MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 72 online users.
» 0 Member(s) | 71 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  KISWAHILI KAMA CHOMBO CHA KUTANGAZA NA KUUZA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KENYA
Posted by: MwlMaeda - 07-28-2021, 08:04 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

KISWAHILI KAMA CHOMBO CHA KUTANGAZA NA KUUZA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KENYA

Mark A. Odawo na Jacktone O. Onyango
Ikisiri
Makala1 hii inatathmini ufaafu wa matumizi ya maneno ya Kiswahili kama anwani ya vituo vya redio vilivyochipuka katika miaka ya hivi karibuni nchini Kenya. Makala inaangalia jinsi ambavyo hali hii inaweza kuchangia uimarishaji wa lugha ya Kiswahili kwa jumla. Tangu azali na hata enzi ya ukoloni, lugha ya Kiswahili imekuwa zana muhimu ya mawasiliano timilifu sio tu katika ukanda wa Afrika Mashariki bali pia kwa umma mkubwa wa kimataifa. Matumizi ya Kiswahili katika shughuli mbalimbali za binadamu yamekuwa mhimili muhimu wa kukuza na kueneza lugha hii (Tuli, 1985). Katika kizazi cha kisasaleo, harakati za kiuchumi zimejifaragua kutoka biashara ya bidhaa na kujumuisha huduma mbalimbali ikiwemo habari. Kama huduma, habari imekuwa nguzo muhimu ya ufanisi. Dhima ya habari katika maendeleo ya dunia ya kisasaleo imeifanya kuwa huduma ambayo wateja wake wanaongezeka kila uchao. Hii ni hali mojawapo iliyochangia kuchipuka kwa vituo vingi vya redio vinavyoitwa vya Kiswahili ambavyo hutoa matangazo yao kwa Kiswahili. Makala hii inajikita katika kuangalia ufaafu na uamilifu wa majina au anwani na kaulimbiu zenye maneno ya Kiswahili kwa vituo vya redio vilivyoanzishwa na vyombo vya habari katika miaka ya hivi karibuni. Makala inaangalia matumizi ya maneno haya ya Kiswahili kutajia vituo vya redio sawa na mikakati ya kutoa mshawasha kwa wasikilizaji kuonea fahari vituo hivi na kuwateka ili waendelee kuvisikiliza. Kwa namna hii, lugha ya Kiswahili hujitokeza kuwa na uwezo wa kutanguliza, kutambulisha, kutangaza na kuuza vituo hivi kwa umma mkubwa wa wasikilizaji. Kadri wasikilizaji wanavyoendelea kusikiliza na kuchangia mijadala katika vituo hivi ndivyo vituo hivi vinavyoendelea kukubalika kuwa maarufu miongoni mwa wasikilizaji. Vivyo hivyo ndivyo lugha ya Kiswahili inavyoendelea kuimarika, kupanuka na kuenezwa na hivyo kuakisi mustakabali bora wa lugha ya Kiswahili.
1 Makala hii iliwasilishwa kwa mara ya kwanza katika Kongamano la Kiswahili la CHAKITA lililofanyika katika Taasisi ya Maendeleo ya Mtaala wa Elimu (KICD), Nairobi, Oktoba 23-24, 2014.
1.0 Utangulizi
Ijapokuwa kuna nadharia tofauti kuhusu chimbuko na kuenea kwa Kiswahili, wataalam wengi wakiwamo Chiraghdin na Mnyampala (1977) na Chacha (1995) wanaafikiana kuwa lugha hii ina kitovu chake pwani na kuwa ilienea kutoka upwa wa bahari ya Hindi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki. Sengo (1995) anadai kuwa Kiswahili ni kizalia cha lugha asili za Waafrika hususan wakazi wa mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki kabla ya majilio ya wageni. Kwa mujibu wa Whiteley (1969), Chiraghdin na Mnyampala (1977), Mbaabu (1985, 1991a) na Ogechi (2002), miongoni mwa zana muhimu za kuenea huku kwa lugha tangu awali ni utawala wa kikoloni, siasa, elimu, biashara, ndoa, machapisho na vyombo vya habari ambavyo mchango wake umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni kutokana na uwezo wake wa kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja.
Zana hizi zinajitokeza kama sehemu muhimu ya shughuli za binadamu ambazo zimesawiri Kiswahili kama chombo muhimu cha mawasiliano timilifu sio tu katika ukanda wa Afrika Mashariki bali pia kwa umma mkubwa wa kimataifa (Tuli, 1985). Kwa kufanya hivi, lugha hii imefanikisha si mahitaji ya watu binafsi tu bali pia malengo ya makundi na taasisi anuwai. Onyango (2014) anasema kuwa lugha ya Kiswahili inatumiwa kuleta maendeleo ya uchumi nchini Kenya kwa kufanikisha mawasiliano ya kibiashara katika sekta mbalimbali ikiwamo sekta ya huduma za benki. Matumizi ya Kiswahili katika shughuli hizi yamekuwa mhimili muhimu wa makuzi, malezi na maenezi ya lugha hii.
Katika kizazi cha kisasaleo, harakati za kiuchumi zimejifaragua kutoka biashara ya bidhaa na kujumuisha huduma mbalimbali ikiwamo habari. Kama huduma ya habari imekuwa nguzo muhimu ya ufanisi, habari za shughuli za kijamii kama vile sanaa na burudani na zile za kiuchumi kama vile kazi, biashara na uzalishaji huwafikia walengwa wengi kwa haraka zaidi kupitia vyombo vya habari. Hivi ni kusema kuwa dhima ya habari katika maendeleo ya dunia ya kisasaleo imeifanya kuwa huduma ambayo wateja wake wanaongezeka kila uchao.
Hii ni hali mojawapo iliyochangia kuchipuka kwa vituo vingi vya redio vinavyoitwa vya Kiswahili na pia kutangaza kwa lugha ya Kiswahili katika miaka ya hivi karibuni nchini Kenya, hasa baada ya masharti ya utoaji wa leseni ya masafa ya utangazaji kulegezwa mwaka 1999. Maswali tunayojiuliza katika makala hii ni: Je, majina haya ya vituo vya redio yanayosheheni istilahi za Kiswahili yanaathiri vipi usikilizaji wa vituo hivi? Kiswahili kinachotumika kufikisha habari kwa walengwa ni cha kiwango gani? Nini hatima na mustakabali wa lugha ya Kiswahili katika mchakato huu wote? Ni katika kujibu maswali haya ndipo makala hii inatathmini ufaafu wa matumizi ya maneno ya Kiswahili kama anwani na kaulimbiu ya vituo vya redio vilivyochipuka kati ya mwaka 1999 na 2014 na jinsi ambavyo hali hii inaweza kuchangia uimarishaji wa lugha ya Kiswahili kwa jumla. Makala inaangalia matumizi ya maneno ya Kiswahili kutajia vituo vya redio sawa na mikakati ya kutoa mshawasha kwa wasikilizaji kuonea fahari vituo hivi na kuwateka ili waendelee kuvisikiliza. Data za makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya kusikiliza vituo vya redio, mahojiano na wasikilizaji na watangazaji wa vituo vya redio na pia mtandaoni. Makala imegawanywa katika sehemu sita zinazofuatana kama ifuatavyo: utangulizi, vituo vya redio vyenye anwani za Kiswahili, kaulimbiu za vituo vya redio, matumizi ya lugha katika vituo vya redio, mapendekezo na hitimisho.
2.0 Vituo vya Redio vyenye Anwani za Kiswahili
Kufikia mwaka 1999, vituo vya redio nchini Kenya vilikuwa 10 pekee. Mwaka 2004 idadi hiyo iliongezeka na kufikia 118 (BuzzKenya.com; Communications Authority of Kenya, 2014). Idadi kubwa ya vituo hivi imeongezeka kuanzia mwaka 2000 wakati sekta ya habari na utangazaji ilipowekwa huru kutokana na masharti ya utoaji wa masafa ya kutangazia kulegezwa na hivyo kuwaruhusu wamiliki binafsi kuanzisha vituo vya redio.
Mbali na kutoa matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili, baadhi ya vituo hivi hutoa matangazo yao kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyingine za kiasili. Kati ya vituo 118, vituo 30 vinatumia Kiswahili kama sehemu za anwani za vituo hivyo. Mbinu ya usampulishaji lengwa imetumiwa kuviteua vituo hivyo 30 ambavyo vimetumiwa katika uchanganuzi na maelezo. Vituo hivi ni Redio Maisha (Nairobi), Redio Jambo (Nairobi), Baraka FM (Nairobi), Redio Salaam (Mombasa), Sauti ya Mwananchi FM (Nakuru), Rehema FM (Nairobi), Redio Pamoja (Nairobi), Bahari FM (Mombasa), Jambo FM (Nairobi), Amani FM (Nakuru), Sifa FM (Voi), Redio Umoja (Nairobi), Redio Kisima (Nyamira), Biblia Husema Redio (Nairobi), Injili FM (Kericho), Mambo FM (Nairobi), Pwani FM (Mombasa), Imani FM (Kitale), Sauti ya Rehema Redio (Sayare Radio) (Eldoret), Milele FM (Nairobi), Pilipili FM (Mombasa), Sema Redio (Kericho), Redio Simba (Kampala, Uganda), Redio Waumini (Kasarani, Nairobi), Risala FM (Garissa), Bahasha FM (Nakuru), Hosana FM (Nairobi), Mwangaza FM (Dodoma, Tanzania), Neema FM (Mwanza, Tanzania), na Rock Mambo FM (Tororo, Uganda). Baadhi ya vituo vya redio vya Tanzania na Uganda vimejumuishwa katika makala hii kwa sababu matangazo yake hufika pia Kenya.
Mifano michache ifuatayo inaonyesha jinsi majina haya ya Kiswahili yanayotumiwa kutajia vituo vya redio yanavyoafiki na kuathiri usikilizaji wa vituo hivi.
i) Redio Jambo
Katika kujinasibisha na wasikilizaji, inazingatiwa kuwa msikilizaji yeyote aliye na jambo linalomkera aliwasilishe katika kituo hiki ili litatuliwe. Kituo hiki huwa na kipindi maarufu kinachoitwa ‘Patanisho’ ambapo wasikilizaji walio na jambo linalotatiza mahusiano yao na wengine wanaruhusiwa kupiga simu ili waweze kupatanishwa kutokana na rai au nasaha za watangazaji pamoja na ushauri wa wasikilizaji wengine wanaoruhusiwa kutoa maoni yao kwa kupiga simu moja kwa moja au kutuma ujumbe mfupi kwa nambari ambayo hutolewa. Aidha, wasikilizaji wanahusishwa katika mijadala ya masuala yanayojiri na kuathiri maisha ya kawaida ya wananchi. Hivyo basi, kituo hiki kimeweza kushawishi wananchi kuwa na ujuzi wa mambo mbalimbali yanayohusu sanaa, michezo, mapenzi na siasa kutegemea usikilizaji wa kituo hiki. Yamkini dhana kama hii inaweza kuhusishwa na vituo kama vile Jambo FM, Mambo FM na Rock Mambo FM.
ii) Redio Maisha
Kituo hiki hujaribu kujitambulisha na masuala yanayowakumba wasikilizaji wake katika maisha yao ya kila siku. Kwamba yeyote anayetaka kujua mambo muhimu yanayohusu maisha ya kisasa hana budi kusikiliza kituo hiki. Katika utangazaji wake, kituo hiki kinaangalia maisha kuwa ‘matamu’ na kwamba mada zote zinazofanya maisha kuwa ‘matamu’ kama vile mapenzi, sanaa na michezo hutokana na kusikiliza kituo hiki. Kwa hiyo, wasikilizaji wanakiona kama kitovu cha maisha.
iii) Milele FM
Kituo hiki hulenga kuwapasha habari na kuwaburudisha wasikilizaji wake wakati wote au ‘milele’ kama ambavyo jina lake linavyoonesha. Kituo hiki ni maarufu kwa nyimbo za dini ya Kikristo na kilishinda tuzo ya kituo kinachocheza muziki mzuri zaidi wa kidini nchini Kenya kwa miaka mitatu iliyopita. Mtangazaji aliyetambuliwa kuwa bora zaidi ni Eva Mwalili (Groove Awards, 2014). Hivi ni kusema kuwa kituo hiki kinawahakikishia wasikilizaji wake ‘uzima wa milele’.
iv) Redio Waumini
Kituo hiki kinajihusisha na matangazo, mijadala na uchezaji wa muziki wenye mada za dini ya Kikristo. Hivi ni kusema kuwa waumini wote wanaweza kutoshelezwa haja zao za kiroho wanaposikiliza kituo hiki. Hivyo basi, kituo hiki kinajitokeza kama chombo cha kuwabadilisha watu ili wawe waumini wa dini ya Kikristo. Hii ndiyo hali ambayo aghalabu hujitokeza katika vituo kama vile Baraka FM, Injili FM, Imani FM, Rehema FM, Sauti ya Rehema Redio (Sayare Radio), Hosana FM, Biblia Husema Redio na Neema FM vinavyolenga kutambulishwa kwa waumini kama vituo vinavyohusishwa na mada za kidini.
v) Sauti ya Mwananchi FM
Kituo hiki kinajitokeza kama mtetezi wa mwananchi kwa kuangazia changamoto zinazowakumba. Kinajaribu kuwapa wananchi muda wa kutosha kutoa kauli zao kuhusu masuala yanayowahusu na kuwaathiri moja kwa moja. Maoni ya wananchi yanapewa umuhimu mkubwa na watangazaji wa kituo hiki. Hali inayojitokeza hapa ni kuwa kituo hiki kinajitokeza kama mtetezi wa wasikilizaji (Mahojiano yetu na Wasikilizaji wa Kituo hicho, tarehe10 Oktoba, 2014, Nakuru).
vi) Redio Umoja
Kituo hiki hujinasibisha na kuleta umoja, mshikamano na mtagusano miongoni mwa wasikilizaji wake licha ya maoni ya wasikilizaji hao kutofautiana wakati mwingine. Kwa hiyo, kituo hiki hujaribu kujenga fikra za maafikiano na utangamano miongoni mwa wasikilizaji pamoja na watangazaji wa kituo hiki. Kinawasawiri wasikilizaji kama wamoja. Kituo hiki kinaonekana kuwa na mkabala ulio sawa na kituo cha Redio Pamoja. Kuna madai kwamba baadhi ya idhaa za redio na wanahabari walichangia katika ghasia zilizofuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007/2008 nchini Kenya maarufu kama PEV (Post Election Violence). Inawezekana kwamba kuanzishwa kwa baadhi ya vituo hivi vya redio ni juhudi za wawekezaji kupata faida na pia kuondoa utengano uliopandwa wakati wa ghasia hizo. Kwa hivyo, hizi ni juhudi za kuleta uwiano na utangamano miongoni mwa Wakenya.
vii) Pwani FM
Kituo hiki kimsingi kinatoa matangazo yake kutoka maeneo ya pwani, ingawa pia, kinaangazia pia masuala yanayosheheni taifa zima. Hata hivyo, kituo hiki huelekea kuonekana ‘miliki’ ya wenyeji wa mwambao wa pwani, hasa maeneo ya Mombasa, Kwale na Malindi, ambao ndio hujihusisha nacho zaidi. Hivi ni kusema kuwa wasikilizaji wake wanakionea fahari kubwa kama ilivyo kituo cha Bahari FM.
viii) Redio Kisima
Kama kisima kinachotoa maji safi kwa matumizi ya binadamu, kituo hiki huwa kama kitovu cha habari zote muhimu anazohitaji msikilizaji kuhusu nyanja zote za maisha. Kituo hiki wakati mwingine huangazia masuala nyeti na mada nzito zinazoamsha hisia na kuwakanganya wasikilizaji kwa nia ya kupata suluhu inayokubalika kwa wote. Mada hizo ni pamoja na ndoa, mapenzi, malezi, lishe na imani. Hii ni kwa sababu kituo hiki kina msingi wake katika dini ya Kiadventista.
ix) Sema Redio
Kituo hiki huonekana kutilia mkazo utoaji wa nafasi kwa wasikilizaji wake kusema jambo lolote na kutoa maoni waliyonayo kuhusiana na matukio ya kila siku katika jamii. Mbali na kusemezana wao kwa wao, wasikilizaji husemezana na kujadiliana na watangazaji wa kituo hiki. Hivyo basi, kituo hiki kinaonekana kuthamini maoni na hoja za wasikilizaji wake kuhusu masuala tofauti yanayowashughulisha.
3.0 Kaulimbiu za Vituo vya Redio
Baadhi ya vituo vya redio vinavyotumia Kiswahili kama anwani yake pia huwa na kaulimbiu zilizoandikwa kwa lugha hii. Japo baadhi ya vituo vya redio havina majina ya Kiswahili, vimeshehenezwa na kaulimbiu zinazohusisha lugha ya Kiswahili. Hapa inabidi tuvuke mipaka ya redio 30 zilizotajwa katika sehemu ya 2.0 na kutaja mifano ya redio tatu ambazo hutangaza kwa Kiswahili kote nchini na hutumia kaulimbiu za Kiswahili ili kuonyesha jinsi zinavyoathiri usikilizaji. Redio nyingi kati ya zile 30 zilizotajwa hazitangazi kote nchini. Ifuatayo ni baadhi ya mifano na jinsi inavyoathiri usikilizaji wa vituo vya redio husika.
i) KBC Kiswahili – Redio Taifa
Kituo hiki kinalenga kutoa habari muhimu zinazogusia masuala ya kitaifa. Hivi ni kusema kuwa kituo hiki kilianzishwa kwa ajili ya taifa zima na kuwa wasikilizaji wote wanaweza kukitumia kutoa sauti au maoni yao kuhusu taifa. Kwa namna hii kituo hiki kinahimiza wasikilizaji kukionea fahari na hivyo kuendeleza fikra za utaifa na uzalendo miongoni mwa wasikilizaji kutokana na kuwashirikisha katika shughuli zinazojenga utangamano.
ii) Redio Citizen – Chemchemi ya Ukweli
Jina la kituo hiki inakieleza kuwa kama chanzo na mbubujiko usio na mwisho wa habari za kina na hakika kuhusu nyanja zote za maisha. Ni kana kwamba kituo hiki ndicho kinachopaswa kuaminika kwa usahihi wa habari kwani huenda vingine vimepungukiwa uwezo huo au vinaweza kupotosha ujumbe.
iii) Redio Maisha – Tuko Mbele Pamoja
Tamko hili hujaribu kusisitiza umoja na utangamano kati ya watangazaji na wasikilizaji. Ujumbe unaofikishwa hapa ni kuwa umoja na ushirikiano ndio nguzo ya ufanisi. Kwamba kadri kituo hiki kinavyoendelea kujiimarisha ndivyo wasikilizaji pia watakavyoweza kuendelea na kwamba kituo hiki huweza kufifia iwapo wasikilizaji hawapo. Kwa hiyo, kituo hiki kinajaribu kujihusisha na kujinasibisha na wasikilizaji kama vipande visivyoweza kutenganishwa.
iv) Q FM – Kata Kiu
Q FM (Kiu FM) ni kituo kinachojifananisha na kinywaji baridi kinachoweza kunywewa ili kukata kiu ya mnywaji. Hali ya wasikilizaji kutopata habari za kina inaangaliwa sawa na kuwa na kiu. Hivyo basi, yeyote anayetaka kupata taarifa za kweli na burudani za kutosha hana budi kusikiliza matangazo kutoka katika kituo hiki ili ‘kukata kiu’ yake. Dhana kuu inayotokana na kaulimbiu hii kimsingi huelekea kuoana na ile ya kituo cha Redio Kisima inayojulikana kama ‘Chota unywe’.
v) Milele FM – Wewe ni Wetu
Ujumbe ulio katika kaulimbiu hii ni ule unaomthamini msikilizaji kama sehemu muhimu ya kituo hiki. Dhana inayojitokeza hapa ni hali ya umoja, mshikamano na utambulisho wa kituo hiki na wasikilizaji wake. Hivi ni kusema kuwa maoni au mchango wa wasikilizaji wa kituo hiki ndiyo yanayojenga msingi wa matangazo ya kituo hiki.
Dhana zinazobainika katika anwani za vituo hivi vya redio na kaulimbiu zake zinaviafiki kwa kuwashawishi wasikilizaji kuendelea kuvisikiliza, kuvionea fahari na kujinasibisha navyo. Kwa njia hii, anwani na kaulimbiu hizi hujitokeza kama mbinu muhimu za kutambulisha na kutangaza vituo hivi kwa wasikilizaji wake.
Marejeleo
Ahmed, S. (2013). “Tungo za Kinahau Zinazotoa Taarifa ya Mpira wa Miguu katika Magazeti ya Kiswahili”, Mulika. Dar es Salaam: Taasisi ya Taaluma za Kiswahili.
BuzzKenya.com <http://buzzkenya.com/Redio-stations-in-kenya/ 25 Septemba 2016>
Chacha, L. M. (1995). “Chimbuko la Kiswahili”, katika BARAGUMU, Juzuu la 2 Nam. 1&2 kur. 1-7.
Chiraghdin, S. na Mnyampala, M. (1977). Historia ya Kiswahili. Nairobi: Oxford University Press.
Communications Authority of Kenya, June 2014. <http://www.ca.go.ke/ 25 Septemba 2016>
Groove Awards, 2014. <www.grooveawards.co.ke 25 Septemba 2016>
King’ei, K. (2000), “Matatizo ya Matumizi ya Lugha katika Vyombo vya Habari: Mifano kutoka Kenya” katika Swahili Forum VII. 45-56.
King’ei, K. na Musau, P. (2000). Utata wa Kiswahili Sanifu. Nairobi: Didaxis.
Marshad, H. (1993). Kiswahili au Kiingereza nchini Kenya? Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
Mbaabu, I. (1985). New Horizons in Kiswahili. Nairobi: Kenya Literature Bureau.
Mbaabu, I. (1991a). Historia ya Usanifishaji wa Kiswahili. Nairobi: Longman Kenya Ltd.
Mbaabu, I. (1991b). “The Impact of Language Policy on the Development of Kiswahili in Kenya, 1930-1990.” Ph.D Thesis, Howard University.
Mbaabu, I. (1995). Usahihishaji Makosa katika Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers.
Mlacha, S.A.K. (mh) (1995). Kiswahili na Vyombo vya Habari. Dar-es-Salaam: TUKI.
Momanyi, C. (2001). “Matumizi ya Kiswahili katika Njia Panda: Mtazamo wa Kiisimu-Jamii,” katika Kiswahili: A Tool for Development – The Multidisciplinary Approach. Eldoret: Moi University Press.
Momanyi, C. (2009). “The Effect of ‘Sheng’ in the Teaching of Kiswahili in Kenyan Schools,” katika Journal of Pan African Studies, 2(8): 127-138.
Musau, P. M. (2001). “Freeing the Airwaves or Cultural Enslavement: The Case of Media in Kenya,” katika Kiswahili: A Tool for Development – The Multidisciplinary Approach. Eldoret: Moi University Press. Pp. 36-42.
Ogechi, N. O. (2002). Mbinu za Mawasiliano kwa Kiswahili. Nairobi: Moi University Press.
Onyango, J.O. (2002). AKS 102: Historical Development of Kiswahili. (Bachelors Module). Institute of Open Learning, Kenyatta University.
Onyango, J. O. (2014). “Kiswahili kama Lugha ya Mawasiliano katika Shughuli za Benki: Changamoto za Tafsiri”. Katika Simala, I., Chacha, L. na Osore, M. (wahr). Miaka Hamsini ya Kiswahili Nchini Kenya. Nairobi: Twaweza Communications. 107-112.
Sengo, T. S. Y. (1995). “Hali ya Kutatanisha ya Kiswahili hivi leo Afrika ya Mashariki”, Makala yaliyotolewa katika Kongamano la Nane la Kiswahili, Chuo Kikuu cha Bayreuth, Mei 26-27, 1995.
Tuli, R. S. K. (1985). Chimbuko la Kiswahili, Kukua na Kuenea kwake Afrika Mashariki. Arusha: Utalii Exporters and Publications.
Waihiga, G. (1999). Sarufi Fafanuzi ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers.
Whitely, W. H. (1969). Kiswahili: The Rise of a National Language. London: Methuen.

Print this item

  SIFA ZA LUGHA YA TAIFA NA LUGHA RASMI
Posted by: MwlMaeda - 07-28-2021, 07:55 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

Lugha ya taifa ni lugha au lahaja iliyoteuliwa miongoni mwa lahaja nyingi zilizopo katika jamiilugha fulani iliyopo katika eneo fulani ili itumike katika mawasiliano ya jamii hiyo. Mara nyingi lugha ya Taifa huteuliwa ili kukidhi haja ya mawasiliano miongoni mwa jamii.

Lugha ya Taifa inakuwa kama nembo ya Taifa husika, hii inachangiwa na suala la lugha ya Taifa kuwa kama kitambulisho cha Taifa husika, kwa mfano, lugha ya Kiswahili nchini Tanzania inakuwa kama nembo ya Taifa, kwa sababu ni sehemu ya utamaduni yaani mila na desturi za Watanzania.
Dhana ya lugha ya Taifa imetumika kiutofauti katika mataifa tofauti tofauti. Kwa kawaida lugha ya Taifa ni lugha kuu, yaani lugha inayotumika katika shughuli za kimahakama, kisiasa, katika ngazi ya Taifa, kwa mfano, nchini Uingereza lugha kuu ni kiingereza lakini ki-welsh kina nafasi yake haswa katika eneo la Wales.
Lugha rasmi ni lugha iliyopewa hadhi maalumu katika nchi fulani, kwa kawaida lugha rasmi ni lugha inayotumiwa haswa na serikali kwa mawasiliano kati ya ofisi zake pia katika matangazo rasmi. Vile vile lugha rasmi ni lugha iliyopewa hadhi maalumu katika eneo fulani au nchi fulani ili itumike katika mazingira maalumu. Mara nyingi lugha rasmi katika Taifa huteuliwa ili itumike kwenye mahakama, bungeni na kwenye shughuli nyinginezo za kiutawala. Lugha inaweza kupewa hadhi maalumu na kuwa lugha rasmi ijapokuwa lugha hiyo haijasambaa eneo kubwa, pia inaweza isiwe na wazungumzaji wengi, kwa mfano, nchini New Zealand Kimaori kiliteuliwa kuwa lugha rasmi mwaka 1987 ijapokuwa lugha hii inazungmzwa na watu wachache.
Katika nchi mbalimbali lugha rasmi imetajwa katika katiba ya Taifa au katika sheria mahususi lakini nchi nyingine hazina sheria juu ya lugha rasmi hata kama hali halisi ipo, kwa mfano, nchini Namibia Kiingereza ni lugha rasmi kufuatana na katiba lakini lugha nyingine pamoja na Kiafrikana na Kijerumani zimetajwa kama lugha za kitaifa zinazoweza kutumiwa pia kama lugha ya mafundisho shuleni.
Zifuatazo ni baadhi ya sifa za jumla za lugha ya Taifa na lugha rasmi:-
Sifa za lugha ya Taifa
– Ni lugha iliyokubalika na wengi katika nchi na inaeleweka na watu wote (wasomi na wasiosoma)
– Ni kiwakilishi cha Taifa katika mawasiliano nje na ndani ya Taifa hilo na pia kitambulisho cha Taifa lenyewe.
– Hutumika kwa namna moja katika makabila mbalimbali ya nchi husika.
– Lugha hiyo ni muhimu iweze kuandikwa katika vitabu na magazeti na iwe inakubalika kutumika katika elimu na fani zingine zisizo za kitaaluma.
– Ni muhimu lugha hiyo iwe ni sehemu ya utamaduni wa nchi husika.
Sifa za lugha rasmi
– Lugha hiyo lazima iwe sanifu.
– Inaweza kuwa lugha ya Taifa au la.
– Haifuati kabila au mchanganyiko wa makabila yaliyopo nchini
-Yaweza kuwa lugha ya kigeni kama vile Kiingereza, Kijerumani au Kifaransa, kuchaguliwa au kuteuliwa kwa lugha hiyo hutegemea utawala uliopo.
Zifuatazo ni tofauti zilizopo kati ya Lugha ya Taifa na Lugha rasmi:
Kigezo cha uwanda wa matumizi, Lugha ya Taifa ina uwanda mpana wa matumizi kwani inatumika nchi nzima bila kujali inatumika wapi au eneo gani na nani anayetumia lugha hiyo. Kwa mfano, lugha ya Kiswahili inatumika kuanzia ngazi ya juu ya Taifa lakini lugha rasmi ina uwanda mdogo kimatumizi kwani hutumika katika shughuli maalumu, kwa mfano, katika utawala, ofisini, elimu kuanzia sekondari mpaka Chuo Kikuu, mfano, kiingereza kwa hapa Tanzania.
Tofauti katika maana, Lugha ya Taifa ni lugha iliyokubaliwa kitaifa itumike katika mawasiliano yake, kwa mfano, lugha ya Kiswahili iliteuliwa kuwa lugha ya Taifa mwaka 1964 lakini lugha rasmi ni lugha iliyoteuliwa na kuchaguliwa na serikali itumike katika shughuli za kiserikali, kwa mfano, kiingereza.
Kigezo cha idadi ya watumiaji, Lugha ya Taifa ina idadi kubwa ya watumiaji, kwa mfano, nchini Tanzania lugha ya Kiswahili inatumiwa na idadi kubwa ya watu katika mawasiliano yao wakati lugha rasmi ina idadi ndogo ya watumiaji, kwa mfano, lugha ya Kiingereza inatumiwa na watu wachache.
Kigezo cha ugumu katika matumizi, Lugha ya Taifa sio ngumu sana katika matumizi yake kwa sababu kwanza inatumika katika shughuli za kila siku katika jamii. Pia imewekwa katika mpango wa lugha na inatumika katika shughuli zote maalumu na zisizo maalumu, hivyo mambo haya yanaifanya lugha ya Taifa kuwa rahisi katika matumizi yake, wakati Lugha rasmi inakuwa ngumu kimatumizi kwa watu wengi kwa sababu haitumiki katika shughuli za kila siku na inaweza isitsumike katika elimu na inatumika kwa shughuli maalumu tu.
Tofauti katika malengo au madhumuni, Lugha ya Taifa lengo kuu ni kuwasiliana ndani ya Taifa au kukidhi haja ya mawasiliano katika nchi husika katika nyanja mbalimbali, kwa mfano, kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii, lakini lugha rasmi lengo lake ni kukidhi haja ya mawasiliano katika shughuli maalumu za kiserikali kama mahakama na ofisi. Kigezo cha utamaduni, lugha ya Taifa ni sehemu ya utamaduni wa nchi husika, lakini lugha rasmi mara nyingi si sehemu ya utamaduni wa jamii husika kwani hukidhi mahitaji ya watu wachache kwa sababu imeteuliwa kutumika katika shughuli maalumu.
Umilisi wa mawasiliano, Lugha ya Taifa mara nyingi watumiaji walio wengi wanakuwa na umilisi wa mawasiliano, kwa mfano, hapa Tanzania lugha ya Kiswahili watumiaji wengi wanaimudu, lakini katika Lugha rasmi watumiaji wanakuwa hawana umilisi wa mawasiliano, kwa mfano, lugha ya kiingereza kwa hapa Tanzania watumiaji wengi hawana umilisi nayo katika mawasiliano.
Kwa kuhitimisha, pamoja na kuwa na tofauti kati ya lugha ya Taifa na lugha rasmi pia zinafanana kwa upande mwingine. Lugha hizi zote hutumika katika shughuli maalumu kama vile mahakamani, bungeni na shughuli nyingine za kiutawala katika nchi. Lugha hizi zote huandaliwa, huratibiwa na kukubaliwa kutokana na mpango wa lugha na sera ya lugha katika nchi husika, pia lugha hizi zote hutumika kukidhi haja ya mawasiliano kutegemeana na uga husika na sehemu husika.
      Marejeo
  • Buliba, A na wenzake (2006), Isimujamii: kwa wanafunzi wa Kiswahili, The Jomo Kenyatta Foundation- Kenya
  • King’ei, K. (2010), Misingi ya Isimu jamii, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Dar es Salaam
  • Msanjila, P.Y na wenzake (2011), Isimujamii, Sekondari na Vyuo TUKI. Dar es Salaam

Print this item

  DHIMA (MATUMIZI) YA REJESTA
Posted by: MwlMaeda - 07-28-2021, 07:50 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

DHIMA (MATUMIZI) YA REJESTA

(i) Rejesta Hutumika Kama Kitambulisho
Rejesta hutofautisha mtindo wa lugha miongoni mwa wazungumzaji. Rejesta inawatambulisha wazungumzaji kuwa wao ni kundi fulani.
Mfano: Rejesta yawahunzi inawatambulisha kuwa wao ni tofauti na wavuvi ambao nao pia wana rejesta yao. Rejesta ya kanisani au msikitini ni tofauti na rejesta ya jeshini, n.k.
(ii) Rejesta Hupunguza Ukali wa Maneno
Rejesta inapotumiwa na kundi la watu, huficha jambo hilo linalozungumziwa lisieleweke kwa wengi. Hivyo hadhira inapuuzwa kwa sababu siyo watu wengi wanaoelewa.
(iii) Rejesta Inatumika Ili Kurahisisha Mawasiliano
Rejesta inatumika ili kurahisisha mawasiliano au kupunguza muda wa kuwashughulikia watu au wateja wengi. Kwa mfano mganga anayegawa dawa hospitalini anaposema “mbili asubuhi, mchana na jioni” akiwa na maana kuwa mgonjwa anywe vidonge viwili asubuhi, viwili mchana na viwili jioni. Hapa amefupisha ili aweze kuwahudumia kwa wakati mfupi wagonjwa wengi wanaosubiri kupata dawa.
(iv) Rejesta Hupamba Lugha Miongoni mwa Wazungumzaji
Kwa mfano,
Rejesta ya Hotelini.
Mhudumu: Nani wali kuku?
Mteja: Mimi hapa!
Mhudumu: Nani ugali-ng’ombe?
Mteja: Mimi hapa!
Mazungumzo haya kati ya mhudumu na mteja licha ya kurahisisha mawasiliano, vilevile yanapamba mazungumzo hayo.
(v) Rejesta Huweza Kuwa Kiungo cha Ukuzaji wa Lugha
Kutokana na matumizi ya rejesta mbalimbali, lugha inayohusika inaweza kuunda msamiati wake. Kuna baadhi ya maneno ya lugha yanayotokana na rejesta mbalimbali.

Print this item

  MAMBO YANAYOSABABISHA KUTOKEA KWA REJESTA
Posted by: MwlMaeda - 07-28-2021, 07:25 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

MAMBO YANAYOSABABISHA KUTOKEA KWA REJESTA

(i) Ubinafsi
Ubinafsi ni tabia aliyonayo mtu, iwe ya muda au ya kudumu. Kila mtu ana namna ya kusema na kuandika au kuzungumza, ambayo humtofautisha na watu wengine. Hali hii huleta ubinafsi katika sauti yake (matamshi), msamiati, maandishi yake na mwisho huleta mtindo wa kipekee ambao ni tofauti na watua wengine. Hii ni sababu ya kwanza inayosababisha rejesta katika lugha. Hapa tunapata rejesta za watu.
(ii) Maingiliano
Makundi ya watu mbalimbali yanapochangamana husababisha mwingiliano miongoni mwao. Na ili kuweza kutofautisha kundi moja na kundi jingine kuna mambo fulani fulani ambayo hutofautiana miongoni mwa makundi hayo na mambo haya huweza kuwa ya kipekee katika kundi moja tu. Mambo hayo katika lugha huhusisha matamshi ya maneno, sarufi (mpangilio wa maneno) n.k. Tofauti hizi husababisha mitindo miwili tofauti miongoni mwa makundi hayo – hivyo husababisha kuzuka kwa rejesta.
(iii) Kupita kwa Wakati
Kila mahali katika jamii, hujitokeza mitindo katika kipindi maalumu. Na hii ni kutokana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii fulani. Kila kipindi cha mpito wa kihistoria huweza kuwa na maneno yake ambayo huwa ni tofauti na kipindi kingine cha kihistoria. Vilevile mitindo ya lugha kutoka kipindi kimoja hadi kipindi kingine huweza kuwa tofauti. Hivyo, rejesta huweza kutokea kati ya kipindi kimoja na kipindi kingine. Mfano, kipindi cha enzi za Ukoloni na kile cha Uhuru, kipindi cha enzi za Azimio la Arusha na kile cha Hali Ngumu ya Maisha au, na kile cha Mfumo wa Mageuzi.
(iv) Shughuli Iliyopo
Hapa hutegemea ni mazingira gani ambapo shughuli hiyo inafanyikia. Mfano misikitini, makanisani, dansini, bandarini, mahakamani, shuleni, nk. Shughuli fulani katika mazingira fulani hutupatia rejesta za mahali.
(v) Tofauti za Hadhi za Wahusika (Uhusiano wa Wahusika)
Mfano wasomi/wasiosoma, mwajiri/mwajiriwa, tajiri/maskini. Hii hali kwa ufupi husababishwa na matabaka yaliyopo katika jamii, tabaka moja na tabaka jingine hutumia lugha ambayo huwa ni tofauti miongoni mwao, na hivyo husababisha rejesta kuzuka miongoni mwa matabaka hayo.
(vi) Matumizi ya Uficho/Tafsida
Hali hii pia husababisha kuzuka kwa rejesta kwani husababisha mitindo mbalimbali ya lugha miongoni mwa wazungumzaji. Kwa mfano vijana wanaweza kutumia maneno haya “silaha yake haina risasi, silaha yake ni butu, silaha yake haiwezi kukata hata kipande cha mkate” wakimaanisha kwamba “uume wake haufai”.
Au
Vijana wa mitaani huweza kusema “Yule anti ni mkarimu kweli kweli, ni mama huruma – anawahudumia vijana wengi, huwashibisha kwa kuwalisha chakula kinono kweli kweli”–wakimaanisha “binti ambaye akitongozwa humkubali kila mwanamme.”
ZINGATIA
Rejesta ni mtindo wa lugha inayotumika mahali penye shughuli fulani ambayo ni tofauti na lugha ya kawaida. Rejesta ya wavuvi, ya washairi, ya wafanyabiashara, ya wahuni, n.k. ni baadhi tu ya mifano. Rejesta zinazotokana na umri, kwa mfano, vijana wana rejesta yao, na wazee wana yao.
Rejesta inayotokana na jinsia, kwa mfano, wanawake wana rejesta yao mbali na ile ya wanaume.
Rejesta zinazohusu watu ni yale mawasiliano yasiyo rasmi ni yalemaongezi ya kawaida ya kila siku au mazungumzo rasmi;
kwa mfano mazungumzo kati ya:
– Vijana wenye rika moja,
– Wazee wenyewe,
– Wanawake wenyewe,
– Wanaume wenyewe,
– Mwalimu na Mwanafunzi,
– Meneja na Wafanyakazi wake,
– Mtu na Mpenzi wake, n.k.
– Marafiki nao wana rejesta yao.
– Rejesta ya mitaani au vijiweni. n.k.

Print this item

  ODC : MADA YA 1: LUGHA NI NINI?
Posted by: MwlMaeda - 07-28-2021, 07:14 AM - Forum: Nukuu - No Replies

ODC : MADA YA 1: LUGHA NI NINI?

YALIYOMO
1.1 UTANGULIZI
 Ukitaka kuelewa  lugha ni nini uwe unawasikiliza watu wanapozungumza lugha ambayo huielewi huku jambo lililozungumzwa linakuhusu moja kwa moja .Katika hali kama hiyo wewe mwenyewe mazungumzo hayo yataonekana ni mwingiliano wa sauti tu ambazo zinakuletea kelele tu.Lakini wahusika yamkini utawaona wakicheka,wakikutazama ,wakihuzunika ,wakioneshana ishara na kuonesha hisia zao.Wewe  yamkini utaambulia kuona ishara na kupata hisia kutokana na uzoefu wa jamii utokayo.kimsingi wao huelewana kwa lugha waitumiayo  hali hii ndio hujumuiswa na kutoa jibu la kwamba lugha ni chombo cha mawasiliano.
Swali la kujiuliza :ni kwa namna gani kelele zinazosikika zikitamkwa mara kadhaa na kwa namna fulani tofauti tofauti ,zinawezesha kuelewana ,kupeana maelekezo ,kuwasilisha ujumbe na kupeana habari kwa kila muhusika wa kelele hizo.Yamkini wazo unaloweza kupata kwa haraka linaweza kuwa lazima kelele zitolewazo na wahusika zina maana fulani ijulikanayo kwa wasemaji /watamkaji wa kelele hizo.Kwa hakika kelele za namna hiyo zikifikia kiwango cha kuweza kufikisha mawasiliano  juu ya masuala  yanayojitokeza katika jamii fulani ndipo kelele hizo huitwa lughaya jamii husika.
1.2 MADHUMUNI YA MHADHARA
                 Baada ya kusoma muhadhara huu utaweza:

(i) kueleza asili ya lugha
(ii) kueleza maana /dhana ya lugha
(iii) kujadili aina za lugha
(iv)kujadili mitazamo mbalimbali ya fasili ya dhana ya lugha
(v) kujadili tabia za  lugha.
(vi) kufafanua sifa za lugha
1.3 KIINI
1.3.1 Asili ya Lugha
Ni dhahiri kuwa kila jamii ina hadithi zake kuhusu jinsi lugha yake ilivyozaliwa/kuanza.Lakini katika historia  kuna hadithi nyingi zinazohusu asili/chimbiko la lugha zote za binadamu.Mojawapo ya hadithi hizo ile inayosimuliwa katika kitabu maarufu kama Biblia inayohusu chanzo cha watu kunena lugha mbalimbali  wakati wa ujenzi wa mnara wa Babeli.Ambapo inasemekana kwamba kulitokea kutoelewana kwa kila mmoja kuzungumza lugha yake na huo ukawa mwanzo wa lugha mbalimbali Duniani.Hadithi hii yaelekea kuwa na ukweli kiimani zaidi kwani watu wa imani hii  huamini kuwa ni kweli  lakini kitaalumu hakuna kigenzo chochote ambacho kinaweza kidhibitisha ukweli huo.
1.3.1.1 Mtazamo wa kiisimu
Kiisimu asili ya lugha huweza kutazamwa kwa namna mbili .namna ya kwanza ni ile  inayoangalia hali za mabadiliko ya binadamu toka kale hadi kupata lugha asili ambazo zote ni kamili  kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya jamii fulani. Katika mtazamo huu inaelezwa kwamba lugha huweza kuzuka kukua na kufa.Namna ya pili ya mtazamo juu ya asili ya lugha ni ule unaozingatia namna motto anavyoipata lugha.Kimsingi ni dhahiri kwamba hakuna motto anayezaliwa akiwa na lugha au uwezo wa kuzungumza lugha fulani . Badala yake kila motto huzaliwa katika hali ya kawaida bila lugha lakini huwa na uwezo wa kupata lugha yeyote ya jamii inayomlea au jamii inayomzunguka.ukiangalia namna hii utagundua kuwa ili mtoto aweze kupata lugha ni lazima awe miongoni mwa jamii ya watu.mpaka sasa wataalamu hawajasema lolote iwapo mtoto ataachwa mahali bila kuwa na mwingiliano na watu /jamii yeyote atakuwa na lugha au atakuwa na athari gani kilugha kutokana na upweke huo.
Katika ujumla wake umejifunza kwamba chimbuko la lugha linafungamana sana na maumbile pamoja na mazingira ya mtu binafsi na jamii yake kwa mda mrefu.katika kipengele cha muda haijajulikana vema muda kamili ni upi na hivyo kupelekea kuwepo na simulizi kuhusu chimbuko la binadamu na lugha yake.
1.3.2 Maaana ya Lugha
Fasili ya lugha kwa mujibu wa wa crystal (1992) anasema :”lugha ni mfumo wa sauti nasibu, ishara au maandishi kwa ajili ya mawasiliano na kujieleza katika jamii ya watu”
Katika fasili yake ametaja mambo makuu matano ambayo ni mfumo,sauti za nasibu, sautialama na ishara,jamii ya wanadamu, mawasiliano na kujieleza/kujitambulisha.
Ili kupata dhana nzima ya fasili hii ni muhimu tuangalia kila kipengele katika fasili yake:
1.3.2.1 Mfumo
Kila lugha ina muundo wake ambao huwa ni fofauti na lugha nyingine.kwa maana hii kila lugha ni kijisehemu cha miundo iliyopo katika kundi zima la miundo ya lugha duniani.miundo hiyo yaweza kuwa jinsi maneno yalivyoundwa jinsi maneno yalivyofuatana.hivyo kila lugha ina ruwaza maalumu.
1.3.2.2 Sauti Nasibu
Hapa ina maana kuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya neno na kile kinachowakilishwa katika lugha.Hivyo maana inayowakilishwa huwa ni ya kinasibu tu au inatokana na makubaliano ya wanajamii/watumiaji wa lugha fulani katika mazungumzo yao ambayo huwa yanatofautiana kutoka rika moja hadi jingine.
   Mfano Neno MEZA halina maana ya moja kwa moja na umbo linalowakilishwa.
1.3.2.3 Sauti, Alama na Ishara
  Kimsingi kila lugha huteua sauti ,alama au ishara zianazowakilisha wazo au ujumbe.lugha nyingi hutumia sauti katika mazungumzo wakati baadhi ya lugha hutumia ishara za maandishi katika mawasiliano na lugha nyingine hutumia alama katika kukamilisha mawasiliano.
1.3.2.4 Jamii ya Wanadamu
Kimsingi ni wanadamu pekee ndio watumiao lugha  na ni jamii zao pekee zinazoteua maneno na kuyapa maana waitakayo katika jamii hiyo sambamba na jinsi gani miundo ya lugha zao wanataka ziwe.Viumbe wengine wana njia za mawasiliano  ambazo zinatofautiana kabisa na njia za mawasiliano ya wanadamu.Hivyo lugha huwa ni kwa wanadamu tuu.
1.3.2.5 Mawasiliano
Katika kueleza dhana nzima ya lugha inafaa kugusa dhima ya lugha hiyo kwa wale waitumiayo.Lugha hutumika kama njia kuu ya mawasiliano.Kwa kupitia lugha watu huweza kutoa  na kupokea ujumbe pamoja na kutolea hisia zao.Kwa kutumia lugha tunasema  tukitakacho ili kukidhi mahitaji yetu.Mawasiliano katika lugha kunaajumuisha kuzungumza ,kuandika,kusoma na hata kutumia mifumo mingine ya ishara.njia zote hizi ni njia za mawasiliano kwa kutumia lugha.
1.3.2.6.Kujieleza/kujitambulisha
Ni dhahiri kabisa kwamba wanajamii huitumia lugha kwa ajili ya mawasiliano katika Nyanja zote za kimaisha ( kisiasa kiuchumi na kiutamaduni)inafaa ikielewa pia kuwa katrika kuizunguma, kuiandika  kuisoma na pengine kuzitumia ishara fulani,mtumiaji kwa namna moja ama nyingine hujitambulisha na kujieleza kwa hadhira kwamba yeye ni nani, anazungumzia nini, na nani,  wa utamaduni gani,na pengine hata eneo analotokea ni wapi?yote haya huweza kudhihirika kutokana na ukweli kwamba lugha huwa na sifa kubwa ya kubeba utamaduni wa mahali lugha inapozungumzwa.hivyo lugha ni kielelezo chako katika mazingira na utamaduni wa unamoishi.ikitokea lugha unayiozungumza si ya utamaduni wako au asili yako, basi utatambulika tu na wanajamii wenye utamaduni wa lugha yao.
Japokuwa watanzania wote twaweza kuzungumza Kiswahili kama lugha ya taifa na ni lugha ya mawasiliano kwa taifa letu lakini wazungumzaji huweza kujitambulisha maeneo watokayo katika sehemu mbalimbali za Tanzania.si jambo geni kusikia wazungumzaji wakisema huyo atakuwa mhehe wa mfundi au mbena wa njombe kwa maana hawa hawana “s” ila wana ‘z’ au huyu mtu wakusini maana hawa hawaa “m” badala yake wana “n.kwa mfano hii lugha huweza kutambulisha eneo mtu atokako.
Katika ufafanuzi  wa dhana ya lugha ni muhimu kuzingatia vipengele vilivyojadiliwa hapo juu ilio kutoa dhana ya lugha kwa upana wake.
 
1.3.3 Aina za Lugha
Kwa kutumia msingi wa kutazama hali halisi na mifumo ya sauti na ishara anayoitumia binadamu kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya lugha katika jamii,wataalamu wa lugha wameafikiana kutenga lugha katika aina kuu mbili ambazo ni lugha asili na lugha unde.
 
1.3.3.1 Lugha za Asili
Lugha asili ni ile lugha inayohusisha mfumo wa sauti zinazotolewa kwa kutumia ala katika chemba ya mdomo wa binadamu Lugha asili ina sifa za kuwa na viwango tofauti katika  muundo wake,na huwa na uwezo wa kuzalisha tungo zisizo na ukomo/kikomo.kwa mujibu wa mwanaisimu John Lyons,lugha asili ina viwango viwili muhimu vya muundo ambavyo ni :
(i)Kiwango cha msingi kinachohusisha vipashio kamili vyenye maana kama vile maneno
(ii)Kiwango kisicho msingi kinachihusisha vipashio ambavyo vyenyewe havina maana lakini hutumika katika kuunda vipashio vipashio vya msingi.vipashio hivi huwa ni sauti katika lugha (Lyons 1970:11-13)
Sifa hii ya uwezo wa kuzalisha tungo zisizo na ukomo kimsingi inahusu hasa uwezo wa binadamu wa kuunda na kuelewa idadi isiyo kikomo ya maumbo ya maneno na sentensi katika lugha  yake.hii hufanyika kiasili bila mhusika kukusudia kutumia kanuni fulani za kisarufi katika lugha yake.Katika uzalishaji huu mtumiaji wa lugha hutumia sauti  fulani ili kupata maneno ya aina fulani.Kwa mfano kwa kutumia sauti i,m,l na a katika mipangilio mbalimbali ,katika Kiswahili tunaweza kupata maneno kama imla,lima,lami.
Pia kwa kutumia muundo wa aina moja kuweza kuzalisha sentensi nyingi mbalimbali.kwa mfano kwa kutumia muundo wa wenye KIIMA, KITENZI NA YAMBWA ianwezekana kupata sentensi kama:
Tembo amemla mtu
Mtu amemla tembo
Mwalimu anasoma gazeti
Mama anapika ugali
Mkulima analima karanga.n.k.
1.3.3.2 Lugha Unde
Lugha unde ni ile inayohusu mfumo wa ishara ambazo binadamu amezibuni na huzitoa kwa kutumia viungo vyake vya mwili kama mikono,vidole kope za macho n,k maandishi pia huingia kwenye kundi la hili kwani ni nyenzo mojawapo anazoziunda mwanadamu ili kikidhi mahitaji yake ya mawasiliano.katika hali ya kawaida lugha hii huwa na maana tofautitofauti kutokana na rika la watu uhusiano wao,mahali, tukio napengine mahitaji yake.
Hadi leo haijajulikana kama wanyama wana aina gani ya lugha kati ya hizi.chakujiuliza ni je wanyama wana lugha ?na kama wanayo ipo katika kundi gani?aidha sifa zilizobainishwa zinaelezea kitu kinachoitwa lugha na kudokeza kwamba si kila njia ya  mawasiliano ni lugha katika  maana ileile ya lugha.
1.3.4  Mitazamo Mbalimbali Juu ya Fasili ya Dhana ya Lugha
Wataalamu wengi wameileza dhana ya lugha tangu miaka ya 1920 na 1930 hususan wanaisimu wa skuli ya isimu-miundo ambao ni Leonard Bloomfield na Edward Sapir.mawazo yao kuhusu ni lugha ni kwamba (i)lugha ni ishara (ii)ishara hizo huzihusisha moja kwa moja na ala za sauti zilizomo katika bomba la sauti,(iii)sauti hizo zimo katika mfumo maalumu,(iv)mfumo huo wa sauti ni wanasibu(V)kwa kutumia mfumo huo wa nasibu, jamii inayoitumia lugha husika huwasiliana.zipo fafanuzi nyingine za lugha ambazo zimejikita katika misingi ya Nyanja totauti ya kitaaluma kama ifuatavyo:
Kwa wanafalsafa wanaona lugha ni chombo cha fikra. Wao huona kwamba mtu hawuzi kufkiri bila kuwa na lugha hivyo lugha ni chombo cha fikra.
Kwa wanazuoni /wanaelimu jamii wanaona kwamba lugha ni namna fulani ya tabia.wao huhusiana namna mtu anavyotumia /anavyoongea na tabia yake kama mtu anaongea maneno yote kwa ukali hiyo ndio tabia yake na tofauti yake ni sahihi.
Kwa wanasaikolojia wanaona lugha ni mlango wa kutambua akili za binadamu wao wanaamini kwamba bila lugha huwezi kutambua akili za watu.
Ama kwa hakika wapo wataalamu wengine ambao huenda wamefafanua zaidi juu ya dhana nzima ya neno lugha ni jukumu,lako kutafua zaidi juu ya dhana hii.
1.3.5 Tabia za Lugha
Ama kwa hakika zipo tabia ambazo zinajitokeza kwa kila lugha ,tabia hizo zinaihalalisha lugha fulani kuwa lugha kwa maana halisi ya lugha.
1.3.5.1 Tabia ya kukua
Lugha ina tabia ya kukua,lugha inavyozidi kutumika katika jamii huongeza maneno kulingana na mahitaji, kitendo hicho hupelekea lugha kuwa na tabia ya kukua.Katika mchakato huu maneno ya zamani hubadilika na maneno mapya hujitokeza,mabadiliko haya hujitokeza kutokana na maendeleo ya kijamii,maendeleo ya sayansi na teknolojia.mabadiliko haya huwa yanajikita katika nyanja zote za kimaisha yaani kisiasa kiuchumi na kiutamaduni,kwa mfano kipindi cha maendeleo ya vyama vingi ndipo tulipopata misamiati ya ngangari ngunguri n.k pia kuna misamiati kama kasheshe,kilimo kwanza,kompyuta n.k.
1.3.5.2 Tabia ya kuathiri na kuathiriwa
Lugha ina tabia ya kuathiri lugha na kuathiriwa na lugha nyingine.kwa kawaida lugha inavyochua maneno fulani kutoka lugha nyingine huwa inaathiri lugha inakochukua maneno wakati lugha inayopokea maneno yale huwa inakuwa inaathiriwa na lugha ile.ni dhahiri kwamba Kiswahili kimeathiriwa na lugha ya kiarabu,kibantu,na kiingereza,wakati huohuo Kiswahili kimeathiri lugha hizo.
1.3.5.3 Tabia ya ubora
Lugha  ina tabia ya ubora .Tabia hii ina maana kwamba  kila lugha ni bora kwa wale wanaoitumia .Hakuna lugha iliyobora kuliko nyingine kwani kwa wale wanaoitumia inawafaa.Ijapokuwa upo uwezekano wa kuwa na bora lugha, bora lugha hujitokeza sana kwenye rejesta ambazo huzingatia mawasiliano ya kundi fulani na hivyo kuwa na bora lugha badala ya lugha bora.
1.3.5.4 Tabia ya kujitosheleza
Lugha ina tabia ya kujitosheleza kulingana na mahitaji ya jamii ambayo inaitumia.Tabia hii hujipambanua wazi kutokana na kujitosheleza kimsamiati kulingana na mahitaji ya jamii husika.
1.3.6 Sifa za Lugha
Lugha huhalalishwa kuwa lugha kutokana na sifa zifuatazo:
(i) Lugha ni lazima imuhusu Mwanadamu
Ama kwa hakika hakuna kiumbe kisichokuwa mwanadamu (mtu)kinachoweza kuzungumza lugha kwa maana halisi ya lugha.Lugha ni chombo maalumu wanachotumia wanadamu kwa lengo kuu la mawasliano.Kwa mantiki hiyo basi sifa kuu ya chombo hiki ni lazima kiwe kinamhusu mwanadamu na si  vinginevyo.
(ii)  Sauti
lugha ambayo inamhusu mwanadamu,huambatana na sauti za binadamu zinazotoka kinywani mwake.Katika jambo hili ni lazima mwanadamu atamke jambo kinyani mwakekwa sauti.Ijapokuwa mwanadamu anaweza kutumia njia nyingine ya maandisha na akawa amefikia lengo lake la mawasiliano.
(iii) Lugha ni lazima iwe na utaratibu maalumu
Kama ilivoelezwa kwenye fasili ya lugha  kuwa lugha ni sauti zenye utaratibu maalumu.ambao hupangwa kwa kufuata utaratibu fulani unaokubalika kwa jamii hiyo ya watu.Kwa maana hiyo basi si kila sauti itokayo kinywani mwa mwanadamu ni lugha,itakuwa lugha iwapo itakuwa imefuata taratibu zinazokubalika katika jamii husika.mfano mtoto anapolia anatoa sauti lakini hatuwezi kusema kulia ni lugha kwa sababu ni sauti inayotoka kinywani la  hasha.Utaratibu wa sauti hizo kwa neon moja hitwa Sarufi.
Mfano:
(a)Hatusemi.
(i)  Juma wimbo anaimba.
(ii) Kitabu changu mimi nimekipoteza.
(b)Jamii imepatana kusema kwa utaratibu ufuatao:
  (i) Juma anaimba Wimbo.
 (ii)Mimi nimekipoteza kitabu changu.
(iv) Lugha huwa na misingi ya Fonimu.
 
