ETIMOLOJIA YA NENO 'ADAWA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ADAWA' (/showthread.php?tid=2515) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'ADAWA' - MwlMaeda - 04-18-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ADAWA' Neno *adawa* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana ya *hali ya kufanya chuki dhidi ya mtu mwengine.* Katika lugha ya Kiarabu neno *adawa* linatokana na neno la Kiarabu *adaawah (soma: adaawatun/adaawatan/adaawatin عداوة)* lenye maana ya *hali ya chuki, uhasama na uadui baina ya wawili au zaidi.* Kinachodhihiri ni kuwa neno *adaawatun عداوة* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *adawa* maana yake ya msingi katika lugha ya asili - Kiarabu haikubadilika. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |