MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO 'DHAMBI' NA 'DHUNUBU

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO 'DHAMBI' NA 'DHUNUBU
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'DHAMBI' NA 'DHUNUBU'

Neno *dhambi* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]*  yenye maana zifuatazo:

1. Tendo la kufanya kinyume na amri za Mwenyeezi  Mungu.

2.  Kufanya makosa katika michezo aghalabu mpira wa miguu.

Neno *dhunubu* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino*  iliyo iliyo wingi wa neno dhambi na aghalabu hutumika katika tenzi na mashairi. Maana ya dhunubu ni uovu tele, dhambi nyingi.

Wingi wa neno *dhambi* katika lugha ya kawaida ni *madhambi*.

Katika lugha ya Kiarabu, neno *dhambi* limetoholewa kutoka neno la Kiarabu ' *dhanbu' (soma: dhanbun/dhanban/ dhanbin ذنب)* lenye maana ya kilicho kinyume cha Sharia/Sheria.

Na neno *dhunubu* limetoholewa kutoka neno la Kiarabu *dhunuubun (soma: dhunuubun/dhunuuban/dunuubin ذنوب)* lenye maana ya dhambi nyingi.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *dhanbun ذنب* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *dhambi* maana yake katika lugha yake asili Kiarabu haikubadilika bali iliongezwa maana ya kufanya makosa katika michezo aghalabu  mpira wa miguu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)