MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO "FURUTU''

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO "FURUTU''
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "FURUTU''

Neno *furutu (furut.u)* katika lugha ya Kiswahili ni *kitenzi si elekezi* chenye maana ya 'zidisha kufanya jambo fulani kuliko kawaida'.

*Mfano:* Kati yenu, Mwanakibibi anafurutu kwa kupenda kujiremba.

Neno hili *furutu*,linatokana na neno la Kiarabu *furtwun فرط* na lenye maana zifuatazo:

1. Kuchupa mpaka, kuzidisha kufanya jambo fulani kuliko kawaida.

2. Kitu kilichoachwa au kutelekezwa.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *furutwun  فرط* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *furutu* maana ya kuzidisha kufanya jambo fulani kuliko kawaida haikubadilika na maana ya Kitu kilichoachwa au kutelekezwa iliachwa.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*