ndio msingi wake. Proposisheni ya hali huwa na
sehemu mbili kuu: Sehemu hizo ni mada
na maoni. Tukianza na mada, hii ni dhana itakayozungumziwa,
ilhali maoni yahusu kitu au matokeo katika kueleza mada na uhusiano katika hali
yake.
Kwa mfano:  ‘Kitabu
ni cha Peter.’
Mada ni kitabu na chahusishwa na dhana Peter kwa uhusiano wa kuwa Peter anakimiliki kitabu kile. Kwa mintarafu hii Peter ndiye mwenye kitabu.
Proposisheni za hali huelezwa
kwa kitenzi cha kuwa ni. Kama vile:
Proposisheni ya hali;
Maelezo;
Gari …umiliki…
mimi
gari
ni langu.
Mbwa
…jin a … fido                                            Jina
la mbwa ni fido.
Msimamizi
…kitambulisho… Bwana John       Msimamizi
ni Bwana John.
John
…mahali …nyumba                                  John yumo
nyumbani.
John
.. maelezo…mkubwa                               John ndiye mkubwa.
Maana ya proposisheni
yaweza kuwa katika matumizi. Mzungumzaji anaweza kuuliza swali, kutoa arifa au
kuamrisha. Proposisheni huwa ni moja lakini matumizi tofauti.
Kwa mfano:
Maana
clekezi: John …
mtenda … aliupiga .. mwathiriwa…mpira
               Arifa:
John alipiga mpira.
              Swali: Je, John alipiga
mpira?.
             Amri: John, piga mpira!
Maana elekezi
haibadiliki lakini matumizi huwa ni tofauti katika kila proposisheni. Matumizi
hayo yapo katika proposisheni za matukio na vilevile katika proposisheni za
hali, ambayo hujulikana kama misukumo ya kiilokusheni katika proposisheni.
Sentensi sahihi, mfuatano wa maneno na uakifishaji ni mambo ambayo huonyesha msukumo
wa kiilokusheni katika proposisheni. Mara nyingi kiimbo huonyesha msukumo wa
kiilokusheni katika mazungumzo. Kwa mfano:
1) Proposisheni ya hali
ambayo inaamrisha: Uwe hapa karibu!
2) Proposisheni ya hali
ambayo yauliza: Je, Maria ni dadake?
3) Proposisheni ya hali
ambayo yaarifu: Mbwa yumo katika chumba
chake.
4) Proposisheni ya
tukio ambayo yauliza swali katika kufanyika: Je, maziwa yaliganda?
5) Proposisheni ya
tukio ambayo yaonyesha tendo la kuamrisha: Wewe,
kimbia haraka!
6) Proposisheni ya
tukio ambayo yatoa arifa katika tajriba: Tulisikia
sauti.
Msukumo wa kiilokusheni
waweza kuoneshwa kwa mfuatano wa maneno, viambishi au  maneno na huibuka hasa kupitia kwa dhamira.
Matumizi ya proposisheni ni muhimu katika kuleta maana kwa sababu mtu huenda
asifahamu maana iliyokusudiwa na msemaji.
Kwa mfano:
Tukio
– kula, mtenda – chui, mwathiriwa – msafiri.
Katika mfano; maana
haiwezi kueleweka ila msemaji afafanue lile jambo analolitamka kuwa sentensi
yenyewe ni Arifa: Kama vile; Kauli: ”Chui alimla msafiri’ au ni sentensi ya
kutaka kuhakikishiwa jambo: Kama vile; Swali:
‘Je, chui alimla msafiri. Jinsi
msemaji anavyosema jambo huchangia katika kuelewa maana. Kuna wakati ambapo
msemaji hutaja msukumo wa kiilokushcni.
Kwa mfano:  Nenda
– Nakuamrisha uende!…Amri.
                     Alikwenda – Nasema kuwa
alikwenda: Arifa.
                    Kwa nini alikwenda? –Nauliza
ni kwa nini alikwenda?: Swali.
Arifa hukusudia kumpa
msikilizaji ujumbe. Swali hukusudia kumpa msikilizaji ujumbe kutoka kwa
msemaji, ilhali amri hukusudia kutoa sheria itakayofuatwa na msikilizaji. Kama
vile: Nakuamrisha, nasema na nauliza ni proposisheni tendaji kwa sababu huonesha kitendo
kinachofanyika, yaani ni maana iliyopo katika proposisheni, ili mawasiliano
yaweze kufaulu.
Maana ya proposisheini
hujumlisha maana kadiri ya vitendo katika kishazi.
Kwa mfano: : “Jengo refu ambalo ni adhimu lilianguka”.
Yadhihirisha proposisheni kuwa:
1) Jengo ni refu.
2)
Jengo ni adhimu.
3)
Jengo lilianguka.
Katika Kiswahili, kila
mojawapo ya kauli hizi zifuatazo ni proposisheni.
Kwa mfano:
                     ‘Alex alikula ndizi.’
                    ‘Ndizi ililiwa na Alex.’
                     ‘Je, Alex, alikula ndizi?’
Matamshi yaliyo katika
mfano hapo juu, yaweza kuchanganuliwa kuwa na kiarifu kinachotaja kundi au hali
na mijadala kadha na wahusika katika tukio au hali fulani. Shughuli ni ya kula.
Mtenda ni Alex. Mtcndwa ni ndizi
Proposisheni ya
uhusiano huzua maana ya umaanisho kati ya proposisheni mbili au makundi ya
proposisheni ambayo yahusiana katika mwingiliano wa kiproposisheni ulipo katika
kauli. Huleta uamuzi na mshikamano mkubwa kuhusu yaliyozugumzwa.
Kwa mfano: “Nina njaa. Twende Westlands”. Kauli hii
ina proposisheni kuwa:
1) Msemaji anahisi njaa.
2)
Msemaji anaonelea wacnde Westlands wapate chakula.
Uhuasiano wa
proposisheni hizi mbili ni kuwa kuna suluhisho la njaa na jinsi ya kusuluhisha.
‘Kwenda kwetu Westlands‘ ni sehemu ya
suluhisho la tatizo langu kuwa ‘naona
njaa’
Leech (1974:18-23),
anasema kuwa hisia za mtu binafsi huwepo kama zinazomhusu mtu anayepokea ujumbe
au kuhusu kitu fulani zitabainika wazi. Maana hisivu yaweza kuibushwa na
proposisheni.
Kwa mfano:: “Samahani kwa kuwakatiza mazungumzo yenu
lakini, ni vyema kama mngepunguza sauti zenu“.
Msemaji wa kauli hii
alikuwa ana hasira kwa sababu ya kelele kutoka kwao, kisha alijaribu kuwa mpole
katika kuwaambia kuwa sauti zao za juu hazimfurahishi kamwe. Vilevile, proposisheni
yaweza kuzua maana katika dhamira. Jinsi mzungumzaji anavyoupanga ujumbe wake
katika mpangilio wake wa maneno na kusisitiza jambo.
 Kwa mfano: 2 .19: (A)
1) ‘Bi Smith ali/adhili
tuzo la kwanza
2) ‘Tuzo la kwanza
lilifadhiliwa na Bi. Smith’
Sentensi ya kwanza ni
katika kauli tendi ilhali sentensi ya pili ni katika kauli tendwa.
Kwa mfano: 2.20: (B)
1)
‘Ndugu yangu amemiliki duka lililo kubwa zaidi mjini Nairobi’
2)
‘Duka lililo kubwa zaidi katika mji wa Nairobi limemilikiwa na ndugu yangu’
Maana ni tofauti
kulingana na kauli zilizotumika, kulingana na mpangilio wa maneno na msisitizo.
Mfano; (A), sentensi ya kwanza ina proposisheni kuwa Bi.Smith ni mtu mabaye ni
muhimu sana ili ufadhili wa tuzo la kwanza uwepo, sentensi ya pili ina
proposisheni kuwa tuzo la kwanza ni lenye umuhimu na sio lazima lifadhiliwe na
Bi. Smith, mbali pia mtu mwingine yeyote anaweza kufadhili. Mfano; (B),
sentensi ya kwanza ina proposisheni kuwa ni ndugu yangu aliye na uwezo wa
kumiliki lile duka kubwa zaidi mjini Nairobi, ilhali katika sentensi ya pili
mtu mwingine yeyote isipokuwa ndugu yangu hana uwezo wa kumiliki duka kubwa
zaidi mjini Nairobi.

MAREJELEO
Abraham, S.
(1996). A Theory o f Structural Semantics’. Mouton and Company Publishers.
Akmajian, A. na
Wenzake. (2004) Linguistics. An lntrodution to Language and Communication. Fifth
Edition: MIT Press, Cambridge.
Atichi, A.R. (2004) The
Semantic Distinctiveness of Kenyan English: UON. Unpublished MA
Thesis.
Atoh, F.O. (2001)
Semantics Analysis of Dholuo Nowns: The Semantics Field Approach. UON.
Unpublished MA Thesis.
Blass, R. (1990)
Relevance Relations in Discource. A Study in Special Reference to Sissala:
Cambidge University
Press.
Brown, G. na Yule, G.
(1983) Discource Analysis: Cambridge University Press.
Bussman, H. (1996)
Route ledge Dictionary o f Language and Linguistics: International
Thompson Publishing
Company.
Cambridge (2008)
Cambridge Advanced Learners Dictionary. Cambridge University.
Carston, R. (2002)
Thoughts and Utterances. The Pragmatics of Explicit Communication. MA:
Blackwell Publishers
Ltd.
Comford, F. M. (1957)
Platos Theory o f Knowledge: Routeledge and Kegan Paul Ltd.
Crystal, D. (2003) A
Dictionary o f Linguistics and Phonetics. Fifth Edition. Oxford: Blackwell
Publishers.
Falsod, R. W. (2002) An
lntrodution to Language and Linguistics. Cambridge University Press.
Fleming, (1998) Google
Search. Powered by The Ultimate Programming Weblog. Sil
lntematinal: http://
worldnet Princeton. Edu/Pert/Webwn.
Fodor, J. D. (1997)
Semantics: Theories o f Meaning in Generative in Generative Grammar:
Harper and Row ,
Publishers.
Fretheim, A. (2000)
Pragmatic Markers and Propositional Attitude: John Benjamin Publishing
Company.
Green, G. M (1996)
Pragmatics and Natural Language Understanding. Second Edition:
Lawrence Erlbaum
Associates Publishers.
Greenbaum, S. na
Wenzake. (1985) A comprehensive Grammar o f English Language: Longman
Group UK Ltd.
Griffin, E. M (1991) A
First look at Communication Theory. Wheaton College: Me Graw- Hill,
Inc. Company.
Hofmann, T. R. (1993)
Realms o f Meaning: An Introduction to Semantics: Longman Group UK
Ltd.
Ifantidou, E. (2001)
Evidentials and Relevance. Volume 86: John Benjamin Publishing
Company.
Kamau, S. K. (2008) An
Analysis o f Truth Conditions in Pragmatics: Relevance Theory
A p p r o a c h . UON.
Unpublished MA Thesis.
Kasher, A. (1998)
Pragmatics. Critical Concepts. Volume V: Communication, Interaction and
Discourse: Routeledge
Publishers.
Katie, W. (2001) A
Dictionary o f Stylistics: Longman Group UK Ltd.
Katz, J.J. (1977)
Propositional Structure and Illocutionary Force. A Study of the contribution of
Sentence meaning and
Speech Acts: The Harvest Press.
Kempson, R. M. (1975)
Pressuposition and The Delimination o f Semantics: Cambridge
University Press.
Larson, M. L. (1984)
Meaning-Based Translation: A Guide to Cross-Language Eqivalence:
University Press of
America, Inc.
Leech, G. (1974)
Semantics: Penguin Books Limited.
Leech, G. N. (1971)
Towards a Semantic Description o f English: Longman Group Ltd.
Linsky, L. (1952)
Semantics and the Philosophy o f Language: University of Illinois Press.
Longmans (1968)
Longmans English Larousse: Longmans, Green and Co. Ltd.
Munga, C. M. (2009)
Sence Relations in Gikuyu: A Lexical Pragmatics Approach. UON
Unpublished MA Thesis.
Ndug’u, M. N. (2009)
Mada na Fokasi katika Kiswahili: Mtazamo wa Muundo wa Taarifa.
UON. Unpublished MA
Thesis.
Ogola, C. A. (2006) A
Pragmatic Analysis of Intercultural Communication Failures. UON,
Unpublished MA Thesis.
Palmer, F. R. (2006) An
Introduction to Language and Linguistics: Cambridge University Press.
Rouchota, V, na Jucker,
H. (1998) Current Issues in Relevance Theory: John Benjamin
Publishing Company.
Saeed, J. L. (2003)
Semantics. Second Edition: Blackwell Publishing Ltd.
Schroeder, H. (2005) Do
we Speak the same Language? A cognitive Pragmatic Explanation of
Cultural
Misunderstanding. In Across Borders: Benefiting from Cultural Differences.
Conference Proceedings.
17^-18th March: 2005.
Sperber, D na Wilson,
D. (1995) Communication and Cognition, 2nd Edition: Blackwell
Publishers.
Sperber, D na Wilson,
D. (2004) A Handout on Relevance Theory (1985-2002): Blackwell
Publishers.
Tuki (1990). Kamusi ya
Isimu na Lugha. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Educational
Publishers and
Distributors Ltd.

Tuki (2006)
English-Swahili Dictionary. Third Edition: Book Printing Services Ltd.
Chanzo>>>>>>>>

Print this item

  NADHARIA YA UHUSIANO: AINA ZA PROPOSISHENI (3)
Posted by: MwlMaeda - 07-23-2021, 08:09 PM - Forum: Nadharia mbalimbali - No Replies

AINA ZA PROPOSISHENI
Fleming (1988:53-57)
anasema kuwa proposisheni ni za aina tatu ambazo ni: Proposisheni ya hakika,
proposisheni ya thamani na proposisheni ya sera. Sehemu hii inadhamiria ama
kuorodhesha aina za proposisheni. Inafuatwa na mjadala kuhusu aina hizi za
proposisheni na hatimaye tutatoa mifano kwa kila mojawapo. Proposisheni ambazo
tutazichanganua ni kama zifuatavyo:
PROPOSISHENI YA HAK1KA
Proposisheni hii ni
tamko ambalo hulenga hasa katika imani ya msikilizaji, kama ni ya kweli ama ni
ya uongo. Jinsi itakavyojadiliwa ndivyo itakavyoibua namna msikilizaji
atakavyoichukulia kuwa ni ya kweli au uongo. Mfano huu hapa chini utatoa
mwangaza zaidi. Kwa mfano: ‘ Vyuo vikuu vyole hupatikana mjini Tamko hili
litategemea jinsi msemaji atakavyoinshawishi msikilizaji. Kama msikilizaji hana
mfano wowote wa Chuo Kikuu anachokijua kuwa mjini, basi atakubali kuwa
proposisheni hii ni ya kweli, lakini kama anakijua Chuo Kikuu chochote ambacho
hakimo mjini basi kwake proposisheni hii itakuwa ni ya uongo. Proposisheni
katika mfano, ni:
1)
Msemaji anamaanisha kuwa vyuo vikuu havipo mahali pengine ila katika miji tu.
2)
Huenda ikawa msemaji anataka kumsawishi msikilizaji kuwa kauli hii ni ya kweli.
3)
Labda msikilizaji hana ufahamu wa kutosha kuhusu vyuo vikuu.
Vilevile, katika mfano
mwingine unaoafikiana na huu.
Kwa mfano: ‘ Wanaume wote ni wabaya’.
Kauli kama hii
itategemea mtazamo wa watu mbalimbali. Kuna wale wanao amini ilhali wengine
wanakataa. Pia itategemea ushawishi kutoka kwa msemaji kuhusu tajriba yake
ikilinganishwa na tajriba aliyonayo msikilizaji kuwahusu wanaume, kisha ataweza
kuamua kauli kama hii inajambo ambalo ni la kweli au la ni jambo la uongo.
Huenda ikawa msemaji amekabiliwa na janga fulani lililo sababishwa na mwanamume
ilhali, msemaji hajawahi kupatwa na jambo lolote baya kutoka kwa mwanamume
yeyote.
Proposisheni katika mfano,
ni kuwa:
1)
Msemaji anajumlisha wanaume wote kuwa ni wabaya.
2)
Msemaji labda ana sababu ya kusema jambo hili.
3)Msemaji
anonekana kuwa na hasira.
PROPOSISHENI YA THAMANI
Proposisheni hii ni
tamko ambalo msemaji hutoa ili kutaka kupata maoni ya kutathmini kama tamko
lake ni nzuri kimaadili au la, ni sawa au si sawa. Msikilizaji hasa
hulinganisha vitu viwili na kuuliza ni kipi kilicho bora zaidi.
Kwa mfano: ‘Kuna mwanafunzi anayekula darasani, ilhali
wengine wanamsikiliza mwalimu’.
Proposisheni katikamfano,
ni kuwa:
1)
Kuna wanafunzi walio darasani.
2)
Kuna mwalimu ambaye anafunza katika darasa hilo.
3)
Mwalimu anapofunza kuna mwanafunzi mmoja ambaye yuala katika darasa hilo.
Kauli hii itategemea
maoni ya msikilizaji ambaye katika proposisheni anayoifahamu ni maadili mema
kumsikiliza mwalimu darasani badala ya kula. Mwanafunzi anafahamu kuwa si sawa
kula darasani kama mwalimu anafundisha, lakini labda analifanya jambo hili kwa
kusudi fulani. Hivyo basi, wasikilizaji wataamua ni jambo lipi lililo bora
zaidi ya lingine. Vilevile, mfano mwingine wenye kueleza jambo lililo sawa na
hili.
Kwa mfano: ‘Kuna mtu anqyepiga gumzo kanisani ilhali
Padre anahuhiri.’
Proposisheni katika
mfano, ni kuwa:
1)
Kuna wakristo walio kanisani kwa ibada.
2)
Kuna mtu mmoja ambaye anazungumza ndani ya kanisa.
3)
Padre anaendelea na shughuli ya ibada huku mtu fulani akipiga gumzo.
Vilevile kauli kama hii
itategemea maoni ya washiriki katika mjadala kama huu. Watu wasio mcha Mwenyezi
Mungu hawataliona kuwa ni jambo baya kufanya kitendo kama hiki. Kwingineko, wanaomheshimu
Mwenyezi Mungu watachukulia kuwa ni dhambi. Hivyo basi, ubora wa tendo kama
hili utategemea mitazamo ya watu walio na tajriba tofauti kuhusu maisha.
PROPOSISHENI YA SERA
Proposisheni hii ni
tamko ambalo hutoa mawazo kuhusu jambo litakalofanywa kama hatua ifaayo.
Msikilizaji hupaswa kupitisha sera mwafaka au kujitolea kwa tendo maalum.
Kwa mfano: ‘Mtuyeyote atakayepoteza kitabu alichokiazima
atanunua kingine ’.
Kauli hii ni kulingana
na sera iliyopangwa na wahusika. Hivyo basi, kauli hii, ina proposisheni kuwa:
1) Kila mmoja wao amekubali tendo maalum la kununua kitabu
atakachokipoteza.
2)
Kuna vitabu ambavyo huazimwa mahali pale.
3)
Kuna masharti fulani ambayo ni lazima yazingatiwe kuhusu kitabu kilichoazimwa.
Vilevile, hakuna mtu
yeyote ambaye ataepuka hatua hii kwa sababu yajumlisha watu wote. Kwingineko,
katika mfano: ‘Mwanafunzi yeyote
atakayechelewa kuwasili shuleni atarudi nyumbani’
Proposisheni katika mfano,
ni kuwa:
1)
Mahali pale ni shuleni.
2)
Kuna wanafunzi ambao huhudhuria shule ile.
3)
Kuna sheria fulani ambazo lazima zizingatiwe kuhusu kuchelewa shuleni.
 
Sera iliyopo katika
shule hii na baadhi ya shule ni kuwa mwanafunzi yeyote anapaswa kuwasili
shuleni kabla ya wakati uliovvekwa kama sheria au mara tu wakati huo
unapowadia. Atakayefanya kinyume na haya basi ataadhibiwa kwa kuambiwa arudi
nyumbani ilhali, wenzake wataendelea na masomo siku hiyo. Hakuna mwanafunzi
yeyote ambaye ni bora zaidi ya wengine kuwa hataadhibiwa.
MAREJELEO
Abraham, S.
(1996). A Theory o f Structural Semantics’. Mouton and Company Publishers.
Akmajian, A. na
Wenzake. (2004) Linguistics. An lntrodution to Language and Communication. Fifth
Edition: MIT Press, Cambridge.
Atichi, A.R. (2004) The
Semantic Distinctiveness of Kenyan English: UON. Unpublished MA
Thesis.
Atoh, F.O. (2001)
Semantics Analysis of Dholuo Nowns: The Semantics Field Approach. UON.
Unpublished MA Thesis.
Blass, R. (1990)
Relevance Relations in Discource. A Study in Special Reference to Sissala:
Cambidge University
Press.
Brown, G. na Yule, G.
(1983) Discource Analysis: Cambridge University Press.
Bussman, H. (1996)
Route ledge Dictionary o f Language and Linguistics: International
Thompson Publishing
Company.
Cambridge (2008)
Cambridge Advanced Learners Dictionary. Cambridge University.
Carston, R. (2002)
Thoughts and Utterances. The Pragmatics of Explicit Communication. MA:
Blackwell Publishers
Ltd.
Comford, F. M. (1957)
Platos Theory o f Knowledge: Routeledge and Kegan Paul Ltd.
Crystal, D. (2003) A
Dictionary o f Linguistics and Phonetics. Fifth Edition. Oxford: Blackwell
Publishers.
Falsod, R. W. (2002) An
lntrodution to Language and Linguistics. Cambridge University Press.
Fleming, (1998) Google
Search. Powered by The Ultimate Programming Weblog. Sil
lntematinal: http://
worldnet Princeton. Edu/Pert/Webwn.
Fodor, J. D. (1997)
Semantics: Theories o f Meaning in Generative in Generative Grammar:
Harper and Row ,
Publishers.
Fretheim, A. (2000)
Pragmatic Markers and Propositional Attitude: John Benjamin Publishing
Company.
Green, G. M (1996)
Pragmatics and Natural Language Understanding. Second Edition:
Lawrence Erlbaum
Associates Publishers.
Greenbaum, S. na
Wenzake. (1985) A comprehensive Grammar o f English Language: Longman
Group UK Ltd.
Griffin, E. M (1991) A
First look at Communication Theory. Wheaton College: Me Graw- Hill,
Inc. Company.
Hofmann, T. R. (1993)
Realms o f Meaning: An Introduction to Semantics: Longman Group UK
Ltd.
Ifantidou, E. (2001)
Evidentials and Relevance. Volume 86: John Benjamin Publishing
Company.
Kamau, S. K. (2008) An
Analysis o f Truth Conditions in Pragmatics: Relevance Theory
A p p r o a c h . UON.
Unpublished MA Thesis.
Kasher, A. (1998)
Pragmatics. Critical Concepts. Volume V: Communication, Interaction and
Discourse: Routeledge
Publishers.
Katie, W. (2001) A
Dictionary o f Stylistics: Longman Group UK Ltd.
Katz, J.J. (1977)
Propositional Structure and Illocutionary Force. A Study of the contribution of
Sentence meaning and
Speech Acts: The Harvest Press.
Kempson, R. M. (1975)
Pressuposition and The Delimination o f Semantics: Cambridge
University Press.
Larson, M. L. (1984)
Meaning-Based Translation: A Guide to Cross-Language Eqivalence:
University Press of
America, Inc.
Leech, G. (1974)
Semantics: Penguin Books Limited.
Leech, G. N. (1971)
Towards a Semantic Description o f English: Longman Group Ltd.
Linsky, L. (1952)
Semantics and the Philosophy o f Language: University of Illinois Press.
Longmans (1968)
Longmans English Larousse: Longmans, Green and Co. Ltd.
Munga, C. M. (2009)
Sence Relations in Gikuyu: A Lexical Pragmatics Approach. UON
Unpublished MA Thesis.
Ndug’u, M. N. (2009)
Mada na Fokasi katika Kiswahili: Mtazamo wa Muundo wa Taarifa.
UON. Unpublished MA
Thesis.
Ogola, C. A. (2006) A
Pragmatic Analysis of Intercultural Communication Failures. UON,
Unpublished MA Thesis.
Palmer, F. R. (2006) An
Introduction to Language and Linguistics: Cambridge University Press.
Rouchota, V, na Jucker,
H. (1998) Current Issues in Relevance Theory: John Benjamin
Publishing Company.
Saeed, J. L. (2003)
Semantics. Second Edition: Blackwell Publishing Ltd.
Schroeder, H. (2005) Do
we Speak the same Language? A cognitive Pragmatic Explanation of
Cultural
Misunderstanding. In Across Borders: Benefiting from Cultural Differences.
Conference Proceedings.
17^-18th March: 2005.
Sperber, D na Wilson,
D. (1995) Communication and Cognition, 2nd Edition: Blackwell
Publishers.
Sperber, D na Wilson,
D. (2004) A Handout on Relevance Theory (1985-2002): Blackwell
Publishers.
Tuki (1990). Kamusi ya
Isimu na Lugha. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Educational
Publishers and
Distributors Ltd.
 
Tuki (2006)
English-Swahili Dictionary. Third Edition: Book Printing Services Ltd.
Chanzo>>>>>[url=http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/bitstream/handle/11295/5896/njue,carolinew_uchanganuziwaproposishenikatikakiswahili:nadhariayauhusiano.pdf?sequence=1][/url]

Print this item

  NADHARIA YA UHUSIANO: ISHARA ZA PROPOSISHENI NZURI (4)
Posted by: MwlMaeda - 07-23-2021, 12:02 PM - Forum: Nadharia mbalimbali - No Replies

ISHARA ZA PROPOSISHENI NZURI

Proposisheni nzuri yapaswa kujadilika na vilcvile kuthibitika. Hi proposisheni itambuiike kuwa bora, basi yapaswa kutimiza mambo haya mawili. Kujadiliwa au kukubaliwa kwa proposisheni ni jambo ambalo litakalotegemea maoni ya watu tofauti tofauti na msukumo walio nao hasa wa kimamlaka, kulihusu jambo hilo na uwezo wao wa kuwasawishi wasikilizaji. Pia proposisheni nzuri yapaswa kuwa na masharti ya kweli au uongo, kisha thamani iliyopo katika proposisheni hiyo ili ifahamike kama ni nzuri au la.
PROPOSISHENI NZURI YAPASWA KUJADILIKA
Mjadala wake ni muhimu ili mambo husika yakubalike au yakatalike katika proposisheni. Msemaji humhimiza msikilizaji katika mjadala dhidi ya proposisheni. Proposisheni kama zitakataliwa au kukubaliwa, ukweli utakubalika hata kama hautathibitika na wanaoshiriki katika mazungumzo. Kwingineko uongo utabaki kuwa si kweli hata kama tutasawishika kuukubali. Kwa mfano: ‘‘Nchiya Kenya niyenye ufisadi’.
Kauli hiyo, ina proposisheni kuwa:
1) Kuna nchi fulani iitwayo Kenya.
2) Nchi hiyo huwa na ufisadi.
Ufisadi wa Kenya ni suala linaloweza kujadilivva kisha likakubaliwa au kukataliwa. Kwingineko, wanaoshiriki katika ufisadi watashikilia msimamo kuwa hakuna hatia yoyote katika ufisadi kwani ni njia mojawapo ya kujisaidia katika umiliki mali kwa kuwanyanyasa vvengine. Kisha, wanaonyanyaswa kupitia kwa ufisadi watahisi kuwa ni jambo ovu na wanapaswa kukabiliana nalo ili kulimaliza haraka iwezekanavyo.
 
Huenda ikawa walio na uwezo watazidi kuwanyanyasa walio wanyonge.
PROPOSISHENI NZURI YAPASWA KUTHIBITIKA
Ukweli wa kauli ni muhimu ili kuthibitisha ukweli wa proposisheni ipasavyo. Uongo wa proposisheni kama hauwezi kuthibitishwa basi vilevile, hata ukweli wake hauwezi kuthibitishwa. Kwa mfano: ‘Kunanyesha’ Kauli ya hiyo, ina proposisheni kuwa:
1) Msemaji huenda ikawa ametazama nje na kuona kuwa kunanyesha.
2) Pengine kuna mingurumo ya radi na matone ya mvua yanayoanguka.
Ni jambo ambalo laweza kuthibitishwa kuwa ni kweli au ni uongo, kwa kutazama nje au kwa kuzingatia
yaliyotajwa na wanaotangaza kuhusu hali ya anga. Mfano mwingine ni kuwa: ‘Yesu Kristu atarudi tena ’.
Proposisheni hapo, ni kuwa:
1) Msemaji ni muumini wa dini ya kikristo.
2) Msemaji huyasikiliza mahubiri ya injili.
3) Msemaji ana imani kwa Yesu Kristo.
4) Msemaji anaamini kuwa Yesu Kristo atarudi.
Kauli kama ya hapo juu; haiwezi kuthibitika kuwa ni ya ukweli au uongo kwa sababu yategemea imani ya watu hasa kutoka dini tofauti. Hivyo basi, ni vigumu kuthibitisha kuwa ni ya kweli v au si ya kweli.

Akmajian na wenzake (2004: 254) wanasema kuna proposisheni ambayo huelcza jambo moja maalum na pia kuna proposisheni ambayo huelezwa kwa ujumla wake. Proposisheni ya jumla yaweza kufanywa ya kweli na mambo tofauti.
Kwa mfano: ‘Nakuahidi kuwa nitafika.’ Proposisheni hii itakuwa ya kweli kama nitatimiza ahadi yangu na kufika. Itakuwa ya kweli pia kama ni mimi nitakaye timiza jambo hilo na wala sitamtuma mtu mwingine.
Proposisheni inayoeleza jambo moja maalum, hulenga jambo mahususi na mtu fulani mahususi.
Kwa mfano: ‘Neil Armstrong ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kufika katika maeneo ya mwezi’ Proposisheni hii ni ya kweli kwani ni jambo linalojulikana kuwa lilitendeka na limo katika hifadhi.

Leech (1969:39-40), anasema kuwa kuna proposisheni mbili maarufu kama; mzunguko na ukinzani. Mzunguko ni aina ya proposisheni ambayo ni ya kweli kulingana na yanayojadiliwa katika jambo linalodokezwa.
Kwa mfano: ‘ Wavulana hukimbia shuleni’. Proposisheni katika mfano huo, unadokeza kuwa:
1) Wavulana hucnda shulcni.
2) Hivyo basi inathibitika kuwa wao hukimbia kuelekea shuleni.
3) Wavulana ambao hukimbia shuleni huenda shuleni.
Ina maana kuwa ni wavulana wote, wala sio baudhi yao au mmoja maalum. Proposisheni nyingine huwa
na madai ambayo yamefanana, nyingine madai yaliyopatana kwa jinsi mambo fulani yaliyofasiriwa na nyingine huwa na madai yanayofiiata mantiki ili kupata wazo la ujumla au pia muungano.
Kwa mfano:
1) ‘Watu ambao wana bahati wanabahati’ – kufanana.
2) ‘ Wenye magari humiliki magari’ – Yafuata mantiki.
3) ‘Mawazo yanayofaa watu huwafaidi wanasayansi
’. – Yafuata ufasiri wa jambo.
4) ‘Tufaha hupendwa na watoto ambao ni wa matajiri’. — Yafuata mantiki pamoja na ufasiri wa jambo.
Ukinzani ni aina ya proposisheni ambayo ni ya uongo kulingana na yanayodaiwa katika jambo lililodokezwa.
Kwa mfano:
1) ‘ Kunanyesha na hakunyeshi ’.
 2) ‘Nduguye John mdogo ni mkubwa kwake kwa umri ’.
Proposisheni hizi zina ukinzani kwa sababu haiwezekani kuwa jambo moja litatendeka na kinyume chake kwa pamoja. Maana ya umbo la kimantiki italingana na mfumo wa mantiki utakaoshughulikiwa.
Vilevile, proposisheni hizi zikielezwa kwa upana zaidi zitarejelea Proposisheni, yadokeza kuwa: maeneo tofauti.
Kwa mfano: ‘Kunanyesha Embu na hakunyeshi Nairobi’. Hivyo basi’ itakuwa hakuna ukinzani tena. Katika proposisheni kuna ukweli ulio na mantiki ambao pia ni ukweli ulio changanuzi ambao ukweli wake hutegemea maana yake.
Kwa mfano:
1 ‘Kapera huyu hajaoa’. – mzunguko.
2) ‘Kapera huyu ameoa’ – ukinzani.
PROPOSISHENI KATIKA MISINGI YA KWELI AU UONGO
Cambridge (2008: 1563-1564), wanasema kuwa ukweli ni jinsi ya ubora uliopo katika jambo lililo la kweli. Ni uhakika uliopo kuhusu hali, tukio au mtu. Husisitiza kuwa jambo ni la kweli, au ni hali ya kuwa katika ukweli. Cambridge (2008: 509), wanaendelea kusema kuwa uongo ni jambo lisilo halisi lakini hufanywa kuonekana kuwa kweli ili kuhadaa watu. Vilevile, kusema uongo kuhusu jambo, ni sawa na kusema jambo
lisilo sahihi, lililo kataliwa au lisilo aminika.
Wilson (1967: 76-79) anasema kuwa proposisheni ni ya kweli kama itatimiza mambo yafuatayo:
1) Mtu anafahamu maana ya jambo liliosemwa.
2) Mtu awe na njia mwafaka ya kuthibitisha jambo lililopo katika proposisheni.
3) Mtu awe na ushahidi unaofaa ili aweze kuliamini jambo hilo.
Kwa mfano: ‘Ni kweli kuwa dunia ni mviringo Kama mtu hafahamu maana katika kauli hivyo basi, hawezi kuthibitisha kuwa ni ya kweli au la. Vilevile, kama mtu hana ushahidi wa kutosha kuhusu jambo, basi itakuwa vigumu  kuthibitisha kuwa kauli hii ni ya kweli. Ni bora kuhakikisha kuwa kila mtu anafahamu maana ya kauli hii na njia mwafaka ya kuthibitisha kisha wanasayansi watafanya utafiti wao ili kuwa na ushahidi thabiti.
Kauli za aina tofauti hueleza mambo kadha kuhusiana na ukweli au uongo wa jambo fulani. Kama vile:
1) Kauli za kuamuru na za mtazamo.
2) Kauli chambuzi.
3) Kauli za thamani.
4) Kauli dhanifu.
AINA ZA KAULI
Fleming (1988:59-63) anasema kuwa kuna aina nne za kauli. Aina hizi ni kama zifuatazo: Kuamuru na mtazamo, chambuzi, thamani na dhanifu.
Kauli hizi tutazijadili kwa kuzieleza maana zake kisha kuzitolea mifano mwafaka kwa kila mojawapo ya aina hizi, ambayo itafafanua zaidi lengo la kauli zenyewe katika mawasiliano. Madhumuni ya kauli hizi hasa ni kumpa msikilizaji athari fulani baada ya kuzisikiza na mwishowe kuzifasiri kama ilivyo kusudiwa. Kwanza, kauli za kuamuru na mtazamo ni zile ambazo hutoa amri au hueleza mambo yanayomhusu msemaji kama; matumaini au analolitamani.
Kwa mfano:
1. ‘Tumikia Mungu na umheshimu Mfalme.’
 2) ‘ Tupendane sote kama ndugu.’
Kauli kama hizo hazina kusudi la kuwa ni za kweli au uongo kwani hasa zaeleza mitazamo ya watu kuhusu mambo fulani. Hivyo basi, mtu anaweza kughairi na kukosa kumtumikia Mungu na kutomheshimu vilevile. Pia, ana hiari ya kutopenda wengine kama ndugu.
Kauli hizi hueleza jambo kuhusiana na mtazamo wa mzungumzaji na wala sio jambo la hakika. Kwa
mfano:
1. ‘Wanaume wote ni sawa.’
2. ‘Wanaume wote ni huru.’
Ili kuthibitisha kauli hizi, itabidi kutazama mambo yote ya kijumla katika wanaume, kama vile; urefu na werevu kisha kuchunguza mambo haya kama ni sawa.
Vivyohivyo, ni jambo bora kubainisha ni jambo lipi litakalosababisha wao kuwa huru. Kama, mwanamume
amepewa hadhi ya juu katika jamii, kuwa yeye ndiye atakayefanya uamuzi wa mambo yote katika familia basi, mwanaume atakuwa na uhuru wa kufanya lolote alitakalo.
Ujumbe waweza kupashwa kupitia kwa kauli ambapo itakuwa muhimu kufahamu ujumbe wenyewe ni wa aina ipi, na jinsi ya kuweza kutambua na kuwa na ushahidi kama jambo ni la kweli au la. Kwa mfano: ‘Mungu ni Baba yetu anayetupenda.’
Kauli kama hii yaweza kuwa ni ya mtazamo ambayo itamaanisha kuwa:
1) Tunapaswa kupendana sote kama ndugu.
2 ) Tushukuru kwa mambo mema katika maisha yetu.
Kauli hiyo, hatuwezi kuithibitisha kuwa ni ya kweli au ya uongo, kwa sababu ukweli wake au uongo wake utategemea mtazamo wa mtu binafsi. Kauli za majaribio ni zile ambazo huwa na ujumbe kuhusu dunia kwa misingi ya tajriba za watu tofautitofauti katika dunia.
Kwa mfano:
1) ‘Mji wa London umo nchini Uingereza.’
2) ‘Dunia huzunguka jua
Jambo lenye uhakika huelezwa kwa kauli hizi na tunaweza kuamua kuwa ni za kweli au za uongo. Kunao
uhakika wa kauli.
Kwa mfano: ‘Jua litachomoza miale yoke kesho.’
Uwezekano uliopo ni kuwa watabiri wa hali ya anga walitabiri kuwa siku itakayofuata kutakuwa na jua. Vilevile, huenda jua likose kuchumuza, kwani Labda hali ya anga yaweza kubadilika. Kwingineko, tunaweza kuwa na jambo ambalo laweza kuhakikishwa.
Kwa mfano: ‘Wanaume wote ni binadamu’. Hii ni kauli ya kweli kabisa kwa sababu jina mwanaume ni la kiumbe ambaye ni binadamu. Hata hivyo hili ni jambo linalojulikana wazi na watu wote kuwa wanaume wote ni binadamu. Tunapaswa kufanya uchunguzi fiilani, ili kuthibitisha baadhi ya kauli.
kwa mfano:
1) ‘Kutanyesha kesho.’
2) ‘Shangazi ni mgonjwa.’
Katika kauli ya kwanza, kipimahewa chaweza kutumika ili kuthibitisha jambo hilo kuwa kutanyesha kesho.
Katika kauli ya pili, shangazi atafanyiwa uchunguzi wa maabara hospital ini ili kuthibitisha ugonjwa wake ni upi. Kabla ya kuthibitisha kauli hizo, kupitia kwa uchunguzi, basi zitakuwa tu ni kauli zenye uwezekano wa
kuwa kweli na baadaye zitathminiwe kuwa ni za kweli au za uongo. Pili, kauli chambuzi ni zile ambazo baada ya kutathminiwa huwa za zingatia kanuni fulani za kimantiki. Kauli hizi hazina ujumbc kuhusu mambo ya ulimwengu na wala haziwezi kuthibitishwa kupitia kwa tajriba ya mtu.
Kwa mfano: ‘Chochote ambacho ni chekundu kina rangi.’ Kauli yenyewe yaeleza kuhusu wekundu, kuwa ishara ya rangi nyekundu kama itatumika basi itabidi kutumia rangi ambayo ni nyekundu kwa kuerejelea kifaa kilekile kimoja.
Kwa mfano: ‘ Taa za trafiki huwa ni rangi nyekundu, rangi ya machungwa na rangi ya kijani kibichi’.
Hivyo basi, katika kuzichora rangi mwafaka zitatumika katika kuwakilisha kila rangi. Vilevile’ katika mfano mwingine:
1) ‘Kuanguka kwa kitu fulani humaanisha kuelekea chini, kama kitu kitaanguka kuelekea juu, basi jambo hilo haliwezekani kamwe, kwani ni jambo ambalo ni kinyume cha kawaida ya mambo.’
2 ) ‘Nina tufaha mbili katika mkono wa kulia na tufaha mbili katika mkono wa kushoto.’
Kauli ya kwanza , ina habari za kisanyansi ambazo zimetafitiwa na kuthibitishwa kuwa kila kitu huanguka kuelekea chini.
Kauli ya pili, yatufahamisha kuwa ninazo tufaha nne, kwani tunafahamu kuwa katika majaribio, mbili kuongeza mbili ni nne.
Tatu, kauli za thamani ni zile ambazo hutumia maneno kwa sababu ya kutathmini au kuependekeza jambo fulani.
Kwa mfano:
1) ‘Ni mtu mzuri.’
2) ‘Haupasrwi kufunya hivyo.’
3) lN i saw a kuwaua wauaji.’
Vigezo vya kutathmini vitategemea uamuzi wa mtu binafsi kuwa kitu ni chenye thamani au la. Uamuzi huu
utategemca vigezo kama mtu ni mwaminifu, mkarimu, mwenye ujasiri, mwenye uwazi katika kusema na kutenda mambo.
Kwa mfano: ‘Maria ni mwanamke mzuri.’ Mtu fulani kumpendekeza Maria kuwa ni mzuri labda vigezo vilivyo hapo juu vilitathminiwa na kuwa vimo katika tabia za Maria. Tunapata mtazamo kuwa yeye ni mwanamke mzuri. Ithibati katika kauli za thamani itategemea tajriba za watu au maarifa kuhusu uhakika wa jambo na
vilevile vigezo vya thamani.
Kwa mfano:  ‘Kuna wale watakaokuwa na vigezo tofauti vya kumtathmini Maria na kwa wao Maria atakuwa mwanamke mbaya.’ Huenda hawakuuona ubora wowote katika tabia za Maria, hivyo kupingana na kauli kuwa Maria ni mzuri. Kwingineko, katika kueleza mifano mingine inayoafikiana na iliyopo hapo juu ni kuwa: ‘Serikaliyetu ni nzuri.’ Kauli hii pia italenga vigezo ambavyo vitatumika kuitathmini serikali yetu, kama vile: ‘Ukarabati wa barabara, elimu ya bure kwa shule za msingi na za upili.’ Vigezo hivi vikitumika, basi tutaipa serikali yetu thamani kwa mtazmo wa kuisifu, na kama vigezo tofauti vitazingatiwa, kama vile: ‘Ufisadi na unyanyasaji wa wafanyikazi,’ tutapata kuwa tunaipa serikali yetu kashfa na kukosa thamani ya kuisifu. Nne. kauli dhanifu ni zile ambazo uthabiti wake utategemea mambo ambayo yatachukulivva kuwa ni ya kufaa. Mambo haya ni yale ambayo hayajakubaliwa lakini yanaweza kujadiliwa kuwa yatakubaiiwa au la. Hueleza mambo ambayo si ya kawaida katika ulimwengu na ambayo ni ya kumiujiza. Kauli nyingi dhanitu hupatikana katika mambo ya kidini. Hata hivyo, kuna kauli dhanifu ambazo hazina uhusiano na mambo ya kidini na hasa zimo katika mambo kamilifu, kama vile: Haki, urembo, na ukweli. Pia, kauli za ubinafsi na hiari.
Kwa mfano: ‘Mungu atawaokoa walio waadilifu.’
Watu watajadili kuwa kauli hii ni sawa au si sawa, ni kweli au ni uongo. Kauli dhanifu inapaswa kukubalika kimaana na kudhibitiwa ili kuwasiliana kuhusu mambo yaliyomo katika ulimwengu wa kawaida na usio wa kawaida.
Kwa mfano: ‘Ni jukumu la mtu binafsi kulichagua alitakalo maishani.’ Kauli hii yaeleza kuwa binadamu ana hiari ya kulichagua jambo alipendalo kulizingatia yeye bila kushurutishwa na mtu yeyote kulifanya asilolitaka. Kwa mfano: ‘Kila mzazi anapaswa kumwelimisha mwanawe.’
Kulingana na kauli hii ni haki ya kila mtoto kupata elimu ambapo kila mzazi anapaswa kugharamia kwa kulipa karo na mahitaji mengine ya kielimu.
Comford (1957: 287- 290) anamnukuu Plato na kusema kuwa kulingana naye, chochote kilicho halisi hakina budi kuwa kweli, kwani si kitu kingine chochote bali ni kitu maalum kilicho halisi, kama vile: ‘Mwendo kama kitu ambacho ni halisi.’ Kauli hii ina maana kuwa mwendo ni kusonga kwa kitu kutoka mahali kilipokuwa na kupiga hatua fulani hadi mahali pengine. Hivyo basi, kwa kuzingatia kauli hii kuhusu mwendo tutatoa mifano kuwa:
1) ‘Mwendo ni kitu ambacho hakipo.’
2) ‘Mwendo ni kitu ambacho kipo.’
Kulingana na kauli hizo, ya kwanza si ya kweli kwa sababu mwendo ni kitu ambacho kipo ilhali kauli ya pili ni kweli kwani yasema kuwa kipo, ni jambo la kweli na hutendeka. Msemaji anatafakari kuhusu kauli ambazo ni za uongo kama zina maana yoyote. Ni vigumu  kwa mtu kuzungumza mambo ambayo hayapo na
ambayo mtu hana uhakika nayo. Hivyo basi, kauli zote ambazo si za kweli hazina
maana yoyote.
Kwa mfano:
1) ‘Chuo Kikuu cha Nairobi kimo mjini Dar es salaam.’
2) ‘”Rais wa Marekuni ni mwanamke.’
Kauli hizo, ni za uongo kwa sababu, kama tunavyofahamu proposisheni tunazozipata kutoka kwa kauli hizi si kweli, kwani katika kauli ya kwanza, Chuo Kikuu cha Nairobi kimo mjini Nairobi nchini Kenya. Dar es salaam ni mji uliopo nchini Tanzania. Kauli ya pili, si ya kweli vilevile kwani Rais wa Marekani anayetawala kwa wakati huu ni mwanamume na wala si mwanamke.
Kauli ambazo ni za kweli huwa na:
1) Jambo ambalo ni la kimsingi katika kauli hiyo.
2) Kitendo kinachoelezwa na kitenzi.
3) Mfumo wote unaohusika na kauli hiyo.
Ni bora basi kuzungumza mambo yaliyohalisi na yaliyopo. Kauli ya kweli na ya uongo, vile vile huwa na kiima na kiarifu chake. Hivyo basi sio kwamba kauli ya uongo haizungumzii chochote hata kama haina maana yoyote, kwani ina kiima chake na kiarifu chake kama vile kauli ya kweli ilivyo. Uamuzi baina ya wanaowasilisha ujumbe na wanaopokea ujumbe ni muhimu kwa sababu wanaweza kuamua kuhakikisha jambo lisilo la kweli likawa la kweli. Watafanya hivyo kwa kusisitiza kuwa ni kweli, ilhali wanajua kuwa ni uongo.
Linsky (1952:15-16) anasema kuwa ukweli katika sentensi wahusu ukubalifu wake katika uhalisi. Sentensi ni ya kweli kama itaweza kuthitibisha hali ya mambo yaliyopo kuwa ni ya kweli.
Kwa mfano: ‘Theluji ni nyeupe’ Tunapaswa kutafakari ni katika masharti yapi ambapo kauli hii ni ya kweli au ni uongo. Proposisheni hii basi ni ya kweli kama theluji ni nyeupe na ni ya uongo kama theluji si nyeupe.
Hata hivyo, tunafahamu wazi kuwa ni kauli ya kweli kwa sababu sote tunajua kuwa theluji ni nyeupe. Ili kupata maelezo mwafaka ya ukweli ni vyema kuhusisha mawazo ya kisemantiki, kama vile; kukidhi mahitaji.
Kwa mfano: ”Nchini mwetu elimu imetiliwa maana na asasi za mambo ya kielimu kuongezeka, ili kukidhi mahitaji ya kielimu.’ Tumeelezwa hapo awali kuwa jukumu la kukidhi mahitaji ni muhimu katika semantiki. Hivyo basi mfano huo, unaeleza kuwa ni mahitaji ya kielimu ambayo hutimiza uchu wa binadamu kwani hutaka kupata elimu zaidi wakati wote. Kauli hiyo, ni ya kweli kwani yaeleza proposisheni kuwa:
1) Elimu ni muhimu nchini mwetu.
2) Asasi za kielimu nchini zimeongezeka.
Vilevile kauli, inakidhi mahitaji ya kielimu ambayo wananchi wengi nchini mwetu wanazidi kuyahitaji.
Kempson (1975: 33-34) anasema kuwa kauli yenye maana katika lugha asili ni kauli yenye masharti ya ukweli katika sentensi za lugha hiyo. Kwa mfano: ‘Mtoto alimkimbilia mamake.’
Kauli hiyo, ina proposisheni kuwa:
1) Aliyckimbiu ni binadamu mwcnyc umri nidogo.
2) Amcfanya kitendo cha kukimbia.
3) Ameelekea kwa mzazi wake ambaye ni wa kike.
Hata hivyo, kauli hii yapaswa kutimiza masharti ili kudai ukweli uliopo katika kauli hiyo. Kauli ambayo inaeleza maana hubainisha kuwa kuna uwezekano wa sentensi hiyo kuwa ya kweli. Katika sinoniminia ambapo sentensi au maneno tofauti yatakuwa na maana sawa, basi masharti yake ya ukweli yatakuwa sawa, kwa hivyo kama sentensi moja ni ya ukweli, vilevile nyingine basi itakuwa ni kweli.
Kwa mfano:
1) ‘Msichana huyu ni mrembo.’
2) ‘Banali huyu ni mrembo. ’
Kauli hizi zina maana sawa kwa sababu msichana pia anaitwa Banati, kauli ya kwanza ni ya kweli, na ya pili vilevile ni ya kweli. Proposisheni zinazotokana na kauli hizi ni za kweli ambazo ni:
1) Kuna msichana ambaye yumo mahali fulani.
2) Msichana mwenyewe ni mrembo.
3) Msichana kwa jina lingine pia huitwa banati.
MAANA KATIKA SENTENSI
Fodor (1977:27-28) anascma kuwa ili kueleza maana ya sentensi ni vyema kuainisha uwezo wake katika ilokusheni na proposisheni zake.
Hali za kauli tofauti huwa za kweli au za uongo. Mtu anapotoa kauli hujihusisha na ukweli uliopo katika proposisheni ili aweze kudai kuwa ni ya kweli. Vilevile, mtu anapofahamu kauli huelewa kuwa mzungumzaji anadai kuwa kitu ni cha kweli na kisha kukifahamu ni kitu kipi anachokidai kuwa ni cha kweli.
Kwa mfano: ‘Kitabu hiki kitakufaa kwa marejeleo.’
                       ‘Sherehe hiyo ilikuwa nzuri sana.’
Proposisheni hizo, ni za kweli kama:
1) Kitabu ni cha marejeleo wala sio cha kuandikia.
2) Kitabu chenyewe kina ujumbe hasa ninaohitaji kurejelea.
3) Sherehe ilikuwepo.
4) Sherehe yenyewe ilinipendeza mimi.
Kama proposisheni zitakuwa hazitimizi mambo haya yanayodaiwa na kauli hizi, basi zitakuwa ni za uongo.
Proposisheni katika sentensi mara nyingi hurejelea masharti ya ukweli katika kauli.
Palmer (1981:196) anasema kuwa chukulizi ya kimsingi katika sentensi au proposisheni huwa ni za kweli au uongo, lakini ukweli au uongo wake hutegemea mtazamo wa mtu binafsi.
Sentensi ya kweli hueleza jambo kinagaubaga kama lilivyo.
 Kwa mfano: ‘John anampenda Mary.’ Kauli hii ni ya kweli ikiwa John anampenda Mary.
Sentensi hii ina proposisheni kuwa :
1) Kuna msichana kwa jina Mary.
2) Kuna mvulana kwa jina John.
3) Mvulana anampenda
Msichana.
Vilevile katika mfano mwingine unaoafikiana na huu ni:
     ‘Barafu huwa baridi.’
Kauli hiyo, ni ya kweli kwa sababu sote tunajua kuwa barafu ni baridi kwa kuigusa na kuhisi kuwa ina baridi.
Kauli hiyo ina proposisheni kuwa:
1) Kuna kitu kwa jina barafu.
2) Barafu yenyewe huwa ni baridi daima.
Proposisheni yapaswa kutimiza masharti fulani ili iwe ya kweli.
Kwa mfano: ‘‘Nguruwe wana mabawa.’ Kauli hii ni ya uongo kwa sababu, sisi sote tunafahamu kuwa nguruwe hawana mabawa. Nguruwe ni aina ya mnyama na kawaida ya wanyama ni kuwa hawana mabawa. Hatahivyo, kuna Popo ambaye tunafahamu kuwa si ndege wala myama kwani ana mabawa hivyo anafanana na ndege ilhali hujifungua wana kama mnyama. Hivyo basi, proposisheni katika kauli hii si ya kweli hasa kama inamrejelea Nguruwe aliyetajwa katika mfano. Kwa kiasi fulani kuna ukweli kuwa nguruwe ni mnyama, lakini kwa upande mwingine kuna uongo kusema kuwa nguruwe wana mabawa kwani hawana.
Kamau, (2008:50-51), anasema kuwa masharti ya ukweli hutegemea muktadha wake katika matumizi.
Mawasiliano hutumika na kueleweka hasa kupitia kwa proposisheni zake. Mtu akitumia lugha bila kuzingatia baadhi ya sheria za lugha hiyo, mawasiliano hayana matatizo.
Kwa vile; matamshi yanapaswa kuwa sawa na mpangilio wa maneno uwe na mantiki. Anaendelea kusema
kuwa kulingana na wanaisimu masharti ya ukweli yanaweza kubainisha uhusiano uliopo baina ya sentensi yoyote ile na proposisheni yenye mantiki.
Kwa mfano:
1) ‘Karanja ni mrefu zaidi ya Kimani.’
2) ‘Kimani ni mrefu zaidi ya Maina.’
Hivyo basi, ni wazi kuwa Karanja ni mrefu zaidi ya Maina kwa sababu Karanja mwenyewe ni mrefu zaidi ya Kimani ambaye pia ni mrefu zaidi ya Maina.
Basi ni kweli kabisa kusema kuwa Karanja ni mrefu zaidi ya Maina. Vilevile, katika mfano mwingine unaoafikiana na huu.
Kwa mfano:
1) ‘Njoki ni mrembo.’
2) ‘Utamuoa Njoki.’
Hivyo basi, ni bayana kuwa Njoki ni mrembo na ndiye utakaye muoa wewe kwa sababu ni msichana ambaye ni mrembo.
Basi ni kweli kusema kuwa msichana mrembo ambaye utamuoa ni Njoki.
Akimajian na wenzake, (2004:243-244) wanasema kuwa kauli katika lugha huwa na maana halisi na hueleza mambo ya kweli au uongo.
kwa mfano: ‘‘Watu wote ambao ni wagonjwa ni watu.’
                    ‘Gari lile lina rangi nyekundu, hivyo basi ni lekundu.’
                    ‘Baadhi ya watu ambao ni wagonjwa si watu.’
                   ‘Gari lile ni lekundu lakini halina rangi.’
Kauli hizo, zina proposisheni za kweli na za uongo.
Kauli ya kwanza na ya pili ni za kweli kwa sababu watu watabaki kuwa watu hata kama ni wagonjwa.
Vilevile, kama gari ni  lekundu basi lina rangi.
Kauli ya tatu na ya nne ni za uongo kwa sababu watu wakiwa wagonjwa hawabadiliki kamwe, bali huwa ni watu daima hata wakipata afueni.
Vivyo hivyo, haiwezekani kuwa gari lekundu halina rangi kwani tayari imeelezwa kuwa gari lenyewe lina rangi nyekundu.
Mahusiano ya kweli huwa na tabia zake ambapo tabia ya kimsingi ni kuwezesha jambo lingine kutendeka.
Sentensi moja husababisha sentensi nyingine kuwa ya kweli ikiwa ukweli wa sentensi ya kwanza umehakikishwa kuwa upo.
Vilevile, sentensi moja husababisha sentensi nyingine kuwa ya uongo kama uongo wa sentensi ya kwanza umehakikishwa kuwa upo.
Kwa mfano:
1) “John ni kapera.’
2) “John hajaoa.’
Proposisheni iliyo katika kauli ya kwanza, yasababisha kuwepo kwa proposisheni katika kauli ya pili. Kapera ina maana ya mwanamume ambaye yumo katika umri wa kuoa lakini hajaoa. Kauli hizi zina proposisheni kuwa:
1) Kuna mtu anayejulikana kwa jina John.
2) John mwenyewe hajaoa.
3) Kutooa kwa John kunamfanya yeye kuwa kapera.
Hivyo basi, proposisheni zilizopo juu ni za kweli kwani kama John ni kapera basi hajaoa. Katika mfano mwingine unao ambatana na huu.
Kwa mfano:
 1) “Sindano nifupi mno.’
2) “Sindano haina urefu wa kutosha.’
Ukweli uliopo katika kauli ya kwanza wahakikisha ukweli kuwepo katika kauli ya pili. Kauli hizi zina proposisheni kuwa kama sindano ni fupi mno ni kweli kuwa haina urefu wa kutosha.
Fasold (2006:142) anasema kuwa maana katika sentcnsi ni proposisheni. Proposisheni ni wazo lililotimia,
ni kauli anibayo yaweza kuwa ya kweli au uongo. Proposisheni ni ya kweli kama kiarifu chake kinaeleza sawasawa kinachorejelewa na kiima. 
Kwa mfano: ‘Catherine Ndereba alikimbia kwa kasi na kushinda mbio hizo.’
Kauli hiyo ina proposisheni kuwa:
1) Runa mwanariadha kwa jina Catherine Ndereba.
2) Mwanariadha mwenyewe alikimbia kwa kasi sana.
3) Mwanariadha huyo alijipatia ushindi katika mbio hizo alizoshiriki.
Mwanariadha kwa jina la Catherine Ndereba arnbaye alikimbia kwa kasi, kisha akawa mshindi katika mbio hizo alizoshiriki, itakuwa ni ya kauli ya kweli kama alishiriki katika mbio hizo na kushinda, ilhali itakuwa ni ya uongo kama hakushiriki kamwe katika mbio hizo.
Masharti ya ukweli ni muhimu kwani huunganisha jambo analojifunza mtu na jambo linalosemwa, kwa sababu nikitoa kauli kama niliyoitaja hapo kumhusu Catherine Ndereba huna budi kuamini kuwa ni mwanariadha na aliwahi kuwa mshindi katika mbio alizoshiriki.
Fretheim (2000:39-40) anasema kuwa kauli hukusudia kumfahamisha msikilizaji ujumbe alio ukusudia msikilizaji na kuwa anao uhakika fulani kuhusu proposisheni itakayofahamika kupitia kwa kauli aliyoitamka. Maelezo tofauti hutumika kurejelea proposisheni moja ambayo huelezwa kwa kauli tofautitofauti.
Kwa mfano:
1) ‘Maria hawezi kumsaidia Piera kupata kazi.’
2) ‘Maria anasema kuwa hawezi kumsaidia Piera kupata kazi.’
3) ‘Maria anaamini kuwa hawezi kumsaidia Piera kupata kazi.’
4) ‘Maria anajuta kuwa hawezi kumsaidia Piera kupata kazi.’
 
Kauli hizo ni za kweli kwani zaeleza hisia za Maria kumhusu Piera. Maria haoni uwezekano wowote kamwe
wa kumsaidia Piera kupata kazi. Kauli hizi zina proposisheni ya Maria kutomsaidia Piera kupata kazi kamwe, ambapo jambo hili limeelezwa kwa njia anuwai. 

MAREJELEO
Abraham, S. (1996). A Theory o f Structural Semantics’. Mouton and Company Publishers.
Akmajian, A. na Wenzake. (2004) Linguistics. An lntrodution to Language and Communication. Fifth
Edition: MIT Press, Cambridge.
Atichi, A.R. (2004) The Semantic Distinctiveness of Kenyan English: UON. Unpublished MA Thesis.
Atoh, F.O. (2001) Semantics Analysis of Dholuo Nowns: The Semantics Field Approach. UON. Unpublished MA Thesis.
Blass, R. (1990) Relevance Relations in Discource. A Study in Special Reference to Sissala: Cambidge University Press.
Brown, G. na Yule, G. (1983) Discource Analysis: Cambridge University Press.
Bussman, H. (1996) Route ledge Dictionary o f Language and Linguistics: International Thompson Publishing Company.
Cambridge (2008) Cambridge Advanced Learners Dictionary. Cambridge University.
Carston, R. (2002) Thoughts and Utterances. The Pragmatics of Explicit Communication. MA: Blackwell Publishers Ltd.
Comford, F. M. (1957) Platos Theory o f Knowledge: Routeledge and Kegan Paul Ltd.
Crystal, D. (2003) A Dictionary o f Linguistics and Phonetics. Fifth Edition. Oxford: Blackwell Publishers.
Falsod, R. W. (2002) An lntrodution to Language and Linguistics. Cambridge University Press.
Fleming, (1998) Google Search. Powered by The Ultimate Programming Weblog. Sillntematinal: 

