MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO "BILADI ''

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO "BILADI ''
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BILADI ''

Neno *biladi* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya *mji* .

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *biladi* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'bilaad* *(soma: bilaadun/bilaadan/bilaadin  بلاد)** likiwa ni wingi wa neno la Kiarabu *baldah (soma: baldatun/baldatan/baldatin بلدة)* lenye maana zifuatazo: 

1. Eneo kubwa la ardhi.

2. Eneo maalumu la ardhi wanalokaa watu fulani lenye miji, vijiji na mipaka inayotambulika; *nchi*.
*Yaa baladii, yaa bilaadii يا بلادي، يا بلدي* Ee nchi yangu!

3. Sehemu ya nchi au mji.

4. Mji mdogo.

5. Chanzo.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *'bilaadun  بلاد*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *biladi* lilichukua kutoka lugha ya Kiarabu maana ya *mji* na kuziacha maana nyingine.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*

Wayzep

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO BALAGHAMU/BELGHAMU

Neno balaghamu/belghamu katika lugha ya Kiswahili ni nomino: Ngeli: li-/ya- yenye maana ya kioevu kizito kilichochanganyika na utandoute kinachotolewa kwa wingi kwa njia ya kupumulia hususan mtu anapougua mafua au kikohozi, mate mazito yanayokuwa kooni ambayo hutoka mtu anapokohoa.

Msemo: Toa balaghamu zako: toa hasira zako.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili balaghamu/belghamu limechukuliwa kutoka neno la  Kiarabu  balghamu soma: balghamun/balghaman/balghamin  بلغم  lenye maana ya mate yaliyochanganyika na kamasi na hutoka kwa njia ya upumuaji, dutu laini ya mate iliyochanganyika na kamasi; kohozi.

Kinachodhihiri ni kuwa neno balghamun بلغم lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno balaghamu/belghamu halikubadili maana katika lugha asili- Kiarabu.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.