MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'ADAWA'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'ADAWA'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ADAWA' 

Neno *adawa*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana ya *hali ya kufanya chuki dhidi ya mtu mwengine.*

Katika lugha ya Kiarabu neno *adawa* linatokana na neno la Kiarabu  *adaawah (soma: adaawatun/adaawatan/adaawatin عداوة)* lenye maana ya *hali ya chuki, uhasama na uadui baina ya wawili au zaidi.*

Kinachodhihiri ni kuwa neno *adaawatun  عداوة*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno *adawa* maana yake ya msingi katika lugha ya asili - Kiarabu haikubadilika.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*