ETIMOLOJIA YA NENO 'AJALI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AJALI' (/showthread.php?tid=2396) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AJALI' - MwlMaeda - 02-10-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AJALI'. Neno *ajali* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino [Ngeli: i-/-zi]* yenye maana zifuatazo: 1. Tukio la ghafla lenye madhara au maafa kwa mtu, watu au mali. 2. Tukio la kifo. *Methali* : *Ajali haina kinga*: Binadamu hana uwezo wa kuzuia maafa. 3. Jambo linalotokana na kudra za Mwenyeezi Mungu; *majaaliwa* . Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ajali*( *soma: ajalun/ajalan/ajalin اجل )* ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Muda maalumu. *Likulli Shay-in Ajaluhu لكل شيء أجله* Kila kitu kina muda wake. 2. Wakati maalumu wa kuisha kitu; *kifo* : *Jaa-a ajaluhu جاء أجله* Kimefika kifo chake. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *ajalun/ajalan/ajalin اجل* llilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *ajali* maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu hazikubadilika bali Waswahili wakaliongezea maana ya tukio la ghafla lenye madhara au maafa kwa mtu, watu au mali na ile maana ya jambo linalotokana na kudra za Mwenyeezi Mungu; majaaliwa. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |