MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO "BILADI ''

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO "BILADI ''
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BILADI ''

Neno *biladi* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya *mji* .

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *biladi* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'bilaad* *(soma: bilaadun/bilaadan/bilaadin  بلاد)** likiwa ni wingi wa neno la Kiarabu *baldah (soma: baldatun/baldatan/baldatin بلدة)* lenye maana zifuatazo: 

1. Eneo kubwa la ardhi.

2. Eneo maalumu la ardhi wanalokaa watu fulani lenye miji, vijiji na mipaka inayotambulika; *nchi*.
*Yaa baladii, yaa bilaadii يا بلادي، يا بلدي* Ee nchi yangu!

3. Sehemu ya nchi au mji.

4. Mji mdogo.

5. Chanzo.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *'bilaadun  بلاد*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *biladi* lilichukua kutoka lugha ya Kiarabu maana ya *mji* na kuziacha maana nyingine.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Messages In This Thread
ETIMOLOJIA YA NENO "BILADI '' - by MwlMaeda - 08-08-2022, 08:08 PM
- - by Wayzep - 10-10-2022, 02:01 AM

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)