ETIMOLOJIA YA NENO "BILADI '' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO "BILADI '' (/showthread.php?tid=2801) |
ETIMOLOJIA YA NENO "BILADI '' - MwlMaeda - 08-08-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BILADI '' Neno *biladi* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya *mji* . Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *biladi* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *'bilaad* *(soma: bilaadun/bilaadan/bilaadin بلاد)** likiwa ni wingi wa neno la Kiarabu *baldah (soma: baldatun/baldatan/baldatin بلدة)* lenye maana zifuatazo: 1. Eneo kubwa la ardhi. 2. Eneo maalumu la ardhi wanalokaa watu fulani lenye miji, vijiji na mipaka inayotambulika; *nchi*. *Yaa baladii, yaa bilaadii يا بلادي، يا بلدي* Ee nchi yangu! 3. Sehemu ya nchi au mji. 4. Mji mdogo. 5. Chanzo. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *'bilaadun بلاد* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *biladi* lilichukua kutoka lugha ya Kiarabu maana ya *mji* na kuziacha maana nyingine. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* - - Wayzep - 10-10-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO BALAGHAMU/BELGHAMU Neno balaghamu/belghamu katika lugha ya Kiswahili ni nomino: Ngeli: li-/ya- yenye maana ya kioevu kizito kilichochanganyika na utandoute kinachotolewa kwa wingi kwa njia ya kupumulia hususan mtu anapougua mafua au kikohozi, mate mazito yanayokuwa kooni ambayo hutoka mtu anapokohoa. Msemo: Toa balaghamu zako: toa hasira zako. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili balaghamu/belghamu limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu balghamu soma: balghamun/balghaman/balghamin بلغم lenye maana ya mate yaliyochanganyika na kamasi na hutoka kwa njia ya upumuaji, dutu laini ya mate iliyochanganyika na kamasi; kohozi. Kinachodhihiri ni kuwa neno balghamun بلغم lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno balaghamu/belghamu halikubadili maana katika lugha asili- Kiarabu. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |