02-10-2022, 05:04 PM
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AJALI'.
Neno *ajali* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino [Ngeli: i-/-zi]* yenye maana zifuatazo:
1. Tukio la ghafla lenye madhara au maafa kwa mtu, watu au mali.
2. Tukio la kifo.
*Methali* : *Ajali haina kinga*: Binadamu hana uwezo wa kuzuia maafa.
3. Jambo linalotokana na kudra za Mwenyeezi Mungu; *majaaliwa* .
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ajali*( *soma: ajalun/ajalan/ajalin اجل )* ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:
1. Muda maalumu. *Likulli Shay-in Ajaluhu لكل شيء أجله* Kila kitu kina muda wake.
2. Wakati maalumu wa kuisha kitu; *kifo* : *Jaa-a ajaluhu جاء أجله* Kimefika kifo chake.
Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *ajalun/ajalan/ajalin اجل* llilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *ajali* maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu hazikubadilika bali Waswahili wakaliongezea maana ya tukio la ghafla lenye madhara au maafa kwa mtu, watu au mali na ile maana ya jambo linalotokana na kudra za Mwenyeezi Mungu; majaaliwa.
*Shukran sana.*
*Khamis S.M. Mataka.*

Mwl Maeda