03-31-2022, 07:24 AM
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALFU' NA 'ALFENI'
Neno alfu katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya mamia kumi, jibu la mia moja ikizidishwa mara kumi.
Neno alfu limechukuliwa kutoka Kiarabu na kuingizwa katika Kiswahili kama lilivyo.
Neno la Kiarabu alfu( soma: alfun/alfan/alfin الف), ni nomino yenye maana zifuatazo:
1. Mia mara kumi.
2. Karne kumi alfu aamin الف عام miaka alfu.
Na neno alfeni, katika lugha ya Kiswahili, ni nomino [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya alfu mbili.
Neno hili alfeni ( soma: alfaani/alfayni) ni la Kiarabu na limeingizwa katika Kiswahili kwa kunakili lahaja za Kiarabu hususan Kiomani na Kiyemeni ambazo neno alfayni hutamkwa alfeni .
Kinachodhihiri ni kuwa maneno ya Kiarabu alfu الف na alfayni/alfeni yalipoingia katika Kiswahili hayakutoholewa wala hayakubadilika maana.
Shukran sana.
Khamis S.M. Mataka.

Mwl Maeda