ETIMOLOJIA YA NENO "FURUTU'' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO "FURUTU'' (/showthread.php?tid=2836) |
ETIMOLOJIA YA NENO "FURUTU'' - MwlMaeda - 09-25-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "FURUTU'' Neno *furutu (furut.u)* katika lugha ya Kiswahili ni *kitenzi si elekezi* chenye maana ya 'zidisha kufanya jambo fulani kuliko kawaida'. *Mfano:* Kati yenu, Mwanakibibi anafurutu kwa kupenda kujiremba. Neno hili *furutu*,linatokana na neno la Kiarabu *furtwun فرط* na lenye maana zifuatazo: 1. Kuchupa mpaka, kuzidisha kufanya jambo fulani kuliko kawaida. 2. Kitu kilichoachwa au kutelekezwa. Kinachodhihiri ni kuwa neno *furutwun فرط* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *furutu* maana ya kuzidisha kufanya jambo fulani kuliko kawaida haikubadilika na maana ya Kitu kilichoachwa au kutelekezwa iliachwa. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |