04-18-2022, 09:11 AM
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ADAWA'
Neno *adawa* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana ya *hali ya kufanya chuki dhidi ya mtu mwengine.*
Katika lugha ya Kiarabu neno *adawa* linatokana na neno la Kiarabu *adaawah (soma: adaawatun/adaawatan/adaawatin عداوة)* lenye maana ya *hali ya chuki, uhasama na uadui baina ya wawili au zaidi.*
Kinachodhihiri ni kuwa neno *adaawatun عداوة* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *adawa* maana yake ya msingi katika lugha ya asili - Kiarabu haikubadilika.
*Shukran sana.*
*Khamis S.M. Mataka.*

Mwl Maeda