Lugha hufuata misingi ya fonimu ,ambapo lugha ina vitakwa au vipashio ambayo huitwa fonimu.wanaisimu wanakubaliana kwa ujumla kwamba fonomu ni sauti yenye uwezo wa kuleta tofauti katika maana ikipachikwa katika neno  la lugha husika.Baadhi ya fonomu za lugha ya Kiswahili:
1./a/,/e/,/i/,/o/,/u/.
Katika neno {tata} tunaweza kupachika fonimu nyingine na tukapata maana tofauti tofauti kama  ifuatavyo:
{tata}={teta}={tita}={tota}={tuta}
Pia katika neno {taa} tunaweza kuzalisha maneno yafuatayo:
{taa}={tea}={tia}=[toa}={tua}
2./p/,/b/,/t/,/d/,/f/,/k/,/g/,/s/,/z/n.k
Tunaweza kupata maneno kama pawa, bawa, tawa, dawa, chawa, jawa, gawa sawa zawa na maneno mengi mengineyo.
(v) Lugha hufuata mpangilio wa vipashio unaoleta maana
Lugha ni lazima iwe na mpangilio wa vipashio mpangilio huo huwa unafahamika na watumiaji wa lugha husika. Katika mpangilio huo ndipo unapotokea muundo wa sentensi kwa maana kwamba ili sentensi iwe na maana ni lazima vijenzi vya sentensi hiyo view kwenye mpangilio unaokubalika.katika lugha ya kiwsahili mpangilio huo huanza na fonomu,neno,kirai,kshazi na hatimaye sentensi.
 (vi) Lugha Husharabu
Lugha husharabu /hushabihiana hii ina maana kwamba lugha huchukua baadhi ya maneno kutoka
Lugha nyingine ili kujiongezea msamiati wake. Tabia hii inazisaidia sana lugha
zinazokua.Katika tabia hii lugha ikishachukua neno kutoka lugha nyingine hulifanya neno lile liendae na maneno mengine ya lugha husika.Kimsingi vitu viwili vinaweza kutokea katika tabia hii,kwanza lugha inaweza kuchua neno kutoka lugha fulani na kulitumia kama lilivyo,pili lugha inaweza kuchukua neno kutoka lugha nyingine na kulirekebisha ili liendane na mfumo mzima wa lugha husika.Vitu vyote hivi kwa neno moja huitwa kusharabu .
(vii) Lugha Inajizalisha
Lugha ina sifa ya kutumia vipashio vyake kujiongezea misamiati/maneno mapya.Kujizalisha kwa lugha huweza kutokea kwa  njia ya  kunyambulishaji na  mara nyingine lugha hujipatia misamiati kutokana na urudufishaji.
Unyambulishaji hufanyika pale vipashio vinapopachikwa kwenye mzizi wa neno ili kuzalisha maneno mengine.
                                       UNYAMBULISHAJI
 
UAMBISHAJI                                                 UNYAMBUAJI
 
                                               MZIZI
 
KIELELEZO                         
Unyambulishaji unahusu kitendo cha kuongeza vipashio mbele na nyuma ya mzizi. Uambishaji katika Kiswahili hutokea kabla ya mzizi wakati unyambuaji hutokea baada ya mzizi.
Katika mzizi{-lim-} inawezekana kufanya unyambulishaji na  kupata maneno kama:
(a)     Yeye Analima
(b)   Wewe Unalima
©    Mimi Ninalima
(d)   Wao wanalima
 
Kutokana na mfano wa hapo juu utaona kwamba uambishaji unaopofanyika unaendana sambamba na upatanishi wa kisarufi kama inavyoonekana katika mfano hapo juu a-d
Hata hivyo katika unyambuaji Kiswahili hujiongezea msamiati kwa kuzalisha maneno mapya,angalia mifano ifuatayo:
(a)pig=>ku-pig-a=>ku-m-pig-a=>tu-li-m-pig-a
(b)pig-i-a=>pig-ish-a=>pig-ish-an-a=>pig-ik-a
© pig-ik-a
 
1.4 Hitimisho
Lugha ni lazima iwe sauti za kusemwa na binadamu. Sauti hizo za
binadamu lazima ziwe na utaratibu maalumu wa kuwasiliana, na
kama hakuna utaratibu maalumu hiyo siyo lugha. Sauti na milioiko mingi duniani, milio ile inayoweza kuwafanya binadamu
wawasiliane ndiyo tunayoita lugha.
Lugha lazima iwe na sifa zinazoambatana na tabia za
binadamu katika utamaduni wake. Vinginevyo lugha husika
itakuwa si asilia

Print this item

  KIDATO CHA PILI: REJESTA
Posted by: MwlMaeda - 07-27-2021, 04:10 PM - Forum: Nukuu - No Replies

