ETIMOLOJIA YA NENO 'AFADHALI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AFADHALI' (/showthread.php?tid=2053) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AFADHALI' - MwlMaeda - 01-07-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFADHALI' Neno *afadhali* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. *Nomino: [Ngeli:i-/i-]* hali yenye unafuu; hali bora zaidi. 2. *Kivumishi:* tamko la kuonesha hali bora na ya kufaa zaidi ikilinganishwa na hali zingine. 3. *Kielezi:* bora kuliko; nafuu kidogo. *Kuna methali:* Afadhali ya Musa kuliko ya Firauni. *Kuna msemo:* Afadhali mchawi kuliko mfitini. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *afadhali* (soma: *afdhwalu/afdhwala افضل)* lina maana zifuatazo: 1. *Kitenzi:* Amefanya bora. 2. *Nomino:* Amekuwa mbora zaidi. 3. *Nomino:* Ziada na wingi. 4. *Nomino:* Kichobaki, salio. Kinachodhihiri ni kuwa neno *afadhali* ( *soma: afdhwalu/afdhwala افضل*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *afadhali* halikubadili maana yake ya msingi katika lugha ya asili - Kiarabu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |