ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALFU' NA 'ALFENI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALFU' NA 'ALFENI' (/showthread.php?tid=2492) |
ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALFU' NA 'ALFENI' - MwlMaeda - 03-31-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'ALFU' NA 'ALFENI' Neno alfu katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya mamia kumi, jibu la mia moja ikizidishwa mara kumi. Neno alfu limechukuliwa kutoka Kiarabu na kuingizwa katika Kiswahili kama lilivyo. Neno la Kiarabu alfu( soma: alfun/alfan/alfin الف), ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Mia mara kumi. 2. Karne kumi alfu aamin الف عام miaka alfu. Na neno alfeni, katika lugha ya Kiswahili, ni nomino [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya alfu mbili. Neno hili alfeni ( soma: alfaani/alfayni) ni la Kiarabu na limeingizwa katika Kiswahili kwa kunakili lahaja za Kiarabu hususan Kiomani na Kiyemeni ambazo neno alfayni hutamkwa alfeni . Kinachodhihiri ni kuwa maneno ya Kiarabu alfu الف na alfayni/alfeni yalipoingia katika Kiswahili hayakutoholewa wala hayakubadilika maana. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |