09-25-2022, 09:54 AM
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "FURUTU''
Neno *furutu (furut.u)* katika lugha ya Kiswahili ni *kitenzi si elekezi* chenye maana ya 'zidisha kufanya jambo fulani kuliko kawaida'.
*Mfano:* Kati yenu, Mwanakibibi anafurutu kwa kupenda kujiremba.
Neno hili *furutu*,linatokana na neno la Kiarabu *furtwun فرط* na lenye maana zifuatazo:
1. Kuchupa mpaka, kuzidisha kufanya jambo fulani kuliko kawaida.
2. Kitu kilichoachwa au kutelekezwa.
Kinachodhihiri ni kuwa neno *furutwun فرط* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *furutu* maana ya kuzidisha kufanya jambo fulani kuliko kawaida haikubadilika na maana ya Kitu kilichoachwa au kutelekezwa iliachwa.
*Shukran sana.*
*Khamis S.M. Mataka.*

Mwl Maeda