MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALFU' NA 'ALFENI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALFU' NA 'ALFENI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALFU' NA 'ALFENI' 

Neno alfu katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya mamia kumi, jibu la mia moja ikizidishwa mara kumi.

Neno alfu limechukuliwa kutoka Kiarabu na kuingizwa katika Kiswahili kama lilivyo.

Neno la Kiarabu alfu( soma: alfun/alfan/alfin الف), ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Mia mara kumi.

2. Karne kumi alfu aamin الف عام miaka alfu.

Na neno alfeni, katika lugha ya Kiswahili, ni nomino  [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya  alfu mbili.

Neno hili alfeni ( soma: alfaani/alfayni) ni la Kiarabu na limeingizwa katika Kiswahili kwa kunakili lahaja za Kiarabu hususan Kiomani na Kiyemeni ambazo  neno alfayni hutamkwa alfeni .

Kinachodhihiri ni kuwa maneno ya Kiarabu  alfu الف na alfayni/alfeni yalipoingia katika Kiswahili hayakutoholewa wala hayakubadilika maana.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.