http:// worldnet Princeton. Edu/Pert/Webwn.
Fodor, J. D. (1997) Semantics: Theories o f Meaning in Generative in Generative Grammar:
Harper and Row , Publishers.
Fretheim, A. (2000) Pragmatic Markers and Propositional Attitude: John Benjamin Publishing Company.
Green, G. M (1996) Pragmatics and Natural Language Understanding. Second Edition: Lawrence Erlbaum Associates Publishers.
Greenbaum, S. na Wenzake. (1985) A comprehensive Grammar o f English Language: Longman Group UK Ltd.
Griffin, E. M (1991) A First look at Communication Theory. Wheaton College: Me Graw- Hill,
Inc. Company.
Hofmann, T. R. (1993) Realms o f Meaning: An Introduction to Semantics: Longman Group UK
Ltd.
Ifantidou, E. (2001) Evidentials and Relevance. Volume 86: John Benjamin Publishing
Company.
Kamau, S. K. (2008) An Analysis o f Truth Conditions in Pragmatics: Relevance Theory
A p p r o a c h . UON. Unpublished MA Thesis.
Kasher, A. (1998) Pragmatics. Critical Concepts. Volume V: Communication, Interaction and Discourse: Routeledge Publishers.
Katie, W. (2001) A Dictionary o f Stylistics: Longman Group UK Ltd.
Katz, J.J. (1977) Propositional Structure and Illocutionary Force. A Study of the contribution of Sentence meaning and Speech Acts: The Harvest Press.
Kempson, R. M. (1975) Pressuposition and The Delimination o f Semantics: Cambridge University Press.
Larson, M. L. (1984) Meaning-Based Translation: A Guide to Cross-Language Eqivalence: University Press of
America, Inc.
Leech, G. (1974) Semantics: Penguin Books Limited.
Leech, G. N. (1971) Towards a Semantic Description o f English: Longman Group Ltd.
Linsky, L. (1952) Semantics and the Philosophy o f Language: University of Illinois Press.
Longmans (1968) Longmans English Larousse: Longmans, Green and Co. Ltd.
Munga, C. M. (2009) Sence Relations in Gikuyu: A Lexical Pragmatics Approach. UON
Unpublished MA Thesis.
Ndug’u, M. N. (2009) Mada na Fokasi katika Kiswahili: Mtazamo wa Muundo wa Taarifa.
UON. Unpublished MA Thesis.
Ogola, C. A. (2006) A Pragmatic Analysis of Intercultural Communication Failures. UON,
Unpublished MA Thesis.
Palmer, F. R. (2006) An Introduction to Language and Linguistics: Cambridge University Press.
Rouchota, V, na Jucker, H. (1998) Current Issues in Relevance Theory: John Benjamin
Publishing Company.
Saeed, J. L. (2003) Semantics. Second Edition: Blackwell Publishing Ltd.
Schroeder, H. (2005) Do we Speak the same Language? A cognitive Pragmatic Explanation of
Cultural Misunderstanding. In Across Borders: Benefiting from Cultural Differences.
Conference Proceedings. 17^-18th March: 2005.
Sperber, D na Wilson,
D. (1995) Communication and Cognition, 2nd Edition: Blackwell Publishers.
Sperber, D na Wilson,
D. (2004) A Handout on Relevance Theory (1985-2002): Blackwell Publishers.
Tuki (1990). Kamusi ya Isimu na Lugha. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Educational Publishers and
Distributors Ltd.
 
Tuki (2006) English-Swahili Dictionary. Third Edition: Book Printing Services Ltd.

Chanzo>>>>>>

Print this item

  DHANA YA NADHARIA
Posted by: MwlMaeda - 07-22-2021, 04:10 PM - Forum: Nadharia mbalimbali - No Replies

Dhana ya Nadharia
Dhana ya nadharia imejadiliwa na wanazuoni mbalimbali ambao wamekuja na mitazamo tofauti tofauti kama ifuatavyo;
Kwa mujibu wa Wamitila, (2003:22) “nadharia ni mawazo, dhana au maelezo yanayotolewa kuelezea hali fulani : chanzo chake, muundo wake, utenda kazi wake na mwingiliano wake wa ndani na nje”
TUKI (2004:300) wanasema “nadharia ni mawazo, maelezo au mwongozo uliopangwa ili kusaidia kueleza, kutatua au kutekeleza jambo fulani”
Fasili hii ya TUKI inafanana kwa kiasi fulani na fasili ya Mdee (2011) anayefasili nadharia kuwa ni mpango wa maneno uliotungwa ili kuelekeza jinsi ya kufanya au kutekeleza  jambo fulani. http://kapeleh.blogspot.com/2014/05/nadh...maana.html
Kwa msingi huo nadharia hubeba mawazo, dhana au maelezo yatolewayo kwa nia au lengo la kueleza hali fulani, chanzo, muundo, utendaji na mwingiliano wa ndani na nje.
Kuna nadharia mbalimbali ambazo zimejadiliwa na wanazuoni mbalimbali, baadhi ya nadharia hizo ni pamoja na nadharia ya maana, nadharia za kifalsafa, kihistoria, nadharia ya fasihi, nadharia za chimbuko la lugha ya Kiswahili, nadharia ya chimbuko na chanzo cha lugha.
Naye Wafula  na Njogu (2007:7) wamefasili dhana ya nadharia kama ni jumla ya maelekezo yanayomsaidia msomaji au mhakiki kuifahamu kazi ya fasihi kwa kufuata utaratibu maalumu. Fasili hii imeegemea hasa katika nadharia ya uhakiki wa fasihi. Pia imetaja vitu muhimu kama vile, maelekezo ambayo ndiyo yanamuongoza msomaji au mhakiki ili asivuke mipaka ya mawazo ya hiyo nadharia aitumiayo ili kufanikisha kazi kwa ufasaha.
Pia Sengo (2009:1) anafasili nadharia kuwa ni wazo kuu, fikra kuu, mwongozo mkuu wa mtu, watu au jamii ya pahala fulani, wakati fulani na kwa sababu fulani. Kwa mantiki hiyo nadharia ni dira au mwongozo wa kulikabili jambo kifalsafa, kidini, kimantiki, kijamii na kiutamaduni.
Ili kuweza kuthibitisha maelezo yaliyotolewa na wataalamu mbalimbali kuhusu dhana ya nadharia ni vyema kuangalia mfano mmojawapo wa nadharia, ambayo ni nadharia ya sarufi. Katika nadharia hii kuna wanaisimu mbalimbali wamejitokeza kuelezea nadharia ya sarufi kwa mitazamo tofauti tofauti ambayo imeweza kuibua nadharia mbalimbali za sarufi kama vile nadharia ya sarufi mapokeo, nadharia ya sarufi msonge na nadharia ya miundo virai.
Katika nadharia ya sarufi mapokeo Mgullu (1999:68) anasema ni sarufi ya kale iliyochambuliwa kwa kutumia vigezo vya lugha za Kilatini na Kigiriki zilizokuwa na mnasaba mmoja, yaani zilikuwa na asili moja. Kwa mantiki hiyo lugha za Kilatini na Kigiriki zilikuwa kama kiolezi cha kuchanganulia lugha nyingine ikiwemo lugha ya Kiswahili. Kwa mfano wanaisimu wa Kilatini waliposema kuna aina nane za maneno na baadhi yao katika lugha ya Kiswahili wakasema kuna aina nane za maneno bila kuzingatia kwamba lugha hutofautiana. Pia nadharia hii ilijikita na sentensi sahili, haikujishughulisha na miundo  kwa marefu na mapana.
Baada ya kuonekana sarufi mapokeo ina udhaifu mkubwa iliibuka nadharia ya sarufi msonge. Mgullu (1999:70) anaiona sarufi hii ni sehemu ya mkabala wa kimapokeo isipokuwa mkabala huu unaiona lugha kuwa ni mfumo mkuu yenye mifumo mingi ndani yake kama vile mifumo midogo ya fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki.
Katika karne ya kumi na nane na kumi na tisa sarufi mapokeo ikafikia kilele ndipo ikaibuka nadharia ya sarufi miundo virai. Nadharia hii inadokeza kuwa tungo imeundwa na viambajengo ambavyo vina uhusiano na vipo kidarajia. Kwa mujibu wa Mgullu (1999:70) isimu muundo imejitokeza sana katika maandishi ya akina Harris, Ferdinand De Saussure, Trubetzkoy na Bloomfield.
Katika mkabala huu lugha ilionekana kuwa na viambajengo kama vile: maneno, kirai, kishazi na sentensi na kwamba viambajengo hivyo vina uhusiano mkubwa na viko katika kidarajia toka chini hadi juu. Kwa mfano
Mkulima bora analima vizuri
Katika sentensi hii kuna uhusiano wa karibu wa viambajengo vifuatavyo; N+V yaani nomino “mkulima” na kivumishi “bora”, hali kadhalika, T+E, yaani kitenzi “analima” na kielezi “vizuri”.
Katika mkabala huu dhana ya uchamko ikaibuka kuonyesha uwezekano wa kuzalisha sentensi bila kufika kikomo. Kwa mfano,
Waziri fisadi amekamatwa jana na rais akiiba fedha za wananchi.
Hivyo ili kuwa na nadharia inayokubalika katika jamii ni muhimu kuzingatia fasili ya Sengo, (2009:1) ambaye anasema kuwa “nadharia ni wazo kuu, fikra kuu, mwongozo mkuu wa mtu, watu au jamii ya pahala fulani, wakati fulani na kwa sababu fulani”.
Kwa mantiki hiyo nadharia ni dira au mwongozo wa kulikabili jambo kifalsafa, kidini, kimantiki, kijamii na kiutamaduni.
Kwa ujumla nadharia huchukuliwa kuwa ni dira ya kumwongoza mtafiti au mchambuzi kulikabili na kulielezea vyema jambo fulani kwa mtazamo unaotazamiwa kuwa imara zaidi kuliko ule wa nadharia nyingine. Nadharia hutoa mwongozo katika utatuzi wa jambo fulani ambalo halijaweza kuhakikishwa ukweli wake. Ni mawazo , maelezo au mwongozo uliopangwa ili kusaidia kutatua au kutekeleza jambo fulani kifalsafa, kidini, kimantiki, kijamii na kiutamaduni.
MAREJEO
http://nenothabiti.blogspot.com/p/fasihi.html by Anonymmous Said, 31 October 2013 at 9:39AM
Sengo, T.S.Y.M (2009) Fasihi za Kinchi. Dar es Salaam: The Trustees of Al Amin Education and Research Academy
TUKI (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es salaam: TUKI
Wamitila, K.W (2003) Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi. Nairobi: Kenya Focus   Publications Ltd
Wafula, R.M & Njogu, K (2007) Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation

Print this item