Rejesta
Kwa ujumla tunaweza kufasili rejesta kama mtindo wa lugha kutegemeana na kazi fulani, muktadha wa matumizi, lengo na uhusiano wa wanaowasiliana. Katika muktadha rasmi rejesta hurejelea upande mmoja kama vile, msamiati wa kiufundi, adabu maalum na matumizi ya lugha fasaha, mfano katika elimu, mahakamani na kadhalika.
Kuwasiliana kwa kutumia Rejesta
Rejesta za Mitaani
Haya ni mazungumzo yanayozungumzwa magengeni nayo hueleweka na wazungumzaji wenyewe. Ni lugha ambayo huchipuka kutokana na kikundi cha watu ambacho ni kidogo. Mfano wa maneno yanayotumika sana mitaani ni kama vile “Mshikaji” (rafiki) Demu” (mwanamke)n.k. Kwa ujumla lugha ya mitaani ni lugha isiyo sanifu, ni lugha iliyojaa maneno ya mitaani ambayo yanaeleweka kwa wazungumzaji wenyewe.
Mazungumzo ya Kwenye Shughuli Maalum (Rejesta za Mahali)
Mazungumzo ya kwenye shughuli maalumu hayafanywi kiholela, bali yanafuata taratibu na kanuni maalum zinazojitokeza katika mazingira haya. Kutokana na kutumiwa kwake kwa muda mrefu kwenye mazingira yale yale.
Mazungumzo ya kwenye shughuli maalumu ni kama vile mazungumzo ya:
  • Maofisini au mahali popote pa kazi
  • Mahakamani
  • Hotelini
  • Hospitalini
  • Msikitini
  • Kanisani n.k
Mazungumzo ya mahotelini yana utaratibu wake ambao katika hali ya kawaida inaweza isieleweke.
Nani wali kuku?
B: Mimi
Chai moja wapi?
B: Hapa
Katika mazungumzo haya A anapouliza “Nani wali kuku”, ana maana kuwa nani anahitaji kula wali na nyama ya kuku”. Hapa hana maana ya kumwainisha mtu aitwaaye “wali kuku”.
Kwa upande wa lugha ya mahakamani ni tofauti na lugha ya hotelini. Lugha ya mahakamani inasisitiza usahihi ili kuondoa migongano miongoni mwa wanaohusika.
Mfano 1
Mfano:
Wakili wa Utetezi: Nakuuliza jaribio la kutaka kupindua serikali litakuwa kosa la namna gani katika sheria za Tanzania?
Kamishna Msaidizi: (Baada ya kupewa kitabu cha sheria za Tanzania na kukisoma) Ni kosa la uhaini.
Wakili wa Utetezi: Ulichukua muda mrefu kufikia jibu hili. Washitakiwa wawili hawahusiani na makosa haya?
Kamishna Msaidizi: Sijui.
Kimsingi hii ni hali ya kawaida kabisa katika mahojiano ya mahakamani. Mara nyingi mahojiano katika mahakama hayaendi haraka sana. Kila mtu anayehusika – hakimu, mwendesha mashtaka, wakili, mdaiwa, shahidi, n.k. hujieleza kwa wazi wazi bila kujali urefu wa maelezo.
Rejesta Zinazohusu Watu
Rejesta zinazohusu watu ni yale mawasiliano yasiyo rasmi, ni yale maongezi ya kawaida ya kila siku au mazungumzo rasmi; kwa mfano mazungumzo kati ya:
  • Vijana wenye rika moja,
  • Wazee wenyewe,
  • Wanawake wenyewe,
  • Wanaume wenyewe,
  • Mwalimu na mwanafunzi,
  • Meneja na wafanyakazi wake,
  • Mtu na mpenzi wake, n.k.
Mazungumzo miongoni mwa marafiki wa rika moja huzungumza lugha ambayo wao wenyewe wanaielewa na sio rahisi kwa mtu wa rika lingine kuielewa lugha hiyo.
Mfano 2
Mfano:
‘Basi, Master jana wikiendi ilikuwa kibaridi sana. Basi nilizamia infoo kwenye zinga la mnuso huko saiti za upanga. Nilifika getini nikakuta baunsa kanyuti chedro likisubiri kumtoa noma kila mzamiaji. Alikuwa mnoko kishenzi. Akatema mkwara mbuzi, nikajibu kwa mkwaradume….akabloo mimi ndani’.
Maana ya Maneno
  • Wikiendi – Mwisho wa wiki
  • Kibaridi –tulivu
  • Kuzamia infoo – Kuingia mahali bila kualikwa
  • Zinga la Mnuso –sherehe kubwa
  • Saiti –sehemu
  • Baunsa limenyuti chedro – Ni mlinzi wa mlangoni ametulia pembeni
  • Noma – Hatari
  • Mnoko kishenzi – kinaa sana
  • Mkwara mbuzi – Vitisho dhaifu (Sani, Toleo Na 49).
Mtu asomapo maelezo hayo, mara moja unaona jinsi vijana hawa wa rika moja waishio mjini wanavyozungumza Kiswahili. Si rahisi kwa mzungumzaji wa Kiswahili sanifu kuielewa kirahisi lugha hiyo.
‘Chai moja wapi?’ hii ni rejesta inayotumika katika muktadha gani?
A Hotelini
B Dukani
C Hospitalini
D Darasani
___ni mazungumzo ya kwenye shughuli maalumu yanayofuata taratibu na kanuni.
A Rejesta za mitaani
B Rejesta za kitarafa
C Rejesta za mahali
D Rejesta za watu
 ‘Je mshtakiwa una utetezi wowote?’ rejesta hii hutumika wapi?
A Msikitini
B Kanisani
C Mahakamani
D Shuleni
___hutumika kuwasiliana katika muktadha maalumu.
A Lahaja
B Rejesta
C Misimu
D Istilahi
Ni rejesta gani zinahusu mazungumzo ya kawaida ya kila siku?
A Rejesta zinazohusu watu
B Rejesta za kitarafa
C Rejesta za mahali
D Rejesta za mitaani
Dhima za Rejesta
Katika kipengele cha utambulisho wa kijamii tunaangalia namna aina ya lugha ya mazungumzo inavyoweza kujidhihirisha miongoni mwa watumiaji wake au kuwatambulisha na kuwatofautisha wanajamii husika. Pia katika utambaulisho wa kijamii tunaangalia vile ambavyo mtu hutambulika katika jamii kulingana na namna anavyoongea kulingana na hadhi, tabaka, na jinsi ambavyo mtu huyo anavyoweza kusababisha mshikamano au mwachano katika mazungumzo. Kwa mfano jamii itamtambua mwanajamii kuwa ni msomi kulingana na mtindo wa lugha ya mazungumzo anaoutumia, au ni mtu wa mtaani kulingana na lugha anayotumia.
Rejesta, ina nafasi kubwa sana katika maendeleo ya kiuchumi kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Hii ni kutokana na kwamba, madhumuni makuu ya mawasiliano katika biashara ni kuwavutia wateja na kuwafanya kuamini kuwa bidhaa ama huduma wanazouziwa ni za kiwango cha juu na ni thamani bora kwa pesa zao. Hivyo lugha ya biashara (rejesta), kwa kawaida ni lugha ya kutangaza uzuri wa bidhaa au huduma, huwa na sentensi au vifungu vifupi, mfano “Okoa mapesa chungu mbovu” pia huwa na lugha ya kupumbaza na kuaminisha, mfano “Kunywa XYZ kufumba na kufumbua afya yako itakurudia”.
Pia rejesta inasaidia sana kurahisisha mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji katika masuala mbalimbali ya kibiashara na hata katika huduma mbalimbali za kijamii. Mfano hospitalini “mbili mara tatu”, hotelini “kuku wali tafadhali”, sokoni “kata nusu” na maeneo mengine.
Baadhi ya rejesta hutumika kupunguza idadi ya maneno hivyo kufanya mazungumzo yawe mafupi na yanayoeleweka kwa urahisi mfano rejesta za hotelini kama vile:- Muuzaji: wapi ng’ombe? Mteja: hapa Muuzaji: wapi chai chapati? Mteja: hapa.
Pia katika kutolea elimu ya dini kanisani na msikitini rejesta ina nafasi kubwa katika kujenga maadili.
Vilevile rejesta ina nafasi ya kupamba mazungumzo, wazungumzaji wengi wanapozungumza hapa na pale hupenda kutumia maneno tofautitofauti ili kufanya mazungumzo yawe ya kuvutia. Mfano mazungumzo miongoni mwa vijana:
Kijana 1: Niaje? Nakuona umechili
Kijana 2: mzuka jembe. Kama kawa… kama dawa!

Print this item

  Elunumitindo na mitindo
Posted by: MwlMaeda - 07-27-2021, 03:51 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

.pdf   Elunumitindo na mitindo.pdf (Size: 144.18 KB / Downloads: 0)

Print this item

  UFAHAMU NA UFUPISHO
Posted by: MwlMaeda - 07-27-2021, 10:41 AM - Forum: Nukuu - No Replies

.pdf   Ufahamu na Ufupisho.pdf (Size: 127.44 KB / Downloads: 5)

Print this item

  UFAHAMU NA UFUPISHO
Posted by: MwlMaeda - 07-27-2021, 10:39 AM - Forum: Nukuu - No Replies

.pdf   Ufahamu na Ufupisho.pdf (Size: 127.44 KB / Downloads: 5)

Print this item

  UFAHAMU NA UFUPISHO
Posted by: MwlMaeda - 07-27-2021, 10:37 AM - Forum: Nukuu - No Replies

.pdf   Ufahamu na Ufupisho.pdf (Size: 127.44 KB / Downloads: 7)

Print this item