Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'AFADHALI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFADHALI'

Neno *afadhali* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino: [Ngeli:i-/i-]* hali yenye unafuu; hali bora zaidi.

2. *Kivumishi:* tamko la kuonesha hali bora na ya kufaa zaidi ikilinganishwa na hali zingine.

3. *Kielezi:* bora kuliko; nafuu kidogo.

*Kuna methali:* Afadhali ya Musa kuliko ya Firauni.

*Kuna msemo:* Afadhali mchawi kuliko mfitini.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *afadhali* (soma: *afdhwalu/afdhwala افضل)* lina maana zifuatazo:

1. *Kitenzi:* Amefanya bora.

2. *Nomino:* Amekuwa mbora zaidi.

3. *Nomino:* Ziada na wingi.

4. *Nomino:* Kichobaki, salio.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *afadhali* ( *soma: afdhwalu/afdhwala افضل*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno *afadhali* halikubadili maana yake ya msingi katika  lugha ya asili - Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)