ETIMOLOJIA YA MANENO 'DHAMBI' NA 'DHUNUBU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO 'DHAMBI' NA 'DHUNUBU (/showthread.php?tid=2522) |
ETIMOLOJIA YA MANENO 'DHAMBI' NA 'DHUNUBU - MwlMaeda - 04-21-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'DHAMBI' NA 'DHUNUBU' Neno *dhambi* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo: 1. Tendo la kufanya kinyume na amri za Mwenyeezi Mungu. 2. Kufanya makosa katika michezo aghalabu mpira wa miguu. Neno *dhunubu* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino* iliyo iliyo wingi wa neno dhambi na aghalabu hutumika katika tenzi na mashairi. Maana ya dhunubu ni uovu tele, dhambi nyingi. Wingi wa neno *dhambi* katika lugha ya kawaida ni *madhambi*. Katika lugha ya Kiarabu, neno *dhambi* limetoholewa kutoka neno la Kiarabu ' *dhanbu' (soma: dhanbun/dhanban/ dhanbin ذنب)* lenye maana ya kilicho kinyume cha Sharia/Sheria. Na neno *dhunubu* limetoholewa kutoka neno la Kiarabu *dhunuubun (soma: dhunuubun/dhunuuban/dunuubin ذنوب)* lenye maana ya dhambi nyingi. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *dhanbun ذنب* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *dhambi* maana yake katika lugha yake asili Kiarabu haikubadilika bali iliongezwa maana ya kufanya makosa katika michezo aghalabu mpira wa miguu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |